read

Katika Zama za Mtume (s.a.w.w)

Maswahaba (r.a) walikuwa wanarejea kwa Mtume (s.a.w.w) katika mambo yanayowatokea, naye alikuwa anawajibu kulingana na sheria ya Mwenyezi Mungu, na sisi tunajua kuwa Mtume (s.a.w.w) asingebaki milele ili watu wamrejee kwa mambo ya kidini na kidunia, alifariki (s.a.w.w) baada ya kutimiza vizuri wajibu wake, na lazima awepo atakaye bainisha vizuri sheria za Mwenyezi Mungu, ubainifu ulio kamili na sahihi ambapo Mwislamu atapata matumaini kwayo na kwamba kauli yake hii ndiyo makusudio ya sheria.

Lakini huyu atakayebainisha ambaye Mwenyezi Mungu ametuandalia ni nani? Swali hilo ndilo limegawa umma katika makundi mengi. Hakika Mwenyezi Mungu hatamkubali mwanadamu isipokuwa aamini uislamu ambao aliuteremsha kwa Mtume wake (s.a.w.w). Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "anayetaka dini isiyokuwa ya Ki-Islamu hatokubaliwa nayo na kesho Akhera atakuwa miongoni mwa wenye hasara."1

Lakini tutapata wapi uislamu huu ambao Mwenyezi Mungu hakubali isipokuwa huo? Je, uko kwa Ash'ariy? Na madhehebu manne? Au uko kwa Shi’a Imamiya? Au uko kwa Salafia? Au uko kwa Mu’utazila? Au uko kwa Mataridiyah? Swali linaendelea vivyo hivyo hadi tufikie kundi la sabini na tatu.

Njoo tuwe pamoja, ewe msomaji mtukufu, ili tumtafute huyu mbainishaji hadi tuchukue dini yetu kutoka kwake na tujivue na dhima yetu mbele ya Mwenyezi Mungu, tutafute mfumo wa Mwenyezi Mungu ambao umeepukana na kasoro na makosa, mfumo ambao umesimama juu ya ukweli na yakini, usio na ziada, upungufu wala mabadiliko. Njoo tuangalie katika hoja za makundi mawili yafuatayo ili tuone nafasi yake katika uislamu ili tusibakie kama wale wanaosema: Hakika sisi tunadhani dhana tu na wala sisi hatuna yakini.2

Ufafanuzi wa Nadharia ya Kwanza

Ni nadharia ambayo inafuatwa na Waislamu wengi hivi leo na wao wanajiita Ahlus-Sunna wal-jamaah, wao katika misingi ya dini (usuul) wanarejea kwa Abul - Hasani Al-Ash'ariy na katika ( furu’u) wanarejea kwa maimamu wanne."3

Abul-Hasan Al-Ash'ariy amezaliwa 270H, na inasemekana amezaliwa 260H na amefariki 324H, na inasemekana 330H, amesoma elimul-kalaam kwa Al-Jabaiy, mmoja wa masheikh wa Mu'utazilah na baada ya miaka 40 katika muutazilah na kwa athari za mijadala mingi pamoja na mwalimu wake Al-Jabaiy; akapata maoni mahsusi yaliyomfanya aache kuwa Mu'utazilah"4 na akaanzisha madhehebu yake yenye msimamo wa kati baina ya watu wa Hadith na Mu'utazilah "wenye kufuata akili, madhehebu yake yakawa ni kutumia akili na kunukuu, madhehebu yake yalienea baada ya karne ya sita Hijiria, Ash'aria wanafuata mmoja wa maimamu wanne wa kifiqihi nao ni:-

Abu Hanifa Nu'umani bin Thabit

Maaliki bin Anasi

Muhammad bin Idrissa As-Shaafiy

Ahmad bin Hanbali

Hawa maimamu hawakuwa katika Ash'ariy; Ash'ariy amezaliwa baada yao kwa miaka mingi, Abu Hanifa alikuwa ni Marijiah, Ibnu Hanbali na Maaliki walikuwa katika Itikadi ya watu wa Hadith.

Ufafanuzi wa Nadharia (Madhehebu) ya Pili

Nayo ni nadharia ambayo inafuatwa na Shi’a Al-Imamiya na wao wana idadi kubwa katika waislamu na wanafuatia baada ya Ash'aria kwa idadi. Shi’a wanachukua uislamu wao - itikadi na fiqihi - kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) na watu wa nyumba yake watukufu (a.s) na wala si vinginevyo, na wanaamini uimamu wa Ahlul-Bait, kifikra na kisiasa; na muda wote wa historia walikuwa wanapinga watawala jeuri, na walipata mateso mengi na kupotoshwa shakhisiya yao na watawala na maulamaa waovu kwa muda wote wa historia ya Ki-Islamu.

Ama ni lini Ushi’a ulianza, hapa kuna rai nyingi katika kuanza kwake5, na ambayo sisi tunaamini ni kwamba wafuasi wa Ali (a.s) walianza katika uhai wa Mtume (s.a.w.w) ambao walikuwa wanamsifu na kumuenzi, kisha jina la Ushi’a likakolea zaidi baada ya hapo.

Amesema Abu Hatimu Ar-Raaziy mwenye kitabu cha Az-Ziynah: “Hakika jina la kwanza lililodhihiri katika Uislamu katika zama ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) ni Shi’a, na hii ilikuwa ni lakabu ya masahaba wanne nao ni:-

Abu Dharri
Salman
Miqidad
Ammar6

Ibnu Khaldun amesema: "Kundi la masahaba lilikuwa linamfuata Ali, na likaona kuwa ana haki zaidi kuliko mwingine, na alipoenguliwa na kupewa mwingine wakachukia juu ya hilo na wakamsikitikia, isipokuwa kaumu kwa kushikamana kwao na dini na kujali kwao umoja hawakuzidisha katika huo mnong'ono zaidi ya kuchukia na masikitiko.7

Dkt. Subhi Swalehe amesema: Kulikuwepo baina ya Masahaba hata wakati wa Mtume (s.a.w.w) na wafuasi wa mtoto wake wa kulea Ali. Kati yao ni:-

Abu Dhar Al-Ghafaar
Miqidad bin Al-Aswad
Jabir bin Abdillah
Ubay bin Kaab
Abu Tufail Omar bin Waail

Abbas bin Abdulmutalib na watoto wake wote Ammar binYaasir na Abu Ayub Al-Answariy8
Na katika waliosema Ushi’a ulianza wakati wa Mtume ni Ustadh Muhammad Kurd Ali katika
kitabu chake cha "Khitwatu shaami."9

Na Muhammad Abdillah Annan katika "Jumuiyat Siriyah" na Abdillah Al-Amin katika kitabu chake "Al-firaqu wal-madhaahibul qadiymah."10

 • 1. Surat Ali-imraan:85
 • 2. Surat Al-jathiya 32
 • 3. Yapasa kuelewa kwamba lakabu ya Ahlus-sunna wal-jamaaah ni pana zaidi Ash’ari anaingia humo Al-
  metaridiyah, Adhahiriyya Al-hashawiyah, na watu wa Hadith, kusema kweli lakabu hii - kwa Ash’ariah ni kwa
  upande wa ujirani (Ukuruba) kwa kujiita kwao lakabu hiyo
 • 4. Alipata sababu zingine labda zilizomsababisha kufuata jambo hili hapa sio mahali pa utafiti wake
 • 5. Baadhi yao wamesema ushi’a umeanza siku ya saqifa na inasemekana siku aliyouliwa Athumani na inasemekana
  umeanzishwa na Abdillahi bin Saba'a ……
 • 6. Raudhaatul jannaat 88
 • 7. Tarikhu Ibnu Khuldun Juz.3 uk 364
 • 8. Anudhumul - islaamiyah, uk 96
 • 9. Khitwatu shaam J 5 uk 251
 • 10. Kwa ufafanuzi wa maudhui haya rejea kitabu chetu"Warakibtus Safina uk. 616 - 619