read

Mwishilizo

Kutokana na mazungumzo haya ni dhamiri kwamba, Mawahhabiya na Wanavyuoni wanaowaunga mkono sio tu kwamba hawauungi mkono msimamo wa Imamu Husayn (a.s.) bali vile vile huyahesabu mauaji yake kuwa ni ya haki kwa sababu kamwasi Yazid na hawapingi kushiriki kwa watu hao kwenye mauaji hayo, na wanaendelea hadi wakathubutu kuyafanya mapokezi ya Ahadith ya watu hawa msingi wa itikadi zao. Wanawasifa wauaji hao. Ingawa watu hawa walihusika kwenye mauaji hayo, wanafanya kuwa Makhalifa kwa makubaliano ya watu.

Wanasema kuwa, iwapo watu watayajali mambo madogo madogo kama hayo, basi itakuwa vigumu kuwapata wapokezi wa Ahadithi. Wale walioyaridhia mauaji ya Imamu Husayn (a.s.) walifanywa kuwa watu wa kuaminika na wakweli. Lakini aliyelipizia kisasi damu hii isiyo na kosa, anachukiwa. Je, ipo haja ya kuendelea kuonyesha ni Madhehebu ipi iliyokuwa ikifuatwa na wauaji wa Imamu Husayn (a.s.)? Hadi hivi sasa Mawahhabiya wakiifuata Fatwa ya Imamu Ghazali wanajaribu kuizuia kumtaja Imamu Husayn (a.s.) ili kwamba matendo yao maovu yaweze kusalia kwenye hali ya kufichikana. (Makala hii imetafsiriwa kutoka kitabu kiitwacho "Karbala Shanasi" cha Kiurdu, kilichoandikwa na Sayyid Saeed Akhtar Rizvi, ukurasa wa 199-220.