read

Hoja ya Hadith

Hadith ya thaqalayni iko wazi katika wajibu wa kushikamana na Kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu na Ahlul-Bait (a.s) kwa pamoja, kusalimika kutokana na upotovu haukupatikana isipokuwa kwa kushikamana navyo kwa pamoja kwa kauli yake (s.a.w.w) "kama mkishikamana navyo" na wala hakusema na kimojawapo, na katika yafuatayo ni maneno ya baadhi ya wajuzi wa Ahlus-sunna ambao wanatilia mkazo tuliyoyasema:

Amesema Sheikh Abdul-Rahman Anakishibandiy baada ya kuwataja Ahlul-Bait "vipi isiwe hivyo na wao ndio nyota za dini, msingi wa sheria zetu, nguzo za masahaba wetu, kwao umedhihiri uislamu na kuenea na kwao umekita mizizi na kumea, kisha imesihi kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: "Hakika mimi nimewaachieni" ....1

Na amesema Aliyul-Qaariy katika "Al-Murqaatu" kuhusu Hadith hii. Na makusudio ya kuchukua kwao ni kushikamana na mapenzi yao na kuhifadhi heshima yao, kuyafanyia kazi waliyoyapokea na kutegemea kauli zao."

Nasema: "Ni dhahiri kwamba Ahlul-Bait aghalabu wanamjua zaidi mwenye nyumba na hali zake, hivyo makusudio ni wenye elimu miongoni mwao wanaofahamu mwenendo wake, wenye kusimama katika njia yake, wenye kujua hukumu zake na hekima yake kwa haya inafaa kuwa wanalingana na kitabu cha Mwenyezi Mungu mtukufu kama alivyosema: "Na anawafundisha Kitabu na hekima."2

Na amesema Atafatazariy katika Sharhul-maqaaswid: "Je, huoni kwamba Mtume (s.a.w.w) amewaunganisha na Kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu katika kushikamana navyo ni kunusurika na upotovu na hakuna maana ya kushikamana na kitabu isipokuwa kuchukua yaliyomo humo miongoni mwa elimu na uongofu vivyo hivyo katika Itrah.3 (kizazi cha Mtume)."

Amesema Al-Munawiy: "Kama mtashikamana na maamrisho ya Kitabu chake na mkakatazika na makatazo Yake na mkaongoka kwa uongofu wa kizazi changu, Na mkafuata mwenendo wao mtaongoka na hamtapotea kamwe."4

  • 1. Al-'Iqidul-Wahiyd " uk:78
  • 2. Rejea Hadith thaqalayni - Tawatur-fiqihu "na makala ambayo ilichapishwa na Darul-taqiryb-misri juu ya Hadith ya thaqalayni
  • 3. Rejea Hadith thaqalayni - Tawatur-fiqihu "na makala ambayo ilichapishwa na Darul-taqiryb-misri juu ya Hadith ya thaqalayni
  • 4. Faidhul – qadiriy J:3 uk:14