read

Mzozo Kati ya Wafuasi wa Madhehebu na Kukufurishana Baadhi Yao Kwa Baadhi

Katika aina ya mzozo baina ya wafuasi wa madhehebu ni kwamba wa Hanbali walikuwa wanachoma moto misikiti ya watu wa Shafi, makhatibu Wakihanafi walikuwa wanawalaani Hanbali na Shafi juu ya mimbari na ilitokea fitina baina ya wa Hanafi na Shafi hata masoko na madrasa zilichomwa moto.1

Yaaqutu Al-Hamuwiy amesema amepokea kutoka kwa Is'bahan: "Uharibifu ulienea katika wakati huu na kabla yake kutokana na wingi wa fitina na ta'asubu baina ya Shafi na Hanafi na vita vilivyoendelea baina ya pande mbili kila kundi liliposhinda lilipora maduka ya kundi jingine, kuchoma moto na kuharibu."

Na amesema kutoka kwa Arayii: "Kulitokea ugomvi baina ya Hanafi na Shafi na vita vikaanza baina yao na ushindi mara zote ulikuwa kwa mashafiy hii ni pamoja na kwamba wao walikuwa ni wachache kwa idadi isipokuwa Mwenyezi Mungu aliwanusuru."2

Mulla Aliyul-qaariy Al-Hanafi amesema: "Imeenea kwa mahanafi kwamba Hanafi akihama kwenda madhehebu ya Shafi anaadhiriwa na ikiwa kinyume anavuliwa toka kwayo tu."3

Amesema Mudhafarul-tuusiy As-Shaafiy: "Kama ningekuwa na mamlaka ningechukuwa jiziya {kodi} kwa Mahanbali."4 Na Abubakari Al-Mughaariy aliwakufurisha Mahanbali wote.5

Wakati ambapo Ibnu Hatim Al-Hanbali amesema: "Ambaye sio Hanbali sio Muislam."6

  • 1. Al-bidayatu wanihayah J: 14, uk 76 Miriiatul-jinan J: 3 uk 343
  • 2. Muujammul - buldan J: 1, uk 209 na J: 3 uk 117
  • 3. Irishadu Naqaad cha As-swanaaaniy, rejea dinul-khalis J:3 uk 355
  • 4. Miriatu-zamaan j: 8 uk 44
  • 5. Shadharaatu dhahab J: 3 Uk: 252
  • 6. Tadhikratul-hufadh J:3 uk 375