read

Mwisho

Ni bora kwa waislamu waadilifu kuacha ambayo wameyaandika wapinzani wa Shi’a dhidi yao na waanze wenyewe kwa akili zao utafiti juu ya ukweli. Vitabu vya Shi’a vimeenea kila sehemu na kuna uwezekano wa kuwasiliana na taasisi zao na maulamaa wao.

Si dai katika utafiti huu kwamba mimi nimefikisha Ushi’a wote kwa ukamilifu wake kwa wasomaji, utafiti ni mpana katika jambo hili na muhtasari huu hauwezi ukaubeba wote.

Na ifuatayo ni baadhi ya orodha ya vitabu tunaiweka mbele ya watafiti kwa anayetaka ziada ya utafiti katika maudhui haya:-

Vitabu vya maulamaa na wasomi wa Kisunni ambao uliwaongoza utafiti wa kielimu na tahakiki kwenye ukweli wa madhehebu ya Ahlul-Baiti (a.s) tumetaja baadhi ya vitabu hivyo katika kurasa zilizotangulia:-

Al- Muraa jaatu - cha Sayyid Sharaf Diyni Al-Amiliy.

Al-Ghadiyr - cha Sheikh Al-Aminiy kina juzuu kumi na moja.

Maalimul-Madrasatain - cha Sayyid Murtadha Al-Askariy.

Al-Imamus-Swadiq (a.s) wal-madhaahibil- aruba'a cha Sheikh Asad Haydar.

Layaaliy bishawaari - Munadharatu wal- hiwar cha Sayyid Muhammad Al- Musawi Shirazi.

Aslu Shi’a wa usuuliha - cha Sheikh Muhammad Husein Kashiful Ghitwaa.

Annasu wal- ijtihaadu - cha Sayyid Sharafu Diyni Al- Amiliy.

Nadhariyatu Al-Khalifataini na Ighitiyali Khalifata Abiy Bakar bisumm" vya Sheikh Najaaha Atwaaiy.

Difau an wahyi as-shariati - cha Sayyid Husein Ar-Rajaa.

Na mwisho wa wito wetu ni kwamba, shukrani zote ni za Mola wa walimwengu na sala na amani zimwendee Muhammad na Ali zake wema watukufu.