read

Mkutano Wa Kumi, Jumamosi Usiku 3 Sha’ban 1345 A.H

Uchambuzi Wa Elimu Ya Umar Juu Ya Sheria Za Kiislam.

Nawab: Asubuhi hii kijana wangu, Abdu’l-Aziz, ambaye ni mwanafunzi katika chuo cha Islamiyya, ametueleza kuwa mwalimu wao ameliambia darasa kuwa Khalifa Umar ibn Khattab alikuwa ndio mwanasheria mkuu wa wakati wake mjini Madina.

Alikuwa na ujuzi kamili wa aya za Qur’ani na maana zake. Alikuwa mbora zaidi ya wanasheria wote mashahuri kama Ali bin Abi Talib. Abdullah bin Mas’ud , Abdullah bin Abbas, Akrama na Zaid bin Thabit.

Hata Ali Bin Abi Talib ambaye ujuzi wake wa Fiqh, alipokabiliana na suala gumu ulikuwa mkubwa, alimtaka ushauri Umar kuhusiana na haki za Waislam. Khalifa kila mara aliyatatua matatizo magumu ya Ali. Sisi sote tunalikubali hili kwa sababu wanachuoni wetu wanasema kwamba Umar alishika nafasi kubwa isiyo kifani katika elimu na ujuzi. Ninakuomba uielezee nukta hii ili sisi sote, pamoja na mwanangu huyo, tuweze kuuelewa ukweli.

Muombezi: Ni ajabu kwamba huyo Mwalimu amesema hivyo. Hata wanachuoni wenu hawajathubutu kudai hivyo kamwe. Kama baadhi ya watu mashabiki kama Ibn Nazm Zahiri alisema hivyo, walipingwa vikali na wanachuoni wenu. Aidha sifa hii haikudaiwa na Khalifa Umar mwenyewe. Hakuna mwanachuoni hata moja wa kwenu aliyeandika jambo hili katika vitabu vyao.

Wapokezi au wanahistoria ambao wameandika chochote juu ya maisha ya Khalifa Umar Bin Khattab wamedokeza juu ya tabia yake ya ujanja, ugumu wa moyo wake na hila zake za kisiasa lakini hawakujishughulisha sana juu ya elimu yake.

Elimu Ya Umar Juu Ya Sheria Za Kiislamu Ilikuwa Dhaifu

Kwa hakika, vitabu vya madhehebu zote vimejaa mifano ambayo inaonyesha wazi kwam- ba Umar hakuwa mjuzi sana katika masuala ya elimu na fiqh. Kila alipokabiliwa na mambo kama hayo alikuwa akitaka ushauri kwa Amiru’l-Mu’minin Ali, Abdullah bin Mas’ud na Mafaqihi wengine wa Madina.

Ibn Abi’l-Hadid anataja jina la Abdullah Bin Mas’ud hasa, miongoni mwa mafaqihi wa Madina, na anasema kwamba Umar alisisitiza kwamba Abdullah wakati wote abaki naye ili kwamba wakati wowote hali ikijitokeza, ataweza kutakiwa ushauri juu ya mambo ya fiqh.

Sheikh: (Kwa hasira). Ni wapi imeandikwa kwamba Umar hakuwa mjuzi wa masuala ya dini na elimu ya fiqh?

Muombezi: Sikusema kwamba Khalifa Umar alikuwa hana ujuzi kabisa. Nilisema kwam- ba hakuwa mjuzi sana katika masuala ya fiqh na elimu. Ninaweza kuthibitisha haya ninayosema.

Sheikh: Utathibitisha vipi kwamba Khalifa Umar alikuwa na elimu dhaifu katika mambo yanayohusiana na fiqh na sheria za kidini?

Muombezi: Kuna hadithi nyingi sana katika vitabu vyenu vya Sahih. Mbali na hili, kuna kukiri kwa Umar mwenyewe ambako amekufanya mara nyingi.

Mwanamke Amnyamazisha Umar Katika Jambo La Sheria.

Jalalud-Din Suyuti kaitka Tafsir Durru’l-Mansur” Juzuu ya 11 uk. 133; Ibn Kathir katika Sherehe yake Juz. 1 uk. 468; Jarullah Zamakhshari katika Tafsir Kashshaf Juz. 1, uk. 357, Fadhil Nishapuri katika Tafsir-Gharibu’l-Qur’an Juz. 1, kuhusiana na Sura ya Nisa (Mwanamke) ya Qur’ani Tukufu, Qartabi katika Tafsir yake Juz. 5, uk. 99. Ibn Maja Qazwini katika Sunan yake Juz. 1, Asadi katika Hashiyya–e-Sunnan Juz. 1, uk. 583; Baihaqi katika Sunan Juz, 7, uk. 233, Qastalani katika Irshadus-Sari-Sharh-e-Sahih Bukhari Juz. 8, uk 57; Muttaqi Hindi katika Kanzu‘l-Ummal Juz. 8 uk. 298; Hakim Nishapuri katika Mustadrak Juz. 11, uk. 177; Abu Bakr Baglani katika Tamhid yake uk. 199; Ajluni katika Kashful-Khufa’ Juz. 1, uk. 270; Qadhi Shukani katika Futuhu‘l-Qadir Juz. 1, uk 407; Dhahabi katika Takhlis-e-Mustadrak, Ibn Abi’l-Hadid katika Sharh-e- Nahjul-Balagha Juz. 1 uk. 61, na Juz. 7, uk. 96; Hamid katika Jam’-e-Bainus-Sahihain, Faqih Wasiti Ibn Maghazili Shafi’i katika Manqib yake; Ibn Athir katika Nihaya yake, na wengineo.

Kwa usahihi wamesimulia, pamoja na tofauti kidogo ya maneno kwamba siku moja Khalifa Umar, akiwa katika kuwahutubia watu alisema: “Ikiwa yeyote ataoa na akaweka kiwango cha Mahari cha zaidi ya dirham 400 kwa mkewe, nitamtwisha ile adhabu iliyoamriwa juu yake na nitakihifadhi kile kiasi kilichozidi kwenye Baitul-Mal (Hazina ya Umma)”

Mwanamke mmoja katika ile hadhara akasema kwa Sauti kubwa: “Umar! Hicho una- chokisema ndio chenye kukubalika zaidi au sheria ya Allah? Je, Allah Mwenye Nguvu hasemi: “Na ikiwa unataka kuwa na mke (mmoja) badala ya mwingine na umempa mmoja wao rundo la dhahabu, basi usichukue chochote kutokana nayo.” (4:20)

Alikwisha kuisikia aya hii na yale majibu makali ya mwanamke huyo, Umar akasema:‘Wewe unayo elimu nzuri ya fiqh na matatizo kuliko Umar, nyote nyie pamoja na hata wale wanamke wanaotawa waliokaa majumbani mwao.’”

Halafu Umar akapanda tena juu ya mimbari na akasema: “Ingawa nimewakatazeni kutoa zaidi ya dirham 400 kama mahari kwa wake zenu, sasa ninawaruhusuni kutoa kiasi chochote mnachotaka zaidi ya kiwango kilichowekwa. Hakuna ubaya ndani yake.”

Hadithi hii inaonyesha kwamba khalifa Umar hakuwa na ujuzi sana juu ya Qur’ani na fiqh. Vinginevyo asingeweza kusema jambo lisilo sahihi waziwazi namna hiyo kiasi kwamba akaweza kunyamazishwa na mwanamke asiyekuwa na elimu.

Sheikh: Hapana sivyo hivyo, ukweli ni kwamba Khalifa alitaka kuwalazimisha watu kupunguza kiwango cha mahari kulingana na Sunna. Ingawa Uislam unaruhusu tutoe kiasi kikubwa, ni vyema tukajieupusha na hilo ili masikini wasiumie. Ilikuwa ni kwa sababu hii kwamba alisema kiasi cha mahali kisiwe kinazidi kile kiasi kilichowekwa kwa wakeze Mtukufu Mtume.

Kunyang’anya Kiasi Chochote Cha Mahari Ni Kinyume Cha Sheria

Muombezi: Hii ni namna ya kisingizio kisicho na maana ambacho hata Umar hakuwa na habari nacho. Vinginevyo angeweza kukubali kosa lake mwenyewe na asingelisema. “Ninyi ni mafakihi wazuri kuliko Umar, nyote nyie, ukijumuisha na wake wa nyumbani.” Vinginevyo pia angeliweza kusema haya unayoyasema sasa.

Mbali na hili, kila mtu anajua kwamba kitendo kilicho kinyume cha sheria hakiwezi kufumbiwa macho kama njia ya kupata matokeo mazuri na ya kisheria. Ni dhahiri ile mali ya mwanamke, ambayo ameimiliki kulingana na kanuni za Qur’ani haingeweza kwa sheria kuporwa kutoka kwake na kuwekwa kwenye Baitu’l-Mal.

Mbali na mazingatio yote hayo, si sheria kutoa adhabu igusayo kimwili kwa mtu ambaye hajatenda kosa. Angalau sijawahi kuona uamuzi wowote kama huo ukifanywa kulingana na kifungu chochote cha Sheria. Naomba unifahamishe kama unaweza kueleza mfano kama huo. Ikiwa hakuna kanuni yoyote katika hukumu za sheria, basi itakubidi ukubali kwamba hilo dai la Mwalimu huyo lilikuwa la uongo.

Umar Kukataa Kifo Cha Mtume Kunathibitisha Kwamba Alikuwa Hazijui Baadhi Ya Aya Za Qur’ani

Kwa bahati mbaya, Umar alikuwa amejenga tabia ya kuwa na hasira, na ili kuwatishia wengine alisema: “Nitakuadhibuni!”

Imam Ahmad bin Hanbal katika Musnad yake; Hamidi katika “Jam’-e-Bainus- Sahihain; Tabari katika Ta’rikh yake, na wanachuoni wengine wamesimulia kwamba alipokufa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), Umar alimwendea Abu Bakr na kumuambia kwamba alikuwa na wasiwasi kwamba kuna uwezekano kwamba Muhammad hakufa.

Huenda amejifanya tu kuwa kafa ili aweze kuwatambua marafiki na maadui zake, au pengine ametoweka kama Musa na atarudi tena kuwaadhibu wale waliokuwa sio waaminifu na watiifu kwake.

Umar aliendelea kusema: “Hivyo kama mtu yeyote atasema kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amekufa, nitamuadhibu.” Abu Bakr alipoyasikia haya akawa naye pia hana uhakika nayo, na watu pia wakachanganyikiwa na tofauti zikazuka miongoni mwao. Wakati Ali alipolifahamu hili, alitokeza mbele ya lile kundi la watu na kusema.

“Enyi watu! kwa nini mnafanya tafarani za kijinga hivyo? Mmeisahau ile Aya tukufu, ndani yake ambamo Allah amemuambia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) “Hakika wewe utakufa, na pia watu wa Umma wako.” (39:30)

Kwa hiyo, kulingana na aya hii Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ameiaga dunia hii.” Hoja hii ya Ali iliwaridhisha watu na wakaamini kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa amekwishafariki kweli. Ndipo Umar akasema: “Ilikuwa ni kana kwamba nilikuwa sijawahi kuisikia aya hii.”

Ibn Athir katika Kamil na Nihaya yake, Zamakashari katika Asasu’l-Balagha, Shahrastani katika Milal wa’n-Nihal (Mugaddama IV) na wengineo wengi wa wanachuoni wenu wameandika kwamba Umar alikuwa akikemea: “Mtukfu Mtume hajafa,” wakati Abu Bakr alipomfikia na kusema: “Je Allah Mwenye Nguvu hasemi: ‘Hakika utakufa na vile vile na watu wa Umma wako.”

Pia anasema ikiwa basi atakufa au kuuawa, mtageuka nyuma juu ya visigino vyenu. (3:144) Umar kisha akawa kimya na akasema: “ Ilikuwa ni kama kwamba sijawahi kuisikia aya hii. Sasa ninaamini kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amekufa.

Amri Ya Umar Ya Kuwapiga Mawe Watu Watano Na Kukatizwa Na Ali

Hamidi anasimulia katika “Jam’-e-Bainus-Sahihain” yake kwamba katika wakati wa Ukhalifa wa Umar, watu watano walikamatwa kwa kosa la uzinzi na kufikishwa kwa Umar. Ilithibitika kwamba watu watano hao wamefanya zinaa na mwanamke fulani.

Umar mara moja akaamuru wapigwe mawe mpaka wafe. Wakati huo Ali akaingia mle Msikitini na baada ya kuwa amesikia kile Umar alichoamuru akamuambia: “Hapa amri yako ni kinyume na sheria ya Allah.”

Umar akasema: “Ali! Zinaa imethibitika. Kifo kwa kupigwa mawe ndio adhabu iliyoag- izwa kwa dhambi hii.”

Ali akasema: “Katika suala la uzinzi, kuna hukumu tofauti katika hali tofauti, kwa hiyo katika kesi hizi zilizopo, hukumu tofauti ni lazima zitolewe.

Umar akamuomba afafanue ni hukumu gani za Allah na Mtume wake juu ya kesi hizo, kwani Umar alimsikia Mtume akisema katika nyakati tofauti: “Ali ndiye mtu mwenye elimu zaidi na hakimu bora.

Ali akaagiza wale watu watano waletwe mbele yake. Aliamuru yule mtu wa kwanza akatwe shingo. Akamuru yule wa pili apigwe mawe mpaka afe. Akaamuru yule wa tatu apigwe viboko 100.

Mtu wa nne alipigwa viboko 50. Na mtu wa tano alipata viboko 25. Umar akiwa ameshangaa na kuduwaa, akasema: “Abu’l-Hasan, vipi umeamua kesi hizi katika njia tano tofauti.”

Mtukufu Imam akasema: “Yule mtu wa kwanza alikuwa ni kafir chini ya ulinzi wa Kiislam. Amefanya zinaa na mwanamke Muislam. Kwa vile amepoteza ulinzi wa Uislam alipaswa kuuliwa.

Yule wa pili alikuwa na mke, kwa hiyo amepigwa mawe mpaka kufa. Yule mtu wa tatu alikuwa hajaoa, hivyo, amehukumiwa kupewa viboko 100. Yule mtu wa nne alikuwa mtumwa ambae anastahili adhabu nusu ya yule mtu huru, ambayo ni viboko

50. Na yule mtu wa tano alikuwa ni mwenda wazimu, hivyo alifanyiwa Ta’ziir - alipewa adhabu hafifu, ambayo ni viboko 25 (kama kumuadabisha)

Kisha Umar akasema: “Kama Ali asingekuwapo, Umar angeangamia: Ewe Abu’l-Hasan! Natumai sitakuwepo hai wakati wewe ukiwa huko miongoni mwetu.”

Umar Kuamrisha Mwanamke Mwenye Mimba Kupigwa Mawe Mpaka Afe Na

Ali Kuingilia Kati

Muhammad Bin Yusuf Ganji Shafi’i katika Kifayatut-Talib Fi Manaqib-e-Amiru’l-Mu’minin Ali Bin Abi Talib; Imam Ahmad Ibn Hanbal katika Musnad; Bukhari katika Sahih yake; Hamid katika Jam’e-Bainus-Sahihain; Sheikh Sulaiman Balkhi katika Yanabiu’l-Mawadda, sura ya 4, uk. 75, kutoka Manaqib ya Khawarizmi; Imam Fakhru’d- din Razi katika Arba’in, uk. 466; Muhibu’d-din Tabari katika Riyazu’n-Nazara, Jz. 2, uk. 196; Khatib Khawarizmi katika Manaqib, uk. 48; Muhammad Bin Talha Shafi’i katika Matalibus-Su’ul, uk. 113; na Imam’l-Haram katika Dhakha’iru’l-Uqba, uk. 80, anankuu riwaya ifuatayo:

Mwanamke mjamzito aliletwa mbele ya Umar Bin Khattab. Katika kuhojiwa alikiri kwamba alikuwa na hatia ya kufanya zinaa, na hivyo Khalifa akaamuru apigwe mawe. Kisha Ali akasema: “Amri yako inatekelezeka kwa mwanamke huyu, lakini huna mamlaka juu ya mtoto wake.”

Umar akamuachia yule mwanamke na akasema: “Wanawake hawana uwezo wa kuzaa mtu kama Ali. Kama Ali asingekuwa hapa, Umar angeangamia.”

Aliendelea kusema: “Allah asiniache niishi kiasi cha kukabiliana na tatizo ambapo Ali hayupo ili alitatue.”

Umar Atoa Amri Mwanamke Punguani Apigwe Mawe - Na Ali Kuingilia Kati

Imam Ahmad bin Hanbal katika Musnad yake, Imam’l-Haram Ahmad Bin Abdullah Shafi’i katika Dhakha ‘iru’l-Mawadda sura ya 2, uk. 75, kutoka kwa Hasan Basri, Ibn Hajar katika Fat’hul-Bari Juz. 12, uk 101; Abu Dawud katika Sunan yake Juz. 2, uk. 227; Munadi katika Faizu‘l-Qadir Juz. 4 uk 257; Hakim Nishapuri katika Mustadrak Juz. 2, uk. 59, Qastalani katika Irshadus-Sari Juz. 10, uk. 9; Baihaqi katika Sunan Juz. 8, uk. 164 Mahibu‘d-Din Tabari katika Riyazu’n-Nazar juz. 2, uk. 196; Khatib Khawarizmi katika Munaqab uk. 48; Muhammad Ibn Talha Shafi’i katika Matalibus-Su’ul; Imam’I-Haram katika Dhakha’irul-Uqba uk. 80; Ibn Maja katika Sunan Juz. 2, uk. 227; Bakhari katika Sahih yake mlango wa la yarjumu’l-Majnun wal-Majnuna, na wengi wa Ulamaa wenu wamesimulia tukio lifuatalo:-

Siku moja mwanamke punguani aliletwa mbele ya Khalifa Umar Bin Khattab. Alikuwa amefanya zinaa na akakubali kosa lake. Umar akaamuru apigwe mawe. Amirul-Muminin alikuwapo pale. Akamuambia Umar: “Unafanya nini wewe? Nimesikia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akisema watu wa aina tatu wako huru kutokana na mkono wa sheria: Mtu aliye- lala mpaka atakapoamka, mwendawazimu mpaka atakapopona na akapata fahamu tena, na mtoto mpaka atakapopata umri.” Kusikia hili, Umar akamuachia huru yule mwanamke.

Ibnu’s-Saman katika Kitabu’l-Muwafiqa ameandika habari nyingi kama hizi. Kuna baadhi ya maelezo ambayo yanasimulia hukumu za Umar takriban 100 za kimakosa na uongo.

Elimu Na Sifa Za Ali

Nuru’d-Din Bin Sabbagh Malaki katika Fusulu‘l-Mahimma Sura ya 3, uk. 17 akiandika kuhusu Ali amesema: “Sura hii ina mambo yanayohusiana na elimu ya Ali. Mojawapo ya vipengele hivyo ni ile elimu ya fiqh (Sha’ria) ambayo juu yake yamesimama matendo ya halali na ya haramu ya mwanadamu.

Ali alielewa undani wa Sheria. Mas’ala yake magumu, yalikuwa ni mepesi kwake na alizielewa tafsiri zake kwa ukamilifu.

Ilikuwa ni kwa sababu hii kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema kuwa Ali ndiye mtu anayefaa zaidi wa Umma huu kwa kufafanua maswali ya sheria. Imam Abu Muhammad Husein ibn Mas’ud Baghawi katika Masabih yake anasimulia kutoka kwa Anas kwamba wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipowateua kila mmoja wa sahaba zake kwenye nafasi maalum, alimteua Ali kwenye cheo cha Hakimu na kusema: “Ali ni Hakimu bora miongoni mwenu wote nyie (masahaba na Umma).

Kwa kweli unapolinganisha maneno ya huyu Mwalimu wa chuo asiyefahamu na Hadithi za wanachuoni wenu wakubwa, utathibitisha kwamba dai lake halina msingi. Mwalimu huyu anadai zaidi ya alivyodai kiongozi wake.

Umar mwenyewe alikuwa daima akionye- sha udhaifu wake dhidi ya Ali. Imam Ahmad Bin Hanbali katika Musnad yake, Imam‘l-Haram Ahmad Makki Shafi’i katika Dhakha’irul-Uqba, Sheikh Sulayman Balkhi Hanafi katika Yanabiu’l-Mawadda Sura ya 56, na Muhibu’d-Din, Tabari katika Riyadhu’n- Nazara, Juz. ya 2, uk. 195, wanamnukuu Mu’awiya akisema: “Kila mara Umar Bin Khattab alipokabiliwa na tatizo gumu, alitafuta msaada wa Ali.”

Abu’l-Hajaj Balawi kati- ka Alif-Ba yake Juz. 1, uk. 222 anaandika kwamba wakati Mu’awiya aliposikia habari za kuuawa Shahidi kwa Ali, alisema “Kwa kifo cha Ali, Fiqh na Elimu vimeanguka.” Vile vile ananukuu Sa’id Bin Masayyab akisema kwamba Mu’awiya alisema: “Umar daima alitafuta kimbilio kwa matatizo ambayo Ali hakuwepo kumsaidia.”

Abu Abdullah Muhammad Bin Ali al-Hakim al-Tirmidhi katika sherhe yake ya Risalat-e- Fathu’l-Mubin anaandika: “Masahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) walimtaka ushauri Ali katika mambo yanayohusiana na hukumu za Qur’ani Tukufu na kukubali fatwa zake.

Umar Bin Khattab amesema katika nyakati tofauti kwamba: “ Kama Ali asingelikuwako, Umar angeangamia.”
Mtukufu Mtume wa Allah (s.a.w.w.) pia amesema: “Mtu mwenye elimu ya juu zaidi miongoni wa Umma wangu ni Ali Bin Abi Talib.”

Yaliyosimuliwa kwenye vitabu vya Hadithi na Historia yanathibitisha kwamba Umar alikuwa amekosa sana elimu ya kawaida na ya fiqh kiasi kwamba alikosea hata kulingana na matatizo ya kawaida. Masahaba ambao walikuwa wa rika lake walimuonya kutokana na udhaifu wake.

Sheikh: Wewe huna huruma kwa kumsingizia Umar mambo kama hayo. Inawezekana kwa Khalifa kukosea katika masuala ya dini?

Muombezi: Ukali huu hautoki upande wangu. Maulamaa wenu wameonyesha ukweli kuhusu jambo hili.

Sheikh: Kama ukiweza tafadhali tujulishe mambo haya kwa vyanzo sahihi ili ukweli uweze kudhihirika wazi.

Muombezi: Kuna mifano mingi ya namna hiyo. Takriban 100 kati ya hiyo imo kwenye vitabu vyenu, lakini nitatoa mmoja kati ya hiyo kama mfano:-

Muslim Bin Hajjaj katika Sahih yake, sura aya Tayamamu; Hamidi katika Jam-e-Bainus –Sahihain, Imam Ahmad Hanbali katika Musnad yake Juz. 4, uk 265, 319, Baihaqi katika Sunan Juz. 1, uk. 209, Abu Dawud katika Sunan Juz. 1, uk 53, Ibn Maja katika Sunan Juz. 1 uk. 200, Imam Nisa’i katika Sunan yake Juz. 1,
uk 59-61, na wengine wa Ulamaa wenu wakubwa kwa njia tofauti na maneno tofauti, wameandika kwamba wakati wa Ukhalifa wa Umar, mtu mmoja alimjia na kusema: Imekuwa ni lazima kwangu nifanye ghusl (josho la tohara) lakini hakuna maji yanayoweza kupatikana. Nitafanya nini katika hali kama hii. Umar akasema: “Mpaka upate maji ya kufanyia josho, vinginevyo usisali.”

Kwa wakati huo Ammar-e-Yasir, Sahaba wa Mtume, alikuwepo. Yeye akasema: “Ewe Umar! Umesahau kwamba katika moja ya safari ambazo wewe na mimi tulitokea kuwa tunahitaji kufanya josho.

Kwa vile maji hayakupatikana wewe hukusali, lakini nilifikiria njia ya tayammum badala ya josho ni kwamba ni budi vumbi lipakwe juu ya mwili wangu wote. Hivyo nilipaka vumbi katika mwili wangu na nikatekeleza Sala.

Tulipokwenda kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), alisema, huku akitabasamu: “Kwa tayammum kiasi hiki kinatosha kwamba viganja vya mikono yote vinaguswa kwenye udongo kwa pamoja na viganja hivyo vifutwe kwenye paji la uso, kisha nyuma ya mkono wa kulia kufutwe na kiganja cha kushoto na kisha nyuma ya mkono wa kushoto ufutwe na kiganja cha kulia.” Sasa kwa nini unamwambia huyu mtu asitekeleze Sala?

Umar aliposhindwa kutoa jibu alisema: “Ammar muogope Allah.” Kisha Ammar akasema, “Unaniruhusu nisimulie hadithi hii? Umar akasema: “Nakuachia ufanye unavyopenda.

Kwa kuzingatia hadithi hii sahihi ambayo Ulamaa wenu wenyewe wameisimulia, utakiri kwa kweli kwamba dai la Mwalimu huyo lilikuwa la uongo mtupu.

Anaweza mtu mwenye elimu nzuri ya fiqh na ambaye amekuwa mara kwa mara pamoja na Mtume na amesikia kutoka kwa Mtume jinsi tayammum inavyopaswa kufanyika wakati maji hayakupatikana, kuja kumuambia Muislam kwamba kama hatapata maji ajiepushe na kuswali Sala zake? Hii ni ajabu hasa kwa vile Qur’ani Tukufu inatuambia sisi kwamba katika hali kama hiyo tunapashwa kufanya tayammum.

Kitendo cha tayammum miongoni mwa Waislam ni maarufu sana kwamba hata Muislam asiye na elimu anajua kwamba, chini ya masharti maalum inachukua nafasi ya kanuni za udhuu na taratibu za josho. Sasa tutasemaje kuhusu Sahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na Khalifa? Je, hapashwi kulijua jambo hili? Katika suala hili mimi sio ninadai kwamba Khalifa Umar aliibadili sheria ya Allah kwa makusudi.

Lakini hili kwa hakika linawezekana: alikuwa dhaifu katika uwezo wake wa kuhifadhi habari na ilikuwa ni vigu- mu kwake kukumbuka Sheria. Na hii ndio ilikuwa sababu, kama Ulamaa wenu walivyoandika, alizoea kumwambia Faqih hodari, Abdullah Ibn Ma’sud: “Unapashwa daima kuwa nami ili kwamba wakati wowote mtu akiniuliza swali, utaweza kumjibu.”
Sasa, enyi waungwana! Mnapashwa kuamua ni tofauti gani iliyopo kati ya mtu ambaye elimu yake ni haba hivyo kwamba hawezi kuelewa maswala mepesi na yule ambaye mara moja tu anayaelewa masuala magumu.

Sheikh: Nani mwingine anaweza kuwa mtu huyo mbali na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)?
Muombezi: Ni dhahiri kabisa kwamba, baada ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hakuna mtu miongoni mwa Masahaba aliyekuwa na elimu kama hiyo ila lile “lango la elimu” ya Mtume, Ali ambaye kuhusu yeye Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mwenyewe amesema: “Ali ndiye mwenye elimu zaidi kati yenu.

Elimu Yote Ilikuwa Iko Dhahiri Kabisa Kwa Ali.

Abu’l’Mu’ayyid Mu’affaq Bin Ahmad Khawarizmi anasema katika Manaqib yake kwam- ba siku moja Umar alimuambia Ali Bin Abi Talib kwa namna ya mshangao kwamba: “Ni vipi kwamba ikiwa swali lolote unaulizwa wewe, unatoa jibu lake bila chembe ya kusita hata kidogo?”

Imam Mtukufu akaufungua mkono wake mbele yake na kusema: “Unaona vidole vingapi? Umar mara moja akasema: “Vitano.” Ali akasema: “Kwa nini hukutafakari juu ya hili?

Umar akasema: “Hakukuwa na haja ya kutafakari kwa vile vidole vyote vitano vilikuwa mbele ya macho yangu.” Kisha Ali akasema: “Basi vivyo hivyo, masuala yote na mambo ya elimu kwangu yanaonekana wazi kabisa. Ninatoa majibu yake bila ya kuwaza.”

Sasa, enyi waungwana! Hivi sio kwa sababu ya hisia za upendeleo tu kwamba, mwalimu huyu anaongoea upuuzi kama huu na kuwapotosha vijana wasio na elimu! Je, inaingia akilini na kukubalika kwamba yule mtu aliyekuwa na ujuzi mkubwa wa elimu na sayansi zote na aliyekuwa ndio “lango la elimu” ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), aweze kumtaka ushauri Umar ili amtatulie matatizo yake?

Mu’awiya Anaitetea Nafasi Ya Ali

Hadithi moja imefanya kunijia, naiweka mbele yenu kama ushahidi wa ziada wa hoja yangu. Ibn Hajjar Makki, mwanachuo anayejulikana kwa kutostahimili kwake anaandika katika kitabu chake Sawa’iq-e-Muhriqa, sura ya 2, Maqsad ya 5, uk. 110 chini ya aya 14, kwamba Imam Ahmad Hanbal amesimulia na pia Mir Seyyed Ali Hamadani katika Mawaddatu’l-Qurba na Ibn Abi’l-Hadid katika Sharh-e-Nahjul’l-Balagha wamesimulia kwamba, mtu mmoja alimuuliza Mu’awiya swali. Mu’awiya akasema: “Muulize Ali juu ya hilo kwani ndiye mtu mwenye elimu zaidi.. “Yule Mwarabu akasema: “Nalipendelea jibu lako wewe kuliko jibu la Ali.”

Mu’awiyya akasema: “Umetamka jambo baya sana: umemkataa mtu ambaye Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mwenyewe amemfunza na ambaye kwake alimuambia: “Unao uhusiano kwangu sawasawa na Harun aliokuwa nao kwa Musa, isipokuwa tu kwamba hakutakuwa na Mtume baada yangu. Na zaidi ya hayo, kila wakati Umar alipotatizwa na masuala magumu, alimuuliza Ali juu yake na kuomba maoni yake.”
Hii inakumbusha ule usemi: “Uadilifu hasa ni ule ambao hata adui anautolea ushahidi.”

Umar Akiri Juu Ya Kutojua Kwake Kuhusu Mas’ala Magumu, Na Kutamka Kwake Kwamba Kama Ali Asingemsaidia Matatizo Yake Yasingeli- Fumbuliwa

Ili kuendeleza kuunga mkono zaidi ubora wa Ali juu ya Umar tunanukuu kile Ulamaa wenu mashuhuri walichosema. Nuru’d-Din Bin Sabbagh Maliki katika Fusulu’l- Muhimma, Muhamamd Bin Talha Shafi’i katika Matalibus-Su’ul; Imam Ahmad Bin Hanbal katika Musnad; Khatb Khawarizmi katika Manaqib Sulayman Balkhi Hanafi kati- ka Yanabiu’l-Mawadda na wengine wengi wameandika kwamba katika nyakati sabini Umar amesema: “Kama Ali asingelikuwepo, Umar angeangamia.”

Nuru’d-Din Maliki katika Fasulu’l-Muhimma anaandika kwamba wakati mmoja mtu mmoja aliletwa kwa Umar. Aliulizwa mbele ya halaiki ya watu: “Umeianzaje asubuhi yako” Yeye akasema: “Niliamka asubuhi hii katika hali hii: Nikiyapenda matamanio na kuichukia haki, nilishuhudia ukweli wa Mayahudi na Wakristo, nikaamini ambacho sijakiona na katika ambacho hakijaumbwa bado.”
Umar akaamuru Ali aletwe mbele yake. Suala hili lilipowekwa mbele ya Amiru’l-Mu’minin, yeye akasema, alichokisema mtu huyu ni sahihi. Anasema anapenda vishawishi. Anamaanisha kwa hili, mali na watoto. Allah anasema ndani ya Qur’ani Tukufu:

وَاعْلَمُوا أَنَّمَا أَمْوَالُكُمْ وَأَوْلَادُكُمْ فِتْنَةٌ وَأَنَّ اللَّهَ عِنْدَهُ أَجْرٌ عَظِيمٌ {28}

“Na jueni kwamba mali zenu na watoto wenu ni mtihani.” (8:28).

Kwa kuchukia haki unamaanisha kifo. Qur’ani inasema:

وَجَاءَتْ سَكْرَةُ الْمَوْتِ بِالْحَقِّ ۖ ذَٰلِكَ مَا كُنْتَ مِنْهُ تَحِيدُ {19}

“Na hofu ya mauti itakuja kwa ukweli.” (50:19)

Kwa kushuhudia ukweli wa Mayahudi na Wakristo anamaanisha kile Allah Anachosema:

وَقَالَتِ الْيَهُودُ لَيْسَتِ النَّصَارَىٰ عَلَىٰ شَيْءٍ وَقَالَتِ النَّصَارَىٰ لَيْسَتِ الْيَهُودُ عَلَىٰ شَيْءٍ وَهُمْ يَتْلُونَ الْكِتَابَ ۗ{113}

“Mayahudi walisema kwamba Wakristo hawakuwa kwenye njia iliyonyooka na Wakristo walisema kuwa Mayahudi hawakuwa katika njia iliyooka.” (2:113).

Hii ni kwamba Madhehebu zote hizi zina zinasingiziana. Hivyo Mwarabu huyu anasema anakubaliana nazo zote, au kwamba anazikataa zote. Anasema kwamba anaamini kile ambacho hajakiona, akimaanisha kwamba anamwamini Allah swt. Mwenye Nguvu zote.

Anaposema kwamba, anaamini katika ambacho hakijaumbwa bado, yaani ambacho hakipo sasa, anaashiria Siku ya Hukumu, ambayo bado haijafikia wakati wake wa kuwepo.

Kisha Umar akasema: “Naomba hifadhi ya Allah kutokana na hali ngumu ambayo Ali atakuwa hayupo kunisaidia.”

Hadithi hii fupi ya kweli imesimuliwa kwa namna inayojieleza nzuri zaidi na ya tofauti, na wengineo kama Muhammad Bin Ganji Shafi’i katika Kifayatut-Talib Sura ya 57, kutoka kwa Hudhaifa Bin Al-Yaman, aliyeinukuu kutoka kwa Khalifa Umar.

Kuna idadi ya matukio kama hayo wakati wa ukhalifa wa Abu Bakr na Umar, ambao wote walikuwa hawana uwezo wa kutoa jawabu sahihi. Alikuwa ni Ali aliyetoa jawabu. Hasa wakati Mayahudi, Wakristo na Wanachuoni wa Sayansi ya asili walipokuja na kujadili masuala magumu, alikuwa ni Ali peke yake aliyeyatatua.

Kulingana na Ulamaa wenu, kama Bukhari na Muslim, kila mmoja katika Sahih yake; Nishapuri katika Tafsiir yake; Ibn Maghazili Faqih Shafi’i katika Manaqib; Muhammad Bin Talha katika Matalibus-Su’ul, Sura ya 4 uk. 13 na 18; Hafiz Ibn Hajar Asqalan (aliyek- ufa mwaka 852 A.H) katika Tahdhibut-Tahdhib (Kilichochapishwa Hyderabad Daccan) uk. 338; Qadhi Fadhlullah Ruzbahar Shirazi katika Ibta’lu’l-Batil, Muhibu’d-Din Tabari katika Riyadhu’n-Nazala Juz. 2, uk. 39, Ibn Kathir katika Ta’rih yake Juz. 7 uk. 369; Ibn Qutayba Dinawazi (aliyekufa 276 A.H.) katika Ta’wil-e-Mukhtalafu’l-Hadith (kili- chochapwa Misri), uk. 201-202; Muhamamd Bin Yusuf Ganji Shafi’i (aliyekufa 658 .A.H). katika Kifayatut-Talib sura ya 57, Jalala’d’Din Suyuti katika Ta’rikhu’l Khulafa uk. 6, Seyyed Mu’min Shabalnji katika Nuru’l-Absar uk 73, Nuru’d-Din Ali Bin Abdullah Samhudi (aliyekua (911 A.H) katika Jawahiru’l-Iqdain, Al-Hajj Ahmad Afindi katika Hidayatu’l-Murtab uk. 146 na 153, Muhammad Bin Ali As-Sabban katika Ishafu’r- Raghbin uk. 52, Yusuf bin Sibti Ibn Jauzi katika Tadhkira Khawasu’l-Ummal, sura ya 6 uk. 37, Ibn Abi’l-Hadid (aliyekufa 655 A.H) katika Sharhe-Nahju’l-Balagha Juz. 1; Mula Ali Qushachi katika Sharh-e-Tajrid, uk. 407; Akht Abu’l-Khutaba Khawarizmi katika Manaqib uk. 48 na 60, hata yule asiyemvumilivu, Ibn Hajar Makki (Kafa 973 A.H) katika Sawa’iq Muhriqa uk. 78; Ibn Hajar Asqalani katika Isaba Juz. 2, uk. 509 na Allama Ibn Qayyim Jauzia katika Turuqu’I-Hikmiyya uk. 47 na 53 wameandika mambo mengi yanay- oonyesha kwamba Umar alipeleka masuala magumu na mazito, hususan masuala magumu ya Mfalme wa Roma, kwa Amiru’l-Mu’minin.
Umar mara kwa mara alipeleka masuala kwa Ali kwa ajili ya ufumbuzi, na alipokuwa akisikia uamuzi wake alikariri kusema: “Ninaomba ulinzi wa Allah kutokana na hali ngumu ambamo Ali huyupo kunisaidia.” Wakati mwingine alisema: “Kama Ali asingekuwapo, Umar angeangamia.”

Ibn Maghazili Shafi’i katika Manaqib yake, na Hamidi katika Jam’-e-Bainus-Sahihain wanaandika kwamba Makhalifa walichukua ushauri kwa Ali katika masuala yote na kwamba alikuwa ndio tegemeo kubwa ambaye alifutu mas’ala magumu ya kidini na kidunia, makhalifa hao walisikiliza kwa makini maelezo na maagizo yake na wakayatekeleza.

Ali Ndiye Aliyefaa Zaidi Kwenye Nafasi Ya Ukhalifa.

Elimu ndiyo kipimo bora zaidi cha kipaumbele. Qur’ani Tukufu kwa uwazi inaeleza. “Ni yeye basi aongozaye kwenye haki anayestahiki zaidi kufuatwa, au ni yule ambaye yeye mwenyewe haendi sawa ila zaidi kufuatwa, au ni yule ambaye mwenyewe hakuongoka ila mpaka aongozwe? Basi sasa mna nini nyie, ni vipi mnavyoamua? (10:35).

Hii ni kwamba, yule aliye na sifa nzuri za uongozi lazima awe ndio kiongozi mkuu wa watu, sio yule ambaye hana ujuzi wa namna ya kuongoza na ambaye yeye mwenyewe anatafuta muongozo toka kwa wengine.

Aya hii ndiyo (hoja) ushahidi mzito kwamba mtu mbora hawezi kufanywa kuwa chini ya mtu dhaifu. Suala la Ukhalifa, Uimam, na Uandamizi wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) unakuja chini ya kanuni kama hii. Hii inashuhudiliwa na aya nyingine ambayo inasema:

قُلْ هَلْ يَسْتَوِي الَّذِينَ يَعْلَمُونَ وَالَّذِينَ لَا يَعْلَمُونَ ۗ{9}

“Je, wale wanaojua na wale wasiojua wako sawa?” ( 39:9)

Kwa Viwango Vyote Ali Alikuwa Ndiye Aliyekuwa Na Haki Zaidi Ya Ukhalifa:

Sheikh: Tunakubali kwa dhati kwamba Ali alikuwa na sifa zote bora kama ulivyozitaja. Hakuna yeyote ila Makhawarij wakaidi, aliyewahi kuukana ukweli huu. Lakini hili nalo linakubalika: Seyyed Ali mwenyewe kwa hiari na furaha alikubali ukhalifa wa makhalifa (watatu wa kwanza) na akaridhia ubora wao na haki yao ya kumtangulia yeye.

Hivyo kuna faida gani ya sisi kuwa na wasiwasi, baada ya miaka 1300, juu ya uamuzi wao na kupigana baina yetu juu ya kwa nini umma uliwachagua Abu Bakr, Umar na Uthman.

Hivyo kuna madhara gani kama tunakuwa kwenye amani na urafiki na kila mmoja kati yetu na kukubali historia ilichokiandika na kile ambacho ulamaa wenu vile vile kwa ujumla wamekikubali: baada ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), Abu Bakr, Umar na Uthman kwa kufuatana, walishika nafasi ya ukhalifa.

Tungeishi pamoja kama ndugu na kwa pamoja tukaukubali ubora wa Ali katika elimu na matendo na uhusiano wake makhsusi na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Katika njia ile ile ambayo Madhehebu zetu nne zimeungana, Mashi’a pia wangeshirikiana nasi.

Hatukatai daima ubora wa elimu ya Ali na tabia, lakini unapaswa ukubali kwamba kulingana na suala la umri, mbinu za kisiasa, uvumilivu na utulivu usoni wa adui, Abu Bakr alikuwa bila shaka ni bora kuliko Ali.

Ilikuwa ni kwa sababu hii kwamba kupitia uamuzi wa pamoja wa Umma, yeye alikalia kiti cha ukhalifa.

Ali alikuwa kijana bado kwa wakati ule na hakuwa na uwezo wa kubeba majukumu ya ukhalifa.

Hata miaka 25 baadae, pale alipochukua ukhalifa, machafuko mengi yalitokea kwa sababu tu hakuwa mwanasiasa mwenye uwezo.

Kiapo Cha Utii Cha Ali Kwa Makhalifa Ni Cha Kulazimishwa.

Muombezi: Kwanza, umesema kwamba Amiru’l-Mu’minin kwa hiari yake alitoa kiapo cha utii kwa wale makhalifa watatu. Kuna simulizi inanijia akilini ambayo ni yenye kufaa kwa mjadala huu.

Katika siku za zamani barabara kuu za Iran zilikuwa zenye hatari, na wale waliokuwa wakienda kuzuru kwenye makaburi matakatifu walikabiliana na matatizo wakati wa safari zao. Msafara fulani uliangukia kwenye makucha ya waporaji, ambao waliiba mali za watu hao.

Walipokuwa wakigawana ngawira miongoni mwao, sanda ya hujaji mmoja ikaangukia mikononi mwa mporaji mzee. Akasema: “Enyi waungwana mahujaji! Sanda hii ni ya nani?

Hujaji mmoja akasema: “Ni yangu” Yule mporaji akasema: “Mimi sina sanda, kwa hiyo tafadhali unipe mimi sanda hii ili iwe ni yangu kihalali. Yule hujaji akasema: “Mali yangu yote ni yako, lakini nirudishie sanda hiyo, kwa vile niko katika hatua za mwisho za maisha yangu na imenichukuwa taabu kubwa kwa matayarisho ya vazi hili kwa ajili yangu kwa ajili ya Akhera. Huu ni utajiri wangu nilioutunza.”

“Yule mporaji akasisitiza kwa mkazo sana juu ya dai lake, lakini yule hujaji alirudia jambo lile lile kwamba hataiachia haki yake ile kwa mtu yeyote yule.” Yule mporaji, akichomoa upanga wake, alianza kumparura yule hujaji kati ya kichwa chake na uso na kusema kwamba angeendelea kumpiga mpaka atakapomuachia yeye sanda hiyo na kusema: “Ni halali.”

Maskini hujaji yule mzee alipigwa hivyo kiasi kwamba alianza kupiga kelele. “Bwana! Halali! Halali! Halali! Ni halali zaidi kuliko maziwa ya mama yake mtu.”

Natumaini mtanisamehe. Lakini nilitaka kuvuta usikivu wenu kwa haya ninayotaka kuelezea. Pengine mmesahau yale ambayo nimeyathibitisha kwenye mikesha iliyopita.

Nilitaja kumbukumbu sahihi za kihistoria, ambazo Ibn Abi‘l-Hadid, Jauhari, Tabari, Baladhuri, Ibn Qutayba, Mas’udi na wengine katika ulamaa wenu wamezihakikisha, kwamba walitishia kuchoma moto nyumba ya Ali, yeye akaburuzwa hadi msikitini na aliamriwa kwa upanga kooni mwake; “Toa kiapo cha utii, vinginevyo utakatwa shingo.” Je, huu ni mfano wa kiapo cha hiari?

Kusiwepo Na “Imani Povu” Katika Dini:

Pili, nimekwishasema mapema kwamba tusiwe na “Imani povu” katika misingi ya dini. Unasema kwamba kwa vile historia inatuambia sisi kwamba makhalifa hawa wanne walikuwa watawala, tungewafuata wazee wetu na tuwe na imani juu yao.

Lakini akili ya kawaida na Hadithi vinatuambia kwamba imani kimsingi isimame juu ya mantiki.

Ninarudia tena kwamba wanahistoria wenu na wetu wameandika kwamba baada ya kifo cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), Umma uligawanyika katika madhehebu mbili. Madhehebu moja ikasema kwamba Abu Bakr angepaswa kufuatwa na ile madhehebu nyingine iliamini kuwa Ali angefuatwa.

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Kumtii Ali ni kunitii mimi, na kutomtii Ali ni kutonitii mimi.” Kwa hiyo utii kwa Ali kulikuwa, kulingana na amri ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kulikuwa ni lazima.

Hivyo ilikuwa ni wajibu wa kila mmoja wa madhehebu zetu mbili kusikiliza hoja za pande hizi mbili na kuchagua njia ya sawa.

Imani Inapaswa Kusisimama Juu Ya Mantiki Na Uchunguzi Wa Dhati.

Imani yangu juu ya Allah imesimama juu ya maarifa. Nimesoma vitabu vya madhehebu na dini mbali mbali. Ninaukubli ukweli kwamba Muhammad alikuwa Mtume wa mwisho kwa msingi wa mantiki na sio kuwafuata wazee wangu kwa mkumbo tu.
Vivyo hivyo, nimejifunza kwa undani mamia ya vitabu vya madhehebu zote, hususan vile vya madhehebu ya Sunni ambavyo ndani yake mna hoja za wazi za kuthibitisha Uimam na Ukhalifa wa Amiru’l-Mu’minina. Ninyi watu mnatupa tu macho juu juu kwenye Aya na Hadithi zenye kumtukuza Ali na kisha mnafanya tafsiri za ajabu ajabu juu yao.

Tatu, unasema kwamba tungekubali mpangilio na historia wa makhalifa: Abu Bakr, Umar, Uthman, na Hodhrat Ali. Lakini huu ni upumbavu. Ubora wa mwanadamu juu ya wanyama ni kutokana na elimu yake na hekima. Kwa hiyo hatuwezi kuwafuata wazee wetu vivi hivi kwa upovu tu.

Kwa mujibu wa ulamaa wenu mashuhuri, ubora wa Ali katika elimu umethbitishwa wazi kabisa. Kwa hiyo, haki ya kutangulia kwake kama Khalifa ni lazima pia ikubaliwe. Madhali alikuwa ndie “Lango la Elimu” ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kumkiuka yeye ni kukiuka toka kwenye uongofu.

Tunakiri kwamba baada ya kifo cha Mtukufu Mtume, Abu Bakr alikuwa Khalifa kwa miaka miwili na miezi mitatu, akifuatiwa na Umar kwa miaka kumi, na Uthman kwa miaka kumi na mbili. Lakini ukweli huu hauondoi nafasi sahihi ya mantiki na hadith. Historia haiwezi kumnyima “Lango la Elimu” ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) haki yake.

Firdaus, Dailami, Abu Nu’aim Ispahani, Muhammad bin Ishaq Muttalabi, mwandishi wa kitabu Maghazi, Hakim, Hamwaini, Khatib Khawarizmi na Ibn Maghazili wanasimulia ama toka kwa ibn Abbas, au Sa’id Khadiri, au Ibn Mas’ud ambao wote wanamnukuu Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akisema: “Watakuja kuulizwa juu ya Uandamizi (Ukhalifa) na Ali Bin Abi Talib.”

Amri Ya Mtume Ya Kumtii Ali.

“Na chochote anachokupeni Mtume, kipokeeni, na kutokana na chochote ana- chokukatazeni kiacheni. (59:7)

Kwa hiyo ni lazima tutii maamrisho ya Mtume Mtukufu. Tunapoangalia kwenye maagizo ya Mtukufu Mtume tunaona (kama ilivyoandikwa kwenye vitabu vyenu vya kuaminika) kwamba miongoni mwa Umma wake wote, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amemwita Ali peke yake lango la elimu yake na ametuamuru sisi tumtii yeye. Kwa kweli amesema kwamba utii kwa Ali ulikuwa sawa na utii kwake.

Imam Ahmad Bin Hanbal katika Musnad yake, Imam‘l-Haram katika Dhakha’iru’l Uqba, Khawarizmi katika Manaqib, Sulayman Hanafi katika Yanabui‘l-Mawadda, Muhammad bin Yusuf Ganji shafi’i katika Kifayatut-Talib na Ulamaa wengine wameeleza kwamba Mtukufu Mtume wa Allah (s.a.w.w.) amesema:

“Enyi Ansar! Niwaonyesheni mtu ambaye mtamuambata na ambaye kamwe hata waongoza kombo?” Watu hao wakasema: “Ndio, hebu tumfahamu mtu huyo.” Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Ni Ali, kuweni rafiki yake, mheshimuni yeye, na mfuateni yeye. Hakika yuko na Qur’ani na Quran iko pamoja naye. Kwa kweli atawaongozeni kwenye njia ya haki na hatakuacheni mpotee. Chochote nilichowaambieni, mimi nimekiambiwa na Jibril.

Vile vile, kama ilivyosimuliwa na ulamaa wenu, Mtukufu Mtume alimwambia Ammar al-Yasir: “Kama wanadamu wote watakuwa upande mmoja, na Ali akawa upande mwingine, unapaswa kutwaa njia ya Ali na uache ya wengine.” Pia, kwa nyakati tofauti na mahali tofauti, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa kurudiarudia amesema: “Yule ambaye anamtii Ali, kwa kweli amenitii mimi. Yule anayenitii mimi anamtii Allah.”

Hakuna Hadithi Inayopatikana Yenye Kuwataja Makhalifa Wengine Kama “Viongozi Wa Umma” Au “Milango Ya Elimu.”

Hakuna hata hadithi moja katika vitabu vyenu ambayo ndani yake Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anasema: “Baada yangu, kiongozi wa kwenye njia ya sawa, au ‘lango langu la elimu’ au Mshika Makamu au Khalifa wangu’ ni Abu Bakr, Umar, au Uthman. Unaweza kutaja Hadith kama hiyo ambayo sio ya kuzushwa na vikundi vya Bakari na Amawi?
Lakini mnatutaka sisi tutoe nafasi ya nne kwa “Lango la Elimu” la Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), “Mrithi na Khalifa” wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa kunukuu maneno ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mwenyewe, na tuwafuate wale ambao juu yao hakuna maagizo yoyote yale. Kama tutafuata ushauri wako, hatutakuwa tumevunja utii kwa Allah na Mtume wake Mtukufu?

Ulamaa Wa Kisunni Hawataki Ushirikiano Na Sisi.

Nne, Umesema kwamba, kama hizi madhehebu nne (Hanafi, Maliki, Hanbali na Shafi’i) tungekuwa nasi tujiunge nanyi. Lakini ninyi watu mnawaita Shia ni Rafidhi, washirikina na makafiri.

Kwa hakika washirikina na waumini hawawezi kuungana. Sisi, hata hivyo, tuko tayari kabisa kushirikiana
na ndugu zetu Sunni. Kwa kweli sharti ni kwamba ninyi na sisi tuwe na uhuru sawa wa kutetea imani zetu
za kidini.

Kama vile ambavyo wafuasi wa madhehebu hizi nne walivyo huru katika matendo yao, wafuasi wa kizazi cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) nao pia wawe huru katika matendo yao. Tunaona kwamba, kati ya madhehebu zenu hizi nne kuna tofauti mbaya sana kiasi kwam- ba baadhi yao wanawaita wengine makafiri na watenda dhambi.

Bado mnawachukulia wao kama ni Waislamu na kuwaruhusu uhuru wa vitendo. Lakini kuwaita maskini Mashi’a washirikina na makafiri, mnawatoa nje ya Kundi la Waislamu na kuwanyima uhuru wao wa kuitekeleza dini yao. Tutategemeaje kuwa na umoja na ushirikiano?

Kusujudu Juu Ya Udongo Kwa Shi’a Kunapingwa Na Wengine Bila Ya Sababu.

Chukua mfano wa kusujudu kwetu kwenye udongo. Ni makelele gani hayo mnayofanya kwa ajili ya udongo huo na turba, kipande kidogo cha udongo wa ardhi tukufu ya Karbala, ambacho juu yake tunaweka vipaji vyetu vya uso wakati wa kusujudu.

Ninyi mnashikilia kwamba ni sanamu na mnatuita sisi waabudu sanamu, ingawa tunasujudu juu ya udongo kwa idhini ya Allah na Mtukufu Mtume wake (s.a.w.w.). Aya za Qur’ani zinatuagiza sisi kufanya sijida, na kusujudu maana yake ni kuweka paji la uso juu ya ardhi. Bila shaka kuna tofauti ya maoni kati yetu na ninyi juu ya vitu ambavyo tunasujudia juu yake.

Sheikh: Basi kwa nini hamfanyi sijida kama wafanyavyo Waislam wengine wote ili kwamba pasiwe na tofauti na kutoelewana huku kukaweza kutoweka.

Muombezi: Kwanza, tafadhali hebu natufahamu kwa nini ninyi Shafi’i mnatofautiana sana na Maliki na Hanbali katika vyote, shuruti za matendo na misingi ya Imani zenu. Wakati mwingine wanafikia mpaka kuitana “Mtenda dhambi” na “Kafir.” Ingekuwa bora kama wote wangekaa pamoja na kupata imani moja, ili kwamba kusiwepo na tofauti.

Sheikh: Ipo tofauti ya maoni miongoni mwa mafakihi, lakini yeyote kati yetu atakayem- fuata yeyote kati ya Mafakihi hawa - Imam Shafi’i, Imam A’zam, Imam Maliki au Imam Ahmad Bin Hanbal - atalipwa na Allah.

Tofauti Kati Ya Madhehebu Manne Zinapuuzwa Bali Shi'a Hawavumiliwi

Muombezi: Tafadhali sana kuwa mwadilifu, huna sababu ya kuwafuata mafakihi hawa wanne ila tu kwamba, baadhi yao walikuwa ni watu wenye elimu. Mnawafuata bila ya kufikiria. Mnaongozwa na pua na bado mnadai kwamba matendo yenu yatalipwa ingawa kuna tofauti katika imani na matendo miongoni mwao.

Tunafuata amri za familia ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), ambao, kulingana na Mtume mwenyewe na wanachuoni wenu wenyewe, walikuwa wenye elimu zaidi nanyi bado mnasema sisi ni makafiri.

Ni lazima mkiri kuwa uadui huu hautokani na tofauti katika maoni. Chanzo chake ni kwamba sisi tunaipenda familia ya Mtume, na maadui zetu wanalea chuki ya siri dhidi yao.

Kiasi ambacho tofauti katika misingi ya Imani na Vitendo vya Ibada vinahusika, ziko nyin- gi mno miongoni mwa madhehebu zenu hizi nne, Nyingi ya fatwa na maimam na mafak- ihi wenu zinapingana na maelekezo ya wazi yaliyomo ndani ya Qur'ani Tukufu.

Lakini hamkutamki neno lolote dhidi ya wale ambao wanatoa fatwa kama hizo na wale wanaozitekeleza. Bado wakati Shi'a wanaposujudu kwenye udongo halisi kulingana na Sheria ya Qur'ani Tukufu, mnawaita makafiri!

Fatwa Za Wanachuoni Wa Sunni Zinakwenda Kinyume Na Maelekezo Ya Qur'ani

Sheikh: Ni wapi wanachuoni wa Fiqh wa Sunni na Maimam wanne wametoa fatwa zina- zokwenda kinyume na Qur'anii Tukufu?

Muombezi: Mara nyingi wametoa amri kinyume na amri za Qur'ani Tukufu na kinyume na maoni (ijma) yaliyokubaliwa na umma. Ulamaa wenu wenyewe wameandika idadi kadhaa ya vitabu juu ya tofauti miongoni mwa madhehebu haya manne. Nakushauri usome kile kitabu maarufu Masa'ilu'l-Khalif fi'l-fiqh cha Sheikhu’t-Ta’ifa Abu Ja’far Muhammad Ibn Hasan Ibn Ali Tusi, ambaye ameandika tofauti zote za mafakihi wa Kiislam kutoka kwenye sura ya Tohara mpaka kwenye sura ya Diyat (Kisasi). Nitatoa mmoja kati ya mifano mingi ya kanuni za kisheria, zilizoamuliwa kinyume na Qur’ani Tukufu.

Seikhh: ndiyo, hebu tupe mfano wa hili.

Katika Kukosekana Maji Kwa Ajili Ya Josho Na Udhu Mtu Afanye Tayammam

Ninyi waungwana mnafahamu kwamba josho la wajibu ni kanuni muhimu ya Kiislam. Kutegemea mazingira, mtu huosha mwili mzima (josho) au sehemu yake (udhu). “Mnaposimama kusali. Osheni nyuso zenu na mikono yenu mpaka kwenye kongo mbili.” (5:6)

Kama vilivyo, tunapaswa tutawadhe kupata udhu kwa maji safi. Wakati hatuna maji, tufanye tayammam, kulingana na Aya:“Na kama msipopata maji basi chukueni udongo (safi) na mpake nyuso zenu na mikono yenu.” (4:43)

Tunapaswa kufanya tayammam kwa udongo safi. Katika suala la awali, maji kwa ajili ya udhuu ni muhimu. Katika suala la pili, maji hayapatikani, au kama kuna sababu nyingine ya udhuru basi, iwe tumo katika safari au tupo nyumbani, tutapaswa kufanya tayammam, kupaka mikono na nyuso kwa vumbi safi, badala ya udhu. Katika nukta hii, mafakihi wote wa Kiislam wanakubaliana, ama wewe Shi’a Ithna Ashari, Maliki, Shafi’i, au Hanbali,

Fatwa Ya Abu Hanifa Kwamba Kama Maji Yasipopatikana Tunaweza Kufanya Josho La Udhu Kwa Kutumia (Nabiz) Kosha La Mtende.

Lakini Imam wenu mkubwa sana, Abu Hanifa (ambaye fatwa zake nyingi sana zimetegemea kwenye dhana) anasisitiza kwamba wakati tukiwa safarini na kama hatuwezi kupata maji, tunapaswa kuoga josho kutumia Nabiz ( maji ya kosha la mtende). Lakini kila mtu anajua kwamba Nabiz ni kosha la mtende na sio halali kuchukua udhu kwa maji yaliyochanganyika.

Qur’ani Tukufu inaagiza kamba ni lazima juu yetu sisi kuchukua udhu kwa ajili ya ibada ya Sala kwa kutumia maji safi. Kama maji hayapatikani, tunapaswa kufanya tayammam.

Imam A’zam Abu Hanifa anasema kwamba tunaweza kuoga josho au udhu kutumia Nabiz. Huu ni uvunjaji wa wazi wa Sheria ya Qur’ani. Kwa upande mwingine , Bukhari katika Sahihi yake ameandika hivi “Sio halali kuchuku udhu kwa Nabiz au kilevi.”

Hafidh: Ninafuata madhehebu Shafi’i na ninakubaliana na wewe kabisa katika suala hili. Kama hakuna maji tufanye tayammam, na hairuhusiwi kuchukua udhu kwa Nabiz. Fatwa hii imezushiwa Imam Abu Hanifa kwa msingi ya umaarufu wa jumla wa hiyo nabiz.

Muombezi: Kwa kujua ukweli halisi unafanya kisingizio hiki. Fatwa hii ya Abu Hanifa imesimuliwa kwa mfululizo sana.

Ninamnukuu Fakhru’d-Din Radhi anayesema katika sherehe yake ya Mafatihul-Ghaib, Juzuu ya 3 uk. 553 kuhusiana na aya hii ya tayammam, mas’ala ya 5; Shafi’i anasema kwamba “Udhu kwa kutumia Nabiz (kosha la mtende) sio halali, na Abu Hanifa anasema kwamba ni halali wakati mtu anapokuwa yuko kwenye safari. Pia Ibn Rushd ameandika fatwa hii ya Abu Hanifa katika kitabu chake Hidayatu’l- Mujtahid.

Sheikh: Utasemaje kwamba fatwa hii ni kinyume na amri ya Qur’ani? Baadhi ya Hadith, zinaithibitisha kwa uwazi kabisa kutoka kwenye kitendo cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Muombezi: Unaweza kutaja Hadithi yeyote yenye kuunga mkono hoja yako?

Sheikh: Katika Hadithi ambayo Abu Zaid, mtumwa wa Amr Bin Harith anasimulia kuto- ka kwa Abdullah Bin Mas’ud kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimuambia, kwenye usiku wa majini (Lailatu’j-Jinn usiku ambapo Mtume alipokea kiapo cha utii kutoka kwa majini) kwamba: “Je, unayo maji kidogo” Yeye ( Abu Zaid) akasema: “Hapana, ipo nabiz kidogo tu” Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Mtende ni msafi, na maji pia ni masafi. Kusema hivyo akachukua wudhu.

Kuna Hadithi nyingine ambayo Abbas Bin Walid Bin Sabihu’l-Halal Damishqi anasimu- lia kutoka kwa Marwan Bin Muhammad Tahir Damishqi ambaye alisimulia kutoka kwa Abdullah bin Lahi’a ambaye ameisimulia kutoka kwa Abdullah Bin Mas’ud ambaye alisema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliniambia katika usiku wa majini “Je unayo maji”

Nikasema: “Hapana, lakini kuna Nabiz katika hiyo ndoo.” Kisha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Mtende ni msafi, na maji yake ni masafi. Nimiminie.” Hivyo nilimmiminia (juu ya viungo vyake), na akachukua udhu nayo.”

Ni dhahiri, kitendo hiki cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ni mfano kwa ajili yetu sisi wa kuufuata. Hakuna kanuni au hoja iliyo bora kuliko vitendo vyake. Ni kwa sababu hiyo kwamba Imam wetu A’zam amekubali uhalali wake.

Muombezi: Pengine ingelikuwa vyema kama ungelinyamaza kimya. Sasa ndugu zetu Sunni watajua kwamba Viongozi wao walikosea. Walitoa fatwa kwa misngi ya dhana tu. Kwanza kabisa, natuchunguze hawa wasimuliaji wa Hadithi hii walikuwa ni nani.

Kwanza, Abu Zaid, mtumwa wa Amir Bin Harith, ni mtu asiyejulikana, na kulingana na wanachuoni au Hadithi, ni mtu asiyekubalika kama alivyoelezwa na Tirmidh na wengineo.

Dhahabi katika Mizanu‘l-itidal yake anasema: “Mtu huyu hajulikani kwetu na hadithi hii ambayo imesimuliwa kutoka kwa Abdullah Bin Mas’ud siyo sahihi.” Hakim anasema; “Hakuna hadithi nyingine iliyosimuliwa na mtu huyu asiyejuliakana.”

Bukhari pia amemtaja kama msimuliaji wa Hadithi asiyetegemewa. Kwa sababu hii, Ulamaa mashuhuri, kama Qastalani na Sheikh Zakariyya Ansari, wameandika katika Sherehe zao za Sahih Bukhari kwamba “udhu sio halali kwa kutumia nabiz au vileo.” Wanaeleza kwamba hadithi iliyorejewa hapo juu ni dhaifu.

Hii hadithi ya pili pia nayo haikubaliki. Kwanza, hakuna mwanachuo, ispokuwa Ibn Maja, aliyeisimula kwa namna hii.

Pili, Ulamaa maarufu hawakuiingiza katika Sunna zao kwa sababu sanadi ya wasimulizi wake ina utata.

Dhahabi katika Mizanu’l-Itiqad yake amenukuu idadi ya kauli zinazoonyesha kwamba Abbas Bin Walid sio wakutegemewa. Hivyo wasanifu na wafasiri wamemkataa yeye moja kwa moja.
Na kuhusu Marwan Bin Muhammad Tahiri, alikuwa ni wa lile kundi lililo potoka la Marhaba. Ibn Hazm na Dhahabi wamethibitisha kwamba alikuwa msimuliaji hadithi asiyetegemewa.

Vivyo hivyo, Abdullah Bin Lahi’a pia ametiliwa mashaka na Ulamaa mashuhuri na wafasiri.
Kwa hiyo pale sanadi ya wasimulizi wa hadithi inapokuwa ni ya asili ya mashaka hivyo kwamba ulamaa wenu wenyewe wanaikataa, hadithi hiyo inapoteza thamani.

Tatu, kwa msingi wa hadithi, ambayo wanachuoni wenu wameisimulia kutoka kwa Abdullah Bin Mas’ud, hakukuwa na mtu yeyote pamoja Mtukufu Mtume kwenye Lailatu’j’Jinn. Abu Dawud katika Sunnan yake, sura ya Udhu, na Tirmidhi katika Sahih yake wanasimulia kutoka kwa Al-Qama kwamba Abdullah Bin Mas’ud aliulizwa: “Ni nani miongoni mwenu aliyekuwa pamoja na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) katika ule usiku wa Lailatu’j-jinn? Yeye akasema: “Hakuna mtu aliyekuwa naye kutoka miongoni mwetu.”

Nne, Lailatu’j-Jinn ulitokea Makkah kabla ya Hijra (kuhama kwa Mtume), ambapo wafasiri wote wanasema kwamba aya ya Tayammam ilishuka Madina.

Hivyo amri hii kwa hakika inaifuta ile amri iliyotangulia huko nyuma. Ilikuwa ni kwa sababu hii kwamba mafakihi wenu wakubwa, kama vile Imam Shafi’i, Imam Malik na wengineo wameitamka kwamba ni haram.

Inashangaza kwamba huyu Sheikh anawasilisha Hadithi dhaifu kama yenye kuaminika usoni mwa Qur’an Tukufu na anajaribu kuthibitisha maelezo ya Abu Hanifa kuwa ya sawa- sawa na sahihi.

Kuosha Miguu Katika Udhu Ni Kinyume Na Sheria Ya Qur’ani

Mbali na kanuni zilizokubalika za udhu zilizotajwa katika Aya ya hapo juu, baada ya kuosha uso na mikono, sehemu ya kichwa na za miguu mpaka kwenye vifundo ni za kupakwa. Aya hii tukufu inasema wazi: “Na pakeni sehemu ya vichwa vyenu na sehemu ya miguu yenu mpaka kwenye vifundo.”

Lakini wanachuoni wenu wote wa fiqh wanashikilia kwamba miguu ioshwe, wakipinga hukumu ya wazi ya Qur’ani. Kuna tofau- ti kati ya kuosha na kupaka.

Sheikh: Kuna Idadi kadhaa ya Hadith zinazoonyesha kwamba miguu ni ya kuoshwa.

Muombezi: Kwanza, hadithi zinazorandana na hukmu za Qur’ani tu ndio zinazokubali- ka. Kwa hakika, kutangua aya wazi ya Qur’ani kwa hadith moja tu haiwezi kamwe kuwa halali. Aya hii tukufu kwa uwazi kabisa inaagiza kupaka, sio uoshaji wa miguu.

Kama utafikiri kwa uangalifu kidogo utaona kwamba aya yote mzima inaelekea wenye maana hiyo hiyo. Inaanza na hukmu ya “osha uso wako na mikono yako.” Hiki kiungo “na” kinaashiria kwamba baada ya kuosha uso, tunapaswa pia kuosha kichwa mikono. Kadhalika, katika hukmu ya pili: “na pakeni sehemu vichwa vyenu na sehemu ya miguu yenu.”

Kupakwa kwa kichwa na kwa miguu kumeunganishwa na kile kiungo “na.” Hii inaonyesha wazi kwamba baada ya kupaka kichwa, na miguu nayo ni lazima ipakwe.

Inapita bila kupingwa kwamba kuosha hakuwezi kubadilishwa na kupaka. Hivyo kama kuosha uso na mikono kulivyo lazima, kule kupaka kichwa na miguu pia ni lazima. Hairuhusiwi kwamba kimoja kipakwa na kingine kioshwe. Vinginevyo, hiki kiungo “Na” kitakuwa hakina maana yoyote.

Hali kadhalika, mbali na maana hizi za wazi, sheria ya Kiislam haibebi hukumu ngumu na zenye uzito. Kuosha miguu ni kugumu zaidi ya kupaka hiyo miguu.

Hukumu ya kidini imedhamiriwa kufanya kuchukua udhu kuwe kwepesi, kama usemi wa aya unavyopendekeza pia. Imam Fakhru’d-Din Razi, mfasiri mkubwa wa Kisunni, anatoa hoja yenye maelezo zaidi kuhusu hali halisi ya ulazima wa kupaka miguu katika udhu. Utafaidika kwa kuisoma hiyo.

Kupaka Juu Ya Soksi Ni Kinyume Na Sheria Ya Wazi Ya Qur’an Tukufu

La ajabu zaidi kuliko kuosha miguu ni kupaka juu ya soksi. Kuna hitilafu miongoni mwa mafaqihi wa Kisunni juu ya kwamba inaweza kufanywa wakati wa safari au ukiwa nyumbani.

Hukmu hii ni kinyume na maelekezo ya Qur’ani ambayo inashurutisha kwamba tunapaswa kupaka miguu na sio soksi. Hukmu hii pia inapingana na hukmu ya awali ya kuosha miguu. Ikiwa kupaka miguu sio halali, kwa nini wamefanya kupaka juu ya soksi kuwa ni halali?

Sheikh: Kuna Hadithi nyingi zinaoonyesha kwamba bwana Mtume alipaka soksi zake. Kwa maana hiyo, mafaqihi wakaichukulia hiyo kama uthibitisho wa uhalali wa kitendo hicho.

Muombezi: nimerudiarudia kushauri kwamba, kulingana na amri ya Bwana Mtume, hadithi inayodaiwa imesimuliwa kutoka kwake ambayo hairandani na Qur’ani Tukufu ni ya kukataliwa. Wazushi hawa na wanasiasa wajanja wametunga Hadithi nyingi. Kwa sababu hiyo, Ulamaa wenu mashuhuri wamekataa Hadithi za namna hii.

Mbali na ukweli kwamba hadithi hizi haziendani na sheria za wazi Qur’ani Tukufu, zenyewe ziko zinapingana. Ulamaa wenu wakubwa wenyewe wameukubali ukweli huu.

Kwa mfano, yule mwenye hekima nyingi, Ibn Rushd Andalusi, katika Badaytu’l-Mujtahid wa Nihayyatu‘l-Muqtasid yake Juz. 1, uk. 15-16, anasema juu ya tofauti hii. “Sababu ambayo wanahitilafiana nayo ni kwamba riwaya juu yao zinapingana zenyewe.” Mahali pengine anasema: “Sababu ambayo wanahitalafiana kwayo ni kwamba, riwaya juu yao haziendani daima.”

Kwa hiyo, kusimamisha hoja juu ya riwaya na hadithi ambazo zinapingana zenyewe na ambazo pia ni kinyume kabisa na maagizo ya Qur’ani ni kichekesho kabisa. Unajua kwamba kati ya hadith ambazo zinapingana zenyewe, ni zile tu ambazo zinakubaliana na Qur’ani Tukufu ndizo zinazokubaliwa. Ikiwa hadithi yoyote inapingana na Qur’ani, hiyo ni ya kutupwa moja kwa moja.

Kupaka Juu Ya Kilemba Ni Kinyume Na Sheria Ya Qur’ani

Aya hii inaeleza wazi kwamba, “Na pakeni sehemu ya vichwa vyenu” (baada ya kuosha uso na mikono). Kwa misingi ya amri hii ya Qur’ani, mafaqihi wa Kishia, kwa kuwafuata Maimam wao, wanashikilia kwamba, kichwa chenyewe ni cha kupakaza katika kuchukua udhu.

Mafaqih wa Shafi’i, Maliki, Hanfi wanapatana. Lakini Imam Ahmad Bin Hanbali, Ishaq, Thawri na Quza’i wamesema kwamba kupaka juu ya kilemba inasihi. Hii imeandikwa na Imam Fakhru’d-Din Razi katika Tafsir-e- Kabir. Mtu yeyote mwenye fahamu anajua kwamba kupakaza juu ya kilemba na kupakaza juu ya kichwa ni mambo mawili tofauti kabisa.

Shi’a Pekee Ndio Wanaolaumiwa Kwa Tofauti Kama Hizo:

Kuna tofauti nyingine za hali ya juu sana miongoni mwa mafaqihi wenu na miongoni mwa madhehebu nne hizi. Ingawa nyingi ya hizo zinapishana waziwazi na maagizo ya Qur’ani, hamtoani makosa kati yenu. Kila mmoja wao yuko huru kudumisha maoni yake.

Hamumuiti Abu Hanifa na mahanafiya kuwa ni washirikina, wanaporuhusu udhu kuchukuliwa kwa Nabiz (Maji ya mtende yaliyochachuliwa) wala hamshutumu tafsir zinazojipinga zenyewe za sheria, ambazo zinavunja hukumu za Qur’ani. Lakini mnawapinga Shi’a ambao, wanawafuata kizazi cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Kwa kweli mnawaita wafuasi ile familia tukufu Rafidhi na Makafiri!

Umesema kwa kukariri katika mikesha iliyopita kwamba ibada za Kishi’a zinathibitisha kuwa wao ni washirikina. Umeuliza kwa nini hatufanyi Sala kama Waislam? Sisi tunaswali Swala zile zile ambazo wewe na Waislam wengine wote wanazosali; rakaa mbili za Al-fajir, (sala ya asubuhi), rakaa nne za Adhuhuri (Sala ya mchana), rakaa nne za Asr (Sala ya alasiri), rakaa tatu za magharibi
(Sala ya wakati wa kuzama jua), na rakaa nne za Isha (Sala ya jioni).

Na kwa tofauti katika kanuni za ibada, zipo tele katika madhehebu zote za Kiislamu. Kwa mfano, kuna tofauti ya wazi kati ya Abu’l-Hasan Ash’ari na Wasil Bin Ata katika misingi na kanuni za ibada.

Pia Maimam wenu wanne (Abu Hanifa, Maliki, Shafi’i na Ahmad Hanbal) na mafaqihi wengine wakubwa kama Hasan, Dawud, Kathir, Abu Sur, Quza’i, Sufyan Thawri, Hasan Basr na Qasim Bin Salam n.k, wana tofauti miongomi mwao.

Katika namna hiyo hiyo, hukumu za Maimam watukufu wa Ahlul Bayt zinatofautiana na kauli za mafaqihi wenu. Ikiwa tafsiri za kisheria za mafaqihi hawa na tofauti zao za maoni zinaweza kushutumiwa, kwa nini shutuma kama hizo zisitolewe dhidi ya madhehebu tofauti za Kisunni?

Kwa Mujibu Wa Ulamaa Wa Kisunni Kusujudu Juu Ya Kinyesi Kikavu

Na Kinyesi Cha Mnyama Ni Halali.

Ulamaa wengi wa Sunni wanazikubali tafsiri za kisheria ambazo zinakiuka amri ya wazi ya Qur’ani na bado wanatoa tafsiri potovu kwa amri zenye kueleweka wazi. Mafaqih wengine wanatoa maoni tofauti. Bado hamzichukulii tafsiri zao au ibada zao kama ni ukafiri. Lakini kuhusiana na ufanyaji wetu wa sijda mnatoa upinzani kwa sauti kubwa, mkisema kwamba, Shi’a ni waabudu sanamu, wakati mnapuuza tamko la ulamaa wenu wenyewe kwamba kusujudu juu ya kinyesi kikavu kunaruhusiwa.

Kusujudu Juu Ya Mazulia Badala Ya Ardhi Ni Kinyume Na Agizo La Qur’ani

Maamuzi ya kisheria ya mafaqih wa Shi’ah, wakiwafuata Maimam wao watukufu, yanakubaliana kwa uwazi na maagizo ya Qur’ani Tukufu. Kwa mfano, mafaqihi wenu wanachukulia mazulia ya sufi, pamba, hariri na mazulia mengine sawa sawa na udogo. Lakini ni wazi kwamba mazulia haya sio udongo wenyewe.

Lakini Shi’ah, kwa utii kwa Maimam wao wa Ahlul-Bayt wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wanasema: “Sijda haisihi juu ya chochote isipokuwa juu ya udongo au vile vitu, vinavyokua kutoka kwenye udongo na havitumiki kwa kula au kuvaliwa.”

Kwa hili mnawakemea na kuwaita washirikina. Kwa upande mwengine hamuiti kusujudu kwenye kinyesi kikavu ni ushirikina. Ni dhahiri kabisa kwamba, kusujudu juu ya udongo kama ilivyoamriwa na Allah na kusujudu juu ya mazulia ni vitu tofauti kabisa.

Sheikh: Ninyi watu mnafanya Sijda kwenye vipande vya udongo wa Karbala. Mnakuwa na vibonge hivyo vidogo vya udongo kutoka nchi ile. Viko kama sanamu, na mnachukulia kusujudu juu yao ni lazima. Kwa kweli, kitendo hiki ni kinyume na taratibu na ibada za Waislam.

Muombezi: Imekuwa ni desturi yako kuwafuata wakubwa wako kiupofu ingawa haipen- dezi mtu muungwana kama wewe kusema kwamba ule udongo halisi wa Karbala ni kama sanamu.

Rafiki yangu mheshimika! Shutuma juu ya imani yoyote ni lazima itegemee juu ya ushahi- di. Kama ungevisoma vitabu vya Ilmu vya Shi’ah, ungelipata jawabu la shutma zako, na usingewapotosha ndugu zetu Sunni kwa upinzani wa uongo.

Shia Hawachukulii Kusujudu Juu Ya Udongo Wa Karbala Kuwa Ni Wajibu

Kama unaweza kutuonyesha kutoka kwenye tafsiri yetu yoyote hadithi moja au tamko linaloashiria kwa kusujudu juu ya udongo wa Karabala ni wajibu, tutayakubali maelezo yako yote kwamba ni sahihi. Kwa kweli, katika vitabu vyetu vyote vya kanuni za kidini, kuna maelekezo ya wazi kwamba, kwa mujibu wa amri ya Qur’ani Sijda ni lazima ifany- we juu ya udongo halisi. Hii inajumuisha vumbi, mawe, mchanga na majani, ili mradi tu isiwe ni madini. Zaidi ya hayo, Sijda inaweza kufanywa juu ya vile vitu vinavyoota kutoka kwenye ardhi, mradi tu havitumiwi kwa chakula au kuvaliwa.

Sheikh: Basi kwa nini mnayo kawaida ya kuwa navyo vibonge vidogo vya udongo toka Karbala na mnafanya Sijda juu yake wakati wa Sala?

Shia Wanakuwa Na Vidonge Vya Udongo Kwa Ajili Ya Kusujudia Wakati Wa Sala.

Muombezi: Kusujudu juu ya udongo safi ni faradhi. Ibada ya Sala kwa kawaida inafanyika kwenye nyumba ambazo zimepambwa na mazulia (makapeti).

Hata kama mazulia hayo yataondolewa, ile ardhi iliyo chini yao kwa kawaida inakuwa na chokaa na vitu vingine ambavyo juu yao sijda hairuhusiwi. Kwa hiyo, tunakuwa na kipande cha udongo ili kwamba tuweze kusujudia. kwa hiyo, tunakuwa na kipande cha udongo ili kwamba tuweze kusujudia juu yake. (Mujtahid wengi wa Shia’h wanachukulia chaki, plasta, chokaa na mawe ya kuchimbuliwa kama vile ageti vyenye kuruhusika tu pale vinapokosekana vile vitu vilivyopendekezwa, lakini hata hivyo vinaondoa mawe yenye madini halisi na madini yaliyosafishwa - Mfasiri).

Sheikh: Tunachokiona ni kwamba, Shi’ah wote wana vidonge vya udongo wa Karbala na wanachukulia kufanya sijda juu yake ni faradhi.

Kwa Nini Tunasujudu Juu Ya Ule Udongo Wa Karbala

Muombezi: Ni kweli kwamba sisi tunasujudu juu ya udongo wa Karbala, lakini sisi hatulichukulii hilo kwamba ni wajibu. Kulingana na maelekezo yaliyomo ndani ya vitabu vyetu vya Fiqh tunachukulia sijda ni wajibu juu ya udongo safi. Hata hivyo, kulingana na Ahlul’Bayt, sajda juu ya udongo safi wa sehemu aliyozikiwa Husain (a.s) kule Karbala, ni bora zaidi

Inasikitisha kwamba baadhi ya watu kwa uovu tu wanashikilia kwamba Shi’ah wana- muabudu Husein. Wanatilia nguvu maoni yao kwa kusema kwamba Shi’ah wanafanya Sajda zao juu ya udongo uliochulikuliwa toka Karbala.

Kwa kweli kamwe hatumuabudu Husain, Ali au Muhammad. Tunamuabudu Allah swt. peke yake, na ni kulingana na amri ya Allah kwamba tunafanya Sajda juu ya udongo halisi tu.

Kusujudu kwetu sio kwa ajili ya Husain. Lakini kutokana na maagizo ya Maimam wasiokosea wa kizazi cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), kusujudu juu ya udongo safi wa Karbala kunapelekea kwenye malipo makubwa juu yetu, lakini sio wajibu.

Sheikh: Utadai vipi kwamba udongo wa Karbala una sifa maalum na kwamba unastahili kupendelewa zaidi ya udongo mwingine?

Sifa Za Hali Ya Udongo Wa Karbala.

Muombezi: Kwanza, ni ukweli kwamba sehemu tofauti zina sifa tofauti. Kila kipande cha ardhi kina sifa maalum ambayo ni mtaalam wa utafiti wa ardhi na mawe (geologist) tu anayezijua. Wasio wataalam hawayajui mambo haya.

Pili, sifa, hali maalum ya udongo wa Karbala zilijulikana kabla ya wakati wa Maimam watukufu. Kilikuwa ni kitu chenye mazingatio maalum katika wakati wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) pia, kama ilivyokuwa imeandikwa kwenye vitabu sahihi vya Ulamaa wenu wenyewe.

Katika Khasa’isu’I-Kubra cha Jalalu’d-Din Suyuti, idadi ya hadithi za Ummu’I-Mu’minin Umm Salma, Ummu’I-Mu’minin Aiyesha, Ummu’I-Mu’Minin Fadhl, Ibn Abbas na Anas Bin Maliki na kadhalika, juu ya udongo wa Karbala zimesimuliwa na Ulamaa wenu mashuhuri na wasimulizi wanaotegemewa kama Abu Nu’aim Ispahani, Baihaqi na Hakim.

Hadithi moja inasema: “Nilimuona Husain amekaa katika paja la babu yake, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliyekuwa na donge jekundu la udongo mkonini mwake.
Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akibusu ule udongo na kulia. Nilimuuliza udongo ule ulikuwa nini? Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), akasema:

“Jibril amenijulisha kwamba mwanangu, huyu Husain, atauawa huko Iraq. Ameniletea udongo huu mimi kutoka kwenye ardhi ile. Ninalia kwa sababu ya mateso yatakayomfika Husein.”

Kisha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akaukabidhi ule udongo kwa Ummu Salma na akamuam- bia: “Pale utakapoona kwamba udongo huu unageuka kuwa damu, utajua kwamba Husain wangu amechinjwa.”

Ummu Salma aliuweka udongo ule kwenye chupa na akaweka uangalizi juu yake mpaka akaona mnamo siku ya Ashura, mwama 61 A.H. kwamba umegeuka kuwa damu. Ndipo akajua kwamba Husain Bin Ali ameuawa shahidi.

Imeandikwa na Ulamaa wenu mashuhuri na mafaqihi wa Kishia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na Maimam waliweka mazingatio maalum juu ya udongo halsi wa Karbala.

Baada ya kuuawa shahidi Imam Husain, Imam Seyyedu’s-Sajidin Zainur’I- Abidin, Ali Bin Husain aliuokota kidogo, akautangaza kuwa ni udongo Mtakatifu na akauweka kwenye begi lake. Imam huyu Mtukufu alitumia kufanya Sajda juu yake na alitengeneza tasbihi kutokana nao na akadhukuru sifa za Allah kwayo.

Baada yake, Maimam wote walaiomfuatia waliuchukulia udongo ule kuwa ni mtakatifu na walitengeneza tasbih kutokana nao na kidongo kidogo cha kusujudia juu yake. Waliwashawishi Shi’ah kufanya sajda juu yake, kwa kuelewa kuwa haikuwa ni wajibu, lakini kwa maoni ya kutarajia kupata malipo makubwa.

Maimam watukufu walisisitiza kwamba kusujudia mbele ya Allah lazima kuwe juu ya udongo safi tu, na kwamba ingekuwa ni bora zaidi kama ingefanywa juu ya udongo ule wa Karbala.

Yule mwanachuoni mkubwa, Abu Ja’far Muhammad Bin Hasan Tusi anaandika katika kitabu chake Misbahu’l-Mutahajjid kwamba Imam Ja’far as-Sadiq aliweka udongo kidogo kutoka kwenye kaburi la Imam Husain katika kitambaa cha rangi ya manjano ambacho alikifunua wakati wa sala na kufanya Sajda yake juu yake. Shi’ah kwa muda mrefu wame- jiwekea udongo huu.

Kisha, kwa kuhofia kwamba ungeweza kunajisika, waliukanda vidonge vidoga au vipande, ambavyo sasa vinaitwa Muhr. Tunavichukulia kwamba ni vitakatifu na wakati wa sala tunasujudu juu yavyo, sio kama tendo la wajibu lakini kwa mtazamo wa sifa yake maalum, vinginevyo tunapokuwa hatuna udongo halisi, tunasujudu juu ya ardhi safi, au jiwe safi. Kwa namna hii, tendo letu la faradhi (sajda) linatimia.

Tunashangazwa na tabia ya Ulamaa wenu ambao hawaoni makosa kwenye fatwa za haya madhehebu manne ya Sunni. Ni kwamba, kama Imam A’ zam anasema kwamba katika kukosekana maji udhu unaweza kuchukuliwa kwa nabiz, Shafi’i, Maliki na Hanbali hawana pingamizi juu yake.

Ikiwa Imam Ahmad Bin Hanbali anaamini kuonekana kwa Allah au anachukulia ni halali kupaka maji juu ya kilemba katika utaratibu wa udhu, ulamaa wa hizo madhehebu zingine hawamshutumu.

Halikadhalika, hawalaumu fatwa za kipekee kama ile ya kuungana katika ndoa na wafulana wadogo wakati wa safari, kusujudu juu ya kinyesi au kitu chochote kilichonajisika, au kuingiliana na mama zao kwa kutumia nguo ya kujifunika.

Lakini tunaposema kwamba kizazi cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wamesema kwamba, kusujudu juu ya udongo wa Karbala ni jambo lenye thamani mnasema kwamba hawa Shi’ah ni washirikina.

Umri Mkubwa Sio Kigezo Cha Ukhalifa.

Sasa nitaijibu hoja yako. Kuzungumzia juu ya umri uliosogea na makubaliano (ijma), ume- sema kwamba kwa sababu ya umri wake, Abu Bakr alistahili kipaumbele. Hata baada ya mikesha kumi, wakati ambamo nimetengua hoja yako kuhusiana na ijima (makubaliano ya pamoja) na upendeleo kutegemea juu ya umri, unaizusha tena hoja hiyo kana kwamba hakuna lililosemwa. Hata hivyo, sitakuacha bila ya kujibiwa.

Ali Ateuliwa Kuwasilisha Aya Za Surat Bara’a (Tawba) Ya Qur’ani Tukufu

Umetoa hoja kwamba Abu Bakr alistahili kipaumbele kwa sababu ya umri wake na mbinu zake za kisiasa, lakini ni vipi kwamba baadhi ya watu waliamua kwamba kwa kusudi kubwa ilikuwa ni sharti kwa mtu kuwa mzee na mwenye mbinu za kisiasa, lakini Allah na Mtume wake hawakulielewa hili. Kwa kukuziwasilisha aya arobaini za mwanzo za Bara’a kwa watu, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimuuzulu Abu Bakri na kumtuma huyo kijana Ali badala yake.

Nawab: Bwana Mheshimika! Tafadhali usiiache nukta hii katika hali ya kutoeleweka vizuri. Tufahamishe ni kwa lengo gani Abu Bakr aliuzuliwa na akachaguliwa Ali mahali pake. Nilipowauliza watu hawa (akiwanyooshea kidole Ulamaa wake) juu ya hili, walitoa jibu la wasi wasi, wakisema kwamba lilikuwa ni jambo lililokuwa halina umuhimu. Tafadhali hebu lielezee jambo ili.

Muombezi: Umma wa Kiislam, pamoja na ulamaa na wanahistori wa madhehebu zote (Shi’ah na Sunni) wanaukubali ukweli kwamba wakati ziliposhuka zile aya za mwanzo za Sura ya Bara’a katika kuwashutumu wanaoabudu sanamu, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimuita Abu Bakr akampa aya hizo, akimuagiza yeye kuzipeleka Makka na kuzisoma kwa watu wa Makka wakati wa Hijja.

Abu Bakr alikuwa amekwenda mwendo mfupi tu wakati Jibril alipotokea na kusema: “Ewe Mtume wa Allah! Allah swt. anatuma salam Zake kwako na anasema kwamba hili suala la Qur’ani Tukufu liwe limepelekwa ama na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mwenyewe au na mtu ambaye anatokana naye.”

Kwa hali hiyo, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akamuita Ali na kumwambia: Mkimbilie Abu Bakr na uchukue zile aya za Bara’a toka kwake na ukaziwasomea waabudu masanamu wa Makka. Ali akaondoka mara moja. Alimkuta Abu Bakr hapo Dhu’l-Halifa na akamfikishia ule ujumbe wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Akazichukua ziel aya toka kwa Abu Bakr na alipofika Makka, akazisoma kwenye mkusanyiko wa watu.

Nawab: Habari hizi zimeandikwa kwenye vitabu vyetu vya Sahih?

Muombezi: Nilikwisha kueleza punde kwamba Umma wote unakubaliana juu ya suala hili. Nitakupa baadhi ya rejea sasa hivi, ili kwamba utakapofikiria juu ya suala hii utaweza kujua kwamba ni suala la maana sana. Waandishi mashuhuri wafutao wameiandika habari hii katika vitabu vyao na kwa ujumla wakathibisha ukweli wake.

Bukhari katika Sahih yake, Jz. ya 4 na 5; Abdi katika Jam-e-Bainus–Sihahis-Sitta, Jz. Ya 2, Baihaqi katika Sunan uk. 9 na 224; Tirmidhi katika Jam’i; Juz 2, uk. 135, Abu Dawud katika Sunan, Khawarizmi katika Manaqib; Shukani katika Tafsir Juz. 11, uk. 319, Ibn Maghazili katika Manaqib, Faqih Shafi’i’ katika Fadha’il yake, Muhammad Bin Talha Shafi’i katika Matalibus-Su’ul uk. 17; Sheikh Sulayman Balkhi Hanafi katika Yanabiu’l- Mawadda Sura ya 18, Muhibu’d-Din Tabari katika Riyazu’n-Nazara uk. 147 na Dhakha’iru’I-Uquba uk. 69, Sibt Ibn Jauzi katika Tadhkira Khawasu’I-Umma uk. 22, Imam Abdu’r-Rahman Nisa’i (mmoja wa Maimam wa Sihah) katika Khasa’isul-Alawi uk. 14 (ameandika hadithi sita zinazohusiana na suala hili); Ibn Kathir katika Ta’rikh-e-Kabir Juz. 5, uk. 38 na Juz. 7, uk. 357 Ibn Hajar Asqalani katika Isaba Juz. 11 uk. 509, Jalalu’d- Din Suyuti katika Durru’I-Mansur Juz. 3, uk. 208, ( katika Sherehe juu ya Aya ya kwan- za ya Bara’a) Tabari katika Jam’uI-Bayan, Juz . 10, uk. 41, (katika Sherehe ya Bara’a); Imam Tha’labi katika Tafsiri-e-Kashfu’I-Bayan, Ibn Kathir katika Tafsir Juz. 11 uk. 333; Alusi katika Ruha’l-Ma’ani Juz 3, uk. 268, yule mkaidi, Ibn Hajar Makki katika Sawa ‘iq uk. 19 Haithami katika Majma’u’z-Zawa’id Juz. 7, uk. 29, Muhammad Bin Ganji Shafi’i katika Kifayatut-Talib uk. 125 Sura ya 62 (akisimulia kutoka kwa Abi Bakr na Hafiz Abi Nu’aim na kutoka kwenye Musnad ya Hafiz Damishqi kama ilivyosimuliwa na Abi Nu’aim katika njia tofauti); Imam Ahmad Bin Hanbal katika Musnad, Juz. 1 uk 3 na 151, Juz. 3, uk. 283 na Juz IV uk. 164-5; Hakim katika Mustadrak, Juz. 2, Kitab Maghazi uk. 51 na katika Juz. 2 ya kitabu hicho hicho uk. 331; Mulla Ali Muttaqi in Kanzu’l-Ummal, Juz. 1 uk 246 mpaka 249 na Fadha’il-i-Ali Juz. 6, uk. 154.

Sababu Ya Kuteuliwa Ali.

Seyyed Abdu’l-Hayy: Kwa nini Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), ambaye vitendo vyake vina- tokana na Allah, asimpangie Ali kazi hii tangu mwanzo?
Muombezi: Kwa vile hakuna sababu juu ya ukweli huu zilizoandikwa, sisi hatujui. Lakini maoni yangu ni kwamba mabadiliko haya yamekusudiwa kuonyesha ubora wa Ali. Kwa kiwango chochote, kwa hakika inatengua lile dai la umri au uzoefu wa kisiasa kuwa ndio zilizokuwa sababu za kumuondoa Ali katika Ukhalifa. Kama Ali angeteuliwa katika kazi hii mwanzoni, lingeonekana ni jambo la kawaida, na isingewezekana kwetu sisi kuwathi- tishia ninyi ubora wa Ali.

Kama umri wa Abu Bakr na uwezo wa kisiasa vingethibitisha ubora wake asingeweza kurudishwa kwenye kazi kama hiyo. Lakini ukweli ni kwamba, kuwasilisha ujumbe wa utume ni kazi ya Mtume au Khalifa wake.

Hadithi Ya Kufuatana Ya Abu Bakr

Seyyed Abdu’l-Hayy: Kwa mujibu wa baadhi ya hadithi, Abu Huraira anasema kwamba Ali alikuwa ameagizwa kwenda Makkah pamoja na Abu Bakr kuwafundisha watu kanuni za Hijja. Ali alikuwa asome zila aya za Bara’a kwa watu. Kuwasilisha ujumbe wa utume kwa namna hii kunaashiria kwamba wote walikuwa cha cheo kinacholingana.

Muombezi: Kwanza, hii ni hadithi ya kughushi ya wafuasi wa Abu Bakr. Wengine hawakuisimulia hii. Pili, umma wote ulikubaliana kwamba Abu Bakr alirudishwa na nafasi yake ikachukuliwa na Ali. Jambo hili limesimuliwa kwa wingi sana katika vitabu vya hadithi vya madhehebu zote. Ni dhahiri, makubaliano ya umma wote ni kwamba ni lazima tutegemee kwenye zile hadithi ziliyosimuliwa kwa wingi na sahihi. Kama kuna hadithi ya peke inayotofautiana na hadithi sahihi, hiyo tuikatae.

Maoni haya yanashikiliwa na watu wote wenye msimamo na wasimuliaji. Kuteuliwa kwa Ali, kurudi kwa Abu Bakr katika hali ile ya huzuni na kukata tamaa, Mtukufu Mtume kumliwaza na kumridhisha yeye kwamba hayo yalikuwa ni matakwa ya Allah - yote haya ni mambo ya kweli ambayo yanakubalika kwa jumla.

Ushuhuda Mwingine Kwamba Umri Sio Kigezo Cha Ukhalifa:

Kuna ushahidi mwingine kwamba haki ya kipaumbele haina uhusiano wa umri. Haki ya upendeleo inapatikana katika elimu na Ucha-Mungu. Yeyote anayezidi katika elimu na Ucha-Mungu atastahiki upendeleo. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Watu wote ni wafu, lakini watu wenye elimu wako hai.”

Kwa sababu hiyo, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimpa Ali nafasi ya kwanza miongoni mwa masahaba na akasema. “Ali ndio lango la elimu.” Ni wazi kwamba lango la elimu ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) lazima awazidi wengine.

Bila shaka, wale waswahaba wengine wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) waliobakia kuwa watiifu kwake, walikuwa wote ni watu waadilifu (wema). Daima hatukatai ile nafasi ya uadilifu wa Masahaba, lakini sifa zao haziwezi kuchukua ulinganisho na sifa za lango la elimu la Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Mtukufu Mtume Alimtuma Ali Kwenda Yemen.

Wanazuoni wenu maarufu wameandika kwa kirefu juu ya Ali kutumwa kwenda Yemen kuwaongoza watu wa huko. Imam Abdu‘r-Rahman, Nisa‘i amesimulia hadithi sita kuhusu suala hili katika Khasa’isu’l-Alawi yake.

Vile vile Abu’I-Qasim Husain Bin Muhammad Raghib Ispahani katika Mahadhiratu‘l- Udaba yake Juz. 2, uk. 212 na wengine, wameandika kwamba wakati Mtukufu Mtume alipomuamuru Ali kwenda Yemen, Ali alijitetea kwamba alikuwa mdogo na alihisi namna ya uzito juu ya kuwekwa juu ya watu wazima wa kabila lake. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akajibu: “Hakika Allah atauongoza moyo wako na kuupa nguvu ulimi wako.”

Kama umri ulikuwa hitajio la kupendekezea, kwa nini basi Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mbele ya Masahaba mashuhuri na watu wazima kama Abu Bakr, alimtuma Hadhrat Ali kwenda Yemen kuwaongoza watu kule?

Baada Ya Mtukufu Mtume Ali Alikuwa Ndiye Kiongozi Wa Umma

Akizungumza na Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w.), Allah akasema katika Qur’ani Tukufu :

إِنَّمَا أَنْتَ مُنْذِرٌ ۖ وَلِكُلِّ قَوْمٍ هَادٍ {7}

Wewe ni muongozaji tu na (kuna) kiongozi kwa kila watu” (13:7)

Imam Tha’labi katika Tafsir-e-Kashfu‘I-Bayan yake; Muhammad Bin Jarir Tabari katika Tafsir yake; Muhammad Bin Yusuf Ganji Shafi’i katika Kifayatu‘t-Talib Sura ya 62, kutoka kwenye Ta’rikh-e-Ibn Asakir; Sheikh Suleyman Balkhi Hanafi katika Yanabiu‘I- Mawadda mwisho wa Sura ya 26 kutoka kwa Tha’labi, Hamwaini, Hakim, Abu’I-Qasim Haskani, Ibn Sabbagh Maliki, Mir Seyyed Ali Hamadani na Manaqib ya Khawarizmi, wakisimulia kwa idhini ya Ibn Abbas, Amiru’l-Mu’minin na Abu Buraid Aslami katika maneno tofauti, wamesimulia hadithi kumi na moja ambazo lengo lake kuu ni kwamba, wakati iliposhuka aya hiyo hapo juu, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), akiweka mkono wake juu ya kifua chake mwenyewe, alisema; “Mimi ndiye yule muonyaji.” Kisha akiweka mkono wake kwenye kifua cha Ali, akasema: “Baada yangu mimi, wewe ndiye kiongozi wa Umma. Wale watakaopokea muongozo toka kwako watakuwa ndio walioongoka.”

Njama Za Maadui

Vile vile umesema baada ya miaka 25, wakati alipokuwa Khalifa, ilikuwa kutokana na ukosefu wake wa uzoefu katika Siasa kwamba ndipo machafuko na umwagaji damu ukatokea. Sina uhakika kwamba una maana gani unaposema siasa. Kama siasa ina maana ya udanganyifu, njama na kuchanganya haki na batili (kama vile watu katika zama zote walivyofanya ili kujipatia Mamlaka), ningeweza kukiri kwamba Ali alikuwa ametolewa mbali kabisa kwenye siasa ya namna hiyo. Kwangu mimi siasa ina maana ya uadilifu na utendaji wa mamlaka halali.

Ali Alichukia Siasa Ya Dhulma - Chafu:

Ali ambaye alikuwa ni mfano wa haki, alijitenga mbali na siasa za kidhalimu. Kama nilivyosema mapema, wakati Amiru‘l-Mu’minina aliposhika ukhalifa dhahiri, mara moja aliwaengua viongozi wote wa awali na watumishi. Abdullah Ibn Abbas (binadamu yake) na wengineo wakasema: “Ingekuwa vema kama ungeiahirisha amri hii kwa siku chache, ili kwamba viongozi na magavana na majimbo waukubali ukhalifa wako. Kisha unaweza kuwauzulu.”

Imam Mtukufu akasema: “Mmenipa ushauri kuhusu siasa ya jambo hili. Lakini hamuelewi kwamba endapo nitayumbishwa na kile kinachoitwa ‘Siasa’ na nikaruhusu watawala waonevu wabaki katika nafasi zao, ingawa iwe ni kwa muda mfupi tu, ningewajibika kuulizwa mbele za Allah kwa ajili ya kipindi hicho. Wakati wa kuulizwa, ningewajibishwa kwa hilo.

Hili haliwezi kutarajiwa kwa Ali.” Ili kurejesha haki, Ali aliamuru mara moja kuuzuliwa kwa watawala waonevu. Hatua hii ilisababisha kuwepo upinzani toka kwa Mu’awiya Talha, Zubair na wengine ambao walipanga maasi na kusababisha ghasia kubwa na umwagaji wa damu katika nchi. Enyi waungwana! Hamlielewi vizuri hili jambo. Kwa vile hamkufanya uchunguzi wa suala hili, mnapotoshwa na wanapropaganda wanaodai kuwa yale maasi wakati wa ukhalifa wa Ali yalitokana na kukosa kwake kuwa na ujuzi wa siasa. La hasha. Kulikuwa na agenda zingine zikifanya kazi.

Vurugu Wakati Wa Ukhalifa Wa Amirul-Mu’minin Zilitokana Na

Uadui Dhidi Yake.

Kwanza, kwa muda wa miaka 25 watu walikuwa wameshawishiwa kumpinga Ali. Ilikuwa ni vigumu kwa hiyo kukubali uandamizi na Ukhalifa wake au kuitambua hadhi yake kubwa. Mfano wa upinzani huu ulitokea katika siku ya kwanza ya ukhalifa wake.

Mtu maarufu mmoja aliingia kwenye lango la Msikiti, na alipomuona Imam juu ya mimbari, akakemea: “Nalipofuke jicho lile ambalo linamuona Ali juu ya mimbari badala ya Khalifa Umar!”

Pili. haikuwa rahisi kwa watu wenye tamaa ya dunia kukubali uadilifu wa Ali, hasa kwa vile matamanio yao yalikwishapewa mwanya huru wakati wa Ukhalifa wa Uthman. Kwa hiyo walisimamisha upinzani dhidi yake, ili kwamba mtu ambaye angetimiza haja zao angewaza kutwaa madaraka.

Matakwa yao yalitimilizwa wakati wa Ukhalifa wa Mu’awiya. Kwa hiyo, Talha na Zubair mwanzoni walitoa kiapo cha utii kwa Ali, lakini walipoona haja zao za kutaka mamlaka hazikutimizwa, wakavunja kiapo chao na wakampinga waziwazi katika vita vya Ngamia (Jamal).

Aisha Kwa Kiasi Kikubwa Alihusika Sana Na Maasi Dhidi Ya Ali

Tatu, historia inatuambia kuhusu ni nani hasa aliyekuwa mchochezi mkuu wa machafuko kuanzia mwanzoni mwa Ukhalifa huo. Je, alikuwa ni mwingine yeyote mbali na Ummu’l- Mu’min Aisha? Hakuwa ni Aisha ambaye kulingana na kauli za wapokezi wa Sunni na Shi’ah kwa pamoja, aliyepanda Ngamia (kinyume na amri ya wazi ya Allah na Mtume wake Mtukufu kwamba akae ndani ya nyumba yake) akafika Basra na akachochea vita kubwa sana?

Unadai kwamba vita vilivyoleta madhara kwa pande zote vilitokana na Ali kukosa upeo wa kisiasa. Hii ni kauli yenye kupotosha sana. Kama Aisha asingefanya maasi dhidi yake, hakuna hata mtu mmoja ambaye angeweza kuwa na ujasiri wa kumpinga Ali, baada ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kuwa amekwishatangaza wazi kuwa “Kupigana dhidi ya Ali ni kupigana dhidi yangu.” Aisha aliwachochea watu kupigana dhidi ya Ali.

Vita Vya Ali Vya Jamal, Siffin Na Nahrwan Vilikuwa Kama Vita Vya Mtukufu Mtume Dhidi Ya Makafiri.

Vita vya Ali dhidi ya maadui na wanafiki huko Basra, Siffin na Nahrwan vilikuwa kama vile vita vya Mtukufu Mtume dhidi ya makafiri.

Sheikh: Ilikuwaje vita dhidi ya Waislamu viwe kama vita dhidi ya makafiri?

Muombezi: Ulamaa wenu mashuhuri kama Ahmad Bin Hanbal katika Musnad yake, Sibt Ibn Jauzi katika Tadhkira, Sulayman Bakhri katika Yanabiu’I-Mawadda, Imam Abdur-Rahman Nisai katika Khasa’isu’l-Alawi; Muhammad Bin Talha Shafi’i katika Matalibus- Su’ul; uhammad bin Talha Ganji Shafi’i katika Kifayatut-Talib Sura ya 37, na Ibn Abi’l-Hadid katika Sharh-e-Nahjul-Balagha wameandika kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alitabiri vita vya Ali dhidi ya “Nakisin, “Qasitin” na “Mariqin” miognoni mwao “nakisin” ilimaanisha Talha, Zubair na wafuasi wao; “Qasitin” ilimaanisha Mu’awiya na wafuasi wake, na “Mariqin” ilimaanisha Khawarij (waliojitoa) wa Nahrwan.

Wote kwa pamoja walikuwa ni waasi ambao kuuwawa kwao kulikuwa ni halali na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliamuru adhabu hiyo hiyo juu yao wakati alipobashiri mapigano ya vita hivyo.

Muhammad Bin Yusuf Ganji Shafi’i katika Kifayatut-Talib sura ya 37, amesimulia hadithi toka kwa Sa’id Bin Jabir, ambaye ameisimulia hadith hii kutoka kwa Ibn Abbas, kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimuambia Ummu Salma: “Huyu ni Ali Bin Abi Talib. Nyama yake ni nyama yangu, damu yake ni damu yangu, na yeye kwangu, ni kama Harun alivyokuwa kwa Mussa isipokuwa tu kwamba hakutakuwa na Mtume baada yangu.

Umm Salma, huyu Ali ni kiongozi wa walioamini, ni kiongozi wa Waislam, ndiye hafidhi wa elimu yangu, mshikamakamu (mwandamizi) wangu na lango la elimu. Ni Ndugu yangu katika dunia hii na Akhera, yuko nami katika sehemu iliyotukuka mno, atapigana dhidi “Nakisin” “Qasitin” na “Mariqin.”

Baada ya kusimulia hadithi hii Muhammad Bin Yusuf anasema kwamba haidthi hii inathibitisha kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa amemjulisha Ali kuhusu vita hivyo dhidi ya makundi yale matatu na kwamba alikuwa amemuamuru Ali kupigana dhidi ya makundi haya matatu.
Makhnaf Bin Salim anasemekana kwamba alisema kuwa wakati Abu Ayyub Ansari (aliyekuwa sahaba maarufu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipokuwa akienda na jeshi kupigana katika vita hivyo, alisema “Abu Ayyub! Ajabu iliyoje juu yako! Wewe ni yule yule mtu aliyepigana dhidi ya washirikina katika upande wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), lakini sasa hivi umejipinda kupigana dhidi ya Waislam!” Kisha Abu Ayyub akasema: “Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliniamuru mimi nipigane dhidi ya makundi haya matatu: nayo ni akina Nakisin, Qastin na Mariqin,”

Imam Abdu’r –Rahman Nisa’i katika Khasa‘isul’l-Alawi, hadithi ya 155, akisimulia kuto- ka kwa Abu Sa’id Khadiri na Sulayman Balhi Hanafi katika Yanabi uk. 59 (sura ya 2) kutoka kwenye Jam’u’l-Fawaid anasema kwamba Abu Sa’id amesema: “Tulikuwa tumekaa na Masahaba, tukimsubiri Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipokuwa anakuja kuelekea kwetu, tuliona kuwa bakozi ya kiatu chake imevunjika. Alibwaga kiatu chake kwa Ali, ambaye alianza kukirekebisha. Kisha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema: Hakika, kuna mmoja kati yenu ambaye atapigana kutetea tafsir halisi ya Qur’ani Tukufu kama nilivyopigana (dhidi ya Makafiri).”

Kisha Abu Bakr akasema: “Mtu huyo ni mimi?” Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema: “La” Kisha Umar akasema: “Je, ni mimi?”

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema; “La! Ni yule mtu anayerekebisha viatu vyangu. Hadithi hii inaonyesha kwamba vita vya Ali vilipiganwa kwa ajili ya tafsiri halisi ya Qur’ani Tukufu. Kwa hiyo ina maana kwamba, ghasia za watu wakati wa ukhalifa wa Ali hazikuwa kutokana na udhaifu wa kisasa wa Amiru’l-Mu’minin bali zilitokana na uadui wa wapinzani wake.

Baada Ya Mtukufu Mtume Ali Alikuwa Ndiye Bingwa Zaidi Wa Mambo

Ya Utawala

Ninyi waungwana mnaweza kuona kwamba inaelimisha zaidi kuyachunguza maagizo Ali aliyoyatuma kwa magavana wake na maofisa wa kijeshi na kiraia. Kwa mfano, zile amri na maagizo aliyotuma kwa Malik Ashtar na Muhammad Bin Abu Bakr kwa ajili ya kuitawala Misri, kwa Uthman Bin Hunaif na Abdullah bin Abbas wa Basra, na kwa Qutham bin Abbas kwa ajili ya kuiongoza Makkah ni mifano ya uongozi bora wa Umma na vile vile haki ya jamii. Nyaraka hizi ni sehemu ya Nahjul’Balagha.

Ali Alikuwa Na Elimu Ya Ulimwengu Wa Ghaib

Ukweli huu umekubaliwa wote, wafuasi wa Ali na maadui zake. Huyu Imam Mtukufu alikuwa ni Imamu’l-Muttaqin (Kiongozi wa wacha Mungu). Alikuwa na elimu kamili ya maana ya Qur’ani Tukufu. Zaidi ya hayo, alikuwa na elimu ya Ghaib.

Sheikh: Haijaniingia akilini vizuri hii kauli yako isiyoeleweka kwamba Ali alikuwa na elimu ya Ghaib. Tafadhali hebu ielezee.

Muombezi: Hakuna utata wowote ndani yake. Kupambanukiwa na Ghaib, maana yake ni kujua siri za ulimwengu (mbingu na Ardhi), ambazo zilijulikana kupitia Neema Tukufu kwa Mitume wote na waandamizi wao. Kila mmoja alipewa kiasi cha elimu ya Ghaib kama Allah alivyoona inatosheleza kwao kwa ajili ya kufikisha ujumbe Wake. Baada ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), Amiru’l-Mu’minin alijaaliwa na elimu kama hiyo.

Sheikh: Kamwe sikutegemea kama utashikilia maoni ya wale Shi’ah wakorofi. Sifa hii imezidi mno kiasi kwamba hata huyo anayesifiwa asingeikubali. Kuwa na elimu ya Ghaib ni sifa inayomhusu Allah peke yake, hakuna katika viumbe vyake anayeweza kuwa na uhusiano nayo.

Muombezi: Kuamini kwamba Mitume wakubwa, na washikamakamu wao, na watumishi wengine watukufu wa Allah walikuwa na elimu ya Ghaib hakuna chochote kinachohusiana na ukorofi. Bali hasa, ilikuwa ni moja ya sifa zao, iliyoonyesha kujitoa kwao kwa Allah. Tunao ushahidi wa wazi wa ukweli huu kutoka kwenye hadithi na Qur’ani Tukufu.

Je Elimu Ya Ghaibu Imetengwa Kwa Allah Tu?

Sheikh: Qur’ani Tukufu inapingana na kauli yako.
Muombezi: unaweza kuzzsoma Aya hizo ambazo zinapingana na kauli yangu?

Sheikh: Kuna Aya nyingi ndani ya Qur’ani Tukufu, ambazo zinaunga mkono maoni yangu. Kwa mfano, Qur’ani Tukufu inasema:“Na ziko kwake funguo za (mambo) yaliyofichikana hakuna anayezijua ila Yeye tu, na anajua yaliyomo barani na baharini, na halianguki jani ila analijua, wala punje ndani ya giza la ardhi, wala chochote cha kijani au kikavu bali yote yamo ndani ya kitabu kidhihirashacho.” (6:59)

Huu ndio ushahidi unaotosheleza sana kwamba hakuna hata mmoja ila ni Allah tu mwenye elimu ya Ghaib.

Ikiwa mtu ataamini mtu mwingine yeyote kuwa na elimu ya Ghaib, amemfanya mmoja wa viumbe Wake kuwa mshirika katika sifa za Allah. Unadai kwamba Ali alikuwa na utambuzi wa yaliyo ghaib.

Hii ina maana kwamba mbali na kumfanya kwako yeye ni mshirika katika sifa za Allah, umekifanya cheo chake kuwa ni cha juu zaidi kuliko kile cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alirudiarudia kusema: “Mimi ni mtu kama ninyi.

Allah pekee ndie aijuaye Ghaib.” Mtukufu Mtume kwa uwazi kabisa alielezea kutokuwa kwake na elimu ya Ghaib. Umeisoma Aya ya Qur’ani inayosema:

فَمَنْ كَانَ يَرْجُو لِقَاءَ رَبِّهِ فَلْيَعْمَلْ عَمَلًا صَالِحًا وَلَا يُشْرِكْ بِعِبَادَةِ رَبِّهِ أَحَدًا {110}

Waambie: Bila shaka mimi ni binaadamu tu kama nyie, ninaletewa Wahyi kwamba Mungu wenu ni Mungu Mmoja tu.....” ( 18:110).

Hii ni kwamba, yaani tofauti pekee kati yenu na mimi ni kwamba, ufunuo (Wahy) kutoka kwa Allah unakuja kwangu mimi.

Mahali pengine Allah anasema:

قُلْ لَا أَمْلِكُ لِنَفْسِي نَفْعًا وَلَا ضَرًّا إِلَّا مَا شَاءَ اللَّهُ ۚ وَلَوْ كُنْتُ أَعْلَمُ الْغَيْبَ لَاسْتَكْثَرْتُ مِنَ الْخَيْرِ وَمَا مَسَّنِيَ السُّوءُ ۚ إِنْ أَنَا إِلَّا نَذِيرٌ وَبَشِيرٌ لِقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ {188}

“Sema: Mimi sina mamlaka ya kujipa nafuu wala ya kujiondolea madhara ila kama apendavyo Allah; na kama ningejua ya Ghaib, bila shaka ningejizidishia mema mengi, wala lisingelinigusa dhara. Mimi sio lolote bali ni muonyaji na mtoaji wa habari njema kwa watu wanaoamini. (7:188)

Na tena anasema:

وَلَا أَقُولُ لَكُمْ عِنْدِي خَزَائِنُ اللَّهِ وَلَا أَعْلَمُ الْغَيْبَ{31}

Wala sikuambieni kwamba nina hazina za Allah, wala kwamba nayajua mambo ya ghaib” (11:31).

Allah anasema tena:

قُلْ لَا يَعْلَمُ مَنْ فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ الْغَيْبَ{65}

“Hakuna hata mmoja katika mbingu na ardhi anayejua yaliyoko ghaibuni ila Allah: Na hawajui ni lini watafufuliwa (27:65)

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mwenyewe alikiri kwamba alikuwa hajui ya ghaib na kwamba elimu yake ilikuwa kwa Allah pekee tu. Unawezaje kudai kamba Ali alikuwa na elimu kama hiyo?

Imani yako ni jaribio la kuukweza ubora wa Ali kuliko ule wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Je, Qur’ani Tukufu haisemi:

وَمَا كَانَ اللَّهُ لِيُطْلِعَكُمْ عَلَى الْغَيْبِ{179}

Wala hakuwa Allah ni mwenye kuwajulisha yaliyo ghaib…” (3:179).

Ni kwa msingi gani wewe unaamini kwamba kuna yeyote, isipokuwa Allah, analiye na elimu ya ghaib?

Muombezi: Utangulizi wa maelezo yako ni sahihi. Lakini umaliziaji uliochukua una makosa. Umesema kwamba mjuzi wa Ghaib ni Allah; kwamba funguo za Ghaib anazo Allah Mwenye nguvu, na kwamba kwa mujibu wa ile aya ya mwisho ya Sura ya Al-Kahf (pango), mwisho wa Mitume, Mitume wengine wote, wandamizi (warithi) wao, na Maimam watukufu walikuwa ni sawa na binaadamu wengine. Katika maumbile yao ya kimwili waliumbwa kama wengine wote.

Mambo yote haya ni kweli, na madhehebu ya Shia inayakubali yote. Pia, aya zote ulizozisoma ni za kweli hasa katika fuo lake halisi. Lakini haya maneno “Mtukufu Mtume ” kutoka kwenye Sura ya Hud yanaashiria kwa Mtume Nuhu. Aya ya 50 ya Sura ya Al-An’am (Ng’ombe) inaashiria kwa Mtume wetu aliyetukuka. Wakati makafiri walipomuuliza ni kwa nini hakukuwa na dalili zozote za yeye kuwa na hazina za Mwenyezi Mungu au elimu ya yaliyoghaib, hii ikateremshwa.

قُلْ لَا أَقُولُ لَكُمْ عِنْدِي خَزَائِنُ اللَّهِ وَلَا أَعْلَمُ الْغَيْبَ وَلَا أَقُولُ لَكُمْ إِنِّي مَلَكٌ ۖ إِنْ أَتَّبِعُ إِلَّا مَا يُوحَىٰ إِلَيَّ ۚ{50}

“Sema! Mimi siwaambii kwamba ninazo hazina za Allah, wala ninayajua ya Ghaib, wala siwaambii kwamba mimi ni malaika, sifuati lolote ila kile kilichofunuliwa kwangu .....”(6:50)

Aya hii ilikuwa ni majibu kwa ile dhana potofu kwamba matendo ya Mtume yanaweza kuathiriwa na mtazamo wa tamaa za kidunia. Na kuhusu elimu ya ghaib, tunaamini kwamba Mitume na washikamakamu wao walikuwa nayo. Siwahusishi na sifa za Allah. Lakini zawadi hii ni sehemu ya wahyi na Ilham (Wahai na msukumo kutoka kwa Allah ) ambavyo viliondoa mapazia ya ujinga toka kwenye uono wao na kufichua ukweli kwao. Nitaelezea hii kwa kirefu.

Elimu Ni Ya Namna Mbili, Ya Dhati (Ya Asili) Na Arzi (Ya Kutafuta)

Sisi Shi’ah wa madhehebu ya Imamiyya tunaamini kwamba elimu ina namna mbili: Dhati na Arzi. Elimu ya Dhati au ya asili ni makhususi kwa Allah. Tunaweza kuitambua lakini hatuwezi kuufahamu ukweli wake. Kwa njia yoyote tutakayoweza kujaribu kuieleza, elimu ya asili iko nje ya ufahamu wa wanaadamu. Arzi, au elimu ya kutafuata ni ile ambayo kwa asili yake mwanadamu hanayo, Ima awe ni Mtume au la. Anakuja kunufaika nayo baadae. Elimu hii pia ni ya aina mbili: Tahsili na ladunni. Tahsili ni ile elimu inayopatikana kwa kusoma na uzoefu.

Ikiwa mwanafunzi ataandamana na utaratibu wa kawaida wa elimu, kwa mfano, anakwenda shule na anajifunza toka kwa mwalimu wake. Kama Allah akipenda, atapata elimu kulingana na juhudi zake za ule muda atakaoutumia kwa kujifunza.

Ladunni inarejea kwenye ile elimu ambayo mtu anaipokea moja kwa moja kutoka kwa Allah. Haijifunzi kupitia kwenye herufi na maneno bali anaipokea moja kwa moja toka kwa Mwenye ukarimu wote. Allah anasema katika Qur’ani:

وَعَلَّمْنَاهُ مِنْ لَدُنَّا عِلْمًا {65}

“Na ambaye tulimfundisha elimu itokayo kwetu.” (18:65)

Shi’ah hawadai kwamba elimu ya ghaib ilikuwa ni ya asili ndani ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) au maimam au kwamba wao waliielewa kama anavyoielewa Mwenyezi Mungu. Tunachokisema ni kwamba Allah hayuko hakufungika au kuwa na mipaka.

Anaweza kutoa elimu na mamlaka kwa yeyote amtakae. Wakati mwingine hutoa elimu mwa mtu kwa njia ya mwalimu na wakai mwingine moja kwa moja kutoka kwake. Hii elimu ya kupewa moja kwa moja inaitwa elimu ya ghaib.
Sheikh: Maelezo yako ya awali ni sahihi. Lakini utashi wa ki-Ungu hauwezi kuruhusu mambo yasiyo ya kawaida kama kumpa mtu elimu ya ghaib moja kwa moja, yaani, bila ya uwakala wa mwalimu.

Muombezi: Hapana, wewe na marafiki zako mmekosea. Kwa hakika mara kwa mara, bila kujua, mnapingana na wengi wa wanazuoni wenu mashuhuri. Allah aliweka juu ya Mitume wake wote na waandamizi wao elimu ya ghaib. Chochote kilichohitajika kwao ili kutekeleza kazi zao.

Sheikh: Kwa kukabiliana na aya hizi za Qur’ani Tukufu, ambazo kwa uwazi kabisa zinakataa wazo la elimu ya ghaib ya mtu, una ushahdi gani kwa kutia nguvu hoja yako hiyo?

Muombezi: Hatuko kinyume na aya hizo za Qur’ani Tukufu. Kila aya ya Qur’ani tukufu ilishushwa kwa sababu maalum ambayo, kulingana na mazingira, ilikuwa wakati mwingine kinyume na wakati mwingine kwa hakika yake (positive).

Hii ndio maana inasemekana kwamba miongoni mwa aya za Qur’ani Tukufu, aya moja inaipa nguvu nyingine. Kwa vile makafiri mara kwa mara walidai miujiza kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), zile aya za kinyume zilizotajwa hapo juu zikashushwa. Ili kuthibitisha lengo halisi aya zenye kujihakiki pia zilshushwa ili kwamba hali iweze kueleweka.

Ushahidi Wa Qur’ani Kwamba Mitume Walikuwa Na Elimu Ya Ghaib

Sheikh: Hii ni ajabu sana. Unasema kwamba kuna ushahidi wa uhakika ndani ya Qur’an kwamba Mitume walikuwa na elimu ya ghaib. Tafadhali zisome aya hizo.

Muombezi: Usishikwe na mshangao. Wewe unazijua.

Allah Mwenye nguvu zote anasema:

عَالِمُ الْغَيْبِ فَلَا يُظْهِرُ عَلَىٰ غَيْبِهِ أَحَدًا {26}

إِلَّا مَنِ ارْتَضَىٰ مِنْ رَسُولٍ فَإِنَّهُ يَسْلُكُ مِنْ بَيْنِ يَدَيْهِ وَمِنْ خَلْفِهِ رَصَدًا {27}

لِيَعْلَمَ أَنْ قَدْ أَبْلَغُوا رِسَالَاتِ رَبِّهِمْ وَأَحَاطَ بِمَا لَدَيْهِمْ وَأَحْصَىٰ كُلَّ شَيْءٍ عَدَدًا {28}

“Ni mjuzi wa yaliyo ghaib! Hivyo hamfichulii yeyote siri zake, ila kwa Mtume ambaye amemridhia; basi kwa hakika humwekea walinzi (watembee) mbele yake na nyuma yake, ili aweze kujua (mtume) kwamba wamekwisha fikisha ujumbe wa Mola wao, na Yeye anayajua yale waliyonayo, na amedhibita idadi ya vitu vyote.” (72:26-28)

Aya hii inaonyesha kwamba Mitume watukuka wa Allah ambao wamejaaliwa na elimu ya ghaib ni wa namna yao pekee.

Pili, ile aya ya Sura ya familia ya Imran, sehemu yake ambayo umeisoma, inathibitisha hoja yangu. Aya nzima inasomeka kama ifuatavyo: Wala hakuwa Allah kuwajulisheni ya ghaib, lakini Allah humchagua katika Mitume wake yule anayempenda, kwa hiyo muamini Allah na Mtume wake, kama mtaamini na mkamcha mungu, basi mtakuja kupata malipo makubwa.” (3: 179)

Aya hizi zote zinaonyesha wazi kwamba Mitume wa Allah walipewa elimu ya ghaib. Ikiwa hakuna yeyote isipokuwa Allah, aliyekuwa na elimu ya ghaib, hiki kifungu “anachagua katika Mitume wake yule ampendaye.” Kingeuwa hakina maana yoyote. Allah anasema katika Sura ya Hud:

تِلْكَ مِنْ أَنْبَاءِ الْغَيْبِ نُوحِيهَا إِلَيْكَ ۖ مَا كُنْتَ تَعْلَمُهَا أَنْتَ وَلَا قَوْمُكَ مِنْ قَبْلِ هَٰذَا ۖ فَاصْبِرْ ۖ إِنَّ الْعَاقِبَةَ لِلْمُتَّقِينَ {49}

“Hizi ni katika habari za ghaib tunazokufunulia wewe, ulikuwa huzijui; wewe wala watu wako kabla ya hii (Qur’ani kuteremshwa). Kwa hiyo kuwa na subira, hakika mwisho (mwema) ni wa wale wamchao (Mwenyezi Mungu).” (11:49)

Katika Sura ya Shura Yeye anasema:

وَكَذَٰلِكَ أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ رُوحًا مِنْ أَمْرِنَا ۚ مَا كُنْتَ تَدْرِي مَا الْكِتَابُ وَلَا الْإِيمَانُ وَلَٰكِنْ جَعَلْنَاهُ نُورًا نَهْدِي بِهِ مَنْ نَشَاءُ مِنْ عِبَادِنَا ۚ وَإِنَّكَ لَتَهْدِي إِلَىٰ صِرَاطٍ مُسْتَقِيمٍ {52}

“Na hivyo ndivyo tulikushushia Wahiy kwa amri yetu. Ulikuwa hujui kitabu ni nini, wala imani (ni nini), lakini tumekifanya (Kitabu hiki) ni nuru, kwayo tunamuongoza tumtakaye katika waja wetu .....” (42:52)

Kama elimu ya ghaib isingekuwepo duniani, ni vipi Mitume walifichua mambo yanasio- julikana na kuwaambia watu juu ya maisha yao ya siri? Je, hakimo ndani ya Qur’ani kile Isa (a.s) alichosema kwa wana wa Israeli?

وَأُنَبِّئُكُمْ بِمَا تَأْكُلُونَ وَمَا تَدَّخِرُونَ فِي بُيُوتِكُمْ ۚ{49}

“Na niwape habari na mnachokula na kile mnachokiweka akiba katika nyumba zenu ..... (3:49)

Kama nitasoma aya zote za Qur’ani Tukufu, zinazounga mkono ukweli huu, itaweza kuchukua muda mrefu. Kiasi hiki kinaelekea kutosheleza.

Sheikh: Maelezo kama haya yanawapa moyo wapiga ramli, wabashiri, watazama viganja na watazamia vyota na waongo wengine wanaowadanganya watu na kujaza mifuko yao na pesa.

Madai Ya Kuwa Na Elimu Ya Ghaib Kupitia Njia Nyinginezo Ni Ya Uongo.

Muombezi: Imani katika kweli haielekezi kwenye matokeo mabaya: Ni ujinga wa watu unaowateka nyara. Kama Waislam wangemfuata yule mwenye elimu, kwa mujibu wa maelekezo ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), hasusan kama wasingelitelekeza lile lango la elimu kuanzia mwanzo kabisa, wasingeliweza kuangukia mateka kwa watu waovu. Qur’ani Tukufu inasema wazi: Yoyote yule amchaguaye kati ya

Mitume.” Neno mtume linaonyesha dhahiri kwamba kuna waja wataule wa Allah ambao wanapokea elimu ya ghaib moja kwa moja kutoka Kwake bila ya kupata kujifunza kupitia njia za kawaida.

Endapo mtu yoyote, ambaye sio mtume au Imam atadai kwamba anaweza kutabiri mambo ya ghaibu kwa njia ya falaki, utazamia viganja au kutupa simbi kuelezea bahati, huyo ni muongo. Waislam wa kweli, ambao wanafuata Qur’ani Tukufu kamwe hawawaamini watu kama hao, wala hawawi mawindo ya ulaghai wao kwani wanajua kwamba hawapaswi kufuata chochote ila Qur’ani Tukufu na wabebaji na wafasiri wa Qur’ani Tukufu, yaani, Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w.) na kizazi chake, ambao wanalingana na Qur’ani.

Kwa kifupi, ikiwa yeyote isipokuwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na waandamizi wake watoharifu atadai kwamba anayo elimu ya ghaibu na akasema kwamba anaweza kutabiri matukio ya baadae, yeye ni mbabaishaji, kwa njia yoyote ile atakayochukua.

Waandamizi Wa Mitume Pia Walikuwa Na Elimu Ya Ghaib.

Sheikh: Kwa vile Mitume walipokea wahyi takatifu walikuwa kulingana na kauli yako wana elimu ya Ghaib. Lakini kwani Ali naye alikuwa Mtume? Au alihusishwa na shughuli za utume ambazo kwazo alijua mambo ya ghaibu?

Muombezi: Kwanza, kwa nini unatupotosha sisi kwa kutumia maneno “kulingana na kauli yako?” Badala ya hayo kwa nini usitumie maneno “kulingana na kauli ya Allah.” Sisemi lolote kwa hiari yangu. Ninazungumzia hukumu za Qur’an Tukufu na kwa misingi ya maeleo ya mfasiri wa Qur’ani Tukufu, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), ninatoa ile maana yake halisi.

Nimewasilisha kwenu, kwa misingi ya ushahidi wa Aya za Qur’an, Mitume na manabii wa Allah walikuwa watu watukufu mno na walikuwa na elimu ya ghaib. Wanazuoni wenu wenyewe mashuhuri wameukubali ukweli huu na wamelazimika kusimulia mifano ya Mtukufu Mtume kuwa na elimu ya ghaib.
Ibn Abi’l-Hadid Mut’azali katika Sharh-e-Nahjul- Balagha Juz. 1, uk. 67 (kilichochapish- wa Misri), anaandika hadithi kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwamba alimuambia Ali: “Baada yangu, utapigana dhidi ya Nakisin, Qasistin na Mariqin.” Anasema kwamba hii ni moja ya uthibitisho wa Utume wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa sababu inatabiri wazi wakati ujao usiojulikana. Matukio yaliyotabiriwa yalitokea karibuni miaka 30 baadae, vilevile haswa kama yalivyotangulia kuelezwa.

Pili, Shi’ah hawadai kamba Amiru‘l-Mu’minin au Maimam Watukufu walikwa Mitume. Tunaamini kwamba Muhammad alikuwa ndiye Mtume wa mwisho wa Allah. Hakuna hata mmoja aliyeshirikishwa naye katika utume. Tunaamini kwamba, ikiwa yeyote angekuwa na imani kinyume na hii, basi huyo sio muumini. Bila shaka, sisi tunaamini katika ule Uimam ki-Mungu aliopewa Ali na kuwatambua (kuwachukulia) watu kumi na moja katika kizazi chake kama Maimam wetu watukufu na Waandamizi wa haki na Makhalifa wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Tunaamini kwamba Allah Mwenye nguvu zote amewajaalia wao na elimu ya ghaib kupitia kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Tunaamini kwamba uoni wa watu wa kawaida umewekewa pazia hivyo kwamba wanaweza kuona tu vitu vyenye kuonekana. Kadhalika hivyo ndio ilivyokuwa kwa mitume na mawasii ila kwamba, kulingana na wakati na mazingira, Allah, Mjuzi wa yote, aliliondoa pazia na akafichua habari muhimu kwao kutoka kwenye ulimwengu wa ghaib.

Na wakati elimu ya Ghaib ilipokuwa sio ya lazima, lile pazia liliwatenga wao pia na huo ulimwengu mwingine.

Hivyo, wakati mmoja Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Kama ningejua ya ghaib, kweli kabisa ningeweza kuwa na wingi wa mazuri.” Yaani, kwa asili hasa, alikuwa hana elimu ya ghaib. Aliijua tu wakati ambapo, kwa rehema za Allah, pazia hilo lilipofunuliwa.

Sheikh: Ni vipi na ni wapi ambapo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anawapa watu habari kuhusu ghaib?

Muombezi: Kwa kuzingatia aya ya Qur’ani ambayo kwayo tayari nimekwishairejea, wewe unamfikiria kwamba Muhammad ni mwisho wa Mitume, ni Murtaza (aliyechaguli- wa) na ni Mtume wa kweli wa Allah?

Sheikh: Hilo ni swali la ajabu. Ni dhahiri kabisa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa ndiye mchaguliwa na wa mwisho wa Mitume.

Muombezi: Basi kwa mujibu wa aya hii tukufu: “Mjuzi wa yaliyo ghaib! Hivyo habain- ishi siri zake kwa yeyote ila kwake yule ambaye anamchagua kuwa Nabii” basi Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa anayo elimu ya ghaib. Aya hii inasema wazi kwamba Allah hutoa elimu Yake ya ghaib kwa mtume wake aliyemchagua.

Sheikh: Ukichukulia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa na elimu ya ghaib, hii inahusiana vipi na madai yako kwamba Ali alikuwa na elimu hii ya ghaib pia?

Muombezi: Tena, kama ninyi watu mtachunguza kwa busara zile hadithi sahihi na Sunna za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), mtaweza kuelewa haraka sana ukweli kuhusu hili na mambo mengine mengi.

Sheikh: Kama ujuzi wetu una mpaka, kwa neema za Allah, wewe unayo akili pana na ulimi fasaha. Tafadhali tusimulie hizo hadithi zinazothibitisha kwamba Ali alikuwa na elimu ya ghaib. Kama elimu ya ghaib ni muhimu kwa mawasii wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), kusingekuwa na ubaguzi katika hali hii. Washikamakamu wote, hususan wale makhalfia wakubwa wangekuwa wanayo elimu ya ghaib, ingawa tunaona hakuna hata mmoja katika makhalifa hao aliyewahi kudai kuwa nayo. Bali, kama Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), walielezea kutokuwa na uwezo kwao wa kuijua. Kwa nini basi unamfanya Ali ni tofauti?

Muombezi: Kwanza, nilikisha kuwaambieni kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hakuna na uwezo wa kiasili wa kujua ya Ghaib. Wakati aliposema “Kama ningeyajua ya ghaib, kwa hakika ningeweza kuwa na wingi wa mema,” alimaanisha kwamba elimu ya ghaib siyo ya asili kwake, kama ilivyokuwa kwa Allah. Wakati Allah alipokuja kuliondoa pazia kutoka kwa Mtukufu Mtume, alikuja kujua mambo yaliyofichika.

Maimam Watukufu Walikuwa Ndio Makhalifa Wa Kweli Na Walikuwa

Na Elimu Ya Ghaib.

Pili, unasema kwamba, kama Ali alikuwa na elimu ya ghaib, hawa makhalifa wengine wangekuwa nayo vile vile. Tunakubaliana na wewe. Tunasema pia kwamba makhalifa wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wangekuwa na elimu zote, ya dhahiri na ya vitu visivy- oonekana.

Kwa kweli uwezo na sifa za makhalifa zingefanana hasa sawa na zile za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) katika mambo yote, isipokuwa lile jukumu la Utume lenyewe na unabii, ambalo linajumuisha uwezo wa kupokea wahyi moja kwa moja. Bila shaka unawaita makhalifa wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) watu wale ambao walichaguliwa tu kuwa hivyo na watu wachache ingawa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa amewalaani, kwa mfano, Mu’awiya.

Lakini tunasema kwamba makhalifa na mawasii wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ni wale ambao wameteuliwa kuwa makhalifa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mwenyewe, kama vile mitume waliotangulia walivyoteua mawasii wao wenyewe.

Hivyo wale makhalifa na mawasii walioteuliwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa amri ya Allah, waliziwakilisha vizuri sana sifa zake, na kwa sababu hiyo walikuwa nayo elimu ya ghaib. Wale makhalifa wa kweli walikuwa watu kumi na mbili ambao majina yao yameandikwa katika vitabu vyenu wenyewe vya hadithi. Nao ni wale wa familia ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na wanamjumuisha Ali na wale kumi na moja wa kizazi chake.

Na ukweli kwamba wale watu wengine hawakuwakuteuliwa Makhalifa unadhihirishwa na kauli yako mwenyewe, ambayo inathibitishwa na Ulamaa wenu wakubwa kwamba walikuwa mara kwa mara wakielezea kutokujua kwao kwa hata mambo ya kawaida, ukiachilia mbali kuitaja elimu ya ghaib.

Lango La Elimu.

Tatu, unaulizia ni hadithi gani inayothibitisha kwamba Amiru’l-Mu’minin Ali alikuwa nayo elimu ya ghaib, kwa kweli zipo hadithi nyingi zinazounga mkono jambo hili. Moja inaitwa “Hadithi ya Madina.” Imehadithiwa na madhehebu zote (Shia na Sunni) takriban kwa wingi sana kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema katika nyakati na matukio mengi kuhusu Ali, kwamba alikuwa ni “Lango la elimu yake.” Haya yalikuwa ndiyo maneno yake; “Mimi ni jiji la elimu na Ali ndie lango lake. Hivyo yoyote anayetaka kutafuta elimu lazima aje kwenye lango.”

Sheikh: Hadidhi hii sio sahihi kwa mujibu wa ulamaa wetu. Hata kama kuna hadithi kama hiyo, lazima itakuwa ni ya pekee, moja ya hadithi dhaifu.

Muombezi: Inasikitisha kwamba unaiita hadithi hii yenye nguvu kwamba ni simulizi iliy- opeke yake, au mojawapo ya hadithi dhaifu. Ulamaa wenu mashuhuri wamelithibitisha hii. Ungelikitazama Jam’u-l-Jawami’y cha Suyuti, Tahdhibu‘I-Ansar cha Muhammad bin Jarir Tabari, Tadhkiratu‘l-Abrar cha Seyyed Muhammad Bukhari, Mustadrak ya Hakim Nishapuri, Naqdus-Sahili cha Firuzabadi, Kanzu’l-Ummal cha Ali Muttaqi Hindi, Kifayatut-Talib cha Ganji Shafi’i, na Tadhkiratu‘l-Muzu’a cha Jamalu’d-Din Hindi. Wanaandika “Ikiwa mtu ataikataa hadithi hii atakuwa kwa hakika amekosa.” Pia katika Rauzatu’l-Nadiya cha Amir Muhammad Yamani, Bahru’l-Asanid cha Hafiz Abu Muhammad Samarqandi na Matalibus-Su’ul cha Muhammad Bin Talha Shafi’i, kwa ujumla wamethibitisha ukweli wa hadithi hii.

Hadithi hii imesimuliwa katika njia nyingi tofauti na kutoka kwenye vyanzo mbali mbali. Wengi wa Masahaba na wafuasi wameisimulia hadithi hii, pamoja na Ali, Abu Muhammad Hasan Bin Ali, mjukuu mkubwa wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), Abdullah Bin Abbas, Jabir Ibn Abdullah Ansari, Abdullah Ibn Mas’ud, Hudhaifu Bin Al-Yaman, Abdullah Ibn Umar, Anas Bin Maliki, na Amr Bin Aas.

Miognoni mwa Tabi’ in (Kizazi cha pili baada ya Masahaba) wafuatao wameisimulia hadithi hii: Imam Zainu’I-Abidin, Imam Muhammad Baqir, Asbagh Bin Nabuta, Jarir Azzabi, Harith bin Abdullah Hamdani Kufi, Sa’d Bin Ta’rifu’l-Hanzali Kufi, Sa’id Bin Jabir Asadi Kufi, Salam Bin Kuhail Hazarmi Kufi, Sulayman Bin Mihran A’mash Kufi, Asim Bin Hamza Saluli Kufi, Abdullah Bin Uthman bin Khisam al-Qari al-Makki, Abdur- Rahman Bin Uthman, Abdullah bin Asila al-Muradi, Abu Abdullah Sanabahi, na Mujahid Bin Jabir Abu’I Hajjaj al-Makhzumi al-Makki.

Mbali na Ulamaa wa Shi’ah, ambao kwa kauli moja wameikamata hadithi hii, wengi wa wasimulizi na wanahistoria wenu mashuhuri wameiandika hadithi hii. Nimeziona rejea kama mia mbili kutoka wa ulamaa wenu ambao wamesimulia hadithi hii tukufu. Nitataja baadhi ya wale Ulamaa mashuhuri na vitabu vyao.

Ulamaa Wa Sunni Ambao Wamesimulia Ile Hadithi Ya “Jiji La Elimu”

(1) Mfasiri na mwanahistoria wa karne ya tatu Muhammad Bin Jarir Tabari (kafa. 310 A.H.): Tahdhibu’I-Athar,
(2) Hakim Nishapuri (kafa 405 A.H): Mustadrak, Juz. 3, uk. 126, 128, 226
(3) Abu ‘Isa Muhammad Bin Tirmidhi (kafa 289 A.H): Sahih
(4) Jalul’d-Din Suyuti (kafa 911 A.H); Jam’u’l-Jawami’y na Jam’us-Saghir Juz. 1, uk. 374
(5) Abu’l-Qasim Sulayman Bin Ahmad Tabrani (kafa 491 A.H): Kabir na Ausat.
(6) Hafiz Abu Muhammad Hasan Samarqandi (kafa 491. A.H): Bahru’l-Asanid
(7) Hafiz Abu Nu’aim Ahmad bin Abdullah Ispahani (kafa 410 A.H): Ma’rifatu’l-Sahaba.
(8) Hafiz Abu Amr Yusuf Bin Abdullah Bin Abdu’l-Bar Qartabi (kafa 463 A.H): Isti’ab Jz.
(9) Abu’l Hasan Faqih shafi’i Ali bin Muhammad Bin Tayyib al-Jalabi Ibn Maghazili (kafa483 A.H): Manaqib
(10) Abu Shuja’ Shirwaih Hamadani Dailami (kafa 509 A.H): Firdausu’l-Akhbar.
(11) Abu’l-Muayyid Khatib Khawarizmi (kafa 568 A.H): Manaqib uk. 49 na Maqtalu’l- Husain Juz, 1. uk. 43
(12) Abu’l-Qasim bin Asakir Ali Bin Hasan Damishqi (kafa 572 A.H): Ta’rikh-e-Kabir.
(13) Abu’l-Hujjaj Yusuf Bin Muhammad Andalusi (kafa 605 A.H): Alif-Bas Juz. 1, uk, 222
(14) Abu’l-Hasan Ali Bin Muhammad bin Athir Jazari (kafa 630 A.H): Asadu’l-Ghaiba Jz.4, uk. 22
(15) Muhibu’d-Din Ahmad Bin Abdullah Tabari Shafi’i (kafa 694 A.H) Riyazu’l-Nuzra, Juz. 1, uk. 129, na Dhakha’iru’l-Uqba uk. 77
(16) Shamsu’d-Din Muhammad Bin Ahmad Dhahabi Shafi’i (kafa 748 A.H) Tadhkiratu’l- Huffaz, Juz, 4, uk 28.
(17) Badru’d-Din Muhammad Zarkashi Misri (kafa 749 A.H.): Faizu’l-Qadir Juz. 3, uk.4
(18) Hafiz Ali Bin Abi Bakr Haithami (kafa 807 A.H): Majma’u’z-Zawaid, Juz. 9, uk. 114 (19) Kamalu’d-Din Muhammad Bin Musa Damiri (kafa 808 A.H): Hayatu’l-Haiwan Juz.1, uk. 55
(20) Shamsu’d-Din Muhammad Bin Muhammad Jazari (kafa 833 A.H): Asnu’l-Matalib uk. 14
(21) Shahabu’d-Din Bin Hajar Ahmad Bin Ali Asqalani (kafa 852 A.H): Tahdhibu’l- Tahdhib Juz. 7, uk. 337
(22) Badru’d-Din Mahmud Bin Ahmad Aini Hanafi (kafa 855 A.H): Umdatu’l-Qari Juz. 7, uk. 631
(23) Ali Bin Hisamu’d-Din Muttaqi Hindi (kafa 975 A.H): Kanzu’l-Ummal, Juz. 6, uk. 156 (24) Abu’r-Ra’uf Al-Munawi Shafi’i (kafa 1031 A.H): Faizu’l-Qadir, Sharh-e-Jami’u’l- Saghir, Juz. 4, uk. 46
(25) Hafiz Ali Bin Ahmad Azizi Shafi’i (kafa 1070 A.H): Siraju’l-Mumir, Jam’us-Saghr Juz. 3. 63
(26) Muhammad Bin Yusuf Shami (Kafa 942 A.H): Subulu’l-Huda wa’l-Rishad fi Asma’I Khairu’l-Ibad.
(27) Muhammad Bin Yaqub Firuzabadi (kafa 817 A.H): Naqdus-Sahih.
(28) Imam Ahmad Hanbal (kafa 241 A.H): Mujaladab-e-Munaqab, na Musnad.
(29) Abu Salim Muhammad Bin Talha Shafi’i (kafa 652 A.H): Matalibu-s-Su’ul.
(30) Sheikhu’l-Islam Ibrahim Bin Muhammad Hamwaini (kafa 722 A.H): Fara’idus- Simtain.
(31) Shahabu’d-Din Dowlat Abadi (kafa 849 A.H ): Hidayatus-Su’ada.
(32) Alama Samhudi Seyyd Nur’d-Din Shafi’i (kafa 911 A.H): Jawahiru’l-Iqdain.
(33) Qazi Fadhl Bin Ruzbahan Shirazi: Ibta’lu’l-Batil.
(34) Nur’d-Din Bin Sabagh Maliki (kafa 855 A.H): Fusulul-Muhimma
(35) Shahabu’d-Din Bin Hajar Makki (Adui mbaya na shabiki, alikufa 974 A.H): Sawa’iq- e-Muhriqa,
(36) Jamalu’d-Din Ata’ullah muhadith-e-Shirazi (kafa 1000 A.H): Arbain
(37)Ali Qari Harawi (kafa 1014 A.H): Mirqat Sharh-e-Mishkat
(38) Muhammad Bin Ali As-Subban (kafa 1205 A.H): Is’afu’l-Raghbin.
(39) Qadhi Muhammad Bin Sukani (kafa 1250 A.H): Fawa’idu’l-Majmu’a fi’l-Ahadithi’l- Muzua.
(40) Shahabu’d-Din Seyyed Mahmud Alusi Baghdadi (kafa 1270 A.H): Tafsir-e-Ruhu’l- Ma’ani.
(41) Imam al-Ghazali:- Ihya’u’l-Ulum
(42) Mir Seyyed Ali Hamadani Faqih-e-Shafi’i: Mawaddatu’l-‘Qurba.
(43) Abu Muhammad Ahmad Bin Muhammad Asimi: Zainu’l-Fata (Sherehe juu ya Sura ‘Hal Ata’)
(44) Shamsu’d-Din Muhammad Bin Abdu’r-Rahman Sakhawi (kafa 902 A.H): Maqasidu’l-Hasana.
(45) Sulayman Balkhi Hanafi (kafa 1293 A.H): Yanabiu’l-Mawadda, Sura ya 14. (46) Yusuf Sibt Ibn Jauzi: Tadhkirat-e-Khawasu’l-Umma.
(47) Sadru’d-Din Seyyed Husain Fuzi Harawi: Nuzahatu’l-Arwah. (48) Kamalu’d-Din Husain Meibudi: Sharh-e-Diwan.
(49) Hafiz Abu Bakr Ahmad Bin Ali Khatib Baghdadi (kafa 463 A.H): Ta’rikh Juz. 2, uk. 377, Juz. 4, uk 348 na Juz. 7, uk. 173.
(50) Muhammad Bin Yusuf Ganji Shafi’i (kafa 658 A.H): Kifayatut-Talib, mwishoni mwa Sura ya 58.

Baada ya kunukuu hadithi sahihi tatu kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), anasema: “Kwa kifupi, wale masahaba waliokuwa na elimu ya juu, kizazi kilichofuatia baada yao, na kile kizazi cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), wote walikiri ubora, elimu pana, na hukmu za Ali.

Ili kuwa na uhakika Abu Bakr, Umar, na Uthman na masahaba wengine waliokuwa na elimu walikuwa wakimuoma yeye kuhusu mas’ala ya kidiini na walifuata ushauri wake katika mambo ya utawala. Walikiri kwamba alikuwa hapitiki katika elimu na maarifa.

Na hadithi hi haimkadirii cha zaidi (ya alivyo) kwani cheo chake mbele ya Allah, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), na waumini ni kikubwa sana zaidi kuliko hivyo, Imam Ahmad Bin Muhamamd Bin Al-Sidiqqi Magharibi katika kuthibitisha hadithi hii tukufu ameandika kitabu, Fathu’l-Mulku’l-Ali bi Sihat-e-Hadith-e-Bab-e-Madinatu’l-Ilm. (Kilichochapishwa na Ilamiyyah Press, Misri, 1354 A.H). Kama hamjatosheka hata sasa hivi, ninaweza kuku- peni rejea zaidi.

Kusimulia Sifa Za Ali Ni Ibada

Seyyed Adil-Akhtar (Mwanachuoni, mwandishi wa vitabu, na kiongozi wa Sunni): Mara kwa mara nimeona katika hadithi kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema kwamba kusimulia sifa za Ali ni ibada. Yule mwanazuoni mkubwa, Mir Seyyed Ali Hamadani Shafi’i, anaandika katika Mawaddatu’l-Qurba yake kwamba, “Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema kwamba Malaika wanauangalia kwa makini makhususi mkusanyiko ambamo ubora na sifa za Ali zinasimuliwa.

Wanaomba rehma za Allah juu ya watu hao. Zaidi ya hayo, kusimulia hadithi za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hilo peke yake ni ibada. Hivyo, ninaomba kwamba utusimulie hadithi zenye maelezo zaidi ili kwamba mkusanyiko huu uwe ni kitovu cha ibada kamilifu zaidi.

Hadithi Ya “Mimi Ni Nyumba Ya Maarifa.”

Muombezi: Ipo hadithi ambayo kwa kweli imesimuliwa kwa mfululizo mkubwa sana. Wasimulizi wa Madhehebu zote wameisimulia. Miongoni mwa ulamaa wenu ambao wameismulia ni Imam Ahmadi Bin Hanbal (katika Manaqib, Musnad), Hakim (Mustadrak), Mulla Ali Muttaqi (Kanzu’l-Ummal Jz. 6, uk. 401, Hafiz Abu Nu’aim Isfahani (Hilyatu’l-Auliya, Juz. 1, uk. 64). Muhammad Bin Sabban Misri (Is’afu’r- Raghibin) Ibn Maghazili Faqih Shafi’i (Manaqib) Jalalu’d-Din Suyuti (Jam’us-Saghir, Jam’ul-Jawami’y na La’aliu’l-Masnua), Abu Isa Tirmidh (Sahih, Jz. 2, uk. 2140), Muhammad Bin Talha Shafi’i (Matalibus-Su’ul), Sheikh Sulayman Balkhi Hanafi (Kifayatut-Talib) Sibt Ibn Jauzi (Tadhkirat-e- Khawasu’l-Umma), Ibn Hajar Makki (Sawa ‘iq Muhriqa) Sura ya 9, Faslu ya 2, uk. 75) Muhibu’d-Din Tabari (Riyazun-Nuzra), Sheikhu’l Islam Hamwaini (Fara’idus-Simtain), Ibn Sabbagh Maliki (Fasulu’l-Muhimma) Ibn Abi’l-Hadid Mu’tazali (Sharh-e-Nahjul-Balagha) na kundi la wengine. Wanathibitisha usahihi wa hadithi hii na wamemnukuu Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akisema : “Mimi ni Nyumba ya maarifa na Ali ni lango lake, hivyo ikiwa mtu ana tamaa ya kupata elimu basi anapashwa kuja kwenye lango.

Muhammad bin Yusuf Ganji Shafi’i ametenga sura ya 21 kwa ajili ya hadithi hii. Baada kutoa vyanzo vyake na rejea zake, anatoa maoni yake binafsi juu yake. Anasema hadithi ina hadhi ya juu sana. Yaani, Allah Mtukufu ambaye ndie chanzo cha maarifa na elimu ya mambo yote na ambaye amefundisha kuhimiza mema na kukataza maovu kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ndiye ambaye pia amezitunuku zawadi hizi juu ya Ali.

Kwa hiyo, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Ali ndiye mlango wa maarifa yangu. Yaani, kama mnataka kufaidika na maarifa yangu budi mgeukie kwa Ali, ili kwamba hali halisi iweze kufichuliwa kwenu.”
Ibn Maghazili Shafi’i katika Manaqib, Ibn Asakir katika Ta’rkih yake (akiandika kutoka wka Masheikh wake mwenyewe), Khatib Khawarizmi katika Manaqib yake, Sheikhu’l- Islam Hamwaini katika Fara’id, Dailami katika Firdaus, Muhammad Yusuf Ganji Shafi’i katika Kifayatut-Talib Sura ya 58 Sheikh Sulayman Balkhi Hanafi katika Yanabiu’l- Mawadda Sura ya 14, na wengineo katika Ulamaa wenu mashuhuri wamesimulia kutoka kwa ibn Abbas na Jabir Ibn Abdullah Ansari kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akiwa amemshika Ali mkono, alisema: “Huyu ni Ali - Bwana na kiongozi wa wacha-Mungu muuaji wa makafiri.

Yeyote atakayemsaidia yeye ni mwenye kuungwa mkono, na yeyote atakayemtupa atakuwa yeye mwenyewe ametupwa.” Kisha Mtukufu Mtume akinyanyua sauti yake, akasema: “Mimi ni Jiji la elimu na Ali ni lango lake.”

Pia Shafi’i anaandika kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Mimi ni jiji la elimu, na Ali ni lango lake, hakuna aingiaye kwenye nyumba ila kupitia kwenye lango.”

Yule mtunzi wa Manaqib-e-Fakhira anasimulia kutoka kwa Ibn Abbas kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), alisema: “Mimi ni jiji la Elimu, na Ali ni lango lake. Hivyo yeyote anayetaka kupata elimu ya dini ni budi aje kwenye lango.” Kisha akasema: “Mimi ni jiji la elimu na wewe Ali ndio lango lake. Anadanganya anayefikiri kwamba atanifikia mimi kupitia njia nyingine kuliko kupitia kwako.”

Ibn ‘Abi’l-Hadid katika Sharh-e-Nahjul-Balagha yake, Abu Ishaq Ibrahim Bin Sa’da’d–Din Muhammad Hamwaini katika Fara’idus-Simtain kutoka kwa Ibn Abbas yule mashuhuri Khatib Khawarizmi katika Manaqib kutoka kwa Amr Bin Aas, Imam’I-Haram Ahmad bin Abdullah Shafi’i katika Dhakha’iru’l-Uquba, Imam Ahmad Bin Hanbal katika Musnad, Mir Seyyed Ali Hamdani katika Mawaddatu’l-Qurba, na vilevile yule mkaidi mkubwa, Ibn Hajar katika Sawa’iq-e-Muhriqa, Sura ya 9, Fasilu ya 11 uk. 75, hadithi ya 9 kutoka kwa Bazaz miongoni mwa zile hadithi arobaini ambazo ameziandika kuhusu sifa za Ali, Tabrani katika Ausat yake kutoka kwa Jabir Ibn Abdullah Ansari, Ibn Adi kutoka

kwa Abdullah Ibn Umar, Hakim na Tirmidhi kutoka kwa Ali wamesimulia kwamba Mtume wa Allah alisema: “Mimi ni Jiji la Elimu, na Ali ni lango lake. Hivyo yeyote anayetafuta elimu hanabudi kuja kupitia langoni.”

Kisha wanasema kuhusu hadithi hiyo hiyo: Watu wasioelewa wamesita kuikubali hadithi hii na wengine wao wamesema kwamba hii ni hadithi ya kughushi.

Lakini pale Hakim (Mtunzi wa Mustadrak) ambaye kauli yake mnaichukulia kuwa ni yenye nguvu, alipoyasikia mambo haya akasema: “Hakika, hadithi hii ni ya kweli.”

Ufafanuzi Wa Hadithi Ya “Lango La Elimu”

Mtunzi wa Abaqatu’l-Anwar, Allama Seyyed Hamid Husain Dihlawi Sahib, amekusanya juzuu mbili zenye kuonyesha vyanzo na usahihi wa hadithi hii. Kila moja ya juzuu hizi ina ukubwa kama juzuu yeyote ya Sahih ya Bukhari.

Sikumbuki ni vyanzo vingapi amevitaja kutoka kwa Ulamaa maarufu wa Sunni kuthibitisha kwamba wasimulizi wa haidthi hii wanafanya mfululizo wa usimuliaji usiokatika,bali ninakumbuka kiasi hiki:

Nilipokuwa ninakisoma kitabu hicho, niliomba dua kwa ajili ya mtu yule maarufu, ambaye alikuwa msomi sana na ambaye alikuwa amechukua uangalifu wake mwingi sana katika ukusanyaji wa kitabu hicho. Kitabu hicho kinathibitisha kwamba Ali alikuwa na hadhi ya kipekee miongoni mwa masahaba wa Mtukufu Mtume.

Sasa, juu ya tafadhali, hebu kuweni wakweli. Hivi ilikuwa ni sawa kuufunga mlango wa elimu ambao Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa ameufungua kwa ajili ya Umma wote? Je! Watu walihalalishwa katika kufungua mlango wa mtu wa chaguo lao, ambaye hakuwa na mahusiano yoyote na kiwango cha elimu ya Ali?

Sheikh: Tumekwishajadili vya kutosha lile jambo la kwamba hadithi hii kwa ujumla inakubaliwa na Ulamaa wetu. Hakuna shaka baadhi ya wasimuliaji wamesema kwamba ni dhaifu, ni hadithi ya peke yake, wakati wengine wametamka kwamba imesimuliwa kwa mfululizo sana. Lakini hii inahusiana nini na “elimu ya Ghaib,” ambayo Ali anafikiriwa kuwa alikuwa anayo?

Ali Alikuwa Na Elimu Ya Ghaib

Muombezi: Hivi hamkukubali mapema kwamba yule mwisho wa Mitume alikuwa ni mbora wa viumbe vyote vilivyoumbwa? Na je! Qur’ani haisemi kwamba Allah hafichui siri zake kwa yeyote “ukiacha kwa yule kati ya Mitume wake ambaye amemchagua? Allah alimuondolea pazia yeye, na akajaalia juu yake yeye elimu ya Ghaib. Hivyo, mbali na aina zingine za elimu, alikuwa nayo elimu ya Ghaib. Wakati Mtukufu Mtume aliposema, “Mimi ni jiji la elimu na Ali ni lango lake,” elimu yote ya jiji ingeweza kupatikana kupitia kwenye “lango la elimu.” Elimu kama hiyo ilichanganya pamoja na ile elimu ya ghaib.

Ali Alijua Maana Ya Dhahiri Na Ya Ndani Ya Qur’ani Tukufu

Miongoni mwa wengine, Hafiz Abu Nu-aim Ispahani katika Hilyatu’l-Auliya, Juz.1 uk. 65 Muhammad Bin Yusufu Ganji Shafi’i katika Kifayatut-Talib Sura aya 74 na Sulaiman Balkh Hanafi katika Yanabiu’l-Mawadda, Sura ya 14 uk. 74 kutoka kwenye Faslu’l-Khitab, anamnukuu Abdullah Ibn Ma’sud yule mwandishi wa wahyi akisema kama: “Hakika, Qur’ani Tukufu imeshushwa juu ya hefufi saba, herufi ambazo kila moja ina maana ya dhahiri na iliyofichika. Kwa hakika Ali anazielewa maana zote za Qur’ani, za dhahiri na ya ndani.

Mtukufu Mtume Alifungua Milango 1000 Ya Elimu Katika Moyo Wa Ali.

Ulamaa wenu wakubwa wemekiri katika vitabu vyao vya sahihi kwamba Ali alikuwa na elimu ya ghaib. Baada ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) yeye alikuwa ni Murtadha (aliyechaguliwa) miongoni mwa Umma wote. Abu Hamid Ghazali katika Kitabu chake Bayan-e-Ilm’l-Ldunni ameandika kwamba Ali alisema: “Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliweka ulimi wake kinywani mwangu. Kutoka kwenye mate ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), milango 1000 za elimu ilifunguliwa kwangu, na kutoka katika kila mlango, milango mingine 1000 ilifunguliwa kwangu.”

Yule kiongozi wenu mashuhuri, Suleyman Balkhi Hanafi katika Yanabiu’l-Mawadda Sura ya 14. uk ,7 anasimulia kutoka kwa Asbagh Ibn Nabuta ambaye amemnukuu AmruI-Mu’minin kwamba alisema: “Hakika, Mtukufu Mtume alinifundisha mimi milango 1000 ya elimu kila mlango ambao ilifungua, milango mingine 1000 kufanya milango milioni moja. Hivyo, ninajua nini kimekwisha tokea tayari na nini kitakachotokea mpaka Siku ya Hukumu.

Katika sura hiyo hiyo anasimulia, kutoka kwa Ibn Maghazili kwa idhini ya huyu wa mwisho mwenyewe, kutoka kwa Abu’s-Sabba, ambaye alisimulia kutoka Ibn Abbas, ambaye amemnukuu Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akisema: “Katika usiku wa Miraj, wakati nilipokuwa mbele za Allah, Alizungumza nami kwa siri. Kila chochote nilichojifunza, nilimfundisha Ali. Yeye ni lango la elimu yangu.”

Yule mwandishi maarufu, Mu’affaq bin Ahmad Khawarizmi, amesimulia vivyo hivyo kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa njia hii: “Jibrail aliniletea busati kutoka peponi. Nilikaa juu yake mpaka nikafikishwa karibu na Mola wangu. Kisha alizungumza nami na akaniambia mambo ya Siri. Kila nilichojifunza nilikifikisha kwa Ali. Yeye ndiye lango la elimu yangu.”

Kisha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akamwita Ali na akasema: “Ali! Kukubaliana na wewe ni kukubaliana na mimi; kukupinga wewe ni kunipinga mimi. Wewe ndio elimu ambayo inaniuganisha mimi na Umma wangu.”

Hafiz Abu Nu’aim Ispahani katika Hilyatu’l-Auliya, Mulla Ali Muttaqi katika Kanzu’l- Ummal, Juz. 6, uk. 392, na Abu Ya’la wanasimulia kutoka kwa Ibn Lahi’a, ambaye alisimulia kutoka kwa Hayy Bin Abd Maghafiri, ambae alisimulia kutoka kwa Abdu’r- Rahman, ambaye alisimulia kutoka kwa Abdullah Bin Umar, ambae alisimulia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipokuwa kwenye kitanda chake cha mauti alisema “Nileteeni ndugu yangu hapa kwangu.”
Wakati Abu Bakr alipomjia, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aligeuzia uso wake kando. Tena akasema, “Niitieni ndugu yangu hapa.” Kisha Uthman akaja, na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akamgeuzia uso pia. Baadhi ya wengine wanasimulia kwamba baada ya Abu Bakr, Umar alikuja na kisha Uthman.

Baada ya hayo, hata hivyo Ali aliitwa ndani. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akamfunika na blanket lake na akapumzisha kichwa chake juu yake.

Wakati Ali alipotoka nje, watu wakamuuliza: “Ali! Ni nini alichokuambia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)?”

Imam akasema, “Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amenifundisha milango 1000 ya elimu na kila moja ya milango hiyo una milango 1000 mingine.

Hafiz Abu Nu’aim Ahmad bin Abdullah Ipahani (kafa 430 A.H) katika Hiliyatul-Auliya yake Jz. 1, uk. 65, akiandika kuhusu sifa za Ali, Muhammad Jazari katika Asnu’l-Matalib uk. 14, na Muhammad bin Yusuf Ganji Shafi’i katika Kifayatut-Talib, sura ya 48, wamesimulia kwa vyanzo vya kuaminika kutoka kwa Ahmad Bin Imran Bin Salma Bin Abdullah kwamba alisema: “Tulikuwa pamoja na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wakati alipoulizia kuhusu Ali Bin Abi Talib. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisiema: “Maarifa yamegawanywa katika sehemu kumi, ambazo tisa zilipewa Ali na moja ilitolewa kwa wanadamu wote.

Pia Mua’ffaq Bin Ahmad Khawarizmi katika Manaqib, Mullah Ali Muttaqi katika Kanzu’l-Umal Juz. 6, uk. 156 na 401 kutoka kwa wanazuoni wengi maarufu, Ibn Maghazili Faqih Shafi’i katika Faza’il na Sulayman Balkhi katika Yanabiu’l-Mawadda kwa vyanzo hivyo hivyo kutoka kwa mwandishi wa Wahyi, Abdullah bin Mas’ud, Muhammad Bin Talha Shafi’i katika Matalibus-Su’ul uk. 14 na wengineo wengi wanasimulia kutoka kwa Hulays Bin ‘Alqama kwamba wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipoulizwa kuhusu Ali alisema:

“Maarifa yamegawanywa katika sehemu kumi ambazo kati ya hizo, tisa amepewa Ali na wanadamu wote wamepata sehemu moja. Katika hiyo sehemu moja, fungu la Ali pia lilikuwa ndio kubwa.”

Pia katika Yanabiu’l-Mawadda, sura ya 14, imesimuliwa kutoka kwenye Sharh-e-Risala Fathu’l-Mubin cha Abu Abdullah Muhammad Bin Ali al-Hakim Tirmidhi kwamba Abdallha Bin Abbas alisimulia hadithi ifuatayo: “Elimu ina sehemu kumi. Sehemu tisa ni za Ali peke yake, na ile ya kumi iliyobakia ni ya wanadamu wote. Katika hiyo sehemu moja pia, Ali aligaiwa fungu kubwa zaidi.”

Pia Muttaqi Hindu katika Kanzu‘l–Ummal Juz. 6, uk. 153, Khatib Khawarimi katika Manaqib, uk 49, na Maqtalu’l- Husain, Juz. 1, uk. 43, Dailami katika Firdausu’l-Akhbar, na Sulayman Balkhi katika Yanabiu’l-Mawadda, sura ya 3, anamuelezea Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwamba alisema; “Baada yangu mimi, miongoni mwa Umma wote, mtu mwenye elimu na hekima zaidi ni Ali Bin Abi Talib.”

Kuikabidhi Elimu Ya Mtume Kwa Ali.

Hatusemi kwamba Ali Bin Abi Talib na hawa watu kumi na moja wa Kizazi chake, hawa Maimam, walipokea elimu moja kwa moja toka kwa Allah kupitia wahyi (ufunuo) kama ilivyokuwa kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Lakini tunaamini kwamba huyu wa mwisho katika Mitume wa Allah alikuwa ndio kitovu cha rehma za Allah. Faida yoyote wanayoipata viumbe inatoka kwa Allah Mwenye uwezo, kupitia kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)

Kwa hiyo elimu yote, pamoja na matukio muhimu ya wakati uliopita na ujao, yalifanywa yafahamike kwao wakati wa uhai wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Elimu nyingine ilikabid- hiwa kwao na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wakati alipokuwa karibu na kuiaga dunia hii.

Maulamaa wenu wamesimulia hadithi kutoka kwa Ummu’l-Mu’minin Aisha kuhusu nukta hii. Mwisho wa hadithi hii yeye alisema: “Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimwita Ali na akamkumbatia na akamfunika kichwa chake na shuka. Nilichomoza kichwa changu mbele na nikajajribu sana kuwasikiliza, lakini sikuweza kuelewa chochote. Wakati Ali aliponyanyua kichwa chake, paji la uso wake lilifunikwa na kijasho chembamba. Watu wakamwamba, Ali Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amekwambia nini kwa muda mrefu wote huo?

Kisha Ali akasema: ‘Hakika Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amenifundisha milango 1000 ya elimu, kila mmoja ambao ulifungua milango mingine 1000.’ Katika siku za mwanzoni za Utume wake (kama nilivyotaja katika mikesha iliyopita)

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliandaa chakula kwa watu arobaini katika ndugu zake wa karibu kwenye Nyumba ya Abu Talib. Baada ya kutangaza Utume wake, Ali alikuwa wa kwanza kutangaza imani yake. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimshika katika mikono yake na akamtemea mate yake mdomoni mwake. Ali baadae alisema kuhusu tukio hili “Mara tu baada ya hili, chemchemi za maji ziliibuka ndani ya kifua changu.” Ulamaa wenu mashuhuri, wenyewe wamesimulia kwamba wakati akitoa hotuba, Imam aliashiria kwenye maana hiyo hiyo akasema; “Niulizeni mimi juu ya lile msilolielewa kabla sijafa. Kifua changu ni hifadhi ya elimu isiyo na mpaka.” Kisha akiashiria kidole kwenye tumbo lake akasema, “Hii ni ghala ya elimu, haya ni mate ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), hiki ndicho Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alichonilisha mimi kama nafaka.”

Muda wote wa maisha yake ya ukubwani Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alitoa elimu na neema kwa Ali katika njia tofauti. Kila elimu Allah aliyompa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), Mtume aliweka ndani ya kifua cha Ali.

Jafr-E-Jami’a Na Asil Yake

Moja ya vyanzo vya neema tukufu ambazo Ali alizipokea kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ilikuja kupatia Jafr-e-Jami’a, kitabu kilichojaa siri za ulimwengu. Ulamaa wenu maarufu,wenyewe wanakubali kwamba kitabu hiki na elimu maalum ni miongoni mwa neema adimu kwa Ali na Maimam watukufu.

Hujjatu’l-Islam Abu Hamid Ghazali ameandikwa kwamba, “Kuna kitabu kutoka kwa bwana na kiongozi wa wachamungu Ali Bin Abi Talib. Jina lake ni Jafar-e-Jam’ud-Dunia wa’l-Akhira. Kitabu hicho kinazo sayansi zote, ukweli na mambo yaliyofumbika, mambo ya ghaib, asili ya vitu na athari zake, asili ya majina na herufi, ambavyo hakuna anayevi- fahamu isipokuwa Ali na watu kumi na moja wa kizazi chake. Ukweli ni kwamba wamerithi kitabu hiki kutoka kwa baba zao.”

Kadhalika, Sulayman Balkhi katika Yanabiu’l-Mawadda, uk. 403, anatoa maelezo marefu kuhusu kitabu hicho, kutoka kwa Muhammad Bin Talha Shafi’i kwenye kitabu chake Durru’l-Munazzam. Anasema kwamba Jafr-e-Jami’a, kina funguo za elimu, kina kurasa 1,700 na ni mali ya Ali Bin Abi Talib pekee.

Pia imeandikwa katika Ta’rikh-e-Ningaristan kutoka kwenye Shar-e-Mawaqif kwamba Jafr na Jami’a ni vitabu viwili ambayo ni mali ya Ali pekee. Vinaelezea, kupitia elimu ya hefufi, matukio yote mpaka mwisho wa dunia. Kizazi chake vile vile, kinatabiri kwa msin- gi wa vitabu hivyo.

Nawab: Tafadhali tupatie habari zaidi kuhusu kitabu hiki cha Jafr.

Muombezi: Katika mwaka wa kumi Hijiria, wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliporudi kutoka Hijja yake ya mwisho, Jibril alimjia na kufahamisha juu ya kifo chake. Kisha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alinyanyua mikono yake juu na akasema, “Ewe Mungu Wangu! Umeniahidi mimi; nawe kamwe si mwenye kurudi nyuma juu ya neno Lako.”

Jibu kutoka kwa Allah likaja: “Mchukue Ali pamoja na wewe, na mkiwa mmekaa juu ya milima ya Uhud, na migongo yenu ikielekea kibla, waite wanyama wa porini. Wataitikia wito wako. Miongoni mwao atakuwepo mbuzi mwekundu, mwenye pembe kubwa. Muamuru Ali amchinje na kumchuna ngozi yake na uigeuze nje ndani. Itaonekana ikiwa imekaushwa.

Kisha Jibril atakuja na kalamu na wino, ambao utakuwa tofauti na wino wa duniani. Mwambie Ali aandike kile Jibril atakachosema. Maandishi hayo pamoja na hiyo ngozi vitadumu hasa katika hali hiyo hiyo na kamwe haitaoza. Daima itabakia salama. Kila itakapofunuliwa itakutwa ni safi” Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikwenda kwenye vilima vya Uhud na akatekeleza maagizo yale matukufu. Jibril alikuja na akaiweka ile kalamu na wino mbele ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), ambaye alimuamuru Ali ajiandae kuandika.

Jibril alimsimulia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) matukio yote muhimu ya dunia naye alimuagiza Ali kuyaandika kwenye ile ngozi. Aliandika hata kwenye ngozi ya mikono na miguu.
Aliandika kila kitu ambacho kilikwisha tokea au kile ambacho kingetokea hadi Siku ya Hukumu. Aliandika majina ya wanae ambao walikuwa hawajazaliwa, na vizazi vyao na majina ya marafiki na maadui zao. Aliandika vile vile kila kile ambacho kingewatokea kila mmoja wao hadi Siku ya Hukumu.

Kisha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akakitoa kile kitabu na elimu ya Jafr kwa Ali na akakifanya ni sehemu ya urithi wa Uimam. Kila Imam kwa zama, alikikabidhi kwa wasii wake.

Hiki ni kitabu kile kile ambacho Abu Hamid Ghazali kuhusu hicho anasema: Jafr-e-Jami’a ni kitabu ambazo kwa jumla ni mali ya Ali na watu kumi na mmoja kwa kizazi chake. Kina kila kitu.”

Nawab: Inawezekana vipi kwamba mambo yote ya dunia yawe ni ya kuandikwa kwenye ngozi ya mbuzi?

Muombezi: Kwanza, hadithi yenyewe inaonyesha kwamba haikuwa ni mbuzi wa kawaida. Alikuwa ni mbuzi mkubwa ambaye aliumbwa kwa madhumuni haya.

Pili, kilichokuwa kimeandikwa hakikuwa ni maandishi ya kwenye vitabu vya kawaida. Kiliandikwa kwa herufi na alama za siri.

Nimekwisha kuwaambieni kwamba mwandishi wa Ta’rikh-e- Nigaristan ameeleza kutoka Sharh-e-Mawaqif kwamba Jafr na Jami’a vina herufi za kialfabeti ambazo kupitia kwazo habari hufichuliwa.

Kisha Mtukufu Mtume wa Allah (s.a.w.w.) alikabidhi ufunguo wa siri hii kwa Ali, ambaye, kwa amri ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), aliikabidhi kwa warithi wake, hao Maimam watukufu.

Ni yule tu ambaye anamiliki funguo hiyo ndiye anaweza kusoma siri za kitabuni humo. Vinginevyo mtu hana uwezo wa kujua chochote cha ghaib. Kwa mfano, Mfalme anampa alama za kutambua siri waziri wake, au viongozi ambao anawatuma majimboni.

Ikiwa ufunguo wa kuzielewa alama hizo unabakia na mfalme au mawaziri, basi hakuna mtu angeweza kutambua maandishi yale yalikuwa na maana gani. Kwa namna hiyo hiyo, haku- na yoyote isipokuwa Ali na wale kumi na mmoja wa kizazi chake, anayeweza kukielewa kitabu cha Jafr-e-Jami’a.

Siku moja Amirul-Mu’minin alimpa kitabu hicho mwanae Muhammad Hanafiyya mbele ya wanae wote wengine wa kiume lakini hakuweza kuelewa chochote ndani yake ingawa alikuwa mtu mwenye elimu ya juu sana na mwerefu.

Nyingi ya amri walizotoa Maimam Maasumini hawa, au habari wakizozieleza, zilitoka kwenye kitabu hicho hicho. Watu hawa watukufu walielewa siri za vitu vyote na waliweza kueleza ni mateso yaliyokuwa yawapate wao, vizazi vyao na Shi’ah wao, kutoka kwenye kitabu hicho hicho. Jambo hili limeandikwa kwa kirefu katika vitabu vy Hadithi.

Imam Ridhaa Alitabiri Kifo Chake.

Maelezo kina ya makubaliano kati ya khalifa Mamun ar-Rashid Abbasi na Imam Ridha yameandikwa katika Sharhe-e-Mawaqif. Baada ya mawawasiliano ya maandishi kwa miezi sita, pamoja na vitisho vya Mamun, Imam Ridha alilazimika kukubali kuwa mrithi wa Khalifa. Mkataba uliandikwa na Mamun akauweka sahihi, ukitamka kwamba, baada ya kifo cha Mamun, Ukhalifa utahamishiwa kwa Imam Ridha.

Wakati karatasi ya mkataba ilipowekwa mbele ya Imam Ridha, yeye aliandika maoni haya yafuatayo juu yake ( Mkataba): “Mimi, Ali Bin Musa Bin Ja’far, natamka hapa kwamba mtumishi wa waumini (Mamun ur-Rashid), (Ajaaliwe kusimama imara kwenye haki na Allah amuongoze kwenye njia iliyonyooka), yeye ameitambua haki yetu, ambayo wengine hawakuitambua, hivyo ameunganisha yale mahusiano ambayo yalikuwa yametengwa, ametoa amani na kuridhika kwa wale watu ambao walikuwa wamefikwa na hofu, badala yake amewahuisha baada ya kuwa walikuwa wameshushwa hadi kwenye maangamizi; amewafanya kuwa wenye ustawi na wenye kuridhika wakati walikuwa wakiendesha maisha ya wasiwasi, ili kwamba aweze kuzipata rehma za Allah na hakika karibuni Allah atatoa malipo mazuri kwa wale, ambao wanatoa shukrani kwake na Yeye habatilishi malipo ya wakweli.
Hakika, amenifanya mimi kuwa mrithi wake na amenitwisha mimi mamlaka makubwa madhali tu niishi baada yake?”

Mwishoni mwake, Mtukufu Imam aliandika: “Lakini Jaf-e-Jami’a inasema kinyume chake, (yaani kwamba, mimi sitaishi kumzidi yeye) na mimi mwenyewe sijui ni vipi wewe na mimi tutakavyotendewa. Ni Allah pekee, anayeamuru, ambaye amri yake ni ya kweli kabisa, na ambaye ndio hakimu bora.

Sa’d Bin Mas’ud Bin Umar Taftazani katika Sharh-e-Maqasidut-Talibin fi-ilm-e-Usulud-Din, akirejea kwenye maneno “Jafr wa Jami’a” yaliyoandikwa kwa mkono wa Imam kwenye mkataba, anatoa maoni kwa undani kwamba Imam alimaanisha kwamba kwa majibu wa Jafr na Jami’a, Mamun hangeweza kuidumisha ahadi yake na dunia iliona ni nini kilichotokea. Yule kipenzi mzawa wa kizazi cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliuawa shahidi kwa njia ya kupewa sumu. Hivyo ukweli na usahili wa elimu ya Imam Mtukufu ulithibitika na ilifahamika kwa kila mmoja kwamba familia hii iliyotukuka ilikuwa na habari juu mambo yote yanayojulikana na yasiyojulikana.

Jibril Alileta Kitabu Kilichofungwa Sili (Sealed) Kwa Ajili Ya Wasii Wa

Mtukufu Mtume:

Moja ya zawadi tukufu zilizopokelewa na Ali kupitia kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ilikuwa ni kitabu kilichofungwa kilicholetwa na Jibril. Mwanachuoni mkubwa na mwana historia, Allama Abu’l-Hasan Ali Bin al-Husain Mas’ud, anayeheshimiwa na madhehebu zote anaandika katika kitabu chake Isbatu’l-Wasiyya hivi: “Jibril na Malaika waaminiwa walileta kutoka kwa Allah Muweza, kitabu kilichofungwa, kwa Mtukufu Mtume na akamwambia: ‘wale wote walioko hapa pamoja nawe, isipokuwa wasii wako, waondoke ili niweze kukupa kile Kitab-e-Wasiyya (Kitabu cha agano la mwisho)’”

Kisha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akawaamuru wale waliokuwa pale kuondoka isipokuwa Amiru’l-Mu’minin, Fatima, Hasan na Husein.

Jibril akasema: “Ewe Mtume! Allah anatuma salam Zake kwako na anasema kwamba hii ndio hati ambayo ndani yake amekufanyia ahadi na amewafanya Malaika Zake kuwa mashuhuda kwayo na kwamba Yeye Mwenye ni shahidi kwayo.”

Kisha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akaanza kutetemeka na akasema: “Salaam ni Yeye na Salaam zinatoka Kwake na Salam zinarudi Kwake.”

Akikichukua kile kitabu kutoka kwa Jibril, akakisoma na akakitoa Ali - Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Hii ni ahadi na dhamana kutoka kwa Mungu Wangu kuja kwangu. Hakika nimetekeleza kazi yangu na nimefikisha ujumbe wa Allah.”

Amirul-Mu’minin akasema: “Mama yangu na baba wawe wenye kutoa kafara maisha yao kwa ajili yako! Nami pia nashuhudia kwenye ukweli wa ujumbe huu. Masikio yangu, macho, nyama na damu vinatoa ushahidi juu ya ukweli huu.”

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akamwambia Ali: “Hapa huu ni Usia wangu kutoka upande wa Allah. Upokee na uwe wewe ni mdhamini wake mbele ya Allah. Ni juu yangu mimi kutimiza wajibu wangu.” Ali akasema: “Nitakuwa mdhamini wake, na ni juu ya Allah kunisaidia mimi.”

Katika kitabu hiki, Amiru’l-Mu’minin ametakiwa kutimiza ahadi zifuatazo; “Kuwa na uraffiki kwa marafiki wa Allah, kuwa mkali kwa maadui wa Allah. Kuwa na subira kwa maonevu, kwa subira sana kuvumilia na kuzuia hasira wakati haki zake zinapoporwa, wakati anapotukanwa na wakati anaposhambuliwa bila haki?

Amiru’l-Mu’minin akasema: “Nakipokea, na nimeridhika nacho. Ikiwa nitaonyeshwa kuvunjiwa heshima, ikiwa hadithi zitakataliwa, ikiwa hukmu za Quran Tukufu zitapuuzwa, ikiwa Ka’ba itabomolewa kusawazishwa na aradhi, na ikiwa ndevu zangu zitapakwa damu ya kichwa changu hata hivyo nitavumilia na kuwa na subira.”

Baada ya hayo, Jibril, Michael na Malaika wengine wa karibu walitangazwa kama mashahidi wa Amiru’l-Mu’minin. Kadhalika Hasan, Husein na Fatima pia walikabidhiwa wajibu huo huo.

Matatizo na hali ambazo zilikuwa ziwakabili, hayo waliyaambiwa kila mmoja wao kwa kirefu. Baada ya hapo lile agano lilifungwa kwa sili ya dhahabu ghafi na kupewa Ali.

Agano hili lina hadithi za Allah Muweza, Hadithi za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) upinzani wa wale wenye kupinga na kubadili hukmu tukufu na matukio na majanga yote yaliy- otokea baada ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Na hivi ndivyo anavyosema Allah: “Na kila kitu tumekiweka ndani ya Imam (Kiongozi) mwenye kudhihirisha yaani Ali”

Kwa kifupi, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alirithisha elimu yake kwa Ali na kwa kizazi chake Ali, Maimam Ma’sumin. Ingekuwa vinginevyo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) asingelimuita Ali “lango la elimu” na asingelisema: “Kama unataka kunufaika na elimu yangu, nenda kwenye mlango wa Ali.”

Kama Imam huyo Mtukufu asingekuwa anamiliki elimu yote Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) asingeweza kutangaza mbele ya wote, marafiki na maadui kwamba: “Niulizeni lolote mnalotaka kabla sijafa na kuwaacheni.”

Hakuna mwingine tena isipokuwa Ali tu aliyeweza kudai kamwe kuwa nayo sifa hii mwenyewe. Wakati wengine ambao waliodai kuwa na elimu walipoulizwa juu ya mambo yanayojulikana na yasiyojulikana walibaki kuaibika.

Hafidh Ibn Abdu’l-Barr Maghribi Andalusi katika kitabu Isti’ab fi Ma’rifati’l-As’hab ame- sema: “Yeyote aliyesema ‘Niulizeni mimi kabla sijafa na kuwaacheni’ alikuwa muongo isipokuwa Ali Bin Abi Talib.”

Abdul’l-Abbas Ahmad Ibn Khallikan Shafi’i katika Wafaya yake na Kitab-e-Baghdad katika Ta’rikh yake Juz. 13, uk. 163 anasimulia kwamba siku moja Maqatil Bin Sulayman, aliyekuwa mmoja wa wanazuoni mashuhuri aliyejulikana kwa uwezo wake wa kujibu maswali haraka, alitangaza mbele ya mkusanyiko wa hadhara kwamba: “Niulizeni mimi kuhusu lolote chini ya mbingu.”

Mtu mmoja alitoa swali hili kumuuliza yeye: “Ni lini Nabii Adam alipofanya Hijja? Ni nani aliyemkata nywele alipomaliza? Maqatil alitatizwa na akabakia kimya.

Mtu mwingine akamuuliza: “Je, mdudu chungu ananyonya chakula kupita tumboni au kupitia njia nyingineyo? Kama ni kupitia tumboni, liko wapi tumbo na utumbo wake?”

Maqatil aliduwaa tena. Akasema: “Allah ameliweka swali hili moyoni mwake, ili kwamba majivuno juu ya elimu yangu yaweze kuwekwa kwenye aibu.”

Ni yule tu ambaye anao uwezo wa uhakika kikamilifu wa kujibu maswali yote anayeweza kudai hivyo. Katika Umma mzima hakuna yeyote isipokuwa Ali Bin Abi Talib aliyekuwa na hadhi hiyo.

Kwa vile alikuwa “lango la elimu” ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), alikuwa na ujuzi kamili wa mambo yote, yanayojulikana na yasiyojulikana kama vile alivyokuwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Kwa hiyo, alikuwa anaweza kusema, “Niulizaeni mimi” naye akatoa majibu ya papo kwa papo na yenye kukinakisha kwa maswali yote. Miongini mwa Masahaba, vile vile, hapakuwa na mtu hata mmoja isipokuwa Ali, ambaye alitoa madai kama haya.

Imam Ahmad Bin Hanbal katika Musnad, Muwaffaq Bin Ahmad Khawarizmi katika Manaqib, yule Khwaja maarufu Sulayman Balkhi Hanafi katika Yanabiu’l-Mawadda, Baghawi katika Mu’jim, Muhibu’d-Din Tabari katika Riyazu’n-Nuzra Juz. 2, uk. 198 na Ibn Hajar katika Sawa’iq uk. 76 wamemnukuu Sa’id Bin Musayya akisema kwamba hakuna yeyote katika Masahaba, isipokuwa Ali Bin Abi Talib aliyewahi kusema: “Niulizeni mimi lolote mnalotaka.”

Tangazo La Ali La Niulizeni Mimi Na Riwaya Za Masunni.

Idadi kubwa ya ulamaa wenu mashuhuri, kama Ibn Kathir katika Tafsir yake, Juz. 4, Ibn Abdul’l-Birr katika Isti’ab, Sulayman Balkhi Hanafi katika Yanabiu’l-Mawadda, Muhiy’d-din Khawarizmi katika Manaqib, Imam Ahmad katika Musnad, Hamwaini katika Fara’id, Ibn Talha katika Durru’l-Manzum, Mir Seyyed Ali Shafi’i katika Mawaddatu’l-Qurba, Hafidh Abu Nu’aim Ispahani katika Hilyatul-Auliya, Muhammad Bin Talha Shafi’i katika Matalibus-Su’ul, Ibn Abi’l-Hadid katika Nuhju’l-Balaghah na baadhi ya wanazuoni wengineo mashuhuri wa Sunni wamesimulia pamoja na tofauti kidogo ya maneno, kutoka kwa Amir Bin Wathila, Ibn Abbas, Abi Sa’id al-Buhturi, Anas Bin Malik na Abdullah Bin Mas’ud kwamba Amiru’l-Mu’minin alitangaza kutoka kwenye Mimbar kwamba: “Enyi watu! Niulizeni mimi chochote mnachotaka kabla sijafa, hakika moyo wangu ndio ghala ya elimu yote. Niulizeni mimi kwa sababu ninayo elimu ya yale yote yaliyopita na ya yale yote yatakayokuja?

Abi Dawud katika Sunan yake uk. 356, Imam Ahmad Bin Hanbali katika Musnad Juz. 1, uk. 278, Bukhari katika Sahih Juz. 1, uk. 46 na Juz. 10, uk. 241 wamesimulia kwa mam- laka kabisa kwamba Ali alisema: “Mnaweza kuniuliza juu ya chochote mnachotaka, ninaielewa asili ya kila jambo ambalo mngeliuliza juu yake.

Madai Ya Ali Kwamba Angeweza Kuhukumu Kesi Kwa Mujibu Wa Taurati Na Vile Vile Kwa Injili.

Sheikh Sulayman Bakhi Hanafi katika Yanabuu’l-Mawadda sura ya 14, uk. 74 anasimulia kutoka kwa Mu’affaq Bin Ahmad Khawarizmi na Sheikhil-Islam Hamwaini anasimu- lia kutoka kwa Abu Sa’id Buhturi kwamba yeye (Abu Sa’id) amesema: “Nilimuona Ali juu ya Mimbar akiwa amevaa joho la Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), upanga na kilemba chake. Alikifunua kifua chake na akasema; “Niulizeni mimi chochote mnachotaka, kabla sijafa, kwa sababu kifua changu kimebeba maarifa mengi sana.

Hili ni tumbo langu ambalo ni ghala ya elimu. Haya ni mate ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), hiki ndicho Mtukufu Mtume alichonilisha kama nafaka. Ninaapa kwa Allah kwamba ikiwa zulia litatandikwa na nikakaa juu yake, hakika nitamuelekeza mfuasi wa Taurati, kwa mujibu wa Taurati. Nitamuelekeza mfuasi wa Injili kwa mujibu wa Injili mpaka Taurati na Injili, zote ziweze kuongea na kutoa ushahidi kwa yafuatayo: Ali amesema ukweli na fatwa ambayo ameitoa ni ya kulingana na kile kilichodhihirishwa ndani yetu. Wakati unapokisoma hicho kitabu huelewi kiasi hiki.

Elimu Ya Ali Kuhusu Aya Za Qur’ani Tukufu.

Sheikhul-Islam Hamwaini katika Faraid na Muayyidud-Din Khawarizmi katika Manaqib yake anasimulia kwamba huyu Imam Mtukufu alisema maneno haya kutoka mimbarini “Niulizeni mimi kuhusu nini msichokielewa kabla sijafa.

Naapa kwa Allah aliyetawanyisha nafaka na akamuumba mwanadamu, kwamba kama mtaniuliza mimi kuhusu aya yoyote, ya Kitabu kitukufu cha Allah, nitakuelezeni juu yake - lini iliposhuka, ni wakati wa mchana au usiku, kituo gani cha njiani, nyikani au mlimani, kumhusu nani iliteremshwa, muumini au dhidi ya mnafiki, nini Allah amemaanisha kwayo, na kama aya hiyo ni ya jumla au ni aya maalum.

Hapa ndipo Ibn Kawwa, Khawarij huyu, akasimama na kusema: Hebu nifahamisha ni nini anachomaanisha Allah kwa kusema, Wale walioikubali Imani na wakatenda matendo mema ndio wabora wa watu.”

Imam Mtukufu akasema: “Aya hii inaashiria kwetu na wafuasi wetu, ambao nyuso zao, mikono na miguu vitakuwa vyenye kung’ara Siku ya Kiyama. Watatambuliwa kwa vipaji vya nyuso zao.”

Imam Ahmad Ibn Hanbal katika Musnad yake na Sheikh Sulayman Balkhi katika Yanabiu’l-Mawadda sura ya 14 uk.74, wanasimulia kutoka kwa Ibn Abbas kwamba Ali alisema maneno haya akiwa mimbarini: “Niulizeni mimi kuhusu nini msichokielewa kabla sijafa. Hakuna aya ambayo kwamba siielewi zaidi kuliko mtu mwingine yeyote anavyoielewa. Ninajua ni vipi na wapi ilikoshukia. Niulizeni kuhusu ghasia yoyote, kwani hakuna ghasia ambayo kwamba simjui aliyeisababisha na ni nani aliyeuawa ndani yake.”

Ibn Sa’d katika Tabaqat Abu Abdullah Muhammad Bin Yusuf Ganji Shafi’i katika Kifayatut-Talib sura ya 52, na Hafidh Abu Nu’aim Ispahani katika Hilyatu’l-Auliya Juz. 1, uk. 68 wanasimulia kwa rejea sahihi kwamba Amirul-Mu’minin alisema: “Wallahi, hakuna aya iliyoteremshwa ila ninajua kwa uhakika ni kuhusu nani imeshushwa, na wapi ilishushwa. Hakika Allah amejaalia juu yangu moyo wenye hekima na ulimi fasaha.”

Katika vitabu hivyo hivyo imesimuliwa kwamba Amiru’l-Mu’minin alisema: “Niulizeni mimi kuhusu Kitabu cha Allah, Hakuna aya hata moja ambayo kwamba sijui iwapo kama imeshushiwa vilimani ama nyikani.”

Elimu Ya Ali Kuhusu Watu Wanaoongoza Au Wanaopotosha

Khawarizmi anasimulia katika Manaqib yake kutoka kwa A’mash, ambaye amesimulia kwamba Ubaya Bin Rab’i alisema: “Ali mara nyingi alizoea kusema ‘niulizeni kuhusu nini msichokielewa kabla sijafa, naapa kwa Mungu Wangu kwamba hakuna mbuga ya kijani au ardhi ya jangwa, au kikundi cha watu kinachopotosha watu mia moja au kuongoza watu mia moja, ila ninawajua.

Ninawajua vizuri zaidi ya yeyote wale wanaoongoza watu au wanaowachochea kwenye maovu hadi Siku ya Hukumu.”

Jalalu’d-din Suyuti katika Ta’rikhu’l-Khulafa uk. 124, Badru’d-din Hanafi katika Umdatu’l-Qari, Muhibu’d-din Tabari katika Riyazu’n-Nuzra Juz. 2, uk. 198, Suyuti katika Tafsir-e-Itqan Juz. 2, uk. 319, na Ibn Hajar Asqalani katika Fathu’l-Bari Juz. 8, uk. 485 na pia katika Tahdhibut-Tahdhib Juz. 7, uk 338 wanasimulia kwamba Ali alisema: “Niulizeni chochote mnachotaka, na ninaapa kwa Allah kwamba nitawaambia mambo yote yatakayotokea hadi Siku ya Kiyama.

Kama mtaniuliza kuhusu Kitabu cha Allah, naapa kwa Mungu Wangu kwamba hakuna aya hata moja ambayo siielewi vizuri. Ninajua iwapo kama aya ilishushwa wakati wa usiku au mchana, nyikani au katika vilima”

Anaweza mtu yeyote, isipokuwa yule mwenye elimu ya ghaib, kutoa madai kama hayo mbele ya wote, marafiki na maadui?

Kutabiri Kwamba Sinan Bin Anas Alikuwa Ndiye Muuaji Wa Imam Husain.

Ibn Abil-Hadid Mut’azali ameandika hadithi hizo hizo katika Sharh-e-Nahjul’l-Balagha Juz. 1, uk. 208 kutoka Gharat cha Ibn Hilal Saqafi. Yeye anasema kwamba mtu mmoja alisimama na akasema: “Hebu nijulishe kuhusu nywele za kichwa changu na ndevu zangu:”

Imam Mtukufu akasema: “Rafiki yangu, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alinifahamisha kwam- ba kuna malaika katika mzizi wa kila unywele wa kichwa chako nayekulaani wewe. Kuna shetani katika mzizi wa kila unywele wa ndevu zako anayekupotosha. Kuna ndama katika nyumba yako atakayemuua mtoto wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).”

Mtu huyu alikuwa ni Anas Nakh’iy, ambaye mwanae, Sinan, alikwua kitoto kidogo wakati wa utabiri wa Ali. Mnamo mwako 61 Hijiria, Sinan alifika Karbala na alikuwa mmoja wa wauaji wa Imam Husain.

Baadhi ya muhadithina wanasema kwamba yule mtu ambaye aliuliza lile swali alikwua Sa’d Bin Abi Waqas na kwamba mwanae (ndama) alikuwa ni yule mlaaniwa Umar Bin Sa’d ambaye alikuwa ndio kiongozi wa majeshi ya Yazid, mtu muhimu katika masaib ya Karbala.

Vile vile inawezekana kwamba wote wawili waliuliza swali hilo katika mikutano miwili tofauti. Simulizi hizi hata hivyo, zinaonyesha kwamba Imam Mtukufu alivuta mazingatio kwenye ukweli kwamba alikuwa anatambua mambo ya Ghaib.

Kuutabiri Ule Ushika Bendera Wa Habib Bin Ammar

Ulamaa wenu mashuhururi, kama Imam Ahmad Bin Hanbal katika Musnad na Ibn Abi’l- Hadid katika Sharh-e-Najur-Balagha, Jz. 1, uk. 208 wamesimulia kwamba wakati wa Ukhalifa wake wa dhahiri, Amirul-Mu’minina alikuwa amekaa katika msikiti wa Kufa pamoja na sahaba zake wakati mtu mmoja aliposema kwamba Khalid Ibn Uwaita alikuwa amefariki huko Wadiyu’l-Qurba.

Mtukufu Imam akasema: “Huyo hajakufa, na hatakufa mpaka aje kuwa kiongozi wa jeshi lililopotoka. Mshika bendera wake atakuwa Habib Bin Ammar.”

Kijana mmoja akasimama kutoka kwenye ule mkusanyiko na akasema: “Mimi ndiye Habib Ibn Ammar, na ni mmojawapo wa marafiki zako wakweli na waaminifu.”

Ali akasema: “Mimi sijasema uongo na kamwe sitakujasema uongo. Nipo, kama imekuwa namuona Khalid, kiongozi wa jeshi lililopotoka, na wewe ndio mshika bendera wake. Watu nyie mtaingia msikitini humu kupitia pale akiashiria kidole kwenye mlango Babu’l-fil) na kitambaa cha bendera hiyo kitachanwa na lile lango la msikiti.”

Miaka ikapita. Wakati wa Ukhalifa wa yule muovu Yazid, Ubaidullah Bin Ziyad akawa ndiye gavana wa Kufa na akatuma majeshi yenye kutisha kwenda kupigana na Imam Husain. Siku moja wengi wa wale waliousikia utabiri wa Amirul-Muuminin kuhusu juu yao Khalid na Habib Ibn Ammar, walikuwa wamekaa Msikitini humo wakati kelele za askari hao na miito yao zikisikika.

Watu hao waliona kwamba Khalid Ibn Uwaita, kiongozi wa lile jeshi lililopotoka wakienda Karbala kupigana dhidi ya mtoto wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), waliingia Msikitini humo kupitia mlango ule ule wa Babu’l-Fil kufanya onyesho. Habib Ibn Ammar alikuwa amebeba bendera. Wakati Habib alipoingia msikitini humo, kitambaa cha bendera yake kilichanwa.Wanafiki walionyeshwa ni jinsi gani elimu ya Ali ilivyokuwa nzito na jinsi ukweli wa utabiri wake ulivyokuwa.

Hivi, dalili hizi na utabiri huu havithibitishi kwamba Ali alikuwa na elimu ya ghaib? Kama utasoma kwa makini Nahju’l-Balagha ambacho ni mkusanyiko wa khutba na semi tukufu za Ali, utagundua kwamba mna utabiri mwingi wa wazi kuhusu majanga na machafuko, mambo kuhusu wafalme wakubwa, maasi ya watu wa Zanj, utawala wa wa-Mongoli, utawala wa Genghis Khan, Maelezo ya uonevu wa makhalifa na matendo yao kwa Shi’ah.”

Ibn Abil- Hadid ameyazungumzia mambo haya katika Nahjul-Balagha Juz.1, uk. 208-211. Yule Mwanazuoni mkubwa Balkhi Hanafi katika Yanabiu’l-Mawadda, vile vile ameyazungumzia jinsi Ali mara kwa mara alivyoonyesha elimu yake nzito ndani ya khutuba zake na utabiri.

Kutabiri Ukandamizaji Wa Mu’awiya

Imam huyu, Mtukufu vile vile alitabiri kwamba Mu’awiya atawashinda watu wa Kufa na atawaamuru kumkataa yeye (Ali). Kwa mfano, Mtukufu Imam alisema; Mara tu, baada yangu, mtu mwenye koo kubwa na tumbo nene atawatawaleni ninyi. Atakula kila atakachokipata, na kama hatakipata, basi atakidai. Hivyo mnapaswa mje mumuuwe yeye huyo.

Lakini kamwe hamtamuua. Hakika, mara moja atawaamrisheni kuniita mimi kwa majina maovu na kuwawekeni mbali na mimi. Hivyo ninawaruhusuni kunitukana mimi kwa sababu ni maneno ya mdomoni tu, ambayo kwangu mimi ni chanzo cha utakaso na kwenu ninyi ni ulinzi dhidi ya madhara ya mtu huyu.

Lakini, kwa vile kujitenga na chuki vinatoka moyoni, msijechukua tabia ya chuki juu yangu. Nilizaliwa katika asili ya Uislam na Umoja wa Allah na nimekuwa wa mwanzo katika mambo ya Imani na Hijra (kuhama).”

Ibn Abi’l-Hadid katika Sharh-e-Nahju’l-Balagha, na wanazuoni wenu wengine wa vyeo vya juu wanathibitisha kwamba yule mtu aliyeashiriwa hapo juu alikuwa ni Mu’awiya Bin Abu Sufyan.
Utawala wake ulipokuwa imara uliwaamuru watu kumtukana na kumkashifu Ali. Mwenendo huu mbaya uliendelea kwa miaka themanini, na Imam Mtukufu alitukan- wa kwenye misikiti, na kwenye khotuba za sala za Ijumaa.

Wakati Umar Bin Abdu-Aziz Amawi alipokuwa Khalifa, hata hivyo, aliikataza tabia hii ya kuchukiza.
Kutabiri kwa Ali juu ya mwenendo huu muovu ni ushahidi mwingine wa kuwa kwake na elimu ya ghaib. Ali alibashiri matukio mengi ambayo yalithibitishwa baada ya miaka mingi.

Kutabiri Mauaji Ya Dhu’th-Thadiyya.

Kabla ya vita vya Nahrwan, Imam Mtukufu alitabiri kuuawa kwa Makhawarij hususan ya Tazmala anayejulikana kama “Dhu’th-Thadiyya.”

Alibashiri pia kwamba kati ya Khawarij hao sio hata watu kumi watakaosalimika na kwamba kati ya wailsam sio watu zaidi ya kumi watakaouawa. Ibn Abil-Hadid na yule mwanazuoni mkubwa, Balkhi, na wengineo wamesimulia kwamba kile alichokisema Imam kilitokea kuwa kweli. Ibn Abil-Hadid katika Shar-e-Nahjul-Balagha Juz. 1, 425 anaandika hivi: “Hii ni moja ya zile hadithi, ambazo zimesimuliwa takriban kwa mfululizo mwingi. Inajulikana sana na imesimuliwa kwa mapana sana. Inachukuliwa kama moja ya miujiza ya Mtukufu Imam.”

Unaona kwa hiyo ile tofauti kubwa sana kati ya Ali na “Makhalifa’ wengine. Kama angekuwa hana elimu ya ghaib, angeweza vipi kutabiri matukio ambayo yalitokea miaka mingi baadae?

Kwa mfano, alitabiri kuuawa kwa Mitham Tammar katika mikono ya Ubaidullah Bin Ziyad, kuuawa kwa Juwairiyya na Rashid Hajari kulikofanywa na Ziyad, na kuuawa kwa Amr Bin Humuq katika mikono ya marafiki wa Mu’awiya. Alitabiri kufa shahidi kwa mwanae, Imama Husain kwa kuwaambia watu wengi vile vile

Utabiri Juu Kufa Shahidi Kwake Mwenyewe, Na Kuhusu Ibn Muljim

Alitabiri vilevile kifo chake menyewe cha kishujaa. Yeye alisema kwamba muuaji wake alikuwa Abdu’r-Rahman Bin Muljim Muradi ingawa mtu yule aliyelaaninwa alidai kuwa mwaminifu na mwenye kumuunga mkono. Ibn Kathir anaandika katika Usudu’l-Ghaiba sura ya 4, uk. 25 na wengine pia wamesimulia kwamba Ibn Muljim alikuja kwa Imam Mtukufu, mashairi yenye kumtukuza Amiru’l-Mu’minin mbele ya Masahaba. Alisema: “Wewe ndio kiongozi wa kweli, uliye huru kutokana na makosa yote na mashaka.

Wewe ni mkarimu na mpole nawe u mtoto wa wale wahenga wenye roho za simba na majasiri ambao walitambulika sana kwa ushujaa tangu mwanzo kabisa; ewe mrithi wa Mtume! Allah amekupa wewe hadhi hii na akajaalia juu yako zile sifa na umaarufu mkubwa ulioko ndani ya Qur’ani Tukufu.

Masahaba walishangazwa sana na ufasaha wake na mapenzi makali. Kisha mtukufu Imam akamjibu kwa ubeti: “Nakushauri unipende kwa moyo mweupe, ingawa ninajua wewe ni mmojawapo wa maadui zangu.”
Ibn Hajar anasema katika Sawaiq-e-Muhriqa uk. 82 kwamba Mtukufu Imam, akimjibu Ibn Muljim kwa ushairi, alisema: “Namuombea yeye kuishi, lakini yeye anataka kuniua.

Huyu rafiki wa wazi anatokana na ukoo wa Murad.” Abdu’l-Rahman akasema: Pengine ulilisakia jina langu na kwamba unalichukia jina langu hilo.”

Imam Mtukufu akasema: Laa sio hivyo, ninajua bila shaka hata kidogo kwamba wewe ni muuaji, na haitachkua muda mrefu kabla hujazipakaza ndevu zangu nyeupe na damu ya kichwa changu. Ibn Muljim akasema: “Kama hivyo ndivyo, unaweza kufanya niuawe.” Masahaba nao pia walisisitiza kwamba angeuawa.

Lakini Mtukufu Imam akasema: “Kamwe haitawezekana. Dini yangu hairuhusu hukumu ya kisasi kabla ya kutendeka hio dhambi. Ninajua kwa yakini kuwa wewe ndio muuaji wangu, lakini hukmu za dini zinahusu matendo ya dhahihri. Kwa vile bado hujatenda tendo la kidhalimo, siwezi kutoa adhabu yoyote juu yako.”

Thomas Carlyle wa Uingereza anaandika katika mfululizo wa hotuba zake za, ‘Juu ya Mashujaa,’ kwamba Ali Bin Abi Talib aliuawa kwa sababu ya uadilifu wake. Yaani ni kwamba, kama angehukumu kisasi kabla ya kutendeka hiyo dhambi, angeweza kwa haki- ka, kubakia salama. Hii ndio iliyokuwa kawaida kwa wafalme wa dunia ambao, mara moja, walimuua yeyote - hata ndugu wa karibu ambaye waemmhisi kuwa ni adui yao.

Tukio hili ni ushahidi mwingine wa ukweli kwamba hakuna yeyote mwenye elimu ya ghaib isipokuwa aliye Mtume au Imam ambaye ni Ma’sum (safika kwa maana ya kuhifadhiwa kutokana na kutokosea). Kama angekuwa mwenye kutokosea tu, kwa kule kuwa kwake mwenye kutambua hali halisi ya mambo, angeweza kusababisha ghasia.

Lakini Mtume au Imam, ambaye pia ni mwenye kutokosea, baada ya kumtambua muuaji wake, huwa hatoi adhabu kabla ya kutendeka hasa kwa hiyo dhambi. Mifano hii yote haitoshelezi kuthibitisha kwamba huyu Imam Mtukufu alikuwa ni utambuzi kamili wa matukio yajayo siku za baadaye?

Ubora Wa Ali

Sheikh Sulayman Balkhi anasimulia mwanzoni mwa Yanabiu’l-Mawadda zile beti za Amiru’l-Muminin ambazo zimechukuliwa toka kwenye Durru’l-Munazzam cha Ibn Talha Shafi’i. Mtukufu Imam alisema; “Kwa hakika, mimi ninayo elimu kamili ya vianzio vyote, na ninashutumiwa kuficha elimu ya viishilizio vyake.

Mimi ndio mfachuaji wa mambo yaliyojificha na yasiyofahamika ninayo mbele yangu kumbukumbu ya yote yaliyopita na ya wakati huu. Kwa kweli ninayo mamlaka juu ya vitu vyote, vikubwa na vidogo, na elimu yangu inazingira ulimwengu wote.

Imam Mtukufu huyu pia alisema: Ninaweza kuwabebesha ngamia sabini kwa mzigo wa sherehe ya Suratul-Fatiha (ya Qur’ani Tukufu).” Mtukufu Mtume amesema: “Mimi ni jiji la elimu na Ali ndio lango lake. Pia Allah Muweza anasema tuingie kwenye nyumba kupitia milangoni. Hivyo yeyote anayetaka kupata elimu hanabudi ya kupitia mlangoni.”

Mbali na mambo mengine, hii mifano miwili inatosha kuthibitisha ubora wa Ali dhidi ya wengine. Angepaswa, moja kwa moja, kumrithi Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kama kiongozi wa Waislam. Wakati ni ukweli unaokubalika kwamba Ali alikuwa ndio aalim mkubwa sana kuliko wote, ni kichekesho kabisa kuchukulia kwamba mtu asiyekuwa na elimu alikuwa na haki ya kushika nafasi yake.

Allah Asingeweza Kukubali Kwamba Mtu Mbora Ashikiwe

Nafasi Yake Na Mtu Duni.

Hata Ibn Abi’l-Hadid katika kitabu chake, kuhusu hotuba ya kwanza anasema: “Mtu mwenye hadhi ndogo alipewa upendeleo juu ya mtu wa hadhi iliyotukuka sana.” Kauli hii ni yeye utambuzi wa ubora wa Imam Mtukufu lakini, ukaidi wake unamlazimisha kuongeza, “Allah amekubali kwamba yule dhaifu awe badala ya yule mbora.”

Kauli hii inahuzunisha, kuja kama ilivyo, kutoka kwa mtu kama Ibn Abi’l-Hadid. Watu wote wenye burasa wataikataa. Madai yake yanapingana na uadilifu wa Allah, lakini kwa hakika Allah ni Muadilifu sana Mwenye hekima.

Hatoi kipaumbele kwa mtu dhaifu na kumruhusu kushika nafasi ya mwenye haki zaidi. Allah anasema katika Qur’ani Tukufu,

قُلْ هَلْ يَسْتَوِي الَّذِينَ يَعْلَمُونَ وَالَّذِينَ لَا يَعْلَمُونَ ۗ{9}

“Sema: wale wanaojua na wale wasiojua wanafanana? (39:9)

Tena anasema: “Hivi basi ni yule anayeongoza kwenye ukweli aliyebora zaidi kufuatwa, au yule ambaye binafsi haendi sawa labda aongozwe?”
Ibn Abi’-Hadid anakubali kwa uwazi kabisa kwamba Ali alikuwa ndio mtu hasa aliyestahi- ki Ukhalifa. Anasema katika Sharh-e-Nahjul-Balagha Juz. 1, uk. 4, “Hakika Ali alikuwa mbora kuliko binadamu wote baada ya Mtukufu Mtume wa Allah (s.a.w.w.). Kuhusu hili swala la Ukhalifa, alikuwa ndie mtu mwenye haki zaidi ya Waislam wote.”

“Jiji La Elimu” Inathibitisha Haki Ya Ali Kuwa Khalifa Wa Kwanza

Zaidi ya hayo, ile kauli yenye kueleweka vyema ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), mwishoni mwa hadithi hii, inathibitisha ubora wa Ali, ikisema: “Yule ambaye anapenda kutafuta elimu ni lazima aje kwenye mlango.” Hili neno “Mlango” hapa bila shaka ni Ali.

Hivyo ni huyu lango kuu la uongozi ambaye Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ametuamuru kum- fuata, ndiye mwenye haki zaidi au yule ambaye watu wa memchagua? Jibu liko wazi. Amri ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) lazima itiiwe. Pili, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) pia aliweka kigezo cha kipaumbele na upendeleo, ambacho ni kule kuwa na elimu ya juu zaidi.

Sheikh: Kama Ali alikuwa na haki ya kipaumbele kwa sababu ya elimu yake ya juu, Mtukufu Mtume Allah (s.a.w.w.), angetamka kwa kupambanua ili kwamba Umma ungejua kwamba utii kwake yeye ulikuwa ni wajibu. Lakini hakuna kauli ya namna hiyo inayoweza kuonekana.

Muombezi: Ninapata uchungu sana kusikia matamshi kama hayo kutoka kwako. Una bahati mbaya ya kuwa na tabia ya kukataa kila kitu - hata ukweli wa wazi - pale unapopin- gana na maoni yako. Ndugu yangu mheshimiwa. Nimekuwa nikizisimulia kauli hizo kwa mikesha kumi iliyopita.

Hadhara hii na baadhi ya magazeti ya hapa yatashuhudia ukweli wa jambo hili. Lakini bado unasema hujaona kauli ya wazi ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Hata vitabu vyenu wenyewe vya Sahih vimejaa tele matamshi ya wazi kuhusu jambo hili. Hebu ngoja nikuulize hivi: Je Umma unahitaji elimu ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na Sirat (hadithi na Suna)?

Sheikh: Hilo ni jambo la dhahiri. Masahaba wote na Umma wanahitaji uongozi, elimu na Sunna na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mpaka Siku ya Kiyama.

Muombezi: Allah akubariki! Kama ingekuwa hakuna hadithi zingine makhsusi ila Hadithi ya Madina, hata hii ingekuwa inatosha kuthibitisha nukta yangu. Mtume kwa uwazi kabisa anasema: “ Mimi ni jiji la elimu na Ali ndie lango lake, yule ambaye anataka kupata elimu hanabudi kuja kwenye mlango huu.”

Kwa Mujibu Wa Mtukufu Mtume Ali Aliwazidi Wengine Wote Katika Elimu.

Ni tamko gani linaweza kueleweka wazi zaidi ya hadithi hii ambamo Mtukufu Mtume anasema kwamba “yeyote anayetaka kupata manufaa ya elimu yangu hana budi kuja kwenye mlango wa Ali kwa sababu yeye ndie lango la elimu!” Sasa kunakaribia kucha.

Kwa usiku mzima nimekuwa wote nimekuwa nikijadili hoja hii kwa shauku kubwa na nimechukua muda wenu wote. Lakini sasa hivi umeipoza jazba yangu. Kama wahenga wako, unakataa kusikiliza, na matokeo yake, ukipuuza maelezo yangu yote yenye kukubalika, unaukataa ukweli uliodhahiri.

Ni tamko gani litakalokuwa bora kuliko hili tamko la kuhusu elimu? Hivi mtu yeyote mwenye akili timamu atatetea kumkataa mtu mwenye hekima kwa kumpendelea mtu asiye na elimu? Bila shaka jibu ni hapana, kwa hiyo, lazima ukubali hoja yangu, ambayo sio hoja yangu tu bali ni kanuni inayokubalika kwa watu wote wenye elimu: kwa vile Ali alikuwa mbora katika elimu na hekima miongoni mwa Umma wote, utii kwake ni wajibu.

Hali kadhalika, kama nilivyokwishataja, ulamaa wenu mashuhuri, kama Imam Ahmad Bin Hanbali (Musnad), Khawarizmi (Munaqab) na pia yule mkaidi, Ibn Hajar Makki katika Sawa’iq wamemnukuu Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akisema: “Katika Umma wangu, Ali Bin Abu Talib amewazidi wengine wote katika elimu.”

Hapakuwa na hata mtu mmoja miongoni mwa Masahaba aliyelingana na Ali katika elimu. Ibn Maghazili Shafi’i katika Munaqab, Muhammad Bin Talha katika Matalibus-Su’ul, Hamwaini katika Fara’id na Sheikh Sulayman Hanafi katika Yanabiu’l-Mawadda, Sura ya 14, wanasimulia kutoka kwa Kalbi kwamba yule mwanazuoni mkuu wa Umma, Abdullah Ibn Abas, alisema: “Elimu ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) inatoka kwenye elimu ya Allah, elimu ya Ali inatoka kwenye elimu ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Elimu yangu na elimu ya masahaba wote, ikilinganishwa na ya Ali, ni kama tone la maji mbele ya zile bahari saba.”

Katika Nahju’l-Balagha, khotuba ya 108, Ali anasema: “Sisi (Maimam ma’sumin) ni Mti wa Utume, ndio makazi ya salama ya ujumbe mtakatifu, mahali pa mashukio ya Malaika, migodi ya elimu na ndio vyanzo vya hekima.”

Ibn Abi’l-Hadid katika Sharh-e-Nahju’l-Balagha yake Juz. 2, uk. 236 akitoa maoni yake kuhusu khotuba hii, anasema: “Sifa hii alikuwa nayo dhahiri Mtukufu Imam kwa vile Mtume wa Allah alisema: “Mimi ni jiji la elimu na Ali ndio lango lake, yeyote anayetaka kupata elimu hana budi kuja kwenye lango hilo.”

Pia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Ali ndio hakimu bora miongoni mwenu.”

Ibn Abi’l-Hadid anaendela kusema: “Welekevu wa hukumu unahitaji aina nyingi za elimu: kiwango chake cha elimu kilikuwa ni cha juu sana kiasi kwamba hakuna yeyote aliyeweza kulingana naye. Kwa kweli hakuna yeyote aliyemkaribia. Hivyo alikuwa na haki ya kudai kwamba: “sisi ni migodi ya elimu ya vyanzo vya hekima.” Kwa hiyo baada ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hakukuwa na yeyote aliyekuwa na haki zaidi ya kudai mambo haya kwa ajili yake binafsi.”

Ibn Abdu’l-Birrr katika Isti’ab Juz. 3, uk. 38, Muhammad bin Talha katika Matalibus- Su’ul uk. 23 na Kadhi Aiji katika Mawaqif, uk. 276 wamemnukuu Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akisema: “Ali ndio hakimu bora miongoni mwenu nyote.”

Suyuti katika Ta’rikhu’l-Khulafa uk. 115, Hafidh Abu Nu’aim katika Hilyatu’l-Auliya Juz.1, uk. 65, Muhammad Jazari katika Asniu’l-Matalib uk. 14, Muhammad Bin Sa’d katika Tabaqa uk. 459, Ibn Kathir katika Ta’rikh-e-Kabir, Juz. ya 7, uk. 359, na Ibn Abdu’l’Barr katika Isti’ab Juz. 4 uk. 38, wanamnukuu Umar Ibn Khattab akisema: “Ali ndie hakimu bora miongoni mwetu.”

Imesimuliwa katika Yanabiu’l-Mawadda kwamba Ibn Talha, mwandishi wa Durru’l-Munazzam anasema: “Huna budi kujua kwamba siri zote na miujiza ya vitabu vitakatifu inakuwamo ndani ya Qur’ani Tukufu. Chochote kilichoko ndani ya Qur’ani Tukufu kimo ndani ya Suratul-Fat’ha. Chochote kilichomo ndani ya Suratul-Fat’ha kimo ndani ya aya ya Bismillah ar-Rahman ar-Rahim (kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa neema, mwenye kurehemu.).

Chochote kilichoko ndani ya aya Bismillah ar-Rahman ar-Rahim kimo ndani ya Ba (B) ya Bismillah. Kila kilicho ndani ya Ba ya Bismillah kimo ndani ya doti iliyoko chini ya Ba ya Bismillah. Ali alisema “Mimi ndio lile doti ambayo iko chini ya herufi Ba ya Bismillah.

Pia Sulayman Balkhi katika Yanbiu‘l-Mawadda anamsimulia ibn Abbas akisema “Safari moja kwenye usiku na mbaramwezi baada ya sala ya Isha, Ali, akinishika mkono alinion- gozea kwenye makaburi ya Baqi na akasema: “Abdullah! Soma” Nikaisoma aya ya Bismillah ar-Rahman ar-Rahim. Yule Imam Mtukufu aliendelea kunielezea siri na miujiza ya ile herufi ya Ba ya kwenye Basimillah mpaka mapambazuko.”

Madhehebu zote kwa pamoja kwamba kuhusiana na elimu yake ghaib na kuwa kwake ndio mrithi wa elimu ya Mitume, Ali anashikilia nafasi ya pekee miongini mwa Masahaba wote. Muhammad Bin Talha Shafi’i katika Matalibus-Su’ul, Khatib-e-Khawarizmi katika Manaqib na Sulayman Balkh Hanafi katika Yanabiu’l-Mawadda wamesimulia kutoka kwenye Durru’l-Munazzam cha Ibn Talha Halbi kwamba Ali alisema: “Niulizeni mimi kuhusu mambo ya ghaib na miujiza isiyojulikana, kwa sababu kwa kweli mimi ndio Mrithi wa elimu ya Manabii Watukufu na Mitume wa Allah.”

Pia Imam Ahmad Bin Hanbal katika Musnad, Ibn Abi’l-Hadid katika Sharh-e-Nahju’l- Balagha na Sulayman Balkhi katika Yanabiu’l-Mawadda wanasimulia kwamba Ali alitamka kutoka kwenye mimbari kwamba: “Niulizeni mimi kuhusu lile msilolielewa kabla sijafa. Ulizeni toka kwangu kuhusu njia za angani kwa sababu, kwa hakika ninajua zaidi kuhusu njia zile kuliko hizi njia za ardhini.”
Ali alifanya hivi zamani sana kabla ya kugunduliwa darubini (Telescope). Watu mara kwa mara walimuuliza yeye kuhusu maumbile ya kwenye anga naye aliyajibu maswali yao.

Maelezo Ya Kanda (Zones ) Za Angani Yanavyokubaliana Na Elimu

Ya Kisasa Ya Unajimu.

Yule mwanazuoni Mkuu wa hadithi, Sheikh Ali Ibn Ibrahim Qummi wa karne ya 3 H.A katika sherehe yake ya Sura ya Saffa (37), yule mwanazuoni mashuhuri, Sheikh Fakhru’d- Din Ibn Tarih Najafi, anayejulikana kwa ucha–Mungu wake, katika Kitabu’l-Lighat Ma’rafat-e-Majma’ul-Bahrain, kilichokusanywa takriban mika 300 iliyopita, na Allama Mullah Muhammad Baqir Majlis, katika Biharu’l-Anwar Juz. 14 wanasimulia kwamba Ali alisema: “Zile nyota zilizoko mbinguni zimejazwa miji kama dunia hii ilivyo.” Sasa tafadhali sana hebu kuwa mkweli. Wakati ule hakukuwa na fikra ya unajimu wa kisasa.

Ulimwengu uliikubali ile dhana ya Ptolem kwamba dunia ndio kitovu cha ulimwengu. Ikiwa mtu alielezea kitu kipya kuhusu maeneo ya nyota na kikaja kuthibitishwa kuwa ni kweli miaka elfu moja baadae, hutaweza kusema kwamba alikuwa na elimu ya ghaib?

Ali Alizimudu Sayansi Zote

Ukweli ni kwamba, baada ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), Ali alikuwa ndio mtu mjuzi zaidi katika falsafa, fasaha ya lugha, fiqih (sharia), unajimu, elimu ya nyota za angani Jafr (ubashiri) hisabati, ushairi, ufasaha wa uongeaji ( rhetonic) na fani ya kuandika kamusi. Katika Sayansi zote, alitoa mchango muhimu sana ambao wataalam katika nyanja hiyo wameuchukua kama msingi wa maendeleo ya zaidi.

Kwa mfano, alimuabia Abu’l-Awadu’d-Du’ali (Mwandishi ambaye kwa jumla anasadikiwa kuhusika na ugunduzi wa irabu (alama) za kiarabu cha maandishi) kwamba kulikuwa na sehemu tatu za uzungumzaji (speech) jina, kitendo, kihusishi.

Pia, aliweka kanuni za sarufi na sintaksi (upangaji na uhusishaji vipasho na maneno) ya lugha ya kiarabu na vile vile maelezo ya utamkaji na msamiati. Na kwa kupanga utamkaji sahihi kwa maandishi, aliilinda Qur’ani kutokana na tafsiri potovu baadae.

Kukiri Kwa Ibn Abi’l-Hadid Ule Ubora Wa Elimu Ya Ali.

Katika utangulizi na Sharh-e-Nahju’l-Balagha cha Ibn Abi’l-Hadid Mut’azali, utakuta jinsi mwanazuoni huyu alivyozikubali na kuzisifu sifa za Ali katika nyanja zote za elimu.

Anasema: “Nitasema nini juu ya mtu huyu ambaye kwake sifa zote zimehusishwa, ambaye ni mfano bora kwa kila taifa kufuata, na ambaye kwake, wote wanataka kujifananisha naye? Yeye kwa hakika ndiye chimbuko la sifa zote. Baada yake, yeyote aliyepata umaarufu, alinufaika kutoka kwake, kwani alifuata nyayo zake.”

Ibn Abi’l-Hadid anasema kwamba ile elimu ya wale mafaqih wakuu wanne, Abu Hanifa, Imam Malik, Imam Shafi’i, na Imam Hanbal imetokana na elimu ya Ali. Anasema “Wale masahaba walioelimika vyema katika fiqhi, waliijifunza hiyo kutoka kwa Ali.”

Nisingependa niwachukulie muda wenu mwingi kwa kunukuu zaidi kutoka kwa mwanachuoni huyu maarufu. Lakini ninawasihi mkasome ule utangulizi wake kwenye Sharh-e-Nahjul-Balagha yake. Mtaweza kugundua jinsi mwanahistoria na mwanachuoni huyu mashuhuri alivyozikubali sifa za Ali. Yeye anasema, “Suala la Ali ni la ajabu. Maishani mwake mwote hajawahi kutamka maneno haya: ‘Mimi sijui.’ Alikuwa na elimu juu ya kila jambo.’”

Mwishoni, mtunzi huyu anasema: “Ukweli huu unaweza kuhesabiwa kama moja ya miu- jiza ya Mtukufu Imam huyu. Elimu kama hii iko nje na uwezo na kuelewa kwa mwanadamu.”

Kuzaliwa Kwa Imam Husain Na Pongezi Za Malaika.

Watu walikuja kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na kumpongeza kwa kuzaliwa kwa Imam Husain. Mmoja wa watu hao akasema: “Ewe Mtukufu Mtume! Tumeona kitu cha ajabu kwa Ali.” Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akauliza, “Mmeona nini?” Yule mtu akasema: “Tulipokuja kutoa pongezi, tulizuiwa na kuambiwa kwamba Malaika 120,000 wamekuja toka mbinguni na walikuwa pamoja nawe. Tulishangazwa kuona ni vipi Ali angeweza kujua hili na vipi ameweza kuwahesabu hao.”

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akatabasamu na akamuuliza Ali ni vipi amejua kwamba Malaika wengi kiasi hicho wamekuja kwake. Imam Mtukufu akasema: “Baba yangu na mama yangu watoe muhanga maisha yao kwa ajili yako!

Kila mmoja wa Malaika aliyekuja kwako na akakusalimu wewe aliongea katika lugha tofauti. Katika kuhesabu, niliona kwamba wamezungumza katika lugha 120,000 hivyo nikajua kwamba Malaika 120,000 walikuja kwako.”

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Ewe Abu’l-Hasan! Allah akuzidishie elimu yako na staha zako.” Kisha, akiwageukia wale watu, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema:

“Mimi ni jiji la elimu, na Ali ndio lango lake. Hakuna tukio kubwa mno na dalili kubwa mno kuliko alivyo yeye. Yeye ni kiongozi wa watu, mbora wa watu, dhamana ya Allah na ghala ya elimu yake. Yeye ni ‘Ahlu-Dhikr’ (wale wanaojua) miongoni mwa wale walioashiriwa kwa maneno ya Allah: ‘Kwa hiyo waulizeni wale wanaojua kama humjui.’ Mimi ni hazina ya elimu na Ali ndio funguo yake. Kwa hiyo yeyote anayetaka kuipata hazina hii aje kwenye ufunguo.”

Kama mtaweza kuonyesha sahaba mmoja au ndugu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anayeweza kushindana na hadhi ya Ali, kwa hakika nitasalimu amri mbele yake. Lakini kama hamtaweza basi itakuwa ni wajibu wenu wa kidini kujiambatanisha wenyewe kwenye haki bila kujali dunia itafikiri nini. Kisha alinyanyua mikono yake kuelekea mbin- guni na akaomba kwa Allah:

“Ewe Allah! Kuwa shahidi yangu kwamba kwa uwazi kabisa nimeielekeza njia ya kwenye haki na nimetekeleza wajibu wanug wa kidinin.

Kukubali Ushi’ah Kwa Nawab Sahib.

Nawab: Bwana Mtukufu, kwa mikesha kadhaa iliyopita tumesikia majadiliano mengi katika majlis hizi. Baadhi yetu tulikuwa tukichambua zile hoja za majadiliano miongoni mwetu kila siku. Ninamshukuru Allah Mwenyezi, kwamba ametuonyesha njia. Zile taarifa potofu kabisa za wapinzani zilitupoteza sisi. Sasa ni wazi kwamba Shi’ah Ithna Ashari wameongoka sawa sawa.

Wote wale ambao tulikuwa tukihudhuria majilis hizi na watu wengi wa mji huu ambao wamezisoma makala za mijadala hii kwenye magazeti tumeonyeshwa ukweli kuhusu Uislam. Bila shaka wote hawawezi kutamka hadharani imani zao kwa sababu ya mahusiano yao binafsi ya shughuli zao na wapinzani, lakini wametueleza sisi kwa siri kwamba wameukubali Ushi’ah.

Lakini baadhi yetu hatuna woga na yeyote na tuko tayari kutangaza kwamba katika mikesha hii tulitaka kudhihirisha mabadiliko yetu ya utii. Hakukuwa na fursa ya kufanya hivyo. Tumezisikia hoja zako zenye mvuto na sasa imani zetu ni imara kabisa.

Tunaomba uturuhusu sasa kulivuta pazia pembeni. Acha majina yetu yaandikwe kama wafuasi wa Bwana wetu, Amiru’l-Mu’minin na hao Maimam kumi na mbili. Tafadhali tangaza kwa watu wa madhehebu ya Shi’ah kwamba sisi tu wamoja pamoja nao.

Uwe shahidi Siku ya Kiyama mbele ya mahakama tukufu ya Haki na mbele ya babu yako aliyetukuka kwamba tunayo imani kamili juu ya Maimam kumi na wawili hawa kama warithi na washika makamu (waandamizi) wa Mtukufu Mtume wa Allah (s.a.w.w.).

Muombezi: Nianayo furaha kwamba baadhi yenu mmeitambua haki. Kwa mujibu wa hadithi iliyoandikwa na Imam Ahmad Bin Hanbal kaitka Musnad yake, Ibn Abi’l-Hadid katika Sharh-e-Nahju’l-Balagha na Muhammad Bin Talha Shafi’i katika Matulibus-Su’ul, na Ibn Maghazili katika Faza’il, na Khawarzmi katika Manaqib, na Sulayman Hanafi katika Yanabiu’l-Mawadda, na wengine wengi, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ametuongoza kwenye njia hii. Alisema: “Njia ya Ali ndio njia ya kwenye ukweli.” Ninatumaini kwam- ba ndugu zangu wengine katika Uislam pia wataacha ushabiki wao.

Nawab: Tunao wingi wa shukrani kwa ufasiri wako wa mambo kwa upole na kisomi. Kuna nukta moja bado ambayo inatusumbua. Inahusu Uimam wa Maimam hawa kumi na mbili na majina yao. Katika mikesha kumi iliyopita, Amiru’l-Mu’min Ali alikuwa ndio kitovu cha mjadala wetu. Kwanza tuambie ile aya ya Qur’ani Tukufu inayothibitisha Uimam wa Maimam hawa kumi na mbili. Pili, je majina ya Maimam hawa kumi na mbili yameandikwa kwenye vitabu vyetu?

Muombezi: Ni swali muafaka na nitafurahi kulijibu lakini sasa ni karibu ya alfajir, na jibu langu haliwezi kuwa fupi sana. Kesho ni siku ya kuzaliwa (wilada) kwa mjukuu wa Mtukufu Mtume, Imam Husain na familia ya Qizilbash imeandaa tafrija katika ukumbi wa Risaldar Imambara pengine huenda nitalijibu swali lako wakati huo.

Nawab: Ninakubaliana kabisa na wewe.