read

Utangulizi wa Chapa ya Pili

Shukrani zote ni za Mola wa viumbe, amani na rehema za Mwenyezi Mungu zimshukie Muhammad na Ahali zake wema watoharifu.

Giza halijaacha kueneza nguvu zake za upofu ili kuzuia mwanga wa nuru tukufu ya Mwenyezi Mungu, na linajaribu kuziba kila njia wanayoifikiria wapenzi watukufu katika kuingia humo, lakini jua linatoa mwanga wake juu ya ardhi bila ya kujali mkusanyiko wa mawingu yenye giza nene, ambayo yameafikiana kuzuia nuru yake.

Hakika haki haiachi kutoa wito wake, na wengi wameshaikubali na imewafungulia milango yake ili wapate humo uongofu na maana bora ya maisha, na mchango wetu katika kuondoa vizuizi ambavyo vinafunika mbingu. Tumeona ni bora kuchapisha kitabu chetu "Warakibtus-Safina'' ambacho kimechapishwa kwa jina la ''Nahawul-Islaamis-Sahihi'' na tumeshakirejea kwa masahihisho ya maudhui yake kwa namna ambayo tunataraji itamridhisha msomaji mtukufu.

Mar'wan Khaliyfat Iribad - Jordan