read

Hadith ya Safina (Jahazi)

Amesema Mtume (s.a.w.w) "mfano wa Ahlul-Bait wangu kwenu ni kama mfano wa Safina ya Nuhu, atakayeipanda ataokoka na atakayeiacha ataangamia.
Wameipokea Hadith hii masahaba nane, na wafuatao wamesema ni sahihi:-Al-Haakim katika Mustadrak J: 3 uk 151.

As-Suyutuy katika Nihayatul-Afadhali fiy Manaaqibil-Aali.1

Atwaybiy katika Sharhul-Mishkaati.2 Ibnu Hajar Ashafi ambapo amesema: "Imekuja kwa njia nyingi baadhi zimezipa nguvu baadhi yake.3

Na ameisha sahihisha Hadith hii Muhammad bin Yusuf Al-Malik maarufu kwa Al- Kafi ambapo alisema baada ya maneno yake na inakuonyesha juu ya Hadith hiyo mashuhuri ambayo ni mutafaqun alaihi juu ya kunukuliwa kwake. Mfano wa watu wa nyumba yangu ni kama mfano wa Safina ya Nuhu atakayeipanda ameokoka na atakayeiacha ataghariki.4

Na Hadith imepokelewa na maulamaa zaidi ya mia moja na hamsini miongoni mwa maulamaa wa Sunni, na wameichukulia kuwa ni katika Hadith za kawaida.5

  • 1. Iko kwenye uchapishaji
  • 2. Rejea khulaswatul abaqaatil anuwaar cha Al-HuseinAl milaaniy uk:43
  • 3. Swaiqul-muhuriqah J: 2 uk 445
  • 4. Rejea Khulaswatul-abaqaatil- anwar uk 247
  • 5. Mfano: Mustadrak J: 3 uk: 151, Al -Muujamul -kabir, Tabrani uk:130, Muujamus swaghir Tabrani, uk :78, Majmau Za Waid cha Haitham J: 9 uk : 168, Jamius swaghir Suyuti , Uyunl akhbar Ibn Qutayba J :1 uk : 211