read

Hoja ya Hadith

Hoja ya Hadith iko wazi kabisa kwamba nusra ni kupanda safina ya Ahlul-Bait, na maana ya kupanda Safina yao ni kuwafuata wao, kuwaiga, kuwasikiliza na kuwatii, amesema Ibnu Hajar Ashafi: "Kufananishwa kwao na safina kama ilivyotangulia ni kwamba atakaye wapenda, akawatukuza kwa kushukuru neema waliyonayo na akachukua uongofu wa Maulamaa wao ameokoka kutokana na giza la ikhitilalifu na atakayeacha hayo ataangamia katika Bahari ya kukufuru neema na ataangamia katika dimbwi la upotovu.1

Hadith

Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w): "Mimi ni Mji wa elimu na Ali ni mlango wake anayetaka elimu basi auendee mlango.2

Amesema Mtume (s.a.w.w): "Nyota ni tumaini la watu wa ardh3ini kutokana na kughariki na Ahlul-Bait ni tumaini kwa umma wangu kutokana na ikhitilafu, kama kabila katika Waarabu litawakhalifu basi watakhitalafiana na watakuwa katika kundi la Ibilisi.

Amesema Mtume (s.a.w.w); "Ali yuko pamoja na Qur'an na Qur'an iko pamoja naye havitatengana hadi vitakaponijia kwenye birika.”4

Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w): "Ali yuko pamoja na haki, na haki iko pamoja na Ali yazunguuka naye popote anapozunguka.”5

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) alimwambia Ali (a.s): "Wewe utaubainishia Umma wangu ambayo humo wamekhitilafiana baada yangu.”6

Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w): "Anayependa kuishi maisha yangu na kufa kama nitakavyokufa na kuishi katika pepo aliyoipanda miti Mola wangu, basi ampende Ali na awafuate Maimamu katika kizazi chake baada yake, hakika wao ni kizazi changu, wameumbwa kutokana na udongo wangu, wameruzukiwa fahamu yangu na elimu yangu, maangamizo kwa wanaokadhibisha fadhila zao katika Umma wangu, wenye kukata kwao udugu wangu Mwenyezi Mungu asiwape shifaa yangu."7

Dalili Kutoka Katika Qur'an

Ilipoteremka kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Hakika wale walioamini na wakafanya vitendo vyema hao ndio viumbe bora."8

Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w): "Ewe Ali! hao ni wewe na wafuasi wako9 na akaongezea katika riwaya: "Hakika wao ndio wenye kufaulu siku ya Qiyama."

Amekwisha tuamrisha Mwenyezi Mungu kushikamana na Ahlul-Bait (a.s) katika kauli yake. "Na shikamaneni nyote na kamba ya Mwenyezi Mungu na wala msifarikiane."10

Makusudio ya kamba katika Aya hii ni vizito viwili (Kitabu na Ahlul-Bait) Hadith ya thaqalayn ni dalili bora juu ya tunayoyasema, na Hadith zimefasiri kamba ya Mwenyezi Mungu kuwa ni Ahlul-Bait (a.s).”11

Ametuamrisha Mwenyezi Mungu kuwauliza wenye kujua kwa kusema, "Waulizeni wanaojua
kama nyinyi hamjui" "12
Na wanaojua tulioamriwa kuwauliza ni wao Ahlul-Bait kama ilivyo katika riwaya.”13

Na ametuamrisha Mwenyezi Mungu kuwa pamoja nao katika kauli yake.

"Enyi mlioamini muogopeni Mwenyezi Mungu na kuweni pamoja na wakweli."14

Amesema Sibtu Ibnul-Jauziy: Wamesema maulamaa wa sira: Maana yake kuweni pamoja na Ali na Ahlul-Baiti wake. Ibnu Abbasi amesema: "Ali ni Bwana wa wakweli."15

Na wao ni ambao ametuamrisha Mwenyezi Mungu Mtukufu kuwatii katika kauli yake.
Mtii Mwenyezi Mungu na mtiini Mtume na wenye mamlaka miongoni mwenu"16 wenye mamlaka ni Ahlul-Bait (a.s)."17

Na wao ndio iliteremka kwao ayatu Tatwihir ambapo Mwenyezi Mungu amewakinga kutokana na uchafu na akawatakasa kabisa, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
"Hapana si jingine, Mwenyezi Mungu anataka kuwaondolea (kuwakinga na) uchafu Ahlul-Bait na kukutakaseni kabisa."18 Aya hii imeshuka kwa Ali, Fatima, Hasan na Husein (a.s)."19

Na Ahlul-Bait ni ambao alitoka nao Mtume wa Mwenyezi Mungu kufanya mubahila na manaswara aliposema Mwenyezi Mungu. 'Atakayekujadili kwa hilo baada ya kukujia elimu, basi sema: "Njooni tuwaite watoto wetu na watoto wenu, wanawake wetu na wanawake wenu, sisi na nyinyi kisha tuombe na tujaalie laana ya Mwenyezi Mungu iwashukie waongo."20

Wafasiri wamekubaliana kuwa Aya hii imeshuka kwa As-habul Kisai, Hasan na Husein walikuwa ni katika watoto wa Mtume (s.a.w.w) na Fatima Zahraa (badala) ya wanawake wote na Ali (a.s) ni katika nafsi yake."21
Na wao ndio ambao Mwenyezi Mungu amefanya mapenzi yao ni wajibu kwa kila mwislamu. Amesema Mwenyezi Mungu: "Sema sikuombeni malipo juu yake isipokuwa kuwapenda jamaa zangu wa karibu.."22 Na makusudio ya jamaa wa karibu ni Aswihabul-kisai. Ali, Fatima, Hasan
na Husein.”23
Na wao ni ambao Mwenyezi Mungu amefaradhisha kuwaswalia. Amesema Mwenyezi Mungu:
"Hakika Mwenyezi Mungu na malaika wake wanamswalia Mtume, enyi mlioamini mtakieni rehma na msalimieni24 Na makusudio ya kumtakia rehma Mtume (s.a.w.w) hapa ni yeye na Ahlul-Bait wake kwa pamoja kama alivyoeleza wazi katika riwaya hii......25

 • 1. Sawaiqul Muhriqa Juz. 2. uk. 446-447
 • 2. Wamesema hadith hii ni sahihi maulamaa wakubwa wa Ahlus-sunna wal- jamaah kama vile Yahya bin Muiyn, Twabariy katika Tahadhiybul- athaar, Al-Haakim katika Mustadrak na Al-Hafidh Al-Ashiariy Muhammad bin Swadiq ametunga kitabu akathibitisha humo usahihi wa Hadith hii akakiita "Fatuhul- mulkil-aliyi biswihati Hadith babu madiynatil-ilmi Aliyi" na rejea Al-Mustadrak J : 3 uk. 126 na 127, Usudul-Ghabah J: 4 uk. 22, Tadhikratul-Khawasi uk. 47 na 48
 • 3. Mustadrak J:3 uk 149 amesema Hadith hii sanadi yake ni sahihi na hawa- jaitoa,Swawaiqul-Muhariqah J: 2 uk. 445 na amesema ni sahihi, Majimau zawaid J: 9 uk 147
 • 4. Al-Mustadrak, J: 3 uk. 124 amesema Hadith hii ni sahihi katika sanad, Tabarany katika Al-Auswat, Swawaiqul Muhuqah J.2 uk. 361
 • 5. Tarikhu Baghidad J: 14 uk 321, Muntakhabul-kanzu J: 5 uk 30 narejea Sunan Tirimidhiy J: 5 uk. 633, Mustadrak J: 3 uk. 124, Majimau zawaid J: 7 uk. 25
 • 6. Mustadrak J: 3 uk 122 na amesema ni sahihi kwa masharti ya Bukhariy na Muslim, Kanzul-ummal J:6, uk 156 Muntakhabul-kanzu J: 5 uk 33 Tarekhu Dimishiq J: 2 uk 488 Kunuzul-haqaiq ya Munawiy uk 188
 • 7. Huliyatul-Aauliyai J: 1 uk 86, Majmau zawaid Juz. 9, uk 108 Tarekh Dimishiq J: 2 uk 95, na rejea Kanzul-Ummal J: 12 uk 104 Hadith No.2625 Muntakhab
 • 8. Suratu Bayina:7
 • 9. Hadithi hii inapatikana takriban katika vitabu ishirini kati ya hivyo ni Shawahidu tanzil cha Shaukaaniy Al-Hanafiy J:2 uk 356-466, Durul- manthur J:6 uk 379, Tafsiri Twabariy J:3 uk 146, Fatuhul-qadir ya Shaukaniy J: 5 uk 477, Ruhul maaniy ya Al-Alusiy J. 30 uk 207 Aswawaiqul mu huriqah uk. 96
 • 10. Suratul -Ali-Imran: 103
 • 11. Rejea Ruhul maaniy J: 4 uk 16, Aswaawaqil-Muhuriqah uk 444, Shawahidu tanzil J: 1 uk 30, 177 - 180, Al-Itihaaf bihubil-ashiraaf" ya Shibrawiy Ashaafiy uk. 76
 • 12. Suratu Nahl: 43
 • 13. Tafsiri Twabariy J: 14 uk: 75, Tafsir Ibnu Kathiyr J:2 uk : 591, Tafsir Qurtubiy J 11 uk : 272, Ruhul Maaniy J: 14 uk. 41, Tafsir Thaalabiy
 • 14. Suratu Tawba 119
 • 15. Tadhikratul-khawas uk 10 na rejea Durul-manthur J: 3 uk 290 Fatuhul qadiri J: 2 uk 295 Ruhul-maaniy
  J: 11 uk 41 na tafsiri Thaalabiy
 • 16. Suratun Nisaa: 59
 • 17. Shawahidu tanzil J:1, k: 148 Hadith No. 202 - 204. Tafsiri Raaziy J: 4 uk 113, Tafsiri Baharul-Muhuyt ya Abu
  Hayaan Al -Andalusiy J: 3, uk 278, Tafsiru Nisaburiy katika Sharhu ya Tafsiru Twabary J: 5 uk 79
 • 18. Suratul - Ahzaab 33
 • 19. Sahihi Muslim kitabu Fadhalis - Swahaba babu Fadhailul-, Ahlul- Baiti Nabiyi, sahihi Tirimidhiy J: 5 uk 663,
  Musnad Ahmad J: 1 uk 330, Al-Mustadrak sahi- haini J: 3 uk. 133,146,147 na 158
 • 20. Suratul Ali- Imran: 61
 • 21. Sahihi Muslim kitabu Fadhail s-swahaba babu min Fadhaili Ali bin Abiy Twalib, Sahihi Tirimidhiy J: 5 uk
  638, Mustadrak J: 3 uk 150
 • 22. Suratus-Shuraa: 23
 • 23. Tafsiri Twabariy J: 25 uk. 16, Tafsiri Ibnu Kathiri J: 4 uk. 112, Tafsiri Zamakhishary J: 3 uk. 467,
  Tafsiri Qurtubiy J: 16 uk 22, Al-Mustadrak J: 3 uk 172
 • 24. Suratl-Ahzaab: 56
 • 25. Sahihul-Bukhariy kitabu Tafsiri babu Qauluhu: inna-llaaha wamalaikatahu Yuswaalunna alaa Nabiy, Sahihi Muslim kitabu Swalaat alaa Nabiy baada Tashahud, Tirimidhiy J: 2 uk. 353