read

Tutamfuata (Tutamqalidi) Nani?

Tukiachilia mbali kauli za maimuamu wanne katika kukataza kufuatwa kwao, tukijaalia kuwa kuna dalili, tutamfuata nani? Je, tumfuate Abu Hanifa au Malik au Shafi au Ahmad? Hakika kilicho bora kimekosekana, na kuchagua kilicho bora bila ya kuwepo kilicho bora ni uharibifu kiakili na kisheria, mfano kama tutamfuata Shafi, hii si ina maana kwamba sisi tumeweka kwa wengine alama ya kuuliza? Na tatizo ni kwamba madhehebu ya Ash’ariy ya kifiqihi ni mahala pa Ikhitilafu, watu wa Hanafiy wanasema ilikuwa ni wa kihanafy, Malik wanasema alikuwa ni wa Malik na shafi kadhalika wanasema ni Shaafiy!

Maimamu na Sunna

Hakika anayefuatilia rai za maimamu wanne anakuta kwamba humo kuna ambayo yanakhalifu sunna, mfano wa hilo ni rai yao katika talaka, inafahamika kuwa talaka tatu kwa tamko moja, Mtume ameifanya kuwa ni talaka moja.1 Lakini Maimamu wanne wameihesabu kuwa ni talaka tatu, itajuzu vipi kwa Mwislamu kuacha kilichosihi kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) na kuchukua kinyume chake?

Al-Muhaqqiq Ibnu Daqiqil-iyd amekusanya mas'ala ambayo madhehebu ya kila mmoja miongoni mwa maimamu wanne yamekhalifu Hadith sahihi mmoja mmoja na kwa pamoja katika mujaladi mkubwa2, Al-Albaniy ametaja mas'ala 55 humo maimamu wanne na wanazuoni wamekhalifu sunna sahihi, na Ibnu Hazim amesema juu ya Hadith ambazo wamezikhalifu maimamu na mafaqihi, kama atazifuatilia mfuatiliaji basi idadi yake ingefikia maelfu."3

Amesema Alaithu bin Saad: Nimehesabu kwa Malik bin Anas mas'ala sabini, yote amekhalifu sunna za Mtume na humo amesema kwa rai yake."4

Kutoka Katika Fiqihi ya Maimamu Wanne

Amesema Abu Hanifa: "Kama mwanaume atakuwa Misri akampa uwakala mtu mwingine aliyeko Andalusi kwamba amuolee mke basi akamuolea, na wala wasikutane aslani katika wanayo yaona watu, kisha mwanamke apate mtoto, nasaba yake itakuwa ni ya mwanamme ambaye yuko Misri."5

Dabusi Al-Hanafiy amesema: "Mtu akimkodisha mwanamke ili azini naye na wala si kwa ajili ya kuwa mtumishi, na akazini naye basi hakuna adhabu juu yake, kwa Abu Hanifa.

Mtu akimuoa mahrimu yake akamwingilia naye anajua au kwa kutojua hakuna adhabu juu yake, kwa sababu sura ya kuhalalisha imesha patikana nayo ni nikahu (ndoa) hata kama hakuruhusiwa, hiyo ni kauli ya Abu Hanifa….6
Malik - kama mtu atanuia kumtaliki (katika Fiqhi) mke na wala asitamke basi atakuwa ameachika.

Zamakhishariy mfasiri maarufu amesema: Wakiuliza madhehebu yangu siyasemi, nayaficha; kuyaficha kwake ni usalama kwangu, wakisema ni Hanafi, nitasema kwamba wanasema mimi nahalalisha pombe nacho ni kinywaji kilichoharamishwa, wakisema ni Malik nitasema wanasema, mimi nahahalisha kula mbwa na wadudu, wakisema ni Shafi nitasema kwamba wanasema mimi nahalalisha kuoa binti * na binti ni haramu, wakisema basi ni Hanbali nitasema, wanasema kwamba mimi ni mzito wa kutatua nachukiza ninasema kuwa Mwenyezi Mungu ana viungo."7

Katika Itikadi ya Ash’ariah

Annawawiy amesema: "Na madhehebu ya Sunni halikadhalika ni kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu sio wajibu kwake kitu chochote, ametukuka Mwenyezi Mungu bali ulimwengu wote ni miliki yake dunia na akhera viko katika mamlaka yake anafanya kwavyo atakalo, kama atawaadhibu wanaotii na wema wote na akawaingiza motoni basi itakuwa ni uadilifu kutoka kwake, na kama atawaneemesha makafiri na akawaingiza peponi basi ni juu yake hilo."8

Hakika itikadi hii ya Ash’ariah haina dalili bali dalili ziko dhidi yake wao kwa kujengea kanuni yao - sio wajibu kwa Mwenyezi Mungu kitu chochote - wamesema kujuzu kwa Mwenyezi Mungu kuwaingiza watiifu motoni na makafiri kuwaingiza peponi, lakini kanuni hii ni mbovu kwani Mwenyezi Mungu ameshawajibisha katika nafsi yake vitu kati ya hivyo ni rehema.

Amesema Mwenyezi Mungu: "Mola wenu amefaradhisha rehema katika nafsi yake."9 Na waliyoyasema kwamba ulimwengu ni miliki ya Mwenyezi Mungu na Dunia na Akhera viko katika mamlaka yake amefanya kwavyo anayotaka ni sahihi, lakini mambo hayafikii awaadhibu vipenzi vyake kwani Mwenyezi Mungu ameahidi pepo zinazotiririka chini yake mito katika Aya nyingi.

"Hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ni ya kweli."10

"Hakika ahadi yake ni yenye kutekelezwa."11

Je, ni kitendo cha Mwenyezi Mungu Mtukufu?

Kadhi Al-iyji amesema katika "Al-Mawaaqifu" katika maqsadu ya saba: Taklifu kwa yasiyowezekana inajuzu kwetu.12

Hii ni itikadi nyingine inayopingana na Qur'an. Amesema Mwenyezi Mungu: "Mwenyezi Mungu haikalfishi nafsi isipokuwa inachokiweza,"13 "Mwenyezi Mungu haikalfishi nafsi isipokuwa kwa kile alichokipa."14

 • 1. Sahihi Muslim, kitabu Twalaaq babu twalaaq thalaath (mlango wa talaka 3)
 • 2. Rejea "Swifatuswalati Nabiyi" cha Al-Albaniy uk. 37
 • 3. Al-Hadith hujatu binafsihi fiy aqaidi wal-ahkaaami cha Al-Albaniy uk. 58
 • 4. Jamiu bayanil ilimi wafadhilihi J: 2 uk 1080
 • 5. Al-ahawalus-shakhisiyat cha Muhyidiyni Abdul-Hamid bahath ya nasaba na rejea kitabu cha Hanafi
 • 6. Taasisu Nadhar uk:148-149 Al-qabaaring Adimishiqiy na tazama:Badaius-swanain cha kasaaniy Al-hanafiy J:4 uk:35
  *Ana kusudia kwamba shaafiy anahalalisha mtu kumuoa binti yake wa zinaa
 • 7. Tarjama ya Zamakhishariy J: 4 katika tafsiri yake ya kashafu uk. 310
 • 8. Sahihi Muslim, sharah ya Nawawiy J: 17 uk 160
 • 9. Suratu Al-An-aam: 54
 • 10. Surat Luquman: 33
 • 11. Surat Mariyam:61
 • 12. Al-Mawaaqifu uk 330
 • 13. Surat Baqarah: 186
 • 14. Surat Twalaq: 7