read

Kauli za Maulamaa Kwa Maimamu

Khatibu Al-Baghdad amepokea kwa Isnad kutoka kwa Wakii amesema: walikutana Sufiyan Thauriy, Shariki, Hasan bin Swaleh na Ibn Abiy Laila; wakamwita Abu Hanifa, akawajia, wakamwambia: "Unasemaje juu ya mtu aliyemuuwa baba yake? Akamuoa mama yake na akanywa pombe akiwa amekaa juu ya kichwa cha baba yake?"

Akasema: "Ni mu'umini." Ibn Abu Laila akamwambia: "Sitokubali shahada yako abadani," Sufiani Thauriy akamwambia: "sitokusemesha kamwe," na Shariki akamwambia: "kama ningekuwa na mamlaka juu yako ningekukata shingo," Hasani bin Swalehe akamwambia: "Uso wangu kwako ni haramu kutazama uso wako abadani" ….. na aliposikia kufariki kwake Sufiyani alisema: "Namshukuru Mwenyezi Mungu ambaye amewapumzisha waislamu kwake.1

Naye amesema Ibnu Abdi Barr juu yake: "katika waliomshutumu na kumkosoa ni Muhammad bin Ismail Al-Bukhariy, amesema katika kitabu chake "Al-Dhuafau wal-matruukina Abu Hanifa Annuman bin Thabit Al-Kuufiy, Naimu bin Hammadi." Amesema ametusimulia Yahya bin Said na Maadh bin Maadhi; tulimsikia Sufian Thauri anasema: "Abu Hanifa alitakiwa atubu, kutokana na kukufuru kwake mara mbili, Nuaim bin Al-fazaariy amesema: "Nilikuwa na Sufiyan bin Uyainah ikaja habari ya kifo cha Abu Hanifa," akasema: "Alikuwa anavunja Uislamu tawi kwa tawi na hakuzaliwa katika Uislamu mtoto muovu kuliko yeye, haya ni ambayo ameyataja Al-Bukhariy.”2

Kutoka kwa Walid bin Muslim anasema: Aliniambia Malik bin Anasi, "Je, Abu Hanifa anataja mji wenu?" Nikasema ndio, akasema, "haifai kuishi katika mji wenu."3

Na anasema Ibnu Abdil-barr juu ya Imam Malik: Ameshazungumza Ibnu Abiyt Dhiib juu ya Malik bin Anasi maneno mabaya na makali nimeona karaha kuyataja, ni mashuhuri kwake aliyasema kwa kupinga kwake kauli ya Malik katika Hadith ya "Al-bay ain bil-khiyar"; Ibrahim alikuwa anazungumza dhidi yake, na Ibrahim bin Yahya alikuwa anaomba dhidi yake, vile vile amezungumza juu ya Malik - katika aliyoyataja As-Saajiy katika kitabu chake Al-Illal - Abdul - Azizi bin Abiy Salamah na Abdurahman bin Zaid bin Aslam na Ibnu Is'haaq na Ibnu Abiy Yahya na Ibnu Abiy Zanad na wakaaibisha madhehebu yake, na wamezungumza juu yake wasio kuwa hao kwa kuacha kwake riwaya ya Saad bin Ibrahim, na riwaya yake kutoka kwa Daud bin Al-Hasyin na Thauri bin Zaid. Na alishutumiwa Shafi na baadhi ya wafuasi wa Abu Hanifa katika rai yake kwa hasadi kwa nafasi ya Uimam wake.

Na watu walimlaumu katika kupinga kwake kupaka juu ya khofu katika safari na pasipokuwa na safari na katika maneno yake juu ya Ali na Athumani na katika fatwa yake katika kuwaingilia wanawake nyuma."4

Ama Shafi ameshazungumza juu yake Yahaya bin Muiyn - Imam wa kurekebisha na kukosoa, amesema sio mkweli;5 Amesema, Ibnu Abdil-barr : Imesihi kutoka kwa Ibnu Muiyn kwa njia nyingi kwamba alikuwa anazungumza juu ya Shafi."6

Na Wao Ni Wafu Vile Vile

Vipi tutawafuata katika dini yetu na wamesha kufa kabla ya miaka elfu moja na mia mbili? Mas'ala yao yaliyoandikwa hayatoshi na zama zinaendelea kubadilika, kila siku kunakuja mas'ala mapya.

Kadhalika Wametofautiana

Hakika maimamu wanne wametofautiana baina yao, kila mmoja ana fiqih mahsusi; na sisi tunafahamu kwamba hukumu ya Mwenyezi Mungu ni moja na sio mbili kwa sababu haki ni moja na sio nyingi, watu wanaweza kutoa hoja kwa Hadith: "Hitilafu katika Umma wangu ni rehema" ili watoe kisingizio cha ikhitilafu iliyodhihiri baina ya maimamu, lakini tukifaradhisha kuwepo kwake inapingana na Qur'an, vipi Mtume atahimiza Umma wake juu ya kutofautiana naye anawasomea kutoka kwa Mola wao Mtukufu; "Nashikamaneni na kamba ya Mwenyezi Mungu nyote na wala msitengane"7 na kauli yake "na wala msiwe kama wale ambao waliofarikiana na kutofautiana baada ya kuwajia ubanifiu8 na kauli yake, Hakika umma wenu huu ni umma mmoja."9

Hadith hii pamoja na kuenea kwake haina sanadi na kwayo anasema Al-Albaniy: "Haina asili muhadithuna wamejitahidi ili wapate sanadi, lakini hawakupata."

Na amenukuu Al-Munawiy kutoka kwa As-Sabakiy kwamba amesema: "Haifahamiki kwa Muhadithyna na sikupata sanadi sahihi wala dhaifu, Amekiri Sheikh Zakariya Al-Answaariy katika Sharh yake katika tafsiri ya Al-Baidhawiy (Q 3/92)."10

Na amesema Ibnu Hazim juu yake: "Na hii ni katika kauli mbaya kwa sababu kama Ikhitilafu ni rehma basi kuafikiana kungekuwa ni bughudha na hili ni ambalo halisemi Mwislamu, kwani hakuna isipokuwa kuafikiana au kufarikiana, na ama ni rehma au bughudha. Na amesema katika sehemu nyingine: "Ni batili uwongo."11

 • 1. Tarikhu Baghidad J: 13 uk 374
 • 2. Al-ilitiqaau uk. 150
 • 3. Al-'ilalu wa maarifatu rijaali "cha Ahmad bin Hambal J: 2 uk 547 kimehakikiwa na kutolewa na Wasiyullah Abbas na akasahihisha Sanad zake.
 • 4. Jamiu bayanil - ilimi wafadhilihi J: 2 uk 1115
 • 5. Jamiu bayanil - iilimi wafadhilihi J: 2 uk 1114
 • 6. Jamiu - bayanil - iilimi wafadhilihi uk 394
 • 7. Suratu Ali-Imran : 103
 • 8. Suratu Ali-Imran :105
 • 9. Suratul-Ambiyai :92
 • 10. Silsalatul-ahaadiythi dhaiyfah J:1, uk 76 Hadith ya 57
 • 11. Al-Ihakam fii Usuuli Ahkaam Juz. 5 uk 64