read

Itikadi ya Shi’a Kwa Ufupi

Itikadi ya Shi’a ni itikadi ya Ki-Islamu aliyokuja nayo Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) kwa misingi yake ifuatayo:-

Tauhid (Upweke)

Shi’a wanamwamini Mwenyezi Mungu Mtukufu, Mola mmoja na wanamkanusha Mungu asiyekuwa yeye na anayemwabudu asiyekuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ni mshirikina, na wao wanamtakasa Mwenyezi Mungu kutokana na kila aibu na upungufu, na wanathibitisha sifa ambazo zinalingana na Utukufu wake, hafanani na chochote, ana majina mazuri, ame epukana na dhulma na upuuzi, mwadilifu, mwenye hekima "Sema, Mwenyezi Mungu ni mmoja, Mwenyezi Mungu ndio mwenye kukusudiwa, hakuzaa wala kuzaliwa na wala hana anayelingana naye."1

Nubuwwah (Utume)

Shi’a waanamini Mitume wote ambao wametumwa na Mwenyezi Mungu na katika itikadi yao ni kwamba atakaye mkanusha mmoja wao basi ni kafiri, na wa mwisho wao na mbora wao ni Mtume wetu Muhammad (s.a.w.w). Mitume ni ma'asum (wamehifadhiwa) kutokana na madhambi madogo na makubwa, hifadhi ya jumla "Hawamuasi Mwenyezi Mungu na wanafanya waliyoamrishwa" na ni wajibu kuwatii "aliyokuleteeni Mtume yachukueni na aliyokukatazeni yaacheni"2 na wao wanawatukuza Mitume na wanawaepusha kutokana na upungufu, na kutokana na waliyonasibishiwa nayo kama vile kauli inayosema kwamba Mtume alikuwa anazunguka kwa wake zake kumi na mmoja kwa muda wa saa moja3 na kwamba yeye (s.a.w.w) alikuwa anamlaani asiyestahili kulaaniwa4 na kwamba alikuwa anawawatesa baadhi ya watu5 na kwamba alikuwa anasahau katika sala yake6, na kwamba alikuwa anajisaidia haja ndogo katika Vichochoro.7

Al -Miad (Siku Ya Mwisho)

Shi’a wanaamini kwamba kuna siku Mwenyezi Mungu atawakusanya viumbe wote na kuwalipa kutokana na vitendo vyao hivyo, waumini wataenda peponi na makafiri wataenda motoni, na wanaamini kaburi, pepo, Mizani, swiratwa......

Al-Adl (Uadilifu)

Uadilifu ni sifa miongoni mwa sifa za Mwenyezi Mungu Mtukufu, Shi’a wanaamini na wanaitakidi kwamba vitendo vyote vya Mwenyezi Mungu ni viadilifu na vyenye hekima na kwamba Yeye hamdhulumu yeyote hata kwa kiasi cha punje ndogo kabisa, kinyume na rai ya Ash’ariah ambao wasema kwamba inawezekana kwa Mwenyezi Mungu kuwa adhibu waumini...

Al-Imamah (Uimamu)

Shi’a wanasema kwamba Mtume (s.a.w.w) kabla ya kufariki alimteua Ali (a.s) kuwa khalifa wa Waislam8"na anafuatiwa na maimamu kumi na moja katika kizazi chake, wataongoza umma baada ya kuondoka Mtume (s.a.w.w) lakini yalitokea mapinduzi ambayo yametajwa katika Qur'an. "Hakuwa Muhammad isipokuwa ni Mtume, walishapita kabla yake Mitume, je, akifa au akiuliwa mtageuka nyuma kwa visigino vyenu? Na atayegeuka kwa visigino vyake, hatamdhuru Mwenyezi Mungu kwa chochote Mwenyezi Mungu atawalipa wenye kushukuru."9

Na maimamu aliowateua Mtume (s.a.w.w) baada yake ni maimamu kumi na mbili. Aliwaashiria katika Sahihi Muslim: "Dini haitaacha kuwa yenye kusimama hadi Qiyama kifike au watakuwa kwenu makhalifa kumi na mbili wote kutoka katika Makuraishi."10

Na kutoka kwa Jabir bin Samra amesema, "nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w), akisema Uislam hautaacha kuwa na nguvu hadi watimie makhalifa kumi na mbili.
Kisha akasema neno sikulifahamu nikamuuliza, baba yangu amesemaje? Akasema, amesema wote ni katika makuraishi."11

Na maimamu wa Ahlul- Bait ni: -

1 Imam Ali bin Abi Talib (a.s)-Amirul-mu'uminina

2 " Hasan Bin Ali -Al-Mujtaba (a.s)

3 " Husen bin Ali Shahid (a.s)

4 " Ali bin Huseini-Zainul-Abidin (a.s)

5 " Muhammadi bin Ali-Al-Baqir (a.s)

6 " Ja'fari bin Muhammadi-As-Swadiq (a.s)

7 " Musa bin Ja'far-Al-Kadhim (a.s)

8 " Ali bin Musa-Ar-Ridhaa (a.s)

9 " Muhammadi bin Ali Al-Jawad (a.s)

10 " Ali bin Muhammadi-Al-Haadiy (a.s)

11 " Hasani bin Ali-Al-Askary (a.s)

12 " Al-Hujjatu bin Hasani-Al-Mahdi (a.s)

 • 1. Suratul- Ikhlas
 • 2. Suratu- Hashr :7
 • 3. Sahih Bukhary kitabul-ghusul babu idha jama'a thuma aada waman Daara alaa nisaihi fiy ghusuli wahidi
 • 4. Sahih Muslim kitabul-biri waswilati wal-aadaabu
 • 5. Sahihi Bukhari kitabu twib babu daawai bi abuwali-Ibil
 • 6. Fatuhul-bar J : 1 uk-328
 • 7. Sahihi bukhary kitabul-adab babu maayajuzu min dhikiri naasi Sahihi kitabu masj wadhiu swalat babu sahau Fiy swalati wasujudi lahu.49 Na kuna dalili zilizo wazi juu hilo katika vitabu vya Ahlus sunna, kwa ziada kuhusu maudhui haya rejea kitabu cha Al- ghadiri,cha Sheikh Al-amin, lhqaqul-haqi cha Tasatary na kitabu chetu warakibtu safinati tunajibu baadhi shubuhati zilizotolewa kama vile,shura,uimamu na Abubakari kuswalisha watu
 • 8. Na kuna dalili zilizo wazi juu hilo katika vitabu vya Ahlus sunna, kwa ziada kuhusu maudhui haya rejea kitabu cha Al-ghadiri,cha Sheikh Al-amin, lhqaqul-haqi cha Tasatary na kitabu chetu warakibtu safinati tunajibu baadhi shubuhati zilizotolewa kama vile,shura,uimamu na Abubakari kuswalisha watu
 • 9. Suratul-Imraan: 144
 • 10. Kitabul-Imaara, babu Anaasu tabaul-quraish Walkhilafatu fiy quraish
 • 11. Kitabul-Imaara, babu Anaasu tabaul-quraish Walkhilafatu fiy quraish