read

Shutuma Kuhusu Imamiya

Hakika walioandika kuhusu Shi’a walikwepa ukweli pale waliporejea vitabu vya wapinzani na wakanukuu kutoka kwao bila ya kuhakiki wala kutazama. Amesema Hamidi Daud Hanafiy: "Anakosea sana anayedai kwamba yeye anaweza kudhibiti juu ya itikadi ya Shi’a Imamia, elimu zao, na adabu zao kwa yale yaliyoandikwa na wapinzani kuhusu wao, vyovyote watavyofikia hawa wapinzani katika elimu na utambuzi, na vyovyote watakavyokuwa na uaminifu wa kie- limu katika kunukuu hoja na kuzifafanua kwa njia safi iliyoepuka na ta'asubu ya upofu, nasema haya nikiwa na uhakika wa usahihi wa ninayoyasema…1

Leo hii tunakuta katika maktaba za Ki-Islam vitabu kiasi 5,000 na makala za kushambulia Ahlul-Bait, na kuwakimbiza watu kutoka kwao, wameeneza picha mbaya juu ya Itikadi yao ambapo wameeleza Ushi’a kama wanavyotaka wao, sio kama ulivyo, na kwa kuwa utafiti wetu huu ni hatua tu, katika njia ya kubainisha haki hakuna budi ya kueleza baadhi ya shutuma ili tuziondoe katika kioo safi cha Ki-Islamu.

Shutuma ya Ghuluu (Kusifu Kupita Kiasi)

Wametuhumiwa wafuasi wa Ahlul-Bait (a.s), kwamba wao wamesema kuwa maimamu ni waungu, na yanayofanana na hayo katika ghuluu. Ukweli ni kwamba kauli hizi ni za baadhi ya makundi ya waliovuka mipaka, lakini yamenasibishwa kwa Shi’a kwa kutokujua au kwa kujifanya kutokujua, na Shi’a kwa kuwafuata maimamu wao (a.s) wamekanusha kauli hizi na wanakufurisha wanaosema hivyo na hizi ni baadhi ya kauli za maimamu wa Ahlul-Bait ambazo zimebainisha msimamo wao kwa ghuluu na maghulaat.

Imam Sadiq (a.s) amemwambia Swalehe bin Sahl: "Ewe Swalehe: Hakika sisi ni waja tumeumbwa tu na Mola, tunamwabudu na tusipomwabudu atatuadhibu.2

Amesema Imam Ridha (a.s): "Mwenyezi Mungu awalaani Maghulaati, ee sio wengine ila ni Wayahud, ee walikuwa ni Manaswara, ee walikuwa ni Majusi, ee walikuwa ni Marjiah, ee walikuwa Haruriyah," akasema, "msikae nao, msiwa-amini, epukaneni nao na Mwenyezi Mungu yuko mbali nao."3

Na amesema Sheikh Al-Mufid mmoja wa maulamaa wa kubwa wa Kishi’a: Maghulat ni katika wanaojidhihirisha na Uislamu, wao ndio wanaomnasibisha Amiril-Mu'uminina na kizazi chao kwenye uungu na Utume na wakamsifu kwa fadhila katika dini na dunia hadi wakaruka mpaka wakatoka katika makusudio na wao ni wapotevu na ni makafiri. Amirul-Mu'uminina aliwahukumu wauliwe na kuchomwa kwa moto, na maimamu walishahukumu kuwa wao ni makafiri na kwamba wametoka katika uislamu."4

Na amesema Mustafa Shakah akitetea Shi’a kwamba wao wanajiepusha mbali na kauli zilizokuja katika ndimi za baadhi ya vikundi, na wanavihesabu kuwa ni katika ukafiri na upotevu."5

Amesema Urufan Abdul Hamid: "Hivyo si vinginevyo isipokuwa ni katika njia ya kuchafua na yenye kufedhehesha kuingiza mafunzo ya Maghulaat katika Mustwalaha wa Kishi’a, na kuanzia hapa ulidhihiri ufisadi wa hukumu za kijeuri ambazo wamezisema baadhi juu ya Shi’a na kwa sura inayopingana na ukweli ambapo wamewazulia. Na katika mfano wa haya amesema Jauladi Zahiyr, Faridi Landar, Ahmed Amin na wengine dhidi ya Shi’a."6

Qur'an Tukufu

Wamedai baadhi ya waandishi, kuwa Shi’a wanasema kuwa Qur'an imepotoshwa, tuhuma hii ni batili, wameijibu maulamaa na wamepinga riwaya zilizopokewa kuhusu jambo hili, hata maulamaa wa Kisuni wametetea Shi’a.

Amesema Dkt. Muhammada Abdilah Daraaz "Vyovyote iwavyo, hakika Msahafu ni mmoja uliopo katika ulimwengu wa Ki-Islamu, likiwepo kundi la Shi’a, tangu muda wa karne 13, na hapa tumetaja Rai ya Shi’a Imamiya."7

Na amesema Sheikh Muhammad Ghazali: "nimesikia kwa hawa wanaosema katika mihadhara ya kielimu, kwamba Mashi’a wana Qur'an nyingine inazidi na kupungua hii yetu maarufu, nikamwambia Qur'an hii iko wapi? Na kwa nini binadamu na majini hawajapata nakala kwa muda wote huu mrefu? Uzushi huu ni wa nini? Uongo huu ni wa nini? Dhidi ya watu na wahyi."8

Amesema Sheikh Saduuq aliyefariki 381 H - (mwanachuoni wa Hadith wa Kishi’a): "itikadi yetu katika Qur'an ambayo ameiteremsha Mwenyezi Mungu kwa Mtume wake Muhammad ni ambayo ipo baina ya Jalada mbili nayo ni ile ile iliyopo katika mikono ya watu na wala sio zaidi ya haya na asemaye kwamba tunasema ni zaidi ya hiyo basi ni muongo;"9 na amesema Sheikh Mufiyd aliyefariki 413 H, "ama kuhusu upungufu wamesema jamaa katika Shi’a kwamba haikupungua neno, aya wala sura,….. Ama ziada inakataliwa kwa uharibifu wake."10

Shi’a wana vitabu vinavyopinga kupotoshwa kwa Qur'an na vinampinga kila anayesema hivyo. Al-Kurki maarufu kwa Muhaqiqu-thaniy ameandika makala katika kupinga kupungua baada ya kupatikana Ijmai juu ya kutokuwa na ziada, na ametunga Agha Barazak Atwahraniy kitabu "Anaqidulatwif fiy nafiy Atahariyf anil-Qur'an-Shariyf."

Ametunga mmoja wa Maulamaa wa Ahlus-sunna kitabu ili kuthibitisha kupotoshwa kwa Qur'an akakiita "Al-furqan" na wakampinga maulamaa wa misri katika wakati wake;11 na zinap- atikana katika vitabu vya Ahlus-sunna riwaya nyingi zinazoashiria kupotoshwa kwa Qur'an na hasa katika Sahihi Bukhariy na Muslim.12

Kutoka kwa Aisha amesema kwamba "ilikuwa katika yaliyoteremshwa katika Qur'an Aya hii): (Ashara radhaati maalumaati yuhramna thuma musakhina bikhamisi maalumaati) na Mtume wa Mwenyezi Mungu amefariki nazo ni katika aya zinazosomwa katika Qur'an.13

Kwa ufupi ni kwamba hakika riwaya hizi ama ziwe kwa Shi’a au kwa Sunni ni riwaya za uongo na zinapingwa na Qur'an imehifadhiwa kutokana na kupotoshwa kwa kuhifadhiwa na Mwenyezi Mungu. Amesema Mwenyezi Mungu: "Hakika tumeiteremsha Qur’ani na hakika sisi ni wenye kuihifadhi"14 Hii ndio rai ya Shi’a, ama msahafu wa Fatmah (a.s), hio sio Qur'an nyingine bali humo kuna riwaya ambazo zinafungamana na mustakabala wa umma wa Ki-Islam……..

 • 1. Katika utangulizi wa Hamid Daudi Hanazi katika "Aqaidul-Imamiya cha mudhafar
 • 2. Sharhe Itikaat Saduuq
 • 3. Uyuunu Akhibar Ridhaa cha Saduq
 • 4. Sharhe Itiiqadi Suduuqu
 • 5. Islamu bila madhaahib
 • 6. Dirasaatu fiyl-firaqiwal-aqaidil-slaamiyatu uk 32
 • 7. Madikhalu ilaa-Qur'anil - kariym uk 39 - 40
 • 8. Difau an aqiidati wa shari'ah. na katika waliotetea Shia dhidi ya tuhuma hii ni Sheikh Muhammad Abu Zahra. Sheikh Rahmatullah Al-Hindi, Ust.Muhamad Madani, na Dkt. Mustafa Rafii
 • 9. Risaalatu itiqaadati
 • 10. Awailul-maqaaati -uk. 55
 • 11. Jarida la Risalatu l-islaam toleo la nne makala ya ustadhi Muhammadul- madainiy uk 382-383
 • 12. Rejea sahihi Bukhariy kitabul-hudud babu rajml- habla mina zinaa. Sahihi Muslim babu lau anna liibni Adam wadiyani laibtaghaa thalithan, na kitabu ridhaa J:4 uk 167,musnad Ahmad J:5 uk-132
 • 13. Sahihi Muslim kitabu ridha'a babu tahriym bikhamsi radhaat
 • 14. Suratul- Hijr:9