read

Kuondoa Kikwazo

Inaonyesha kuna kikwazo mbele yetu na ni lazima tukiondoe kabla ya kuingia ndani ya maudhui kwani mtu anaweza kusema: "Hakika kutoa maoni katika maudhui kama haya, humo kuna kupinga fikra za watu wengine na viongozi wa madhehebu.

Hakika maneno haya yanahitaji msimamo, utafiti wetu huu sio mwingine isipokuwa ni utafiti wa kielimu na jaribio la kufikia ukweli halisi na wala hatukusudii kumuudhi yeyote, na hata kama utafiti wetu utakhalifu moja ya madhehebu ya Ki-Islamu au mmoja wa viongozi, hili halimaanishi kuwa na uadui nao bali lengo la hilo ni kubainisha kukosea kwao, kosa ambalo limetokana na utafiti safi wa kielimu, na humo hakuna uadui dhidi ya yeyote wala kugusa shakhisiya ya yeyote.

Na kugundua kosa ni maendeleo makubwa kwetu katika kusonga mbele kuelekea kwenye ukamilifu.

Hakika mshangao wangu unazidi kwa mtu ambaye anafumba macho yake na kuziba masikio yake hali ya kuwa anatafuta siasa ya mbuni akidhani kuwa atanusurika kutokana na hatari inayomuandama! Hakika Hadith ya 'Umma utagawanyika mafungu 73' hayaepukiki lazima tukubali hilo, na kuvua mila ambazo zimefunika akili zetu ni hatua ya awali kuelekea kwa Mwenyezi Mungu.