read

Taqiya

Inawezekana kufahamu kimakosa taqiya ndiko ambako kume sababisha baadhi kuwashambulia Shi’a, hakika Shi’a hawakujificha vitabu vyao vya rejea ambavyo humo wamechukua itikadi yao vime-enea, na wao wamevichapisha na kuvisambaza kwa watu wa madhehebu mbalimbali, taqiya sio udanganyifu, hadaa na unafiki kama wanavyoita baadhi lakini nikuficha itikadi katika baadhi ya nyakati kwa kuzuia adha kwa wengine.

Sheikh Mufiyd ameelezea kuwa; "ni kuficha haki na kustiri itikadi humo na kuwaficha wapinzani na kuacha kuidhihrisha, kwa yale yanayoleta madhara katika dini na Dunia. Na hivyo ni faradhi kama akijua kuwa kuna madhara au akipata dhana yenye nguvu, asipojua kuwa kuna madhara kwa kuidhihirisha haki wala hajapata dhana yenye nguvu juu ya hilo, sio wajibu kufanya taqiya."1

Na taqiya ambayo kwayo wametuhumiwa Shi’a imeruhusiwa katika uislam, anasema Mustafa Rafi: Taqiya ni kitendo cha kisheria katika uislam, kama ambavyo iliruhusiwa katika zama zilizotangulia kwa jamii zote, umma na dini, na dalili ya kuruhusiwa kwake ni kauli ya Mwenyezi Mungu: ni "Waumini wasiwafanye makafiri kuwa ni marafiki badala ya waumini na anayefanya hivyo hana chochote kwa Mwenyezi Mungu isipokuwa mkiogopa kwao madhara."2 Hii ina maana kuwa inajuzu kuamiliana nao kwa kufanya taqiya ili kujilinda na adha zao.3

Na amesema Razi katika tafsiri ya Aya "Ila antataquu min hum tuqaatu." Imepokewa kutoka kwa Hasan kwamba anasema: "Taqiya inajuzu kwa waumini hadi siku ya Qiama, na kauli hii ni bora, kwa sababu kuzuia madhara kwa nafsi ni wajibu kadir iwezekanavyo. Masahaba wamefanya taqiya ambayo wanaifanya Shi’a, huyu ni Ammar bin Yaasir (r.a) alidhihirisha kwa ulimi wake ukafiri; hali moyo wake umetulizana kwa Imani, basi ikateremka kauli yake Mwenyezi Mungu "isipokuwa aliyelazimishwa na moyo wake umetulizana kwa imani;"4 na Mtume wa Mwenyezi Mungu akamwambia: "kama watarudia basi rudia kusema hivyo kwani Mwenyezi Mungu ameteremsha kwa ajili yako (Aya ya ) Qur'an na amekuamuru urudie kama watarudi kwako.

Wafuasi wa Ahlul-Bait (a.s) na kwa matokeo ya hali ngumu ambazo zilipita kwao walikuwa wanafanya taqiya kama alivyofanya Ammar (r.a) na sheria hii ambayo imeshuka kwa ajili ya Ammar ni sheria kwa Waislam wote ambapo zingatio ni kwa ujumla wa tamko na sio kwa ajili ya sababu mahsusi.

Mustafa Raafiy amesema katika kutetea Shi’a; "Hakika wale ambao wanawalaumu Shi’a Imamiya kwa kufanya taqiya kwa ajili ya kuhifadhi maisha yao na damu zao, wanawatuhumu kwa tuhuma kali kwa sababu ya kufanya kwao taqiya badala ya kupigana jihadi na kupambana, je, hawa wanaotuhmu hawakutazama nyuma ili waone kwa yakini kwamba taqiya imeruhusiwa na inaendelea tangu kwa Nuhu, Mu'umini wa Al-Firauni, Musa, ambaye alitoka Misri akiwa na hofu akijificha ambapo amesema, "Basi nikakimbia kutoka kwenu nilipowaogopa.."5

Na kwa ndugu yake Haruna aliposema (kaumu imenionea na walikaribia kuniuwa"6 Na kwa Lut aliposema: "Kama ningekuwa na nguvu kwenu au nijifiche katika ngome madhubuti.."7 hadi kwa mwisho wa Mitume, Mtume Muhammad bin Abdillah (s.a.w.w). Je, yeyote atajaribu kuwatuhumu hawa Mitume? Na wengi wao ni katika Ulul-Azmi kwa kukimbilia kwao kwenye udanganyifu na kuacha jihadi kama wapinzani wanavyowatuhumu Shi’a Imamiya? Mimi sidhani kama binadamu mwenye akili, mwadilifu hataona udhuru wao katika kutumia taqiya bali ataona ni wajibu kwao kufanya taqiya badala ya kuwanasibisha kwa sababu yake kwenye udanganyifu, hila na unafiki.8

  • 1. Taswihihul-itiqaad uk:115
  • 2. Suratul Imraan: 23
  • 3. Islaamunaa fiy taufiyq baina sunna wa Shiati uk : 135
  • 4. Suratu Nahl: 106
  • 5. Suratu Shu'araa: 21
  • 6. Suratul - Aaraf: 150
  • 7. Suratu Hud: 80
  • 8. Islaamunaa 133 - 134