read

Hoja za Pande Mbili Katika Mizani

Imethibitika kwamba hakuna dalili ya kufuata madhehebu manne na wengine katika wanaojiita Ahlus-sunna juu ya usahihi wa manhaji yao, sio katika Qur'an wala katika Sunna. Ama wafuasi wa Ahlul-Bait (a.s) wanayo hazina kubwa kati ya dalili za Qur'an na Sunna juu ya wajibu wa kuwafuata wao, kama tutaweka hoja za Shi’a katika mizani na tukaweka hoja za Ash'ariah (ambazo hazipo) katika upande mwingine wa mizani basi upande wa hoja za Shi’a ungekuwa ni mzito kwa Hadith ya Thaqalayni (vizito viwili) peke yake.

Na kwa hiyo tunaona kwamba ni wajibu kuwafuata Ahlul-Bait na kuchukua kutoka kwao, na wajibu huu ni kutekeleza amri ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake (s.a.w.w) katika wajibu wa kuwafuata wao, nao ndio sababu ya pekee ya kufaulu siku ya Qiyama.