read

Siasa na Nafasi Yake

Linaweza kujitokeza swali katika akili kama Maimamu wamekataza watu kuwafuata wao kwa nini leo tunaona waislamu wanawafuata? Jawabu ni kwamba siasa ndio sababu, serikali dhalimu zililazimisha madhehebu manne kwa watu, wakalazimishwa kufanya ibada kwa mujibu huo, na zikayapiga vita madhehebu mengine na katika hilo, anasema mwanahistoria Al-Muqaariyzi: "Uliendelea utawala wa Makadhi wanne kuanzia mwaka 566 Hijiria hadi haikubaki Miji ya Ki-Islamu, Madhehebu inayojulikana katika madhehebu ya Ki-Islaamu yasiyokuwa hayo, na maulana wao walitoa fatwa katika Miji kuwa ni wajibu kufuata madhehebu haya na kuharamisha yasiyokuwa hayo, na yameendelea kufuatwa hadi leo. Na Bibiris akatangaza wazi kufungwa kwa mlango wa Ijitihadi na amri yake inaendelea pamoja na kwamba ufalme wake umeshaondoka.”... 1

Abdul-Mutaaliy Aswaydiy amesema: "Hakika mimi naweza kuhukumu hapa kuzuia ijitihadi kumepatikana kwa njia za udhalimu na kwa wasila wa mabavu na kwa kutoa mali na hakuna shaka kwamba njia hizi kama zingetumika kwa yasiyokuwa madhehebu haya manne ambayo tunayafuata leo yangebaki na watu wengi wanaoyafuata, vile vile, na leo yangekuwa yanakubalika kwa anayeyapinga.”2

  • 1. Al-khutwatul Al maqaariziy J: 2 Uk: 333
  • 2. Maydanul- ijitihadu uk: 14