read

Utangulizi wa Chapa ya Kwanza

Shukrani zote ni za Mwenyezi Mungu ambaye aliwatuma Mitume wake kwa ubainifu na akateremsha pamoja nao vitabu na mizani hali ya kuwa ni rehema na uongofu kwa watu. Rehema za Mwenyezi Mungu zimshukie mteule Muhammad na Ahali zake waongofu rehema ya daima isiyo na mipaka, idadi wala kikomo.

Baada ya kuchapishwa kitabu chetu "Warakibtus-Safina'' watu walikipokea kwa mapokezi mazuri na wakakisifu kwa sifa nzuri, na wakushukuriwa ni Mwenyezi Mungu, baadhi yao wakanishauri kukifupisha kitabu, fikra hii inaweza ikawa sawa, kwani kitabu hicho kinazidi kurasa mia sita na sio kila mtu anaweza kukisoma au kukinunua, kwa sababu hii ndipo nikakifupisha.

Ama kitabu cha asili kinazungumzia kisa cha kuhama kwangu kutoka madhehebu kwenda madhehebu mengine, kwa ajili ya kuutafuta uislamu sahihi nalo ni jaribio la kufikia katika mfumo wa Mwenyezi Mungu ambao umefafanua uislamu kupitia njia tatu za kifikra zilizopo na ambazo zinaonekana katika medani nazo ni:-

1-Kufuata maimamu wanne wa Kiash'ariy

2-Kufuata Salafu (Salafia)

3- Kufuata Ahlul - bait (Shi'atul- imamiyah)

Na kwa kuwa utafiti huu ni muhtasari, nimelazimika kuutoa katika njia mbili ya kwanza na ya tatu, na anayetaka kusoma nadharia ya salafia ni juu yake kurejea katika kitabu chetu (Warakibtus - Safina).

Namuomba Mwenyezi Mungu anipe taufiq ya kuandika kitabu maalum juu ya salafia katika wakati mfupi ujao, na awanufaishe waislamu na utafiti huu, hakika yeye ni mbora wa kuon- goza na mbora wa kunusuru.