read

Utaratibu Wetu Katika Utafiti

Utaratibu wetu katika utafiti huu ni kulitaka kila kundi lilete hoja yake kutoka katika kitabu na Sunna juu ya usahihi wa madai yake kwa sababu ni wajibu kwa hao watu kuuchukua Uislam wao kwao, utarat- ibu wetu ni Qur'an, anasema Mwenyezi Mungu: "Sema leteni dalili zenu kama nyinyi ni wa kweli”1 na “ambaye mizani ya amali zake njema itakuwa nzito, Basi atakuwa na maisha mazuri."2

Kwa kuongezea haya tutataja matatizo muhimu katika misingi ya makundi haya mawili kama yatapatikana: "Wabashirie waja wangu ambao wanasikiliza kauli kisha wanafuata iliyo nzuri zaidi; hao ndio ambao wameongozwa na Mwenyezi Mungu na hao ndio wenye akili."3

  • 1. Suratu Tawba: 199
  • 2. Surat ul Qaari'ah: 7
  • 3. Surat Zumar 17 na 18