read

Baadhi ya Maulamaa wa Ahlus-Sunna Kujiunga na Madhehebu ya Ahlul - Bait (a.s)

Kuenea kwa vitabu katika siku za hivi karibuni na kuanza kwa mijadala baina ya Waislamu jambo hili limesaidia kuweka wazi ukweli huu - haki ya kufuatwa madhehebu ya Ahlul-Bait (a.s) kwa wengi miongoni mwa maulamaa wa Sunna au wataalamu wao, kwa ajili hiyo jopo la hawa maulamaa wamejiunga na madhehebu ya Ahlul-Bait (a.s) na wametunga vitabu vilivyojaa dalili zilizo wazi, na haya ni majina ya baadhi yao:

Sheikh Muhammad Maraiy Al-Antwakiy ana kitabu Limadha ikhtartu madhihabash-Shi’ati madhihabi Ahlul-bait (a.s)

Sheikh Muhammad Amin Al- antwakiy ana kitabu Fiy twariqatiy ilaa tashayyui

Dkt. Muhammad Al-Tijaaniy as-Sammawiy Al-Tunisiy ana vitabu vingi kati ya hivyo ni: Thumma ihtadaitu

Al-Ustadh Swaib Abdul Hamid, ana vitabu vingi kati ya hivyo ni: Ibnu Taimiyah, hayatuhu, aqaiduhu, mauqifuhu min-Shi’ati Ahlul-Bait (a.s)

Wakili Ahmad Husein Yaaqub Al- urduniy, ana kitabu Al-muwajahatul-kaamilah Ma'a Rasuuli wa Aalihi

Sheikh Said Ayub ni katika maulamaa maarufu Misri ana kitabu Maalimul-fitan Juzuu mbili

Ustadh Idrisa Al Huseiny Al-magharibiy ana kitabu Al-intiqalus-swaabu fiyl Madhihabi wal-mu'utaqadi

Dkt. As'ad Qasimu kutoka Palestina ana kitabu: Haqiqatu Shi’a'ati al ithnaa shariati

Dkt. Muhammad Bayumiy Mahraaniy wa Misri ana kitabu 'Al-imamatu Ahlul-bait (a.s) juzuu tatu na ana vitabu zaidi ya sitini

Sheikh Mu'utasim Sayyid Ahmad kutoka Sudan ana kitabu "Haqiqatu dhai'atu rihilatiy nahawi madhihabi Ahlul-bait

Mwandishi Muhammad Abdul Hafidh kutoka Misri ana kitabu Limadha anaa Jafariy

Dkt. Ahmad Rasimu Annafiysi ana kitabu Atariyqu ilaa madhi-habi Ahlul -bait

Al -Ustadh Muhammad Al-Kathir ana kitabu Asalafiyatu baina Ahlus-Sunna wal -Imamiyah

Sheikh Rashid Rahmani Al-Hindiy ana vitabu vingi kati ya hivyo ni: Limaa Aswibahatu shi'iyan

As-Sayyid Yasin Al-Mayuti Al-Badaraniy kutoka Syria ana kitabu Yaa laita qaumiy Ya'alamuuna

Al Ustadh Abdul-mu'umin Muhammad Al Hasany kutoka Sudani ana kitabu Binuri Faatimata ihtadaitu

Al Ustadh Mutawakil Muhammad Ali kutoka Sudan ana kitabu Wadakhaltu Tashayu'an Sujadan

As-Sayyid Husein Al-Rajaah kutoka Syria ana kitabu Difau min Wahyi Shariati Dhidu dairati Sunnati wa Shi'ati

"Hakika sisi tuliposikia uongofu tuliuamini, atakayemwamini Mola wake basi hataogopa upungufu wala vitisho."1

  • 1. Suratul- Jinn: 13