read

Mkutano Wa Nane; Alkhamisi Usiku ( 1 Shaban, 1345 A.H.)

Sayyid Abdu’l-Hayy: Mheshimiwa, usiku uliopita ulichangia katika kutokuelewana miongoni mwa Waislamu.

Muombezi: Nieleze jinsi nilivyofanya hivyo.

Sayyid: Wakati unaelezea “sisi wenyewe”, uliwagawanya Waislamu kwenye makundi mawili: Waislamu na waumini. Lakini waislamu wote ni kitu kimoja na wako sawa. Wale wanaosema maneno “Hakuna mungu isipokuwa Allah na Muhammad ni Mjumbe Wake,” hao ni ndugu.

Hawapasi kutenganishwa katika makundi mawili kwa sababu hili lina mad- hara kwa Uislamu. Mashi’a wanajiita wenyewe waumini, na wanatuita sisi Waislamu. Lazima utakuwa umeona kwamba kule India Mashi’a wanaitwa waumini na Masunni wanaitwa Waislamu.

Ukweli ni kwamba ‘Uislamu na ‘Iman’ ni maneno yanayofanana kwa sababu Uislamu maana yake kukubali amri za dini. Utambuzi huu ndio ukweli wa ‘Iman.’ Umma wote umekubali kwamba Uislamu ni Iman halisi. Umekwenda kinyume na maoni ya wengi.

Tofauti Kati Ya Uislamu Na Imani

Muombezi: Kwanza, rejea yako juu ya watu wa kawaida haina maana ya watu wa umma wote kwa ujumla. Inarudi kwa watu wa kawaida wa kundi la Masunni.
Pili, maelezo yako kuhusu Uislamu na Imani sio sahihi. Sio Mashia tu wanaohitalifiana na Masunni bali hata ma-Ash’ari, Mu’tazali, Mahanafi, na Mashafii vile vile wana maoni tofauti kuhusu hilo.

Tatu, mimi kwa kweli sielewi ni kwa nini mwanachuoni kama wewe unakimbilia pingamizi zisizo na maana. Mgawanyo huu katika makundi mawili umefanywa na Allah katika Qur’ani Tukufu. Pengine umesahau lile suala linalohusiana na Masahaba wa kuliani na Masahaba wa kushotoni waliotaja katika Qur’ani Tukufu ambayo inasema: Wakaaji wa jangwani wanasema: ‘tumeamini.’ Sema: ‘Hamjaamini bali semeni, tumenyenyekea (tumesilimu); lakini imani bado haijaingia nyoyoni mwenu.’” (Qur’ani; 49:14)

Kwa hakika lazima uelewe kwamba aya hii iliteremshwa katika kuwalaumu lile kabila la jangwani la Bani Asad, ambao walikuwa Waislamu kwa majina tu. Wakati wa mwaka wa ukame, walijazana mjini Madina, na ili kupata msaada walidai kwamba wao ni waumini. Lakin nyoyoni mwao walikuwa si waumini kwa Allah na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Aya hii inathibitisha kwamba kuna makundi mawili ya Waislamu.

Waislamu waaminifu, ambao wamekubali uhalisi wa Imani, na wale ambao wanatamka imani maneno kwa mdomo tu. Katika nyanja yetu ya kijamii kundi la mwisho wanapasika na usalama na manufaa ya sheria zilizokusudiwa kwa Waislamu wote.

Lakini, kwa mujibu wa amri za Qur’ani Tukufu, hawapasiki na malipo yoyote katika akhera. Kutamka kwao kwamba hakuna mungu ispokuwa Allah na Muhammad ni Mjumbe Wake, na kujionyesha kwao katika jambo la kwamba wao ni Waislamu, hakuna maana ya kweli.

Sayyid: Umesema sawa, lakini Uislamu bila Imani hauna maana, kama vile ambavyo Imani bila Uislamu haina ubora. Allah anasema katika Qur’ani Tukufu: “Na msimwambie anayekutoleeni salamu: Wewe sio muumini......’” (Qur’ani; 4:94).

Aya hii inathibitisha kwamba lazima tumtendee mtu kwa mujibu wa mtu anavyoonekana kwa nje. Kama mtu yeyote atasema, “Hakuna mungu isipokuwa Allah na Muhammad ni Mjumbe wa Allah,” lazima tukubali imani yake. Hii yenyewe ni ushahidi mzuri kwamba Uislamu na Imani ni maneno yanayofanana.

Muombezi: Aya hii iliteremshwa kuhusiana na mtu mahususi, imma Usama Bin Zaid au Muhallam Bin Jasama-e-Laisi, ambaye inasemekana aliuwa mtu katika vita, mtu ambaye ametamka, “Hakuna mungu isipokuwa Allah.” Aliuawa kwa dhana kwamba alitamka maneno haya kwa woga. Lakini kwa vile unafikiri kwamba iko katika hali ya ujumla, sisi vile vile tunawaona Waislamu wote kuwa ni safi.

Labda kwa kweli pale tunapowaona wakikiuka ile misingi ya dini. Lakini kuna tofauti kati ya Uislamu na Imani kwa sababu kuna daraja mbali mbali za Imani. Imam Ja’far Bin Muhammad As-Sadiq anasema katika hadithi ya Umar na Zubair: “Amma kuhusu Imani kuna masharti, daraja, na hatua. Baadhi ya hizo ni dhaifu na udhaifu wao uko wazi; baadhi ni nzuri zenye uzito; baadhi zimetimia na zimefikia ukamilifu.”

Imani dhaifu ni hatua ya kwanza kabisa ambayo kwamba mtu hupita kuingia katika Uislamu kutoka kwenye ukafiri. Daraja za juu za Imani zinawezekana. Rejea zake zimeta- jwa katika baadhi ya hadithi. Miongoni mwao ni hadithi katika Usul Kafi na Nahju’l- Balagha kutoka kwa Amir wa Waumini (Ali) na Ja’far Bin Muhammad As-Sadiq ambaye amesema: “Allah ameigawanya Imani katika daraja saba ambazo ni wema, ukweli, kusadikisha kwa moyo, kujisalimisha kwenye utashi wa Allah, utii, elimu, na uvumilivu.

Sifa hizi saba zimegawanywa bila ulingano miongoni mwa wanadamu. Mtu ambaye anazo sifa zote hizi ni muumini kamili. Kwa hiyo, Uislamu uko katika kundi la kwanza la Imani, ambamo kuna tamko la mdomo la imani katika utume wa Muhammad na Upweke wa Allah. Imani haijaingia katika moyo wa mtu kama huyo. Mtume wa Allah alikiambia kikundi cha watu: ‘Enyi watu! Ninyi ni miongoni mwa wale ambao mmekubali Uislamu kwa ndimi zenu, lakini bado kwa nyoyo zenu.’”

Ni dhahiri kwamba Uislamu na Imani viko tofauti. Lakini hatutakiwi kupekuwa nyoyo za watu wengine. Nilisema usiku uliopita kwamba dalili ya muumini ni vitendo vyake.

Lakini hatuna haki ya kuchunguza kuhusu vitendo vya Waislamu. Hata hivyo tunalazimika kuonyesha tabia za Imani, ili kwamba wale ambao wamezama katika usingizi waweze kutiwa moyo wa kutekeleza wajibu wao.
Hivyo wataelewa ukweli wa Imani na watajua kwamba wokovu katika akhera utakuja tu kwa kufanya matendo mema, kama hadithi inavyosema: “Imani maana yake kukiri kwa ulimi, kusadikisha katika moyo, na kutenda kwa viungo vyetu.” Kukiri kwa ulimi na kusadikisha moyoni ni vitangulizi vya vitendo.

Naam tunajua kwamba ulimwengu huu mbaya ni utangulizi tu wa ulimwengu ujao. Njia ya wokovu kwa ajili ya mtu huyo imefungwa katika akhera mpaka awe ni mtu mwenye kufanya matendo mema hapa duniani. Allah (swt) anasema katika Qur’ani Tukufu:

وَالْعَصْرِ {1}

إِنَّ الْإِنْسَانَ لَفِي خُسْرٍ {2}

إِلَّا الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ وَتَوَاصَوْا بِالْحَقِّ وَتَوَاصَوْا بِالصَّبْرِ {3}

“Naapa kwa Zama! Hakika mwanadamu yumo katika hasara, isipokuwa wale walioamini na wakatenda matendo mema…” (103:1-3)

Kwa ufupi, kwa mujibu wa Qur’ani Tukufu, uchamungu ndio msingi wa Imani. Na kama mtu hana matendo mema katika sifa yake, kukubali kwake kwa mdomo au kusadikisha kwenye moyo bado kutamuacha mbali na Imani. Kama ni kweli kwamba inatupasa kumchukulia kila mtu kuwa ni Mwislamu, yule ambaye anasema , “Hakuna mungu isipokuwa Allah na Muhammad ni Mjumbe wa Allah,” kwa nini mnawachukilia Mashi’a kama makafiri?

Hakika Mashi’a wanaamini katika upweke wa Allah, utume wa Muhammad, Kibla moja, Kitabu kimoja. Wanatekeleza matendo yote ya wajibu, wanatekeleza saumu kama ilivyoelekezwa, wanakwenda kuhiji, wanatoa khums na zakat (kodi za kidini), wanaamini kufufuliwa katika mwili, na Siku ya Hukumu.

Je, ninyi sio ndio mnaosababisha utengano miongoni mwa Waislamu? Mnawatenga mamilioni ya Waislamu na kuwaita makafiri ingawa hamna hata chembe ya ushahidi kuun- ga mkono madai yenu. Hamtambui kwamba hizi ni mbinu za maadui ambao wanataka kusababisha migogoro miongoni mwa Waislamu kwa njia za uwongo kama huu.

Ukweli ni wamba hatuna tofauti katika misingi ya imani isipokuwa katika Uimamu na ukhalifa. Na vipi ingekuwa kama kungekuwa na tofauti katika matendo ya imani? Hitilafu kama hizo zipo miongoni mwa madhehebu zenu nne, nazo ni mbaya zaidi kuliko zile zilizoko kati yetu na ninyi. (haitakuwa sahihi sasa kuonyesha tofauti kati ya madhehebu za Hanafia na Maliki au kati ya Shafi’i na Hanbal.).

Kwa maoni yangu mimi, ninyi hamna hata chembe ya ushahidi kuthibitisha ushirikina au ukafiri wa Mashi’a. Kosa pekee la Mashi’a lisilosameheka, kwa mujibu wa kile walichoeneza Khawariji na Manasibi, kwa njia ya Bani Umayyah ni kwamba Shi’a hawapoto- shi katika kutafsir hadithi.

Hawawapi nafasi watu kama Abu Huraira, Anas, na Samura kuwa kati ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na sisi. Hata maulamaa wenu wenyewe na makhalifa wenu wakubwa waliwashutumu kama waongo.

Kosa kubwa wanalohusihswa nalo Mashia ni kwamba wanafuata kizazi cha Mtume, Ali na Maimamu kumi na mbili, na sio hao Maimamu wanne. Lakini ninyi hamna ushahidi kutoka kwa Mtume unaoonyesha kwamba ni lazima Waislamu wawafuate Ash’ari, au Mu’tazali katika misingi ya imani na Maliki, Hanafi, Hanbal nau Shafi’i katika matendo ya ibada.

Kwa upande mwingine kuna maelekezo mengi kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) yanayotuambia kwamba kizazi na Ahlul’l-Bayt wa Mtume wanalingana na Qur’ani Tukufu, na kwamba umma lazima ushikamane nao.

Miongoni mwa hadithi hizo ni ‘Hadith Thaqalain’, ‘Hadth-e-Safina’, ‘Hadith-e-Bab-e-Hitta’. Je, unaweza kunukuu hadthi moja tu ambayo kwayo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema kwmba baada yake yeye watu wake lazima wamfuate Abu’l-Hasan Ash’ari na Wasil Bin Ata, na kadhalika, katika misingi ya imani na mmojawapo wa Maimamu wanne – Malik Bin Anas, Ahmad Bin Hanbal, Abu Hanifa, au Muhammad Bin Idris Shafi’i katika matendo ya ibada?

Sheikh Suleiman Balkhi Hanafi katika kitabu chake Yanabiu’l-Mawadda, Sura ya 4, anasimulia kutoka kwa Fara’id Hamwaini akinukuu kutoka kwa Ibn Abbas kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimuambia Amirul-Mu’minin (Ali): “Ewe Ali! Mimi ni Jiji la elimu na wewe ni Lango lake. Hakuna mtu awezaye kuingia katika jiji bila kwanza kuingia katika lango.

Ni mwongo yule anayedai kunipenda mimi ambapo akiwa ni adui yako, kwa sababu wewe watokana na mimi na mimi natokana na wewe. Nyama yako ni nyama yangu, damu yako ni damu yangu, nafsi yako ni nafsi yangu, haiba yako ndio haiba yangu mimi.

Amebarikiwa yule mtu ambaye anakutii wewe, ole wake yule ambaye anakuasi wewe. Rafiki yako ni mwenye kunufaika, na adui yako yuko kwenye hasara. Mtu ambaye yuko pamoja na wewe amefuzu, na mtu ambaye yuko mbali na wewe amepotea. Baada yangu mimi, wewe na Maimamu wote katika kizazi chako ni kama Safina ya Nuh: ambaye atapanda humo ataokolewa, na yeyote yule ambaye atakataa kupanda humo ataangamia. Mfano wao (Maimamu) ni kama nyota: wakati nyota moja inapozama, nyingine hutokeza. Mpangilio huu utaendelea mpaka Siku ya Kiyama.”

Imeelezewa wazi kabisa katika Hadith-e-Thaqalain (inayokubaliwa na madhehebu zote) kwamba “Kama mtashikamana na Ahlul’-Bayt, kamwe hamtapotea.” Hata shupavu Ibn Hajar Makki anaandika katika matokeo ya utafiti wake katika Sawa’iq Muhriqa, Sura ya 2 sura ndogo,1, uk. 92, kuhusiana na aya ya Qur’ani Tukufu:

وَقِفُوهُمْ ۖ إِنَّهُمْ مَسْئُولُونَ {24}

“Na wasimamisheni hakika hao wataulizwa. (37:24)

Na Sheikh Suleiman Balkhi Hanafi vie vile amenukuu kutoka kwenye Sawa’iq katika kitabu chake Yanabiu’l-Mawadda, Sura ya 95, uk. 296, (kilichochapishwa Istanbul) akisema kwamba hadithi hii imesimuliwa katika njia tofauti. Ibn Hajar anasema: “Hakika, hadithi ya kushikamana na ‘Vitu Viwili Vizito’ (Thaqalain) imesimuliwa katika njia tofauti, imesimuliwa na Masahaba zaidi ya 25 wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).”

Ibn Hajar anasema kuhusiana na aya hiyo hapo juu ya Qur’ani kwamba Siku ya Hukumu, watu watauliza kuhusu Wilayat ya Ali na kizazi cha Mtume.

Anaandika kwamba kwa mujibu wa baadhi ya vyanzo, hadithi hii ilisimuliwa katika siku ya Arafa, na baadhi wanasema ilisimuliwa wakati Mtume yuko katika kitanda cha mauti na nyumba yake ikiwa imejaa Masahaba wake. Wengine wanasema ilikuwemo ndani ya hotuba yake ya mwisho baada ya Hija ya muago.

Ibn Hajar anatoa maoni yake kuhusiana na sehemu mbalimbali ilikosimuliwa hadithi hii: “Hakuna kutokulingana katika uwezekano kwamba Mtume katika kupenda kwake kuonesha Utukufu wa Qur’ani na kizazi chake kitukufu, alirudia rudia hadithi hii katika sehemu hizi na nyingine tofauti. Imesimuliwa kwa usahihi kabisa kwamba Mtume alisema: ‘Ninakuachieni miongoni mwenu vitu viwili vizito: kama mkivifuata, kamwe hamtapotea. Na viwili hivyo ni Kitabu cha Allah (Qur’ani) na Ahlul-Bayt wangu.’

Tabrani ameisimulia hadithi hii na nyongeza hii: “Angalieni jinsi mtakavyojihusisha na viwili hivi: Qur’ani na Ahlul’l-Bayt, hivyo msijaribu kuwatangulia, vinginevyo mtaangamia. Msiwapuuze, vinginevyo mtaharibikiwa. Msijaribu kuwafundisha, kwani wao wanajua zaidi kuliko ninyi.”

Hata Ibn Hajar mshupavu, baada ya kunukuu kutoka kwa Tabrani na wengine, anaandika: “Mtume aliita Qur’ani na kizazi chake, ‘Vizito Viwili ’ kwa sababu viwili hivi ni vizito mno na vitukufu katika kila kipengele.” Mtume vile vile alisema: “Namshukuru Allah ambaye ameijaza mioyo ya Ahlul’l-Bayt wangu kwa hekima.” Na Mtume vile vile alisema katika hadithi iliyotajwa huko mwanzoni: “.....Na kamwe msijaribu kuwafundisha (kizazi changu) kitu chochote kwa vile ni wenye elimu zaidi ya ninyi wote.

Muwaone ni bora kwa maulamaa wenu wote kwa sababu Allah amewaumba safi (watoharifu) na amewatambulisha kwenye umma kuwa na uwezo za kimiujiza na sifa nyingi nyingine zisizo na idadi.”

Kuna nukta moja katika hadithi hii ambayo inasisitiza kushikamana kwa Ahlul’l-Bayt: yaani, kwamba mfuatano wa vizazi vya Ahlul’l-Bayt, hautakatika mpaka Siku ya Hukumu.
Inashangaza kwamba baadhi ya watu wanakiri kwamba watu wa Ahlul’l-Bayt wana elimu kubwa lakini wanakiuka amri za Mtume na kuwafanya kama viongozi wao; wale watu wengine ambao hawana haki ya kutangulizwa. Je, mnaweza ninyi au sisi kubadisha Qur’ani Tukufu? Je, tunaweza kuchangua kitabu kingine chochote?

Sayyid: Hapana, haiwezekani kamwe. Hii ni amana ya Mtukufu Mtume, ujumbe mtukufu, na chanzo kikuu kabisa cha mwongozo.

Muombezi: Mwenyezi Mungu akubariki! Umezungumza kweli kabisa. Wakati tukiwa hatuwezi kuibadili Qur’ani tukufu na kuiwekea kitabu kingine badala yake, kanuni hiyo hiyo ni lazima ifuatwe kuhusiana na wale ambao wanalingana na hiyo Qur’ani tukufu. Hivyo, ni kwa mujibu wa kanuni gani ambayo kwamba wale ambao hawatokani na kizazi cha Mtume walikubaliwa kuwapita wale wa kizazi chake?

Nataka jibu rahisi kwa swali hili ili tuweze kujua iwapo kwamba wale makhalifa watatu - Abu Bakr, Umar, na Uthman - walitokana na Ahlul-Bayt wa Mtume (s.a.w.w.), na kwamba walijumuishwa katika hadith zile tulizozitaja (ya Thaqalain, Safina na Bab-e-Hitta). Kama wameingizwa, basi lazima tuwafuate, kwa mujibu wa maagizo ya Mtume.

Seyyed: Hakuna anayeamini kwamba yeyote kati ya makhalifa hao, mbali na Ali, walikuwa wameingizwa kwenye Ahlul-Bayt wa Mtume. Kama ilivyo, makhalifa hao watatu waliotajwa walikuwa ni masahaba wazuri wa Mtume (s.a.w.w.)

Muombezi: Je, Mtume alituambia tufuate mtu maalum au kikundi cha watu? Ikiwa kundi moja linasema kwamba ni jambo lenye manufaa kufuata watu wengine, hivi tumtii Mtume ama tufuate uangalifu kama ulivyoamuliwa na umma?

Seyyed: Ni dhahiri kwamba utiifu kwa Mtume ni wajibu wa lazima.

Muombezi: Baada ya kwamba Mtume ametuelekeza tufuate Qur’ani tukufu na kizazi chake, kwa nini wamependelewa kufuatwa wengineo? Je, Abul-Hasan Ali bin Isma’il Ash’ari, Wasil bin Ata, Malik bin Anas, Abu Hanifa, Muhammad Idris Shafi’i na Ahmad Hanbal walitokana na kizazi cha Mtume au Amirul-Mu’minin Ali na wale kumi na moja toka kwenye kizazi chake?

Seyyed: Ni wazi kabisa, hakuna ambaye amewahi kamwe kusema kwamba watu hawa wanatokana na kizazi cha Mtume, lakini walikuwa mafaqihi maarufu na watu wachamungu wa umma.

Muombezi: Lakini kwa mujibu wa makubaliano ya pamoja ya umma, maimamu hawa kumi na mbili ni kizazi cha moja kwa moja cha Mtukufu Mtume. Ulamaa wenu wenyewe wanakubali kwamba wao wanalingana na Qur’ani tukufu, na kwamba utii kwao unaongoza kwenye uongofu. Zaidi ya hayo, Mtukufu Mtume alisema kwamba wao ndio wenye elimu zaidi kati ya watu.

Kwa kuzingatia kanuni hizi mbili zenye nguvu, ni majibu gani watakayotoa wakati Mtume atakapowauliza ni kwa nini walikiuka miongozo yake yeye, na wakawaachia watu wengine kukitangulia kizazi chake?
Kuna maagizo yoyote kutoka kwa Mtume kwamba hawa Ashari na Mu’tazila wawafuate viongozi wao au kwamba Maliki, Hanbali, Hanafi na Shafi’i wawafuate viongozi wao katika matendo ya ibada? Hakuna yoyote kiasi kwamba aliyataja majina yao kwa miaka 300 baada ya kifo cha Mtume.

Ni baada ya hapo tu, kwa sababu za kisiasa au nyinginezo ambazo mimi sizitambui, wao ndipo wakatokea uwanjani. Lakini hawa Maimam na kizazi cha Mtukufu Mtume walikuwa wakijulikana vema wakati wa uhai wa Mtume mwenyewe. Ali, Hasan, Husein na Fatima walikuwa wakijulikana kama Ahlul-Kisa’a, yaani “watu wa chini ya shuka.” Walikuwa ni wao ambao kwa sifa zao ile “Aya ya Utakaso” - Ayat-Tathiira - ilishuka kwa ajili yao. Hivi inafaa kweli, kuwaita wale wanaowafuata Ali, Hasan, Husein na wale Maimam wengine kuwa ni makafiri? Mmewafadhilisha wale ambao hawatokani na kizazi cha Mtume juu ya wale ambao walikuwa mafaqihi wakamilifu, wa kupigiwa mfano.

Ni majibu gani mtakayotoa kwenye mahakama tukufu ya haki mtakapoulizwa ni kwa nini mliwapotosha watu, kwa nini mliwaita wafuasi wa Ahlul-Bayt makafiri na wazushi?

Mnatutia makosani kwa sababu sisi sio wafuasi wa kanuni za kiimani za wa-Hanafi, Maliki, Hanbali au Shafi’i. Na bado hamumfuati Ali, licha ya maagizo ya wazi na ya dhahiri kabisa kutoka kwa Allah na Mtume wake kwamba mnapaswa kufanya hivyo. Bila ya sababu nzuri za maana, mnafuata moja ya madhehebu nne hizi na mmeifunga milango elimu ya sharia - fiqh.

Sayyed: Tunategemea juu ya Maimam hawa wanne kwa namna ileile kama ninyi mnavyotegemea kwa Maimam kumi na mbili.

Muombezi: Vizuri sana! ni jambo zuri kiasi gani hilo ulilosema! Idadi ya Maimam kumi na mbili haikuainishwa na Mashi’a au ulamaa wao karne nyingi baada ya kifo cha Mtume. Hadithi nyingi zilizosimuliwa na kutoka kwenye vyanzo vya wote, Shi’a na Sunni, zinathibitisha kwamba Mtume mwenyewe aliiainisha idadi hiyo ya Maimam kuwa ni kumi na mbili.

Miongoni mwa ulamaa wenu ambao wamesimulia jambo hili ni Sheikh Sulayman Qanduzi

Hanafi, ambaye anaandika katika Yanabiul-Mawadda yake, Sura ya 77, kuhusiana na tamko hili: “Watakuwepo makhalifa kumi na mbili baada yangu.”

Yahya bin Hasan katika Kitabul-Umma amesimulia kwa njia ishirini kwamba Mtukufu Mtume amesema kwamba warithi wake watakuwa ni kumi na mbili kwa idadi, na wote watatokana na Quraishi. Imesimuliwa kwa njia tatu ndani ya Sahih Bukhari, katika njia tisa ndani ya Sahih Muslim, kwa njia tatu ndani ya Sunnan Abu Dawuud, kwa nji moja ndani ya Sunnan-Tirmidhi, na kwa njia tatu ndani ya Jam’-e-Bainas-Sahihain ya Hamidi.

Wako ulamaa wenu wengi, kama vile Hamwaini katika Fara’id, Khawarizmi na ibn Maghazili kila mmoja katika Manaqib yake, Imam Tha’labi katika Tafsiir yake na ibn Abil-Hadid ndani ya Sharh Nahajul-Balaghah, na Sayyid Ali Hamadani Shafi’i katika Mawaddatul-Qubra, Mawadda 10.

Wote wamesimulia hadithi kumi na mbili zilizosimuliwa na Abdullah ibn Abbas, Ubaya bin Rabi’i, Za’id bin Haritha, Abu Huraira na Amirul- Mu’minin Ali. Wote hawa wanasimulia kwa njia tofauti, lakini maneno yale yale kwamba Mtume amesema kwamba idadi ya warithi wake na Maimam watakuwa w12 na kwamba wote watatokana na Maquraishi.

Baadhi ya hadith zinasema kwamba wao watatokana na Bani Hashim. Katika baadhi ya riwaya yale majina mahususi ya warithi kumi na mbili hao pia yametajwa. Wengine wao wanatoa idadi tu. Nimetoa kati ya hadith nyingi za ulamaa wenu. Sasa je, mnaweza kuta- ja hadith moja tu ambayo inaashiria kwamba idadi ya warithi wake watakuwa wanne tu? Hata kama ingekuwepo hadith moja tu kama hiyo, sisi tutaikubali kuliko ile ya kwetu wenyewe.

Bila kuzingatia ukweli kwamba hamuwezi kunukuu hadith hata moja kuhusu maimam wenu wanne, kuna tofauti kubwa sana kati ya Maimam wa Shi’a na hao Maimam wenu. Maimam wetu kumi na mbili ni warithi walioteuliwa ki-mbinguni.

Kuhusu maimam wenu, ni kiasi hiki tu kinachoweza kukubalika: walikuwa na elimu ya fiqhi (sharia za kiislam) na waliweza kutafsiri Qur’ani tukufu na hadith. Baadhi yao, kama Abu Hanifa, kulingana na kukiri kwa ulamaa wenu wenyewe, walikuwa hawakujuishwa miongoni mwa wasimuliaji wa hadith, mafaqih, au mujtahidi, bali walikuwa ni watu waliotegemea juu ya rai zao wenyewe.

Hii peke yake ni ushahidi wa kukosa kwao kuwa na elimu. Kwa upande mwingine, Maimam wa Shi’a ni waongozaji walioteuliwa ki-mbinguni, warithi walioagizwa, wa Mtukufu Mtume.

Kwa kweli katika kila zama wanakuwepo baadhi ya mafaqihi wenye elimu ya hali ya juu na wanachuoni miongoni mwa Mashi’a ambao wanazitafsiri amri za Allah, wakizingatia Qur’ani tukufu, hadith na makubaliano ya maoni.

Tunafuata fat’wa za ulamaa kama hao. Ingawa mafaqihi wenu walikuwa wanafun- zi wa, na walipata nyingi ya elimu yao, kutoka kwa Maimam wa Shi’a, ninyi mnawafuata wahenga wenu ki-kichwakicha tu, wale kati ya wanafunzi wao, ambao walikengeuka kut ka kwenye misingi ya elimu na wakategemea kukisia kwao.
Sayyed: Unawezaji kudai kwamba Maimam wetu walipata manufaa ya elimu yao kutoka kwa Maimam wenu?

Muombezi: Ni ukweli wa kihistoria kwamba Imam Ja’far as-Sadiq aliwazidi wengine wote katika elimu. Yule Aalim mashuhuri, Nuru’d-Din bin Sabbagh Maliki anakiri ndani ya kitabu chake, Fusulul-Muhimma kwamba Mtukufu Imam alikuwa akijulikana na kuonekana wazi kwa elimu yake. Yeye anaandika: “Watu walipata elimu ya nyanja mbali mbali kutoka kwake. Watu walikuja kutoka nchi za mbali kupata maelekezo. Akajulikana sana katika nchi zote na ulamaa walisimulia hadith nyingi kutoka kwake kuliko kwa mtu mwingine wa Ahlul-Bayt .....”

Kundi kubwa la watu mashuhuri wa umma, kama Yahya bin Sa’id ibn Jarih, Malik bin Anas, Sufyan Thawri, Abu Ainiyya, Abu Ayyub Sijistani, Abu Hanifa, na Saba - wote wamesimulia hadith zake.

Kamalu’d-Din Abi Talha pia anaandika katika Manaqib yake kwamba maulamaa maarufu na viongozi wa kidini wamenukuu hadith kutoka kwa mtukufu Imam na wamepata elimu kutoka kwake. Miongoni mwao anataja majina ya wale waliotajwa kwenye Fusulul-Muhimma. Hata maadui walikiri fadhaili za mtukufu Imam. Kwa mfano, Maliki katika Fusulul-Muhimma na hususan Sheikh Abu Abdu’r-Rahman Salmi katika Tabaqatul- Masha’ikh yake anaandika:

“Hakika, Imam Ja’far as-Sadiq aliwapita wenzie wote wa wakati wake. Alikuwa na elimu ya kisilika na ujuzi katika dini, uchamungu kamilifu katika ulimwengu, kujizuia kutokana na matamanio yote ya kidunia, na hekima ya kina kikubwa.”

Na Muhammad bin Talha Shafi’i ameziandika sifa hizi zote za mtukufu Imam katika Matalibus-Su’ul yake, Sura ya 6, uk. 81: “Mtu huyu mwenye elimu kubwa alitokana na viongozi mashuhuri wa Ahlul-Bayt. Alijaaliwa na elimu nzito na alikuwa wakati wote katika hali ya kumkumbuka Allah. Alisoma Qur’ani tukufu mara kwa mara na alitoa tafsiri yake.

Wafuasi wake walijikusanyia lulu kutoka kwenye bahari ya elimu yake. Aligawanya muda wake wakati wa mchana na usiku katika miundo mbalimbali ya ibada. Kumtembelea yeye kulikuwa kama ukumbusho wa akhera.

Kuisikiliza hotuba yake kulimuongoza mtu kupata uchamungu, na kufuata maelekezo kulimuongozea mtu kwenye kupata pepo. Uso wake mng’aavu ulijulisha kwamba alitokana na familia ya Mtukufu Mtume. Usafi wa vitendo vyake pia ulionyesha kwamba anatokana na Ahlul-Bayt wa Mtume.

Wengi wa ula- maa wamepokea hadith na kupata elimu kutoka kwake. Miongoni mwao walikuwa ni Yahya bin Sa’id Ansari, ibn Jarih, Malik bin Anas, Sufyan Thawri, Ibn Ainiyya, Sha’ba na Ayyub Sijistani. Wote walishukuru kwa bahati njema na fursa ya kusoma kutoka kwake.”

Kuhusishwa Kwa Ushi’a Na Imam Ja’far As-Sadiq

Nawab: Mashi’a wanaamini katika Maimamu kumi na mbili. Kwa nini Ushi’a unahusish- wa na jina la Imam Ja’far Sadiq na kuitwa madhehebu ya Ja’far?

Muombezi: Kila Mtume, kwa mujibu wa amri ya Mungu, huteua mrithi wake. Muhammad alimtangaza Ali kuwa mrithi wake na akaamuru umma kumtii yeye. Lakini baada ya kifo cha Mtume, Ukhalifa ulichukuliwa na Abu Bakr, Umar na Uthman.

Wakati wa ukhalifa wao, isipokuwa wakati wa siku za mwanzo, Abu Bakr na Umar walimtaka ushauri Ali juu ya masuala yote mazito na kutenda kwa kufuata ushauri wake.

Aidha, maulamaa wakubwa na wanachuoni maarufu wa dini nyingine ambao walikuja Madina kwa ajili ya kutafuta elimu ya dini walikinaishwa kabisa na majadiliano yao na Ali. Katika maisha yake yote, Ali aliendelea kuuhudumia Uislamu katika njia nyingi. Baada ya kuuliwa kwake shahidi, wakati Bani Umayya walipokuwa watawala, uimamu kwa ukatili mkubwa ukakandamizwa.

Imam Hasan Mujtaba, Imam Husein, Imam Zainu’l-Abidin, na Imam Muhammad Baqir walikuwa waathirika wa ukatili mkubwa wa Bani Umayya. Njia zote za kuwafikia wao zilifungwa isipokuwa kwa wafuasi wao wachache, wengine hawakuweza kunufaika kutokana na elimu yao. Kila mmoja wao aliuawa.

Hata hivyo, wakati wa mwanzo wa karne ya pili baada ya Hijra, chini ya shinikizo kubwa la ukatili wa Bani Umayya, watu waliasi dhidi ya yao. Mapigano makali ya umwagaji damu yalifuatilia kati ya Bani Abbas na Bani Ummaya. Wakati ambapo Bani Umayya walikuwa wamejishughulisha katika kuulinda utawala wao, hawakuweza kuendeleza unovu wao kwa Ahlul’l-Bayt. Kwa hiyo, Imam Ja’far akajitokeza kutoka kwenye kule kutengwa alikokuwa amefanyiwa na Bani Umayya. Aliwaelekeza watu kuhusiana na sheria za dini.

Wapenda elimu 4000 walijikusanya kuizunguka mimbar yake na kuzima kiu yao kutoka kwenye bahari ya elimu isiyo na kikomo ya mtukufu Imam. Baadhi ya masahaba zake wameandika kanuni mia nne ambazo zinajulikana kama ‘Usul-e-Arba Mia – yaani hukumu mia nne. Yafi’iy Yamani anaandika kwamba Imam Ja’far aliwapita wote katika elimu yake. Jabir Ibn Hayyan Sufi, aliandika mkusanyo wa kurasa elfu moja, akiorodhesha takriban vijitabu 500 juu ya mafundisho ya Imamu Ja’far.

Baadhi ya mafaqihi wakubwa wa ki-Sunni vile vile walikuwa ni wanafunzi wake. Abu Hanifa, Malik Bin Anas, Yahya Bin Sa’id Ansari, Ibn Jarih, Muhammad Bin Ishaq, Yahya Bin Satid Qattan, Sufyan Bin Uyayna, Sufyan Thawri – wote hawa walinufaika kutoka kwenye elimu yake kubwa mno. Ukubwa huu wa uchanuaji wa elimu ulitokea wakati huu kwa sababu Bani Umayya walizuiya mwenendo wa wazazi wake, na kwa bahati mbaya Bani Abbas wangeliwazuiya kizazi chake kuzungumza kwa uhuru.

Ukweli wa wa Ushi’a uliwekwa wazi na sifa za Ahlul’l-Bayt wa Muhammad zilitangazwa na Imamu Ja’far Sadiq. Kwa hiyo, madhehebu hii ikaja kujulikana kama “Ja’faria,” lakini hakuna tofauti kati ya Imamu Ja’far na yeyote katika Maimamu wanne miongoni mwa wahenga zake waliomtangulia au Maimamu sita waliokuja baada yake. Wote walikuwa viongozi wa kiro- ho waliowekwa na Mungu.

Ingawa marafiki na maadui wote kwa pamoja walitambua ubora wake katika elimu na ukamilifu wake katika sifa zote, viongozi wenu waliopita walikataa kumfanya kama mwanachuoni mkubwa wa dini na mtu mkamilifu wa zama zake.

Walikataa kutambua madhehebu yake sambamba na madhehebu nyingine nne ingawa yeye alishikilia daraja la juu zaidi katika elimu uchaji kama ilivyokubaliwa na maulamaa wenu wenyewe. Kwa vile alitokana na Ahlul’l-Bayt wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), alikuwa na haki ya kupata kipaumbele juu ya wengine.

Pamoja na mambo yote haya, maulamaa wenu washupavu wameonesha dharau sugu kama hii kwa kizazi cha Mtume wao kiasi kwamba wanachuoni wenu wa daraja za juu kama Bukhari na Muslim, hawakuweza kuandika hata hadithi moja kutoka kwa faqih huyu au Ahlul-Bayt.

Aidha, hawakunukuu hadithi yoyote kutoka kwa Imam yoyote au Sa’dat (mabibi) wa kizazi kitukufu: Alawi, Husaini, Abidi, Musawi, Ridhawi, au kutoka kwa maulamaa kama hawa na mafuqahaa kama, Zaid Bin Ali Bin Husein, yule Shahid, Yahaya Bin Zaid, Muhammad Bin Abdullah, Husein Bin Ali, Yahya Bin Abdullah bin Hasan na kaka yake Idris, Muhammad Bin Ja’far Sadiq, Muhmmad Bin Ibrahim, Muhammad Bin Zaid, Abdullah Bin Hasan, Ali Bin Ja’far (Arizi) na wengine, wote hao ambao walikuwa maula- maa na mafaqih wakubwa na ambao walitokana na familia ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Kwa upande mwingine, wamenukuu hadithi kutoka kwa watu kama Abu Huraira, ambaye tabia yake mnaijua ninyi wote, na kutoka kwa yule mwongo mkubwa na mzushi, Akrama, yule Khawariji. Maulamaa wenu wenyewe wamethibitisha kwamba watu hawa walikuwa waongo na bado wanakubali hadithi zao kwa mioyo yao yote. Ibn Bayyit anaandika kwamba Bukhari amenukuu hadithi nyingi kufikia kiasi cha hadithi 12,000 kutoka kwa Khawariji na Nasibiyya, kama Imamu bin Hattan, mwenye kuvutiwa na Ibn Muljim, muuwaji wa Amir wa Waumini.

Wafuasi wa Imam-e-Adhma (Abu Hanifa), Imamu Malik, Imamu Shafi’i na Imamu Hanbal huwaona hawa kama Waislamu safi ingawa hakuna hata mmoja aliyetokana na Ahlul-Bayt wa Mtume, na kila mmoja wa madhehebu zile iko huru kuchukuwa njia zake mwenyewe ingawa kuna tofauti kubwa katika misingi na halikadhalika katika matendo ya ibada miongoni mwao.

Ni masikitiko makubwa kiasi gani kwamba wanawaita wafuasi wa Ja’far Bin Muhammad As-Sadiq makafiri! Na katika sehemum zote zinazotawaliwa na Masunni, ikiwemo Makka, ambayo kwa kuihusu Allah anasema: Yeyote anaingia humo yuko huru,” hawako huru kuelezea imani yao au kutekeleza Sala zao.

Hivyo ninyi watu wema mnapaswa muelewe kwamba sisi Shi’a sio chanzo cha hitilafu zilizoko katika Uislamu; hatukuleta mtengano miongoni mwa Waislamu. Kusema kweli, migogano mingi hutokea upande wenu. Ni niyni mnaowaita Waislamu milioni 100 makafiri, ingawa ni waumini waaminifu sambamba na ninyi.

Hafidh: Ni kweli, kama ulivyosema, kwamba mimi sio mtu dhalimu. Nakubali kwamba kumekuwepo na vitendo viovu kwa sababu ya ushupavu. Ningependa kusema bila kujidai au kumpendeza yeyote kwamba nimenufaika sana kutokana na mazungumzo yako na nimejifundisha vya kutosha.

Lakini kwa idhini yako, niruhusu niseme kitu kimoja, ambacho ni malalamiko, na halikadhalika ni utetezi wa madhehebu stahiki ya Sunni. Unaweza kuniambia ni kwa nini wahubiri na maulamaa wa ki-Shi’a kama wewe hamchungi watu wenu wa kawaida kutokana na kutoa maneno ambayo hupelekea kwenye ukafiri? Matokeo yake ni kwamba wengine hupata nafasi ya kutumia neno kafiri dhidi yao.

Mtu anaweza kuwa shabaha ya mashambulizi kwa sababu ametoa maelezo yasiyo sahihi. Hivyo ninyi watu vile vile msiwafanye Masunni kuwa shabaha ya mashambulizi yenu. Mashi’a husema mambo ambayo huathiri nyoyo za Masunni, ambao kwa kulipiza huhusisha ukafiri kwa Mashi’a.

Muombezi: Naomba unieleze ni maelezo gani au vitendo gani hupelekea kwenye ukafiri vinavyofanywa na Mashi’a?

Hafidh: Mashi’a kuwakosoa Masahaba wakubwa na baadhi ya wake safi wa Mtume, ni dhahiri hicho ni kitendo cha ukafiri. Kwa vile Masahaba wamepigana kwa miaka mingi pamoja na Mtume dhidi ya makafiri, ni wazi kwamba huduma yao ilikuwa safi kabisa kutokana na maadili yasiyokamilika. Kwa hakika wanastahiki Pepo, hususan wale ambao walipata baraka za Mungu. Kwa muijibu wa Qur’ani Tukufu : “Hakika Allah aliridhishwa sana na waumini wakati walipokula kiapo cha utii kwako chini ya mti” (Qur’ani 48;18) Hakuna shaka kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliwaheshimu. Mtu ambaye anakataa ubora wao hakika amepotea. Qur’ani inasema: Wala hazungumzi kwa mata- manio yake. Hayakuwa haya ila ni ufunuo uliofunuliwa.” (Qur’ani; 53:3-4) Mtu kama huyo anamkataa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na Qur’ani Tukufu, na mtu ambaye anamkataa Mtume na Qur’ani Tukufu hapana shaka yoyote ni kafiri.

Muombezi: Nilitegemea kwamba nukta kama hizo zisingeletwa katika mkutano huu wa hadhara. Majibu yangu yanaweza kuwafikia watu wasio na elimu na wanaweza wakaeneza propaganda potovu. Ingekuwa vizuri kama tungejadili masuala haya kwa faragha. Nitakuja kwako siku moja na tutalitatua tatizo hili kwa faragha.

Hafidh: Nasikitika, lakini watu wetu wengi katika mikesha kadhaa iliyopita wamesisitiza kwamba nukta hii ijadiliwe. Majadiliano yako siku zote ni yenye busara. Kama utatoa majibu mazuri yenye mvuto, hakutakuwa na matokeo mabaya. Vinginevyo ukubali kushindwa na hoja yetu.

Nawab: Ni sawa sawa. Wote tunataka suala hili litatuliwe hapa hapa na sasa hivi.

Muombezi: Nakubaliana tu matakwa yenu. Si kutarajia mtu mwenye uwezo kama wewe, baada ya maelezo kamili ambayo nimeyatoa katika usiku wa masiku yaliyopita juu ya suala la ukafiri ungeihusisha madhehebu ya Shi’a na ukafiri. Tayari nimewasilisha kwa ukamilifu uthibitisho kwamba Shi’a Ithna Ashari ni wafuasi wa Muhammad na kizazi chake kitukufu. Umeleta masuala mbalimbali. Nitajibu kila moja ya hayo kwa kuyatenganisha.

Kuwalaumu Masahaba Haina Maana Ya Ukafiri

Kwanza umesema kwamba ukosoaji wa Mashi’a juu ya Masahaba na baadhi ya wake wa Mtume hupelekea kwenye ukafiri. Sielewi msingi wa maelezo haya. Kama ukosoaji unaungwa mkono na ushahidi, unaweza kukubaliwa. Na hata kama mtu akitoa madai ya uwongo, hii haimfanyi kuwa kafiri. Ataitwa mwenye dhambi, kama mtu anayekunywa pombe au anayefanya zinaa. Na hakika kila kosa dhidi ya sheria ya Mungu linasameheka.
Ibn Hazm Zahiri Andalusi (amezaliwa 456 A.H.) anasema katika kitabu chake Al-Fasl fi’l- milal wa’n-Nihal sehemu ya 3, uk. 227: “Kama mtu anamtukana Sahaba wa Mtume kwa ujinga, si wa kulaumiwa. Kama akifanya hivyo hali ya kuwa ana elimu juu ya hilo, ni mwenye dhambi kama wenye dhambi wengine ambao hufanya zinaa, wizi, nk.

Naam kama akiwalaani kwa makusudi, kwa vile walikuwa Masahaba wa Mtume, atakuwa kafiri kwa sababu tabia kama hiyo ni sawa na uadui dhidi ya Allah na Mtume Wake. Vinginevyo, kuwatukana tu Masahaba hakuwezi kuwa sawa na ukafiri.”

Kwa hiyo, Khalifa Umar alimuomba Mtume amruhusu kumkata kichwa Hatib, aliyekuwa mnafiki, ingawa alikuwa ni mmoja wa Masahaba wakubwa, muhajir, na mbaye alishiriki katika vita ya Badir. Kwa kule kumtukana na kumhusisha na unafiki, Umar hakuitwa kafiri.

Basi vipi inawezekana kwamba Mashi’a waitwe makafiri kwa kuwatukana baadhi ya Masahaba, tukichukulia kwa muda huu kwamba unayosema ni sahihi. Aidha, maulamaa wakubwa wa madhehebu yenu wameikataa nukta yenu hii.

Miongoni mwao ni Kadhi Abdu’r-Rahman Shafi’i, ambaye katika kitabu chake Muwafiq amekataa hoja ya maulamaa wenu washupavu kuhusu ukafiri wa Mashi’a. na Muhammad Ghazali anaandika kwamba kwalaani na kuwatukana Masahaba kamwe sio ukafiri; hata kuwalaani Masheikh wawili (Bukhari na Muslim) hakuwezi kuwa sawa na ukafiri.

Mulla Sa’d Taftazani anaandika katika Sharhe Aqa’id-e-Nas’i kwamba, “ baadhi ya watu wasio na uvumilivu wanasema kwamba wale ambao wanawatukana Masahaba ni makafiri. Ni vigumu kukubali mtazamo huo. Ukafiri wao hauthibitishwi kwa sababu baadhi ya maulamaa wamewapendelea, wakapuuza matendo yao maovu, na kutoa utetezi wa kipumbavu katika kuwaunga mkono.

Wamesema kwamba Masahaba wa Mtume walikuwa hawana dhambi yoyote, ingawa maelezo haya yalikuwa kinyume na ukweli wa mambo. Wakati mwingine walipigana wenyewe kwa wenyewe. Husda na kupenda madaraka mara kwa mara kuliwasababishia kufanya matendo maovu.

Hata baadhi ya Masahaba wakubwa hawakuwa huru kutokana na vitedno viovu. Hivyo, kama kwa msingi wa ushahidi fulani mtu akawakosoa, hapaswi kulaumiwa kwa hilo. Baadhi ya watu, kwa sababu waliwapendelea Masahaba walificha maovu yao, lakini baadhi wameandika matendo yao maovu na kuwalaumu.”

Mbali na hili, Ibn Athir Jazari, mwandishi wa Jam’ul-Usul, amewajumuisha Mashi’a kati- ka madhehebu ya ki-Islamu, basi mnawezaje kuwaita makafiri? Wakati wa kipindi cha Makhalifa wa kwanza, baadhi ya watu waliwalaani Masahaba kwa ajili ya matendo yao maovu. Hata hivyo, Makhalifa hawakuamuru wauawe kwa ukafiri wao.

Kwa hiyo, Hakim Nishapuri katika kitabu chake “Mustadrak”, sehemu ya 4, uk. 335, 354, Imamu Ahmad Hanbal katika “Musnad”, sehemu ya 1, uk. 9, Dhahabi katika “Talkhise Mustadrak”, Kadhi Ayaz katika “Kitab-e-Shifa”, sehemu ya 4, sura ya 1, na Imamu Ghazali katika “Ihya’u’l- Ulum”, Jz. 2, anataarifu kwamba wakati wa Ukhalifa wa Abu Bakr, mtu mmoja alikuja kwake na akatoa lugha chafu na laana dhidi yake kiasi kwamba wale waliokuwepo pale walishikwa na hasira. Abu Barza Salmi alimuomba Khalifa kama angemruhusu ili amuuwe yule mtu kwa sababu amekuwa kafiri. Abu Bakr alisema kwamba haiwezekani kufanya hivyo kwa vile hakuna mtu yeyote isipokuwa Mtume anayeweza kupitisha hukumu kama hiyo.

Makhalifa Wenyewe Hawakuchukulia Kulaniwa Wao Kuwa Ni Ukafiri

Kwa kweli, mabwana wakubwa wa ki-Sunni huwakiuka hata wale ambao wanawaunga mkono. Makhalifa wenyewe walisikia matusi lakini hawakuwalaumu watu kwa ukafiri au kuamuru wauawe. Aidha, kama kumlaani Sahaba ni sababu ya ukafiri, kwa nini msimuite Mu’awiya na wafuasi wake makafiri? Walimlaani na kumtukana mkamilifu zaidi wa Masahaba, Ali Bin Abu Talib. Kuwa na uchaguzi wa upendeleo katika suala hili huonesha tu kwamba lengo lako ni kitu kingine. Unataka kupigana dhidi ya Ahlul-Bayt na wafuasi wao! Kama kuwalaani Masahaba ni ukafiri, kwa nini msimlaumu Ummu’l-Mu’minin Aisha kwa ukafiri?
Wanahistoria wenu wote wamesema kwamba alikuwa mara kwa mara akimtukana Khalifa Uthman na kwa uwazi akatangaza: “Muuwenu mzee huyu mpumbavu, kwani hakika amekuwa kafiri.” Hata hivyo, kama Shi’a atasema kwamba ilikuwa vema kwamba Uthman aliuawa kwa sababu alikuwa kafiri, mara moja mtasimama dhidi yake.

Lakini wakati Aisha alipomuambia Uthman mbele yake kwamba yeye ni Na’thal na kafiri, Khalifa hakumkataza kufanya hivyo wala Masahaba hawakumkemea. Wala ninyi hamuoni kwamba alifanya kosa.

Nawab: Mheshimiwa, unamaanisha nini kwa neno Na’thal?

Muombezi: Firuzabadi, ambaye ni mmoja wa maulamaa wenu mwenye daraja ya juu, anatoa maana yake katika Qamusu’l-Lughat kama ‘mzee mjinga’. Vile vile kulikuwa Myahudi aliyekuwa na ndevu ndefu mjini Madina aliyekuwa akiitwa kwa jina hilo, ambaye alifananishwa na Uthman. Mfafanuzi juu ya Qamus, Allama Qazwini, vile vile anatoa maana hiyo hiyo, anasema kwamba Ibn Hajar katika kitabu chake Tabsiratu’l-Muntaha, anaandika, “Nathal Myahudi mwenye ndevu ndefu aliyeishi Madina; alifanana sana na Uthman.”

Khalifa Abu Bakr Alimtukana Ali

Mwisho, kama mtu anayemtukana Sahaba ni kafiri, kwa nini Khalifa Abu Bakr, mbele ya Masahaba na mkusanyiko wa Waislamu, alimtukana Sahaba bora zaidi, Ali Bin Abi Talib? Mnatukuza sifa za Abu Bakr ingawa mlipaswa kumlaumu.

Hafidh: Kwa nini unamsingizia lawama hii ya uwongo? Ni lini Khalifa Abu Bakr alimtukana Khalifa Ali?

Muombezi: Samahani! Sisi hatusemi kitu chochote mpaka tuwe tumefanya utafiti wa kutosha. Pengine ungetazama Sharhe Nahjul-Balagha, Jz. 4, uk. 80, ambapo imeandikwa kwamba Abu Bakr, akimdhihaki Ali kutoka kwenye mimbari ya Msikiti, alisema: “Yeye (Ali) ni mbwa mwitu, ushahidi wake ambao ni mkia wake.

Anasababisha matatizo, anapu- uza umuhimu wa matatizo makubwa, na kuchochea watu kufanya vurugu. Anaomba msaada kutoka kwa wanyonge na kukubali usaidizi kutoka kwa wanawake. Yeye ni kama Ummi’t-Tahal (kahaba mmoja wa siku za ujahilia, kama alivyoelezwa na Ibn Abil-Hadid) ambaye kwamba wanaume wa familia yake walikuwa wanapenda kufanya naye zinaa.”

Sasa mnaweza kulinganisha matusi ya Abu Bakr kwa Ali na ukosoaji unaofanywa na Mashi’a dhidi ya Masahaba. Kama kumtukana Sahaba yeyote ni sawa na ukafiri, basi Abu Bakr, binti yake Aisha, Mu’awiya na wafuasi wake wanapaswa kuitwa makafiri. Kama hakumfanyi mtu kuwa kafiri, basi huwezi kuwaita Mashi’a makafiri kwa jambo hilo.

Khalifa Umar Alishikilia Kwamba Kumlaani Mwislamu Sio Ukafiri

Aidha, kwa mujibu wa hukumu za wanachuoni wenu wakubwa na Makhalifa, wale ambao wanawatukana Makhalifa sio makafiri. Imam Ahmad Hanbal katika Musnad yake, Jz. 3, Ibn Sa’d Katib katika Kitab-e-Tabaqat, Kadhi Ayaz katika kitabu chake Shifa, sehemu ya 4 ya sura ya 1, wanasimulia kwamba, gavana wa Khalifa Umar, Ibn Abdul-Aziz, aliandika kutoka Kufa kwamba mtu mmoja amemtweza na kumtukana Umar Ibn Khattab, Khalifa wa pili.

Gavana huyo alitaka ruhusa ya kumuuwa huyo mtu. Umar Ibn Khattab akajibu kwamba hairuhusiwi kumuua Mwislamu kwa kutukana au kumlaani Mwislamu yeyote isipokuwa mtu ambaye anamtukana Mtume.

Kwa Mujibu Wa Abul-Hasan Ash’ari Hata Kumuita Allah Au Mtukufu Mtume (S.A.W.W.) Kwa Majina Mabaya Sio Ukafiri

Baadhi ya maulamaa wenu wakubwa, kama, Abu’l-Hasan Ash’ari na wafuasi wake, wanaamini kwamba kama mtu ana imani katika moyo wake na bado akaonyesha ukafiri (km. Kwa kuabudu kiyahudi au kikristo, kwa mfano) au akasimama na kupigana dhidi ya Mtume, au akamuita Allah au Mtume kwa majina mabaya, hata hivyo sio kafiri.
Imani maana yake kuamini ndani ya moyo na kwa vile hakuna mtu anayeweza kuujua moyo wa mtu mwingine, haiwezi kusemwa iwapo ule ukafiri wa dhahiri unatoka moyoni au la. Maulamaa wa ki-Ash’ari vile vile wamejadili masuala haya katika vitabu vyao. Ibn Hazm Andalusi ameandika kwa urefu kuhusu nukta hizi katika kitabu chake Kitabu’l-Fazl (sehemu ya 4, uk. 204, 206). Kwa kuzingatia ukweli huu, ninyi mna haki gani ya kuwashutumu Mashi’a kwa ukafiri?

Masahaba Wengi Walitukanana Wenyewe Kwa Wenyewe Lakini Hawakuchukuliwa Kama Makafiri

Katika vitabu vyenu sahihi, kama Musnad cha Imamu Ahmad Bin Hanbal, Jz. 2, uk. 236; Siratul-Halabiyya, Jz. 2, uk. 107, Sahih Bukhari, Jz. 2, uk. 74, Sahih Muslim, Kitab-e-Jihad wa Asbabu’n-Nuzul Wahid, uk. 118, kuna hadithi nyingi zinzoonesha kwamba Masahaba wengi walitukanana wenyewe kwa wenyewe mbele ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Lakini Mtume hakuwaita watu hawa makafiri. Aliwaonya. (hadithi za kuhusu mizozo hii na uadui wa wao kwa wao zimeandikwa katika vitabu vya Sunni tu, sio katika vitabu vya Shi’a).Kwa mtazamo wa maneno haya, natumaini kwamba mmetosheka kwamba kulaani au kumtukana Sahaba yeyote hakumfanyi mtu kuwa kafiri. Kama tunamlaani mtu fulani bila sababu, tutakuwa ni watenda dhambi, sio makafiri. Na kila dhambi inaweza kusamehewa.

Mtukufu Mtume (S.A.W.W.) Aliyajua Matendo Yote Mabaya Na Mazuri Ya Masahaba

Pili, umesema kwamba Mtume aliwaheshimu na kuwastahi Masahaba wake. Hii ni sahihi. Kwa nyongeza, Waislamu wote na wasomi wanakubali kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alijua matendo mema na mabaya ya watu. Aliyaridhia matendo yao mema. Kwa hiyo, aliheshimu uadilifu wa Nushirwan na ukarimu wa Hatim Ta’i. Kama alimheshemu mtu fulani, ilikuwa ni kwa sababu ya matendo yake mazuri.

Lakini kule kuridhiwa anakooneshwa mtu kwa kufanya tendo jema, hakuthibitishi kwamba mwisho wake utakuwa wa mafanikio.

Pengine atafanya matendo mabaya siku za baadae. Kama akifanya, kumkemea kabla ya kufanya, sio uadilifu, hata kama ingejulikana kwamba atafanya uovu katika siku zijazo.

Ali alijua uovu na mwisho wa ushenzi wa mlaaniwa Abdu’r-Rahman Ibn Muljim Muradi na kwa kurudia rudia alimuambia kwamba yeye ndiye muuaji wake. Wakati mmoja kwa uwazi alisema: “Napenda aishi, lakini amedhamiria kuniua mimi, na rafiki huyu muovu anatokana na ukoo wa Murad.”

Maelezo haya yameandikwa na Ibn Hajar Makki kuelekea mwisho wa sehemu ya 1 ya Saw’iq, uk. 72. Bado Ali hakukusudia kumuadhibu. Hivyo, hadithi ambayo inaonesha kwamba stahili ya kitendo makhususi au maelezo sio lazima iwe yenye athari wakati wote unaokuja.

Sifa Ya Kuwa Mmojawapo Kwenye Bai’at-E-Ridhwan

Tatu, umesema kwamba kwa vile Masahaba walikuwa katika Bai’at-e-Ridhwan na wakachukua kiapo chao cha utii kwa Mtume, hawakustahili lawama, bali walistahiki kusifiwa kwa sababu wao ndio wanaorejewa kwenye aya tukufu uliyoisoma (48:18).

Wanachuoni watafiti na maulamaa wametoa maoni kwa mapana sana juu ya suala hili, wakisema kwamba ridhaa ya Mungu ya aya hii inahusika tu kwenye kitendo kile makhususi, Bai’at (kiapo cha utii), na kwamba haiendelei bila kikomo.

Ninyi wenyewe mnaelewa kwamba wakati wa tukio la Bai’at kule Hudabiyya, walikuwepo watu 1500, ambao kati yao baadae idadi ya watu walijumuishwa katika ‘aya za unafiki.’

Allah aliwaahidi moto wa milele. Je, inawezekana kwambwa Allah na Mtume wameweza kuridhia baadhi ya watu na kwamba baadhi yao (ya watu hao hao) waje wabakia motoni milele? Kwa hiyo ina maana kwamba ile ridhaa ya Mungu hakuwa kwa ajili ya Bai’at-e-Shajara (kiapo cha utii chini ya mti) peke
yake, bali ilitegemea juu ya imani nyofu na matendo mema.

Wale ambao wameamini katika upweke wa Mungu (Tawhid) na Utumme (Nubwat) na wakala kiapo cha utii walistahiki radhi za Mungu. Walitangazwa kuwa watu wa Peponi. Lakini wale waliokula kiapo cha utii bila imani, au ambao hawakula kiapo, wanastahili ghadhabu Yake. Hakika, Masahaba walifanya matendo mazuri, na kwa ajili ya matendo yao mazuri (kama kula kiapo chini ya mti) lazima wasifiwe. Na hata kama muumini, awe yeye ni Sahaba au la, akifanya kosa, anaweza kukosolewa.

Mashi’a Wanakubali Ubora Wa Masahaba

Madhehebu ya Shi’a siku zote imeelezea matendo mema ya Masahaba. Aidha, hukubali matendo mema hata ya wale ambao wamekuwa ni shabaha ya ukosoaji mkali. Kwa mfano, inatambua kile kiapo chao cha utii cha chini ya mti, kuhama kwao pamoja na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), kushiriki kwao katika vita, lakini vile vile hulaumu na kushutumu matendo yao mabaya.

Hafidh: Ninashangazwa kukusikia wewe ukisema kwamba, Masahaba wa Mtume walifanya matendo maovu. Mtume alitangaza kila mmoja wao ni mlezi na kiongozi wa jumuiya. Alisema katika hadithi mashuhuri kwamba: “Hakika masahaba wangu ni kama nyota; kama mnafuta yeyote kati yao, mtakuwa mmeongoka.” Imani yenu kwa dhahri sio ya kawaida, na hatukubali imani isiyo ya kawaida.

Hadithi Ya “Kuwafuata Masahaba” Yachunguzwa

Muombezi: Ninalazimika kujadili baadhi ya vipengele vya hadithi hii kabla sijaendelea kujibu. Kwa kweli, hakika hatuwezi kuzungumza kuhusu chanzo, usahihi, au udhaifu wa hadthi kwa njia ya kukosoa, kwani tutatoka kwenye mada kuu. Majadiliano yetu yataan- galia kwenye maana yake. Wale amabao wamebarikiwa heshima ya kumuona Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), au ambao wamesimulia hadithi kutoka kwake, wanaitwa Sahaba, iwe walikuwa ni wahamiaji (Muhajir) kutoka Makka au wale waliowasaidia (Ansar) kule Madina au wengine. Kutokuelewana kukubwa mwiongoni mwenu ni kwamba, kwa sababu ya nia zenu nzuri juu ya

Masahaba, mnawachukuliya wote kuwa wameepukana na makosa yote ingawa ukweli ni kinyume chake. Miongoni mwa Masahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), walikuwepo wema na wabaya, ambao Allah na Mtume Wake walikuwa wanawafahamu vizuri sana. Hili linaweza kuthibitishwa vizuri na ile Sura ya Munafiqun (wanafiki) na aya za sura nyingine, kama Tawba ambayo vile vile inajulikana kama Al-Bara’a (Kinga) na Ahzab (koo), ambazo ziliteremshwa kwa ajili ya kuwalaumu Masahaba ambao walikuwa wanafiki na waovu.

Maulamaa wenu mashuhuri wenyewe wameandika katika baadhi ya makosa na matendo mabaya ya Masahaba katika vitabu vyao sahihi. Hisham Bin Muhammad Sa’yib Kalbi, mmoja wa ulamaa mashuhuri wa madhehebu yenu ameandika kitabu juu ya makosa na kasoro za Masahaba. Wanafiki ambao wamelaumiwa na Allah (swt) na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) walikuwa ndumila kuwili, ambao walikuwa Waislamu kwa nje tu.

Nyoyo zao zilikuwa imechafuliwa na dhulma na upotofu; na wote hao walijumuishwa katikakundi la Masahaba. Hivyo tutawezaje kuwa na nia njema kwa Masahaba wote? Na vipi tutakuwa na hakika kwamba kumfuata yeyote kati yao kutahakikisha uwongofu? Je, sio ukweli kwamba katika suala la Aqaba kulikuwa na Masahaba ambao walionekana kuwa waaminifu lakini walikusudia kumuua Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)?

Suala La Aqaba Na Mpango Wa Kumuua Mtukufu Mtume (S.A.W.W.)

Hafidh: Baadhi ya maulamaa wanalichukilia suala la Aqaba kuwa ni ubunifu wa Mashi’a.

Muombezi: Ni vibaya sana kwako wewe kutegemea juu ya imani za baadhi ya watu ambao wana mawazo ya ki-Khawariji na Manasibi. Suala hili kwa uwazi kabisa linaju- likana kwa wote kiasi kwamba maulamaa wenu wenyewe wamelikubali.
Tafadhali hebu rejea kwenye Dala’ilu’n-Nubuwat kilichoandikwa na Hafidh Abu Bakr Ahmad Bin Husain Baihaqi Shafi’i, ambaye ni mmoja wa wanachuoni na mafaqihi wenu maarufu.

Ameandika kisa cha Batn-e-Aqaba kwa nyororo (sanad) sahihi ya wasimuliaji; na vile vile Imamu Ahmad Bin Hanbal, kuelekea mwisho wa Jz. 5 ya Musnad yake, anataarifu kutoka kwa Abu Tufail, na Ibn Abi’l-Hadid anaandika katika Sharhe yake ya Nahju’l-Balagha, na ina- julikana kwa maulama wote kwamba, Mtukufu katika usiku huo alilaani kikundi cha Masahaba.

Nawab: Lilikuwa ni jambo gani, na ni nani hao ambao walitaka kumuua Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)?

Muombezi: Maulamaa wakubwa wa madhehebu zote wameandika kwamba njiani wakati Muhammad anarudi kutoka vita ya Tabuk, wanafiki kumi na wanne walikula njama ya kumuua. Mpango ulikuwa ni kumsukuma kutoka kwenye ngamia wake angukie kwenye mporomoko wakati akipita Aqaba wakati wa usiku, uchochoro mwembamba ambao mtu mmoja tu anaweza kupita. Wakati walipojaribu kutekeleza mpango wao Malaika Jibril alimjulisha Mtume juu ya mpango huo. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akamtuma Hudhaifa Nakha’I kujificha nyuma ya mlima.

Wakati wale wahaini walipowasili na kuzungumza wenyewe pamoja, aliwatambua wote. Saba miongoni mwao wanatokana na Bani Umayya. Hudhaifa alirudi kwa Mtume na kuwataja wote.

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akamuamuru kuiweka siri njama hiyo, na akasema Allah ndiye mlizi wao. Katika sehemu ya kwanza ya usiku Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alianza safari, akifuatiwa na jeshi lake.

Ammar-e-Yasr alimwongoza ngamia kwa mbele na Hudhaifa alikuwa akimswaga kwa nyuma. Wakati walipofikia kile kichochoro chembamba, wale wanafiki walimtupia ngamia mifuko yao ya ngozi iliyojaa mchanga (au makopo ya mafuta), ikatoa sauti kubwa, wakidhania kwamba mnyama yule aliyetishika atamtupa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) chini ya ule mporomoko mkali.

Lakini Allah (swt) alimkinga na wahaini wakakimbia na kutokomea katika kundi. Je, watu hawa hawakuwemo mwiongoni mwa Masahaba? Je, ni kweli kwamba kuwafuata wao maana yake ni njia ya wokovu? Wakati tunapozungumza kuhusu Masahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wa Allah kwa nini tufumbie macho makosa yao?

Mtume Kamwe Hakutuamrisha Tuwafuate Waongo

Mikesha iliyopita nilitaja tabia ya Abu Huraira, nikiwaeleza kwamba Khalifa Umar alimtandika viboko kwa sababu alizoea kusimulia hadithi za uwongo kutoka kwa Mtume. Je, hakuwa miongoni mwa Masahaba? Je, hakusimulia idadi kubwa ya hadithi kwa uongo? Halikadhalika, hawakuwa Masahaba wengine kama Sumra Bin Junda wamejumuishwa miongoni mwao? Je, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wa Allah anaweza kuamuru jumuiya kufuata waongo na waghushaji?

Kama hadithi hii ni sahihi, yaani, kwamba kama tukimfuata yeyote katika masahaba, tutaongoka, basi tafadhali tujulishe ni yupi tumfuate, kama masa- haba wawili wanakwenda njia mbili tofauti.

Au kama kuna makundi mawili kila moja linapigana dhidi ya jingine, au kila moja kinyume na jingine, ni yupi ambaye itatupasa sisi kumuunga mkono?

Hafidh: Kwanza, masahaba watukufu wa Mtume wa Allah hakuwa maadui wenyewe kwa wenyewe. Na hata kama mmoja alimpinga mwingine, lazima tuupime ukweli huo vizuri. Yule ambaye ni safi na ambaye maelezo yake yana mantiki zaidi anapaswa kufuatwa.

Muombezi: Kama, kwa mujibu wa maelezo yako, tunafanya uchunguzi makini na kuona kwamba mmoja wao ni ni safi na yuko katika upande wa haki, basi kundi la upande mwingine la masahaba lazima liwe chafu na kwenye upande wa makosa. Basi hadithi hii kimsingi inapoteza sifa kwa sababu haiwezikani kwamba masahaba wasiokubaliana wanaweza wote kuwa vyanzo vya uongofu.

Upinzani Wa Masahaba Huko Saqifa

Kama hadithi hii ni sahihi kwa nini mnaleta upinzani dhidi ya Mashi’a, kwa sababu wao wamefuata kundi la Masahaba kama Salman, Abu Dharr, Mikidadi, Ammar-e-Yasir, Abu Ayyub Ansar, Hudhaifa Nakha’i na Khuzaima Dhu’sh-Shahadatain, nk., ambao nimewataja katika mikesha iliyopita? Kwa hakika watu hawa hawakula kiapo cha utii kwa Abu Bakr. Kwa hiyo, kati ya Masahaba waliopingana wenyewe kwa wenyewe, ni nani waliokuwa upande wa haki? Kwa vyovyote vile kundi moja lilikuwa upande wa makosa ingawa hadithi uliyonukuu hutuambia kwamba tunaweza kufuata yeyote kati ya Masahaba na kuongoka.

Upinzani Wa Sa’d Bin Ubaida Kwa Abu Bakar Na Umar

Je, Sa’d Bin Ubaid hakuwa mmoja wa Masahaba ambao hawakula kiapo kwa Abu Bakr na Umar? Wanahistoria wote wa Shi’a na Sunni kwa pamoja wanashikilia kwamba yeye alikwenda Syria na akaishi kule mpaka katikati ya kipindi cha Ukhalifa wa Umar, ndipo ali- uawa. Kwa hiyo kumfuata yeye na kumpinga Abu Bakr na Umar, kwa mujibu wa hadithi hii, ni njia ya wokovu.

Talha Na Zubair Walimkabili Ali Huko Basra

Je, Talha na Zubair sio miongoni mwa Masahaba waliokula kiapo cha utii chini ya mti? Je, hawakumpinga mrithi wa haki Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), Khalifa wa nne anayekubaliwa kwa mujibu wa imani yenu? Je, hawakuwa Masahaba hawa ni wenye kuhusika na umwagaji wa damu ya Waislamu wasio idadi? Sasa, tafadhali tujulishe ni lipi katika makundi haya mawili ya Masahaba ambao walipigana wenyewe kwa wenyewe ambalo kweli limeongoka. Kama utasema kwamba, kwa vile makundi yote yalikuwa na utii yalikuwa katika upande wa haki, utakuwa umekosea. Haiwezikani kudai kwamba makundi yanayopingana yote yawe yameongoka.

Kwa hiyo ina maana kwamba Masahaba ambao walikuwa upande wa Ali walikuwa kwa hakika wao ndio walioongoka. Kundi lililokuwa ule upande mwingine lilichukuwa njia ya makosa; na huu ni uthibitisho mwingine wa kukataa maelezo yako kwamba Masahba wale wote ambao walikuwepo katika Bai’at-e-Ridhwan, chini ya mti, walikuwa wameongoka.

Miongoni mwa wale ambao walikula kiapo cha utii walikuwa hawa wawili, Talha na Zubair, ambao vile vile walipigana dhidi ya khalifa wa haki. Kwa hakika wamepigana dhidi ya mtu ambaye kuhusu yeye Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Ewe Ali, kupigana dhidi yako ni kupigana dhidi yangu.” Je, hii si sawa na kupingana dhidi ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)? Basi vipi unasema kwamba neno Ashab au kuwepo chini ya mti wa kiapo ni uthibitisho wa wokovu?

Mu’awiya Na ‘Amr Ibn Al-As Walizoea Kumlaani Na Kumtukana Ali

Muawiya na Amr al-As walikuwa Masahaba lakini bado walipigana dhidi ya mrithi wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na kumlaani na kumtukana Ali katika mikutano ya hadhara na hata katika hutuba zinazotolewa baada ya Sala ya Ijumaa. Walifanya hivyo licha ya ukweli, kama ilivyoandikwa na maulamaa wakubwa wa madhehebu yenu katika vitabu vyao sahihi, kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alirudia rudia kusema: “Yule ambaye anamtukana au kumlaani Ali, ananitukana mimi. Yule ambaye ananitukana mimi anamtukana Allah.”

Mwanachuoni Taftazani kwa kinaganaga alishughulikia suala hili katika Sharhe Maqasid. Yeye anaandika kwamba kwa vile Masahaba walikuwa maadui wenyewe kwa wenyewe, baadhi yao walikuwa wamepotea kutoka kwenye njia ya haki. Baadhi yao kwa ajili ya husda na matamanio ya kidunia, walifanya aina zote za makosa ya kiukatili.

Ni wazi kwamba Masahaba wengi, ambao hawakuwa ma’sum (wasiokosea) walifanya matendo maovu. Lakini baadhi ya maulamaa kwa sababu wanawapendelea, walijaribu kuficha makosa yao. Kuna hoja nyingi za kukataa hadithi hii iliyoko kwenye mjadala. Hakuna shaka kwamba hadithi hii ni ya kughushi. Maulamaa wenu wengi wameonyesha wasiwasi wao kuhusu usahihi wa vyanzo vyake.

Vyanzo Vya Hadithi “Masahaba Wangu Ni Kama Nyota” Ni Dhaifu

Baada ya kunukuu hadithi hii katika kitabu chake Sharhush-Shifa, Jz. 2. uk. 91, Kadhi Ayaz anasema kwamba Darqutni katika kitabu chake Faza’il na Ibn Abdu’l-Birr wasema kwamba hadithi hii sio sahihi.

Vile vile imesimuliwa kutoka kwa Abd Bin Hamid katika Musnad yake ambaye ananukuu kutoka kwa Abdullah Ibn Umar kwamba Bazar alikataa kukubali usahihi wa hadithi hii. Vile vile alisema kwamba Ibn Adi ananukuu katika kitabu chake Kamil pamoja na rejea zake mwenyewe kutoka kwa Nafi, na yeye kutoka Abdullah Ibn Umar, kwamba vyanzo vya hadithi hii ni dhaifu sana. Baihaqi vile vile ameelezwa kwamba aliandika kuwa habari ya hadithi hii inajulikana sana lakini vyanzo vyake ni dhaifu.

Miongoni mwa vyanzo vya hadithi hii ni Harith Bin Ghazin, ambaye tabia yake inaju- likana, na Hamza Ibn Abi Hamza Nussairi, ambaye alishutumiwa kwa kuongopa. Udhaifu wa hadithi hii uko wazi. Ibn Hazm vile vile anasema kwamba hadthi hii ni ya kubuni na ni yenye kukataliwa. Hivyo katika majadiliano yetu hatuwezi kutengemea juu ya hadithi kama hii yenye nyororo (asnad) dhaifu ya vyanzo. Hata tukichukulia kwamba hadithi hii ilikuwa sahihi, isingeweza kutumika katika maana ya ujumla; ingeashiria tu kwa wale Masahaba watiifu na wachamungu ambao kwa mujibu wa amri ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wamefuata Kitabu cha Allah na kizazi kitukufu cha Mtume.

Masahaba Hawakuwa Ma’sum (Wasio Kosea)

Nikiwa nimeyasema haya, kama nitawakosoa baadhi ya Masahaba, msinichukulie mimi kama si mwadilifu. Hata hivyo wao walikuwa ni wanadamu, na iliwezekana wao kukosea.

Hafidh: Sisi pia tunaamini kwamba Masahaba hawakuwa ma’sum, lakini wakati huo huo ni ukweli unaokubalika kwamba wote kwa pamoja walikuwa ni watu wema. Hawakufanya makosa yoyote.

Muombezi: Madai yako ni mno, kama ukisisitiza kwamba wote walikuwa waadilifu na walioepukana na makosa, kwa vile katika vitabu sahihi vilivyoandikwa na maulamaa wenu wanahoji dhidi ya hilo. Wanatuambia kwamba hata baadhi ya Masahaba wakubwa wakati mwingine walifanya makosa.

Hafidh: Hatuzitambui taarifa kama hizo. Tafadhali tueleze kuhusu taarifa hizo kama unaweza.

Muombezi: Tukiyaacha yale waliyoyafanya wakati wa zama za ujinga (yaani, kabla ya kuja kwa Uislamu), wamefanya maovu mengi baada ya kusilimu. Inatosha kutaja tukio moja tu kwa njia ya mfano. Maulamaa wenu wakubwa wanaandika katika vitabu vyao sahihi kwamba katika ule mwaka wa kuiteka Makka (8 A.H.) baadhi ya wale Masahaba wakubwa walijiingiza katika burudani ya sherehe na shamra shamra na kwa siri wakany- wa pombe.

Hafidh: Hiki kwa hakika ni kisa cha kubuni. Wakati pombe ilikuwa imetangazwa kuwa ni haramu, Masahaba wa kuheshimika hawakuhudhuria japo hafla kama hizo, sembuse kuta- ja unywaji wa tembo.

Muombezi: Haikubuniwa kamwe na wapinzani. Kama itakuwa imebuniwa kwa hali yoyote ile, basi ilifanywa hivyo na ulamaa wenu wenyewe.

Nawab: Kama kulikuwa na hafla kama hiyo, majina ya huyo mwenyeji na wageni vilevile yatakuwa yametajwa. Unaweza kuelezea nukta hiyo?

Muombezi: Ndio, maulamaa wenu wenyewe wameielezea hiyo.

Kunywa Pombe Kwa Masahaba Kumi Katika Mkutano Wa Siri

Ibn Hajar katika kitabu chake Fathu’l-Bari, Jz. 10, uk. 30, anaandika kwamba Abu Talha Zaid Bin Sahl alitayarisha hafla ya pombe katika nyumba yake na akakaribisha watu kumi. Wote walikunywa pombe na Abu Bakr alisoma baadhi ya mashairi kuwasifia baadhi ya makafiri ambao waliuliwa katika vita ya Badr.

Nawab: Je, majina ya wageni yametajwa vile vile? Kama ndivyo, tafadhali tujulishe.

Muombezi: (1) Abu Bakr Bin Abi Kuhafa, (2) Umar Ibn Khattab, (3) Abu Ubaida Garra, (4) Ubai Bin Ka’b, (5) Sahl Bin Baiza, (6) Abu Ayyub Ansari, (7) Abu Talha (mwandaaji), (8) Abu Dajjana Samak Bin Kharsa, (9) Abu Bakr Bin Shaghuls, (10) Anas Bin Malik, ambaye alikuwa na umri wa miaka 18 wakati ule na ambaye alikuwa ndiye mgawaji wa pombe hiyo. Baihaqi katika Sunan yake, Jz. 8, uk. 29 vile vile amesimulia kutoka kwa Anas mwenyewe kwamba yeye alikuwa ndiye mdogo kuliko wote wakati huo na alikuwa akiwapimia pombe. (Kufikia hapa kukawa na vurumai kubwa ndani ya mkutano huo.)

Sheikh: Naapa kwa jina la Allah kwamba kisa hiki kimebuniwa na maadui!

Muombezi: Umehamaki sana na umetoa kiapo cha kufuru! Lakini hauko katika makosa ya moja kwa moja kabisa. Masomo yako yana kikomo. Kama ungesoma kwa mapana zaidi, ungejua kwamba maulamaa wako mwenyewe wameandika yote haya. Sasa yakubidi uombe msamaha wa Allah.

Sasa ninalazimika kuelezea mambo kwa mujibu wa maelezo ya maulamaa wenu wenyewe. Muhammad Bin Isma’il Bukhari katika Sahih yake (akifafanua juu ya Ayat-e-Khamr, ‘aya inayohusu pombe’, katika sura ya Ma’ida ya Qur’ani Tukufu); Muslim Ibn Hajar katika Sahih yake (Kitab-e-Ashraba Bab-e-Tahrimu’l-Khamr); Imamu Ahmad Bi Hanbal katika Musnad yake, Jz. 30, uk. 181 na 227; Ibn Kathir katika Tafsir yake, Jz. 11, uk. 93; Jalalu’d- Din Suyut katika Durr’l-Mansur, Jz. 2, uk. 321; Tabari katika Tafsir yake, J. 7, uk. 24; Ibn Hajar Asqalani katika Isaba, Jz. 4, uk. 22 na Fathu’l-Bari, Jz. 10, uk. 30; Badru’-d-Din Hanafi katika Umdatu’l-Qari, Jz. 10, uk. 84; Baihaqi katika Sunan yake, uk. 286 na 290; na wengine wameandika ukweli huu pamoja na maelezo marefu.

Sheikh: Pengine mambo haya yalitokea kabla pombe haijafanywa haramu.

Muombezi: Tunayoyapata kutoka kwenye vitabu vya Tafsir na historia yanaonesha kwamba hata baada ya aya za kuharamisha pombe baadhi ya Waislamu na Masahaba waliendelea kunywa pombe iliyokatazwa.

Muhammad Bin Jarir Tabari anasimulia katika Tafsir-e-Kabir, Jz. 2, uk. 203, kutoka kwa Abil Qamus Zaid Bin Ali, ambaye alisema Allah ameteremsha mara tatu aya zinazokataza pombe. Katika aya ya kwanza anasema:

يَسْأَلُونَكَ عَنِ الْخَمْرِ وَالْمَيْسِرِ ۖ قُلْ فِيهِمَا إِثْمٌ كَبِيرٌ وَمَنَافِعُ لِلنَّاسِ وَإِثْمُهُمَا أَكْبَرُ مِنْ نَفْعِهِمَا ۗ{219}

Wanakuuliza kuhusu ulevi na kamari. Sema: katika hivyo mna dhambi kubwa na manufaa kwa watu, lakini dhambi zake ni kubwa kuliko manufaa yake…” (2:219)

Lakini Waislamu hawakuacha pombe mara moja. Wakati mmoja watu wawili, wakiwa wamelewa, walisali Swala zao na kuzungumza mambo yasio kuwa na maana, aya nyingine iliteremshwa, isemayo:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَقْرَبُوا الصَّلَاةَ وَأَنْتُمْ سُكَارَىٰ حَتَّىٰ تَعْلَمُوا مَا تَقُولُونَ{43}

“Enyi ambao mmeamini! msikaribie Sala hali mmelewa, mpaka myajue mnayo yasema…” (4:43)

Hata baada ya aya hii, unywaji wa pombe uliendelea, lakini watu hawakusali wakiwa wamelewa. Siku moja mtu mmoja alikunywa pombe (kwa mujibu wa taarifa ya Bazar, Ibn Hajar na Ibn Mardawiyya mtu huyo alikuwa ni Abu Bakr) na akatunga shairi kwa ajili ya makafiri ambao waliuawa katika vita ya Badir.

Wakati Mtume aliposikia hili alikasirika sana. Alikwenda kule inakofanyika hafla hiyo na akataka kumpiga. Yule mtu akasema, “Naomba kinga ya Allah kutokana na ghadhabu ya Allah na Mtume Wake. Allah awe shahidi yangu, sitakunywa pombe tena.” Kisha aya ifuatayo ikateremshwa:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّمَا الْخَمْرُ وَالْمَيْسِرُ وَالْأَنْصَابُ وَالْأَزْلَامُ رِجْسٌ مِنْ عَمَلِ الشَّيْطَانِ فَاجْتَنِبُوهُ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ {90}

“Enyi ambao mmeamini! Bila shaka ulevi, na kamari na kuabudu masanamu na kupiga ramli, ni uchafu katika kazi ya shetani. Basi jiepusheni navyo, ili mpate kufanikiwa.” (5:90).

Miongoni mwa Masahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) walikuwepo wazuri na wabaya kama ambavyo wapo miongoni mwa Waumini na Waislamu wengine. Wale miongoni mwao ambao walijaribu kumtii Allah na Mtume Wake walifikia daraja ya juu. Wale ambao walifuata tamaa za kidunia walikuwa wakidharauliwa na wengine. Hivyo wale ambao wanakosoa Masahaba wa kidunia, wanafanya hivyo kwa sababu fulani.

Yale matendo maovu ya baadhi ya masahaba, ambayo yameandikwa katika vitabu sahihi vya maulamaa wenu wenyewe, vile vile yanafaa kulaumiwa kwa mujibu wa ushahidi wa Qur’ani Tukufu. Mashi’a wanawalaumu katika misingi hiyo. Kama kuna majibu ya mantiki kwenye hoja hii, tuko tayari kuikubali.

Uvunjaji Kiapo Wa Masahaba

Inashangaza kwamba hata baada ya kusikia sifa zao za kulaumika (nimetaja chache tu kati ya nyingi) bado mnaendelea kuniuliza kuhusu maovu yao! Sasa ningependa kuwasilisha mfano mwingine wa matendo yao ya kuchikiza, ambayo yameandikwa katika vitabu vyote vya madhehebu zote: “Uvunjaji wa kiapo”. Allah amelifanya ni wajibu suala la mtu kutekeleza ahadi. Anasema: “Na timizeni ahadi ya Allah mnapo ahidi, wala msivunje viapo baada ya kuvithibitisha…” (16:91)

Na tena Allah amewaita wale ambao wanaovunja kiapo walaaniwa. Anasema: “Na wale ambao wanavunja ahadi ya Allah baada ya kuzifunga, na wanayakata yale ambayo Allah ameamrisha yaungwe, na wanafanya ufisadi katika nchi; hao ndio watakaopata laana, na watapata nyumba mbaya.” (13:25)

Hivyo ni wazi kutoka kwenye aya za Qur’ani Tukufu na kutoka katika idadi kubwa ya hadithi kwamba kuvunja kiapo ni dhambi kubwa, hususan kiapo kilichofanywa kwa Allah na Mtume wake. Uzito wa kosa hili ulikuwa mkubwa sana kwa Masahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Hafidh: Ni kiapo gani cha utii ambacho Masahaba walifanya na Mtume na wakakivunja? Itawezaje kuwa chini ya mashambulizi ya aya za Qur’ani? Nadhani kwamba kama utaliangalia suala hili kwa makini utakubali kwamba mambo yote haya ni ubunifi mtupu wa Mashi’a. Masahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) walikuwa wameepukana na makosa yote haya.

Katika Qur’ani Tukufu “Wakweli” Humaanisha Muhammad Na Ali

Muombezi: Nimekuambieni mara kwa mara kwamba Mashi’a wamejifunga kuwafuata viongozi wao. Vinginevyo hawawezi kuwa Mashi’a. Qur’ani Tukufu imetoa ushahidi wa ukweli wa viongozi wao. Maulamaa wenu mashuhuri kwa mfano, Imamu Tha’labi na Jalalu’d-Din Suyut katika vitabu vyao vya Tafsir, Hafiz Abu Nu’aim Ispahani katika kitabu chake Ma Nazal mina’l-Qur’ani fi Ali, Khatib Khawarizmi katika Manaqib, Sheikh Sulayman Balkhi Hanafi katika Yanabiu’l-Mawadda, sura ya 39, akisimulia kutoka kwa Khawarizmi, Hafiz Abu Nu’aim na Hamwaini na Muhammad Bin Yusuf Ganji Shafi’i katika Kifayatut-Talib, sura ya 62, wote wamenukuu kutoka kwenye kitabu cha historia cha mwanachuoni mkubwa Muhaddith-e-Sham kwamba katika aya Tukufu,

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّهَ وَكُونُوا مَعَ الصَّادِقِينَ {119}

“Enyi mlioamini! Mcheni Allah na kuweni pamoja na wakweli”. (9:119)

Wakweli maana yake Muhammad na Ali. Hivyo wafuasi wa familia hii tukufu hawawezi kuwa waongo au waghushaji kwa sababu ni yule mtu tu ambaye hana sababu za kweli na na zenye nguvu ndiye anaweza kusema uwongo au kughushi visa vya uwongo na kupata kitu cha kutegemea juu ya njia hii. Wanachosema Mashi’a kimeandikwa na maulamaa wenu wenyewe.

Kwanza mnapaswa kuwakataa maulamaa wenu, ambao wameandika mambo haya. Lau maulamaa wenu wasingeandika kuhusu uvunjaji wa kiapo wa Masahaba katika vitabu vyao sahihi, nisingelitaja hilo katika mkutano huu.
Hafidh: Ni nani katika maulamaa wa ki-Sunni ambaye ameandika kwamba Masahaba walivunja kiapo cha utii. Maneno matupu hayawezi kusaidia.

Muombezi: Mimi sio ninazungumza tu. Hoja yangu ni yenye mantiki kamili. Masahaba walivunja kiapo chao cha utii mara nyingi. Walivunja kiapo cha utii ambacho kwacho Mtume wa Allah aliwaamuru wao, cha muhimu zaidi ni kiapo cha utii kule Ghadir-e-Khum.

Hadithi Ya Ghadir Na Asili Yake

Maulamaa wote, wa Shi’a na Sunni wanakubali kwamba, katika mwaka wa 10 wa Hijra, Mtume wa Allah akiwa anarudi kutoka kwenye hija yake ya mwisho, aliwakusanya pamoja Masahaba wote pale Ghadir-e-Khum siku ya 18 Dhi’l-Hijja. Baadhi ya wale ambao walikuwa wametangulia waliitwa warudi kwa amri ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na wale ambao walikuwa nyuma walingojewa.

Maulamaa wenu wengi wanahistoria na vyanzo vya Shi’a wanaioa idadi ya watu 70000, na baadhi ya maulamaa wenu wengine, kwa mfano, Tha’labi katika kitabu chake cha Tafsir, Sibt Ibn Jauzi katika Tadhkirat’u-Khasa’isi’l- Umma fi Ma’rifati’l-Aimma na wengine wameandika kwamba walikuwepo watu 120,000 waliokusanyika pale.

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliamuru itengenezwe mimbari. Alipanda katika mimbari na akatoa hotuba ndefu, ambayo sehemu yake kubwa ikiwa imejaa sifa na tabia za Amir’l-Muminin. Alisoma takribani aya zote zilizoshuka kwa ajili ya kumsifu Ali na akawakumbusha watu cheo kitukufu cha umakamu wa Amirul-Mu’minin.

Kisha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema: Enyi watu! Je, mimi sina mamlaka zaidi juu ya nafsi zenu kuliko ninyi wenyewe?” Rejea hii ni kwenye aya tukufu, “ Mtume ni bora zaidi kwa waumini kuliko nafsi zao…” (33:6)

Mkusanyiko ule ukajibu kwa sauti moja “Hakika, Ewe Mjumbe wa Allah!” Kisha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akatangaza: “Yule ambaye mimi ni (maula kwake) mwenye kumtawalia mambo yake, huyu Ali ni (maula kwake) mwenye kumtawalia mambo yake.” Baada yakusema hivi alinyoosha mikono yake na akaomba kwa Allah. “Ewe Allah, kuwa rafiki kwa yule ambaye ni rafiki kwake (yaani Ali) na kuwa adui kwa yule ambaye ni adui kwake (yaani Ali) msaidie yule ambaye anamsaidia yeye na mtelekeze yule ambaye anamtelekeza yeye.”

Kisha hema lilikitwa kwa amri ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ambaye alimuamuru Kiongozi wa waumini Ali kukaa ndani ya hema. Umma wote uliamriwa kutoa kiapo cha utii kwa Ali.

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema kwamba ametoa maelekezo haya kulingana na amri ya Allah. Mtu wa kwanza kutoa kiapo ni siku hiyo alikuwa ni Umar. Kisha Abu Bakr, Uthmani, Talha, na Zubair walifuatia, na watu wote hawa waliendelea kutoa kiapo cha utii kwa muda wa siku tatu (yaani wakati ambapo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alibakia pale).

Hafidh: Unaweza kuamini kwamba tukio la umuhimu kama wa namna hiyo limetokea kama inavyodaiwa na wewe na kwamba hakuna hata mmoja katika maulamaa maarufu aliyelisimulia hilo?

Muombezi: Sikutazamia maelezo kama haya kutoka kwako. Habari ya Ghadir Khum iko wazi kama mwanga wa mchana na hakuna yeyote ila shupavu na mtu mkaidi ndiye awezaye kuleta fedheha kwa kukataa tukio kama hili. Suala hili muhimu limeandikwa kwenye kumbukumbu na maulamaa wenu wote wachamungu katika vitabu vyao sahihi. Ningependa kutaja hapa baadhi ya majina ya waandishi na vitabu vyao ili uelewe kwam- ba maulamaa wenu wote maarufu walitegemea hadithi hii.

1. Imam Fakhru’d-Din Razi – Tafsir-e-Kabir Mafatihu’l-Ghaib.
2. Imam Ahmad Tha’alabi – Tafsir-e-Kashfu’l-Bayan.
3. Jalalu’d-Din Suyuti – Tafsir-e-Durru’l-Manthur.
4. Abu’l-Hasan Ali Bin Ahmad Wahidi Nishapuri – Asbabu’n-Nuzul.

5. Muhammad Bin Jarir Tabari – Tafsiru’l-Kabir.
6. Hafidh Abu Nu’aim Ispahani – Ma Nazal Mina’l-Qur’ani fi Ali na Hilyatu’l-Auliya.
7. Muhammad Bin Isma’il Bukhari – Ta’rikh, Jz. 1, uk. 375.
8. Muslim Bin Hajjaj Nishapuri – Sahih, Jz. 2, uk. 325.
9. Abu Dawud Sijistani – Sunan.
10. Hafidh Ibnu’l-Iqda – Kitabu’l-Wilaya.
11. Ibn Kathir Shafi’i Damishqi – Ta’rikh.
12. Imam Ahmad Ibn Hanbal – Musnad Jz. 4, uk. 281&371.
13. Abu Hamid Muhammad Bin Muhammad Al-Ghazali – Sirru’l-Alamin.
14. Ibn Abdu’l-Birr – Isti’ab.
15. Muhammad Bin Talha Shafi’i – Matalibus-Su’ul, uk. 16.
16. Ibn Maghazili Faqih Shafi’i – Manaqib.
17. Nuru’d-Din Bin Sabbagh Maliki – Fusulu’l-Muhimma.
18. Husain Bin Mas’ud Baghawi – Masabihus-Sunna.
19. Abu’l-Mu’ayyid Muwafiq Bin Ahmad Khatib Khawarizmi – Manaqib.
20. Majdu’d-Din Bin Athir Muhammad Bin Muhammad Shaibani – Am’u’l-Usul.
21. Hafidh Abu Abdu’r-Rahman Ahmad Bin Ali Nisa’i – Khasa’isu’l-Alawi na Sunan.
22. Sulaiman Balkhi Hanafi – Yanabiu’l-Mawadda, Sura ya 4.
23. Shahabu’d-Din Ahmad Bin Hajar Makki – Sawa’iq Muhriqa na Kitabu’l-Manhu’l- Malakiyya, hususan Sawa’iq, sehemu ya 1, uk. 25. pamoja na ushupavu wake mkubwa, anasema: “Hii ni hadithi ya kweli; ukweli wake hauwezi kutiliwa shaka. Hakika imesimuliwa na Tirmidhi, Nisa’i na Ahmad, na kama ikichunguzwa, vyanzo vyake ni vizuri vya kutosha.”

24. Muhammad Bin Yazid Hafiz Ibn Maja Qazwini – Sunan.
25. Hafidh Abu Abdullah Muhammad Bin Abdullah Hakim Nishapuri – Mustadrak.
26. Hafidh Sulaiman Ibn Ahmad Tabrani – Aust.
27. Ibn Athir Jazari – Usudu’l-Ghaiba.
28. Yusuf Sibt Ibn Jauzi – Tadhkiratu’l-Khasa’isu’l-Umma, uk. 17.
29. Abu Umar Ahmad Bin Abi Abd Rabbih – Iqdu’l-Farid.
30 Allama Samhudi – Jawahiru’l-Iqdain.
31. Ibn Taimiyya Ahmad Bin Abdu’l-Halim– Minhajus-Sunna.
32. Ibn Hajar Asqalani – Fathu’l-Bari na Tahdhibut-Tahdhib.
33. Abdu’l-Qasim Muhammad Bin Umar Jarrullah Zamakhshari – Rabiu’l-Abrar.
34. Abu Sa’id Sijistani – Kitabu’d-Darayab Fi Hadithi’l-Wilaya.
35. Ubaidullah Bin Abdullah Haskani – Du’atu’l-Huda ila Ada Haqqi’l-Muwala.
36. Razin Bin Mu’awiya Al-Abdari – Jam Bainus-Sahihis-Sitta
37. Imam Fakhru’d-Din Razi anasema katika Ktabu’l-Arba’in kwamba jumuiya yote kwa pamoja
wanathibitisha hadithi hii.
38. Muqibili – hadithu’l-Mutawatira.
39. Suyut – Ta’rikhu’l-Khulafa.
40. Mir Sayyid Ali Hamadani – Mawaddatu’l-Qurba.
41. Abu Fath Nazari – Khasa’is’u’l-Alawi
42. Khwaja Parsa Bukhari – Faslu’l-Khitab.
43. Jamaluddin Shirazi – Kitabu’l-Arba’in.
44. Abdul Ra’ufu’l-Manawi – Faizu’l-Qadir fi Sharh-i-Jamius-Saghir.
45. Muhammad Bin Yusuf Ganji Shafi’i – Kifayatut-Talib, sehemu ya 1.
46. Yahya Bin Sharf-Nauwi – Tahzibu’l-Asma wa’l-Lughat.
47. Ibrahim Bin Muhammad Hamwaini – Fara’idus-Simtain.
48. Kadhi Fadhlullah Bin Ruzhahan – Ibtalu’l-Batil.
49. Shamsuddin Muhammad Bin Ahmad Sharbini – Siraju’l-Munir.
50. Abul Fath Shahristani Shafi’i – Milal wa’n-Nihal.
51. Hafidh Abu Bakr Khatib Baghdadi – Ta’rikh.
52. Hafidh Ibn Asakir Abul-Qasim Damishqi – Ta’rikh-i-Kabir.
53. Ibn Abi’l-Hadid Mutazali – Sharhe Nahju’l-Balagha
56. Ala’uddin Samnani – Urwatu’l-Wuthqah.
57. Ibn Khaldun – Muqaddima.
58. Mawlana Ali Muttaqi Hindi – Kanzu’l-Ummal.

59. Shamsuddin Abul Khair Damishiqi – Asanu Matalib.
60. Sayyid Sharif Hanafi Jurjani – Sharh-i-Mawaqit
61. Nizamuddin Nishapuri – Tafsir-I-Ghara’ibu’l-Qur’ani.

Hadithi Ya Ghadir Imesimuliwa Na Tabari, Ibn Iqda Na Haddad

Nimesimulia vyanzo nilivyoweza kukumbuka. Lakini zaidi ya Maulamaa wenu wakubwa mia tatu wameisimulia hadithi ya Ghadir, aya za baligh (kuhubiri), kamalu’d-Din (ukamilifu wa dini), na mazungumzo katika eneo la Msikiti, kutoka kwa Masahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) zaidi ya mia moja.

Kama tungetakiwa kueleza majina ya wasimuliaji wote hawa, yangetengeneza kitabu kamili. Hata hivyo, kiasi hiki, kinatosha kuthibitisha kwamba hadithi hii inakubaliwa na wote kama hadithi ya kweli.

Baadhi ya Maulamaa wenu wakubwa wameandika vitabu juu ya suala hili. Kwa mfano, mufasir mashuhuri na mwanahistoria wa karne ya nne hijiriya, Abu Ja’far Muhammad Bin Jarir Tabari (amekufa 310 A.H.), anatoa maelezo kamili ya hadithi ya Ghadir katika kitabu chake “Kitabu’l-Wilaya” na ameisimulia kupitia sanad sabini na tano za wapokezi.

Hafidh Abu’l-Abbas Ahmad Bin Sa’id Abdu’r-Rahman Al-Kufi, mashuhuri kwa jina la Ibn Iqda (amekufa 333 A.H.), amesimulia hadithi hii sharif katika kitabu chake “Kitabu’l- Wilaya” kupitia sanad 125 za wapokezi kutoka kwa Masahaba 125 wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Ibn Haddad Hafidh Abu ‘l-Qasim Haskani (amekufa 492 A.H.), katika kitabu chake “Kitabu’l-Wilaya”, amesimulia kwa urefu hadithi ya Ghadir sambamba na kushuka kwa aya za Qur’ani. Kwa ufupi, wanachuoni wenu wote wateule na maulamaa wa daraja za juu (isipokuwa idadi ndogo ya wapinzani washupavu - wakaidi), wamenukuu asili ya hadithi hii kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.),ambaye alimtangaza Ali kama makamu wake siku ya mwezi 18 Dhu’l-Hijja katika mwaka wa hija yake ya mwisho.

Vile vili ni ukweli kwamba Khalifa Umar alikuwa wa kwanza miongoni mwa Masahaba kuonesha furaha yake juu ya tukio hili. Huku akiwa ameushika mkono wa Ali, alisema: “Hongera ewe Ali! Asubuhi hii imeleta neema kubwa kwako. Umekuwa maula wangu na maula wa waumini wote wanaume na waumini wanawake.”

Ushauri Wa Jibril Kwa Umar

Mwanafiqh wa ki-Shafi’i, Mir Sayyid Ali Hamadani wa karne ya nane hijiriyya, mmoja wa wanachuoni wa kutengemewa wa madhehebu yenu, anaandika katika kitabu chake “Mawaddatu’l-Qurba,” Mawadda ya 5, kwamba idadi kubwa ya Masahaba wamemnukuu Khalifa Umar katika sehemu tofauti akisema:

“Mtume wa Allah alimfanya Ali Maula, mkuu na kiongozi wa taifa (la ki-Islamu). Alitangaza katika mkutano wa hadhara kwamba yeye (Ali) ni maula wetu. Baada ya kuomba kwa ajili ya rafiki zake na kuwalaani adui zake, alisema: ‘Ewe Allah! Wewe ni shahidi wangu.’ (yaani, ‘Nimekamilisha jukumu langu la utume.’).

Katika tukio hili kijana wa kupendeza mwenye kunukia uzuri alikuwa amekaa kando yangu. Aliniambia, ‘Hakika Mtume wa Allah amefungamana na agano ambalo hakuna yeyote wa kulivunja isipokuwa mnafiki. Hivyo Umar! Jiepushe kutokana na kulivunja.’

Nilimueleza Mtume wa Allah kwamba wakati anaongea na mkusanyiko ule wa watu, kijana wa kupendeza, mwenye kunukia uzuri alikuwa amekaa kando yangu na kwamba aliniambia kitu kama hicho.

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema, ‘hakuwa wa kizazi cha Adam, bali alikuwa Jibril, (ambaye alitokea katika umbo hilo). Alitaka kusisitiza kuhusu nukta ambayo nimeitangaza kuhusu Ali.’”

Sasa nataka kutafuta haki kutoka kwenu, je, ilikuwa sahihi kwa wao kuvunja angano imara na Mtume wa Allah ndani ya miezi miwili, kuenda kinyume na kiapo chao kitakatifu cha utii kwa Ali, kuchoma moto nyumba yake, kuchomoa panga dhidi yake, kumfedhehesha, kumburuza mpaka msikitini kumlazimisha kula kiapo cha utii?

Hafidhi: Sikutengemea kwamba mwanachuoni wa kuheshimiwa na Sayyid mstaarabu kama wewe ungelihusisha mambo ya kidunia kwa Masahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliwatangaza wao kwamba ni chanzo cha uongofu kwa ajili ya umma wakati aliposema: “Masahaba wangu ni kama nyota; kama mkimfuata yeyote kati yao, mtaongoka.”

Hadithi Ya “Kuwafuata Masahaba” Sio Sahihi

Muombezi: Kwanza ningekuomba usirudie kitu kile kile kila mara. Punde tu ulihoji kutoka kwenye hadithi hii hii na nimekupa majibu yake.

Masahaba kama watu wengine walikuwa ni wenye kufanya makosa. Hivyo wakati wanathibishwa kwamba wao sio masum (wasiokosea), kwa nini mtu ashangae, kama pamoja na ushahidi sahihi, mambo ya kidunia yanahusishwa kwao? Pili ili kuisafisha akili yako, nitakupa majibu tena, ili kwamba usije ukategemea juu ya hadithi hiyo baadae. Kwa mujibu wa utafiti wa maulamaa wenu wakubwa, hadithi hii si ya kutegemewa, kama nilivyoelezea mapema.

Kadhi Ayaz Maliki ananukuu kutoka kwa maulamaa wenu wakubwa kwamba kwa vile wasimuliaji wa hadithi hii hujumuisha majina ya watu wajinga na wasio na elimu, Harith Bin Qazwin na Hamza Bin Abi Hamza Nasibi, ambao wameonekana kuwa ni waongo, hadithi hii haifai kusimuliwa. Vile vile, Kadhi Ayaz, katika Sharh-e-Shifa na Baihaki katika kitabu chake “Kitab”, wametamka kwamba hadithi hii ni ya kughushi na wamekichukulia chanzo chake kama kisichoaminika.

Baadhi Ya Masahaba Walikuwa Ni Watumwa Wa Tamaa Zao Na Waligeuka

Dhidi Ya Haki

Tatu, kamwe sijasema kitu chochote cha ukorofi, ninasema tu kile ambacho maulamaa wenu wamekiandika. Nakushauri usome Sharh-e-Maqasid ya Fazil Taftazani, ambamo ndani yake anaelezea kwa uwazi kwamba kuna mifano mingi ya uadui miongoni mwa Masahaba, ambayo huoneshsa kwamba baadhi yao walikuwa wamegeuka kuwa watenda dhambi na madhalimu. Hivyo tunaona kwamba watu si wakuheshimiwa tu kwa sababu eti walikuwa Masahaba wa Mtume.

Heshima ya kweli iko kwenye matendo yao na tabia zao. Kama hawatokani na wanafiki, bali walikuwa watii na waaminifu kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hakika lazima watukuzwe na waheshimiwe. Tutaweka mavumbi ya miguu yao kwenye macho yetu.

Hivyo, enyi wapenda haki, je, mnathibitisha kwamba hadithi nyingi kwenye vitabu vyenu sahihi zinazohusu kupigana dhidi ya Amiru’l-Mu’minin Ali, kama vile asemavyo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): “Kupigana dhidi ya Ali ni kupigana dhidi yangu,” zote hizi ni za uwongo? Au mnakiri kwamba hadithi hizi ni za kweli kikamilifu hasa? Je, hazikuandikwa pamoja na vyanzo vya kuaminika katika vitabu vyenu vya maulamaa wenu wenyewe wa mashuhuri?

Hatuhitaji kutaja kwamba hadithi hizi zimeandikwa na maulamaa wa ki-Shi’a pamoja na maoni kamili ya wote pamoja katika vitabu vyao vyote. Kama mnakubali hadithi hizi, lazima mkubali kwamba Masahaba wengi walikuwa wachupa mipaka na wenye dhambi kama Mu’awiya. Umar Ibn As, Abu Huraira, Samra Bin Jundab, Talha, Zubair wote hawa ambao waliasi na wakipigana dhidi ya Ali, kwa kweli waliasi dhidi ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mwenyewe.

Na kwa vile wamepigana dhidi ya Mtume, kwa hakika walipotea kutoka kwenye njia iliyo nyooka. Hivyo, kama tunasema kwamba baadhi ya Masahaba walikuwa watumwa wa tamaa zao, hatukuwa tumekosea, kwa sababu tulichokisema kilikuwa ni kweli. Mbali na hili, hatuko wenyewe tu katika kushikilia kwamba baadhi ya Masahaba walikuwa wenye dhambi, madhalimu na wachupa mipaka. Tunategemeza msimsmo wetu juu ya vitabu vya maulamaa wenu wenyewe wakubwa.

Maoni Ya Imamu Ghazali Kuhusu Masahaba Kuvunja Kiapo Kilichochukuliwa Siku Ya Ghadir-E-Khum.

Kama utachunguza kitabu cha “Sirru’l-Alamin” kilichokusanywa na Abu Hamid Bin Muhammad Ghazali Tusi, kamwe hutapinga kile ambacho ninasema. Hata hivyo, ninalaz- imika kunukuu sehemu ya tansifu yake ya nne kwa kuunga mkono maelezo yangu.

Anasema: “Ushahidi na mantiki vikawa na mwanga, na kuna makubaliano ya wote pamoja miongoni mwa Waislamu kuhusiana na matini (maandiko) ya hotuba ya katika siku ya Ghadir-e-Khum kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: ‘Yule ambaye ni maula kwake (ambaye namtawalia mambo yake), Ali ni maula wake (mwenye kumtawalia mambo yake).’

Kisha Umar mara moja akasema, ‘Hongera, hongera, Ewe Abu’l-Hasani! Wewe ni maula wangu na vile vile maula wa waumini wote wanaume na wanawake.’”

Aina hii ya pongezi kwa uwazi inaonesha kukubaliwa kwa amri ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), na kukubaliwa kwa uongozi na ukhalifa wa Ali. Lakini baadae walizidiwa na tamaa zao za kidunia. Kupenda utawala na mamlaka kuliwanyima huruma.

Walijichukulia wenyewe kumchagua Khalifa kule Saqifq-e-Bani Sa’dat. Walitaka kupandisha bendera ya kizazi chao wenyewe na kuteka nchi ili kwamba majina yao yaweze kuhifadhiwa katika historia. Walilewa tamaa ya madaraka. Walipuuza maamrisho ya Qur’ani, na maagizo ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Waliuza dini yao kwa ajili ya dunia hii. Biashara mbaya iliyo- je waliyofanya na Allah!

Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipokuwa katika kitanda chake alichofia aliomba apewe kalamu na wino ili kwamba aweze kufafanua suala mrithi. (Allah anisamehe kwa kulisema hili), Lakini Umar alisema: “Muacheni mtu huyu. Anaweweseka.” Hivyo wakati ambapo Qur’ani Tukufu na hadithi hazikuweza kuwasaidia, walitegemea juu ya Ijma (makubaliano ya wote pamoja).

Lakini hii vile vile ni batili kwa sababu Abbas, kizazi chake, Ali, mke wake na watoto wao hawakujihusisha na wale ambao wamekula kiapo cha utii kwa Abu Bakr. Halikadhalika, watu wa Saqifa vile vile walikataa kula kiapo kwa Khazraji, na Ansar vile vile waliwakataa wao.

Enyi watu mnaoheshimiwa! Tafadhali kumbukeni, Mashi’a hawadai chochote isipokuwa kile ambacho maulamaa wenu wa haki wanacho kidai.

Lakini kwa vile mnatuchukia sisi, mnaona makosa katika yale tunayo yasema, hata yawe ya mantiki kiasi gani. Lakini kamwe hamuwalaumu maulamaa wenu ni kwa nini wameandika mambo kama haya ingawa kwa kweli wameufichua ukweli na wakachapisha ukweli huu kwenye kurasa za historia.

Sheikh: Sirru’l-Alamin haikuandikwa na Imamu Ghazali. Cheo chake kilikuwa cha juu sana kwa yeye kuweza kuandika kitabu kama hicho, na maulamaa wakubwa hawaamini kwamba kitabu hiki kiliandikwa na yeye.

Sirru’l-Alamin Ni Kitabu Cha Imamu Ghazali

Muombezi: Maulamaa wenu wengi wamekiri kwamba kitabu hiki kiliandikwa na Imamu Ghazali. Yusufu Sibt Ibn Jauzi alikuwa muangalifu sana katika rejea zake kwa wanachuoni wengine (na vile vile alikuwa mshabiki wa dini yake). Katika kitabu chake “Tadhkira Khawasu’l-Umma”, uk. 36, anajadili kutoka kwenye maelezo hayo hayo ya Imamu Ghazali katika kitabu chake “Sirru’l-Alamin” na ananukuu dondoo hiyohiyo ambayo nimeinukuu.

Kwa vile hakuna maoni yaliyofanywa kuhusu maelezo hayo, inaonesha kwanza, kwamba anakubali kitabu hiki kimeandikwa na Imamu Ghazali. Pili, vile vile anakubaliana na maoni yake, ambayo kwa ufupi nimeyaelezea, ingawa yeye mwenyewe ameyaelezea kwa urefu. Kama asingekubaliana nayo angeyatolea ufafanuzi.

Lakini hakika maulamaa wenu mashabiki wanapokutana na maelezo kama haya ya manachuoni wakubwa na wakashindwa kuyakataa kimantiki, amma husema kwamba kitabu hicho hakikuandikwa na mwandishi huyo, au kwamba ni ubunifu wa Mashi’a. Au hata wakati mwingine wanakwenda mbali zaidi kufikia kusema kwamba watu hawa waadilifu wote walikuwa wenye dhambi na makafiri.

Rejea Kwenye Cheo Cha Ibn Iqda

Kuna ushahidi kwamba maulamaa wenu wengi waliteswa kwa sababu tu walisema ukweli. Maulamaa mashabiki na watu wasio wasomi wa madhehebu yenu huchukulia kuwa ni haramu kusoma vitabu visivyofuata desturi na kanuni. Wandishi wa vitabu kama hivyo waliweza hata kuuawa kama ilivyokuwa kwa Hafidh Ibn Iqda Abu’l-Abbas Ahmad bin Muhammad Bin Sa’id Hamadani ambaye alikufa 303 A.H.

Alikuwa mmoja wa maulamaa wenu wakubwa. Wanachuoni mashuhuri wa madhehebu yenu, kama Dhahabi na Yafi’i, wamemkubali na wakasema kwmba amejifunza hadithi 300,000 pamoja na vyanzo vyao, na kwamba alikuwa mchamungu mkubwa.

Katika mkusanyiko wa hadhara katika mji wa Kufa na Baghdad katika karne ya tatu A.H., alisimulia kwa uwazi makosa ya Masheikh wawili (Abu Bakr na Umar). Kwa sababu hiyo watu wakamuita Rafizi na wakajizuia kunukuu hadithi kutoka kwake. Ibn Kathir Dhahabi na Yafi’i wanaandika kuhusu yeye: “Sheikh Ibn Iqda alikaa katika Msikiti wa Basra (Msikiti maarufu ulioko kati ya Baghdad na Kadhmain) na akasimulia kasoro na makosa ya Masheikh wawili (Abu Bakr na Umar) kwa watu. Kwa ajili hii hadithi zilizosimuliwa na yeye zimekataliwa.

Vinginevyo hakuna shaka ya yeye kwamba ni mtu mkweli na mchamungu.” Al-Khatib Baghdad vile vile alimsifia katika “Ta’rikh” yake lakini mwishoni akasema: “Kwa vile alielezea kasoro na makosa ya Masheikh wawili (Abu Bakr na Umar) yeye alikuwa ni Rafizi.” Hivyo watu nyie msiwe katika mawazo kwamba ni Mashi’a tu ambao wanafichua ukweli wa masuala haya. Maulamaa wenu wakubwa kama Imamu Ghazali na Ibn Iqda walizoea kuonyesha kasoro katika Masahaba wakubwa.

Rejea Kuhusu Kifo Cha Tabari

Katika kila zama ya historia kumekuwa na mifano ya maulamaa ambao wameteswa au kusumbuliwa kwa sababu ya kuongea au kuandika kwao ukweli. Kwa mfano yule mfasiri na mwanahistoria maarufu, Muhammad Ibn Jarir Tabari, ambaye alikuwa ni fahari ya maulamaa wenu, alikufa katika mwaka wa 310 A.H. mjini Baghdad.

Lakini kwa sababu utawala uliogopa machafuko ya raia, walikataa jeneza lake kutolewa mchana. Alizikwa kwa lazima wakati wa usiku ndani ya nyumba yake mwenyewe.

Kuuwawa Kwa Nasa’i

Mfano mwingine wa mateso ulikuwa ni kuuawa kwa Imamu Abdu’r-Rahman Ahmad Ibn Ali Nasa’i. Alikwa ni mtu wa heshima na anachukuliwa kama mmoja wa Maimamu wa Sahih Sitta (vitabu sahihi sita). Anatokana na maulamaa wenye vyeo vikubwa wa madhehebu yenu katika karne ya tatu A.H. Wakati alipofika Damascus katika mwaka wa 303

A.H., aliona kwamba, kwa sababu ya Bani Umayya, wakazi wa sehemu ile walikuwa wakilikashifu jina la Amiru’l-Mu’minin Ali Bin Talib kwa uwazi kabisa baada ya kila salat ya faradhi, hususan katika hotuba za salat za jamaa. Alisikitishwa sana kwa kuiona hali hii na aliamua kukusanya hadithi zote za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) zenye kumsifia Amirru’l-Mu’minin pamoja na nyororo za vyanzo vyao, zote zile ambazo alizikumbuka.

Kutokana nazo hizo, aliandika kitabu, “Khasa’isu’l-Alawi,” katika kutetea cheo kitukufu na sifa bora za Ali. Alikuwa kila mara akiwasomea watu kutoka juu ya mimbari, hadith kutoka kwenye kitabu chake, zenye sifa za Mtukufu Imam Ali.

Siku moja wakati alipokuwa anasimulia sifa za hali ya juu za Ali, kundi la wafanya vurugu lilimburuza kutoka kwenye mimbari na kumpiga sana.

Walimpiga mateke kwenye korodani zake na kukamata kwa nguvu uume wake, wakamburuza nje ya Msikiti na wakamtupa mtaani kwenye barabara. Kwa matokeo ya majereha haya alikufa baada ya siku chache. Mwili wake ulichukuliwa ukapelekwa Makka ambako alizikwa. Matukio haya ni matokeo ya uadui na ujinga.

Sasa naomba msamaha kwamba nimesukumwa nje mbali kidogo kuto- ka kwenye nukta yangu. Nilichomaanisha ni kwamba nafasi ya Wilayat (Umakamu) wa Amiru’l-Mu’minin haikuandikwa na maulamaa wa ki-Shi’a peke yao tu. Maulamaa wenu mashuhuri vile vile wamesimulia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mbele ya watu 70,000 au 120,000, alinyanyua mkono wa Ali na akamtambulisha kama Imamu (Kiongozi na mlezi) wa watu.

Mashaka Ya Sunni Kuhusu Maana Ya Maula

Hafidh: Hakika hukuna shaka kuhusu tukio hili na matini ya hadithi hii, lakini wakati huo huo haina umuhimu ambao ufasaha wako wa hisia unaonesha. Mbali na hili, kuna baadhi ya mashaka kuhusiana na matini ya hadithi hii. Kwa mfano neno maula, umetuambia kwamba lina maana: “Mtu ambaye ana mamlaka makubwa juu ya wengine”, ingawa inajulikana kwamba katika hadithi hii maula maana yake “mpenzi, msaidizi na rafiki.”

Mtume alijua kwamba Ali alikuwa na maadui wengi na hivyo alitaka kuwashauri watu kwamba yeyeyote yule ambaye alimpenda au alikuwa rafiki au msaidizi wake, Ali vile vile alimpenda na alikuwa rafiki yake na msaidizi wake.

Sababu iliyomfanya atake kiapo cha utii kwa watu ilikuwa kwamba hakutaka wao wamsabibishie Ali matatizo.

Muombezi: Nafikiri wakati mwingine bila sababu unachukuwa tabia ya viongozi wako waliokutangulia. Kama utaufikiria ukweli huu kwa makini, ukweli wa suala hili utakuwa wazi.

Hafidhi: Ni mambo gani yanayothibitisha maoni yako? Tafadhali tujulishe.

Maana Ya Maula Kama “Kiongozi” “Bwana” Kutokana Na Aya Ya - Ya Ayyuha’r-Rasul Baligh.

Muombezi: Ushahidi wa kwanza ni Qur’ani Tukufu na uteremshwaji wa aya: “Ewe Mtume! Fikisha uliyoteremshiwa kutoka kwa Mola wako. Na ikiwa hukufanya hayo basi hukufikisha ujumbe wake. Na Allah atakulinda na watu…” (5:67)

Hafidh: Utadai vipi kwamba aya hii iliteremshwa siku hiyo na kwa madhumuni haya?

Muombezi: Maulamaa wenu wote wanaoheshimika wameikubali: Jalalu’d-Din Suyuti: “Durru’l-Mansur;” Jz. 2, uk. 298; Hafidh Ibn Abi Hatim Razi: “Tafsir-e-Ghadir”; Hafidh Abu Ja’far Tabari: “Kitabu’l-Wilaya”; Hafidh Abu Abu Abdullah Mahamili: “Amali”; Hafidh Abu Bakr Shirazi: “Ma Nazala mina’l-Qur’an Fi Amiri’l-Mu’minin”; Hafidh Abu Sa’id Sijistani: “Kitabu’l-Wilaya”; Hafidh Ibn Mardawiyya: “Tafsir-e-Ayah”; Hafidh Abul- Qasim Haskani: “Shawahidut-Tanzil”; Abu’l-Fatha Nazari:“Khasa’isu’l-Alawi”; Mu’inu’d-Din Meibudi: “Sharh-e-Diwan”; Kadhi Shekani: “Fathu’l-Ghadir”; Jz. 3, uk. 57; Sayyid Jamalu’d-Din Shirazi: “Arba’in”; Badru’d-Din Hanafi: “Umdatu’l-Qari Fi Sharh-e-Sahih Bukhari”, Jz. 8, uk. 584; Ahmad Tha’labi: “Tafsir Kashfu’l-Bayan”; Imamu Fakhru’d-Din Razi: “Tafsir-e-Kabir”, Jz. 3, uk. 636; Hafidh Abu Nu’aim Ispahani: “Ma nazala mina’l-Qur’ani Fi Ali; Ibrahim bin Muhammad Hamwaini: “Fara’idus-Simtain”; Nizamu’d-Din Nishapuri, Tafsir, Jz. 6, uk. 170; Sayyid Shahabud-Din Alusi Baghdadi: “Ruhu’l-Ma’ani, Jz. 2, uk. 348; Nuru’d-Din Bin Sabbagh Maliki: “Fusulu’l-Muhimma”, uk. 27; Ali Bin Ahmad Wahidi: “Asbabu’n-Nuzul”, uk. 150; Muhammad Bin Talha Shafi’i: “Matalibus-Su’ul”, uk. 16; Mir Sayyid Ali Hamadani Shafi’i: Mawadda ya 5 kutoka “Mawaddatu’l-Qurba”; Sheikh Sulaiman Balkhi Hanafi: “Yanabiu’l-Mawadda”, sura ya 39.
Kwa ufupi, kwa kadiri ninavyojua mimi, maulamaa wenu mashuhuri thalathini wameandika katika vitabu vyao sahihi na katika sharhe zao kwamba aya hii tukufu iliteremshwa siku ya Ghadir-e-Khum kumhusu Amiru’l-Mu’minin Ali.

Hata Kadhi Fazl Bin Ruzbahan, pamoja na uadui wake na ushabiki, anaandika: “Hakika imethibitishwa katika vitabu vyetu sahihi kwamba wakati aya hii ilipoteremshwa, Mtume wa Allah akiwa ameushika mkono wa Ali alisema: ‘Kwa yeyote yule ambaye mimi ni maula (bwana) wake, huyu Ali vile vile ni maula wake.’”

Hata hivyo, inashangaza kwamba Kadhi huyu huyu mpotofu katika “Kashf Ghumma” ana- toa taarifa ya ajabu kutoka kwa Razi Bin Abdullah: “Wakati wa uhai wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) tulizoea kusoma aya hii hivi: ‘Ewe Mtume wetu (Muhammad) fikisha yale uliy- oteremshiwa kutoka kwa Mola wako, yaani kwamba Ali ni bwana wa waumini. Kama hutafanya, basi utakuwa hukufikisha ujumbe wake.’”

Vile vile Suyuti katika Durru’l-Mansur kutoka kwa Ibn Mardawiyya, Ibn Asakir na Ibn Abi Hatim kutoka kwa Abu Sa’id Khudiri, Abdullah Ibn Mas’ud (mmoja wa waandishi wa Wahyi) na Kadhi Shukani katika Tafsir-e-Fathu’l-Ghadir wanasimulia kwamba wakati wa uhai wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wao vile vile walisoma aya hiyo katika njia hiyo hiyo.

Kwa ufupi hili onyo lililomo katika aya hii linasema: “Kama hukufanya basi utakuwa hukufikisha ujumbe (kabisa)…” huonesha kwamba ujumbe ambao Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliamriwa kuutoa ulikuwa wa umuhimu mkubwa sana.

Kwa hakika ulikuwa ni muhimu kwa ukamilifu wa utume wenyewe. Kwa hiyo, kwa hakika suala katika mjadala lilikuwa habari ya uimamu, utunukiaji wa mamlaka juu ya mtu ambaye angewaongoza watu kwa mujibu wa mafundisho ya Uislamu baada ya kifo cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Kushuka Kwa Aya “Siku Ya Leo Nimekukamil- Ishieni Dini Yenu”

Pale Ghadir-E-Khum

Mazingira ya pili ambayo yanathibitisha nukta yangu ni kule kushuka kwa aya:

الْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ وَأَتْمَمْتُ عَلَيْكُمْ نِعْمَتِي وَرَضِيتُ لَكُمُ الْإِسْلَامَ دِينًا ۚ{3}

“Siku ya leo nimekukamilishieni dini yenu na kukutimizieni neema yangu kwenu na kuwachagulieni Uislamu kuwa ndio dini yenu.” (5:3)

Hafidh: Lakini ni jambo linalokubalika kwamba aya hii iliteremshwa siku ya Arafa, na hakuna hata mmoja katika maulamaa aliyedai kwamba aya hii iliteremshwa siku ya Ghadir.

Muombezi: Nakuomba usifanye haraka isiyo na maana katika kuukataa ukweli huu. Kama mambo yalivyo, nakubali kwamba baadhi ya maulamaa wenu wamesema kwamba aya hii iliteremshwa siku ya Arafa, lakini idadi kubwa ya ulamaa wenu waheshimika vile vile wamesema kwamba iliteremshwa siku ya Ghadir.

Vile vile baadhi ya ulamaa wenu wana maoni ya kwamba pengine aya hii iliteremshwa mara mbili, mara ya kwanza pale mwishoni mwa siku ya Arafa na tena siku ya Ghadir.

Kwa hiyo, Sibt Ibn Jauzi anasema katika Khawasu’l-Umma, uk. 18: “Inawezekana kwamba aya hii iliteremshwa mara mbili, mara ya kwanza katika siku ya Arafa na mara nyingine katika siku ya Ghadir-e-Khum, kama vile aya ya: ‘Kwa jina la Allah Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu, ilivyoteremshwa mara mbili, mara ya kwanza mjini Makka na mara nyingine tena mjini Madina.”

Wanachuoni wenu wakuaminika, kama Jalalu’d-Din Suyuti katika “Durru’l-Mansur,” Jz. 2, uk. 256 na Itqan, Jz. 1, uk. 31; Imamu ‘l-Mufassirin Tha’labi katika “Kashfu’l-Bayan”; Hafidh Abu Nu’aim Ispahani katika “Ma Nuzala Mina’l-Qur’ani Fi Ali”; Abu’l-Fatha Nazari katika “Khasa’isu’l-Alawi”; Ibn Kathir Shami katika “Tafsir” Jz. 2, uk. 41 akimfu- ata Hafidh Ibn Mardawiyya: Muhammad Bin Jarir Tabari, Mwanachuo, mfasiri na mwanahistoria wa karne ya tatu A.H. katika “Tafsir-e-Kitabu’l-Wilaya”;
Hafidh Abul’l- Qasim Haskani katika Shawahid-ut-Tanzil; Sibt Ibn Jauzi katika “Tadhkira-e-Khawasu’l- Umma uk. 18; Abu Ishaq Hamwaini katika “Fara’idus-Simtain” sura ya 12; Abu Sa’id Sijistani katika “Kitabu’l-Wilaya”; Al-Khatib-e-Baghdadi katika “Ta’rikh-e-Baghdad, Jz. 8, uk. 290; Ibn Maghazili Faqih Shafi’i katika “Manaqib”, sura ya 14 na Maqtalu’l-Husain, sura ya 4, wote wameandika kwamba katika siku ya Ghadir-e-Khum Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimteuwa Ali kwa amri ya Mungu kwenye cheo cha Wilaya (Makamu).

Aliwaeleza watu kila kile ambacho aliamriwa kukisema kuhusu Ali na akainua mikono yake juu kiasi kwamba weupe wa makwapa yake ulionekana. Aliwahutubia watu hivi: “Mpongezeni Ali kwa sababu ni Amir wa waumini. Jumuiya yote ilitekeleza amri hii. Walikuwa hawajaachana kila mmoja kuchukua njia yake wakati aya iliyotajwa hapo juu iliposhuka.

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alifurahishwa mno kwa kuteremshwa aya hii. Hivyo, wakati akiwahutubia watu alisema: “Allah ni Mkubwa, Ambaye ameikamilisha dini kwa ajili yao na amekamilisha neema Zake kwao na ameridhishwa na Utume wangu na umakamu wa Ali baada yangu.”

Imamu Haskani na Imamu Ahmad Bin Hanbal wametoa maelezo kamili ya tukio hili. Kama ninyi, waheshimiwa, mngeacha mawazo yenu yaliyojipandikiza juu ya suala hili, mtaweza kuzielewa aya tukufu na hadith, ambazo huonesha kwamba neno “Maula” maana yake walii (bwana) yaani, mtu aliye na mamlaka juu ya wengine wote.

Kama maula au wali haikumaanisha mtu ambaye ana mamlaka makubwa juu ya wengine, neno liliofuatia “baada yangu” lingekuwa halina maana. Na maneno haya ambayo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliyarudia rudia kuyasema kutoka kwenye ulimi wake mtuku- fu, yanathibitisha kwamba maula na wali humaanisha “mtu ambaye ana mamlaka makubwa juu ya wengine wote”, kwa sababu alisema kwamba cheo kile haswa kilitolewa kwa Ali baada yake.

Tatu, unaweza kuyaangalia yale mazingira. Katika jangwa lile lenye joto, ambako kulikuwa hakuna hifadhi kwa ajili ya wasafiri, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akakusanya umma wote. Watu walikaa kwenye vivuli vya ngamia, miguu yao ikiwa imefunikwa, katika joto kali linalochoma la jua. Katika hali hii Mtume alitoa hotuba ndefu, ambayo Khawarizmi na Ibn Mardawiyya katika “Manaqib” zao na Tabari katika “Kitabu’l-Wilaya” na wengine wameisimulia.

Je, inaleta maana kufikiria kwamba Mtume angetaka maelfu ya wafuasi wake kukaa siku tatu katika jangwa linalochoma kwa ajili ya kula kiapo kwa Ali kuonesha tu kwamba Ali alikuwa rafiki yao? Kwa hakika hakukuwa na mtu hata mmoja katika jumuiya yote ambaye alikuwa bado haujui ule uhusiano wa karibu kati ya Mtume na Ali au hajasikia kuhusu habari zake (kama nilivyokwishaeleza mapema).

Kuteremshwa kwa aya ya Qur’ani iliyoko kwenye mjadala kwa mara ya pili, hususan katika mazingara tofauti pamoja na maelekezo hayo makali kwamba watu wangeweza kuwekwa kwenye takilifu kubwa na mashaka, isingeweza kuwa na maana tu kwamba lazima wao wawe marafiki wa Ali.

Itakuwa utekelezaji huu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ama ulikusudiwa kuonesha umuhimu mkubwa sana, au ulikuwa ni upuuzi. Na hakika Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) yuko mbali na matendo yote ya kipuuzi.

Kwa hiyo ni jambo la busara kuhitimisha kwamba, matayarisho haya hayakufanywa hivi hivi kwa ajili ya kuelekeza tu kwamba watu lazima wafanye urafiki na Ali. Kwa hakika tukio hili linaashiria kukamilika kwa ujumbe wa Mtume: kuthibitishwa kwa Uimamu, chanzo cha mwongozo wa umma baada ya kifo cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Maoni Ya Sibt Ibn Jauzi Kuhusu Maana Ya Neno Maula

Baadhi ya ulamaa wenu mashuhuri wasifika wamikiri kwamba maana ya msingi ya neno Maula ni “bwana.” Miongoni mwao ni Sibt ibn Jauzi, ambaye baada ya kutoa maana kumi za neno hilo katika kitabu chake Tadhkiratul-Khawas, Sura ya 2, uk. 20, anasema kwamba kati ya zote hizo, ile maana ya kumi ndio inayoendana na kile alichokimaanisha Mtukufu Mtume kukisema.

Yeye anasema: “Hadithi hii inamaanisha haswa utii; hivyo hii maana ya kumi ndio iliyo sahihi, na yenyewe ina maana ya ‘bwana mwenye mamlaka juu ya wengine.’ Kwa hiyo hadithi hii ina maana ya yeyote yule ambaye mimi ni bwana (maula) kwake, Ali pia ni bwana (maula) kwake.’”

Katika kitabu cha Marajul-Bahrein Hafidh Abul-Faraj Yahya bin Sa’id Saqafi anaitafsiri kwa maana kama hiyo hiyo. Yeye anasimulia hadithi hii kwa vyanzo vyake kutoka kwa viongozi wake, ambao wamesema kwamba, Mtukufu Mtume, akiwa amemshika Ali mkononi alisema:

“Yeyote yule ambaye mimi ni bwana (Maula) juu ya nafsi yake, Ali naye pia ni bwana (Maula) juu ya nafsi yake.” Sibt ibn Jauzi anasema, “Hadith ya Mtukufu Mtume inayosema kwamba Ali anayo mamlaka au ni bwana juu ya nafsi za waumini wengine inathibitisha wazi Uimam au Umakamu wa Ali na kwamba utiifu kwake yeye ni wajibu.”

Maoni Ya Ibn Talha Shafi’i Kuhusu Maana Ya Neno Maula

Muhammad Bin Talha Shafi’i katika “Matalibus-Su’ul” katikati ya sehemu ya 5, sura ya 1, uk. 16, anasema kwamba neno maula lina maana nyingi, kwa mfano: “bwana”, “msaidizi”, “mrithi”, “muaminifu”, na kiongozi”. Kisha anasema kwamba hadithi hii tukufu inaitolea tafsri ya ndani aya ya Mubahila, (3:61). Ndani yake Allah (swt) amemuita Ali ‘nafsi’ ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Kulikuwa hakuna utenganisho kati ya nafsi ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na nafsi ya Ali kwa vile amezichanganya mbili hizi kwa kijina kiashiri- acho kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Muhammad Bin Talha anaongeza: “Katika hadithi hii Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anaonesha kwamba wajibu wowote walionao waumini kumhusu yeye, wanao wajibu huo vile vile kumhusu Ali. Kwa vile Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ni hakika alikuwa bwana wa waumini katika mambo yao yote, msaidizi wao, kiongozi, na mtawala – yote haya yakiwa vidoke- zo vya neno maula – basi ina maana kwamba alimaanisha kitu hicho hicho kwa Ali (as).

Na hii kwa hakika ni nafasi ya juu sana, cheo kitukufu mno, ambacho kilitolewa maalumu kwa Ali. Ni kwa sababu hii kwamba Siku ya Ghadir Khum ilikuwa ni siku ya idd (siku kuu) shangwe kwa ajili ya wapenzi na marafiki wa Ali.”

Hafidh: Kwa mujibu wa maelezo yako, kwa vile neno maula lina maana nyingi, itakuwa ni makosa kuamua kwamba lilitumika katika suala hili kuonesha maana moja “bwana”, na kuziweka kando hizo maana nyingine.

Muombezi: Unatambua vema kanuni za msingi za wanachuoni kwamba wakati ambapo neno linaweza kuwa na maana nyingi tofauti, linakuwa na maana moja tu ya msingi na kwamba maana nyingine zinakuwa ni vinyambulika.

Kwa mfano, walii wa nikah (ndoa) maana yake mtu anayesimama kama wakili, au mdhamini. Walii wa mwanamke ni mume wake, walii wa mtoto ni baba yake ambaye ana mamlaka kamili juu yake. Wali ahd (mrithi mstahiki) wa mfalme maana yake “mtu ambaye haki yake ya kutawala haiwezi kukataliwa kama ataishi baada ya baba yake.”

Mbali na hili pingamizi lako linakurudia wewe, juu ya ni kwa nini umeweka mpaka kwenye maana yake “rafiki” na “msaidizi” wakati lina maana nyingine nyingi.

Hivyo hili uainishaji huu bila ya lengo maalumu ni batili. Pingamizi ulilofanya linakurudia wewe mwenyewe na sio kwetu kwa sababu maana ambazo tumezibainisha hazikukosa kuwa na lengo maalum lililoainishwa.

Aya za Qur’ani Tukufu, hadith, na maoni ya wanachuoni, vyote vinathibitisha maana hiyo hiyo tuliyoitoa. Miongoni mwa hizi ni zile sababu ambazo maulamaa wenu wakubwa, kama Sibt Ibn Jauzi, Muhammad Ibn Abi Talha Shafi’i wamezitoa kuhusiana na maana yake.

Aidha, imesimuliwa kwa idadi kubwa ya hadithi kutoka kwenye vyanzo vyenu na vyangu kwamba aya hii tukufu ilikuwa inasomwa hivi kimaana:
“Ewe Mtume wa Allah! Fikisha kile ambacho kimeteremshwa kwako kutoka kwa Mola wako kuhusu wilaya ya Ali (umakamu) na kuwa kwake bwana wa waumini.”

Jalalu’d-Din Suyuti, ambaye ni mmoja wa maulamaa wenu mashuhuri amekusanya hadithi hizi kwenye kitabu chake, “Durru’l-Mansur”.

Hoja Aliyoitoa Ali Ndani Ya Msikiti Wa Kufa Iliyoko Juu Ya Msingi Wa

Hadith Ya Ghadir

Kama hadith hii na neno maula havikuwa uthibitisho wa Ali kama Imamu na Khalifa, Amirul-Mu’minin asingerudia mara kwa mara kuhoji kutokana nayo. Kwa hakika katika mikutano ya kamati za washauri alizirejea kama ushahidi wa Uimamu wake, kama walivyoandika: Khatib Khawarizmi katika “Manaqib” yake uk. 217; Ibrahim Ibn Muhammad Hamwaini katika “Fara’id” sura ya 58; Hafidh Ibn Iqda katika “Kitabu’l- Wilaya”; Ibn Hatim Damishqi katika “Durru’n-Nazim”, na Ibn Abi’l-Hadid katika “Sharhe-e-Nahju’l-Balagha, Jz. 2, uk. 61. Cha umuhimu haswa ni ule ushahidi uliotolewa na masahaba thelathini kule Rahba. Maulamaa wenu mashuhuri wamesimulia majadiliano aliyoyafanya Ali pamoja na Waislamu kule Rahba-e-Kufa (yaani, katika uwanja wa msikiti wa Kufa). Ifuatayo ni sehemu ya orodha ya wale ambao wameandika tukio hili:

Imam Ahmad Hanbal katika “Musnad” yake sehmu ya 1, uk. 129; Ibn Athir Jazari katika “Asadu’l-Ghiba,” Jz. 3, na Jz. 5, uk. 206 na 276; Ibn Qutayba katika “Ma’arif” uk. 194; Muhammad Bin Yusuf Ganji Shafi’i katika “Kifayatu’l-Talib”; Ibn Abi’l-Hadid katika “Sharh-e-Nahju’l-Balagha”, Jz. 1, uk. 362; Hafidh Abu Nu’aim Isfahani katika “Hilyatu’l- Auliya, Jz. 5, uk. 26; Ibn Hajar Asqalani katika “Isaba,” Jz. 2, uk. 408; Muhbu’d-Din Tabari katika “Dhakh’ir-e-Uqba”, uk. 67; Imamu Abdur-Rahman Nisa’i katika “Khasa’isu’l-Alawi”, uk. 26; Allama Samhudi Katika “Jawahiru’l-Iqdain”; Shamsu’d-Din Jazari katika “Asnu’l-Matalib”, uk, 3; Sulaimani Balkhi Hanafi katika “Yanabiu’l- Mawadda, sura 4; Hafidh Ibn Iqda katika “Kitabu’l-Wilaya. Ali alisimama mbele ya watu na akawataka kutoa ushahidi kuhusu kile walichosikia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akisema kuhusu yeye pale Ghadir-e-Khum.

Mashaba thelathini, pamoja na watu wa Badir kumi na mbili (wale ambao wamepigana katika vita ya Badr), walisimama na wakasema kwamba waliona katika Siku ya Ghadir-e-Khum Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akiushika mkono wa Ali akiwaambia watu: “Je, mnajua kwamba ninayo mamlaka makubwa juu ya waumini kuliko waliyonayo katika nasi zao wenyewe?” wote wakasema:

“Ndio.” Kisha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Kwa yeyote yule ambaye mimi ni maula wake
(mwenye kumtawalia mambo yake), basi huyu Ali ni maula wake (mwenye kumtawalia mambo yake).”

Hali Ya Huzuni Kwa Wale Ambao Hawakuthibitisha Hadith Ya Ghadir

Watu watatu kutoka katika mkusanyiko huu hawakutoa ushahidi wa tukio hili. Mmoja wao alikuwa Anas Bin Malik, ambaye alisema kwamba amedhoofika kwa uzee amesahau mambo yote kuhusu tukio hilo. Ali aliwalaani watu wale watatu.

Alisema: “Kama mnasema uwongo, Allah akupeni ukoma, ambao hata vilemba vyenu havitaweza kuuficha.” Haukupita muda Anas aliposimama kutoka sehemu aliyokuwa amekaa ukoma ukatokea mwilini mwake. (kwa mujibu wa baadhi ya taarifa alipatwa na upofu na ukoma pamoja).

Hoja Ya Nne: “Je, Mimi Sina Mamlka Makubwa Juu Yenu Kuliko Mliyo

Nayo Kwenu Wenyewe?”

Muombezi: Nne, njia ambayo hadithi hii imesimuliwa yenyewe inaonesha kwamba neno maula maana yake ni “bwana”. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) katika hotuba yake kule Ghadir, aliwauliza watu: Je mimi sina mamlaka makubwa juu yenu kuliko mliyonayo kwenu wenyewe?”

Hii inarejea kwenye yale maneno ya Qur’ani Tukufu: “Mtume ana mamlaka makubwa juu ya waumini kuliko waliyo nayo juu yao wenyewe.” (33:6)
Aidha, kuna hadithi ya kutengemewa katika vitabu vya madhehebu zote ambayo inansmu- lia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Hakuna muumini ambaye kwamba sina mamlaka makubwa juu yake katika ulimwengu huu na katika Akhera, kuliko aliyonayo mwenyewe.” Wote wakajibu kwa sauti moja kwamba ana mamlaka makubwa juu yao kuliko waliyonayo wao wenyewe.

Baada ya hapo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Yule ambaye mimi ni mawla (namtawalia mambo yake) huyu Ali ni mawla wake (mwenye kumtawalia mambo yake). Hivyo kutokana na muktadha wa hadithi hii hufuatia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimaanisha “mamlaka” au “ubwana juu ya wengine” wakati alipotumia neno maula.

Hafidh: Katika vitabu vingi hakuna kumbukumbu kama hiyo ya Mtume kuwa amewahi kusema maneno haya: Je, mimi sina mamlaka juu yenu kuliko mliyonayo juu yenu wenyewe?”

Muombezi: Katika kusimulia hadithi ya Ghadir, wasimuliaji wametumia maneno tofauti kidogo, lakini kadiri ya hadithi za Shi’a zinavyohusika, maulamaa wote wa ki-Shi’a wanasema kwamba matini na muktadha wa hadithi ya Ghadir ni kama ilivyosimuliwa hapo juu.

Na katika vitabu sahihi vingi vya Sunni, vilivyoandikwa na maulamaa wenu wakubwa, kama Sibt Ibn Jauzi katika “Tadhkira-e-Khawasu’l-Umma” uk. 18; Imamu Ahmad bin Hanbal katika “Musnad” yake; Nuru’d-Din Sabagh Maliki katika “Fusulu’l-Muhimma”; na kundi la wengi wengine ambao wamesimulia hadithi ya Ghadir, maneno “Je, mimi sina mamlaka makubwa juu yenu kuliko mliyonayo wenyewe” hupatikana humo.

Sasa kwa ajili ya baraka nawasilisha hapa Tarjuma ya hadihti hii ambayo imesimuliwa na Imamu Ahmad Bin Hanbal katika Musnad yake, Jz. 4, uk. 281, kutoka kwa Bara’a Bin Azib. Yeye alisema: Nilikuwa nasafiri na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Tulifika Ghadir. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akatangaza: ‘Kusanyikeni kwa ajili ya Sala.’ Ilikuwa ni kawai- da kama kulikuwa na kitu muhimu ambacho kilikuwa kitokee punde, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliwaamuru watu kukusanyika kwa ajili ya Sala.

Wakati watu wakiwa wamekwishakutanika na Sala imekwisha kutekelezwa, Mtume alizoea kutoa hotuba. Sehemu maalumu ilitayarishwa kwa ajili ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kati kati ya miti miwili. Baada ya kumalizika kwa Sala Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akiwa amenyanyua mkono wa Ali juu kupita kichwa chake, alizungumza na watu waliokusanyika pale:

‘Je, mnajua kwamba mimi ni bwana wa waumini na nina haki zaidi juu ya kuliko waliyo nayo wao wenyewe juu ya nafsi zao.’ Wote wakasema, ‘Ndio, tunajua hivyo.’ Alisema tena, ‘Je, mnajua kwamba nina haki zaidi juu ya klia muumini kuliko aliyo kuwa nayo yeye mwenyewe?’ Wote wakajibu, ‘Ndio tunalijua hilo.’ Baada ya hapo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema, ‘Yeyote yule ambaye mimi ni maula wake (mwenye kumtawalia mambo yake) huyu Ali ni maula wake (mwenye kumtawalia mambo yake).’ Kisha akamuomba Allah: ‘Ewe Allah! Kuwa rafiki kwa yule ambaye ni rafiki kwake (yaani, Ali) na kuwa adui kwa yule ambaye ni adui kwake.’

Mara tu kufuatia hili, Umar Bin Khattab alikutana na Ali na akasema, ‘Hongera, Ewe mwana wa Abu Talib! Sasa umekuwa maula wa waumini wote wanaume na wanawake.’”

Vile vile Mir Sayyid Ali Hamadani Shafi’i katika “Mawaddatu’l-Qurba” Mawadda ya 5; Sulaimani Balkhi katika “Yanabiu’l-Mawadda” na Hafidhi Abu Nu’aim katika kitabu chake “Hilya” wameandika hadithi hii pamoja na tofauti kidogo katika maneno.

Hafidhi Abu’l-Fatha, ambaye kutoka kwake Ibn Sabbagh vile vile amenukuu katika kitabu chake Fusulu’l-Muhimma, amesimulia hadithi hii katika maneno haya: “Enyi watu! Allah Swt ni Maula wangu, nami ninayo mamlaka makubwa juu yenu kuliko mliyonayo juu yenu wenyewe. Inakupaseni mfahamu kwamba yeyote yule ambaye mimi ni maula kwake na huyu Ali vile vile ni maula wake.”

Ibn Maja Qazwini kaika “Sunan” yake na Imamu Abu Abdu’r-Rahman Nisa’i katika kitabu chake “Ahadith” (uk. 81, 83, 93, 24) wameisimulia hadithi hii kwa namna hiyo hiyo. Na Zaid Ibn Arqam anaandika katika hadithi yake Na. 84 kwamba Mtume wa Allah alisema katika hotuba yake: “Je, mnajua kwamba ninayo mamlaka makubwa juu ya waumini wote, wanaume na wanawake, kuliko waliyonayo wao wenyewe?”

Wote wakasema: “Tunashuhudia kwamba unayo mamlaka makuu juu ya kila muumini kuliko aliyonayo yeye mwenyewe.” Katika wakati huo Mtume akasema: “ Kwa yeyote yule ambaye mimi ni maula (bwana) kwake huyu Ali vile vile ni maula (bwana) wake.” Kisha akaunyoosha mkono wa Ali. Kwa nyongeza Abu Bakr Ahmad Bin Al-Khatib Baghdadi (amekufa 462 A.H.), katika kitabu chake “Ta’rikh-e-Baghdad, Jz,. 8, uk. 289, 290, amesimulia hadithi ndefu kutoka kwa Abu Huraira kwamba kama mtu yeyote atafun- ga siku ya mwezi 8 Dhu’l-Hijja (Siku ya Ghadir), atalipwa malipo ya funga ya miezi sita. Kisha hapo akaindika hadithi hiyo hapo juu katika njia hiyo hiyo.

Mashairi Ya Hasan Mbele Ya Mtukufu Mtume

Mazingira ya tano kuthibitisha wilaya (umakamu) ya Ali ni usomaji wa mashairi ambayo Hasan Bin Thabit aliyasoma kwa ruhusa ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), katika mkusanyiko wa watu ambapo cheo cha Ali cha umakamu kilitajwa. Sibt Ibn Jauzi na wengine wameandika kwamba wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliposikia beti hizo, alisema: “Ewe Hasan! Kadiri unavyoendelea kutusaidia au kutusifia sisi kwa ulimi wako, basi ruhul-quds yule roho tukufu naye vile vile atakuwa anakusaidia wewe.”

Mfasiri mashuhuri na msimuliaji wa hadithi wa karne ya nne A.H., Hafidh Ibn Mardawiyya (amekufa 352 A.H.), katika “manaqib” yake; mkuu wa Mimamu, Muwaffaq Bin Ahmad Khawarizmi katika “Manaqib” yake na “Maqtalu’l-Husain,” sehemu ya 4; Jalalu’d-Din Suyuti katika “Risalatu’l-Azhar fi ma Aqdahush-Shu’ara” na wengi katika wanachuoni wenu, wasimuliaji wa hadithi, na wanahistoria wanasimulia kutoka kwa Abu Sa’id Khudri kwamba katika Siku ya Ghadir-e-Khum, baada ya hotuba ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na uteuzi wa Ali kama mrithi wake, Hasan Bin Thabit alisema: “Je, unaniruhusu nisome mashairi juu ya tukio hili?” Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema:

“Ndio, soma pamoja na baraka za Allah.” Hivyo alisimama sehemu iliyonyanyuka kidogo na akasoma kwa mfululizo beti zilizotungwa.maana ya beti hizo ni kama ifuatavyo:

“Katika Siku ya Ghadir-e-Khum Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliwakusanya watu pamoja, na niliisikia sauti yake ikiwaita. Mtume akawambia, ‘Ni nani maula wenu na walii?’ Watu wakasema kwa uwazi, ‘Allah ni Maula wetu na wewe ni walii (mlinzi) wetu na hakuna anayekataa ukweli huu.’ Hivyo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akamuambia Ali: “Simama! Ninaridhika na wewe kuwa imamu (makamu) na hadi (mlezi) baada yangu.

Hivyo yeyote yule ambaye mimi ni maula wake huyu Ali vile vile ni maula wake. Kwa hiyo, ninyi watu wote lazima muwe watiifu na waminifu katika kumsaidia yeye.’ Kisha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akaomba kwa Allah: ‘Ewe Allah! Kuwa rafiki kwa yule ambaye ni rafiki kwake (Ali) na kuwa adui kwa yule ambaye ni adui kwake.’”

Mashairi haya ni ushahidi wa wazi kwamba siku ile masahaba wa Mtume hawakulitafsiri neno maula katika njia nyingine yoyote isipokuwa ya Imamu na kwamba Ali atakuwa Khalifa baada ya Mtume kufariki.

Kama neno maula halikuwa na maana ya Imamu au bwana juu ya wengine, basi Mtume mara moja angelimkatiza Hasan wakati anasoma ubeti, “Ninaridhika na wewe kuwa Imamu na mlezi baada yangu”, na angemuambia kwamba amekosea na kwamba hakuwa na maana kwamba Ali atakuwa Imamu na mrithi baada yangu, na kwamba kwa neno maula alimaanisha “rafiki” au “msadizi”.

Lakini kwa kweli Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimuunga mkona kwa kusema, “Ruhu’l-Qudus naye vile vile atakusaidia.” Mbali na hili, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa uwazi alielezea nafasi ya uima- mu au wilaya (umakamu) wa Ali katika hotuba yake.

Inakubidi uichunguze hotuba ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliyoitoa kaita Siku ya Ghadir-e-Khum na ambayo imeandikwa kwa ukamilifu na Abu Ja’far Muhammad Ibn Jarir Tabari (amekufa 310 A.H.) katika kitabu chake “Kitabu’l-Wilaya”.

Anaandika kwamba Mtume alisema: “Sikilizeni na mtii. Hakika, Allah swt ni Maula wenu na Ali ni imamu wenu. Mpaka Siku ya Hukumu uimamu utabakia kwenye familia yangu, kizazi cha Ali.”

Masahaba Wavunja Ahadi Yao Waliyoweka Siku Ya Ghadir

Maana yoyote mtakayoitoa kwa neno maula, ni ukweli unaokubalika kwamba Masahaba waliweka ahadi kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) katika siku ile. Kuna kupatana kabisa kati ya madhehebu hizi mbili juu ya nukta hii. Basi kwa nini walivunja ahadi hiyo? Hata tukichukulia tu kwa muda huu kwamba kwa kusema maula Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimaanisha “rafiki” au “msaidizi” tu, kwa kumuogopa Allah hebu tuambieni kama mnafikiri kwamba urafiki ule ulimaanisha kwamba waje wachome moto nyumba ya Ali, kuitishia familia yake, na na kumtishia yeye kwa panga zilizochomolewa!

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alitoa maelekezo ya wazi kwamba Masahaba lazima wale kiapo cha utii kwa Ali. Unafikiria kwamba alikusudia kwamba wao kwa hiyo waje wamtese mkwe wake mwenyewe? Baada ya kifo cha Mtume, hawakuvunja kiapo chao? Je, wale waliovunja kiapo, kwa maoni yenu ninyi, hivi walitimiza masharti ya urafiki? Je, waliisoma aya 25 sura ya 13, Al-Ra’d (Radi) ya Qur’ani Tukufu? “Na wale wanaovunja ahadi za Allah baada ya kuzifunga, na wanakata yale ambayo kwamba Allah ameamrihsa yaungwe, na wanafanya ufisadi katika nchi; hao ndio watakaopata laana, na watapata makazi mabaya.” (13:25)

Masahaba Wavunja Ahadi Kule Uhud, Hunain, Na Hudaibiyya

Katika vita ya Uhud na Hunain, wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipowafanya Masahaba wote waahidi kwamba siku hiyo hawatakimbia, je, sio hakika kwamba walikimbia? Walikimbia kutoka kwenye uwanja wa vita na wakamuacha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kukabiliana na adui. Hili limeandikwa na wanahistoria wenu wenyewe, kama Tabari, Ibn Abi’l-Hadid, na Ibn A’same Kufi. Je, huku sio kuvunja kiapo chenye uzito mkubwa?

Naapa kwa Allah kwamba mnawatoa makosa bure Mashi’a wakati tunaposema yale tu ambayo wanahistoria wenu mashuhuri wameyasema.

Mashi’a Wanawalaumu Masahaba Wale Tu Ambao Vitendo Vyao Havikuwa Vya Haki

Sielewi ni kwa nini ninyi watu mmekuwa mkitushambulia kwa karne nyingi. Mnachoandika chochote ninyi kinakubaliwa, lakini kama tukiandika yale ambayo maulamaa wakubwa wa Sunni waliyo andika, tunaitwa makafiri kwa sababu tu tunakosoa dhulma za baadhi ya Masahaba.

Hata hivyo, kama ukosoaji wa Masahaba humaanisha Urafidha, basi kwa dhahiri Msahaba wote walikuwa Marafidhi, kwa sababu wote kila mmoja alikosoa vitendo vibaya vya mwenziye. Hata Abu Bakr na Umar walifanya hivyo.

Baadhi ya Masahaba wa Mtume walikuwa waumini wachamungu na walikuwa waki- heshimiwa sana. Wengine waliendekeza matamanio yao machafu na walilaumiwa. Kama unataka ushahidi wa kihistoria wa ukweli huu, nashauri kwamba usome Sharh-e-Nahju’l- Balagha ya Abi’l-Hadid, Jz. 4, uk. 454, 462, na usome majibu ya marefu ya Zaid kwa ukinzani wa Abu’l-Ma’ali Juwaini, ambayo Abu Ja’far Naqib ameyaandika.

Hapo ndipo utakapojua ni kiasi cha migogoro ilyokuwepo miongoni mwa Masahaba, ambao kwa hakika walilaaniana wenyewe kwa wenyewe kama waovu na makafiri.

Kukimbia Kwa Masahaba Kule Hudaibiyya

Katika maelezo yake ya suala la Hudaibiyya, Ibn Abi’l-Hadid, katika Sharh-e-Nahju’l- Balagha, na wengine miongoni mwa wanahistoria wenu vile vile wameandika kwamba, baada ya kukamilika kwa mkataba ule wa amani, Masahaba wengi akiwemo Umar Bin Khattab, walionesha kuchukia kwao kuhusiana na masharti ya mkataba.Walimueleza Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwamba walikuwa hawakuridhika na mkataba wa amani na walitaka kupigana. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akawaambia kama walitaka kupigana walikuwa wako huru kufanya hivyo.
Hivyo walishambulia. Lakini Masahaba wakashindwa vibaya na wakakimbia milimani na hawa hata hawakurudi kumlinda Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Ndipo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimuambia Ali achomoe upanga na kuwafukuza Makuraishi.

Walipomuona Ali mbele yao, Makuraishi walirudi nyuma. Baadae Masahaba waliokimbia walirudi na kuomba msamaha kwa Mtume.

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akawaambia: “Kwani mimi sikujueni ninyi! Nyie sio watu wale wale ambao walitetemeka kwa hofu katika vita vya Badir mpaka Allah swt akatuma malaika kwa ajili ya kutusaidia! Ninyi sio Masahaba wangu wale wale ambao katika Siku ya Uhud mlikimbia milimani na mkaniacha bila ulinzi? Ingawa niliendelea kuwaita, lakini ninyi hamkurudi.”

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akawahesabia udhaifu wao wote, na waliendelea kuelezea masikitiko yao kwa ajili ya vitendo vyao. Ibn Abi’l-Hadid anasema mwishoni mwa kazi yake ya kuandika kwamba karipio hili lilielekezwa haswa dhidi ya Umar, ambaye hakuamini ahadi zozote zilizowekwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Kisha anaandika kwamba, kwa mwanga wa maelezo ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), Khalifa Umar lazima alikimbia kutoka kwenye vita ya Uhud kwa sababu katika mazungumzo yake Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alilitaja hilo pia.

Sasa mnaweza mkaona wenyewe kwamba kama tukielezea ukweli huu, ambao umeandikwa na maulamaa wenu wakubwa kama Abi’l-Hadid na wengine, mara moja tunalengwa kushambuliwa (eti) kwa sababu tumemtukana Khalifa, lakini hakuna kikwazo kwa Abi’l- Hadid. Kwa kweli hatuna nia ya kumtukana mtu yeyote. Sisi tunasimulia mambo ya kihistoria tu, na mnatuangalia kwa macho ya dharau. Mnayapuuza mambo hayo.

Mashi’a Watatafuta Fidia Ya Hali Ya Mambo Siku Ya Hukumu

Mashi’a watakuwa na malalamiko mengi Siku ya Hukumu dhidi ya Ulamaa wenu. Ulimwengu utatoweka, lakini lazima msimame mbele ya Mahakama Adilifu ya Allah kwa ajili ya kujibu uonevu wenu.

Hafidh: Tafadhali niambie ni kwa uonevu upi ambao mtatafuta haki Siku ya Hukumu?

Muombezi: Kuna mifano ambayo naweza kuionesha. Wakati Siku ya Hukumu Tukufu itakapowadia, kwa hakika nitaitafuta haki.

Hafidh: Nakuomba usichochee mihemuko ya (watu) wengine. Tuambie ni uonevu gani uliokupata.

Muombezi: Uonevu na dhulma sio jambo geni leo kwetu sisi. Lakini msingi wake ulijengwa mara tu baada ya kufariki kwa babu yetu, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Haki ya bibi yetu mdhulumiwa, Fatima Zahra ambayo aliachiwa na baba yake, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), kwa ajili ya kuwalea watoto wake, iliporwa. Hakuna kujali kokote kulikofanywa kwa ajili ya malalamiko na upingaji wake wa dhati. Hatimaye alifariki katika ujana wake akiwa amevunjika moyo.

Hafidh: Tafadhali, unawachochea watu bila sababu yoyote. Tuambie ni haki gani ya Fatima iliyoporwa? Tafadhali kumbuka kwamba kama utashindwa kuthibitisha dai lako, kwa kiasi fulani utashindwa katika Mahakama Tukufu ya Haki. Jione uko katika Mahakama ya Mungu ya Uadilifu na utetee kesi yako.

Muombezi: Siku moja tutakuwa mbele ya Mahakama Tukufu. Tunategemea kupata haki. Kama wewe pia unayo hisia ya uadilifu, basi yakupasa kama hakimu muadilifu kusikiliza hoja yangu bila chuki. Naamini utakubali uhalali wa dai letu.

Hafidh: Naapa kwamba sina chuki au ukaidi. Hakika umeona katika mikesha hii kwamba sihoji kipumbavu. Wakati niliposikia hoja zenye mantiki nilizikubali.

Kunyamaza kwangu kwenyewe kulikuwa kunaonesha kwamba nimekubaliana na mwenendo huu wa haki. Kwa asili mimi sio mtu wa kupenda mizozo.

Nakiri kwamba kabla sijakutana na wewe hapa, nilitaka nikushinde. Lakini nimevutiwa mno na usafi wako, upole wako, tabia nzuri, wepesi na hisia ya kweli, kiasi kwamba nimeweka nadhiri mbele ya Allah kwamba nasalimu amri kukubali ukweli wote wenye mantiki ingawa msimamo huu utavunja mioyo juu ya matarajio ya wengine.

Niamini mimi, sioyule mtu wa ule usiku wa kwanza. Nakueleza kwa ukweli na uwazi kabisa kwamba hajo zako zimeacha athari ya ndani mno katika moyo wangu. Kwa dhati kabisa natumaini kwamba nitaweza kufa pamoja na mapenzi na upendo kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na kizazi chake, ili kwamba niweze kusimama kwa furaha na kuridhia mbele ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Muombezi: Naam, hakika msimamo kama huo ulikuwa unategemewa kwa mwanachuoni kama wewe. Hakika mimi pia nimevutiwa sana na maelezo yako, na imejengeka kwangu hisia ya urafiki kwa upande wako. Sasa ningependa kuleta ombi kwako. Natumaini utalikubali.

Hafidh: Ndio, tafadhali.

Muombezi: Usiku huu ningetaka niwe hakimu na wengine wawe mashahidi, ili kwamba uweze kuamua bila chuki yoyote iwapo dai langu ni haki. Baadhi ya waumini wasio na ujuzi wanasema kwamba hakuna maana kujadili suala ambalo limetokea miaka 1,300 iliyopita. Hawajui kwamba masula yanayohusiana na elimu yanajadiliwa katika kila zama.

Majadiliano ya haki hufichua ukweli na madai ya urithi yanaweza kufanywa kisheria na mwenye kurithi, kwa wakati wowote ule. Kwa vile mimi ni mmoja wa warithi, nataka kukuuliza swali. Tafadhali nakuomba unipe jibu la haki.

Hafidh: Ndio, nitapendezewa sana kusikia maelezo yako.

Muombezi: Kama kwa amri ya Mungu baba anampa mtoto wake mali, na, baada ya kifo cha baba, kama mali ile inachukuliwa kutoka kwa mtoto ambaye anamiliki mali ile, je, itakuwa ni aina gani ya madai?

Hafidh: Kitendo cha mnyang’anyi kitakuwa sio cha haki kabisa. Lakini unamkusudia nani wakati unaposema muonevu na muonewa?

Fadak Na Uporwaji Wake

Wakati ngome ya Khaibar iliposhindwa na kutekwa, malodi, makabaila na watu mashuhuri wa Fadak walikuja kwa Mtume. Fadak ilikuwa ni eneo katika bonde la milima ya Madina. Lilikuwa na vijiji saba ambavyo vimeenea mpaka kwenye mwambao wa bahari. Vingi vilikuwa na rutuba sana na kulikuwepo na chemchem nyingi zenye miti (oasisi).

Kulikuwepo na mkataba wa amani na watu unaosema kwamba nusu yote ya Fadak itakuwa chini ya miliki yao na nusu nyingine itakuwa mali ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Ukweli huu umesimuliwa na Yaqut Hamawi, mwaandishi wa “Majimu’l-Buldan”, katika kitabu chake “Futuhu’l-Buldan, Jz. 6, uk. 343; Ahmad Bin Yahya Baladhuri Baghdadi (alikufa 279 A.H.) katika kitabu chake “Ta’rikh”; Ibn Abi’l-Hadid Mu’tazali katika Sharhe yake ya “Sharh-e-Nhju’l-Balagha”, (iliyochapishwa Misir), Jz. 4, uk. 78, akinukuu kutoka kwa Abu Bakr Ahmad Bin Abdu’l-Aziz Jauhari; Muhammad Bin Jarir Tabari katika kitabu chake “Ta’rikh-e-Kabir” na wengine wengi katika muhadithina na wanahistoria wenu.

Kuteremshwa Kwa Aya Ya “Mpe Haki Yake Jamaa Wa Karibu”

Wakati Mtume aliporudi Madina, Jibril aliteremsha aya ifuatayo: “Na mpe jamaa yako wa karibu haki yake, na masikini, na msafiri; wala usitumie ovyo kwa fujo.” (7: 26)

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alitafakari juu ya umuhimu wa wahayi huu. Jibril alitokea tena na akamjulisha kwamba Allah ameamuru kwamba: “Fadak itolewe kwa Fatimah.” Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akamuita Fatima na akasema: “Allah emeniamuru kuitoa Fadak kama zawadi kwako.” Hivyo mara moja alimpa Fatima umiliki wa Fadak.
Hafidh: Tafadhali fafanua unachosema kuhusu tukio ambalo aya hii tukufu imeteremshwa. Je, imeandikwa kwenye vitabu vya historia na tafsir vya Shi’a, au vile vile umeiona (habari hii) katika vitabu vyetu vya kutegemewa?

Muombezi: Mkuu wa wafasir, Ahmad Tha’labi katika kitabu chake “Kashfu’l-Bayan”; Jalalu’d-Din Suyuti katika “Tafsir” yake, Jz. 4, akisimulia kutoka kwa Hafidh Ibn Mardawiyya; yule mufasir mashuhuri Ahmad Bin Musa (aliyekufa 352 A.H.) Akisimulia kutoka kwa Abu Sa’id Khadiri na Hakim Abu ‘l-Qasim Haskani; Ibn Kathir; Imadu’d-Din Isma’il; Ibn Umar Damishqi; Faqih-e-Shafi’i katika kitabu chake cha “Ta’rikh”, na Sheikh Sulaimani Balkhi Hanafi katika “Yanabiu’l-Mawadda”, sura ya 39, akisimulia kutoka “Tafsir-e-Tha’labi”, “Jam’u’l-Fawaid” na “Uynu’l-Akhbar” wote wanasimulia kwamba wakati aya, “Na mpe jamaa yako wa karibu haki yake…”, ilipoteremshwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wa Allah alimuita Fatima na akampa Fatima Fadak kubwa kama zawadi kwake. Kwa hiyo, kadiri Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alivyoishi, Fadak ilibakia katika miliki ya Fatima. Bibi yule mtukufu aliikodisha ardhi ile; mapato yake yalikusanywa katika awamu tatu.

Kutoka katika hesabu hii alichukuwa pesa ya kutosha kwa ajili ya chakula chake na cha watoto wake na akagawanya alubaki kwa watu masikini wa Bani Hashim. Baada ya kifo cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), maofisa wa Khalifa anayetawala walinyakua mali hii kutoka kwa Fatima. Nakuulizeni enyi waheshimiwa, mnieleze katika jina la uadilifu mtakiitaje kitendo hiki?

Hafidh: Hii ndio mara ya kwanza nimesikia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimpa Fatima Fadak kwa amri (ya Allah).

Muombezi: Inawezekana kwamba hukuweza kusikia kuhusu (suala) hili. Lakini kama ambavyo nimekuambia, wengi wa maulamaa wenu wakubwa wameandika kuhusu suala hili katika vitabu vyao vya kutegemewa. Ili kuthibitisha nukta hii kwa uwazi nakurejeshea kwa Hafidh Ibn Mardawiyya, Waqid na Hakim (Angalia Tafsir na Ta’rikh zao); Jalalu’d-Din Suyut “Durru’l-Mansur, Jz. 4, uk. 177; “Kanzu’l-Umma” ya Mullah Ali Muttaqi na maelezo mafupi ambayo ameandika juu ya ‘Kitabu’l-Akhlak’ ya “Musnad” ya Ahmad Bin Hanbal kuhusu tatizo la Sila-e-rahm; na “Sharh-e-Nahju’l-Balagha” ya Ibn Hadid,

Jz. 4. Maulamaa wote hawa wamesimulia katika njia tofauti, isipokuwa maelezo kutoka kwa Abu Said Khudr, kwamba aya hiyo hapo juu ilipoteremshwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliitoa Fadaka na kumpa Fatima Zahra.

Hoja Kutoka Hadith Ya ‘La Nurith’ – Hatuachi Urihti

Hafidh: Ni ukweli unaokubalika kwamba Mahalifa waliinyang’anya Fadak juu ya msingi wa hadithi inayojulikana sana iliyosimuliwa na Abu Bakr, ambaye alitamka kwamba yeye mwenyewe amemsikia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akisema: “Sisi Mitume hatuachi urithi wowote nyuma yetu; chochote tunachoacha kama urithi ni sadaka” (yaani, ni mali ya umma).

Fadaka Ilikuwa Zawadi – Sio Urithi

Muombezi: Kwanza, sio mali ya urithi bali ni zawadi. Pili, hiyo hadithi inayodaiwa kuwa ni ya Mtume haikubaliki.

Hafidh: Utatoa hoja gani ya kuikataa hadithi hii?

Muombezi: Kuna sababu nyingi za kuikataa hadithi hii.

Hadithi ‘La Nurith’ Ni Ya Kubuniwa

Kwanza kabisa, yeyote yule aliyeiandaa hadithi hii, aliitamka bila kufikiria kuhusu yale maneno aliyotumia. Kama angekuwa muangalifu kuhusu hadithi hii, kamwe asingelisema: “Sisi Mitume hatuachi urithi wowowte”, kwa sababu angelijua kwamba uwongo wake ungefichuliwa na maneno haya haya ya hadithi hii ya kubuni.
Kama angetumia maneno “Sikuacha urithi wowote nyuma,” hadithi yake ya majaribio ingekuwa yenye kuelekea kuwa ya kweli zaidi.

Lakini wakati ametumia wingi “Sisi Mitume…” tunawajibika kuchunguza ukweli wa hadithi hii. Sasa kwa msingi wa maelezo yako mwenyewe tunarejea kwenye Qur’ani Tukufu kwa ajili ya mwongozo. Tunaona kwamba kuna idadi ya aya ambazo zinatueleza kwamba kwa kweli mitume waliacha urithi. Hii inathibisha kwamba hadithi hii ni ya kutupwa moja kwa moja.

Fatima Alitetea Madai Yake

Katika kitabu chake “Kitab-e-Saqifa” mwanachuoni mkubwa na muhadithina, Abu Bakr Ahmad Bin Abdu’l-Aziz Jauhari, ambaye kuhusu yeye Abi’l-Hadid anasema katika kitabu chake “Sharh-e-Nahju’l-Balaghah” kwamba alikuwa ni mmoja wa maulamaa wakubwa na muhadithina wa Masunni; Ibn Al-Athir katika kitabu chake “Nihaya”; Mas’ud katika “Akhbaru’z-Zaman” na katika “Ausat”; Ibn Abil-Hadid katika “Sharh-e-Nahju’l- Balaghah” Jz. 4, uk. 78, akinukuu kutoka kitabu cha Abu Bakr Ahmad Jauhari “Saqifa” na Fadak katika njia tofauti na kutoka kwenye idadi ya vyanzo, baadhi ambavyo hurejea kwa Imamu wa tano Muhammad Baqir kupitia kwa Siddiq Sughra Zainab-e-Kubra na baadhi ambavyo hurejea kwa Abdullah Ibn Hasan kutoka kwa Siddiq Kubra Fatima Zahra na kutoka kwa Ummu’l-Mu’minin Aisha na vile vile kutoka kwa Muhammad Bin Imran Marzabani, yeye kutoka kwa Zaid bin Ali bin Husein; yeye kutoka kwa baba yake, na yeye kutoka kwa baba yake, Imam Husein; na yeye kutoka kwa mama yake maarufu, Fatima Zahra; na maulamaa wengine wengi wa madhehebu yenu wamesimulia hotuba ya Fatima mbele ya mkusanyiko mkubwa wa Waislamu. Wapinzani walifadhaishwa wakati waliposikia hoja zake na hawakuweza kujibu. Kwa vile walikuwa hawana majibu ya kutoa walianzisha ghasia.

Hoja Ya Fatima Ya Kukataa Hadith ‘La Nurith’

Moja ya hoja za Fatima za kukataa hadithi hii ilikuwa kwamba, kama hadithi hii ingekuwa ni ya kweli, basi kwa nini kulikuwa na aya nyingi mno kuhusu urathi wa mitume.

Alisema: “Katika sehemu moja Qur’ani inasema: “Na Suleimani alikuwa mrithi wa Daudi.’” (27:16)

Kuhusu Mtume Zakariya Qur’ani Tukufu inasema:

فَهَبْ لِي مِنْ لَدُنْكَ وَلِيًّا {5}

يَرِثُنِي وَيَرِثُ مِنْ آلِ يَعْقُوبَ{6}

“…Basi nipe mrithi kutoka kwako, ambaye atarithi kutoka kwangu na mrithi (vile vile) wa nyumba ya Yaaqub…” (19:5-6)

Kuhusu maombi ya Zakariya Qur’ani Tukufu inasema:

وَزَكَرِيَّا إِذْ نَادَىٰ رَبَّهُ رَبِّ لَا تَذَرْنِي فَرْدًا وَأَنْتَ خَيْرُ الْوَارِثِينَ {89}

فَاسْتَجَبْنَا لَهُ وَوَهَبْنَا لَهُ يَحْيَىٰ{90}

“Na Zakariya alipomuomba Mola Wake: ‘Mola Wangu, usiniache peke yangu (bila mtoto), na Wewe ndiye Mbora wa wanaorithi.’ Basi tukamkubalia na tukampa Yahya…” (21:89-90)

Baada ya haya akasema: “Ewe mtoto wa Abu Qahafa! Je, imo ndani ya Kitabu cha Allah kwamba wewe ni mrithi wa baba yako na mimi ninanyimwa urithi wa baba yangu? Umefanya kashfa kubwa mno. Enyi watu! Je, mmekiacha kwa mkusudi Kitabu cha Allah (Qur’ani Tukufu) na kukipuuza moja kwa moja? Je, mimi sio mtoto wa Mtukufu Mtume? Kwa nini unaninyima mimi haki yangu?

Kwa nini aya zote hizi za urithi, ambazo zimekusudiwa kwa watu wote kwa ujumla na hususan kwa Mitume zimejumuishwa katika Qur’ani Tukufu? Je, si kweli kwamba aya za Qur’ani zitabakia bila kubadilishwa mpaka Siku ya Hukumu?

Je, Qur’ani haisemi: “.....na ndugu wa nasaba wana haki zaidi wao kwa wao katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu.....” (8:75) na: “Allah anakuusieni juu ya watoto wenu! Mtoto mwanaume atapata vigawanyo viwili vya mwanamke…” (4:11) na: Mmelazimishwa, mmoja wenu anapofikiwa na umauti, kama ameacha mali, kuwausia wazazi wake wawili na jamaa wa karibu kwa uadilifu. (Huu) ni wajibu kwa wamchao Mwenyezi Mungu” (2:180).

Basi kwa nini mimi hasa hasa niwe nimenyimwa urithi wa baba yangu? Je Allah ameteremsha aya maalumu kwako, ambazo zinamuondoa baba yangu (kutoka kwenye haki yake hii). Je, wewe unajua maana ya nje na ya ndani ya Qur’ani Tukufu kuliko baba yangu Muhammad na binamu yake Ali?”

Utetezi Wa Fatimah Hauna Mafanikio

Wakati waliponyamazishwa na hoja hizi na ukweli wa mambo, wakawa hawana majibu. Walikimbilia kwenye hila na lugha ya matusi.

Alilia huku akisema: “Leo mumeuvunja moyo wangu. Siku ya Hukumu nitafungua mashitaka dhidi yenu katika Mahakama Tukufu ya Haki na Allah Mwenye nguvu zote ataamua kesi hiyo kwa uadilifu.

Allah ndiye Hakimu bora zaidi. Muhammad ndiye mkuu na bwana; muda wa ahadi, wetu na wenu ni Siku ya Ufufuo.

Siku hiyo muonevu atakuwa mwenye hasara, na toba yenu haitawasaidia kitu. Kwani kwa kila kitu kuna muda maalumu uliopangwa na mtajua muda mfupi tu ujao nani atapatwa na adhabu ya dharau.”

Khalifa Alitumia Lugha Chafu

Hafidh: Nani atathubutu kukashifu kipande cha mwili wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), Fatima Zahra? Hili siliamini. Hila na udanganyifu inawezekana, lakini kutumia lugha ya matusi haiwezikani. Tafadhali usiseme vitu kama hivyo.

Muombezi: Hakuna mtu aliyekuwa na ujasiri wa kusema vitu kama hivyo isipokuwa Khalifa wako, Abu Bakr. Akiwa ameshindwa kujibu hoja nzito za Bibi huyo muonewa, mara moja alipanda kwenye mimbari na kumtukana Fatimah na mume wake na binamu yake Mtume, kipenzi cha Allah na cha Mtume Wake, Amiru’l-Mu’minin Ali.

Hafidh: Nadhani riwaya hizi za kizushi zimeenezwa na mashabiki wa kidini.

Muombezi: umekosea. Riwaya hizi hazikuenezwa na mashabiki wa ki-Shi’a. Maulamaa wakubwa wa Sunni ndio waliozisambaza.

Kwa kiasi chochote cha kukosa uvumilivu wanachoweza kuwa nacho watu wetu wa kawaida, kamwe huwa hawabuni hadithi.

Kama utachunguza vitabu vyenu vya sahihi, utakiri kwamba maulamaa wenu wakubwa wameyakubali mambo haya.

Ibn Abi’l-Hadid Mu’tazali katika “Sharh-e-Nahju’l-Balagha” Jz. 4, uk. 80, iliyochapishwa Misri, akisimulia kutoka kwa Abu Bakr Ahmad Bin Abdu’l- Aziz Jauhari, ameandika kwa urefu kuhusu Abu Bakr kupanda juu ya mimbari baada ya malalamiko ya upinzani wa Ali na Fatimah.

Kupingana Kwa Ali Na Abu Bakr

Wanachuoni wengi wamesimulia kwamba, wakati Fatimah alipomaliza kutetea hoja yake, Ali akaanza upingaji wake katika mkusanyiko wa hadhara wa Waislamu katika Msikiti wa Madina, akielekea upande alikokuwa Abu Bakr, alisema:

“Kwa nini unamnyima Fatimah urithi wa baba yake, ingawa alikuwa ndiye mmliki wake na alikuwa anaimiliki mali hiyo wakati wa kipindi cha uhai wa baba yake?”

Abu Bakr akajibu: “Fadak ni ngawira ya Waislamu. Kama Fatimah atatoa ushahidi kamili kwamba ni mali yake, kwa hakika nitampa; vinginevyo, nitamnyima mali hiyo.”

Mtukufu Imamu akasema: “Je, sio ukweli kwamba wakati unatamka hukumu kuhusu Waislamu, kwa ujumla, unapitisha hukumu inayokinzana mno kuhusiana na sisi.?”

“Je, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hakusema kwamba dhima ya kuthibitisha inakuwa juu ya mdai na ile ya utetezi juu ya mdaiwa? Umepuuza hukumu ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na kinyume na sheria ya dini, unataka mashahidi kutoka kwa Fatimah ambaye alikuwa katika umiliki wa mali hiyo tangu wakati wa uhai wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Aidha, je, maneno ya Fatimah, ambaye ni mmoja wa Ashab-e-Kisa (Watu wa Shuka) na ambaye amejumuishwa katika aya ya utakaso, sio ya kweli?”

Kama watu wawili wangetoa ushahidi kwamba Fatimah amefanya makosa fulani, hebu niambie ungemshughilikia vipi?” Abu Bakr akasema: “Ningetoa adhabu juu yake kama ambavyo ningefanya kwa mwanamke yeyote.”

Mtukufu Imamu akasema: “Kama ungefanya hivyo, ungekuwa kafiri mbele ya Allah, kwa sababu ungekuwa umekataa ushahidi wa Allah kuhusu usafi wa Fatimah. Allah anasema:

‘Hakika, hakika, Allah anataka kukuondoleeni kila aina ya uchafu, Enyi Watu wa Nyumba na kuwatakaseni kwa utakaso halisi.’ Je, aya hii haikuteremshwa katika kutukuza sisi?”

Abu Bakr akasema: “Kwanini isiwe hivyo?” Imamu akasema: “Je, inawezekana kwamba Fatimah, ambaye usafi wake umethibitishwa na Allah, angeweza kutoa madai ya uwongo kwenye mali ndogo kama hii? Unakataa ushahidi wa mtu aliyetakaswa na unakubali ushahidi wa Bedui ambaye anakojoa juu ya kisigino cha mguu wake mwenyewe!”

Baada ya kusema haya, Imam akarudi nyumbani kwake akiwa amekasirika. Malalamiko yake yaliamsha hisia za watu. Kila mtu alisema: “Ukweli uko pamoja na Ali na Fatimah.

Wallahi Ali anasema kweli. Kwa nini binti ya Mtume afanyiwe fedheha kiasi hicho?”

Ufidhuli Wa Abu Bakr

Ibn Abi’l-Hadid anasimulia kwamba watu walivutiwa sana upingaji wa Ali na Fatimah na wakaanza kuleta fujo. Abu Bakr ambaye aliona kwamba wale watu wawili watukufu tayari wameondoka pale Msikitini alipanda mimbari na akasema:

“Enyi watu! Kwa nini mnachanganyikiwa hivi. Kwa nini mumsikilize kila mtu? Kwa vile tu nimekataa ushahidi wao, wanazungumza upumbavu. Ukweli ni kwamba yeye ni mbweha ambaye amesalitiwa na mkia wake mwenyewe.

Anasababisha kila aina ya vurugu. Anapuuzia uzito wa vvurugu na kuchochea watu kufanya fujo na ghasia. Anatafuta msaada kutoka kwa wanyonge. Anatafuta msaada kutoka kwa wanawake. Yeye ni sawa na Ummu’t-Tihal ambaye watu wa nyumbani kwake mwenyewe walipendelea kuzini naye.”

Je, maneno haya si matusi ya kufedhehesha? Je, yanakubaliana na sifa, heshima, mapenzi na huruma ambavyo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema vinawastahikia familia yake? Mpaka lini mtabakia na imani hii potofu na ushabiki? Mpaka lini mtawapinga Mashi’a na kuwaita Marafidhi na makafiri kwa sababu tu wanakosoa maneno na vitendo vya watu ambavyo vimeandikwa katika vitabu vyenu?

Historia Inahukumu Mtu

Lifikirieni suala hili kwa uadilifu. Je, ufedhuli ule wa sahaba mzee wa Mtume ulikuwa ni wa haki? Lugha mbovu na ya matusi ya Mu’awiya, Marwan na Khalid hazikuwa za kuhuzunisha hivyo kama ile ambayo inakuja kutoka kwenye mdomo wa mtu ambaye anaitwa “sahaba wa kwenye pango.”

Watukufu Waislamu! Hatukuwepo katika wakati ule. Tunasikia majina ya Ali, Abu Bakr, Umar, Uthman, Talha, Zubair, Mu’awiya, Marwan, Khalid, Abu Huraira, nk. Hatuna urafiki wala uadui na yeyote kati yao. Tunaona mambo mawili: kwanza, wale ambao walipendwa na Allah na Mtume Wake na ambao kwao heshima na utii vimeamriwa juu yao. Pili, tunapima matendo na kauli zao. Kisha tunaamua bila upendeleo. Tunajizuia kuruhusu upendeleo wetu kwa mtu fulani kupotosha uamuzi wetu.

Mshangao Wa Hadid Juu Ya Abu Bakr Kuwakashifu Ali Na Fatimah

Sio sisi peke yetu ambao tumeshitushwa na tabia kama hii. Hata maulama wenu waadilifu wanashangazwa kuyaona haya. Ibn Abi’l-Hadid anaandika katika “Sharh-e-Nahju’l- Balagha” yake, Jz. 4, uk. 80, kwamba maneno ya Khalifa yalimjaza na mshangao. Alimuuliza mwalimu wake Abu Yahya Naqib Ja’far Bin Yahya Bin Abi Zaidu’l-Basari, maneno haya ya Khalifa yalikuwa yanamhusu nani. Yeye alisema kwamba kauli hizo hazikuwa za kupitia. Uhusikaji wake ulikuwa wa wazi.

Ibn Hadid akasema: “Kama ungekuwa wa wazi, nisingeuliza.” Hapo alicheka na akasema: “Mambo haya yalisemwa dhidi ya Ali.”Ibn Hadid akayarudia maneno haya kwa mshangao: “Maneno yote haya yalisemwa dhidi ya Ali?” Mwalimu wake akasema: “Ndio, Ewe mwanangu! Hivi ndivyo utawala unavyomaanisha.”

Kumuudhi Ali Ni Kumuudhi Mtukufu Mtume

Kuhusu wote wawili Ali na Fatimah, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema kwamba shida zao ni shida zake yeye pia. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Yule ambaye anatawasumbua hawa wawili ananisumbua mimi, na mtu anayenisumbua mimi anamsumbua Allah.” Vile vile imeandikwa katika vitabu vyenu sahihi kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Yeyote yule ambaye anamtukana Ali ananitukana mimi, ambaye ananitukana mimi anamtukana Allah.”

Muhammad bin Yusuf Ganji Shafi’i, katika kitabu chake “Kifayatut-Talib” Sura ya 10, anasimulia hadithi ndefu kutoka kwa Ibn Abbas, ambaye alikiambia kikundi cha Wasiria ambao walikuwa wakimlaani Ali kwamba yeye alimsikia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akisema kumhusu Ali: “Yeyote yule anayekutuka wewe amenitukana mimi, na yeyote anaye nitukana mimi amemtukana Allah, na ambaye anamtukana Allah atatupwa moja kwa moja Motoni.”

Baada ya hadithi hii alinukuu hadithi nyingine nyingi kutoka kwenye vyanzo sahihi ambazo zote zinathibitisha kwamba wale ambao wanamtukana Ali ni makafiri. Sura ya 10 ya kitabu hiki inaitwa: “Kuhusu ukafiri wa mtu ambaye anamtukana Ali.”

Vile vile Hakim katika kitabu chake, “Mustadrak”, Jz. 3, uk. 121, ameinukuu hadithi hii hii. Hivyo kwa mujibu wa hadithi zote hizi, wale ambao wanamlaani Ali, wanamlaani Allah na Mtume Wake. Wote hao (kama Mu’awiya, Bani Umayyah, Manasibi, Khawariji) wenyewe wamelaaniwa.

Basi, sasa kiasi hiki kinatosha. Hakika Siku ya Hukumu kwa hakika itafika. Kwa vile wahenga wetu walioonewa walichukuwa njia ya ukimya na kuacha uamuzi juu ya Siku hiyo, sisi vile vile tutabakia kimya.

Kuna nukta ya pili ambayo inakataa ‘hadithi hii ya kudhaniwa’ “Sisi hatuachi urithi…” Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Mimi ni jiji la elimu na Ali ni lango lake; na mimi ni nyumba ya hekima na Ali ni mlango wake.” Madhehebu zote zimelikubali hili.

Hakika mtu ambaye alikuwa ni lango la elimu ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alielewa hadithi zote na maelekezo ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), hususan zile zinahusiana na matatizo ya mirathi.

Kwani ustawi wa taifa zima hutengemea juu ya hadithi hizi. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) vile vile alisema: “Mtu ambaye anataka kupata elimu lazima aje kwenye mlango wa Ali.”

Kama elimu yake ingelikuwa sio kamili, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) asingesema kwamba Ali alikuwa hakimu bora katika Umma mzima. Alisema: “Ali ni mbora miongoni mwenu wote katika kuzitafsiri sheria.” Hadithi hii imeandikwa katika vitabu vyenu vyote vya sahihi.

Hivi Mtukufu Mtume angeweza kutangaza ubora wa ubingwa wa mtu wa sheria kama mtu huyo alikuwa hayaelewi matatizo ya mirathi na haki za watu? Sehemu ya lengo la Mtukufu Mtume lilikuwa ni kuleta mageuzi ya kijamii kwa ajili ya watu katika dunia hii na amani na starehe kwa ajili yao katika akhera.

Angeweza vipi basi kumfanya yeye Ali kuwa Amirul-Mu’minin na kisha bado asimfikishie desturi kama hii ambayo inaathiri utaratibu wote wa kijamii?

Sheikh: Hakuna kati ya vitu hivi viwili kilichothibitishwa kwa mujibu wetu. Hadithi ya Jiji la elimu haikubaliwi na maulamaa wetu mashuhuri na mas’ala ya umakamu na urithi (wa nafasi ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)) pia vile vile yamekataliwa na wale maulamaa wakubwa.

Bukhari na Muslim katika kukusanya kwao hadithi na wengine miongoni mwa maulamaa wakubwa, wanasimulia kutoka kwa Ummu’l-Mu’minin Aisha kwamba, kichwa cha Mtume wakati wa kifo chake kilikuwa kimelala kifuani mwake mpaka alipokata roho. Alieleza kwamba hakutengeneza wosia. Lau angelitengeneza wosia Ummu’l-Mu’minin angesimulia na suala la wosia lingeliweza kutatuliwa.

Hadithi “Mimi Ni Jiji La Elimu Na Ali Ni Lango Lake”

Muombezi: Kuhusu hadithi hii umekuwa sio mkweli hata kidogo. Nilikwishakuambia tayari kwamba madhehebu zote kwa pamoja zinakubaliana kwamba hii imesimuliwa takiriban kwa mwendelezo kamili. Maulamaa wenu wafuatao wamethibitisha usahihi wa hadithi hii:

Imam Tha’labi, Firuzabadi, Hakim Nishapuri, Muhammad Jazari, Muhammad Bin Jarir Tabari, Suyuti, Sakhawi, Muttaqi Hindi, Muhammad Bin Yusuf Ganji Shafi’i, Muhammad Bin Talha Shafi’i, Kadhi Fadhl Bin Ruzbahan, Munawi, Ibn Hajar Makki, Khatib Khawarizmi, Sulaiman Qanduzi Hanafi, Ibn Maghazil Faqih Shafi’i, Dailami, Ibn Talha Shafi’i, Mir Sayyid Ali Hamadani, Hafidh Abu Nu’aim Ispahani, Sheikhu’l-Islam Hamwaini, Ibn Abi’l-Hadid Mu’tazali, Tibrani, Sibt Ibn Jauzi na Imam Abdu’r-Rahman Nisa’i.

Umakamu Ulitunukiwa Juu Ya Ali

Kuhusu mas’ala ya umakamu, kuna kauli nyingi za kuaminika zinayothibitisha kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alitengeneza wosia wake. Hakuna mtu mwenye ujuzi anayekataa jambo hili.

Nawab: Khalifa wa Mtume pia ni makamu wake, mtu ambaye aliendesha mambo yake ya ndani. Kwa mfano, walilipa posho kwa wake za Mtume. Kwa nini unasema kwamba Ali aliteuliwa kuwa makamu?

Muombezi: Unasema kweli. Ni wazi kwamba Khalifa wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa pia ni makamu wake. Wakati wa mikesha iliyopita nimewasilisha hoja zangu na kauli za kuaminika kuhusiana na ukhalifa. Kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimteua Ali kuwa Khalifa wake na makamu wake ilikuwa ni sahihi kabisa.

Ambapo wengine walikuwa wanajishughisha na mambo yao na njama za kisiasa, huyo makamu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alishughulika na taratibu za mazishi ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Baadaye alijishughulisha katika kurudisha fedha za amana na vitu vingine vya thamani na kuangalia masuala mengine ambayo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa ameyakabidhi kwake.

Hili liko wazi mno kiasi kwamba hakuhitajiki uthibitisho wowote. Maulamaa wetu wote wanakubalina kuhusiana na jambo hili.

Hadithi Kuhusu Ushika Umakamu

Ili kuthibitisha hoja yangu ngoja nirejee kwenye baadhi ya hadithi:

(1) Kuunda udugu:Imam Tha’labi katika kitabu chake “Manaqib” na “Tafsir”, Ibn Maghazili Faqih Shafi’i katika “Manaqib” yake na Mir Sayyid Ali Hamadani katika kitabu chake “Mawaddatu’l-Qurba” (Mawadda ya 6) anasimulia kutoka kwa khalifa wa pili, Umar bin Khattab, ambaye anasema kwamba wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipokuwa anaanzisha undugu kati ya masahaba, alisema: “Huyu Ali ni ndugu yangu katika ulimwengu huu na kesho akhera. Miongoni mwa kizazi changu yeye ni khalifa wangu; ni mrithi wangu (makamu) katika Umma wangu. Yeye ndiye mrithi wa elimu yangu; ndiye mlipaji wa deni langu. Kilicho chake ni changu pia; kilicho changu ni chake pia; manufaa yake ni manufaa yangu na hasara yake ni hasara yangu. Yule ambaye ni rafiki yake kwa hakika ni rafiki kwangu na ambaye ni adui kwake kwa hakika ni adui kwangu.”

(2) Kuuliza kwa Salman: Sheikh Suleiman Balkhi Hanafi katika sura ya 15 ya “Yanabiu’l-Mawadda” amesimulia hadithi ishirini katika kuunga mkono umakamu wa Ali kutoka kwa Imam Tha’labi, Hamwaini, Hafidh Abu Nu’am, Ahmad Bin Hanbal, Ibn Maghazili, Khawarizmi na Dailami. Nawasilisha baadhi ya hizo kwa ajili ya mwongozo wenu. Anasimulia kutoka kwenye Musnad ya Ahmad Bin Hanbal (na Sibt Ibn Jauz katika Tadhkirat-e-Khawasu’l-Umma, uk. 26, na Ibn Maghazili Shafi’i katika Manaqib yake vile vile wamesimulia hadithi hizi) kwamba Anas Ibn Malik amese- ma: “Nilimuomba Salman amuulize Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ni nani mrithi wake (wasii). Salman akamuuliza Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), “Ewe Mtume wa Allah! Ni nani makamu wako?” Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema, “Ewe Salman! Ni nani mrithi wa Salman?” Akasema, “Yusha Bin Nun.” Kisha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema, “Makamu wangu na mrithi wangu, ambaye atalipa madeni yangu na atakayekamilisha ahadi zangu, ni Ali Bin Abi Talib.

(3) Kila Mtume alikuwa na Mrithi wake, Ali ni Mrithi wangu: Imesimuliwa kutoka kwa Muwaffaq Bin Ahmad, ambaye ananukuu kutoka kwa Buraida kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Kila Mtume alikuwa na makamu na mrithi, na kwa hakika, makamu na mrithi wangu ni Ali.” Muhammad Bin Yusuf Ganji Shai’i katika kitabu chake “Kifayatut-Talib”, sura ya 62, uk. 131 ananukuu hadithi hiyo hiyo ambayo vile vile imesimuliwa na Muhadith wa Syria katika kitabu chake “Ta’rikh”.

(4) Ali ni mwisho wa Mawasii: Sheikhu’l-Islam Hamwaini anasimulia kutoka kwa Abu Dharr Ghifari, ambaye amesema, “Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema, ‘mimi ni mwisho wa Mitume na wewe, Ewe Ali, ni mwisho wa mawasii mpaka Siku ya Hukumu”.

(5) Ali ni makamu wangu kutoka kwenye kizazi changu: Imesimuliwa kutoka kwa Khatib Khawarizmi, ambaye anasimulia kutoka kwa Ummu’l-Mu’minin Ummi Salama, ambaye amesema; “Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: ‘Allah amechagua mrithi kwa ajili ya kila Mtume na baada yangu mimi makamu wangu kutoka kwenye kizazi changu na Umma wangu ni Ali.’”

(6) Ali alitetea cheo chake katika hotuba: Imesimuliwa kutoka Maghazili Faqih Shafi’i, ambaye anasimulia kutoka kwa Asbagh Bin Nabuta, mmoja wa Masahaba wakubwa wa Amiru’l-Muminin, na Muslim na Bukhari vile vile wamenukuu kutoka kwake kwamba bwana wake Amiru’l-Mu’minin amesema katika moja ya hotuba zake: “Enyi watu! Mimi ni Imam (kiongozi) wa viumbe wote.

Ni mrithi wa (makamu) wa mbora mno wa viumbe; mimi ndio baba wa kizazi kilicho takasika kabisa na chenye kuongoza; mimi ni ndugu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.); mrithi wake, rafiki yake muaminifu na mwenza wake wa karibu. Mimi ni bwana wa waumini; ni kiongozi wa wale ambao wana nyuso angavu, mikono angavu na miguu angavu; mimi ni mkuu wa Mawasii wote. Kupigana dhidi yangu ni kupigana dhidi ya Allah. Kufanya amani na mimi ni kufanya amani na Allah. Utii kwangu ni utii kwa Allah; urafiki na mimi ni urafiki na Allah; wafuasi wangu ni marafiki wa Allah; na wasaidizi wangu ni wasidizi wa Allah.”

(7) Allah alinifanya mimi Mtume na Ali makamu wangu: Vile vile Ibn Maghazili Shafi’i katika “Manaqib” yake anamnukuu Abdullah Bin Mas’ud kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Ujumbe wa utume uliishilizwa kwangu mimi na Ali; katu hakuna kati yetu sisi aliyewahi kusujudu mbele ya sanamu; hivyo Allah alinifanya mimi Mtume na Ali kuwa makamu.”

(8) Umakamu wa Ali ni sehemu ya kanuni ya kiapo cha utii kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): Mir Sayyid Ali Hamadani Shafi’i anaandika katika kitabu chake “Mawaddatu’l-Qurba” Mawadda ya 4, kutoka kwa Atba Bin Amir Jahni, ambaye amesema: “Tunatoa kiapo cha utii kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), tukukiri ukweli kwamba hakuna mungu isipokuwa Allah. Ni Mmoja na mshirika na hakika Muhammad ni Mtume Wake na Ali ni makamu Wake. Hivyo kama tunaacha chochote kati ya mambo haya matatu tutakuwa makafiri.”

(9) Ninawaita watu kwenye haki na Ali anaitia nuru: Katika Mawaddatu’l-Qurba hiyo hiyo, vile vile imeandikwa kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Hakika Allah ameteua makamu kwa kwa ajili ya kila Mtume: Seth, makamu wa Adamu; Joshua, makamu wa Musa; Simon Petro makamu wa Yesu; na Ali ni makamu wangu; na makamu wangu ni mbora wa makamu wote. Nawaita watu kwenye haki na Ali anaitia nuru.”

Allah Alimteua Ali Kutoka Miongoni Mwa Watu Wote Kuwa Makamu Wangu

Mwandishi wa Yanabi ananukuu kutoka kwenye Manaqib ya Muwaffaq Bin Ahmad Khawarizmi, ambaye alisimulia kutoka kwa Abu Ayyub Ansari, ambaye amesema kwam- ba wakati Mtume wa Allah alipokuwa yu mgonjwa kitandani, Fatimah alikuja na kuanza kulia. Kisha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Ewe Fatimah, wewe umebarikiwa makhususi na Allah ambaye amekupa mume ambaye Uislamu wake ni wa mbele zaidi, ambaye elimu yake ni bora kuliko ya mtu yeyote yule, na ambaye uvumilivu wake unapita uvumilivu watu mengine wote.

Kwa hakika Allah swt. Amewapa upendeleo maalumu watu wa ulimwengu huu. Kutoka miongoni mwao Alichagua na kuniteua mimi kama Mtume na Mjumbe Wake. Kisha akawapa baraka nyingine maalumu na kutoka miongoni mwa watu akamchagua mume wako. Na amenifunulia kwamba nikuoze wewe kwake na nimfanye makamu wangu.”

Ahlul-Bayt Wamejaaliwa Sifa Saba Zisizo Na Ushindani

Baada ya kuandika hadithi hii katika Manaqib yake, Ibn Maghazili Faqih Shfi’i anaandika maneno haya ya nyongeza, ya Mtukufu Mtume: “Ewe Fatimah! Sisi Ahlul-Bayt tumejaaliwa sifa saba, ambazo hakuna katika vizazi vya wanadamu kilichokuwa nazo, na hakuna miongoni mwa vizazi vyao kitakachokuwa nazo. Mtume mtukufu mno miongoni mwa Mitume anatokana na sisi, na ni baba yako. Makamu wangu ni mbora mno kwa makamu wengine wote, na ni mume wako. Shahidi (aliyejitolea mhanga) anayewapita mashahidi wengine wote, na ni ami yako, Hamza.

Kutoka miongoni mwetu sisi (Ahlu’l-Bayt) kuna mtu ambaye ana mbawa mbili ambazo kwazo anaruka kwenda popote anapopenda, huko Peponi, na ni binamu yako, Ja’far. Kutokana na sisi kuna wajukuu wawili ambao ni mab- wana wa vijana wa Peponi, na ni watoto wako. Na ninakuambia, kwa jina la Allah ambaye anamiliki uhai wangu, kwamba Mahdi wa Umma huu, ambaye kwamba Isa Bin Mariamu atasali Salat nyuma yake, atakuwa ni katika kizazi chako.”

Mahdi Ataijaza Ardhi Na Uadilifu

Ibrahim Bin Muhammad Hamwaini, baada ya kusimulia hadithi hii alinukuu maneno haya ya nyongeza: Baada ya kumtaja Mahdi Mtume alisema: “Ataujaza ulimwengu huu na uadilifu wakati utakapokuwa umejaa ukatili na dhulma. Ewe Fatima! Usihuzunike na usilie.

Kwa sababu ya mapenzi na heshima yangu kwako, Allah swt., ni mpole zaidi kwako kuliko mimi. Amekupa wewe mume mwenye mafanikio ya hali ya juu mno ya kiroho, na aliye tukuka mno katika hadhi ya kifamilia, mwenye huruma sana kwa watu, muadilifu mno katika kushughulikia mambo ya watu, na msahihi mno katika maamuzi yake.” Nafikiri kiasi hiki kinatosha kuridhisha udadisi wa Nawab Sahib na kuondoa kuelewa vibaya kwa Sheikh Sahib.

Wakati Wa Kifo Chake, Kichwa Cha Mtukufu Mtume (S.A.W.W.) Kilikuwa Juu Ya Kifua Cha Amir-Ul-Mu’minin (A.S.)

Amma kwa madai ya kwamba wakati wa kifo cha Mtume, kichwa chake kilikuwa juu ya kifua cha Ummu’l-Mu’minin Aisha, sio kweli. Maulamaa wenu wenyewe wameonesha kwamba wakati wa kifo cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kichwa chake kilikuwa kimeegamia juu ya kifua cha Amirul-Muminin.

Sheikh: Ni katika kitabu kipi ambacho maulamaa wetu wameandika habari hii?

Muombezi: Soma “Kanzu’l-Ummal”, Jz. 4, uk. 55 na Jz. 6, uk. 392 na 400; na “Tabaqa” cha Muhammad Bin Sa’d Katib, sehemu ya 2, uk. 51; “Mustadrak” cha Hakim Nishapuri, Jz. 3, uk. 139; Talkhis-e-Dhahab; Sunan ya Ibn Shabih; “Kabir” cha Tabari; Musnad ya Imam Ahmad Hanbal, Jz.3; “Hilyatu’l-Auliya” cha Hafidh Abu Nu’aim. Pamoja na tofau- ti ndogo ya maneno, maandishi yote haya yanasimulia kutoka kwa Ummu’l-Mu’minin Umm Salma na Jabir Ibn Abdullah Ansari kwamba wakati wa kifo chake, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimuita Ali na kuweka kichwa chake juu ya kifua cha Ali mpaka alipofariki.

Kwa nyongeza ya maneno haya, kuna maelezo ya Amiru’l-Mu’minin mwenyewe ambayo yameandikwa katika kitabu chake cha Nahju’l-Balagha. Ibn Abi’l-Hadid katika “Sharhe Nahju’l-Balagha” yake, Jz. 2, uk. 561 anaeleza kwamba Mtukufu Imam kwa uwazi kabisa alisema: “Hakika roho ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) iliondoka ulimwenguni hapa wakati ambapo kichwa chake kilikuwa juu ya kifua changu; alivuta pumzi yake ya mwisho akiwa mikononi mwangu.

Hivyo nilifuta mikono yangu kwenye uso wangu.” Ibn Abi’l-Hadid katika Jz. 2, uk. 562, ya kitabu chake anafafanua juu ya maelezo haya ya Imamu Ali, kwamba wakati kichwa cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kilipokuwa juu ya kifua cha Ali, matone kadhaa ya damu ya Mtume yalidondoka chini, ambayo Ali aliyafuta kwenye uso wake.

Na katika ukurasa wa 590 wa kitabu hicho hicho, katika kuandika kwake kuhusu mazishi ya Fatimah, anasema kwamba Ali alizungumza na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Hakika nilikulaza kwenye kaburi; roho yako ilikutoka kati ya shingo na kifua changu.”

Maelezo yote haya sahihi na hoja nzito zinazothibitisha wazi kwamba maelezo ya Aisha hayawezi kukubaliwa. Ni ukweli unaojulikana kwamba Aisha alimpinga Amiru’l-Mu’minin kuanzia mwanzo kabisa. Insha-Allah nitaelezea kuhusu hili vile vile kama hali itahitaji hivyo.

Kudadisi Kuhusu Urithi Au Umakamu Unaofuatia Mara Moja

Hadithi hizi kwa uwazi zinaonesha kwamba Allah aliteuwa mitume na makamu. Vile vile alimteua Ali kama makamu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Aidha, mrithi hapa ina maana ya ukhalifa, sio urithi wa hivi tu wa kifamilia. Kwa hiyo makamu alipewa mamlaka kamili juu ya watu binafsi na jamii katika mambo yao yote, mamlaka kama yale yale aliyokuwa nayo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Maulamaa wenu wote mashuhuri wameukiri uongozi huu wa Umma, ambao ulitolewa kwa Ali. Hakuna aliyeukataa isipokuwa mashabiki wachache na maadui, ambao wamekataa kukubali sifa za hali ya juu za Mtukufu Imam. Ibn Abi’l-Hadid anasema katika Sharhe yake ya “Nahju’l-Balagha”, Jz. 1, (iliyochapishwa Misri): “Kwa mujibu wetu sisi hakuna shaka kwamba Ali alikuwa wasii (makamu) wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), na kwa maoni yetu, mtu anayepinga ukweli huu ni yule tu ambaye ana chuki au uadui dhidi yake.”

Mashairi Ya Baadhi Ya Masahaba Kuhusu Umakamu

Ibn Abi’l-Hadid ananukuu idadi ya mashairi ambayo huthibitisha umakamu wa Amiru’l-Mu’minin. Miongoni mwa hayo ni mashairi mawili ya Abdullah Bin Abbas, ambaye yeye amesema:

“Mbali na kuwa kwako wewe ni Ahlu’l-Bayt, vile vile wewe ni wasii (makamu) wake, na pale mtu anakukabili wewe katika uwanja wa vita, wewe ndiye mpiganaji bora.”

Ananukuu mashairi ya Khazima Bin Thabit: “Mbali na ukweli kwamba umejumuishwa katika Ahlu’l-Bayt wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), vile vile wewe ni mrithi (makamu) wake wa kufuatia mara moja, na ushahidi wa yote yale yaliyokuja kwake.” Vile vile ananukuu shairi la Sahaba, Abu’l-Hakim Tihan, ambaye alisema: “Hakika, ni yule mrithi (makamu) wa mara moja wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ambaye ndiye Imam na bwana wetu. Pazia zimeondolewa na siri zimefichuliwa.”

Pengine hii inatosha. Kama unataka kuona mashairi zaidi juu ya nukta hii unaweza kusoma kitabu hicho hicho. Kama anavyosema Ibn Abi’l-Hadid kama asingekuwa anaogopa kukikuza mno kitabu hiki, angejaza kurasa zaidi kwa mashairi haya yanayothibitisha umakamu wa Ali. Hivyo ina maana kwamba, umakamu na utume hutegemeana. Hii ni hatua baada ya cheo cha utume na hii ndio maana ya Mamlaka ya Mungu.

Wosia Wa Mtukufu Mtume (S.A.W.W.) Kuhusu Umakamu Wa Ali Katika

Vitabu Vyote Sahihi

Sheikh: Kama riwaya hizi ni sahihi, kwa nini hatuoni rekodi kama hiyo ya wosia na uthibitisho wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), kama tulivyo na zile ambazo zimeachwa na Abu Bakr na Umar wakati wa vifo vyao?

Muombezi: Unaweza kujionea kwa urahisi kuhusu masuala haya kutoka kwenye vitabu sahihi vya Shi’a, ambavyo vimeandika masuala haya kwa umoja wa maoni kutoka kwa Ahlu’l-Bayt, lakini kwa vile tumekubaliana katika usiku wa kwanza kwamba tusichukue njia ya hadithi za upande mmoja, inanipasa kurejea kwenye baadhi ya hadithi ambazo zinapatikana katika vitabu sahih vyenu wenyewe kama vile “Tabaqa” cha Ibn Sa’d, Jz. 2, uk. 61; “Kanzu’l-Ummal” cha Ali Muttaqi, Jz. 4, uk. 54, na Jz. 6, uk. 155, 393, 403; Musnad ya Imam Ahmad Hanbal, Jz. 4, uk. 164; na “Mustadrak” cha Hakim, Jz. 3 uk. 59, 111.

Mbali na hivi, wanachoni wenu mashuhuri kama Baihaqi katika Sunan na Dala’il yake, Ibn Abdu’l-Barr katika Isti’ab, Tabrani katika Kabir na Ibn Mardawiyya katika kitabu chake cha Ta’rikh kadhalika na wengine wamesimulia kwa maneno tofauti, yale maelekezo na maagizo ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), ambaye alisema: “Ewe Ali! Wewe ni ndugu yangu na waziri wangu; utalipa madeni yangu. Utatimiza ahadi zangu na utatekeleza majukumu yangu.

Utaikosha maiti yangu, utalipa madeni yangu na kunihifadhi kaburini.” Mbali na riwaya hizi za wazi, kuna idadi nyingine kubwa za maagizo au amri, ambazo zilitamkwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kuhusiana na suala hili.

Mtukufu Mtume Alizuiwa Kuandika Wosia Wake Wakati Wa Kifo Chake

Sheikh: Qur’ani Tukufu inasema: “Mmeandikiwa mmoja wenu anapofikiwa na mauti, kama akiacha mali afanye wosia kwa wazai wake jamaa zake kwa namna nzuri inayopendeza. Ni wajibu haya kwa wachamungu.” (2:180)

Kwa hiyo ilikuwa muhimu kwa Mtume kufanya wosia na kuteua mrithi wake wa mara moja. Wakati alipoona kifo chake kinakaribia kwa nini asifanye wosia wake kama walivyofanya Abu Bakr na Umar?

Muombezi: Kwanza, kwa maneno, Wakati mmojawenu anapokaribiwa na kifo” je, una maana ya dakika za mwisho za uhai? Katika wakati huo ni aghalabu mtu yeyote kuwa na akili timamu na akawa na uwezo wa kutekeleza majukumu yake kwa makini. Hakika maelezo haya yanaashiria kwenye wakati wa dalili na ishara za uzee, udhaifu na ugonjwa vinapojitokeza.

Pili, kauli yako hii tena imenitonesha hisia zangu na kunikumbusha msiba ambao hauwezi kusahaulika, Mtukufu babu yangu, Mtume wa Allah, alisisitiza umuhimu wa Waislamu kufanya wosia. Alisema: “Yule ambaye atakufa bila kufanya wosia, anakufa kifo cha kijinga, iwapo kutatokea kutokuelewana miongoni mwa warithi.” Wakati wa kipindi chake cha miaka 23 ya maisha ya kijamii alirudia rudia kumtangaza ‘wasi’ wake, yule mtu ambaye Allah alikuwa amemteua kama mwandamizi.

Wakati yeye mwenyewe alipokuwa katika kitanda chake alichofia alitaka kurudia kile ambacho amekitangaza mara nyingi sana ili kwamba Umma usije ukapotoshwa na kuangukia kwenye makundi yenye kugombana. Inasikitisha kwamba wanamizengwe wa kisiasa walimpinga na kumzuia kutekeleza wajibu wake wa kidini. Matekeo yake ni kwamba, hata wewe pia unapata fursa ya kuuliza kwa nini Mtume hakufanya wosia.

Kutotiiwa Kwa Amri Ya Mtume Hakuaminiki

Sheikh: Nafikiri maelezo yako haya hayana msingi wa kweli. Kwa hakika hakuna anayeweza kumzuia Mtume kutekeleza wajimu wake. Qur’ani Tukufu kwa uwazi kabisa inasema!: “Chochote anachokupeni Mtume kipokeeni, na chochote kile ambacho anakukatazeni, jiepusheni nacho.” (59:7) Vile vile katika aya nyingine nyingi utii kwa Mtume umefanywa kuwa ni suala la wajibu.

Kwa mfano, Allah anasema: “Mtiini Allah na mtiini Mtume.” Ni dhadhiri kabisa, kukataa kumtii Mtume wa Allah ni ukafiri. Hivyo, Mashaba na wafuasi wa Mtume wasingeweza kumzuia kutangaza wosia wake. Inawezekana hadithi hii ni ya kughushi, ambayo imesambazwa na makafiri kuthibitisha uzembe wa Umma.

Riwaya Sahihi Kuhusu Mtume Kuzuiwa Kuandika Wosia Wake

Muombezi: Tafadhali usijifanye kuwa mjinga. Hii sio riwaya ya kughushi. Ni hadithi inayojulikana, ambayo madhehebu zote za ki-Islamu wanaikubali.

Hata Bukhari na Muslim, ambao walikuwa waangalifu sana kuhusu hadithi yoyote kama hiyo, ambayo ingeweza kutishia maoni yao wenyewe, wamesimulia tukio hili katika vitabu vyao vya hadithi.

Wanaandika kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), wakati akiwa katika kitanda chake alichofia, aliomba karatasi na wino ili kwamba aweze kutoa maelekezo fulani yaandikwe kwa ajili yao ambayo yangewahifadhi wao wasipotee baada ya kifo chake. Baadhi ya wale waliokuwepo,wakishawishiwa na mwanasiasa, walisababisha vurugu kiasi kwamba Mtume akakasirika sana na akawaamuru waondeke.

Sheikh: Siwezi hata kwa dakika moja kuliamini hili. Nani atathubutu kiasi hicho kuweza kumpinga Mtume wa Allah? Hata kama mtu wa kawaida akitaka kuandika wosia wake, hakuna mtu anayeweza kumzuia.

Vipi mtu ataweza kumzuiya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kufanya wosia wake? Kutomtii yeye ni ukafiri. Kwa vile wosia wa watu wakubwa wa jumuiya ni chanzo cha mwongozo, hakuna mtu ambaye angeweza kuuzuia usitekelezwe. Khalifa Abu Bakr na Umar walifanya wosia wao, na hakuna mtu aliyewazuiya kufanya hivyo. Narudia tena, siiamini riwaya hii.

Muombezi: Unaweza ukaiamini au usiiamini. Kusema kweli kila Mwislamu anashangaa kuisikia. Kila mtu, wa taifa lolote au jumuiya awezayo kuwa, anapigwa na mshangao kusikia tukio kama hili.

Ibn Abbas Analia Kwa Sababu Mtukufu Mtume (S.A.W.W.) Alizuiwa Kuandika Wosia Wake

Hili sio suala la huzuni kwako wewe na sisi tu peke yetu. Masahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) vile vile walisikitikia tukio hili la msiba. Bukhari, Muslim, na maulamaa wengine wakubwa wa madhehebu yenu wamesimulia kwamba Abdullah Bin Abbas mara kwa mara alitokwa na machozi na alisema:

“Oh! Alhamisi ile! Oh! Alhamisi ile! Jinsi gani ilivyokuwa katika Alhamisi ile!” Kisha alilia sana kiasi kwamba ardhi ilitota kwa machozi yake.

Watu walimuuliza ilitokea nini siku ya Alhamisi kinachomfanya alie. Yeye alijibu kwamba, wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akiwa amelala katika kitanda chake alichofia, aliomba karatasi na wino ili kwamba aweze kuandika wosia, ambao ungewazuia kupotea baada yake, baadhi ya wliokuwepo walimzuia kufanya hivyo na hata walithubutu kusema kwamba Mtume alikuwa anaweweseka (Allah anisamehe!). Alhamisi ile haiwezi kusahauliwa. Hawakumruhusu Mtume kuandika wosia wake na walimuudhi kwa kauli zao.

Umar Alimzuia Mtukfu Mtume Kuandika Wosia Wake

Sheikh: Ni nani aliyemzuia Mtume wa Allah kufanya wosia wake?

Muombezi: Alikuwa ni Khalifa wa pili, Umar Bin Khattab, ndiye ambaye alimzuia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kufanya wosia wake.

Sheikh: Nashukuru sana kwamba umenituliza. Maelezo haya yananisumbua sana. nilikuwa na mwelekeo wa kusema kwamba riwaya hizi zimeghushiwa na Mashi’a, lakini nilinyamaza kwa sababu ya kukuheshimu. Sasa nakuambia kile kilichoko moyoni mwangu. Nakushauri usieneze visa hivi vya kubuni.

Muombezi: Nakushauri usikubali au kukataa mambo bila kuangalia sawa sawa. umefanya haraka isiyo na sababu katika suala hili na umewashutumu Mashi’a wasio na hatia kwa ughushaji.

Vitabu vyenu wenyewe vimejaa riwaya tele ambazo zinaunga mkono haya maoni yetu.

Vyanzo Vya Hadithi Ya “Kuzuiwa Kwa Wosia”

Kama utaviangalia vitabu vyenu wenyewe, utaona kwa maulamaa wenu wenyewe wa kusifika, wamesimulia tukio hili. Kwa mfano, Bukhari, katika Sahih yake, Jz. 2, uk. 118; Muslim, katika Sahih yake (mwishoni mwa Kitab-e-Wasiyya); Hamidi katika Jam’i Bainus-Sahihain; Imam Ahmad Bin Hanbal, katika Musnad, Jz. 1, uk. 222; Ibn Abi’l- Hadid, katika Sharh-e-Nahju’l-Balagha, Jz. 2, uk. 563; Kirmani, katika Sharh-e-Sahih Bukhari; Nuwi katika Sharh-e-Muslim; Ibn Hajar, katika Sawa’iq; Kadhi Abu Ali; Kadhi Ruzbahan; Kadhi Ayaz; Imam Ghazali, Qutbu’d-Din Shafi’i; Muhammad Ibn Abu’l-Karim Shahrastani; Ibn Athir; Hafidh Abu Nu’aim Ispahani; Sibt Ibn Jauzi; na wengine katika maulamaa wenu kwa ujumla wamethibitisha habari hii ya msiba. Wameandika kwamba wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anarudi kutoka kwenye hija yake ya mwisho, alishikwa na maradhi. Wakati kikundi cha Masahaba kilipokuja kumuona, alisema: “Nileteeni wino, na karatasi, ili nikuandikieni wosia ambao hautawafanya ninyi mpotee baada yangu.”

Umar Alisema: “Mtu Huyu Anaweweseka, Inatutosha Sisi Qur’ani”

Imamu Ghazali ameandika katika kitabu chake Sirru’l-Alamin, Maqala ya 4, ambapo kwayo Sibt Ibn Jauzi vile vile anainukuu katika kitabu chake Tadhkirat, uk. 36, na wengine wengi wa maulamaa wenu wakubwa wamesimulia kwamba, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliwataka watu kumletea wino na karatasi, na kwa mujibu wa baadhi ya hadithi alisema: “Nileteeni wino na karatasi ili nikuondoleeni kutoka katika mawazo yenu mashaka yote ya ukhalifa baada yangu; yaani nitakuambieni ambaye anayestahiki ukhalifa baada yangu.”

Kufikia hapa, wao wanaandika, Umar akasema, ‘Muacheni mtu huyu, kwani kwa hakika anaweweseka (Allah anisamehe!); Kitabu cha Allah kinatutosha sisi.’”

Mtukufu Mtume (S.A.W.W.) Anawaamuru Masahaba Wanaozozana Wamuondokee

Baadhi ya Masahaba walikubaliana na Umar, na baadhi wakakubaliana na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Kulikuwa na ghasia kubwa na rabsha kiasi kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Niondokeeni; haifai kwenu kuonyesha hasira mbele yangu.”

Hii ilikuwa ndio vurugu ya kwanza miongoni mwa Waislamu mbele ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) katika kipindi chake chote cha miaka 23 ya huduma yake ngumu sana. Chanzo cha tatizo hili kilikuwa ni Khalifa Umar, ambaye alipanda mbegu ya kutokuelewana miongoni mwa Waislamu.

Leo wewe na mimi, ndugu wawili katika Uislamu, matoleo yake tunakabiliana wenyewe kwa wenyewe katika upinzani.

Kumuita Mtukufu Mtume (S.A.W.W.) “Mtu Huyu” Ilikuwa Ni Dharau Kubwa

Sheikh: Haikutegemewa kwa mtu kama wewe kuwa jasiri kiasi hicho cha kuweza kusema maneno ya uzushi kuhusu mtu mkubwa kama Khalifa Umar.

Muombezi: Tuambie iwapo nilionesha ufidhuli wowote katika kusimulia mambo ya kihistoria kutoka kwenye vitabu vyenu wenyewe. Je, unafikiri kwamba Khalifa Umar alikuwa fidhuli wakati alipomzuia Mtume kuandika wosia wake? Je, alikuwa fidhuli wakati alipomkashifu Mtume mbele yake?

Mshairi mmoja amesema kwa usahihi kabisa: “Unaona kibanzi katika macho yangu, lakini huoni boriti kwenye macho yako mwenyewe.” Je, Allah swt. Hasemi kwamba: “Muhammad si baba wa yeyote katika watu wenu, bali ni Mtume wa Allah na mwisho wa Mitume?” Jina la Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) lazima siku zote litajwe kwa heshima ipasayo na kwa staha. Lazima aitwe “Mtume wa Allah” au “Mwisho wa Mitume.”

Lakini Umar hakuonesha heshima juu ya amri hii ya Mungu, badala yake akamuita Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kama “mtu huyu.” Sasa hebu sema kwa jina la Allah iwapo hiyo dharau ilitendwa na mimi au na Khalifa?

Neno ‘Hajar’ Lililotumiwa Na Umar Lina Maana Ya Kuweweseka

Sheikh: Kwa nini unasema kwamba Hajar maana yake ni kuweweseka?

Muombezi: Wafasiri wote na maulamaa wenu wakubwa wanatoa maana ya Hajar kama ni kuweweseka. Kwa mfano, Ibn Athir katika kitabu chake Jam’u’l-Usul, Ibn Hajar katika Sharh-i-Sahih Bukhari, na waandishi wengine wa ukusanyaji wa hadithi wanatoa maana hiyo hiyo. Mabwana waheshimiwa! kama mtu anasema “mtu huyu anaweweseka” kuhusu Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wa Allah, je, hakuvunja adabu na amri ya Qur’ani?

Dharau Dhidi Ya Mtukufu Mtume (S.A.W.W.) Ni Ukafiri

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa hakupoteza utume wake wala uma’sum wake. Kama mtu atatafsir maneno yake kama “kuweweseka,” je hiyo haimaanishi kwamba mtu kama huyo hamuamini Allah na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)?

Sheikh: Je, ni sahihi kwa kutambua cheo chake kama Khalifa kumuona ni mwenye makosa kwa kusema kwamba hakumuamini Allah na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)?

Muombezi: Wakati unaposikia kwamba Mtume anashutumiwa kwa kuweweseka huna kipingamizi. Lakini mtu aliyekalia ofisi ya ukhalifa akitajwa na maulamaa wenu wengi kwamba alimkashifu Mtume, kwa mara moja unawatia Mashi’a kwenye makosa, badala ya kuyaweka makosa ambako kwa haki yanastahili.

Maulamaa wenu wenyewe kama Kadhi Ayaz Shafi’i katika Kitab-e-Shifa; Kirmani katika Sharh-e-Sahih Bukhari, na Nuwi katika Sharh-e-Sahih Muslim wameandika kwamba mtu ambaye ametumia maneno haya kwa uwazi hana imani kwa Mtume wa Allah.

Hivyo kama mtu yeyote akimpinga Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), hususan kwa maneno ya matusi au akisema kwamba alikuwa akiweweseka, tunaona dhahiri kabisa kwamba alikuwa hana imani kwa Mjumbe wa Allah.

Fitina Ya Kwanza Katika Uislamu Mbele Ya Mtukufu Mtume (S.A.W.W.)

Unaniuliza ni kwa nini ninamlaumu kwa kusababisha kutokuelewana miongoni mwa watu. Maulamaa wenu wenyewe wamelikubali jambo hili. Mwanachuoni mkubwa Husein Meibudi anasema katika Sharh-e-Diwan kwamba ghasia za katika Uislamu kutokea kwa mara ya kwanza mbele ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mwenyewe, wakati alipokuwa katika kitanda chake alichofia.
Matatizo yalianza wakati Umar alipomzuia Mtume kuandika wosia wake Shahrasan anasema katika kitabu chake Milal wa Nihal, Muqaddama ya 4 kwamba upinzani kati ya makundi mawili ya Waislamu ulianza wakati Umar alipokataa kuruhusu wino na karatasi kuletwa kwa Mtume kitandani kwake alipofia. Ibn Abi’l-Hadid alithibitisha ukweli huu katika kitabu chake Sharh-e-Nahju’l-Balagha Jz. 2, uk. 563.

Je, Mtume Angeweza Kuzungumza Upuuzi?

Sheikh: Kama Khalifa Umar amesema maneno haya, sioni kwamba ni kukosa heshima. Wakati mtu anaumwa sana anaweza kuweweseka. Kama akizungumza maneno yasioeleweka, tunaweza kuyaita mazungumzo yake kama ni ya kuweweseka. Katika hali hii hakuna tofauti kati ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na watu wengine.

Muombezi: Unatambua sana kwamba Mitume wote ni ma’sum na kwamba tabia hii hubakia mpaka kufa. Mtume Muhammad kwa hakika alikuwa ma’sum katika tukio hili wakati aliposema alitaka kuwakinga watu wake kutokana na kupotea baada ya kifo chake.

Kama utaziangalia aya tukufu za Qur’ani ambazo zinasema: “Na hasemi kwa matamanio (yake); hayo (maneno) bali ni wahyi ulioshushwa (kwake).” “Na lazima mfanye yale aliyoyaamrisha Mtume juu yenu…” “Na mtiini Allah na mtiini Mtume…”, wewe mwenyewe kwa uwazi utaelewa kwamba kuzuia wino na karatasi kuletewa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), kwa hakika ilikuwa ni upinzani kwa Allah. Huo ni ukweli unaokubali- ka kwamba neno kuweweseka lilikuwa ni tusi la wazi, na Khalifa kumuita kama “mtu huyu” bado lenyewe ni tusi zaidi.

Maneno “Mtu Huyu Anaweweseka” Yalikuwa Ni Matusi Zaidi

Sasa ningependa uniambie ungejisikia vipi kama mtu katika mkutano huu, atakuashiria wewe aseme “mtu huyu anaweweseka.” Wewe na mimi hatuko huru kutokana na makosa na tunaweza kuweweseka. Je, utaiita hiyo ni tabia nzuri au ni kutukana? Kama mazungumzo ya namna hii ni ya matusi katika hali hii, itakubidi ukubali kwamba ufidhuli wowote kama huo dhidi ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ulikuwa ni matusi ya hali ya juu.

Na hakuna mtu anayeweza kukataa ukweli kwamba ni wajibu wa kidini wa kila Mwislamu kuwa mbali na mtu ambaye tabia yake kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ilikuwa ya kuchukiza na kifidhuli kiasi hicho, wakati Allah amemuita katika Qur’ani Mtume Wake na Mwisho wa Mitume.

Kama utaachilia mbali chuki zako, je, akili zako za kawaida zitasema nini kuhusu mtu ambaye badala ya kumuangalia Mtume kama Mtume wa Mungu na Mwisho wa Mitume, anasema “mtu huyu anaweweseka?

Khalifa Hawezi Kutolewa Lawamani Kwa Kumkosea Adabu

Mtukufu Mtume (S.A.W.W.)

Sheikh: Tuchukulie tunakubali kwamba alikuwa katika makosa. Lakini kwa vile alikuwa Khalifa wa Mtume na alitekeleza busara zake kwa ajili ya usalama wa dini, alikuwa yuko huru kutokana na lawama zote.

Muombezi: Kwanza, kauli yako kwamba kwa vile alikuwa Khalifa na alitekeleza busara zake hayapasiki kabisa, kwa sababu katika siku ambayo alisema maneno hayo, yeye hakuwa Khalifa. Huenda pengine alikuwa hata hajauota.

Pili, kauli yako kwamba alitekeleza busara zake vile vile inashangaza. Je, hukufikiria kwamba mbele ya amri ya wazi, busara haina nafasi? Kwa kweli ni kosa ambalo kwamba mtu hawezi kusamehewa.

Tatu, umesema kwamba amefanya hivyo kwa ajili ya usalama wa dini. Kwa hakika inashangaza sana ulamaa kama wewe kuweza kupoteza hisia zote za uadilifu.

Ni Mtukufu Mtume (S.A.W.W.) Aliyekuwa Akihusika Na Usalama Wa

Dini Na Sio Umar.

Bwana mheshimiwa! Nani aliyekuwa na wajibu wa kuihifadhi dini – ni Mtme wa Allah au Umar Bin Khattab? Je, akili yako ya kawaida inakubali hoja ya kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) (baada ya kuelezea masharti ya “Hamtapotea baada ya kuandika wosia huu”) hakuweza kuelewa kwamba kuandika wosia kulikuwa ni kinyume cha dini, au kwamba Umar alikuwa akiilewa vizuri zaidi na akamzuia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kuandika wosia huu? Kushangaza kulikoje! Unajua vizuri kabisa kwamba utokaji nje wowote kwenye misingi ya dini ni dhambi kubwa, na haiwezi kusahemeka.

Sheikh: Hapana shaka kwamba Khalifa Umar alizitathmini hali na mazingira ambayo yalikuwepo katika dini na akafikia uamuzi kwamba kama Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ataandika kitu chochote, ingesababisha hitilafu kubwa na machafuko. Hivyo ilikuwa kwa ajili ya msaada na faida ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mwenyewe kwamba alizuia asipelekewe wino na karatasi.

Muombezi: Madhumuni ya hoja yako yanaelekea kuwa kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), ambaye alikuwa ma’sum, wakati alipokuwa anaulekeza Umma huu, alikuwa hana habari ya kutosha ya uwezekano wa mgogoro baada ya kifo chake, na kwamba Umar alimuongoza katika sula hili. Lakini Qur’ani inatuambia: “Haiwi kwa muumini mwanamume wala muumini mwanamke kuwa na hiari katika jambo, Allah na Mtume Wake wanapokata shauri katika jambo lao. Na mwenye kumuasi Allah na Mtume Wake, basi hakika amepotea upotofu ulio wazi.” (33:36)

Khalifa Umar aliasi amri ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), kwa kumzuia kuandika wosia wake. Aidha alikuwa fidhuli kwa kusema kwamba Mtume alikuwa anaweweseka. Ufidhuli huu uliumiza hisia za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kiasi kwamba aliwaambia watu waondeke mbele yake.

Qur’ani Tukufu Peke Yake Haitoshi Kwa Ajili Ya Mwongozo Wetu

Sheikh: Lakini nia nzuri ya Khalifa iko dhahiri katika maneno yake ya mwisho, “Kitabu cha Allah kinatutosha sisi (yaani, hatukuwa na haja ya maandishi ya Mtume wa Allah).”

Muombezi: Kwa hakika, maneno haya ndiyo uthibitisho mzuri wa ukosefu wake wa imani na kutokuijua kwake Qur’ani Tukufu. Lau angelijuwa ukweli wa Qur’ani Tukufu angelijua kwamba Qur’ani peke yake haitoshi kwa mambo yote.

Imeweka kanuni za msingi, lakini maelezo kwa urefu yameachwa kwa watarjuma na wafasiri wake. Qur’ani ina amri ambazo ni zenye kuendelea – (nasikh), na zilizofutwa - (mansukh), za jumla (‘am), haswa - mahususi (khass), zenye mipaka (muqayyad), zenye utata (mutashabih), halisi (mutlaq), mukhtasari (mujmal), au wazi (Mu’awwil).

Itawezekana vipi kwa mtu wa kawaida kupata maana kamili kutoka kwenye hii Qur’ani bila msaada wa baraka za kimungu na tafsiri iliyotolewa na wafasiri wake? Kama Qur’ani peke yake ilikuwa inatosha kwa ajili ya Umma, kwa nini aya hii iliteremshwa: “Lazima mfanye yale aliyowaamrisha Mtume kufanya; na lazima mjiepushe na yale ambayo amekukatazeni.” Allah vile vile anasema katika Qur’ani Tukufu: “…na kama wangelilipeleka kwa Mtume na kwa wenye mamlaka kati yao, bila shaka wale wanaochunguza miongoni mwao wangeliweza kulijua…” (4:83)

Kwa hiyo ina maana kwamba Qur’ani peke yake isingeweza kukidhi madhumuni yake bila ufafanuzi wa wafasiri wake, yaani, Muhammad na kizazi chake kitoharifu. Hapa tena ninaweza kurejea tena kwenye hadithi inayokubaliwa na wote (ambayo niliinukuu pamoja na baadhi ya vyanzo vyake katika mikesha iliyopita) ambayo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ameirudia hata katika wakati wake wa kufariki akisema:

“Ninaacha nyuma yangu Vitu Viwili Vizito: Kitabu cha Allah na Ahlu’l-Bayt wangu. Kama mtashikamana katika viwili hivi kamwe, kamwe hamtapotea baada yangu; kwani hakika Viwili hivi, kamwe havitaachana vyenyewe kwa vyenyewe mpaka vinifikie katika chemchemu ya Kauthar.”

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ambaye alikuwa akipewa msukumo na Allah, hakuiona Qur’ani kwa kujitenga pekee kuwa ni yenye kutosha kwa ukombozi wetu. Alisema kwamba ni lazima tushikamane na Qur’ani na Ahlul’l-Bayt kwa vile (viwili hivyo) visingetengana mpaka Siku ya Hukumu, na kwamba hivi vilikuwa ni vyanzo vya mwongozo kwa ajili ya watu. Lakini Umar akasema kwamba Qur’ani peke yake inatutosha sisi. Hii inaonyesha kwam- ba hakukitupa tu kizazi kitoharifu bali pia aliikataa amri ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Qur’ani Tukufu Vile Vile Hutuambia Tuwatake Ushauri Ahl Dhikr,

Yaani Ahlul-Bayt

Tunapaswa kumtii nani katika suala hili? Hakuna mtu mwenye akili ambaye atasema kwamba tuiache kando amri ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na kumfuata Umar. Basi kwa nini mmekubali maoni ya Umar, mkapuuza amri ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)? Kama Kitabu cha Allah kilikuwa kinatosha, kwanini tumeamriwa kuwauliza watu wa dhikir, kama Qur’ani Tukufu inavyosema: “…Basi waulizeni wenye kufahamu ikiwa ninyi hamjui.” (16:43)

Ni wazi kwamba ‘dhikr’ maana yake ni Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) au Qur’ani Tukufu na ‘watu wa dhikr’ maana yake Ahlu’l-Bayt wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Nilikwishafafanua katika mikesha iliyopita pamoja hoja halali na vyanzo sahihi kwamba maulamaa wenu wakubwa kama, Suyuti na wengine, wamesimulia kwamba “watu wa dhikr” maana yake Ahlul’l-Bayt.

Kukataliwa Maneno Ya Umar Na Qutbud-Din Shirazi

Qutbu’d-din Shirazi ambaye ni mmoja wa wanachuoni wenu wakubwa, anasema katika kitabu chake “Kashfu’l-Ghuyub”: “Ni ukweli unaokubalika kwamba hatuwezi kufanya maendeleo katika njia bila ya mwongozo. Tunashangaa madai ya Khalifa Umar kwamba, kwa vile tunayo Qur’ani kati yetu, hatuhitaji mwongozo wowote. Ni kama vile mtu akise- ma kwamba, kwa vile tunavyo vitabu vya madawa, basi hatuhitaji mganga.

Ni dhahiri kabisa utetezi huu ni wa uongo, kwa sababu mtu ambaye hawezi kutatutua tatizo lake kwa kusoma vitabu vya madawa, lazima amuone mganga kwa ushauri. Hali inakuwa hiyo hiyo katika suala la Qur’ani Tukufu. Kila mtu hawezi kupata faida kutoka kwenye Qur’ani Tukufu kwa uwezo wake mwenyewe. Lazima awaendee wale wenye elimu ya Qur’ani Tukufu.”

Qur’ani Tukufu inasema: “…Na lau kuwa wangelipeleka kwa Mtume na kwa wenye mamlaka kati yao, wale wanaochunguza wangelijua…” (4:83)

Kusema kweli kitabu halisi ni moyo wa mtu ambaye ana elimu, kama Qur’ani Tukufu inavyosema: “Bali hii (Qur’ani) ni Aya zilizo wazi katika vifua vya wale waliopewa elimu…” (29:49)

Kwa sababu hiyo Ali alisema: “Mimi ni Kitabu cha Allah kinachozungumza, na hii Qur’ani ni Kitabu kilicho kimya.” Hivyo kwa mujibu wa watu wenye elimu Umar alikosea. Ilikuwa ni dhulma kubwa kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wa Allah kwamba alizuiwa kuandika wosia wake.

Abu Bakr Hakuzuiwa Kuandika Wosia Wake

Amma kuhusu madai yako ya kurudia rudia kwamba Abu Bakr na Umar hawakuzuiwa kuandika wosia wao, nakiri kwamba ni kweli. Inashangaza, kwa vile wanahistoria na wanahadith wote wameandika katika vitabu vyao sahihi, kwamba Khalifa Abu Bakr, wakati wa kufariki kwake, alimuambia Uthman bin Affan aandike kile anachosema.

Ilikuwa ni wosia wake. Aliandika kila alichoambiwa na Abu Bakr. Umar na wengine vile vile walikuwepo katika tukio hilo. Hakuna aliyepinga. Umar hakusema: “Kitabu cha Allah kinatutosha sisi; hatuhitaji wosia wa Abu Bakr.” Lakini hakumruhusu Mtukufu Mtume wa Allah (s.a.w.w.) kuandika wosia wake.

Hii inaonesha kwamba tabia hii chafu na kumzuia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kuandika wosia wake haikuwa chochote bali ni njama za kisiasa.
Ibn Abbas alikuwa na haki kabisa ya kulia. Ulimwengu wote wa ki-Islamu unapaswa kutoa machozi ya damu. Kama Mtume angelipewa nafasi ya kuandika wosia wake, suala la ukhalifa lingetatuliwa kwa uwazi kabisa. Matangazo ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliyokuwa akiyatoa huko nyuma yangelithibitishwa. Lakini wanasiasa waliasi dhidi yake na kumzuia.

Sheikh: Kwanini unadai kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alitaka kusema kitu kuhusu ukhalifa?

Muombezi: Kabla ya kufariki kwa Mtume, sheria zote za dini zilikuwa zimewekwa wazi. Aya ya “Ukamilisho wa Dini” imelifanya hili kuwa wazi. Naam, kwa hakika suala la ukhalifa lilikuwa katika hali ambayo kwamba alitaka kuhakikisha kwamba kusingekuwa na utatanishi kuhusiana nalo.

Nilikwisha kuambieni kwamba Imamu Ghazali katika kitabu chake “Sirru’l-Alamin (Maqala ya 4) ameandika kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Nileteeni wino na karatasi ili niweze kuwaondolea mashaka yoyote mawazoni mwenu kuhusu ukhalifa na kwamba niweze kurudia kuwaambieni ni nani anastahiki cheo hicho.”

Maneno yake “Ili kwamba msije mkapotea baada yangu” yanathibitisha kwamba lengo la wosia wake lilikuwa ni mwongozo wa Umma. Katika suala la mwongozo, hakuna msisitizo uliohitajika isipokuwa katika kuhusiana na ukhalifa na uimamu.

Mbali na hili hatusisitizi nukta ya kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alitaka kusema kitu kuhusu huo ukhalifa au uimamu. Kwa hakika alitaka kuandika kitu kuhusiana na mwongozo wa watu ili kwamba wasije wakapotea baada yake. Basi kwa nini hakuruhusiwa kuandika wosia wake? Hata kama tukichukulia kwamba kumzuia kufanya hivyo ilikuwa sahihi, je ilikuwa ni lazima vile vile kumfedhehesha na kumtukana?

Hivyo Ni Wazi Kwamba Ali Alikuwa Mrithi Wa Mara Moja Wa

Mtukufu Mtume (S.A.W.W.)

Mambo haya yanafanya kuwa wazi kabisa kwamba Ali alikuwa mrithi wa mara moja wa Mtukufu Mtume wa Allah (s.a.w.w.). Ingawa Mtume alitangaza mara kwa mara jambo hili huko nyuma, alitaka katika hatua hii ya mwisho kuiandika katika wosia wake ili kwamba majukumu ya umma yaweze kuwa salama. Lakini wanasiasa walijua alichotaka kufanya kwa hiyo wakamzuia kufanya hivyo na wakamfedhehesha.

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) Mtume alisisitiza katika hadithi nyingi kwamba Allah (swt) aliteua waandamizi wa mitume: Adamu, Nuh, Musa, Isa na wengine, na kwamba alimteua Ali kama mwandamizi kwa jili yake. Vilevile alisema Ali ni mrithi na mwandamizi wangu wa mara moja baada yangu katika Ahlu’l-bayt na umma wangu.”

Sheikh: Kama riwaya hizi zitachukuliwa kuwa kweli, basi hazikusimuliwa kwa mwen- delezo kamili. Vipi utaweza kupata chanzo kutoka kwenye riwaya hizo?

Muombezi: Makubaliano ya maoni kuhusu wosia wa Mtume kwa mujibu wetu yanathibitishwa na maelezo ya kizazi kitukufu cha Mtume. Aidha, utakumbuka kwamba nilikuelezeni katika mikesha iliyopita kwamba maulamaa wenu huichukulia riwaya ya pekee kama sahihi. Mbali na hilo katika riwaya hizi, kama hakuna mapatano haswa ya maneno, basi kwa hakika kuna kupatana kwa maana ya jumla.

Hadithi Ya ‘La Nurith,’ Yakataliwa.

Mbali na hayo, unaambatanisha umuhimu usio na sababu kwenye mwendelezo wa riwaya (Mutawatir). Wakati unaponyamazishwa na hoja zetu, unakimbilia nyuma ya haja ya mutawatir. je unaweza kuthibitisha umutawatir wa hadithi ya “la nurith?” (hatuachi warithi)?

Wewe mwenyewe unakiri kwamba msimuliaji wa hadithi hii alikuwa ni Abu Bakr au Aus Bin Hadasan. Lakini mamilioni ya wana-tawhiid na Waislamu wanyofu katika kila zama wameikataa hii inayoitwa ati ni hadithi. Uthibitisho mzuri wa uwongo wa hadhithi hii, ni kwamba alikataliwa na lango la elimu ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), Ali na kizazi chote cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).
Watu hawa walidhibitisha kwamba hadithi hii ilikuwa ni ya kubuni. Kama nilivyokwisha sema awali, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Kwa kila Mtume kuna mwandamizi na mrithi, hakika Ali ni mwandamizi na mrithi wangu”

Ukhalifa Ni Mali Ya Mrithi Wa Elimu

Kama unasema kuwa urithi wao hakuwa na maana ya urithi wa mali bali ule wa elimu (ingawa imethibitishwa kwamba walimaanisha urithi wa mali) hoja yangu inakuwa dhahiri zaidi. Mrithi wa elimu wa Mtume alistahili cheo cha ukhalifa zaidi kuliko mtu yeyote kati ya wale ambao hawakuwa na elimu ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Pili, Imethibitisha kuwa Mtume alimfanya Ali kuwa mwandamizi na mrithi wake wa mara moja, kwa mujibu wa hadithi ilivyosimuliwa na maulanaa wenu wenyewe. Allah alimteua kwenye cheo hiki. Je,ingewezekana kweli Mtume kupuuza kumtaja mwandamizi na mrithi wake? Aidha inashangaza kwamba katika kutatua masuala yanayohusiana na sheria za dini, Abu Bakr na Umar walikubali uamuzi wa Ali. Maulana wenu wenyewe na wana historia wameziandika hukumu zilizotolewa na Ali wakati wa uhalifa wa Abu Bakri, Umar na Uthman.

Hafidh: Inashangaza sana kwamba unadai kuwa makhalifa hakujua sheria za dini na kwamba Ali alikuwa akiwakumbusha mara kwa mara.

Mwombezi: Hakuna cha kushangaza kuhusu hilo. Kuzijua zote zote ni vigumu sana. Isingewezekana kwa mtu kuwa na elimu kamilifu kama hiyo isipokua kama angekuwa ni Mtume wa Allah au lango la elimu ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Maulamaa wenu wenyewe wakubwa wamesimulia mambo haya kwenye vitabu vyao sahihi. Ninatoa mfano ili kwamba watu wasiojua wasije wakadhani tunasema mambo hayo ili kuwaudhi wao.

Hukumu Ya Ali Kuhusu Mwanamke Ambaye Alizaa Mtoto Baada Ya Ujauzito Wa Miezi Sita

Imamu Ahmad Hanbal katika Musnad yake; Imamul-Haram Ahmad bin Abdullah Shafi’i katika kitabu chake Dhakha’ir-e-Uqba; Ibn Abil-Hadid katika Sharh-e-Nahaju’l-Balagha; na Sheikh Suleiman Hanafi katika kitabu chake Yanabiu’l-Mawadda, sura 56, akinukuu kutoka kwa Ahmad Bin Abdullah; Ahmad bin Hanbal; Qala’i na Ibn Saman wanasimulia tukio lifuatalo:

Umar alitaka kumpiga mwanamke mawe kwa sababu alizaa mtoto baada ya ujauzito wa miezi sita. Ali akasema, “Allah anasema ndani ya Qur’ani tukufu kwamba ule muda, kuanzia kushika mimba, mpaka muda ulioagizwa wa kunyonyesha unachukua kipindi cha miezi thelathini. Kwa vile kipindi cha kunyonyesha ni miaka miwili, muda wa ujauzito ni miezi sita.” Hivyo Umar akamwachia huru yule mwanamke na akasema, ‘Kama Ali asingekuwepo hapa Umar angeangamia.’”

Katika sura hiyo hiyo ananukuu kutoka kwenye Manaqib ya Ahmad Bin Hanbali: “Wakati Umar anapokabiliwa na tatizo gumu na akawa hawezi kulielewa, alitegemea juu ya ujuzi wa Ali” Idadi ya matukio kama haya yalitokea wakati wa ukhalifa Abu Bakr na Uthman.

Wakati watakapotatazika katika matatizo fulani, walimwita Ali kama mwamuzi wa halali. Wao wenyewe walitenda kwa mujibu wa uamuzi wake. Sasa unaweza kushangaa kwa nini hawakuukubali ushahidiwa Ali katika suala la Fadak. Sasa katika suala lile walichagua kufuata matamanio yao na wakaipora haki ya Fatima.

Hadithi Ya ‘La Nurath,’ Haikutumika Kwenye Mali Nyingine

Hoja ya tatu kudhibitisha uwongo wa hadithi hii ni maelezo na kitendo cha Abu Bakr mwenyewe. Kama hadithi hii ingelikuwa sahihi vitu vyote ambavyo Mtume ameviacha vingekuwa vimetwaliwa. Na warithi wasingekuwa na haki katika vitu vyote alivyoviacha, lakini Abu Bakr alitoa nyumba ya Fatima na kumpa yeye (Fatima) na vilevile akatoa nyumba za wake za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na kuwapa Aisha, Hafsa na wengine kama urithi wao.

Kurudisha Abu Bakr Fadak Kwa Fatima Na Kuingilia Kati Kwa Umar.

Mbali na haya, kama hadithi hii ilikuwa sahihi na kama Abu Bakr aliamini kuwa ni amri ya Mtukufu, basi kwa nini, baada ya kuitwaa Fadak (ambayo aliichukulia kwamba ni sada- ka inayo wahusu Waislamu) aliandika hati kwamba mali hiyo irudishwe kwa fatima? Baadae Khalifa Umar aliingilia kati na kuichanachana hati ile.

Hafidhi: Haya n maelezo ya pekee. Sijawahi kusikia kwamba Khalifa aliirudisha Fadak. Ni kipi chanzo cha taarifa hii?

Muombezi: Mpaka sasa utakuwa unaelewa kwamba kamwe sifanyi madai yoyote ambayo siwezi kulitetea kwa ukamilifu. Ibn Abi’l Hadid katika Sharh-e-Nahju’l-Balagha na Ali Bin Burhanud-Din Shafi’i katika kitabu chake Ta’rikh Siratu-l-Halabiyya Jz. 3, uk. 391 anaandika kwamba Abu Bakr alitokwa na machozi kwa ajili ya hotuba ya Fatima yenye kutia hamasa.

Alilia kwa sababu ya masaibu ya Fatima na hatimaye aliandika hati akieleza kwamba mali hiyo inarudishwa kwake Fatima. Lakini Umar akaichana hati hati ile. Hata hivyo inashangaza zaidi kwamba Umar huyo huyo, ambaye wakati wa ukhalifa wa Abu Bakri alipinga kurudisha kwa Fadak, yeye aliirudisha kwa warithi wake wakati wa ukhalifa wake. Kadhalika makhalifa wa Amawi na Bani Abbas vilevile waliirudisha kwa warithi wa Fatimah.

Hafidhi: Unachosema kwa kweli kinashangaza. Inawezekana vipi kwamba Khalifa Umar, ambaye kwa mujibu wa maelezo yako, yeye alipinga vikali sana kurudishwa kwa Fadak kwa Fatima, leo aliirudisha kwa warithi wa Fatima?

Muombozi: Kwa hakika inashangaza mno. Nawasilisha kwa ruhusa yako, riwaya za ulamaa wenu wenye sifa kutoka kwa makhalifa ambao waliirudisha na kuichukua tena Fadak.

Kurudisha Fadak Kwa Khalifa Kwa Kizazi Cha Fatimah

Mwanahadithi na mwanahistoria ajulikanaye sana wa Madina, Allama Samhudi (alikufa 911A.H.) katika kitabu chake “Ta’rikhu’l-Madina” na Jaqut Bin Abdullah Rumi katika kitabu chake Mu’ajamul-Buldan, wanaeleza kuwa wakati wa ukhalifa wake, Abu Bakri alichukua umiliki wa Fadak. Umari wakati wa utawala wake akairuidisha kwa Ali na Abbas.

Kama Abu Bakr aliihodhi kwa amri ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na akachukulia kama ni mali ya Waislam,
ni kwa kanuni ipi ambayo Umari aliaminisha mali ya Waislamu wote kwa mtu mmoja binafsi?

Sheikh: Pengine nia yake katika kuitoa mali hiyo kwa mtu binafsi, ilikuwa kwamba itabakia katika hifadhi ya Waislamu.

Muombezi: Wakati mwingine shahidi anakuwa mwereru zaidi kuliko mdaiwa ambaye anamtolea ushahidi. Khalifa hukuwa na mawazo kama hayo. Kama mali hiyo ilirudishwa kwa ajili ya matumizi Waislamu, ingeandikwa hivyo katika historia. Lakini wanahistoria wenu wakubwa wanaandika kuwa ilitoewa kwa manufaa ya Ali na Abbas. Ali alipokea Fadak kama mrithi wake wa haki, sio kama Mwislamu binafsi. Mwislamu mmoja hawezi kumiliki mali ya Waislamu wote.

Kurudishwa Fadak Na Umar Ibn Abdul-Aziz

Sheikh: Pengine rejea hiyo ni kwa Umar Ibn Abdul-Aziz.

Muombezi: Ali na Abbas hawakuwa hai wakati wa Umar Ibn Abdu’l-Aziz. Hiyo ni hadithi nyingine tofauti. Allama Samhudi katika kitabu chake Ta’rikhul-Madina na Ibn Abil-Hadid katika kitabu chake Sharh-e-Nahju’l-Balagha, Jz. 4, uk. 81, anasimulia kutoka kwa Abu Bakr Jauhari kwamba wakati Umar Bin Abdu’l-Aziz alipochukuwa nafasi ya ukhalifa alimwandikia Gavana wake wa Madina kurudisha Fadak kwa kizazi cha Fatima.
Kwa hiyo alimwita Hasan bin Hasanu’l-Mujtaba (na kulinga na riwaya nyingine alimuita Imam Ali Ibnu’l-Husein) na akairudisha fadak kwake. Ibn Abi’l-Hadid anaandika kuhusu hili katika kitabu chake Sharh-e-Nahju’l-Balagha, Jz. 4, uk. 81 katika maneno yafuatayo:

“Hii ilikuwa mali ya kwanza ambayo iliporwa kinyume cha sheria na kisha ilitolewa na kupe- wa kizazi cha Fatima na Umar Bin Abdu’l-Aziz.” Ilibakia katika miliki yao kwa muda mrefu mpaka Khalifa Yazid Ibn Abdu’l-Malik alipoipora tena. Kisha Bani Umayya wakaikalia. Wakati ukhalifa ulipokwenda kwa Bani Abbas, Khalifa wa kwanza wa Bani Abbas, Abdullah Saffa, alitoa Fadak kwa watoto wa Imam Hasan ambao waligawanya mapato yake kwa mujibu wa haki za urithi, kwa kizazi cha Fatima.

Kurudishwa Fadak Kwa Kizazi Cha Fatima Na Abdullah Mahdi Na

Mamun Bani Abbas

Wakati Mansur alipowatesa watoto wa Imam Hasan, aliipora Fadak kutoka kwao tena. Wakati mwanae Mahdi alipokuwa Khalifa, aliirudisha tena kwao. Wakati Musa bin Hadi alipokuwa Khalifa aliipora tena Fadak. Mamunu’r-Rashidi wa Bani Abbas alipokichukua kiti cha ukhalifa aliagiza Fadak kutoewa kwa kizazi cha Ali. Yaqut Hamawi ananukuu maagizo ya Mamun katika kitabu chake Mamun katika kitabu chake Mu’ajamu’l Buldan.” Mamun aliandika kwa Gavana wake wa Madina: “Hakika, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wa Allah aliitoa Fadak kwa binti yake Fatima. Ukweli huu umethibitishwa na kujulikana wazi kwa kizazi cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).”

Mshairi ajulikanae sana, Di’bal Khuza’i, alikuwepo pia wakati huo. Alisoma baadhi ya mashairi, la kwanza ambalo likiwa na maana: “Leo wote tunayo furaha na shangwe. Mamum amerudisha fadak kwa Bani Hashim.”

Uthibitisho Kwamba Fadak Ilitolewa Kwa Fatima

Imimethibitishwa na hoja zisizokanushika kwamba Fadak ilitolewa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kumpa Fatima. Iliporwa bila haki yoyote. Lakini makhalifa wa baadae, katika misingi ya uadilifu au mitazamo ya kisiasa waliirudisha kwa kizazi cha Bibi yule aliyeonewa.

Hafidh: Kama Fadak ilitolewa kwake kama zawadi, kwa nini aliidai kama urithi na asiseme chohote kuhusu zawadi?

Muombezi: Kwanza aliidai kama zawadi. Lakini mashahidi walipohitajika kutoka kwa mmiliki wa mali, kinyume na mafundisho ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wa Uislamu, alitoa mashahidi. Ushahidi wao ulikataliwa. Hivyo alilazimika kutafuta kinga chini ya sheria ya mirathi.

Hafidhi: Nina wasiwasi umekosea. Hatujaona kumbukukmbu yoyote ya madai ya Fatimah kwamba Fadak ilikuwa zawadi.

Muombezi: La, sijakosea. Jambo hili halikusimuliwa kwenye vitabu vya Shi’a tu, bali pia katika vile vilivyoandikwa na maulama wenu wakubwa. Imeandikwa katika Siratu’l- Halabiyya, uk. 39, kilichokusanywa na Ali Bin Burhanud-Din Halabi Shafi’i (amekufa 1044 A.H) kwamba kwanza Fatima alipingana na Abu Bakr kwamba yeye (Fatima) alimiliki Fadak na kwamba yeye alipewa na Mtukufu Mtume wa Allah (s.a.w.w.). Kwa vile ushahidi ulikataliwa alilazimika kudai haki yake kwa mujibu wa sheria za mirathi. vilevile Fakhru’d-din Razi katika “Tafsiri-e-Kabir” kuhusu madai ya Fatimah; Yaqut Hamwani katika kitabu chake Mu’ajamu’l-Buldan; Ibn Abi’l-Hadid Mu’tazali katika Sharh-e- Nahjul-Balagha, Jz. 4, uk. 80, kutoka kwa Abu Bakr Jauhari na yule shupavu Ibn Hajar katika Sawa’iq-e-Muhriqa, uk. 21, chini ya kichwa cha maneno Shuhubhati-e-Rafza, Shubha ya 7, anasimulia kwamba dai la kwanza la Fatimah lilikuwa kwamba Fadak ilikuwa zawadi. Wakati mashahidi wake walipokataliwa aliudhika sana na akasema kwa hasira kwamba hatazungumza tena na Abu Bakr na Umar.

Na hivyo ndivyo ilivyokuwa - hakuwaona tena na wala hakusema nao. Wakati wa kifo chake ulipokaribia alielezea bayana katika wosia wake kwamba asihudhurie hata mmoja wao katika sala yake ya jeneza. Ami yake Abbas, aliendesha ibada ya mazishi, na akazik- wa usiku. Kwa mujibu wa vyanzo vya Shi’a na kwa mujibu wa maelezo ya Maimam watukufu, Ali ndiye aliendesha ibada ya mazishi.

Hoja Kwamba Abu Bakr Alitenda Kwa Mujibu Wa “Aya Ya Ushahidi”

Na Majibu Yake.

Hafidhi: Naam kwa kweli hapana shaka kwamba Fatimah alikasirika sana, lakini Abu Bakr Siddiq si wakulaumiwa sana. Aliwajibika kutenda kwa mujibu wa sheria za kidini zilizowazi. Kwa vile “aya ya ushahidi” ni ya umuhimu wa jumla, na mdai lazima alete wanaume wawili au mwanaume mmoja na wanawake wawili au wanawake wanne kama mashahidi, na kwa vile katika suala hili idadi ya mashadi ilikuwa haitoshi, Khalifa asingeweza kutoa hukumu inayompendelea Fatima.

Muombezi: Hafidhi Sahib amesema kwamba Khalifa aliwajibika kutenda kwa mujibu wa sheria za dini, na kwa vile ushaidi kamili haukupatikana hakuweza kutoa hukumu. Nitajibu nukta hii, na naomba ninyi muwe waadilifu katika kupima kauli yangu.

Kudai Mashahidi Kutoka Kwa Wamiliki Ilikuwa Ni Kinyume Cha Sheria

Kwanza ulisema Abu Bakr ‘alilazimika chini ya sheria za kidini.’ Unaweza tafadhali ukaniambia ni amri ipi ya dini inayohitaji mashahidi kutoka kwa mtu ambaye amiliki mali? Imethibitishwa kwamba Fatimah alikuwa katika umiliki wa Fadak.

Kama ilivyoelezwa na maulamaa wenu wote, kuhitaji mashahidi kwa Abu Bakr kutoka kwa Fatima ilikuwa kinyume cha sheria za dini. Je, sheria zetu za dini hazisemi kwamba ushahidi lazima utolewe na mlalamikaji na sio yule mwenye kushikilia mali? Pili, hakuna anayekataa ile maana ya jumla ya aya ya ushahidi, lakini pia ina maana makhususi.

Hafidh: Una maanisha nini kwa maana yake makhususi?

Muombezi: Ushahidi wa hili ni riwaya iliyoandikwa katika vitabu vyenu sahihi vya hadithi, kuhusiana na Khazima Ibn Thabit. Alitoa ushahidi katika kumuunga mkono Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) katika kesi inayohusiana na uuzaji wa farasi. Mwarabu mmoja alitoa madai dhidi ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na ushahidi wake (Khazima) wa pekee ulichukuliwa kama wa kutosha. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akampa jina (lakabu) la Dhu’sh-Shahadatain kwa sababu alichukuliwa kama aliye sawa na mashahidi wawili waadilifu. Mfano huu unaonesha kwamba ‘Aya ya Ushahidi’ inaruhusu hali ya kipekee katika mazingira fulani.

Wakati Khazima, muumini mmoja binafsi na sahaba kutoka mion- goni mwa umma, alifanywa wa kipekee kwenye Aya hiyo, Ali na Fatima ambao walikuwa Ma’asum kwa mujibu wa ‘Aya ya utakaso’ walikuwa katika nafasi nzuri zaidi kufaidi upendeleo huu wa kipekee. Kwa hakika wao walikuwa mbali kutokana na uwongo wa aina yoyote. Kukataa ushahidi wao ilikuwa ni kukataa ushahidi wa Allah swt.

Kukataa Mashahidi Wa Fatima Ilikuwa Ni Kinyume Na Sheria Ya Kidini

Hadhrat Fatima alidai kwamba Fadak ilitolewa kwake kama zawadi na baba yake na kwamba ilikuwa katika miliki na usimamizi wake wakati wa uhai wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Alitakiwa kutoa mashahidi. Alimtoa Amirul-Mu’uminin Ali Bin Abi Talib na Hasan na Husein kama mashahidi wake.

Lakini ushahidi wao ulikataliwa. Je, kitendo hiki hakikuwa cha kidhalimu? Haieleweki ni kwa vipi mtu yeyote aweze kukataa ushahidi wa Ali. Allah katika Qur’ani Tukufu anasema lazima tuwe na Ali, yaani, lazima tumfuate yeye. Zaid-e-Adl alikuwa mfano halisi wa ukweli kwa sababu ya ukweli wake uliozidi mno.

Halikadhalika, Ali aliitwa ‘mkweli’ kwani Allah anavyosema: “Enyi mlioamini! Mcheni Allah na kuwenu pamoja na wakweli.” (9:119) Neno ‘Wakweli’ hurejea kwa Mtume Muhammad, Ali na Ahlu’l-Bayt watukufu.

‘Wakweli’ Inaashiria Kwa Mtume Muhammad Na Ali

Hafidh: Ayah hii inathibitisha vipi maoni yako, ambayo yangemaanisha kwamba kumfu- ata Ali ni wajibu kwetu?
Muombezi: (1) Wanachuoni wenu maarufu wameandika katika vitabu na tafsiri zao kwamba Aya hii iliteremshwa kwa kumsifia Muhammad na Ali. ‘Wakweli’ hurejea kwa watu hawa wawili watukufu, na kwa mujibu wa riwaya nyingine linamaanisha Ali; riwaya nyingine zinasema kwamba hurejea kwa kizazi cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Imam Tha’labi katika tafsir yake Kashfu’l-Bayan, Jalalu’d-Din Suyuti akisimulia kutoka kwa Ibn Abbas katika kitabu chake Durru’l-Manthur, Hafidh Abu Sa’id Abdu’l-Malik Bin Muhammad Khargushi akisimulia kutoka kwa Asma’is katika Sharafu’l-Mustafa, na Hafidh Abu Nu’aim Ispahani katika kitabu chake Hilyatu’l-Auliya anasimulia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Hawa wakweli ni Muhammad na Ali.”

Sheikh Sulayman Hanafi katika Yanabiu’l-Mawadda, sura ya 39, uk. 1191, akisimulia kutoka kwa Muwaffaq Bin Ahmad Khawarizmi, Hafidh Abu Nu’aim Ispahani, na Hamwaini wakisimulia kutoka kwa ibn Abbas, ambaye alisema: “Katika Aya hii ‘wakweli’ ni Muhammad na kizazi chake.”

Na Sheikhu’l-Islam Ibrahim Bin Muhammad Bin Hamwaini, mmoja wa wanachuoni wenu mashuhuri, katika kitabu chake Fara’idus-Simtain, Muhammad Bin Yusuf Ganji Shafi’i katika Kifayatut-Talib, sura ya 62, na Muhadith Sham katika Ta’rikh yake, akisimulia kutoka kwenye vyanzo vyake anaandika: “Pamoja na wa kweli, yaani, ni pamoja na Ali Bin Abi Talib.”

(2) Allah anasema:

وَالَّذِي جَاءَ بِالصِّدْقِ وَصَدَّقَ بِهِ ۙ أُولَٰئِكَ هُمُ الْمُتَّقُونَ {33}

“Na yule ambaye aliyeleta ukweli, na yule aliyeusadikisha kama, hao ndio wamchao (Mwenyezi Mungu).” (39:33)

Jalalu’d-din Suyuti katika Durru’l-Manthur, Hafidh Ibn Mardawiyya katika Manaqib, Hafidh Abu Nu’aim katika Hilyatu’l-Auliya, Muhammad ibn Yusuf Ganji Shafi’i katika Kifayatut-Talib, sura ya 62, na Ibn Asakir katika Ta’rikh yake, akisimulia kutoka kwenye vitabu mbali mbali vya wafasiri, anasimulia yafuatayo kutoka kwa Ibn Abbas na Mujahid: “Yule anayeleta ukweli ni Muhammad, na yule ambaye anauthibitisha ni Ali Bin Abi Talib.”

(3) Allah anasema katika Sura ya al-Hadid (chuma) ya Qur’ani Tukufu: “Na (kwa) wale waliomuamini Allah na Mtume Wake, hao ndio Masidiki na Mashahidi mbele ya Mola wao; watapata malipo yao na nuru yao…” (57:19)

Imam Ahmad Hanbal katika “Musnad”na Hafidhi Abu Nu’aim Ispahan katika “Manazil Mina’l-Qur’ani fi Ali” anasimulia kutoka kwa Ibn Abbas kwamba Aya hii tukufu iliteremshwa katika kumsifia Ali ikimtaja kama aliye ni miongoni mwa wakweli.

(4) katika Suratun-Nisa (wanawake) Allah anasema: “Na wenye kumtii Allah na Mtume Wake, basi hao watakuwa pamoja na wale aliowaneemesha Allah miongoni mwa manabii na masidiki na mashahidi na watu wema, na hao ndio marafiki wema.” (4:69) Katika aya hii vilevile wakweli inaashiria kwa Ali.

Kuna hadithi nyingi zilizosimuliwa na maulamaa wetu na wenu, zikionesha kwamba Ali alikuwa ndiye mkweli wa umma na kwa kweli ndiye aliyetukuka mno miongoni mwa wakweli.

Ali Ametukuka Zaidi Miongoni Mwa Wakweli (Masidiq)

Wengi wa maulamaa wenu wakubwa wameandika katika vitabu vyao kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Kuna masidiki wakubwa watatu - Hiziqil, yule Mu’mini wa watu wa Firauni, Habibu Najjar wa Suratal-Yasin, na Ali Bin Abi Talib ambaye ni mbora wa wote.”

Wameandika hadithi hii hawa wafuatao wote: Imamu Fakhru’d-Din Razi katika Tafsiri Kabir: Imam Tha’labi katika Kashfu’l-Bayani; Jalalud-Din Suyuti ndani ya Durru’l-Manthur; Imam Ahmad bin Hanbal katika Musnad; Ibn Shirwaih katika Firdaus; Ibn Abi’l-Hadid katika Sharh-e-Nahju’l-Balagha, Jz. 2, uk. 451; Ibn Maghazil Shafi’i kati- ka Manaqib; na Ibn Hajar Makki katika Sawaiq-e-Muhriqa (hadithi 30 kati ya hadithi 40 ambazo amefafanua juu ya ubora wa Ali) akinukuu kutoka Bukhari ambaye anasimulia kutoka kwa Ibn Abbasi, isipokuwa kifungu cha mwisho.

Vilevile Sheikh Suleiman Balkhi katika “Yanabiu’l-Mawadda” sura ya 42, akinukuu kuto- ka Musnad ya Imam Hanbal; Abu Nu’aim Ibn Maghazili Shafii; yule msemaji mkubwa Khwarizmi, akinukuu kutoka kwa Abu Laila na Abu Ayyub Ansari, katika Manaqib yake, Ibn Hajar katika Sawai’q (na kundi la wengine) anasilia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema:

“Kuna Masidiki watatu - Habib Najjar, yule Mu’umin wa Sura ya Yasini ambaye alisema: ‘Enyi watu! Wafuateni Mitume;’ Hizqil, Muumini wa watu wa Firauni ambaye alisema “Je, mnamuua mtu ambaye anamuabudu Allah? na Ali Ibn Abi Talib ambaye ndiye mbora zaidi wa wote hao.”

Watu wanashangaa kuona jinsi uwelewa wako unavyokandamizwa na ukaidi wako. Ninyi wenyewe mnathibitisha kwa hadithi mbali mbali zenye kuafikiana na Qur’ani Tukufu kwamba, Ali alishikilia cheo cha juu miongoni mwa watu wakweli (Siddiq) na bado mnawaita watu wengine Siddiq ingawa hakuna hata aya moja ambayo imesimuliwa kuhusu kuwa kwao wakweli (masidiq).

Enyi waungwana! tafadhalini kuweni waadilifu. Hivi ilikuwa ni sahihi kuukataa ushahidi wa mtu ambaye Allah anamwita ‘Sidiq’ ndani ya Qur’ani, ambaye sisi tumeamriwa kumfuata?

Ali Yuko Pamoja Na Haki Na Quran.

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Ali yuko siku zote pamoja na haki na haki inamzunguka Ali.” Khatibu Baghdad katika kitabu chake “Ta’rikh,” Jz. 4, uk. 321, Hafidhi Ibn Mardawiyya katika ‘Manaqib,’ Imam Ahmad Bin Hanbal katika Musnad, Fakhru’d-Din Razi katika Tafsiri-e-Kabir, Jz. 1, uk. 111, Ibn Hajar Makki katika Jam’us-Saghir, Jz. uk. 74, 75, 140 na Sawa’iq-e-Muhriqa sura ya 9, Fasli ya 2, Hadith ya ishirini na moja akisimulia kutoka Ummi Salama na Ibn Abbas vilevile katika Yanabiu’l-Mawadda, Sura ya 65 uk. 185, akichukua kutoka “Jam’us-Saghir” ya Jalalu’d-Din Suyuti, kwa nyongeza katika “Tarikhu’l-Khulafa” uk. 116, Faidhu’l-Qadir, Jz. 4, uk. 358 akisimulia kutoka kwa Ibn Abbas, “Manaqibus-Sab’in,” uk. 237, hadithi ya 44 akinukuu kutoka kwa mwandishi wa Firdaus; Sawa’iq-e-Muhriqa, sura 59, sehemu ya 2, uk. 238, akisimulia kutoka kwa Ummi Salama na Muhammad Bin Yusufu Ganji Shafi’i katika Kifayatut-Talib, baadhi yao wakisimulia kutoka kwa Umm Salama, wengine kutoka Aisha, na wengine kutoka kwa Muhammad Bin Abu Bakr wote wanasimulia kwamba wamemsikia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akisema:

“Ali yuko pamoja na Qur’ani na Qur’ani ipo pmoja na Ali; kamwe hakutakuwa na tofauti kati ya viwili hivyo, na viwili hivyo havitatengana vyenyewe mpaka vinifikie kwenye hodhi ya Kauthar.”

Baadhi ya wapokezi wamesimulia maneno haya: “Haki wakati wote iko pamoja na Ali na yeye Ali wakati wote yupo pamoja na haki. Hakutakuwa na tofauti kati ya viwili hivyo, navyo viwili hivi havitatengana.”

Ibn Hajar anaandika katika Sawa’iq-e-Muhriqa, Sura ya 9 sehemu ya 2, uk. 77, kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) juu ya kitanda chake alichofia, alisema: “Ninakuachieni baada yangu vitu viwili. Kitabu cha Alla pamoja na kizazi changu, Ahlu’l-Bayt wangu.”

Kisha wakati huku akiwa ameushika mkono Ali, aliunyanyua juu na akasema: “Huyu Ali yuko pamoja na Qur’ani an Qur’ani iko pamoja na Ali. Viwili hivi havitatengana mpaka vinifikie kwenye hodhi ya Kauthar. Kisha nitakiuliza kila kimoja chao kuhusu suala la uandamizi (Urithi),”

Vile vile imesimuliwa kiujumla kwamba Mtume alisema: “Ali yuko pamoja na haki na haki siku zote iko na Ali. Huzungukana wenyewe kwa wenyewe.” Sibt Ibn Jauzi, katika Tadhkrat-e-Khawasu’l-Umma, uk. 20, anasimulia kuhusiana na ‘Hadith-e-Ghadir’ kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Haki imfuate Ali, katika upande wowote atakaokwenda.”

Sibt ibn Jauz akitoa maoni kuhusiana na hili anasema: “Hadithi inathibit- sha kwamba kama kuna tofauti yeyote kati ya Ali na Sahaba yeyote mwingine, basi haki itakuwa pamoja na Ali.”

Utii Kwa Ali Ni Utii Kwa Allah Na Mtume Wake Mtukufu

Imeandikwa katika vitabu ambavyo vimetajwa na katika vitabu vyenu vingine sahihi kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mara kwa mara alisema: “Yeyote ambaye anamtii Ali hakika ananitii mimi. Na yeyote anayenitii mimi, hakika anamtii Allah. Yule ambae hamtii Ali hakika hanitii mimi, na yule ambaye hanitii mimi hakika hamtii Allah.”

Abu’l-Fat’h Muhammad Bin Abdu’l-Karim Shahrastani anaandika katia kitabu chake “Milal-wa-Nihal” kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Ukweli ni kwamba Ali siku zote yuko juu ya haki, na wale wanaomfuata yeye wako juu ya haki.”

Pamoja na riwaya zote hizi za wazi, ambazo zimeandikwa katika vitabu vyenu wenyewe sahihi, je, si kweli kwamba kukataa kukubaliana na Ali kulikuwa ni sawa na kukataa kukubaliana na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)?”

Khalifa Abu Bakr Hakufuata Sheria Ya Ushahidi Katika Kesi Nyingine.

Hoja ya pili ambayo umeileta ni kwamba Khalifa alilazimika kutenda kwa mujibu wa mtazamo wa nje wa kanuni ya dini kwa vile “aya ya ushahidi” katika maana yake ya kijumla ilitumika katika suala hili.

Kwa hiyo, kwa kutokuwepo kwa mashahidi, asingeweza kutoa “mali ya Waislamu” kumpa Fatima, kwa msingi wa madai yake peke yake. Bali alikuwa na tahadhari sana kwamba alidai, kinyume cha sheria ya kidini, mashahidi kutoka kwa mmiliki haswa wa mali hiyo.

Kwanza nilikwisha kuwelezeni kwamba Fadak haikuwa Mali ya Waislamu. Alipewa Fatima na baba yake kama zawadi na kushikiliwa kiumiliki na yeye.

Pili, kama kweli khalifa alitaka kufuata sheria ya dini, basi angeifuata hasa katika masula yote. Kwa nini alifuata sera ya undumilakuwili? Alizoea kutoa mali ya Waislamu kwa wengine kwa kukubali tu madai ya mdomo bila kuchukua ushahidi wa shahidi yeyote. Lakini katika suala la mali ya Fatima alichukua tahadhari isiyokuwa ya kawaida.

Ibn abi’l -Hadid ameandika katika Sharh-e-Nahju’l-Balagha, Jz. 4, uk. 25, kwamba alimuuliza Ali ibnul-Fariqi, mwalimu katika Madrasa ya Gharbi huko Baghdad, iwapo Fatima alikuwa katika haki na alizungimza ukweli kuhusu madai yake. Alisema: ‘Ndio?’ Nikasema: ‘Kama alikuwa na haki na alisema kweli, kwa nini Khalifa hakurudisha Fadak kwake? Yeye (Fariqi) alitabasamu (ingawa kamwe hajafanya utani) na akasema kwamba kama angeirudisha Fadak kwa Fatima siku ile, kesho yake angelikuja kudai ukhalifa kwa ajili ya mumewe.

Halafu Khalifa angelazimika kurudisha haki ile vile vile, kwa vile angekuwa amekwishakubali ukweli wake katika suala liliopita.

Kwa mujibu wa wanachuoni wenu wakubwa, hali ilikuwa wazi kabisa. Walikuwa wamekubali ukweli kwamba kuanzia siku ya kwanza haki ilikuwa pamoja na muonewa Fatimah, lakini manufaa yao ya kisiasa yalihitaji kwamba lazima wamnyime bibi huyu asiye na hatia haki yake.

Abu Bakr Atoa Mali Kwa Jabir Bila Ya Kuita Mashahidi

Hafidhi: Ni lini ambapo Khalifa alitoa mali ya Waislamu bila shahidi yeyote?

Muombezi: Wakati Jabir alipodai kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa amemuahi- di kwamba atalipwa kutokana na ngawira aliyochukuliwa kutoka Bahrain, alipewa dinar 1500 kutoka Baitul-Mal (Hazina ya Umma) bila ya kuleta kikwazo au kutaka shahidi yeyote kutoka kwake.

Hafidhi: Kwanza sijaona riwaya kama hiyo. Pengine ipo kwenye vitabu vyenu. Pia utawezaje kudai kwamba mashahidi hawakuhitajiwa?
Muombezi: Ni ajabu kwamba hakuiona riwaya hii. Riwaya hii ya Jabir bin Abdullah Ansari ni moja ya hoja za maulamaa katika kuunga mkono maoni yao kwamba riwaya ya pekee ya sahaba muadilifu inakubalika.

Kwa sababu hiyo, Sheikhu’l-Islam Hafiz Abdu’l-Fazl Ahmad Bin Ali bin Hajar Asqalani anasema katika kitabu chake Fathu’l-Bari Fi Sharh-e-Sahihu’l-Bukhari: Riwaya hii inathibitisha kwamba simulizi ya sahaba mwadilifu inakubaliwa hata ingawa inamnufaisha yeye mwenyewe binafsi, kwa sababu Abu Bakr hakutaka shahidi kutoka kwa Jabir katika kuunga mkono madai yake.

Bukhari anaandika taarifa hiyo katika maelezo marefu mno katika Sahih yake. Katika mlango wa ‘Man Yakfal un mayyit dainan’ na na Kitabu’l- Khuma fi Bab-e-ma Qata an-Nabi mina’l Bahrain,’ anaandika kwamba wakati ngawira ya Bahrain ilipoletwa Madina, Abu Bakr alitangaza kwamba yeyote yule ambaye aliahidiwa pesa na Mtume wa Allah au yeyote ambaye ana madai ambayo hayajatoshezwa aje apokee haki yake. Jabir alikuja na akasema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliniahidi kwamba wakati Bahrain itakaposhindwa na kuwa chini ya usimamizi wa Waislamu, nitapewa zawadi kuto- ka kwenye ngawira hiyo.

Hivyo mara moja Abu Bakri alimpa dinnar 1,500 bila ya kuitisha ushahidi wewote, juu ya msingi tu wa madai yake. Jalalud-Din Suyuti vile vile ameandika tukio hili katika kitabu chake “Ta’rikhu’l-Khulafa” katika sehemu juu ya ukahlifa wa Abu Bakr.

Enyi watu waadilifu: Tafadhali nakuombeni mnifahamishe kwa jina la Allah kama huu haukuwa utovu wa uadilifu. Isipokuwa kama kulikuwepo na chuki fulani ikifanya kazi, vipi ilikuwa halali kwa Abu Bakr kuihalifu “aya ya ushahidi” na kumpa Jabir pesa juu ya msingi wa madai yake peke yake? Mbali na hili, Bukhari katika Sahih yake na wengine wengi kati ya maulamaa na wanachuoni wenu wa sheria, wanakubali ushahidi mmoja wa sahaba muadilifu hata kama unatoa manufaa binafsi kwake mwenyewe.

Lakini wanayaona madai ya Ali kwamba hayakubaliki kwa misingi kwamba alitaka kitu kwa manufaa yake mwenyewe. Je, Ali hakuwa mtu mkamilifu miongoni mwa masahaba? Kama mtaliangalia suala hili kwa uadilifu mtakubali kwamba haikuwa tu unyimaji wa haki, bali yote yalikuwa ni mabavu na hila iliyowazi.

Hafidhi: Na fikiri Abu Bakr hakuhitaji mashahidi kutoka kwa Jabir kwa sababu alikuwa mmoja wa wale Masahaba waliofundishwa kwa karibu na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Kwa hakika amemsikia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akisema: “Kama mtu yeyote akitoa maelezo ya uwongo kuhusu mimi makazi yake yatakuwa motoni.” Akifahamu onyo hili kali, ni wazi kabisa kwamba Sahaba aliyefundishwa kwa karibu na muumini, asingeweza kuchukua hatua ya kimakosa kama hilo na asingeweza kuhusisha maelezo ya uwongo kwa Mtume wa Allah.

Muombezi: Je, Jabir alikuwa karibu na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) au Ali na Fatima, ambao walifundishwa maalum na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)?

Ali Na Fatima Walikuwa Wahusika Wa Aya Ya Utakaso

Hafidhi: Ni wazi kwamba Ali na Fatima walikuwa karibu zaidi na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wa Allhah, kwa sababu walikuwa chini ya mafundisho yake kuanzia kuzaliwa kwao hasa.

Muombezi: Hivyo itakubidi kukubali kwamba Ali na Fatima lazima walikuwa wafuasi makini wa onyo hili na wasingeweza kwa msingi wa hadith ya Mtume, kufanya madai yoyote ya uwongo.

Na ni wajibu juu ya Abu Bakr kukubali madai ya Fatima kwa vile cheo cha watu wote hawa wawili kilikuwa juu zaidi sana kuliko cha Jabir (kama ambavyo mwenyewe unakiri). Kwa kweli cheo chao kilikuwa cha juu zaidi kwa Masahaba wote wengine. Walikuwa wastahiki wa “Aya ya Utakaso” na walikuwa watu ma’sum.

Aya hii inadhihirisha utohara wa watu watano hawa watukufu: Muhammad, Ali, Fatimah, Hasani na Huseini. Kwa kweli maulamaa wenu wakubwa vile vile wameshuhudia ukweli wa watu hawa watukufu.

Ama kuhusu Amiru’l-Muminin, nimekwisha kukuambieni kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimuita ‘Mtu Mkweli wa Umma wote,’ na Allah vile vile amemuita ‘mkweli’ katika Qur’ani Tukufu.
Kuhusu ukweli wa Fatimah Zahra, vile vile kuna hadithi nyingi za namna hiyo. Miongoni mwao ni iliyosimuliwa na Hafiz Abu Nu’aim Ispahani katika kitabu chake “Hilyatu’l-Auliya,” Jz. 2, uk. 42, kutoka kwa Aisha ambaye alisema: “Sijamuona mtu yeyote mkweli zaidi kuliko Fatimah isipokuwa baba yake.”

Hafidhi: Madai yako kwamba aya hii imeshuka kwa kuwasifia watu wale watano hayawezi kukubalika. Katika midahalo hii umeonesha ujuzi mkubwa kuhusu vitabu vyetu.

Unapaswa kukubali kwamba katika suala hili umekosea, kwa vile wafasiri kama Kadhi Baidhawi na Zamakhshari wanaamini kwamba aya hii tukufu iliteremshwa kwa kuwasifia wake za Mtume. Na kama kuna riwaya yoyote isemayo kwamba iliteremshwa kwa kuwasifia watu wale watano, basi itakuwa ni dhaifu. Sababu ni kwamba aya yenyewe kama ilivyo inajithibitisha kinyume na maana hiyo. Muktadha wa “Aya ya Utakaso” umeunganishwa na wake (wa Mtume) na sehemu ya kati haiwezi kuondolewa kwenye muktadha huo.

Kuthibitisha Kwamba Aya Ya Utakaso Haikuwa Kwa Kuwasifia Wake Za Mtume.

Muombezi: Dai lililoletwa na wewe linakanushika katika mitazamo mingi. Umesema kwamba sehemu ambazo zimetangulia na zinazofuatia zimehusishwa na wake za Mtume, na hivyo Ahlul’l-Bayt wameondolewa katika aya hii tukufu. Najibu hivi kwamba, kama inavyotokea mara kwa mara katika mazungumzo yetu, tunahamisha nadhari yetu kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine na kisha kurudi kwa mtu yule wa kwanza.

Kuna mifano mingi kuhusu suala hili katika mashairi ya waandishi wakubwa na washairi wa Kiarabu. Katika Qur’ani Tukufu yenyewe kuna mifano mingi ya aina hii. Kwa kweli, kama utachunguza sura iliyoko kwenye mjadala, al-Ahzab baada ya kuhutubia wake za Mtume, nadhari inahamishwa kwa waumini.Kisha mwishowe, wake za Mtume wanahutubiwa. Muda hauniruhusu kuwasilisha ushahidi uliofafanuliwa zaidi kuelezea nukta hii zaidi.

Pili, kama aya hii ilikuwa inahusu wake za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), vijina vilivyotumi- wa ndani yake vyingelikuwa vya kike. Lakini kwa vile vijina vyilivyotumika ni vya kiume, tunajua kwamba kuashiria huko sio kwa ajili ya wake za Mtume, bali kwa kizazi cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Nawab: Kama Fatimah vile vile amejumuishwa katika kundi hili kwa nini dhamiri ya kike haikutumika?

Muombezi: (Akiwageukia maulamaa) Mabwana: mnajua kwamba aya hii, ingawa Fatimah ni mmoja wa wanaotajwa, dhamiri ya kiume inatumika kwa sababu ya wingi wa wanaume. Yaani katika kundi la wanaume na wanawake, uzito zaidi unawekwa kwa wanaume.

Katika aya hii utumiaji wa dhamiri ya kiume wenyewe ni uthibitisho kwamba maelezo haya sio dhaifu, bali yana nguvu kamili. Mbali na hili, kwa kuangalia wingi wa jamaa wa kiume, kijina lazima kiwe katika dhamiri ya kiume kwa sababu katika Watukufu Watano kuna mwanamke mmoja na wanaume wanne.

Naam hakika lau kama aya hii ingekuwa kuhusu wake za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), utumiaji wa dhamiri ya kiume kwa ajili ya wanawake ungelikuwa ni kosa kabisa. Mbali na hili, uamuzi uliotolewa kutoka kwenye hadithi sahihi katika vitabu vyenu wenyewe ni kwamba aya hii tukufu iliteremshwa kwa sifa ya kizazi sio kuhusu wake zake.

Ingawa alikuwa mshabiki sana, Ibn Hajar Makki anasema katika kitabu chake, “Sawa’iq- e-Muhriqa” kwamba wafasiri wengi wanaamini kwamba aya hii iliteremshwa kwa sifa ya Ali, Fatimah, Hasan
na Husein.

Wake Za Mtume Hawakujumuishwa Katika Ahlul-Bayt

Tukiziweka pembeni hoja hizi, wake za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hawakujumuishwa katika Ahlul-Bayt.

Imesimuliwa katika Sahih Muslim na Jam’u’l-Usul kwamba Hasan Ibn Samra alimuuliza Zaid Ibn Arqam iwapo wake za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) walijumuishwa katika Ahlul- Bayt wake.
Zaid akasema: “Kwa jina la Allah, hapana. Mke anabakia na mumewe kwa kipindi fulani, lakini wakati akimuacha, anakwenda kwenye nyumba ya baba yake, huungana na familia ya mama yake, na anakuwa ametoka kabisa kwa mumewe.

Ahlul-Bayt ni wale jamaa wa familia ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ambao kwamba sadaka kwao ni haramu. Hawatatengana na Ahlul-Bayt popote watakapokwenda.”

Mbali na maafikiani ya maoni ya wote pamoja miongoni mwa Ithna’shari Shia kuhusu kizazi hicho kitukufu, kuna hadithi nyingi zilizoandikwa katika vitabu vyenu wenyewe, ambazo zinalikataa wazo la kwamba wake za Mtume wamejumuishwa katika Ahlul-Bayt.

Hadithi Nyingi Zinazohusu “Aya Ya Utakaso” Ikiwa Katika Kuwasifia

Watukufu Watano

Imamu Tha’labi katika “Tafsir-e-Kashfu’l-Bayan”; Imamu Fakhru’d-Din Razi katika “Tafsir-e-Kabir”, Jz. 6, uk. 783; Jalalu’d-Din Suyuti katika “Durru’l-Mansur”, Jz. 5, uk. 199 na “Khasa’isu’l-Kubra”, Jz. 2, uk. 264; Nishapuri katika “Tafsiir”, Jz. 3; Imamu Abdu’r-Razzaq ar-Ra’sani katika “Tafsir Rumuzu’l-Kunuz; Ibn Hajar Asqalani katika “Isaba”, Jz. 4, uk. 208; Ibn Asakir katika “Ta’rikh” Jz. 4, uk. 204 na 206; Muhibu’d-Din Tabari katika “Riyazu’n-Nuzra,” Jz. 2, uk. 188; Muslim Bin Hajjaj katika “Sahih”, Jz. 2, uk. 133 na Jz. 7, uk. 140; Nabhani katika “Sharaful-Mu’ayyid”, chapa ya Beiruti, uk. 10; Muhammad Bin Yusuf Ganji Shafi’i katika “Kifayatut-Talib”, sura ya 100, pamoja na hadithi sahihi sita na Sheikh Suleimani Balkhi Hanafi katika “Yanabiu’l-Mawadda”, sura ya 33, kutoka kwenye Sahih Muslim akitegemea juu ya hadith ya Ummu’l-Muminin Aisha; hadithi kumi kutoka Tirmidhi, Hakim Ala’u’d-Dowlat Semnani, Baihaki, Tibrani, Muhammad Bin Jarir, Ahmad Bin Hanbal, Ibn Abi Shaiba, Ibn Munzir, Ibn Sa’d, Hafidh Zarandi, na Hafidh Ibn Mardawiyya kama hadithi za Ummu’l-Muminin Ummi Salma, Umar Bin Abi Salma (ambaye alilelewa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), Anas Bin Malik, Sa’d Bin Abi Waqqas, Wathila Ibn Asqa, na Abu Sa’id Khudri wamesema kwamba “Aya ya Utakaso” imeteremka kwa sifa ya watukufu watano.

Hata Ibn Hajar Makki, pamoja na kuwa mpinzani wa Shia katika hali nyingi amekubali maana yake halisi katika njia saba. Anasema katika “Sawa’iq-e-Muhriqa” kwamba aya hii iliteremshwa kwa sifa ya Muhammad, Ali, Fatimah, Hasani na Huseini, na kwamba watu hawa tu, watukufu watano ndio waliokusudiwa katika aya hii.

Sayyid Abu Bakr Bin Shahbu’d-Din Alawi katika kitabu chake “Kitab-e-Rashqatus- Sa’adi min Bahr-e-Fadha’il Bani Nabiu’l-Hadi” (imechapisha na A’lamiyya Press, Misr, 1303 A.H.) sura ya 1, uk. 14-19, anasimulia kutoka kwa Tirmidhi, Ibn Jarir, Ibn Munzir, Hakim, Ibn Mardawiyya, Baihaqi, Ibn Hatim, Tibrani, Ahmad Bin Hanbal, Ibn Kathir, Muslim Bin Hajjaj, Ibn Abi Shaiba, na Samhudi katika misingi ya uchunguzi wa vitabu vya maulamaa wenu, kwamba aya hii iliteremshwa kwa sifa ya watu watano watukufu hawa.

Katika Jam’i-Bainus-Sihahus-Sitta, Muata cha Imamu Malik Bin Anas, Sahih Bukhari na Muslim, Sunan ya Abu Dawud na Sijistani, na Tirmidhi, Jam’ul-Usul na vitabu vingine, maulamaa na wanahistoria wenu kwa ujumla wanakiri kwamba aya hii iliteremshwa kwa sifa ya hawa watukufu watano. Na kwa mujibu wa madhehebu yenu, hadithi hii imesimuli- wa bila kukatishwa.

Hadithi Ya Ummi Salama Kuhusu ‘Harrira’ (Chakula Kitamu Cha Kimiminika) Cha Fatimah Na Kushuka Kwa “Aya Ya Utakaso”

Wasimuliaji wengi wa hadithi wamesimulia tukio linalohusiana na harrira. Miongoni mwao ni Imam Tha’labi katika “Tafsir” yake, Imam Ahmad Bin Hanbal katika “Musnad”, na Ibn Athir katika “Jam’u’l-Usul,” akinukuu kutoka “Sahih Tirmidhi na Sahih Muslim”: wote wanasimulia kutoka kwa mke wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), Ummul-Mu’minin Ummi Salama, ambaye alisema: “Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa nyumbani kwangu wakati Fatimah alipomletea kikombe cha harrira.

Wakati huo alikuwa amekaa kwenye baraza ambayo amezoea kulala. Alikuwa na joho la Khaibari chini ya miguu yake. Nilikuwa ninaswali chumbani mwangu. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimuambia Fatimah amuite mumewe na watoto wake.
Mara tu Ali, Hasan na Husein waliingia ndani na wote wakashirikiana ilie harrira. Jibril akajitokeza na kuteremsha aya hii tukufu kwa Mtume: “…Allah anapenda kuwaondoleeni uchafu enyi watu wa nyumba! Na kuwatakasa kwa utakaso kabisa…” (33:33)

“Kisha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akawafunika wote kwa joho lake, akanyanyua mikono juu mbinguni, na akasema: ‘Ewe Allah, hawa ndio wanaokifanya kizazi changu. Waondolee kila aina ya uchafu na uwatakase kwa utakaso ulio kamili.’”

Ummi Salama anasema kwamba alisogea mbele na akatamani kuingia katika lile joho akisema: “Ewe Mtume wa Allah, na mimi vile vile naweza kujiunga katika kundi hili?”

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akajibu akasema: “Hapana, bakia kwenye sheemu yako, wewe uko kwenye wema.” Hii ilikuwa na maana kwamba hakuweza kujumuishwa miongoni mwa Ahlul’l-Bayt na kupata cheo chao, lakini mwisho wake ulikuwa uwe mzuri. Imamu Fakhru’d-din Razi katika Tafsiir yake anaongeza kwamba Mtume alisema: “Dhambi zote zimezuiwa kwako” na “Umepewa majoho ya baraka.”

Kwa hakika inashangaza sana kwa maulamaa wenu wasio waadilifu, ambao wanaandika katika vitabu vyao sahihi kwamba Ali na Fatimah walijumuishwa katika “Aya ya Utakaso” (na uchafu mkubwa mno ni kusema uwongo). Bado wanakataa Uimamu wa Ali (uandamizi/urithi) na kukataa ushahidi wake katika kumuunga mkono Fatimah kuhusu madai yake ya Fadak. Haijulikani ni kwa kigezo gani wadai haki wanaunda hukumu.

Fadak Iliporwa Kwa Sababu Za Kisiasa

Sasa ngoja turudi kwenye nukta yetu ya mwanzo. Je, ilikuwa sahihi kukataa maelezo ya Ali na Fatimah na kuwanyima haki yao, lakini kukubali madai ya Jabir bila kusita kokote ingawa yeye alikuwa Mwislamu wa kawaida tu?

Hafidh: Kamwe haiwezi kukubalika kwamba Khalifa wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), ambaye alikuwa karibu mno na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), angeshawishika kuipora Fadak. Hakika Fadak haikuwa na maana kwa Khalifa, ambaye alikuwa na Baitu’l-Mal (Hazina ya Umma) ya Waislamu chini ya usimamizi wake.

Muombezi: Ni wazi kabisa kwamba hakuihitaji. Lakini kundi la kisiasa la wakati ule liliiona kwawmba ni muhimu kuiharibu familia tukufu ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Waliwafanyia watu hawa watoharifu kila aina hofu, mateso na umasikini, ili kwamba wasiweze kuufikiria ukhalifa. Watu wapenda dunia hufanya chochote kilicho lazima kuwafanya wastawi katika ulimwengu huu.

Wanasiasa hawa walitambua kwamba kama familia hii kubwa ingekuwa inamiliki utajiri wa kidunia, watu kwa hakika wangeelekea upande wao. Mitazamo ya kisiasa iliwasukuma kuipora Fadak na kufunga njia zao zote za mapato ya kifedha.

Khums Yapigwa Marufuku

Miongoni mwa vitu vilivyopigwa marufuku kwa ajili yao ilikuwa ni khums, ambayo kwayo msisitizo mkubwa umewekwa ndani ya Qur’ani. Kwa vile Allah amekataza sadaka kwa ajili ya Mtume na kizazi chake, mlango wa khums ulifunguliwa kwa ajili yao. Anasema katika Qur’ani, Sura ya 8, Anfal (Ngawira za kivita).

وَاعْلَمُوا أَنَّمَا غَنِمْتُمْ مِنْ شَيْءٍ فَأَنَّ لِلَّهِ خُمُسَهُ وَلِلرَّسُولِ وَلِذِي الْقُرْبَىٰ وَالْيَتَامَىٰ وَالْمَسَاكِينِ وَابْنِ السَّبِيلِ إِنْ كُنْتُمْ آمَنْتُمْ بِاللَّهِ وَمَا أَنْزَلْنَا عَلَىٰ عَبْدِنَا يَوْمَ الْفُرْقَانِ يَوْمَ الْتَقَى الْجَمْعَانِ ۗ{41}

“Na jueni kwamba kitu chochote kile mnacho kipata, moja ya tano yake ni kwa ajili ya Allah na Mjumbe Wake na jamaa wa karibu na yatima na mwana njia.” (8:41)

Matumizi haya yaliwekwa ili kwamba kizazi cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kiweze kuishi kwa amani na kisije kikahitaji msaada wa jumuiya yao. Lakini mara tu baada ya kufariki kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), walinyimwa fursa hii pia.
Khalifa Abu Bakr alizuia haki hii Ahlul’l-Bayt na kusema kwamba khums lazima itumike kwa ajili ya vifaa vya vita. Hivyo familia ya Mtume ilifanywa ikose msaada kutoka sehemu zote.

Imamu Shafi’i Muhammad Bin Idris anazungumzia kuhusu hili katika kitabu chake, “Kitabu’l-Umm” uk. 69: “Kizazi cha Mtume ambao kwamba Allah aliwapa fungu la khums badala ya sadaka, hawawezi kupewa mgao wowote, mkubwa au mdogo, kutoka kwenye sadaka za wajibu. Imekatazwa kwao kuzikubali. Wale ambao kwa makusudi huwapa sadaka hawatasamehewa kutokana na majukumu yao.

Kwa kuwanyima haki ya khums, sadaka ambayo imekatazwa kwao, haitakuwa halali. Hata katika wakati wa Khalifa Umar Bin Khattab, kizazi cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) walinyimwa madai yao ya haki kwa msingi kwamba kiasi cha khums kilikuwa ni kikubwa sana na kwamba kisingeweza kutolewa kwa jamaa wa karibu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Iliamuliwa kwamba pesa hizo lazima zitumike katika matumizi ya jeshi. Wananyimwa haki hii hadi leo.

Hafidh: Imamu Shafi’i anasema khums lazima igawanywe katika mafungu matano: fungu moja linakwenda kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), ambalo hutumika kwa matumizi na mahitaji ya Waislamu, fungu la pili ni kwa ajili ya jamaa zake wa karibu na mafungu matatu yaliyobakia ni kwa ajili ya mayatima, mafukara, na wasafiri.

Muombezi: Wafasiri kwa ujumla wanakubali kwamba wakati wa uhai wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aya hii iliteremshwa kwa ajili ya msaada wa kizazi na jamaa wa karibu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Khums ilitumika kwa matumizi yao. Kwa mujibu wa kanuni ya Shia, katika utiifu kwenye desturi iliyofutwa na familia ya Mtume na Maimamu watukufu, na vile vile kwa kuafikiana na maana ya aya tukufu iliyotajawa hapo juu, khums inagawanywa katika mafugu sita.

Mafugu matatu yaliyokusudiwa kwa ajili ya Allah, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na jamaa zake wa karibu yanaenda kwa Imam na, katika ghai- ba yake (huenda) kwa mwakilishi wake, mujtahid. Ni faqihi muadilifu na mzoefu, ambaye hutumia pesa kwa ajili ya faida ya Waislamu, kwa mujibu wa busara zake mwenyewe. Mafungu matatu yaliyobakia yanagawanywa kwa mayatima, mafukara na wafuasi safi wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Lakini baada ya kufariki Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), haki hii walinyimwa kizazi chake. Maulama wenu wenyewe wakubwa kama, Jalalu’d-din Suyuti, katika “Durru’l-Mansur, Jz. 3; Tabari, Imam Tha’labi katika “Tafsir-e-Kashful’l-Bayan”, Jarullah Zamakhshari katika “Kashshaf”, Qushachi katika “Sharh-e-Tajrid”, Nisa’i katika “Kitab-e-Alfiy,” na wengine kwa pamoja wanakubali ukweli kwamba mabadiliko haya yaliingizwa kwa ujanja wa wanasiasa baada ya kifo cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Hafidh: Unaona kwamba mujtahid ana haki ya kutumia busara zake, je, Khalifa Abu Bakr na Umar hawakutumia maamuzi zao na kujaribu kuwasaidia Waislamu?

Khalifa Hawezi Kupitisha Amri Yenye Kuvunja Amri Ya Wazi Ya Allah Na Mwendo Wa Mtume

Muombezi: Naam hakika mujtahid anayo haki ya kutengeneza hukumu, lakini hawezi akageuza sheria ya wazi. Je, unapendelea maoni ya Khalifa Abu Bakr na Umar kuliko yale yaliyomo kwenye aya ya Qur’ani iliyoko kwenye mjadala na mwenendo wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)? Tafadhali kuwa muadilifu na tuambie iwapo walikuwa na matilaba fulani makhususi nyuma ya yote haya.

Mtu mwenye akili za kawaida atashawishika kuamini kwamba haya hayakuwa mambo ya kawaida, bali yalilienga katika kuifanya familia ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kukaa bila msaada.

Allah Amemfanya Ali Shahidi Wa Mtukufu Mtume (S.A.W.W.)

Mbali na yote haya, Allah amemtangaza Ali kuwa shahidi wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Anasema katika Qur’ani: “Basi je, mtu ambaye ana dalili ya wazi itokayo kwa Mola wake, inayo fuatwa na shahidi anayetoka Kwake…ulinzi na rehma?” (11:17)
Hafidh: Kadiri ambavyo elimu yangu inakwenda, “ambaye ana dalili wazi kutoka kwa Mola Wake” maana yake Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na “shahidi” maana yake Qur’ani Tukufu. Kwa nini unadai kwamba hapa “shahidi” maana yake Ali?

Muombezi: Sielezei maoni yangu binafsi kuhusu aya za Qur’ani. Tulichokijua kutoka kizazi cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ni kwamba “shahidi” hapa maan yake Ali. Maulamaa na wafasiri wana maoni hayo hayo. Maulamaa wenu mashuhuri wameandika takriban hadithi thelathini katika kuliunga mkono hili. Kwa mfano, Imam Abu Ishaq Tha’labi anaandika hadithi tatu katika kitabu chake cha “Tafsir”; Jalalu’d-din Suyuti anaandika kati- ka kitabu chake “Durru’l-Mansur” kutoka kwa Mardawiyya, Ibn Abi Hatim, na Abu Nu’am; Ibrahim Bin Muhammad Hamwaini anaandika katika kitabu chake “Fara’idus- Simtain” kutoka kwenye vyanzo vitatu; Sulaimani Balkhi Hanafi anaandika katika kitabu chake “Yanabiu’l-Mawadda” kutoka kwa Tha’labi, Hamwaini, Khawarizmi, Abu Nu’aim, Waqidi na Ibn Abdullah Ansari na wengineo; Hafidh Abu Nu’aim Ispahani anasimulia kutoka vyanzo vitatu tofauti; Ibn Maghazili Faqih Shafi’i, Ibn Abi’l-Hadid Mu’tazali, Ibn Muhammad Bin Yusuf Ganji Shafi’i (tazama kitabu chake “Kifayatut-Talib” sura ya 62) na wengine katika maulamaa wenu wanasimulia pamoja na tofauti kidogo ya maneno kwamba “shahidi” katika aya hii maana yake Ali Bin Talib.

Khatib Khawarizmi anaandika katika kitabu chake “Manaqib” kwamba watu walimuuliza Ibn Abbas ni nini kilichomaanishwa na “shahidi”. Yeye alisema: “Hii inarejea kwa Ali, ambaye alitoa ushuhuda kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).”

Hivyo, kwa mujibu wa shuhuda za vitabu vyenu wenyewe vya kutegemewa, ilikuwa ni wajibu kwa jumuiya kukubali ushahidi wa Ali.

Allah Mwenyewe amemuita shahidi wa Mtume. Kama vile Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alivyokubali ubora uliowazi wa Khazima Bin Thabit na akaulinganisha ushahidi wake sawa na Waislamu wawili na akampa cheo cha Dhush-Shahadatain, Allah swt. vile vile ameelezea katika aya hii cheo kitukufu cha Ali na akamtambulisha kama “shahidi” kwa ajili ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Mtu hushangaa ni katika misingi ipi ya dini watu hawa waliamua kukataa ushahidi wa Ali.

Je, unaweza kukubali hukumu yao kwamba Ali Bi Abi Talib, ambaye alikuwa akikirihish- wa mno na mali za dunia hii na ambaye adabu na tabia yake ilikubaliwa na marafiki na maadui halikadhalika, alikuwa mtu wa kidunia? Hata maneno yasiopendeza yalitumiwa dhidi yake, ambayo siwezi kuyasema. Yote yameandikwa katika vitabu vyenu.

Hivyo kutumia maneno “masilahi yake binafsi yalihusika katika kesi hiyo,” walikuwa wanajaribu kushawishi watu kwamba inawezekana kwa Ali kutoa ushahidi wa uwongo kwa ajili ya faida ya mkewe na watoto wake. (Allah ayasamehe maneno yangu!) Ajabu iliyoje kwamba ingawa Allah amemtambulisha kwama shahidi wa kuaminika, watu hawa wajanja walikataa ushahidi wake.

Maumivu Makali Ya Kiakili Ya Ali

Ingawaje Qur’ani inatambulisha uaminifu wa Ali, aliteseka kwa sababu ya shutuma za wanasiasa. Alisema katika khotuba yake ya Shiqshiqayya: “Nilivumilia maumivu makali. Ilikuwa kama ninachomwa katika jicho na kukabwa roho.” Maneno haya yanathibitisha vya kutosha na zaidi mateso makali ya Mtukufu Imam.

Alisema: “Naapa kwa jina la Allah kwamba mtoto wa Abu Talib ni mwenye kupenda mno kifo kuliko alivyo mtoto anyonyaye ziwa la mama yake.” Wakati maaluni Abdu’r-Rahman Ibn Muljim Muradi alipompiga dharuba la kichwa kwa upanga wenye sumu, yey Imam alisema: “Kwa Mola wa Kaaba, mimi ni mshindi.”

Mabwana, kile kilichotokea kilipaswa kisitokee. Lakini leo sio sahihi kwa ulamaa wenye busara kama ninyi kusababisha matatizo zaidi kwa mtu mpendwa mno wa Allah na Mtume Wake na kusababisha kutokuelewana miongoni mwa watu wasio na ujuzi. Mnajua kabisa kwamba kumbughudhi Ali Bin Abi Talib kwa hakika ni kumbughudhi Mtukufu Mtume wa Allah (s.a.w.w.).

Hadithi Inayowalaumu Wenye Kumbughudhi Ali

Imamu Ahmad Bin Hanbal katika Musnad yake, Imamu Tha’labi katika Tafsir yake na Sheikhu’l-Islam Hamwaini katika kitabu chake Fara’id wamesimulia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Yule ambaye anamuonea Ali, ananionea mimi. Enyi watu, yeyote yule anayemuonea Ali atafufuliwa Siku ya Hukumu kama Myahudi au Mkiristo.”

Ibn Hajar Makki katika uk. 78 wa sehemu ya 2, sura ya 9, Hadithi ya 16 kutoka kwa Sa’d Ibn Abi Waqqas na Muhammad Bin Yusuf Ganji Shafi’i katika Kifayatut-Talib, sura ya 68, anasema kwa kutegemea juu ya maandishi sahihi kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Yule ambaye anambughudhi Ali, kwa hakika ananibughudhi mimi.”

Nakumbuka hadithi nyingine. Niruhusuni niisimulie. Kusimulia hadithi ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na kuisikia ni ibada. Hadithi hii imeandikwa na Bukhari katika Sahih yake; Imamu Ahmad Bin Hanbal katika Musnad yake; Mir Seyyid Ali Hamadani Shafi’i katika Mawaddatu’l-Qurba; Hafidh Abu Nu’aim Ispahsni katika Maa Nazala Mina’l- Qur’ani fi Ali; Khatib Khawarizmi katika Manaqib na Ibn Maghazili Shafi’i katika Manaqib yake wameisimulia hiyo.

Hakim Abu’l-Qasim Haskani vile vile anaisimulia kutoka kwa Hakam Abu Abdullah Hafidh, yeye kutoka kwa Ahmad Bin Muhammad Bin Abi Dawud Hafidh, yeye kutoka kwa Ali Bin Ahmad Ajali, yeye kutoka kwa ‘Ibad Bin Yaqub, yeye kutoka kwa Artat Bin Habib, yeye kutoka kwa Abu Khalid Wasti, yeye kutoka kwa Zaid Bin Ali, yeye kutoka kwa baba yake, Ali Bin Husein, yeye kutoka kwa baba yake, Husein Ibn Ali, yeye kutoka kwa baba yake, Ali Ibn Abi Talib; kila mmoja wa wasimuliaji hawa alisema kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: huku akiwa ameshika unywele wa ndevu zake:

“Ewe Ali, yeyote ambaye ataumiza unywele wako mmoja, hakika ananiumiza mimi; yule ambaye ananiumiza mimi hakika anamuumiza Allah, na yule ambaye anamuumiza Allah analaaniwa Naye Allah swt.”

Sayyid Abu Bakr Bin Shahabu’d-din Alawi katika kitabu chake Rashfatus-Sa’adi min Bahr-e-Faza’il Bani Nabiu’l-Hadi, (kimepigwa chapa na A’lamiyya Press, Misri, 1303 A.H.) sura ya 4, uk. 60, anasimulia kutoka Kabir cha Tabrani, Sahih ya Bin Habban, na Hakim kutoka kwa Amiru’l-Mu’minin, kwamba Mtukufu Mtume wa Allah (s.a.w.w.) alisema: “Laana ya Allah iwe juu yake yule ambaye ananihuzunisha mimi kuhusiana na kizazi changu.”

Ali Alibughudhiwa Na Kutukanwa

Mabwana, fikirieni yaliyo tokea. Ushahidi wa Ali ulikataliwa hadharani. Mali ya Fatimah ilipokonywa. Pigo hili la uonevu liliumiza sana hisia za Fatimah kiasi kwamba aliutoka ulimwengu huu katika umri wake mdogo wa ujana, akiwa amejawa na masononeko.

Hafidh: Ni wazi kwamba mwanzoni Fatimah alikuwa amesononeka mno, lakini mwishowe wakati alipoona kwamba hukumu ya Khalifa ilikuwa sahihi, hakuwa na hasira tena. Hatimaye aliutoka ulimwengu huu akiwa ameridhika kikamilifu na kutosheka.

Fatimah Alibakia Na Hasira Juu Ya Abu Bakr Na Umar Mpaka Kifo Chake

Muombezi: Kama unayosema ni sahihi, kwa nini maulamaa wenu wakubwa wameandika kinyume chake? Kwa mfano, wanachuoni wawili wa kutegemewa, Bukhari na Muslim, wanaandika katika Sahih zao kwamba Fatimah alimkataa Abu Bakr kwa sababu alikuwa amekasirika. Kwa sababu ya kutoridhika kwake hakuzungumza naye kwa muda wa uhai wake wote uliobakia. Wakati alipofariki, mume wake, Ali, alimzika usiku. Hakuruhusu Abu Bakr kujumuika kwenye mazishi yake na kumsalia.

Muhammad Bin Yusuf Ganji Shafi’i amesimulia kisa hicho hicho katika kitabu chake “Kifaya,” sura 99. Vile vile Abu Muhammad Abdullah Bin Muslim Bin Qutayba Dinawari katika kitabu chake “Imama was-Siyasa”, uk. 14, anaandika kwamba, wakati Fatimah alipokuwa mgonjwa kitandani, alisema kumuambia Abu Bakr na Umar: “Allah na Malaika wawe mashahidi wangu kwamba ninyi wote (wawili) mmenisononesha. Wakati nitakapokutana na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa hakika nitamlalamikia dhidi yenu.” Vile vile vitabu hivi vinaandika: “Fatimah alimkasirikia Abu Bakr na alikataa kuonana naye muda wote wa uhai wake uliobakia.”

Mbali na haya, kuna riwaya nyingi nyingine na hadithi zilizoandikwa katika vitabu vyenu sahihi.

Huzuni Ya Fatimah Ni Huzuni Ya Allah Na Mtume

Kuna hadith inayojulikana sana iliyosimuliwa na maulamaa wenu wengi, kama Imam Ahmad Bin Hanbal katika Musnad; Sulaiman Qanduzi katika Yanabiu’l-Mawadda; Mir Sayyid Ali Hamadani katika Mawaddatu’l-Qurba; Ibn Hajar katika Sawa’iq, akisimulia kutoka kwa Tirmidhi, Hakim na wengine, pamoja na tofauti ndogo ya maneno, kwamba Mtukufu Mtume wa Allah (s.a.w.w.) Amesikika mara kwa mara akisema: “Fatimah ni sehemu ya mwili wangu, ni nuru ya macho yangu, yeye ni tunda la moyo wangu, ni moyo wangu katikati ya mbavu zangu mbili.

Yule ambaye anamhuzunisha Fatimah ananihuzunisha mimi; yule ambaye ananihuzunisha mimi, anamhuzunisha Allah; yule ambaye anamkasirisha yeye ananikasirisha mimi; kinachomuumiza Fatimah huniumiza mimi.”

Ibn Hajar Asqalani, katika kitabu chake “al-Isaba fi tamyiz as-Sahaba”, ananukuu kutoka kwenye Sahih za Bukhari na Muslim kwamba Mtukufu Mtume wa Allah (s.a.w.w.) alisema: “Fatimah ni sehemu ya mwili wangu; kinachomuumiza yeye, huniumiza mimi; kile ambacho huendeleza ufanisi wake wa kiroho, huendeleza ufanisi wangu wa kiroho.”

Muhammad Bin Talha Shafi’i katika kitabu chake “Matalibus-Su’ul”; Hafidh Abu Nu’aim Ispahani katika Hilyatu’l-Auliya, Jz. 2, uk. 40, na Imamu Abdu’r-Rahman Nisa’i katika kitabu chake “Khasa’isu’l-Alawi,” wanasimulia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alise- ma: “Hakika Fatimah, bint yangu ni sehemu ya mwili wangu; kinachomfurahisha yeye, hunifurahisha mimi; kinachomchukiza yeye hunichukiza mimi.”

Abu’l-Qasim Husain Bin Muhammad (Raghib Ispahani) anasimulia katika kitabu chake “Mahadhirratu’l-Ubada,” Jz. 2, uk. 204, kwamba Mtukufu Mtume wa Allah (s.a.w.w.) alisema: Fatimah ni sehemu ya mwili wangu; kwa hiyo anayemkasirisha yeye ananikasirisha mimi.”

Hafidh Abu Musa Bin Muthanna Basri (alikufa 252 A.H.) katika kitabu chake “Mu’ajam”; Ibn Hajar Asqalani katika “Isaba”, Jz. 4, uk. 35; Abu Ya’ala Musili katika Sunan yake; Tibrani katika “Mu’ajam”; Hakim Nishapuri katika “Mustadrak”, Jz. 7, uk. 154; Hafidh Abu Nu’aim Ispahani katika “Fadha’ilus-Sahaba”; Hafidh Ibn Asakir katika “Ta’rikh-e- Shami”; Sibt Ibn Jauzi katika “Tadhkira”, uk. 175; Muhibu’d-din Tabari katika “Dhakha’ir”, uk. 39, Ibn Hajar Makki katika “Sawa’iq”, uk. 105 na Abu Irfanu’s-Subban katika “As’afu’r-Raghibin”, uk. 171, wamesimulia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema kumwambia binti yake, “Ewe Fatimah, hakika, kama ukikasirika Allah Naye vile vile anakasirika; kama ukifurahi, Allah vile vile anafurahi.”

Muhammad Bin Ismail Bukhari katika Sahih yake, katika sura ya Manaqib Qarabat-e- Rasulullah, uk. 71, ananukuu kutoka kwa Miswar Bin Makhrama ambaye alisema kwam- ba, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Fatima ni sehemu ya mwili wangu, hivyo yeyote yule anayemkasirisha Fatima, hakika, ananikasirisha mimi.”

Kuna hadithi nyingi kama hizo zilizoandikwa kwenye vitabu vyenu sahihi, kama Sahih Bukhari; Sahih Muslim; Sunan ya Abu Dawud; Tirmidhi; Musnad ya Imamu Ahmad Hanbal; Sawa’iq-e-Ibn Hajar; na Yanabiu’l-Mawadda cha Sheikh Sulaiman Balkh. Utaoanisha vipi hadithi hizi na riwaya ambazo zinasema kwamba Fatima hakuutoka ulimwengu akiwa amewakasirikia watu hawa?

Tuhuma Kuhusu Ali Kukusudia Kumuoa Bint Ya Abu Jahl

Sheikh: Hadithi hizi ni sahihi, lakini vile vile imesimuliwa kuhusu Ali kwamba wakati alipokusudia kumuoa binti ya Abu Jahl, Mtume wa Allah akamkasirikia na akasema: “Yeyote yule anayemhuzunisha Fatimah ananihuzunisha mimi, na yeyote anayenihuzunisha mimi ni mtu aliyelaaniwa na Allah.
Muombezi: Lazima tukubali au tukatae mambo kwa kutumia akili ya kuzaliwa na busara. Allah anasema katika Qur’ani: “Kwa hiyo wape habari njema waja wangu wale ambao wanaosikiliza maneno, kisha wakafuata yale yaliyo mazuri; hao ndio wale ambao Allah amewaongoza, na hao ndio watu ambao wanafahamu.”

Riwaya ilisimuliwa na wahenga wenu. Leo mnaunga mkono maneno yao bila kupima ubora wao. Ninawajibika kukupa jibu fupi. Kwanza, maulamaa wenu wenyewe wamekubali ukweli kwamba Ali alijumuishwa katika “aya ya utakaso” na alikuwa ameto- harika kikamilifu. Pili, katika “aya ya Mubahila”, Allah amemuita “nafsi” ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kama tulivyokwisha kulijadili katika mikesha iliyopita.

Tumeonesha kwamba alikuwa vile vile “mlango wa elimu ya Mtukufu Mtume wa Allah (s.a.w.w.)” na alikuwa anaelewa kwa ukamilifu amri na sheria za Qur’ani. Alijua kwamba Allah alisema katika Sura ya Ahzab ya Qur’ani Tukufu: “Na haiwapasi ninyi kwamba mumpe matatizo Mjumbe wa Allah.”

Kwa vile hii ni kweli, Ali angewezaje kufanya au kusema kitu chochote ambacho kingemuudhi Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)? Na mtu atafikiriaje kwamba mfano halisi wa ubora, yaani Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) atachukizwa na shaksiya ya mtu huyo aliyetukuka ambaye alipendwa na Allah? Na je, atachukizwa na kitendo ambacho kimeruhusiwa na Allah, kama Anavyosema katika Qur’ani Tukufu:“…basi oeni wanawake wale ambao wanaonekana wazuri kwenu, wawili, au watatu au wanne”?

Amri hii ya nikah (ndoa) ni ya umuhimu wa jumla na imekusudiwa kwa ajili ya umma wote halikadhalika na kwa ajili ya mitume na waandamizi. Na kama tukichukulia kwam- ba Amiru’l-Mu’minin alikuwa na kusudio lolote kama hilo, ilikuwa ni ruhusa kwake.

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) asingeweza kuzuia tendo lolote linaloruhusiwa, wala hakutumia maneno kama hayo. Mtu yeyote mwenye akili, baada ya kuzingatia kwa makini, ataweza kujua kwamba riwaya hii ni moja ya riwaya za kughushi za Bani Umayya. Wanachuoni wenu wakubwa wanaukubali ukweli huu.

Uzuaji Wa Hadithi Wakati Wa Kipindi Cha Mu’awiyah

Ibn Abi’l-Hadid Mu’tazali ananukuu riwaya kutoka kwa kiongozi na mwalimu wake, Abu Ja’far Iskafi Baghdadi, katika kitabu chake “Sharh-e-Nahju’l-Balaghah”, Jz. 1, uk. 358, kwamba Mu’awiya Bin Abu Sufyani aliunda kikundi cha Masahaba na tabi’in (kizazi cha pili ambacho kilifuata mara tu baada ya Mtume) kwa madhumuni ya kughushi hadithi zenye kumlaani Ali.

Madhumuni yao yalikuwa ni kumfanya mlengwa wa shutuma ili kwamba watu wajitenge mbali naye. Miongoni mwao walikuwamo Abu Huraira, Amr Bin Aas, Mughira Bin Shaiba, Urwa Bin Zubair, mmoja
wa tabi’in vile vile alikuwa pamoja nao. Abu Ja’far Iskaf vile vile amerejea kwenye baadhi ya hadithi
zao za kughushi.

Akizungumzia kuhusu Abu Huraira, anasema kwamba alikuwa ni mtu ambaye alisimulia hadithi yenye maana ya kuonesha kwamba Ali alitaka kumuoa binti wa Abu Jahl wakati wa uhai wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Hili likamasirisha Mtume, na akasema juu ya mimbar, “Rafiki wa Allah na adui wa Allah hawawezi kuwa pamoja. Fatimah ni sehemu ya mwili wangu. Yule ambaye anamhuzunisha yeye ananihuzunisha mimi. Yule ambaye anataka kumuoa bint ya Abu Jahl lazima atafute kutengana na binti yangu.”

Baada ya hili, Abu Ja’far anasema kwamba hadithi hii inajulikana kama hadithi ya Karabis, kwa vile kila hadithi isiyo na msingi inaitwa karabis (kilugha, muuzaji wa nguo).

Ibn Abi’l- Hadid anasema kwamba hadithi hii imesimuliwa katika Sahih mbili ya Bukhari na Muslim kutoka kwa Miswar Bin Makhrama za-Zahr.

Na Sayyid Murtaza Alamu’l-Huda, ambaye alikuwa mmoja wa maulamaa wakubwa wa Mashi’a, anasema katika kitabu chake “Tanzia’u’l-Anbia wa’l-A’imma” kwamba riwaya hii ilisimuliwa na Husein Karabisi, ambaye anajulikana kwa upinzani wake mkali kwa Ahlul’l-Bayt watukufu.

Alitokana na Nawasib na alikuwa mmoja wa maadui wakubwa wa familia hii tukufu. Riwaya yake haikubaliki. Kwa mujibu wa hadithi zilizosimuliwa katika vitabu vyenu sahihi, adui wa Ali ni mnafiki (munaafiq). Munafiq kwa mujibu wa Qur’ani Tukufu, ni kiumbe muovu kabisa. Kwa hiyo hadithi yake haina ubora wowote.

Mbali na hili, hadithi zinazowalaani watu wanasababisha maudhi kwa Fatimah hazikomei kwenye maelezo ya Karabisi au ile riwaya ya kughushi ya Abu Huraira kuhusu binti ya Abu Jahl.

Kuna hadithi nyingi nyingine juu ya suala hili. Miongoni mwazo ni ile iliyosimuliwa na Parsa wa Bukhara katika kitabu chake, “Faslu’l-Khitab”; moja iliyisimuliwa na Imamu Ahmad Bin Hanbal katika Musnad yake na Mir Sayyid Ali Hamadani Shafi’i katika Mawadda 13 ya Mawddatu’l-Qurba, kutoka kwa Salman Muhammadi, kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Mapenzi ya Fatimah yana manufaa kwetu sisi katika sehemu mia moja, nyepesi mno ya hizo ikiwa ni Kifo, Kaburi, Mizani, Sirat (daraja) na Kusailiwa.

Hivyo, kama binti yangu Fatimah, yuko radhi na mtu fulani, mimi vile vile niko radhi naye huyo. Kama nikiwa radhi na mtu fulani, Allah vile vile atakuwa radhi naye. Kama binti yangu Fatimah hayuko radhi na mtu fulani, mimi vile vile sitakuwa radhi naye. Kama siko radhi naye, Allah vile vile hatakuwa radhi naye. Ole wake yule anayemuonea Fatimah na mume wake. Ole wake yule anayemuonea Ali na Fatimah na Mashi’a wao.”

Nawaulizeni ni uamuzi gani mtakaochukua katika mwanga wa hadithi hizi sahihi na hadithi zilizoandikwa na Bukhari na Muslim kwamba Fatimah alibakia amewakasirikia Abu Bakr na Umar mpaka kufa kwake.

Kuelewa Vibaya Kuhusu Hasira Za Fatima Kwamba Sio Za Kidini

Hafidh: Naam kwa hakika hadithi hizo ni sahihi na zimeandikwa kwa urefu katika vitabu vyetu sahihi. Kwa hakika hata mimi vile vile niliitilia shaka riwaya ya Karabisi kwamba Ali alitaka kumuoa binti ya Abu Jahl. Mimi sikuiamini, na sasa kwa hakika ninashukuru sana kwamba umenitatulia tatizo hili.

Pili, katika hadithi hizi “hasira” maana yake ni hasira za kidini na sio hasira za mambo ya kawaida ya kidunia. Hasira yake kuhusiana na Abu Bakr na Umar, ambayo imeandikwa katika vitabu vyetu vyote sahihi, haikuwa ya kidini. Yaani, Fatimah hakuwa na hasira na Abu Bakr na Umar kwa sababu walivunja amri yoyote ya kidini. Kwa hakika, kama mtu yeyote aliamsha hasira zake za kidini, angepasika na laana ya Mtume wake.

Lakini kwa kweli hasira ya Fatimah ilitokana na mabadiliko katika hali yake, ambayo kila mtu mwenye hisia huhisi wakati akishindwa kufikia lengo lake. Kwa vile Fatimah alitoa maombi kwa ajili ya Fadak na Khalifa hakukubali madai yake, kwa kawaida aliathirika kwalo na akajisikia hasira kwa wakati ule. Lakini baadae chuki hii ndogo ilitoweka katika mawazo yake, na aliridhika na uamuzi wa Khalifa.

Uthibitisho wa kuridhika kwake ni ukimya wake. Na wakati Ali alipochukua hatamu za ukhalifa, pamoja na mamlaka yote makubwa aliyokuwa nayo, hakuirudisha Fadaka chini ya miliki yake. Huu pia ni uthibitisho kwamba aliridhika na uamuzi wa makhalifa waliopita.

Fatimah Alikuwa Huru Kutokana Na Kujiambatanisha Na Mambo Ya Kidunia

Uombezi: Kwanza, umesema kwamba hasira ya Fatimah haikuwa ya kidini bali ilikuwa ya kidunia. Umeelezea mtazamo huu bila uchunguzi makini.

Kwa mujibu wa kanuni za aya za Qur’ani na hadithi za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), hakuna muumini mkamilifu angethubutu kuonesha chuki kama hiyo, achilia mbali kumtaja Fatima, ambaye utukufu wake uko wazi kutoka kwenye “Aya ya Utakaso” “Aya ya Mubahila” na Surat Hal Ata ya Qur’ani Tukufu (76: 1).

Kuna hadithi nyingi katika vitabu sahihi vya kwenu na vya kwetu, kwamba Fatimah alikuwa na cheo cha juu sana cha imani, na kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa uwazi alisema kuhusu yeye: “Hakika, Allah amemjaza kwa imani bint yangu, Fatimah, kuanzia kichwani mpaka miguuni.”

Hasira Ya Fatimah Imechochewa Na Dini

Muumini yeyote, mwamume au mwanamke, ambaye alama yake maalumu ni kuukubali ukweli, kamwe hataonesha hasira wakati hakimu akitoa amri ya haki. Wala muumini kama huyo hatashikilia kwenye hasira hizo na ghadhabu mpaka kifo chake akisisitiza katika wosia wake kwamba wale wote ambao kwa njia yotote walihusika na amri hizo wasiruhusiwe kujuinga katika sala yake ya mazishi.

Aidha, Fatimah ambaye kuhusu usafi wake Allah Mwenyewe anautolea ushahidi, asingeweza kamwe kufanya madai ya uwongo, hivyo kwamba hakimu aweze kulikataa dai lake.

Pili, kama hasira ya Bibi Fatimah ilikuwa tu ni “hasira ya kidunia” kama unavyoiita, au kuchukizwa kwake kwa kukataliwa dai lake, hasira yake ingelishuka mara moja, hususan baada ya kujuta kulikooneshwa na wale ambao walihusika na hasira yake hiyo. Kusingelikuwa na huzuni katika moyo wake.

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Moja ya alama za muumini ni kwamba kwa kawaida huwa haweki mfundo wa moyo uliojengeka juu tamaa za kimwili, dhidi ya mtu yeyote.” Vile vile Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Kama muumini akitokea kufanya kosa, muumini aliyechukizwa nalo hatakuwa na chuki kwake kwa zaidi ya siku tatu.”

Hivyo Fatimah Zahra aliye mkweli na safi, ambaye kwa mujibu wa ushuhuda wa Allah swt., amejazwa imani kutoka kichwani mpaka miguuni, kamwe asingeweza kuwa na kinyongo dhidi ya mtu yeyote. Na inakubaliwa na madhehebu zote kwamba Fatimah aliutoka ulimwengu huu akiwa amemkasirikia Abu Bakr na Umar. Hivyo inamaanisha kutokana na hili kwamba hasira ya Fatimah ilikuwa ya kidini kabisa.

Wakati alipoona kwamba hukumu inapitishwa dhidi yake kwa kuvunja amri ya Allah na ya Mtukufu baba yake, alijihisi kukasirika mno kwa maudhi ya kidini na hii ndio ile hasira inayoleta ghadhabu ya Allah na Mtume Wake.

Ukimya Wa Fatimah Haukuashiria Kuridhika Kwake

Tatu, umesema kwamba kwa vile ukimya wa Fatima ulimaanisha aliridhiana na uamuzi huo. Hapa tena umekosea. Ukimya sio lazima uwe na maana ya kukubaliana. Wakati mwingine ukatili wa mkandamizaji hulazimisha kukubali.

Fatima si kwamba alihuzunishwa tu, bali aliutoka ulimwengu huu akiwa amekasirika. Wote wawili, Bukhari na Muslim wameandika: “Fatimah alimkasirikia Abu Bakr. Alijitenga naye na hakuzungumza naye kwa maisha yake yote yaliobakia.”

Ali Hakuwa Huru Kutenda Wakati Wa Kipindi Cha Ukhalifa Wake

Nne, umesema kwamba kwa sababu Ali, wakati wa ukhalifa wake, hakuchukuwa umiliki wa Fadak na kuirudisha kwa kizazi cha Fatimah, hii inaashiria kukubaliana kwake na uamuzi wa Makhalifa waliopita. Hata hapa pia umekosea. Mtukufu Imam alikuwa hayuko huru kutenda wakati wa kipindi chake cha ukhalifa ili aweze kuzuia bidaa yoyote au kurudisha haki yoyote. Wakati wowote alipotaka kuchukua hatua kama hiyo, kulikuwa na upinzani wa mara moja.

Kama angeirudisha Fadak kwa kizazi cha Fatimah, wapinzani wake, hususani Mu’awiya na wafuasi wake, wangelidai kwamba Ali anafanya kinyume na mwenendo waliofuata Abu Bakr na Umar. Mbali na hili, ili kupitisha hukumu kama hizo, mamlaka na uhuru vilikuwa ni muhimu sana.

Lakini watu hawakumruhusu kuwa na uwezo kama huo. Asingeweza kuanzisha kitu chochote ambacho kingevunja kanuni na mwenendo wa Makhalifa waliotangulia. kutokuwa kwake na uwezo Ali, kuko wazi katika mifano miwili ifuatayo.

Kwa vile Makhalifa waliotangulia waliiondoa mimbari kutoka mahali pake ambapo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliiweka, Mtukufu Imam alikusudia kuirudisha kwenye sehe- mu yake ya asili.

Lakini watu walimpinga na hawakuweza kuvumilia kitu chochote kilicho kinyume na mwenendo wa Abu Bakr na Umar, hata kama kingekuwa hakiafikiani na mwenendo wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Halikadhalika, wakati Mtukufu Imam alipowakataza watu kusali swala ya tarawehe kwa jamaa, walimpinga na wakadai kwamba Ali alitaka kubadilisha mwenendo wa Khalifa Umar.

Nawab: Mheshimiwa! Tarawehe ilikuwa ni kitu gani ambacho Ali alikataza isiswaliwe kwa jamaa?

Muombezi: Kilugha tarawehe ni wingi wa tarawia, ambayo maana yake “kikao”. Baadaye ikajakuwa na maana ya “kukaa kwa ajili ya kupumzika” baada ya rakaa nne za sala za usiku wakati wa mwezi wa Ramadhan. Kisha ikaja kumaanisha rakaa nne za sala ya sunna (iliyopendekezwa). Ni kanuni ya wazi katika sheria ya ki-Islamu kwamba ni sala za wajib tu ndizo ambazo huswaliwa kwa jamaa, ambapo zile za sunna kuzisali kwa jamaa imekatazwa.

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mwenyewe alisema: “Hakika kusali nafila (sunna) katika jamaa wakati wa usiku katika mwezi wa Ramadhani ni uzushi (bid’a). Namaz-e-Chasht (wakati mwingine hujulikana kama Dhuha na husaliwa kabla ya adhuhuri, au jua linapochomoza na kupanda kidogo) ni dhambi. Enyi watu! Msisali sala za nafila (sunna) katika mwezi wa Ramadhan kwa jamaa na msisali Namaz-e-Chasht (Dhuha).

Kwa kuwa na uhakika, kufanya kitendo kidogo cha ibada kwa mujibu wa sunnah ni bora kuliko kufanya kitendo kikubwa ambacho ni uzushi (bid’a). Naifahamike kwenu wote kwamba kila bid’a ni upotovu na kila upotovu unaongozea kwenye moto.”

Usiku mmoja wakati wa ukhalifa wake katika mwaka wa 14 A.H. Umar aliingia msikitini. Aliona kwamba watu walikuwa wamekusanyika pale. Akawauliza ni kwa nini wameku- sanyika. Wale watu wakasema wamekusanyika ili kuswali sunna. Umar akasema: “Kitendo hiki ni bid’a, lakini ni bid’a nzuri.”

Bukhari ananukuu katika Sahih yake kutoka kwa Abdu’r-Rahman Bin Abdu’l-Qari kwam- ba wakati Khalifa alipowaona watu wanasali kila mmoja peke yake, aliwaambia kusali kwa jamaa kunafaa zaidi. Alimuamuru Ubayy Bin Ka’b kuongoza sala hiyo kwa jamaa. Wakati alipokuja msikitini usiku uliofuatia, aliwaona watu wanasali jamaa kwa kutii amri yake. Akasema: “Uzuri ulioje wa bid’a hii.”

Ikawa ni jambo la kawaida mpaka wakati wa Amiru’l-Mu’minin. Yeye aliikataza, akisema kwamba kwa vile haikuwepo wakati wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), kwa hivyo ilikatazwa, kwa hakika isiruhusiwe kuendelea.

Wakati alipokuja Kufa, watu wa Kufa walimuomba Mtukufu Imam kuwateulia mtu kwa ajili ya kuongoza sala za nafila wakati wa usiku wa mwezi wa Ramadhani. Imamu aliwakataza kusali sala hiyo kwa jamaa. Pamoja na amri hiyo, kwa vile watu walikuwa wamezoea hivyo, hawakufuata amri ya Imamu.

Mara tu Imamu alipoondoka kwenye sehemu ile, walijikusanya pamoja na wakamteuwa mmoja wao kuongoza sala katika jamaa.

Punde tu habari zilimfikia Imamu, ambaye alimuita Hasan mtoto wake mkubwa na alimtaka achukue jambia na akawakataze watu wale kusali sunna kwa jamaa. Wakati watu walipoona hivyo, walipiga makelele wakisema: “Ewe Ali! Hasan amekuja, na haturuhusu sisi kuswali.”

Ingawa walijua kwamba jambo hili la kusali sala za sunna katika jamaa halikuwepo wakati wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), hawakufuata amri ya Ali ambayo iliafikiana na amri za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Sasa vipi Ali angeweza kuirejesha Fadak kwa kizazi cha Fatimah? Kama angelifanya hivyo, na aseme ilichukuliwa isivyo halali, watu wangepiga kelele kwamba Ali Bin Abi Talib amevutwa na mapenzi ya dunia na anapora haki ya Waislamu kwa ajili ya watoto wao.

Hivyo aliona ni bora kuwa na subira. Kwa vile mdai halisi alikuwa ametoweka ulimwenguni hapa, madai yake aliyaahirisha, ili kwamba wakati Imamu wa mwisho mwenye kuongozwa kimungu atakapokuja kurudisha haki kwa wahusika wake wa halali, na yeye atapata haki yake. Katika hali ya mambo kama hayo, ukimya wa Mtukufu Imamu haukuwa na maana kwamba aliridhika na uamuzi huo.

Kama angekichukulia kitendo cha Makhalifa waliotangulia kuwa ni cha haki, asinglihoji suala lake mbele yao. Vile vile, asingeelezea machungu yake na kuudhika kwake, na asigemuomba Allah kuwa muamuzi wake.

Imeandikwa katika Nahju’l-Balagha kwamba katika barua aliyompelekea Gavana wa Basra Uthman Bin Hunaif Ansari, Ali aliandika: “Miongoni mwa vitu ambavyo kwamba mbingu hutupa kivuli chake juu yake ni Fadak, ambayo ilikuwa kwenye milki yetu. Lakini kundi moja likaonesha uchoyo, na upande mwingine, Fatimah na watoto wake waliacha kuendelea na madai yao. Na Allah Ndiye Hakimu aliye bora.”

Umesema kwamba Fatimah aliridhika na uamuzi huo katika siku zake za mwisho za uhai wake na akawasamehe wale ambao walihusika na suala hili. Nina wasiwasi hapa umekosea. Kwani kama ambavyo imethibitishwa mapema bila mashaka yoyote kwa hadithi zenye kutegemewa kwamba Bibi madhulum alibakia ni mwenye kukasirika mpaka alipofariki.

Abu Bakr Na Umar Walijaribu Kumtembelea Fatimana Kuelezea Maoni

Yao Lakini Hawakufanikiwa

Kuthibitisha maoni yangu ningependa kuwasilisha riwaya ifuatayo: Abu Muhammad Abdullah Bin Muslim Bin Qutayba Dinawari (alikufa mwaka 276 A.H.) katika kitabu chake “Ta’rikh-e-Khilafa’i’r-Rashidin” kijulikanacho kama ‘Al-Imama was-Siyasa’, Jz. 1, uk. 14 na wengine miongoni mwa maulamaa wenu, kama Ibn Abi’l-Hadid, wanaandika katika vitabu vyaovya sahih: “Umar alimuomba Abu Bakr waende pamoja naye kumtembelea Fatimah. Kwa hakika walikuwa wamemkasirisha sana. (baadhi ya riwaya zinasema alikuwa ni Abu Bakr aliyemuomba Umar kwenda naye kumtembelea Fatimah. Hii inaonekana ni yenye kukubalika zaidi).

Kwa ufupi wote kwa pamoja walikwenda kwenye mlango wa Fatumah lakini yeye hakuwaruhusu wamuone. Wakati walipomuomba Ali angilie kati yeye alinyamaza kimya, lakini aliwaruhusu kuingia ndani. Wakati walipoingia ndani na kumsalimu, aligeuzia uso wake ukutani. Abu Bakr akasema: “Ewe pande la ini la Mtume! kwa jina la Allah, nauthamini uhusiano wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na wewe zaidi kuliko uhusiano wangu mimi na binti yangu Aisha.

Lau ingelikuwa nife mapema baada ya Mtukufu Mtume wa Allah (s.a.w.w.). Najua cheo na daraja yako zaidi kuliko mtu mwingine yeyote. Kama nimekunyima haki yako ya kurithi, ni kwa sababu ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), ambaye mimi mwenyewe nimemsikia akisema: ‘Sisi Mitume hatuachi urithi wowote. Tunachoacha ni sadaka (kwa ajili ya Waislamu).’

Fatima akamuambia Amiru’l-Muminin kwamba atawakumbusha hadithi ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na kuwataka waseme kwa jina la Allah kama hawakumsikia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akiisema: “Furaha ya Fatuma ni furaha yangu, hasira ya Fatima ni hasira yangu. Hivyo mwenye kumpenda binti yangu Fatima ananipenda mimi; mwenye kumfurahisha Faima ananifurahisha mimi. Mwenye kumchukiza Fatima, ananichukiza mimi.”

Wote wakasema: ‘Ndio tumesikia maneno hayo kutoka kwa Mtukufu Mtume wa Allah (s.a.w.w.).’ Kisha Fatimah akasema: ‘Namuomba Allah na malaika Wake kushuhudia kwamba ninyi wote mumenichukiza na hamkunitendea haki. Wakati nitakapokutana na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), hakika nitamlalamikia juu yenu ninyi wote.’

Abu Bakr Alitambua Uzito Wa Hasira Ya Fatimah

Abu Bakr akiwa ameguswa na maneno haya, alianza kulia na akasema: ‘Najikinga kwa Allah kutokana na hasira ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).’ Fatimah alianza kulia na alisema: “Naapa kwa jina la Allah kwamba nitaomba laana ya Allah iwe juu yenu katika sala zangu zote.’

Baada ya kusikia haya, Abu Bakr alitoka nje huku akilia, watu wakamzunguuka na kumliwaza. Yeye akawaambia: ‘Ole wenu. Ninyi wote mna raha, mmekaa na wake zenu kwa raha, lakini mimi niko katika hali hii ya unyonge. Sihitaji kiapo chenu. Kiondoeni kutoka kwangu.
Kwa jina la Allah, baada ya kile nilichokiona na kusikia kutoka kwa Fatimah, sitaki Mwislamu yeyote apate shida ya mzingo wa kiapo cha utii kwangu.’”

Riwaya hizi zilizosimuliwa na maulamaa wenu wenyewe wa kuheshimika, huonesha kwamba madhulumat Fatimah alikuwa amewakasirikia Abu Bakr na Umar mpaka saa ya mwisho ya uhai wake.

Fatima Alizikwa Usiku, Ikiwa Ni Ushahidi Wa Hasira Yake Ya Kudumu Kwa

Abu Bakr Na Umar

Ushahadi wa wazi kabisa wa hasira ya Fatimah kuhusiana na jambo hili, ni kwamba alimuusia mumewe Amiru’l-Mu’minin Ali kama ifuatavyo: “Asiruhusiwe hata mtu mmoja katika wale watu ambao walinidhulimu na kupora haki yangu, kushiriki katika mazishi yangu. Hakika ni maadui wangu na maadui wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Usimruhusu yeyote kati yao au washirika wao kusalia jeneza langu. Nizike usiku wakati watu wakiwa wamelala.”

Bukhari anaandika katika Sahih yake kwamba Ali alitekeleza wosia wa Bibi Fatimah na akamzika usiku kimya kimya. Watu walijaribu kwa bidii zao zote kutaka kujua alipozikwa Fatimah, lakini walishindwa kujua. Inakubaliwa na wote kwamba Fatimah alizikwa usiku kwa mujibu wa wosia wake. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliacha binti mmoja ili awe kama kumbukumbu yake.

Maulamaa wenu wanakubali kwamba alisema: “Fatimah ni sehemu ya mwili wangu. Yeye ni urithi na amana yangu. Mheshimuni yeye kama mnavyoniheshimu mimi. Kamwe msifanye kitu chochote kitakachoamsha hasira zake dhidi yenu. Kama anawakasirikia ninyi, mimi vile vile nitawakasirikia.”

Mir Sayyid Ali Hamadani Faqih Shafi’i anaandika katika kitabu chake, “Mawaddatu’l- Qurba” kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Wale ambao wanamkasirisha Fatimah nitawashughulikia kwa ukali sana Siku ya Hukumu. Furaha ya Fatimah ni furaha yangu, na hasira ya Fatimah ni hasira yangu.

Ole wake yule ambaye anakasirikiwa na Fatimah.” Huzuni ilioje kwamba matamko yote haya, umma si kwamba umempuuza tu, bali vilevile wamempokonya haki yake na kumsabibishia mateso makubwa.

Hata wakati ambapo alikuwa msichana mdogo, alitamka: “Nilipatishwa na matatizo mengi mno kiasi kwamba kama siku zingepatwa na matatizo kama hayo, basi zingegeuka kuwa usiku.”