read

Mkutano Wa Saba Jumatano Usiku 29 Rajab, 1345 A.H.

Sayyid Abdu’l-Hayy (Imam wa Msikiti wa jamaa wa Sunni): Mikesha fulani iliyopita ulitoa maelezo fulani ambayo kwamba Hafidh Sahib alitaka uthibitisho, lakini kwa ujanja ulikwepa kujibu au ulifanya watu miogoni mwetu wachanganyikiwe, na suala lote likawa ni lenye kukera.

Muombezi: Tafadhali nifahamishe ni lipi kati ya maswali yenu ambalo limeachwa bila kujibiwa, kwani sikumbuki ni suala gani unalolirejelea.

Sayyid: Wewe hukusema katika baadhi ya mikesha iliyopita kwamba Ali alikuwa na umoja wa ‘nafsi’ pamoja na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na hivyo alikuwa mbora wa cheo kwa mitume wote?

Muombezi: Ni kweli. Hayo yalikuwa ni maelezo yangu, na ni katika imani yangu.

Sayyid: Basi kwa nini hukujibu swali letu?

Muombezi: Umekosea sana. Inashangaza kwamba umekuwa ukisikiliza kwa ukaribu majadiliano yetu, lakini bado sasa unanilaumu kwa kuchukuwa njia ya ujanja au kuchanganya akili zenu. Kama utaangalia kwa makini utaelewa kwamba sijasema kitu chochote cha kupotosha, lakini ma-Mulla hawa wasomi waliuliza maswali ambayo nililazimika kuyajibu. Sasa kama una swali lolote la kuuliza, unaweza kufanya hivyo, na kwa msaada wa Allah, nitalijibu.

Sayyid: Tunataka kujua vipi inawezekanaje kwamba watu wawili wanaweza kuungana kiasi kwamba muungano wao unawafanya kuwa mtu mmoja na yule yule.

Tofauti Kati Ya Muungano Wa Kuwazika Na Muungano Halisi

Muombezi: Kwa hakika, haiwezikani kwa watu wawili kuunda muungano halisi. Wakati niliposema kwamba Amiru’l-Muminina Ali ana muungano wa “nafsi” pamja na Mtume, hupaswi kuuchukualia kama muungano halisi, kwa sababu kamwe hakuna mtu aliyedai hivyo, na kama mtu yeyote akiuamini atakuwa amekosea kabisa. Muungano nilioutaja ni wa kuwazika tu, sio halisi, na unakusudia kuonesha kwamba wote wawili wana ubora ule ule wa nafsi na muruwa, sio mwili huo mmoja.

Hafidh: Basi kwa mujibu wa kauli hii wote lazima watakuwa ni mitume, na kutokana na usemavyo, wahayi lazima utakuwa umekuja kwa wote.

Muombezi: Hiyo ni dhana potofu ya dhahiri. Hakuna Shi’a hata mmoja mwenye imani kama hiyo. Nisingetegemea wewe kujiingiza katika mazungumzo kama haya na kupoteza wakati wetu. Nimekuelezeeni tu kwamba wanahusiana katika masuala yote ya sifa na ubora, isipokuwa sifa zile ambazo kuziondoa kwake kuna amri au misingi makhususi.

Jambo hilo la pekee ni utume na sifa zake zote zilizoambatanishwa nao - mojawapo ikiwa ni upokeaji wa wahayi, na kwa kupitia huo ni mawasilisho ya Maamrisho ya Mungu.

Pengine umesahau maelezo yangu katika mikesha iliyopita, ambamo nilithibitisha kupitia Hadithi ya Cheo (Manzila) kwamba Ali alikuwa na cheo cha utume, lakini kwamba alifu- ata na alipasika kwenye dini na mafundisho yaliyofundishwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Cheo chake katika utume hakikuwa zaidi ya kile cha Harun wakati wa Musa.

Hafidh: Lakini kama unaamini katika usawa wa Ali pamoja Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) katika mambo yote ya sifa na ubora, inafuatia kwamba lazima uamini usawa wake katika masuala ya utume na sifa zilizoambatanishwa nao.

Muombezi: Inaweza kuelekea hivyo, lakini kama unafikiria kwa makini utaona kwamba sio hivyo. Kama nilivyothibibitisha mapema kutoka kwenye aya za Qur’ani, utume ni wa vyeo tofauti, na Manabii na Mitume wa Allah wanazidiana kati ya mmoja na mwingine katika ubora wa vyeo.
Kama Qur’ani Tukufu inavyoeleza kwa uwazi: “Mitume hao Tumewatukuza baadhi yao juu ya wengine…” (2:253). Na kikamilifu zaidi katika cheo kwa Mitume wote ni cheo maalumu cha Muhammad, kama Allah alivyosema: “Muhammad sio baba wa yeyote katika wanaume wenu, bali ni Mtume wa Allah na mwisho wa Manabii, na Allah ni mjuzi wa kila kitu” (33:40).

Ni kwa ukamilifu huo wa utume ambao umepelekea kwenye ukomo wa utume. Hivyo katika sifa hii ya ukamilifu, hakuna mtu yeyote anayeweza kujumuishwa humo. Katika mambo mengine yote ya ubora, kuna ushirikiano na usawa, ambao kwamba kuna uthibitisho mwingi.

Sayyid: Unaweza ukaleta hoja yoyote kutoka kwenye Qu’an kuthibitisha madai haya?

Aya Ya Maapizano (Mubahila) Inathibitisha Umoja Wa Nafsi Ya Ali Na Ya Mtukufu Mtume (S.A.W.W.)

Muombezi: Hakika, hoja yetu ya kwanza ni kutoka Qur’ani Tukufu, ambayo ni ushahidi wa ki-Mungu wenye nguvu sana, yaani aya ya maapizano (Ayatul-Mubahila) ambayo kwayo Allah anasema:

فَمَنْ حَاجَّكَ فِيهِ مِنْ بَعْدِ مَا جَاءَكَ مِنَ الْعِلْمِ فَقُلْ تَعَالَوْا نَدْعُ أَبْنَاءَنَا وَأَبْنَاءَكُمْ وَنِسَاءَنَا وَنِسَاءَكُمْ وَأَنْفُسَنَا وَأَنْفُسَكُمْ ثُمَّ نَبْتَهِلْ فَنَجْعَلْ لَعْنَتَ اللَّهِ عَلَى الْكَاذِبِينَ {61}

Watakao kuhoji katika haya baada ya kukufikia elimu hii waambie: Njooni tuwaite watoto wetu na watoto wenu, na wanawake zetu na wanawake zenu, na nafsi zetu na nafsi zenu, kisha tuombe kwa unyenyekevu tutake laana ya Allah iwashukie waongo.” (3:61)

Maulamaa wenu wakubwa, kama vile Imamu Fakhuru’d-Din Razi, Imamu Abu Ishaq Tha’labi, Jalalu’d-Din Suyuti, Qadhi Baidhawi, Jarullah Zamakhshari, Muslim bin Hujjaj, na wengine wengi, wameandika kwamba aya hii tukufu iliteremshwa siku ya maapizano, ambayo ilikuwa mwezi 24 au 25 Dhu’l-Hijja katika mwaka wa 9 A.H.

Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipowalingania Uislamu Wakristo wa Najran, wao waliwateua watu wao wenye elimu sana kama vile Seyyed, Aqib, Jasiq, Alqama na kadhalika, idadi yao ikiwa ni zaidi ya watu sabini na wakawatuma kwenda Madina pamoja na watu 300 kati ya wafuasi wao, ili kukutana na Mtukufu Mume na kujifunza Uislamu ulikuwa ni nini. Waliingia katika mjadala wa kielimu na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na walishangazwa na hoja zake nzito.

Alithibitisha ukweli wa ujumbe wake kutoka kwenye vyanzo vyao vyenye kuaminika na akasema kwamba, Isa mwenyewe alitabiri kuwasili kwake (Muhammad) kwa ishara mbali mbali, na Wakristo walikuwa wanangojea kutimia kwa utabiri wa Isa ambao kwa mujibu wake, mtu huyo atatokea akiwa amepanda ngamia kutokea milima ya Faran (katika Makka) na atahamia kwenye sehemu iliyopo kati ya ‘Ayr na Uhud (ambayo ilikuwa ni Madina).

Hoja hzi ziliwavutia sana Wakristo, lakini mapenzi yao ya heshima za kidunia yaliwazuia kuukubali ukweli. Basi Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliwaeleza amri ya Allah, ambayo walikubaliana nayo kama njia ya kumaliza mjadala na kwa ajili ya kubainisha kati ya wakweli na waongo.

Kuwasili Kwa Mtukufu Mtume (S.A.W.W.) Kwa Ajili Ya Maapizano

Kwa mujibu wa makubaliano yao ya pamoja, siku iliyofuatia kundi lote la Wakristo, pamoja na wanachuoni wao zaidi ya sabini, walimngojea Mtume nje ya milango ya Madina. Walitegemea kwamba yeye angekuja kwa fahari na idadi kubwa ya wafuasi wake ili kuwahofisha.

Lakini milango ilipofunguliwa, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alijitokeza akiwa na kijana wa kiume kuliani kwake, mwanamke mwenye heshima kushotoni kwake, na watoto wawili mbele yake.

Walibakia chini ya mti, wakiwakabili Wakristo. Asqaf, mtu mwenye elimu zaidi mwiongoni mwa Wakristo, aliuliza hao ni watu gani ambao Muhammad ame- toka nao.
Alijulisha kwamba kijana wa kiume ni mkwe wake na binamu yake, Ali Bin Abi Talib, yule mwanamke ni binti yake, Fatima, na watoto wawili ni watoto wa binti yake, Hasan na Husein.

Wakati akiwahutubia Wakristo, kiongozi wao, Asqaf, alisema: “Tazameni, jinsi Muhammad anavyojiamini! Amekuja pamoja na jamaa zake wa karibu, watoto, na wapenzi wake, kwenye shindano hili la kiroho la kuapizana. Kwa jina Mungu, kama angelikuwa na shaka au hofu kuhusu msimamo wake, kamwe asingewachagua hawa. Sasa siwashauri kuingia kwenye mashindano dhidi yake. Lau si kuwa na hofu na Mfalme wa Rumi, tungeikubali imani ya Uislamu. Ingelifaa zaidi kukubaliana nao juu ya masharti yao na kurudi nyumbani.” Wote walikabaliana naye. Kwa hiyo, Asqaf alituma ujumbe kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), akisema: “Hatutaki kushindana na wewe, bali tunataka kufanya amani na wewe.” Mtume alikubali mapendekezo yao.

Mkataba uliandikwa na Amiru’l-Muminin, Ali Ibn Abi Talib. Wakristo walikubali kulipa kodi ya mwaka katika muundo wa daraya 2,000, kila moja ikiwa na thamani ya takriban dirham 40 (dirham moja ilikuwa sawa na ½ wakia ya dhahabu), na mithqal 1000 za dhahabu (mithqal ilikuwa sawa na 1/6 wakia ya dhahabu).

Nusu ya hii ilkubaliwa ilipwe mwezi wa Muharram na nusu nyingine katika mwezi wa Rajab. Baada ya mkataba kusainiwa na pande zote, Wakristo walirudi nyumbani kwao. Wakati wakiwa njiani, mmoja wa wanachuo wao aitwaye Aqib alisema kuwaambia masahaba zake: “Kwa jina la Mungu, ninyi na mimi tunajua kwamba huyu Muhammad ni Mtume yule yule wa Mungu ambaye alikuwa akitazamiwa, na chochote anachosema kinatoka kwa Mungu.

Naapa kwa jina la Mungu kwamba yeyote aliyeshindana na Mtume wa Mungu aliangamia, na hakuna katika vijana wao na wazee wao aliyebakia hai. Kwa hakika kama tungeshindana nao, wote sisi tungeliuawa na asingebakia hai Mkristo yeyote ulimwenguni. Kwa jina la Mungu, wakati nilipowaangalia niliziona nyuso ambazo kama zingemuomba Mungu, wangeweza kusogeza milima.

Hafidh: Ulichosema ni kweli kabisa na kinakubaliwa na Waislamu wote, lakini hakina uhusiano na suala tunalojadili, yaani, kwamba Ali alikuwa ameungana kiroho na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Stahili Ya Ali, Fatima, Hasan Na Husein Inathibitishwa Na Aya Ya Maapizano

Muombezi: Ninahoji kutokana na neno “nafsi zetu” katika aya hii tukufu, kwani kutokana na aya hii masuala mengi yanatatuliwa.

Kwanza, njia ya haki iliyolinganiwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) imethibitishwa. Yaani, kama asingekuwa katika upande wa haki, asingethubutu kutoka kuja kwenye shindano wala wale Wakristo maarufu wasingelikimbia kutoka kwenye uwanja wa Mubahila.

Pili, vile vile aya hii huthibitisha kwamba Hasan na Husein walikuwa ni watoto wa Mtume wa Allah (s.a.w.w.) kama nilivyokwishataja katika mazungumzo yangu katika usiku wa kwanza.

Tatu, huthibitisha kwamba Amiru’l- Mu’minin, Ali, Fatima, Hasan na Husein walikuwa kiroho ndio watu watukufu zaidi miongoni mwa viumbe wote, na wapenzi mno wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), kwani hata wanachuoni washabiki na wapinzani wakubwa wa madhehebu yenu, kama Zamakhshari, Baidhawi, na Fakhru’d-Din Razi, na wengine wameandika katika vitabu vyao.

Hususani Jarullah Zamkhshari, akiandika kuhusu aya hii tukufu, anatoa maelezo yanayojitosheleza kuhusu kukusanyika kwa “viumbe watano” hawa na kusema kwamba, aya hii ni uthibitisho mkubwa wa ubora wa Ashab-i-Ayba, watu watano ambao walikusanyika chini ya blanketi pamoja na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Nne, inaonesha kwamba Amiru’l-Muminin, Ali aliwapita masahaba wengine wote kwa ubora na cheo, kwa sababu Allah amemuita katika aya hii tukufu kama nafsi ya Mtume. Ni dhahiri kwamba, maneno “nafsi zetu” hayamaanishi nafsi ya Mtume mwenyewe, kwa sababu kuita maana yake kumwita mtu mwingine; mtu kamwe haambiwi ajiite mwenyewe. Kwa hiyo, neno hili huelekeza kwa mtu mwingine ambaye ni kama nafsi ya Mtume mwenyewe.

Na kwa vile, kwa mujibu wa maoni ya pamoja ya wafasiri wa kuaminika na muhadithina wa madhehebu zote, hakuna mwingine yeyote isipokuwa Ali, Fatima, Hasani na Husein ndio walikuwepo pamoja na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) katika maapizano, usemi katika aya hii tukufu, “watoto wetu na watoto wenu, wanawake wetu na wanawake wenu” huashiria Hasan na Husein na Fatima kwa mpangilio huo, na mtu mwingine angeweza kutambuliwa kama “nafsi zetu” katika kundi hili tukufu alikuwa ni Amiru’l-Muminin, Ali. Kwa hiyo, maneno haya “nafsi zetu” huthibitisha muungano wa nafsi kati ya Mtume Muhammad na Ali.

Kwa vile mungano halisi wa nafsi mbili hauwezikani, Allah kumuita Ali ‘nafsi’ ya Mtume Muhammad maana yake ni muungano wa kutwaliwa wa nafsi mbili.

Unajua vizuri sana kwamba kimsingi ni bora kulitambua neno kwa dhana ya karibu kuliko na ile ya mbali, na dhana ya karibu sana maana yake kuhusiana katika fadhila zote isipokuwa zile ambazo zimeondolewa kwa sababu fulani. Na tayari tumekuambieni kwamba ni utume maalumu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na upewaji wa Wahyi juu yake, ambavyo ni vitu vya kipekee kwake tu. Kwa hiyo, hatumchukulii Ali kama mshirika wake kuhusiana na sifa hizi mbili.

Lakini kwa mujibu wa aya hii tukufu, Ali anashirikiana pamo- ja na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) katika fadhila nyingine zote, na kwa uhakika Allah (swt) amemjaalia Ali kupitia kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa baraka Zake zote. Hii peke yake inathibitisha muungano wa nafsi zao, ambao tulitaka kuuthibitisha.

Hafidh: Kwa nini unasisitiza kwamba aya hii haimaanishi kuita ‘nafsi’ yake mwenyewe? Kwa nini dhana hii isiwe bora kuliko dhana nyingine?

Muombezi: Ni matumaini yangu kwanba hutapoteza muda katika mazungumzo yasiyo na mantiki na kutoka nje ya njia ya uadilifu. Kwa kweli uadilifu huhitaji kwamba kama tumekubaliana juu ya nukta fulani, lazima tuendelee mbele. Sikutegemea mtu wa cheo chako na elimu yako kujiingiza katika mjadala bandia. Kama ujuavyo wewe mwenyewe na kwa mujibu wa wanachuoni wote, nafsi moja inafananishwa na nafsi nyingine kwa njia ya dhana. Miogoni mwa watu wasomi ni kawaida kudai muungano wa dhana, kama nilivyoeleza mwanzo.

Mara kwa mara inaonekana kwamba mtu mmoja anamuambia mwingine: “Wewe ni maisha yangu na nafsi yangu mwenyewe.” Hususan katika lugha ya hadith na simulizi, uhusiano huu mara kwa mara umekuwa ukielezewa kuhusu Amiru’l-Muminin, Ali, na kila simulizi kama hiyo ikuchukuliwa kwa peke yake ni uthibitisho wa kuonesha ukweli wa msimamo wangu.

Simulizi Zaidi Na Hadith Kama Ushahidi Wa Umoja Wa Msingi Wa Mtukufu Mtume (S.A.W.W.) Na Ali

Imamu Ahmad bin Hanbal, katika Musnad yake, Ibn Maghazili, mwanachuoni wa ki-Shafi’i katika Manaqib yake, na Muwafiq Ibn Ahmad Khawarizmi katika Manaqib yake, wanasimulia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Ali anatokana na mimi na mimi natokana na Ali; yeyote anayempenda yeye, amenipenda mimi; na ambaye ananipenda mimi, amempenda Allah.” Vile vile Ibn Maja katika Sunan yake, sehemu ya 1, uk. 92; Tirmidhi katika Sahih yake; Ibn Hajar katika kitabu cha Hadithi cha 5 cha “Hadithi Arobaini” zinazohusu fadhaila za Amiru’l-Muminin zilizosimuliwa katika Sawa’iq kutoka kwa Imamu Ahmad Bin Hanbal, Tirmidhi, Imamu Abu Abdu’r-Rahman Nisa’i, na Ibn Maja; Imamu Ahmad Bin Hanbal katika Musnad, juzuu ya 4, uk. 164; Muhamad Ibn Yusuf Ganji Shafi’i katika sura ya 67 ya Kifayatut-Talib kutoka Musnad ya Ibn Samak, juzuu ya 4, na Mu’jim Kabir cha Tibrani; na Imamu Abudu’r-Rahman Nisa’i katika Khasa’is, na Sulaiman Balkhi Hanafi katika Yanabiu’l-Mawadda kutoka kwenye Mishkat – wote wamesimulia kutoka kwa Jash Bin Junada as-Saluni kwamba wakati wa hijja ya muago, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema kule Arafa: “ Ali anatokana na mimi, na mimi natokana na Ali. Hakuna mtu anayenifidia mimi (yaani, hakuna awezaye kufanya kazi ya ujumbe wangu) isipokuwa mimi na Ali.”

Sulaimani Balkhi Hanafi katika Yanabiu’l-Mawaddat, sura ya 7, anasimulia kutoka Zawa’id-e-Musnad cha Abdullah Bin Ahmad Bin Hanbal kutoka kwa Ibn Abbas kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema kumuambia Ummu’l-Mu’minin Salma: “Ali anatokana na mimi na mimi natokana na Ali. Nyama yake na damu yake inatokana na nyama yangu na damu yangu. Yuko kwangu mimi kama alivyokuwa Harun kwa Musa. Ewe Umm Salma! Sikiliza, na uwe shahidi kwamba huyu Ali ni bwana na mkuu wa Waislamu.”
Hamidi katika kitabu chake Jam’Bainus-Sahihain na Ibn Abi’l-Hadid katika Sharhe- Nahju’l-Balagha wanasimulia kwamba, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Ali anatokana na mimi na mimi natokana na Ali. Ali kwangu mimi ni kama kichwa kilivyo kwa mwili; mtu anayemtii yeye, ananitii mimi; na mtu anayenitii mimi, anamtii Allah.”

Muhammad Bin Jarir Tabari katika Tafsir yake na Mir Sayyid Ali Hamdani, mwanachuoni wa ki-Shafi’i, katika Muwadda ya 8 cha Muwaddatu’l-Qurba, wanasimulia kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ambaye alisema: “Hakika Allah (swt) aliisaidia imani hii ya ki-Islamu kupitia Ali, kwa vile yeye anatokana na mimi, na mimi natokana na yeye, na aya hii tukufu imeteremshwa kwa ajili yake.

‘Basi je, yeye ni kama mtu ambaye ana dalili za wazi kutoka kwa Mola wake na kufuata ushahidi kutoka Kwake?’” (11:17)

Sheikh Sulaimani Balkhi Hanafi ameainisha katika sura ya 17 ya kitabu chake Yanbiu’l-Mawdda kuhusu suala hili hili chini ya maelezo mafupi: “Kuhusu Ali kuwa kama nafsi ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na hadithi kwamba Ali anatokana na mimi, na mimi natokana na Ali.’” Katika sura hii amesimulia hadithi 24 katika njia tofauti na kwa maneno tofauti kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), ambaye alisema Ali alikuwa kama nafsi yake mwenyewe.

Kuelekea mwishoni mwa sura hii, alisimulia hadithi kutoka kwenye Manaqib kama ilivyosimuliwa na Jabir, ambaye alisema kwamba, alimsikia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akisema kwamba, Hadhrat Ali anazo sifa ambazo kwamba kama mtu anakuwa na moja kati ya hizo, ingelitosha kuthibitisha murwa wa mtu huyo na ubora wake.

Na kwa sifa hizo ilimaanishwa hadithi za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kuhusiana na yeye kama vile: “Yeyote yule ambaye mimi ni mwenye kumtawalia mambo yake basi huyu Ali ni mwenye kutawalia mambo yake”, au “ Ali yuko kwangu mimi kama alivyokuwa Harun kwa Musa”, au “Ali anatokana na mimi na mimi natokana na Ali” au “Ali yuko kwangu mimi kama nafsi yangu ilivyokuwa kwangu, utii kwake ni utii kwangu”, au “Kupigana dhidi ya Ali ni kupigana dhidi ya Allah, na kufanya amani na Ali ni kufanya amani Allah”, au “Rafiki wa Ali ni rafiki wa Allah, na adui wa Ali ni adui wa Allah”, au Ali ni Hujjat (udhihirisho) wa Allah juu ya viumbe Wake”, au “ Mapenzi kwa Ali ni imani, na uadui dhidi yake ni ukafiri”, au “Kundi la Ali ni kundi la Allah, nakundi la maadui wa Ali ni kundi la Shetani;” au “Ali yuko pamoja na haki, na haki pamoja naye, (na hivyo) havitengani”, au “ Ali ndiye mgawaji wa Pepo na Moto”, au “Mtu anayejitenga na Ali, amejitenga na mimi, na anayejitenga na mimi, anajitenga na Allah”, au “Wafuasi wa Ali wataokolewa Siku ya Hukumu.”

Mwishowe, alinukuu hadithi nyingine yenye maelezo marefu kutoka kwenye Manaqib ambayo mwishoni mwake Mtume anasema: “Naapa kwa jina la Allah ambaye ameweka utume juu yangu, na kunifanya mimi mbora wa viumbe Wake: Ewe Ali! Hakika wewe ni Hujjat (udhihirisho) wa Allah kwa ajili ya watu, mdhamini Wake, mjuzi wa siri Zake, na Khalifa juu ya waja Wake.”

Kuna hadithi nyingi kama hizo kwenye vitabu vyenu. Maneno “nafsi zetu” kwa uwazi huonesha ushirikiano wa karibu kati ya Mtume na Ali katika masuala yote ya ubora.

Nafikiri kwamba aya hii ni ushahidi tosha wa msimamo wangu. Aidha, swali lako la pili linajibiwa na aya hiyo hiyo. Tumethibisha kwamba, ukiondoa utume na Wahyi, ambavyo vinamhusu Mtume tu peke yake, Ali alishirikishwa pamoja naye katika masuala yote ya ubora. Vile vile ina maana kwamba katika sifa za hali ya juu za ubora Ali alikuwa mbora zaidi ya Masahaba na kwa mtu yeyote katika umma huu. Kwa hakika aya hii inathibitisha kwamba anawapita Mitume wote wengine waliopita, kama vile ambavyo Mtume anawapi- ta Mitume wote wengine.

Kwa Vile Mtukufu Mtume Alikuwa Mbora Kwa Mitume Wote Wengine Na Ali Pia Alikuwa Mbora Kwao

Katika Ihya’u’l-Ulum ya Imam Ghazali, Sharhe Nahjul-Balaghah ya Ibn Abil-Hadid Mu’tazil, Tafsir ya Imam Fakhrud-Din Razi, na Tafsir za Jarullah Zamakhshari, Baidhawi, Nishapuri na kadhalika, utaikuta hadith hii ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): “Wanachuoni wa umma wangu ni kama mitume wa Bani-Israili.” Katika hadith nyingine amesema: “Ulamaa wa umma wa Mtukufu Mtume walikuwa sawa au bora kuliko mitume wa Bani-Israil kwa sababu tu kwamba chanzo chao cha elimu kilikuwa ndio kiini hasa cha elimu, Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w.).

Kwa hiyo, Ali ibn Abi Talib bila shaka alikuwa mbora kwa mitume, kwa vile Mtukufu Mtume amesema: “Mimi ni Jiji la elimu na Ali ni lango lake.” Vile vile amesema: “Mimi ni nyumba ya hekima na Ali ni lango lake.” Wakati Ali mwenyewe alipoulizwa kuhusu jambo hili, yeye alieleza baadhi ya vipengele vya ubora wake kwa mitume wa Bani-Israil.

Mnamo mwezi 20 ya Ramadhan, wakati Ali alipokuwa katika kitanda chake cha umauti kufuatia lile shambulizi la Abdul-Rahman Ibn Muljim Muradi, alimtuma Imam Hasan kuwaita wale Mashi’a waliokuwa wamejikusanya kwenye mlango wa nyumba yake. Walipoingia ndani, walikuzunguka kitanda chake huku wakilia kimya kimya. Ali akasema: Mnaweza kuuliza swali lolote mnalolitaka kabla sijakuacheni, lakini maswali yenu yawe mafupi.” Mmoja wa wale waliokuwepo pale alikuwa ni Sa’sa’a bin Suwhan.

Wanachuoni wenu maarufu kabisa kama Ibn Abdul-Birr na Ibn Sa’ad, wameandika kuhusu maisha na tabia yake, wamemtegemea yeye Sa’sa’a, wakithibitisha kwamba yeye alikuwa ni mtu mwenye elimu kubwa.

Sa’sa’a alimwambia Ali: “Naomba unifahamishe ni nani mbora, ni wewe au Adam.” Imam Mtukufu akasema: “Haifai kwa mtu kujisifia mwenyewe, lakini kulingana na kauli adili- fu: ‘Na neema za Mola Wako alizokujaalia zisimulie,’ ninakwambia kwamba mimi ni bora kuliko Adam.” Alipoulizwa ni kwa nini imekuwa hivyo, Ali alieleza kwamba Adam alikuwa na kila namna ya huruma, starehe na neema kwa ajili yake ndani ya Pepo.

Alitakiwa tu kujizuia kutokana na chakula kile kilichokatazwa. Lakini hakuweza kujizuia na akala kutoka kwenye mti ule. Matokeo yake yeye alifukuzwa kutoka peponi. Mwenyezi Mungu hakumkataza yeye Ali kutokana na kula ngano (ambayo, kwa mujibu wa imani ya Kiislam ndio ‘mti’ uliokatazwa).

Lakini kwa kuwa yeye hakuwa na mwelekeo kwenye dunia ya mpito, yeye alijizuia kwa hiari yake mwenyewe kula ngano. (Hoja ya kauli hii ya Ali ilikuwa kwamba ubora wa mtu mbele ya Mwenyezi Mungu ulitegemea kwenye uchamungu na utii, na kwamba kilele cha uchamungu kinaegemea katika kujizuia hata kwa kile ambacho kinaruhusiwa kihalali).

Sa’sa’a akauliza: “Ni nani mbora, wewe ama Nuh?” Ali akajibu: “Mimi ndiye mbora. Nuh aliwalingania watu wake kumuabudu Mwenyezi Mungu lakini hawakutii. Kitendo chao cha aibu kilikuwa ni kumtesa yeye. Yeye aliwalaani na akamuomba Mwenyezi Mungu:

‘Ewe Mola Wangu! usiabakishe hata mtu mmoja juu ya ardhi miongoni mwa madhalimu hawa.’ Baada ya kifo cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), ingawaje watu walinisababishia matatizo makubwa, mimi sikuwalaani kamwe. niliyabeba mateso yao kwa subira kubwa.” Sa’sa’a akauliza: “Ni nani aliye mbora, wewe ama Ibrahim?” Ali alijibu: “Mimi na mbora, kwani Ibrahim alisema:

‘Mola Wangu! nionyeshe jinsi unavyofufua wafu. (Mungu) Akasema: Kwani huamini? Akasema: Hasha! bali ili moyo wangu utue ..... (2:260) Imani yangu ilikuwa kiasi kwamba nilisema: ‘Hata kama pazia la yale yaliyo ghaibu linge- funuliwa, imani yangu isingeongezeka.’”

Sa’sa’a akauliza: “Ni nani mbora, wewe au Musa?” Imam Mtukufu akajibu: “Mimi ndiye mbora, kwani wakati Mwenyezi Mungu Mtukufu alipomtuma Musa kwenda Misri kumlingania Firauni kwenye haki, Musa alisema: ‘Mola Wangu! Kwa hakika niliuwa mmoja wao, kwa hiyo naogopa wataniuwa. Na ndugu yangu Harun ni fasihi zaidi ulimi wake kuliko mimi. Basi mtume aende pamoja nami kunisaidia, ili anisadikishe. Hakika mimi na hofu watanikadhibisha.’ (28: 33-34)

Mtukufu Mtume aliniagiza mimi, kwa amri ya Allah kwenda Makka kuzisoma aya za Sura ya Al-Bara’a kutoka juu ya Ka’aba kwa makafiri wa Quraishia.

Mimi sikuwa na hofu, ingawaje kulikuwa na watu wachache ambao walikuwa hawajapoteza ndugu yao wa karibu kwa upanga wangu. Kwa kuitii amri yake, niliitekeleza kazi hiyo peke yangu. Nilizisoma aya za al-Bara’at na nikarejea.”
Sa’sa’a akauliza tena: “Ni nani mbora, wewe au Isa (ibn Mariam)?” Ali akasema: “Mimi ni mbora, kwani wakati Mariam alipokuwa mjamzito kwa Rehma za Mwenyezi Mungu, na wakati wake wa kujifungua ukakaribia, ulishushwa wahyi kwake: ‘Ondoka katika Nyumba hii tukufu, kwani Nyumba hii ni nyumba ya ibada, sio mahali pa kuzalia watoto.’

Matokeo yake aliondoka kwenye Nyumba tukufu hiyo na akaenda kwenya kichaka ambako alijifungua mtoto Isa. Lakini wakati mama yangu mimi, Fatima binti al-Asad, alipojisikia uchungu wa uzazi ndani ya eneo la Ka’aba tukufu, aling’ang’ania kwenye ukuta na akamuomba Mwenyezi Mungu kwa jina la Nyumba ile na mjenzi wa Nyumba ile, ili apunguziwe maumivu yake. Mara ufa ukajitokeza katika ukuta huo, na mama yangu akasikia sauti ya kimuujiza ikimwambia, “Ewe Fatima! Ingia kwenye Nyumba ya Ka’aba.” Yeye akaingia ndani na mimi nikazaliwa ndani ya Ka’aba tukufu.’”

Kioo Cha Mitume Yote Kama Ilivyoonyeshwa Na Hadith Ya Ufananisho

Imesimuliwa vilevile katika vitabu vya ulamaa wenu kwamba Ali alikuwa ni kioo cha sifa za hali ya juu za mitume wote waliotangulia. Ibn Abil-Hadid Mu’tazili ndani ya Sharhe Nahjul-Balaghah yake, Jz. 11, uk. 449, Hafidh Abu Bakr Faqih Shafi’i, Ahmad bin Husein Baihaqi katika Manaqib, Imam Ahmad bin Hanbal ndani ya Musnad, Imam Fakhrud-Din Razi katika Tafsir al-Kabir kuhusiana na aya ya Mubahila, Muhui’d-Din Ibn Arabi ndani ya Yawaqit al-Jawhir, suala la 32, uk. 172; Sheikh Suleyman Balkhi Hanafi katika Yanabiul-Mawadda, mwanzoni mwa Sura ya 40 kwa idhini ya Musnad ya Ahmad bin Hanbal, Sahih ya Baihaqi, na Sharhil-Mawaqif wat-Tariqatil-Muhammadiyya, Nuru’d-Din Maliki katika Fusulul-Muhimma, uk. 120; kutoka kwa Baihaqi; Muhammad bin Talha Shafi’i ndani ya Matalibus-Su’ul uk. 22; na Muhammad bin Yusuf Ganji Shafi’i katika Kifayatut-Talib, Sura ya 23, wamesimulia kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) pamoja na tofauti kidogo ya maneno, hapa na pale, akisema kwamba: “Yeyote anayetaka kuiona elimu ya Adam, uchamungu wa Nuh, unyenyekevu wa Ibrahim, utukufu wa Musa, au ule utiifu wa Isa (Yesu), anaweza kumuangalia Ali ibn Abi Talib.”

Mir Seyyed Ali Hamadani amesimulia hadith hiyohiyo pamoja na nyongeza kidogo katika Mawaddatul-Qurba yake, Mawadda 8. Anasimulia kutoka kwa Jabir kwamba Mtume (s.a.w.w.) amesema. “Kwa hakika Mwenyezi Mungu amekusanya sifa tisini za mitume kwa Ali, ambazo hakumpa mtu mwingine yeyote.”

Yule Hafidh mkubwa Muhammad bin Yusuf Ganji Shafi’i, baada ya kunukuu hadith hii, anatoa maelezo haya: “Ali alikuwa sawa na Adam katika elimu kwa vile Mwenyezi Mungu amemfundisha Adam kila kitu, kama anavyosema ndani ya Qur’ani Tukufu, ‘Na akamfundisha Adam majina .....’(2:31).

Hali kadhalika, Ali alikuwa na elimu ya mambo yote. Kwa sababu ya elimu iliyoshuka moja kwa moja kutoka kwa Allah swt., Adam alipewa ukhalifa wa Allah, kama Qur’ani tukufu inavyosema: “..... Nitajaalia khalifa juu ya ardhi..... (2:30).

Kwa kuwa elimu ya Adam iliongozea kwenye ubora wake, hivyo kwamba hata Malaika walisujudu kwa heshima juu yake, Ali pia alikuwa mtukufu sana wa viumbe wote na khalifa baada ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Elimu ya Ali ni sawa na ya Nuh kwa vile Ali alikuwa mkali dhidi ya makafiri na mpole kwa waumini. Allah amemsifia ndani ya Qur’ani:

“Na wale walio pamoja naye wana nyoyo imara dhidi ya makafiri, na wapole miongoni mwao wenyewe.” (48: 29).

Huu ni ushahidi mwingine kwamba aya hii ilishuka kwa kumsifia Ali, kama nilivyosema mapema. Nuh alikuwa mkali sana kwa makafiri, kama Qur’ani tukufu anavyosema: “Na Nuh akasema: ‘Mola Wangu! usibakishe hata mkazi mmoja juu ya ardhi miongoni mwa makafiri.’” (71:26).

Ali alikuwa sawa na Ibrahim katika utulivu wa moyo. Qur’ani tukufu inasema: “Kwa hakika, Ibrahim alikuwa mpole sana wa moyo.” (9:114).

Ali alikuwa na sifa zote ambazo Mitume wengine walikuwa nazo mmoja mmoja. Hadithi hii inayokubaliwa na wote huthibitisha kwamba Ali alikuwa na fadhail za hali ya juu sana, ambazo kila moja ya hizo ilikuwa sawa na sifa za juu sana za Mitume.
Ni wazi kwamba, mtu ambaye alikuwa na fadhaila za juu sana za mitume wote, basi aliwapita wote kwa cheo. Sheikh Sulayman Balkhi Hanafi katika Yanabiu’l-Mawadda, Sura ya 40, ananukuu kutoka kwenye Manaqib ya Khawarizmi kutoka kwa Muhammad Bin Mansur, ambaye alisema kwamba alimsikia Ahmad Ibn Hanbal akisema: “Kulikuwa hakuna sifa kama hizo kwa Sahaba yeyote wa Mtume, kama zilivyokuwa kwa Ali Bin Abu Talib.”

Muhammad Bin Yusuf Ganji Shafi’i vile vile anasimulia maneno yenye maana hiyo hiyo. Ibn Abi’l-Hadid Mu’tazali katika Sharhe-Nahju’l-Balagha, juzuu ya 1, uk. 46, anasema: “Ali alikuwa ndiye mtu mwenye kufaa sana katika nafasi ya Wilaya (Ulinzi) kwa fadhaili za ubora wake. Ukimuondoa tu Mtume wa Allah, alikuwa ni mtu mwenye kustahiki sana kwa cheo cha Khalifa.”

Ali kwa hakika alikuwa mwenye kustahiki zaidi kwa Ukhalifa, lakini aliwekwa kando kwa mbinu za kisiasa za watu duni. Angalau wangelimjulisha Ali kwamba walikuwa wakifanya mkutano huko Saqifa Bani Sa’da kuangalia juu ya suala muhimu la kumchangua Khalifa. Hawakufanya hivyo ili kumnyima haki yake ya urithi.

Kukubaliwa Kwa Abu Bakr Na Watu Wote

Hafidh: Je, sisi ni madhalimu au ni wewe? Unasema kwamba masahaba waliwachagua wale ambao wamepora Ukhalifa. Kwa hakika unafikiri kwamba sisi ni wajinga ambao kibubusa tunawafuata wazee wetu. Lakini kuna uthibitisho gani wenye nguvu kama “Ijma” – makubaliano ya wote kwa ujumla? Masahaba wote na Umma, pamoja na Ali, walimchagua Abu Bakr na wakala kiapo cha utii kwake.

Kwa hakika makubaliano ya pamoja ya watu ni ya mwisho na kukubaliana nayo ni lazima. Mtume alisema: “Watu wangu hawakubaliani katika (jambo lenye) kosa; watu wangu hawakubaliani katika upotofu wa kutoka kwenye njia iliyonyooka.” Hivyo hatukuafuata wazee wetu kibubusa. Ukweli ni kwamba katika siku ya kwanza baada ya kifo cha Mtume, Umma kwa pamoja uliamua katika mkutano kumsimamisha Abu Bakr kama Khalifa. Kwa sababu ilikuwa ni ukweli uliokubaliwa, lazima na sisi tuukubali.

Mumbezi: Tafadhali tujulishe Ukhalifa umeegemezwa katika misingi ipi?

Hafidh: Iko wazi. Uthibitisho mzuri wa kuwepo ukhalifa baada ya Mtume ni “Ijma” (makubaliano ya wote kwa ujmla) ya Umma ambayo kwayo ukhalifa umekuja kupatikana. Mbali na haya, sifa bora sana kwa Abu Bakr na Umar kwa ajili ya ukhalifa ilikuwa ni kuko- maa kwao kiumri. Ali, pamoja na fadhaili zote na ukaribu kwa Mtume, ilikuwa arukwe kwa sababu ya ujana wake.

Na, ili kuwa waadilifu na wenye haki, haikuwa sawa kwa kijana kuyaweka pembeni madai ya masahaba watu wazima. Na hatuchukilii kuachwa huku kwa Ali kama ni kushindwa kwake, kwani ubora wake kwa upande mwingine hukubaliwa na wote. Vile vile kuna hadithi iliyosimuliwa na Khalifa Umar kutoka kwa Mtume, ambaye alisema: “Utume na uongozi haviwekwi pamoja katika familia moja.” Kwa hiyo, Ali alinyimwa ukhalifa kwa sababu anatokana na familia ya Mtume. Alikuwa hafai kwa ajili ya cheo hicho.

Hoja Dhidi Ya Uhalali Wa “Ijmai”

Muombezi: Nimeshangaa kwamba unaweza kuleta hoja za kijinga kama hizi. Kwanza, unasema kwamba Ijmai, makubaliano ya Umma, ndio hoja yenye nguvu zaidi, na kwa kuunga mkono nukta yako umesimulia hadithi. Neno ‘ummai’ maana yake ‘umma wangu,’ hivyo hadithi hiyo (tujaalie kuwa ni ya kweli) inamaniisha kwamba wakati umma wote unapokubaliana kwenye jambo fulani, uamuzi wao hauwezi kuwa na makosa. Siwezi kukubaliana na hili. Allah aliutofautisha ummah huu kwa sababu ya ukweli kwamba mion- goni mwao kutakuwepo na kundi lililoongoka. Mwakilishi wa Allah atakuwa miongoni mwao. Wakati umma unapokusanyika pamoja, kundi lile lililoongoka litakuwa miongoni mwao.

Lakini hadithi hii (hata kama ni ya kweli) haioneshi ushahidi wowote kwamba Mtume aliitoa haki yake mwenyewe na kuruhusu ummah kuchagua Khalifa. Na hata kama Mtume alikuwa ameuchia ummah kuchagua Khalifa, haki hii itakuwa inaachiwa ummah wote. Kwa vile Waislamu wote hunufaika kutokana na Ukhalifa, lazima wangelikuwa na haki ya kuelezea maoni yao katika kumchagua Khalifa. Kwa hiyo, kukusanyika kwa ummah wote baada ya Mtume kufariki kungelikuwa muhimu ili kwamba kwa idhini yao ya pamoja, mtu mkamilifu angeweza kuchaguliwa kuwa Khalifa.
Je, kulikuwapo na mkusanyika kama huo wa Waislamu? Je, hii ndiyo njia ambayo Abu Bakr aliyofikia kuwa ukhalifa?

Hafidh: Abu Bakr alibakia kwenye ukhalifa kwa zaidi kidogo ya miaka miwili. Wakati wa kipindi hiki Waislamu kwa jumla walikula kiapo cha utii kwake. Hii yenyewe ina maana ya maoni ya pamoja miongoni mwao, ambayo ni uthibitisho wa uhalali wa Ukhalifa wake.

Muombezi: Unajaribu kuliepuka suala lenyewe. Swali langu halikuwa kuhusu kipindi chote cha Abu Bakr. Nilikuwa nauliza kuhusu uamuzi uliochukuliwa katika Saqifa ya Bani Sa’da. Je, mkusanyiko ule pale ulikusanya ummah wote, au kulikuwa na watu wachache tu ambao walikula kiapo cha utii?

Hafidh: Ni dhahiri kwamba kulikuwa na masahaba wachache mashuhuri wa Mtume, laki- ni baadae Ijmai ilipita.

Muombezi: Je, Mtume, mtu anayefaa zaidi kuongoza ummah, aliitoa haki yake kwa upande wa ummah wake? Je, alitoa haki yake ili kwamba watu wa ukoo wa Aus, ambao walikuwa maadui kwa ukoo wa Khazraj, wale kiapo cha utii kwa ajili ya hofu ya maadui wao kushika madaraka? Je, aliacha haki yake ili kwamba watu wake waunde serikali kwa misingi ya hofu na ulafi? Je, unaweza kuita kikundi hiki kidogo cha watu kuwa ndio ummah? Je, Waislamu wa Makka, Yemen, Jeddah na miji mingine hawakuwa sehemu ya ummah? Je, hawakuwa na haki ya kutoa maoni yao kuhusiana na ukhalifa? Kama kulikuwa hakuna hila, kwa nini wasingojee na kupata msimamo wa Waislamu wote katika suala muhimu kama hili la Ukhalifa? Katika njia hii, Ijmai kwa maana yake halisi ingewza kupatikana. Hata leo, ili kusimamisha serikali ya kidemokrasi au kuchagua kiongozi wa taifa, hufanyika uchaguzi mkuu.

Wananchi wanapiga kura zao, na kiongozi anachaguliwa kwa wingi wa kura. Viongozi wa nchi zilizostaarabika na watu wote wastaarabu watauche- ka utaratibu wenu huu wa “Ijmai” usio na mpangilio mzuri.

Hafidh: Kwa nini unajiigiza katika mazungumzo yasiyopendeza? Ijmai ina maana kwamba kulikuwa na mkusanyiko wa watu wenye akili na masahaba wakubwa ambao waliku- tana ndani ya Saqifa.

Muombezi: Unasema kwamba Ijmai ilimaanisha kwamba kulikuwa na mkusanyiko wa watu wenye akili na masahaba wakubwa wa Mtume, lakini huna msingi wowote kwa maelezo haya isipokuwa hadithi uliyoitaja. Ni wapi hadithi imetaja watu wenye akili au masahaba wakubwa? Narudia kwamba neno “umma” maana yake ni umma wote, sio idadi ndogo ya Masahaba, hata kama wakiwa wana elimu.

Hata kama unayosema yakiwa ni kweli, kwamba “Ijmai” maana yake “mkusanyiko wa watu wenye akili na masahaba wakubwa,” je, watu wenye akili na masahaba wakubwa wa Mtume walikomea kuwa ni hao watu wachache tu ambao walikusanyika chini ya paa dogo la Saqifa siku hiyo? Je, kulikuwa hakuna watu wengine wenye akili na masahaba wakubwa katika ulimwengu wa ki-Islamu? Na je, wote kwa pamoja walipiga kura kwa ajili ya Khalifa?

Hafidh: Kwa vile suala la Khalifa lilikuwa ni jambo nyeti, watu walikuwa wanahofia kwamba huenda kukatokea machafuko. Ilikuwa haiwezekani kuwaarifu Waislamu katika sehumu nyingine. Wakati Abu Bakr na Umar waliposikia kwamba baadhi ya Ansar wamekusanyika kule, na wao vile vile walikwenda kule kuzungumza. Kwa sababu Umar alikuwa mwanasiasa mweledi, aliona kwamba inafaa kwa ummah kula kiapo cha utii kwa Abu Bakr.

Wengine walimfuata na kula kiapo cha utii kwa Abu Bakr, lakini kikundi cha Ansar na watu wa ukoo wa Khazraj wanaomuunga mkono Sa’d Bin Ubaida, hawakula kiapo cha utii na wakaondoka Saqifa. Hiyo ndio ilikuwa sababuya kwa nini walifanya haraka.

Muombezi: Hivyo na wewe unakubali, kama wanahistoria na maulamaa wenu walivyokubali, kwamba katika siku ya Saqifa, wakati mashauri ya msingi yalipokuwa yanafanyika kulikuwa hakuna “Ijmai”. Kwa ajili ya maslahi ya kisiasa, Abu Bakr alimpendekeza Umar na Abu Ubaida Bin Jarra, na wao pia, kwa kulirudisha pendekezo hilo, wal- itaja jina la Abu Bakr, wakimuambia kwamba yeye anastahiki zaidi kwa nafasi hiyo. Wao mara moja tu wakala kiapo cha utii kwake.

Baadhi ya watu wa ukoo wa Aus waliokuwa pale vile vile walikula kiapo cha utii kwa Abu Bakr kwa msimamo wao wa uadui dhidi ya ukoo wa Khazraj, na vile vile walihofia kwamba Sa’d bin Ubaida angeweza vinginevyo kuwa Amir. Kwa njia hii uungaji mkono ulipanuka na kuwa mkubwa. Hata hivyo, kama Ijmai ingekuwa ni hoja yenye nguvu kuweza kutegemewa, wangelisubiri mpaka umma wote – au, kama ulivyosema: watu wenye akili – wakusanyike pale kupata idhini ya umma wote.

Hafidh: Nimekuambia kwamba hofu ya machafuko ililazimisha kundi hili kutenda kama walivyofanya. Watu wa ukoo wa Aus na Khazraj wamekusanyika katika Saqifa na walikuwa wakigombana wenyewe kwa wenyewe. Kila mmoja wao anataka kuamua uhuru wa dola ya ki-Islamu kwa ajili yao wenyewe.

Muombezi: Nakubaliana na unayoyasema. Muhammad Bin Jarir Tabari (tazama Ta’rikh yake, Jz. 2, uk. 457) na wengine wameandika kwamba, Waislamu hawakukusanyika chini ya Saqifa kumchagua Khalifa wao. Koo za Aus na Khazraj zilitaka kujichagulia Amir wao wenyewe. Abu Bakr na Umar wakanufaika kutokana na tofauti zao.

Kama kweli walikusanyika kujadili Ukhalifa, kwa kweli wangeliwaita Waislamu wote kutoa maoni yao juu ya suala hilo. Kama ulivyosema: Hawakuwa katika hali ya kuweza kuwajulisha Waislamu wote, na muda ulikuwa unakimbia. Ilikuwa kweli kwamba walikuwa hawana mawasiliano ya mara moja na Makka, Yemen, Ta’if, au miji mingine ya mbali ya Waislamu.

Lakini je, walikuwa hawana hata njia ya kuwasiliana hata na Jeshi la Usama Bin Zaid, ambalo lilikuwa limepiga kambi nje kidogo ya Madina? Hivi wasingeweza kuwaarifu masahaba wakubwa wa Mtume ambao walikuwa kule? Mmoja wao alikuwa mtu maarufu, Kamanda wa jeshi la Waislamu, aliyechguliwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mwenyewe. Abu Bakr na Umar walikuwa chini yake.

Wakati Usama aliposikia kwamba, kwa hila watu watatu wamemchagua Khalifa bila kuwashauri watu wengine, au hata kuwajulisha, na kwamba walikuwa wamekula kiapo cha utii kwa mtu moja, alipanda farasi wake mpaka kwenye mlango wa Msikiti na akesema kwa sauti kubwa: “Vurugu yote hii ni ya nini? Kwa amri ya nani mmemchagua Khalifa? Kulikuwa na umuhimu gani, wa watu wachache ambao bila kuwashauri masahaba, wamemchagua Khalifa?”

Umar akajitokeza mbele kumtuliza na kusema: “Usama! Kazi hiyo imekwisha. Kiapo cha utii kimekwishatolewa. Usisababishe vurugu sasa miongoni mwa watu.

Na wewe mwenyewe pia ule kiapo cha utii.” Usama akakasirika, na kusema: “Mtume amenifanya mimi Amir wenu,” akasema. “Inawezekana vipi Amir aliyeteuliwa na Mtume atoe heshima ya utii kwa watu wa chini ambao waliwekwa chini ya amri yake?” Ingawa mengi zaidi yalitokea, kiasi hiki kidogo kinatosha kuthibitisha hoja yangu.

Ali Alikosa Kuarifiwa Kwa Makusudi Kuhusu Mkutano Wa Saqifa

Kama unasema kwamba Jeshi la Usama vile vile lilikuwa mbali na mji wa Madina na kwamba muda ulikuwa unakimbia, je, utadai kwamba umbali kutoka Saqifa na Msikitini na kwenye makazi ya Mtume vile vile ulikuwa mkubwa? Kwa nini hawakumuarifu Ali, au Abbas ami yake Mtume mwenye kuheshimiwa? Kwa nini hawakuwashauri Bani Hashim, kizazi cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)?

Hafidh: Katika namna zote hali wakati ule ilikuwa ngumu kiasi kwamba hawakuthubutu kuwa wazembe na kuondoka Saqifa.

Muombezi: Samahani, walikuwa nao muda wa kutosha. Waliacha makusudi kumuarifu Ali, Bani Hashim, na masahaba wakubwa.

Hafidh: Unasemaje kwamba walifanya makusudi kuacha kuwaarifu?

Muombezi: Dalili moja ya wazi ni kwamba Umar alifika kwenye mlango wa nyumba ya Mtume lakini hakuingia ndani.

Hafidhi: Kwa hakika kisa hiki kimebuniwa na Marafidhi.

Muombezi: Angalia ukurasa wa 456 Ta’rikh, ya Muhammad Bin Jarir Tabari, Jz. 2, mmoja wa Maulamaa wenu wakubwa. Anaandika kwamba Umar alifika mlangoni kwa nyumba ya Mtume lakini hakuingia ndani. Alituma ujumbe kwa Abu Bakr: “Njoo haraka; nina shughuli muhimu na wewe.” Abu Bakr akamtumia jibu kwamba hakuwa na muda. Umar akutuma ujumbe mwingine: “Tunakabiliwa na mgogoro. Kuwepo kwako ni muhimu.” Abu Bakr akatoka nje na Umar akamueleza kwa siri kuhusu kukusanyika kwa Ansar ndani ya Saqifa na akasema kwamba walipaswa kwenda huko mara moja.

Wote wakaondoka, na njiani wakakutana na Abu Ubaida wakamchukuwa na kuongozana naye. Kwa ajili ya Allah hebu jaribu kuwa muadilifu. Kama walikuwa hawakupanga njama, kwa nini Umar aende mpaka kwenye mlango wa nyumba ya Mtume na kisha asiingie ndani? Wangeliweza kuomba msaada. Je, katika Umma wote alikuwepo Abu Bakr tu, ambaye alikuwa na hakima zote, na kwamba masahaba wengine na kizazi cha Mtume walikuwa ni wageni ambao hawakustahiki kujulishwa kuhusu suala hili?

Je, Ijma yenu hii kwa haki inaundwa na watu watatu? Ni wapi katika sehemu yoyote ya ulimwengu ambako utaratibu kama huu unakubalika? Tuchukulie kwamba watu watatu au kikundi chochote cha watu, wakakusanyika katika mji na wakaunda Ijma na kisha wakamchagua kiongozi wa nchi.

Je, ni wajibu juu ya Maulamaa na wasomi wa miji mingine yote kuwatii? Au hata kama baadhi ya watu wenye ujuzi na wasomi ambao hawakuchaguliwa na wengine kutoa mawazo, je, ni lazima kwamba wasomi na maulamaa wote waliobakia wawafuate wao? Je, ni sahihi kukandamiza hisia za umma wote kwa tabia ya vitisho vya kundi moja la watu? Kama kwa upande mwingine, katika mijadala ya kielimu, kundi la watu wakafichua kwamba Ukhalifa haukithibitshwa na sheri za dini au za asili, ni haki kuwaita Rafidhi?

Unasema kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliliacha suala la Ukhalifa juu ya umma au kwa “wasomi” wa Umma, kama unavyoita. Je, wasomi wa Umma wanaundwa na Abu Bakr, Umar na Abu Ubaida Jarra? Kila mmoja akipendekeza jina la mwingine, na kisha wawili kati yao wakamkubali wa tatu. Na hiyo ikawa mwisho. Je, ni wajibu kwa Waislamu wote kuwafuata wao? “Wachache,” “wengi,” na “Ijma” humaanisha vitu tofauti kabisa.

Kama mkutano wa kushauriana unafanywa kwa ajili ya kuangalia tatizo fulani, na idadi ndogo ya watu ikatoa wazo moja, ambapo ile idadi kubwa ya watu ikatoa wazo jingine, kisha inasemwa kwamba, moja ni maoni ya wachache. Maoni ya idadi kubwa ya watu yanaitwa maoni ya wengi, na kama wote (bila tofauti yoyote) wakatoa kauli moja, inaitwa “Ijmai”.

Je Ijmai ilifikiwa ndani ya Saqifa au baadae Msikitini, au baada ya hapo katika mji wa Madina? Kama, hata hivyo, kwa kustahi matakwa yako, tukiondolea mbali haki za umma wote na kusema kwamba maoni ya wasomi na masahaba wa Mtume yalikuwa yanatosha kwa ajili ya Ijmai, nauliza je! Kulikuwa na Ijmai amabayo kwamba wasomi wote na masahaba mashuhuri wa Mtume walishiriki? Je, kikundi kidogo kile kule Saqifa kilikubaliana wote katika maoni yao? Jawabu lake lazima litakuwa ni hapana.

Mwandishi wa “Mawaqif” mwenyewe amekiri kwamba kulikuwa hakuna Ijmai wakati wa Ukhalifa wa Abu Bakr, na kwa yakini vile vile kulikuwa hakuna maoni ya wote miongoni mwa wanachuoni wa Madina. Sa’d Bin Ubaida Ansari, kizazi chake, masahaba mashuhuri wa Mtume, Bani Hashim wote, rafiki zao, na Ali Bin Abu Talib, - wote walimpinga Abu Bakr kwa muda wa miezi sita. Watu hawa katu hawakula kiapo cha utii kwake.

Mjini Madina, makazi ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), hakuna Ijmai iliyofikiwa ambayo kwayo wasomi na masahaba walimuunga mkono Abu Bakr kama Khalifa. Wanahistoria wenu mashuhuri wenyewe, kama Imamu Fakhru’d-Din Razi, Jalalu’d-Din Suyuti, Ibn Abi’l-Hadid Mu’tazali. Tabari, Bukhari na Muslim, wameandika kwamba Ijma kamwe haikutokea hapo Madina.

Bani Hashim, Bani Umayya, na masahaba kwa ujumla – isipokuwa hao watu watatu walio- taja hapo juu – hawakuwepo Saqifa ili kupiga kura zao. Aidha, wengi waliupinga uamuzi huo kwa nguvu sana. Kusema kweli, baadhi ya masahaba wakubwa ambao walikataa kula kiapo cha utii kule Saqifa, walikwenda msikitini na kulalamika kwa Abu Bakr. Miongoni mwa muhajirina walikuwa ni; Salman Farsi, Abu Dharr Ghifari, Mikidadi bin Aswad Kindi, Ammar-e-Yasir, Buraida Aslami, na Khalid Bin Sa’id Bin Aas Amawi.

Miongoni mwa Ansari walikuwa; Abu’l-Hathama bin Tihan, Khuzaima Bin Thabit Dhu’sh- Shahadatain, Abu Ayyub Ansari, Ubai bin Ka’b, Sahl Bin Hunaif, Uthman Bin Hunaif, ambao walipingana na Abu Bakr ndani ya Msikiti. Nimetoa tu kwa mukhtasari mfupi juu ya matukio haya.

Hakuna Ijmai ya aina yoyote iliyofikiwa. Ijma inayosemwa ya wasomi na masahaba mashuhuri wa Madina ni uwongo mtupu.

Kwa kutegemea juu ya vyanzo vyenu wenyewe, nitakupa ordha ya majina ya wale ambao walipinga Ukhalifa. Ibn Hajar Asqalani na Baladhuri, kila mmoja katika Ta’rikh yake, Muhammad Bin Khawind Shah katika kitabu Rauzatus-Safa, Ibn Abdu’l-Birr katika Isti’ab na wengine wanasema kwamba , Sa’d Bin Ubaida na sehemu ya Makhawarij na kikundi cha Makuraishi hawakula kiapo cha utii kwa Abu Bakr.

Aidha, watu kumi na nane ambao walikuwa Masahaba wakubwa na mashuhuri wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hawakula kiapo cha utii kwa Abu Bakr. Walikuwa ni Mashi’a wa Ali Bin Abu Talib. Majina ya watu hao kumi na nane ni haya yafuatayo:

1. Salman Farsi
2. Abu Dharr Ghifari
3. Mikidadi Bin Aswad-e-Kindi
4. Ammar Yasir
5. Khalid Bin Sa’idbin al-Aas
6. Buraida Aslami
7. Ubaid Bin Ka’b
8. Khuzaima Bin Thabit Dhush-Shahadatain
9. Abu’l-Hathama Bin Tihan
10. Sahl Bin Hunaif
11. Uthmani Bin Hunaif Dhush-Shahadatain
12. Abu Ayyub Ansari
13. Jabir Ibn Abdullah Ansari
14. Hudhaifa bin Yaman
15. Sa’d Bin Ubaida
16. Qais Bin Sa’d
17. Abdullah Bin Abbas
18. Zaid Bin Arkam

Na Yakubi anaandika katika Ta’rikh yake: “ Kikundi cha Muhajirina na Ansari kilijitenga bila kula kiapo cha utii kwa Abu Bakr, na walikuwa ni wafuasi wa Hadhrat Ali. Miongoni mwao walikuwa ni Abbas Bin Abu’l-Muttalib, Fazl Bin Abbas, Zubair Ibnu’l-‘Awwam Bin As, Khalid Bin Sa’id, Miqdadi Bin Umar, Salman Farsi, Abu Dharr Ghifari, Ammar Yasir, Bara’a Bin Azib, na Ubai Bin Ka’b.

Je, watu hawa hawakuwa wasomi wa Umma? Ali, Abbas, ami yake Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na watu wengine mashuhuri wa ukoo wa Bani Hashim – je, watu hawa hawakuwa ni wenye busara na waaminifu? Ilikuwa Ijma ya aina gani hiyo, ambayo ilifanyika bila ushauri wa watu hawa? Wakati Abu Bakr anachaguliwa kwa siri siri, na Masahaba wengine mashuhuri hawakujulishwa, je, hii inakuwa ni Ijma? Au ni njama za kisiasa?

‘Hadith Thaqalain’ Na ‘Hadith Safina’

Aidha, Bani Hashim, familia ya Mtume, hawakuwepo pale Saqifa. Uamuzi wao wa thamani hauwezi kukataliwa kwa mtazamo wa hadithi iliyosimuliwa katika mikesha iliyopita, na inayokubaliwa na madhehebu zote. Mtukufu Mtume alisema: “Ninakuachieni kati yenu vitu viwili vizito: Kitabu cha Allah (Qur’ani Tukufu) na Ahlul Bayt wangu (watu wafamilia tukufu: Ali, Fatimah, na kizazi chao).

Kama mkishikama na viwili hivi, kamwe, kamwe hamtapotea baada yangu.” Watu hawa hawakuunga mkono Ukhalifa wa Abu Bakr. Kwa nyongeza, kuna hadithi nyingine mashuhuri ijulikanayo kama Hadith-e-Safina, ambayo niliitaja katika mikesha iliyopita.

Mtume alisema: “Ahlul Bayt wangu ni kama safina ya Nuh. Yeyote anayeipanda ameokolewa, na anayeipa mgongo ameangamia.” Hadithi hii inaonesha kwamba, kama ambavyo watu wa Nuh waliokolewa kutokana na mafuriko makubwa kwa Safina yake, watu wa Mtume wetu wataokolewa kutokana na mabalaa kwa kushikamana na watu wa familia ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Ibn Hajar katika kitabu chake “Sawa’iq-e-Muhriqa”, Sura ya 50, akifafanua juu ya aya ya 4, (kati ya aya tano anazofafanua), ananukuu hadithi mbili kutoka kwa Ibn Sa’d kuhusu wajibu wa kuwafuata Ahlul Bayt watukufu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Katika moja ya hadithi hizo Mtume alisema: “Mimi na Ahlul Bayt wangu ni mti wa Peponi ambao matawi yake yako katika ardhi; hivyo mwenye kutafuta njia ya kuelekea kwa Allah lazima ajiambatan- ishe nao.”

Katika hadithi ya pili Mtume alisema: “Miongoni mwa Umma wangu katika kila zama kuna watu waadilifu kutoka kwenye Ahlul Bayt wangu ambao huondoa uchafu unaoletwa kwenye dini na watenda maovu na ambao hufutilia mbali madai ya uwongo ya wenye kuchupa mipaka na tafsir za watu wasio elimika.

Naifahamike kwenu kwamba Maimamu wenu kwa hakika ndio wale ambao wataokuelekezeni kwa Allah. Hiyvo lazima muwe waangalifu kuhusu wale mnaowachukuwa kuwa viongozi wenu.”

Kiini cha hadithi za aina hii ni kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa anauambia Umma wake: “Mpaka muwafuate Ahlul Bayt wangu, vinginevyo maadui watakupotezeni.” Watu ambao wangeweza kushawishi Ijmai, kiapo cha utii, na uteuzi wa Khalifa, walipinga utaratibu ulioulezea.

Sasa hiyo ilikuwa ni Ijmai ya aina ngani? Masahaba wakubwa, wasomi, na kizazi cha Mtume walikuwepo hapo Madina wakati wa Saqifa. Hivyo hakuna shaka kwamba suala hili halikuamuliwa kwa wingi wa kura, wachilia mbali Ijma. Ibn Abdu’l-Birr Qartabi, mwanacuoni mkubwa wa madhehebu yenu, katika kitabu chake “Isti’ab”, Ibn Hajar katika “Isaba”, na Maulamaa wengine wanaandika kwamba, Sa’d Bin Ubaida, ambaye alikuwa ni mgombea wa Ukhalifa, kwa msimamo mkali kabisa alikataa kula kiapo cha utii kwa Abu Bakr na Umar. Hakutaka kusababisha vurugu, hivyo aliondoka na kwenda Syria.

Kwa mujibu wa riwaya katika “Rauzatus-Safa”, kwa uchochezi wa mtu maarufu, yeye aliuawa. Kwa mujibu wa wanahistoria, mtu ambaye alitenda jinai hiyo ni Khalid Bin Walid. Baada ya kumuua Malik Bin Buwaira na kumuoa mke wake, wakati wa mwanzo wa Ukhalifa wa Abu Bakr, Umar akawa ni mwenye kumchukia sana, wakati Umar alipokuwa khalifa, Khalid akamuua Sa’d Bin Ubaida kwa ajili ya kutaka kupata upendeleo wa Umar.

Hafidh: Kwa vile kulikuwa na hatari ya vurugu, na hawakuweza kupata mawasiliano kwa umma wote, walilazimika kutegemea juu ya hao watu wachache waliokuwepo Saqifa ambako kiapo cha utii kilichukuliwa. Baadaye Umma waliuridhia (Ukhalifa huo).

Muombezi: Kama kulikuwa hakuna njia za kuwasiliana na Masahaba mashuhuri wa Mtume (saw), na wasomi wa Umma ambao walikuwa nje ya Madina, tafadhali tuambie kwa ikhlasi: Kama kulikuwa hakuna njama katika suala hili, kwa nini wasiwaite wale walio kuwepo mjini Madina kwenye mkutano wa Saqifa? Je, haikuwa ni muhimu kwao kupata ushauri wa Abbas, Ali ibn Abu Talib, na Bani Hashim? Je, maoni ya Umar na Abu Ubaida Bin Jarra yalitosha kwa ulimwengu wote wa ki-Islam? Hoja yako iliyotegemea juu ya Ijma, iwe ya jumla au makhususi, haikubaliki. Wasomi na Masahaba wakubwa hawakushiriki kwayo, badala yake waliipinga.

Kama nilivyosema: ‘Ijmai’ maana yake ni kwamba asiwepo hata na mtu mmoja ambaye hakubaliani na wengine. Katika ‘Ijma’ hii umekiri kwamba wasomi kwa ujumla hawakushiriki.

Imamu Fakhru’d-Din Razi katika “Nihayatu’l-Usul” anasema kwamba, kulikuwa hakuna Ijmai ya makubaliano katika Ukhalifa wa Abu Bakr na Umar, mpaka baada ya kuuawa kwa Sa’d Bin Ubaida.

Nashindwa kuelewa vipi unaiita Ijmai hii ya kuwazika kuwa ni uthibitisho kwa ajili ya uhalali wa Ukhalifa. Dai lako la pili, kwamba Abu Bakr alikuwa mtu mzima kuliko Ali na kwa hiyo alikuwa anafaa zaidi kwa ajili ya Ukhalifa ni dhaifu kuliko hoja ya kwanza.

Kama umri ulikuwa sharti juu ya Ukhalifa, basi walikuwepo watu wazima wengi kuliko Abu Bakr na Umar. Kwa hakika Abu Qahafa, baba yake Abu Bakr alikuwa mkubwa kuliko mtoto wake, na alikuwa yu hai wakati ule. Kwa nini asichaguliwe kuwa Khalifa?

Hafidh: Umri wa Abu Bakr ukiungana na uwezo wake, ulimfanya kuwa chaguo la sawa sawa. Wakati kulikuwa kuna mzee, mwenye ujuzi, mtu anayependwa na Mtume katika Umma, kijana mdogo asiye na uzoefu hawezi kupewa amana ya uongozi.

Muombezi: Kama hiyo ingekuwa ni kweli, basi shabaha ya upinzani wako ni Mtume mwenyewe. Wakati alipoondoka kwenda kwenye vita vya Tabuk,wanafiki kwa siri walipanga kufanya maasi mjini Madina wakati akiwa hayupo. Kwa hiyo aliteua mtu mzoefu kushika nafasi yake ili aweze kudhibiti hali mjini Madina na kuivunja ile mipango ya wanafiki. Nakuomba utueleze, Mtume alimuacha nani katika nafasi yake mjini Madina kama mrithi na Khalifa wake?

Hafidh: Inajulikana sana kwamba alimfanya Ali khalifa na mrithi wake.

Muombezi: Je, Abu Bakr, Umar na masahaba wengine wazee zaidi hawakuwepo Madina wakati huo? Ndio. Na bado Mtume akamfanya kijana mdogo, Ali, kuwa Khalifa na mrithi wake.

Kwa ajili ya kusoma baadhi ya aya za Sura ya Al-Bara’a, ya Qur’ani Tukufu kwa watu Makka, mtu pengine angefikiri kwamba, mtu mzoefu lazima angekuwa anafaa kwa kazi hiyo. Lakini Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimurudisha mzee Abu Bakr kutoka kwenye nusu ya safari yake, na akamuamuru yule kijana mdogo, Ali kutekeleza jukumu hili muhimu. Mtukufu Mtume akasema kwamba Allah amemwambia kwamba mtu wa kuwasilisha hiyo Qur’ani tukufu lazima awe ni yeye mwenyewe Mtume au mtu ambaye anatokana naye.

Halikadhalika, kwa ajili ya kuwaongoza watu wa Yemen, kwa nini Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimtuma Kiongozi wa Waumini Ali badala ya mzoefu zaidi Abu Bakr, Umar, au wengine waliokuwepo pale? Na katika matukio mengi kama haya, wakati wakiwepo Abu Bakr, Umar na wengine, alimteua Ali kutekeleza majukumu makubwa.

Hivyo ina maana kwamba ukhalifa unaousisitiza ni ustahili. Imenijia hivi punde tu kwamba uthibitisho wa nguvu wa kukataliwa kwa ukhalifa wa watu hawa ni upinzani wa ile inayoitwa ijmai kwa Ali, ambaye kwa mujibu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), alikuwa ni mwenye kubainisha kati ya haki na batili.

Maulamaa wenu mashuhuri wamesimulia hadithi nyingi kuhusiana na suala hili. Sheikh Suleimani Balhki Hanafi katika kitabu chake “Yanabiul-Mawadda”, Sura ya 16 akinukuu kutoka “Kitabus-Sabi’in-Fi-Fadha’il-e-Amiru’l-Mu’minin,” Imamu’l-Haram Abu Ja’far Ahmad bin Abdullah Shafi’i, katika hadithi ya 12 iliyosimuliwa kutoka Firdaus ya Dailami ya hadithi ya sabini, Mir Sayyid Ali Hamadani Shafi’i katika Mawaddatu’l-Qurba, Mawadda ya 6, Hafidh katika kitabu chake “Amali”, Muhammad bin Yusuf Ganji Shafi’i katika kitabu chake “Kifayatut-Talib,” Sura 44 anasimulia pamoja na hitilafu ndogo kati- ka maneno, kutoka kwa Ibn Abbas, Abi Laila Ghifari, na Abu Dharr Ghifari kwamba, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema (kifungu cha mwisho kikiwa sawa katika kila hadithi): “Punde tu baada ya kuondoka kwangu kwenye ulimwengu huu, yatatokea machafuko.

Wakati yakitokea, lazima mumfuate Ali Bin Abi Talib kwa vile atakuwa mtu wa kwanza kukutana na mimi na kupeana mikono na mimi katika Siku ya Hukumu. Yeye ametukuka kwa daraja na ni mwenye kubainisha kati ya haki na batili.”

Wakati Mtume alipofariki, machafuko makubwa yalitokea. Muhajirina na Ansar walitaka kupata Khalifa kutoka upande wao. Kwa mujibu wa maelekezo ya Mtume, Umma uli- paswa kumleta Ali ili kwamba aweze kubainisha kati ya haki na batili.

Hafidh: Hadith hii ina simulizi pekee (Hadith Ahad) na kwa hiyo si ya kutegemewa.

Muombezi: Nilikwisha jibu pingamizi lako kuhusu hadithi pekee. Maulamaa wa ki-Sunni huchukulia hadithi kama hiyo kama hoja ya msingi, hivyo huwezi kuikataa katika misingi hiyo. Mbali na hilo, sio hadithi hiyo pekee katika jambo hili.

Kuna riwaya nyingi kama hizo zilizosimuliwa na Maulamaa wenu wenyewe ambazo zinaelekeza kwenye maana hiyo hiyo, ambzo baadhi yake nimezitaja katika mikesha iliyopita. Kwa kuzingatia kikwazo cha muda wetu kuwa mfupi, nitakomea katika kutaja tu hapa baadhi ya majina ya waandishi. Moja ya riwaya hizi inasimuliwa na Muhammad Bin Talha Shafi’i katika kitabu chake “Matalibus-Su’ul”, Tabari katika “Tafsir Kabir,” Baihaqi katika “Sunan” yake, Nur’d-Din Maliki katika kitabu chake “Fusul’l-Muhima”, Hakim katika kitabu chake “Mustadrak,” Hafidh Abu Na’im katika kitabu chake “Hilya”, Ibn Asakir katika kitabu chake “Ta’rikh Ibn Asakir”, Ibn Abi’l-Hadid katika Sharhe yake ya “Nahju’l-Balagha”, Tabrani katika kitabu chake “Ausat”, Muhibu’d-Din katika kitabu chake “Riyaz

Hamwaini katika kitabu chake “Fara’id”, Suyuti katika kitabu chake “Durr-e-Mansur”, kutoka kwa Ibn Abbas, Salman, Abu Dharr na Hudhifa – wote wanasimulia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), akinyoosha mkono wake kuelekea kwa Ali Bin Abi Talib, alisema:

“Hakika huyu Ali ndiye mtu wa kwanza ambaye alitangaza imani yake kwangu na wa kwanza ambaye atakayepeana mikono na mimi katika Siku ya Hukumu. Yeye ni Siddiq-e-Akbar (mkweli mkubwa) na Faruq wa Umma huu (mtambuzi wa Umma huu). Atabainisha kati ya haki na batili.”

Hadith “Ali Yuko Pamoja Na Haki Na Haki Iko Pamoja Na Ali”

Muhammad Bin Yusuf Ganji katika Sura ya 44 ya kitabu chake “Kifayatut-Talib” anasimulia hadithi hiyo hiyo pamoja na nyongeza ya maneno: “Na ni mtawala juu ya waumini na ni mlango wangu kwa ajili ya kupitia waumini; na ni Khalifa (mrithi) wangu baada yangu.”

Ganji Shafi’i anasema kwamba Muhadith-e-Sham (mwanahadithi wa Syria) anazo hadithi mia tatu zenye kumsifia Ali. Vile vile imeandikwa na Muhammad Bin Talha Shafi’i katika kitabu chake “Matalibus-Su’ul”, Khatib Khawazimi katika “Manaqib,” Sam’ani katika “Fadha’ilus-Sahaba”, Ibn Sabbagh Malik katika “Fusulu’l-Muhimma”, Khatib Baghdadi katika “Ta’rikh-e-Baghdad”, Jz. 14, uk. 21, Hafidh Mardawaih katika “Manaqib”, Dailami katika “Firdaus”, Ibn Qutayba katika “Imama was-Siyasa”, Jz. 1, uk.111, Ganji Shafi’i katika “Kifayatut-Talib”, Imamu Ahmad Hanbal katika “Musnad”, na maulamaa wenu wengi wamesimulia kwamba, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Ali yuko pamoja na haki na haki iko pamoja na Ali popote ageukiapo.” Katika vitabu hivyo hivyo vile vile kuna hadith nyingine iliyosimuliwa na Sheikh Sulemani Qunduzi Hanafi, katika Sura ya 20 ya “Yanabiu’l-Mawadda”, kutoka kwa Hamwaini kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Ali yuko pamoja na haki na haki iko pamoja na Ali.”

Hafidh Abi Nai’im Ahmad ibn Abdullah Ispahani katika kitabu chake “Hiyatu’l-Auliya” Jz. 1, uk. 63, anasimulia kwamba, Mtume alisema: “Enyi kundi la Ansar! Je, nikuelekezeni kwa mtu ambaye kama mkishikamana naye kamwe hamtapotea?” Wote wakasema: “Ndio, Ewe Mtume wa Allah”. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Mtu huyo ni Ali. Mpendeni kama mnavyonipenda mimi, na mheshimuni kama mnavyoniheshimu mimi, yale niliyokuambieni yalikuwa ni amri ya Allah iliyosimuliwa kwangu na Jibril.”

Lengo la ujumla la hadithi hizi ni kuonyesha dalili za upendeleo wa Mtume kuhusiana na mrithi wake. Mtume aliamrisha Umma wake kugeukia kwa Ali baada yake na kumfuata yeye. Kwa mwanga wa hadithi kama hizi, tueleze upinzani wa Ali kwa Abu Bakr una maanisha nini kwako. Kwa hakika inasikitisha sana na kushangaza kwamba haraka kubwa mno ilifanywa katika siku ya Saqifa. Kila mtu mwenye akili ambaye anajua yaliyotokea katika siku hiyo amefadhaika mno. Kama kulikuwa hakuna njama, kwa nini wasingoje (angalau kwa saa chache) ili kwamba Ali Bin Abi Talib, Bani Hashim, na Abbas waweze kuelezea maoni yao juu ya Ukhalifa?

Hafidh: Kulikuwa hakuna njama. Kwa vile walihofia vurugu, walifanya haraka kuamua suala la Ukhalifa kwa ajili ya usalama wa Uislamu.

Muombezi: Una maana kwamba Abu Ubaida Jarra, mchimba kaburi wa zamani wa Makka, na wengine walikuwa na wasiwasi zaidi na usalama wa Uislamu kuliko Abbas, ami yake Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anayeheshimiwa, na Ali Bin Abi Talib? Una maana kwamba kama wangelingojea kwa muda kidogo, au kama Abu Bakr na Umar, wakiwashughulisha watu, wangemtuma Abu Ubaida kumjulisha Abbas na Ali juu ya hali hii mbaya, hilo lingefanya Uislamu uangamie?

Tafadhali jaribu kuwa mkweli. Kama wangewakaribisha watu wanaostahili huko Saqifa, nafasi yao ingelikuwa salama zaidi. Kusingelikuwa na hitilafu katika Uislamu kama ilivyo leo.

Baada ya miaka 1335, sisi ndugu wa ki-Islamu tusingezozana wenyewe kwa wenyewe kama tulivyo usiku huu, bali tungekuwa tumeungana katika kumpinga adui yetu wa pamoja. Sehemu kubwa ya msingi wa jengo hili lenye kasoro la Uislamu uliwekwa siku hiyo. Ilikuwa ni kwa ajili ya haraka za watu wale watatu za kutaka kukamilisha mipango yao ya siri.

Nawab: Bwana mheshimiwa, tafadhali tueleze kwa nini walifanya haraka. Kwa nini wasi- wajulishe hata watu waliokuwa Msikitini au katika nyumba ya Mtume?

Muombezi: Sababu sio za kutafuta mbali. Walifanya haraka kwa sababu walijua kwamba kama wakingojea Waislamu wote waje, au angalau hata watu mashuhuri wa jeshi la Usama Bin Zaid, masahaba mashuhuri wa Mtume waliokuwepo mjini Madina, au Bani Hashim, jina la Ali, miongoni mwa mwa mengine, lingependekezwa. Uwezekano wa kisiasa wa Abu Bakr na Umar ungelipunguzwa sana.

Hivyo basi waliharakisha mipango yao ili kwamba, wakati ambapo Bani Hashim na masahaba mashuhuri wakiwa wanajishughulisha na taratibu za mazishi ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), wao walifanikiwa katika kumteua Abu Bakr kuwa Khalifa juu ya msingi wa kura za watu wawili! Waliucheza mchezo huo, na usiku huu hapa ninyi watu wazuri mnaupa jina la “ijmai!” Hata ulamaa wenu wakubwa, kama Tabari, Ibn Abil-Hadid na wengine wameandika kwamba Umar alisema: “Ukhalifa wa Abu Bakr ulisimamishwa kwa haraka sana. Allah atusaidie!”

Amma kwa madai yenu mengine, ambayo mnayatoa kutoka kwa khalifa Umar, kwamba utume na utawala haviwezi kuchanganywa kwenye familia moja, vile vile yanakataliwa kwa mujibu wa Qur’ani Tukufu:

أَمْ يَحْسُدُونَ النَّاسَ عَلَىٰ مَا آتَاهُمُ اللَّهُ مِنْ فَضْلِهِ ۖ فَقَدْ آتَيْنَا آلَ إِبْرَاهِيمَ الْكِتَابَ{54}

“Au wanawahusudu watu kwa yale aliyowapa Allah kutokana fadhila Zake? Basi tuliwapa ukoo wa Ibrahim Kitabu na hikma na tukawapa mamlaka makubwa.” (4:54)

Hadithi hii ambayo inahusishwa na Khalifa Umar, ni ya kubuniwa. Mtume kamwe hajasema neno lenye kukinzana na amri ya Qur’ani Tukufu. Aidha, ukhalifa hauwezi kutenganishwa na utume kwa sababu Khalifa wa kweli ni mfano wa sheria ya Mungu inayofanya kazi ulimwenguni. Kuuchukulia ukhalifa kama kazi ya kisiasa tu iliyotenganishwa na utume ndio kosa lenyewe hasa lililofanywa na Abu Bakr na Umar.

Kama Harun, ndugu yake Mtume Musa, angeweza kuondolewa kwenye ukhalifa wa Musa, Ali vile vile angeweza kunyimwa ukhalifa wa Mtume. Na kwa vile utume na ukhalifa, kwa mujibu wa Qur’ani, vilichanganywa juu ya Musa na Harun, hapana shaka ulichanganywa juu ya Muhmmad na Ali. Hadithi yenu hii ilibuniwa na Bani Umayya. Kama utume na ukhalifa usingeweza kuchanganywa katika familia moja, basi kwa nini katika Majilis-e- Shura (Kamati ya ushauri) Khalifa Umar alimpendekeza Ali kwenye ukhalifa? Hata hivyo, ninyi vile vile mnamkubali kuwa ni Khalifa wenu wa nne!

Ni ukinzano wenye kushangaza kwamba kwa kumetegemea juu ya hadithi ya Umar, mnakataa kuchanganywa utume na ukhalifa, lakini wakati Umar mwenyewe alipoidhinisha hali hii miaka michache baadae, mkaiunga mkono! Je, mnaweza kupinga na kuunga mkono pendekezo lile lile moja? Mnasema kwamba utume na utawala havichanganywi katika familia moja, ingawa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amefanya kuwa ni wajibu kwa Umma wake kufuata kizazi chake. Alisema kwamba kuwa na uadui nao ni kupotea njia.

Amesema katika mara nyingi, “Ninakuachieni vitu viwili vizito: Kitabu cha Allah (Qur’ani Tukufu) na Ahulul-Bayt wangu. Kama mkifungamana na viwili hivi, kamwe hatapotea baada yangu.” Hadithi hii sahihi imekubaliwa na madhehebu zote. Nimeitaja katika mikesha iliyopita pamoja na vyanzo vyake.

Hadithi Ya Safina – Hadithi Ya Saqifa

Wakati wa mafuriko makubwa yeyote yule ambaye alichukuwa hifadhi katika safina ya Huh aliokolewa. Yeyote yule ambaye aliipa mgongo akaacha kuipanda aligharikishwa, ikiwa ni pamoja na mtoto wa Nuh. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) vile vile aliwatambulisha kizazi chake kama Safina ya Nuh, akimaanisha kwamba watu wa umma wake katika wakati wa mitihani lazima wajiambatanishe na kizazi chake.

Kwa hiyo, kwa mujibu wa maamrisho haya ya wazi, umma katika hitilafu zao zote, wanapaswa kutafuta manufaa ya Ahlul-Bayt wa Mtume. Ali Bin Abu Talib, kwa mujibu wa Mtume alikuwa ndiye msomi zaidi na mtu bora zaidi miongoni mwao. Kwa nini hawakumjulisha wakapata kushauriana naye? Lakini wapi! Hawakufanya hivyo. Wanasiasa walinyakuwa mamlaka na wakamnyima Ali haki yake ya kudumu.

Sheikh: Ni kwa misingi ipi unasema kwamba wangelimfuata Ali na kwamba maoni na ijmai ya masahaba ingelipaswa kuachwa?

Muombezi: Sijasema kwamba maoni ya Masahaba na ijma yao haipaswi kuheshimiwa. Tofauti moja kati yenu na mimi ni kwamba mara tu mnaposikia jina la sahaba, hata kama akiwa ni mnafiki, kama Abu Huraira, ambaye Khalifa Umar alimpiga na kumuita mwongo, mnamuinamia kwa heshima. Nawaheshimu mashaba wale tu ambao wanachukuana na masharti ya uswahiba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Aidha nimeonesha kwamba kulikuwa hakuna ijma ndani Saqifa. Kama mnaweza kupinga hoja yangu, sasa ni wakati wa kufanya hivyo. Nitakubaliana na muafaka wa hadhara hii. Kama mnaweza kuonyosha kutoka kwenye vitabu nyenu kwamba ndani ya Saqifa, umma wote au watu wasomi wenye akili wa umma walikusanyika pamoja na kukubaliana kwamba Abu Bakr awe Khalifa, tutakuwa tayari kulibali hilo.

Na kama ukiondoa watu wawili (Umar na Abu Ubaida) na watu wachache wa kabila la Aus, hakuna mtu mwingine aliyekula kiapo cha utii, lazima mkubali kwamba sisi Mashi’a tumeongozwa sawasawa. Tunaliacha kwenye maoni ya kisomi kuamua iwapo masahaba watatu walikuwa na haki ya kushikilia hatamu za umma wote. Wawili walikula kiapo kwa wa tatu, na baadae wakawatishia wengine kwa panga, moto, na fadheha, kuwalazimisha kukubali utashi wao.

Je, Ijmai Inapaswa Kukubaliwa Kwa Sababu Ya Kigezo Cha Yaliyopita?

Sheikh: Hatujui kama kulikuwa na uzembe kwa upande wao kwa sababu hatukuwepo kule siku hiyo. Katika muda huu mrefu hatuwezi kutambua walikuwa katika shinikizo la aina gani. Leo pamoja na hali hiyo kuwa ni ukweli uliothibiti, sio neno iwapo kama ijma ilikamilishwa katika hatua za pole pole. Hatupaswi kupinga. Lazima tukubaliane na watu wale na tufuate njia waliyotuonyesha.

Muombezi: Uzuri ulioje wa hoja hiyo! Unatutaka sisi tufikirie kwamba Uislamu hauna misingi? Kama watu wawili au watatu wakiunda mpango na wakaungwa mkono na watu wengine, je, ni jukumu la Waislamu kuwafuata wao? Je, hiyo ndio maana ya dini ya Mtume wa Uislamu? Qur’ani Tukufu inasema: “…Basi wabashirie waja wangu, wale ambao husikiliza maneno, wakafuata lililo bora lao…” (39:17-18)

Uislamu umesimama juu ya misingi ya kweli na hoja, sio juu ya kufuata kibubusa, naam kwa hakika si kwa kumfuata Abu Ubaida, mchimba kaburi. Mtume alituonesha njia. Alisema kwamba wakati umma ukiwa umegawanyika, lazima tumfuate mtu ambaye ameongozwa. Unatuuliza ni kwa nini ni wajibu juu yetu kumfuata Ali. Tunajibu kwamba wajubu huo umetegemea juu ya aya za Qur’ani na hadithi zilizoandikwa katika vitabu vyenu wenyewe.

Hadithi Za Mtukufu Mtume (S.A.W.W.) Zinazowahimiza Waumini Kumfuata Ali

Kuna hadithi nyingi ambazo hufanya wajibu juu ya umma kumfuata Ali. Mojawapo ya hizo imesimuliwa na Ammar-e-Yasr, ambayo imeandikwa na maulamaa wenu wafuatao katika vitabu vyao: Hafidh Abi Nu’aim Ispahani katika “Hilya”; Muhammad Bin Talha Shafi’i katika “Matalibus-Su’ul”; Baladhuri katika “Ta’rikh”; Sheikh Sulaiman Balkhi Hanafi katika “Yanabiu’l-Mawadda”, Sura ya 43, kutoka kwa Hamwaini; Mir Sayyid Ali Hamadani Shafi’i katika “Mawaddatu’l-Qubra”, Mawadda ya 5; Dalami katika “Firdaus”. Wanasimulia hadithi ndefu yenye maelezo kinaganaga ambayo haiwezi kusimuliwa hapa kwa ukamilifu. Inaweza kuelezewa kwa ufupi tu kwamba, wakati walipomuuliza Abu Ayyub kwa nini alikwenda kwa Ali na hakuchukua kiapo cha utii kwa Abu Bakr, yeye ali- jibu kwamba siku moja alikuwa amekaa na Mtume wakati Ammar-e-Yasir alipokuja na kumuuliza Mtume swali.

Katika kuendelea na mazungumzi yao, Mtume akasema: “Ewe Ammar! Kama watu wote watakwenda njia mmoja, na Ali peke yake akaenda njia nyingine, itakupasa kumfuata Ali. Ewe Ammar! Ali hatakuruhusu wewe kupotea kutoka kwenye njia ya mwongozo na hatakuongoza kwenye upotovu; Ewe Ammar! Utii kwa Ali ni utii kwangu, na utii kwangu ni utii kwa Allah.” Katika mwanga wa Maamrisho haya, na katika mwanga wa upinzani wa Ali kwa Abu Bakr, je, watu siwangemfuata Ali? Hata kama Bani Hashim, Bani Umayya, Masahaba mashuhuri, watu wajuzi wenye elimu wa umma, Muhajirina, na Ansari wasingekuwepo pamoja naye (na walikuwa pamoja naye) watu wangelimfuata Ali.

Hafidh: Wakati wa mjadala wetu, umesema vitu viwili vya ajabu. Kwanza, umerudia rudia kumuita Abu Ubaida “mchimba kaburi.” Unaweza kuthibitisha kwamba hii ilikuwa taaluma ya bwana mkubwa huyu? Pili, umesema kwamba Ali, Bani Hashim, na masahaba hawakula kiapo cha utii kwa Abu Bakr, walimpinga. Lakini wanahistoria na wanahadithiwote wameandika kwamba Ali, Bani Hashim na masahaba wa Mtume walikula kiapo cha utii kwa Abu Bakr.

Muombezi: Sio sisi peke yetu tunaodai kwamba Abu Ubaida alikuwa mchimba kaburi. Imo katika vitabu vyenu wenyewe. Unawza kurejea kwenye Al-Bidayya wa’n-Nihaya, Jz. 5, uk. 266-267 (kitabu) kilichokusanywa na Ibn Kathir Shami, ambaye anasema kwamba, kwa vile Abu Ubaida amezoea kuchimba kaburi za watu Makka, Abbas alimtuma mtu kumtafuta Abu Talha, mchimba kaburi wa Madina, na mtu mwingine kumtafuta Abu Ubaida, ili kwamba wote wawili waweze kuchimba kaburi la Mtume.

Kulazimishwa Kwa Ali Na Bani Hashim Kula Kiapo Baada Ya Miezi Sita

Unasema kwamba Ali, Bani Hashim, na masahaba wa Mtume walikula kiapo cha utii kwa Abu Bakr. Umesoma maneno “walikula kiapo cha utii,” lakini hukuelewa ni kwa nani na vipi walivyokula kiapo. Wanachuoni wenu wote wa hadithi na wanahistoria wakubwa wameandika kwamba Ali na Bani Hashim walikula kiapo cha utii (kwa nje), lakini hilo limefanywa baada ya miezi sita, na hata hivyo chini ya vitisho vikubwa.

Hafidh: Sio vyema kwa mtu mtukufu kama wewe kutumia maneno ambayo hutumiwa na Mashi’a wa kawaida kwamba, Ali aliburuzwa kutoka kwenye nyumba yake na alitishiwa kuuawa kama asingekula kiapo cha utii. Ukweli ni kwamba katika siku chache za mwan- zo za ukhalifa kwa utashi na kwa furaha alikubali ukhalifa wa Abu Bakr.

Muombezi: Ali na Bani Hashim hawakula kiapo cha utii kwa mara moja. Wanahistoria wenu wameandika kwamba Ali alikula kiapo cha utiibaada ya kifo cha Hadhrat Fatima. Bukhari katika katika Sahih yake, Jz. 3, Sura ya Ghazawa Khaibar, uk. 37, na Muslim Bin Hujjaj, katika Sahih yake, Jz. 5, uk. 154, wameandika kwamba Ali alikula kiapo cha utii baada ya kifo cha Fatima.

Baadhi ya maulamaa wenu wanaamini kwamba Fatima alikufa siku 75 baada ya kifo cha Mtume. Ibn Qutayba vile vile anashikilia maoni hayo hayo, lakini wanahistoria wenu wengi wanadai kwamba alikufa miezi sita baada ya kufariki kwa Mtume. Kwa hiyo ina maana kwamba kiapo cha Ali kilikuja wakati fulani baada ya miezi 3 au 6 baada ya kufariki kwa Mtume.

Mas’udi katika kitabu chake “Murujus-Sahab”, Jz. 1, uk. 414, anasema: “Hakuna mtu kutoka Bani Hashim aliyekula kiapo cha utii kwa Abu Bakr mpaka baada ya kifo cha Bibi Fatima. Ibrahim Bin Saqafi anasimulia kutoka kwa Zuhri kwamba Ali hakula kiapo cha utii kwa Abu Bakr mpaka miezi sita baada ya alipofariki Mtume, na watu hawakuwa na ujasiri wa kumshawishi isipokuwa baada ya kifo cha Bibi Fatima. Ibn Abi’l-Hadid katika Sharhe Nahju’l-Balagha anasimulia jambo hilo hilo.

Kwa hali yoyote, maulamaa wenu wenyewe wanasisitiza kwamba kiapo cha Ali hakikuwa cha haraka bali kilikuja tu baada ya muda fulani kupita na hata hivyo ni wakati mazingira yalipomlazimisha kufanya hivyo. Ibn Abi’l-Hadid, katika Sharhe Nahju’l-Balagha, Jz. 2, uk. 18, anasimulia kutoka kwa Zuhri, kutoka kwa Aisha, ambaye amesema: “Ali hakula kiapo cha utii kwa Abu Bakr kwa muda wa miezi sita, na hakuna mtu kutoka Bani Hashim aliyekula kiapo mpaka Ali alipofanya hivyo.”

Ahmad Bin A’sam-e-Kufi Shafi’i katika “Futuh” na Abu Nasr Hamidi, katika “Jam’a Bainus-Sahihain” anasimulia kutoka kwa Nafiy, akinukuu kutoka Zuhri, ambaye alisema: “Ali hakula kiapo cha utii mpaka baada ya miezi ya kufariki kwa Mtume (s.a.w.w.).”

Ali Aliburuzwa Kutoka Nyumbani Kwake Na Nyumba Yake Ikachomwa Moto

Hafidh: Ni wapi maulamaa wetu waliposema kwamba Ali aliburuzwa kutoka kwenye nyumba yake na nyumba ikachomwa moto, kama kwa kawaida inavyoaminiwa na Mashi’a? wanalisimlia hili kwa mhemuko mkubwa katika majlis zao za kidini. Vile vile huchochea hisia za watu kwa kusema kwamba Fatima aliteswa na hatimaye akaharibu mimba yake.

Muombezi: Waheshimiwa mliohudhuria mnawashutumu Mashi’a, mkijaribu kuficha makosa ya viongozi wenu waliotangulia. Mnasema kwamba hadithi hizi zimebuniwa na Mashi’a. Ukweli ni kwamba kwa amri ya Abu Bakr, Umar na wenzake walikwenda nyumbani kwa Ali, wakamtisha kwa upanga, wakamburuza mpaka Msikitini na wakamlazimisha kula kiapo cha utii kwa Abu Bakr. Ukweli huu umeandikwa na maulamaa wenu wenyewe. Kama mnataka, nitakusimulieni. Hatusemi kitu chochote kutoka kwenye vitabu vyetu. Tunasema kile mnachosema ninyi.

Hafidh: Ndio, tafadhali endelea. Tuko tayari kusikiliza.

Hoja Kumi Na Mbili Zinazounga Mkono Ukweli Kwamba Ali Alichukuliwa Kupelekwa Msikitini Kwa Ncha Ya Upanga

Muombezi:

(1) Abu Ja’far Baladhuri Ahmad Bin Yahya Bin Jabir Baghdadi, mmoja wa wanahadithi na wanahistoria wenu wa kutengemewa, anaandika katika kitabu chake cha Ta’rikh - Historia kwamba, wakati Abu Bakr alipomuita Ali ili kula kiapo cha utii, Ali alikataa. Abu Bakr alimtuma Umar akiwa na kijinga kwenda kuchoma moto nyumba ya Ali.

Fatima akaja mlangoni na kusema: “Ewe mtoto wa Khattab! Umekuja kuichoma nyumba yangu?” Akasaema: “Ndio, hili lina athari zaidi kuliko kitu chochote alichokifanya baba yako.”

(2) Izzu’d-Din Ibn Abi’l-Hadid Mu’tazili, na Muhammad Bin Jarir Tabari, wanasimulia kwamba Umar alikwenda kwenye mlango wa nyumba ya Ali pamoja na Usay Bin Khuza’i, Salama Bin Aslam na kikundi cha watu. Kisha Umar akaita, “Tokeni nje! Vinginevyo nitaichoma nyumba yenu!”

(3) Ibn Khaziba anataarifu katika kitabu chake “Kitab-e-Gharrar” kutoka kwa Zaid Bin Aslam, ambaye alisema: “Nilikuwa mmoja wa wale waliokwenda pamoja na Umar tukiwa na vijinga vya moto mpaka kwenye mlango wa nyumba ya Fatima. Wakati Ali na watu wake alipokataa kula kiapo cha utii, Umar alimuambia Fatima: ‘Yeyote yule aliyeko ndani ya nyumba atoke nje.

Vinginevyo nitaichoma nyumba na yeyote aliyemo ndani.’ Ali, Hasani, Husein, Fatima, na kikundi cha Masahaba wa Mtume, na Bani Hashim walikuwemo ndani. Fatima akasema: ‘Utaichoma nyumba yangu moto pamo- ja na mimi mwenyewe na watoto wangu?’ Akasema: ‘Ndio, Wallahi, kama hawatoki nje na kula kiapo cha utii kwa Khalifa wa Mtume.’”

(4) Ibn Abd Rabbih, mmoja wa maulamaa wenu mashuhuri, anaandika katika kitabu chake “Iqdu’l-Farid,” Jz. 3, uk. 63, kwamba Ali na Abbas walikuwa wamekaa nyum- bani kwa Fatima. Abu Bakr akamuambia Umar: “Nenda ukawalete watu hawa. Kama wakikataa kuja, pigana nao.” Hivyo Umar akaenda nyumbani kwa Fatima na vijinga vya moto. Fatuma akaja mlangoni na akasema: “Umekuja kuchoma nyumba yetu?” Akasema: “Ndio…” na kadhalika.

(5) Ibn Abi’l-Hadid Mu’tazili katika sharhe yake ya Nahju’l-Balagha, Jz. 1, uk. 134, akinukuu kutoka kitabu cha Jauhari, “Kitab-e-Saqifa” ameandika kwa kinaganaga kuhusu suala la Saqifa-e-Bani Sa’ad: “Bani hashim na Ali walikuwa wamekusanyika nyumbani kwa Ali. Zubair pia alikuwemo kwa vile naye alijiona kama ni mmoja wa Bani Hashim. Ali alizoea kusema, ‘Zubair alikuwa siku zote pamoja nasi mpaka wato- to wake walipokuwa wakubwa. Wao wakamgeuza dhidi yetu’. Umar akaenda nyumbani kwa Fatima na kikundi cha watu. Usayd na Salma vile vile walikuwa pamoja naye.

Umar akawataka watoke nje wachukue kiapo cha utii. Wao wakakataa. Zubair akachomoa upanga wake na akatoka nje. Umar akasema: ‘Mkamateni mbwa huyu.’ Salma Bin Aslam akamnyang’anya upanga huo na akautupa kiambazani. Kisha wakambururuza Ali kumpeleka kwa Abu Bakr. Bani Hashim wengine wakamfuata na walikuwa wanangojea kuona Ali atafanya nini.

Ali alikuwa akisema kwamba yeye ni mtumishi wa Allah na ndugu yake Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Hakuna aliyemsikiliza. Walimpeleka kwa Abu Bakr, ambaye alimtaka kula kiapo cha utii kwake. Ali akasema: ‘Mimi ndiye ninayestashiki zaidi katika nafasi hii, na sitakula kiapo cha utii kwako.

Ni wajibu juu yako kula kiapo cha utii kwangu. Umeichukuwa haki hii kutoka kwa Ansar kwa kutegemea uhusiano wako na Mtume (s.a.w.w.). Na mimi vile vile, kwa msingi huo huo, nalalamika dhidi yako. Hivyo kuwa muadilifu. Kama unamuogopa Allah, kubali haki yangu, kama Ansar walivyofanya kwa yako. Vinginevyo, itakupasa ukubali kwamba unanidhulumu kwa makusudi.’

Umar akasema: ‘Hatutakuacha mpaka ule kiapo cha utii.’ Ali akasema: ‘Mmekula njama wote vizuri sana. Leo unamuunga mkono, ili kwamba kesho aweze kuurudsha ukhalifa kwako. Naapa Wallahi kwamba sitakubaliana na maombi yenu na sitakula kiapo cha utii (kwa Abu Bakr). Yeye anapaswa atoe kiapo cha utii kwangu.’

Kisha aliwageukia watu na akasema: ‘Enyi Muhajirina! Muogopeni Allah. Msipore haki ya mamlaka ya familia ya Muhammad. Haki hiyo imeamriwa na Allah. Msimuondoe mtu anayestahiki kutoka katika nafasi yake. Kwa jina la Allah sisi Ahlul-Bayt tuna mamlaka makubwa katika suala hili kuliko mlivyo ninyi. Kuna mtu miongoni mwenu ambaye ana ujuzi juu ya Kitabu cha Allah (Qur’ani), Sunna ya Mtume, na sheria za dini yenu.

Ninaapa Wallahi sisi tunavyo vitu vyote hivi. Hivyo msifuate nafsi zenu mkaja mkapotea kutoka kwenye ukweli.’” Ali alirudi nyumbani bila kula kiapo cha utii na akajitawisha mwenyewe nyumbani kwake mpaka Fatima alipofariki. Hapo tena, alilazimishwa kula kiapo cha utii.

(6) Abu Muhammad Abudullah Bin Muslim bin Qutayba Bin Umar Al-Bahili Dinawari, ambaye alikuwa mmoja wa maulamaa na Kadhi rasmi wa mji wa Dinawari, anaandika katika kitabu chake mashuhuri “Ta’rikhu’l-Khulafati Raghibin wa Daulati Bani Umayya”, kijulikanacho kama “Al-Imama was-Siyasa”, Jz. 1, uk. 13: “Wakati Abu Bakr alipofahamu kwamba kundi la watu walio na uadui kwake wamekusanyika katika nyumba ya Ali, alimtuma Umar kwao. Wakati Umar alipompigia kelele Ali atoke nje na kula kiapo cha utii kwa Abu Bakr, wote walikataa kutoka nje.

Umar alikusanya kuni na kusema ‘Naapa kwa jina la Allah, ambaye ana uhai wangu katika miliki Yake, amma mtatoka nje, au nitaichoma nyumba pamoja na wote waliomo ndani.’ Watu wakasema: “Ewe Abu Hafsa! Fatima vile vile yumo ndani.’ Akasema: ‘Hata akiwemo, nyumba nitaichoma moto tu.’

Hivyo wote wakatoka nje na kula kiapo cha utii, isipokuwa Ali, ambaye alisema: ‘Nimeweka nadhiri kwamba, mpaka nitakapomaliza kuikusanya Qur’ani, sitatoka nje ya nyumba wala kuvaa nguo kiukamilifu.’ Umar hakulikubali hili, lakini malalamiko ya huzuni ya Fatima na kubezwa na wengine, kulimlazimisha kurudi kwa Abu Bakr.

Umar alimhimiza kumlazimisha Ali atoe kiapo cha utii. Abu Bakr alimtuma Qanfaz mara kadhaa kumuita Ali, lakini safari zote alikatishwa tamaa. Mwishowe Umar, na kundi la watu walikwenda kwenye mlango wa nyumba ya Fatima. Wakati Fatima aliposikia sauti zao, alipiga kelele: ‘Ewe baba yangu, Mtume wa Allah!

Ni mateso gani haya tunayopata kuto- ka kwa mtoto wa Khattab na mtoto wa Abi Quhafa!’ Wakati watu hao walipoyasikia malalamiko ya Fatima, baadhi yao walirudi nyuma mioyo yao ikiwa imevunjika, lakini Umar alibaki pale na baadhi ya watu wengine mpaka mwishowe wakamburuza Ali kutoka nje ya nyumba.

Walimchukuwa Ali na kumpeleka kwa Abu Bakr, na akamuambia achukue kiapo cha utii kwake. Ali alisema: ‘Kama sikula kiapo cha utii kwako utanifanya nini?’ Wakasema: ‘Tuna apa kwa jina la Allah kwamba tutaivunja shingo yako.’ Ali akasema: ‘Mtamuuwa mtumishi wa Allah na ndugu wa Mtume?’ Umar akasema: ‘Wewe sio ndugu wa Mtume wa Allah.’
Wakati haya yakijiri, Abu Bakr alinyamaza kimya. Kisha Umar akamuuliza Abu Bakr iwapo yeye (Umar) alikuwa hafuati amri yake katika suala hili. Abu Bakr akasema kwamba muda Fatima yuko hai hatamlazimisha Ali kula kiapo cha utii kwake. Kisha Ali aliweza kufikia kaburi la Mtume, ambako akiomboleza na kulia, alimueleza Mtume kile ambacho Harun alimueleza ndugu yake (Mtume Musa), kama ilivyoandikwa katika Qur’ani Tukufu:

قَالَ ابْنَ أُمَّ إِنَّ الْقَوْمَ اسْتَضْعَفُونِي وَكَادُوا يَقْتُلُونَنِي{150}

‘..Ewe mtoto wa mama yangu! Hakika watu hawa wamenidharau, na wakakaribia kuniuwa…’( 7:150)

Fatima Aliwaambia Abu Bakr Na Umar Kwamba Anawalaani

Hao Wote Katika Kila Sala

Baada ya kuelezea Suala hili kwa urefu, Abu Muhammad Abdullah Bin Qutayba anasema kwamba Ali hakula kiapo cha utii na akarudi nyumbani. Baadae Abu Bakr na Umar walik- wenda nyumbani kwa Fatima kumbembeleza na kuomba msamaha wake.

Fatima akasema: ‘Allah awe ni shahidi wangu kwamba ninyi wawili mmenikosea. Ninawalaani katika kila Salat, na nitaendelea kuwalaani mpaka nitakapomuona baba yangu na kumlalamikia dhidi yenu.”

(7) Ahmad Bin Abdu’l-Aziz ni mmoja wa maulamaa wenu. Ibn Abi’l-Hadid anaandika kuhusu yeye katika maneno yafuatayo: “Alikuwa mtu msomi, mwanahadithi na mwandishi mkubwa.” Yeye anaandika katika kitabu chake, Kitab-e-Saqifa, na Ibn Abi’l- Hadid Mu’tazili vile vile anamnukuu katika Sharhe Nahju’l-Balagha, Jz. 1, uk. 9, kutoka kwa Abi’l-Aswad, ambaye amesema:

“Kundi la Masahaba na Muhajirina mashuhuri walielezea kuhusu kuudhiwa kwao na ukhalifa wa Abu Bakr na wakauliza ni kwa nini wao hawakushauriwa. Vile vile Ali na Zubair walionyesha hasira zao, wakakataa kula kiapo cha utii na wakarudi nyumbani kwa Fatima. Fatima alilia kwa nguvu na akawasihi kwa taadhima sana, lakini bila mafanikio yoyote. Walichukuwa upanga wa Ali na wa Zubair wakazirusha kwenye ukuta na kuzivunjilia mbali. Kisha wakawaburuza mpaka Msikitini na kuwalazimisha kula kiapo cha utii.”

(8) Jauhari anasimulia kutoka kwa Salma bin Abdu’r-Rahman kwamba wakati Abu Bakr aliposikia kwamba Ali, Zubair, na kundi la Bani Hashim walikuwa wamekusanyika nyumbani kwa Fatima, alimtuma Umar kwao. Umar alikwenda mpaka mlangoni mwa nyumba ya Fatima na akaita kwa sauti kubwa: “Tokeni nje, vinginevyo, naapa nitai- choma nyumba yenu!”

(9) Jauhari, kwa mujibu wa Ibn Abi’l-Hadid katika sharhe ya Nahaju’l-Balagha, Jz. 2, uk.

19, anasimulia kutoka kwa Sha’bi: “Wakati Abu Bakr aliposikia kuhusu mkusanyiko wa Bani Hashim katika nyumba ya Ali, alimuambia Umar: ‘Wewe na Khalid nendeni mkamlete Ali na Zubair waje wale kiapo cha utii.’ Hivyo Umar aliingia nyumbani kwa Fatima na Khalid akabakia nje. Umar akamuambia Zubair ‘Upanga huu ni wa nini?’ Akajibu, ‘Nimeupata kwa ajili ya kula kiapo kwa Ali.’

Umar akaunyakua upanga ule na kuutupa kwenye jiwe ndani ya nyumba na kuuvunja. Kisha akamtoa nje kwa Khalid. Alirudi tena ndani ya nyumba ambako kulikuwa na watu wengi, akiwemo Miqdadi, na Bani Hashim wote. Akimsemesha Ali, alisema: ‘Nyanyuka! Ninakupeleka kwa Abu Bakr. Lazima ule kiapo cha utii kwake.’ Ali akakataa. Umar akamburuza mpaka kwa Khalid. Khalid na Umar wakamlazimisha katika barabara ambayo ilikuwa imejaa watu ambao walishuhudia kitendo hiki. Wakati Fatima alipoona tabia hii ya Umar, yeye pamoja na wanawake wengi wa Bani Hashim (ambao walikuja kumliwaza), walitoka nje.

Walikuwa wakiomboleza na kulia kwa vilio vya sauti ya juu. Fatima alikwen- da msikitini ambako alimuambia Abu Bakr: ‘Mapema ilioje umewafukuza Ahlul Bayt wa Mtume wa Allah. Naapa kwa jina la Allah, sitazungumza na Umar mpaka nitakapomuona Allah (yaani Siku ya Hukumu).’

Fatima alionesha kuchukizwa kwake mno na Abu Bakr na hakuzungumza naye kwa muda wote uliokuwa umebakia wa maisha yake.” (Tazama Sahih Bukhari, sehemu ya 5 na 7).

(10) Abu Walid Muhibu’d-Din Muhammad bin Muhammad Bin Ash-Shahna Al-Hanafi (amekufa 815 A.H.), mmoja wa maulamaa wenu wakubwa anaandika katika katika kitabu chake, “Raudhatu’l-Manazir Fi Khabaru’l-Awa’il wa’l-Awakhir” kuhusiana na suala la Saqifa: Umar alikwenda nyumbani kwa Ali akiwa amejiandaa kuichoma nyumba moto pamoja na wote waliokuwemo ndani yake. Umar alisema: Ingieni kwenye kile ambacho umma umeingia.”

Tabari, katika kitabu chake Ta’rikh Jz. 2, uk. 443, anasimulia kutoka kwa Ziyad Bin Kalbi kwamba, “Talha, Zubair, na baadhi ya Muhajirin walikuwa nyumbani kwa Ali. Umar bin Khattab alikwenda huko na kuwataka watoke nje. Kama hawakutoka, alisema, angeichoma nyumba moto.”

(12) Ibn Shahna, katika “Hashiyya-e-Kamil” ya Ibn Kathir, Jz. 11, uk. 112, anaandika kuhusiana na suala la Saqifa kwamba: “Baadhi ya Masahaba wa Mtume, na Bani Hashim, Zubair, Atba Bin Abi Lahab, Khalid Bin Sa’id Bin As, Mikidadi Bin Aswad Kindi, Salman Farsi, Abu Dharr Ghifari, Ammar Bin Yasir, Bara’a Bin Azib, na Ubai Bin Ka’b walikataa kula kiapo cha utii kwa Abu Bakr. Walijikusanya katika nyumba ya Ali. Umar Bin Khattab alikwenda kule kwa nia ya kuichoma nyumba. Fatima akamlalamika. Umar akasema: “Ingia kule ambako wengine wameingia.”

Hizi ni sampuli tu za ukweli mwingi wa kihistoria ulioandikwa na wanahistoria wenu. Suala hili lilikuwa linajulikana sana kiasi kwamba washairi wa zamani wamelitaja. Mmoja wa washairi wenu, Hafidh Ibrahim wa Misr, anasema katika shairi la kumsifu Umar: “Hakuna mtu mwingine bali Abu Hafsa (Umar) ambaye angelikuwa na ujasiri wa kumuambia mkuu wa ukoo wa Adnan (Ali) na jamaa zake, akisema: ‘Kama mkishindwa kula kiapo cha utii, nitaichoma nyumba yenu, hata Fatima mwenyewe.’”

Hafidhi: Hadithi hizi zinaonyesha tu kwamba walichukuwa vijinga vya moto kuwatisha na kuwatawanyisha wapinzani wa ukhalifa. Kusema kwamba nyumba ya Ali ilichomwa moto na matokeo yake Fatima kuharibu mimba yake, ni maneno yaliyobuniwa na Mashi’a.

Riwaya Kuhusu Kuharibika Mimba Ya Fatima

Muombezi: Ungesoma Kitab-e-Isbatu’l-Wasiyya, kilichokusanywa na Abi’l-Hasan Ali Bin Husain Mas’udi, mwaandishi wa Muruju’dh-Dhahab. Aliandika kwa urefu sana kuhusu tukio la siku hiyo: “Walimzingira Ali na kuchoma mlango wa nyumba yake. Walimburuza kumtoa nje ya nyumba na wakambana mbora wa wanawake, Fatima, kati ya mlango na ukuta kwa nguvu sana kiasi kwamba Muhsin, mtoto wake ambaye alikuwa hajazaliwa, akafa kwa mimba yake kuharibika.”

Mashi’a hawakuyabuni mambo haya. Kilichotokea kimehifadhiwa katika kurasa za historia. Kuharibika kwa mimba ni habari za kweli.

Vile vile unaweza kurejea kwenye Sharhe Nahju’l-Balagha, Jz, 3, uk. 351. Ibn Abi’l-Hadid anaandika kwamba alimuambia mwalimu wake, Abu Ja’far Naqib, kwamba wakati Mtume alipoelezwa kwamba Hubbar Bin Aswad amevipiga vitoto vya binti yake (vikiwa tumboni bado) kwa mkuki, ambapo kwa sababu hiyo Zainab akaharibu mimba yake, Mtume aliruhusu yeye auwawe. Abu Ja’far akasema: ‘Lau Mtume wa Allah angelikuwa hai bado, kwa hakika angeamuru adhabu ya kifo vile vile kwa yule ambaye amemtisha Fatima kiasi kwamba mtoto wake Muhsin, alikufa kwa mimba yake kuharibika.’”

Hafidhi: Sielewi inasaidia lengo gani la manufaa kwa kusimulia visa hivi. Mambo ya aina hii husababisha kutokuelewana kwa pande hizi mbili.

Muombezi: Unakataa kusimulia kwangu mambo haya. Lakini ninafanya hivi kukana shutuma za waandishi waovu wanaowapoteza ndungu zetu ambao hawana ujuzi, na kuwaiTa Mashi’a makafir na kusema kwamba mambo haya yalikuwa ni ubunifu wa Mashi’a. Hatusemi kitu chochote kuhusu Ali mbali na kile ambacho Mtume amesema kuhusu yeye.

Tuliwaeleza katika mikesha iliyopita kwamba tunamchukulia Ali kama mja mtiifu wa Allah, makamu na mrithi wa Mtume aliyeteuliwa kwa utaratibu wa Mungu. Unadai kwamba hakuna maana ya kusimulia mambo haya. Kama msingezileta nukta hizi, tusingezijadili.

Kama msingesema usiku huu kwamba hizi ni imani za Shia bila hoja ya msingi kwazo, nisingelazimika kuiambia hadhara hii kwamba hizi ni imani za maulamaa wa ki-Sunni wasio na upendeleo.

Nawab: Mheshimiwa, tunaamini kwamba Husein, ash-Shahid, alikuwa ameongoka sawa-sawa na kwamba aliuawa kwa dhulma na maofisa wa Bani Umayya. Lakini kuna baadhi ya watu, hususan miongoni mwa vijana wetu, ambao wanasema kwamba vita vya Karbala vilikuwa ni vya kijeshi (kisiasa), na sio kadhia ya kidini. Inasemekana kwamba Husein Bin Ali alielekea Kufa kutafuta mamlaka, na ni jukumu la kila serikali kuzima hatari kama hizo.

Kwa hiyo, Yazid alizuia tishio hili. Walimtaka Mtukufu Imamu kula kiapo cha utii bila masharti kwa Khalifa Yazid, ambaye kwamba utii kwake ilikuwa ni wajibu. Walimtaka aende Syria akaishi kule na Khalifa kwa heshima au arudi mjini kwake (Madina).

Lakini hakufuata ushauri wao, na hatimaye aliuawa. Wanahitimisha kwamba maombolezo yoyote kwa ajili ya mtu wa kidunia kama huyu, ambaye aliuawa kwa ajili ya mapenzi yake ya mamlaka, sio tu hayana maana, bali pia ni bid’a. Je, una jibu kwenye nukta hii? Unakanusha vipi wazo la kwamba vita vya Karbala havikuwa kilele cha harakati za kisiasa?

Imamu Husein Kamwe Hakutamani Nguvu Za Kisiasa

Muombezi: Kila tendo zuri au baya linategemea elimu yetu juu ya Allah. Wapinzani lazi- ma kwanza wamtambue Allah, na kisha lazima wakubali Kitabu cha Mungu, Qur’ani. Kutokana na kukubali huko, ina maana kwamba tunatambua kwamba chochote kile kilichoko ndani ya Kitabu ni sahihi. Mtu yeyote anayeamini kwamba Husein Bin Ali alishaw- ishiwa na malengo ya kidunia anakataa ukweli wa Qur’ani Tukufu. Allah (swt) ametoa ushahidi wa usafi wa Husein katika Qur’ani Tukufu. Anasema: “…Allah anapenda kuwaondoleeni uchafu, Enyi watu wa nyumba (Ahlu’l-Bayt)! Na kuwatakaseni kwa utakaso ulio safi kabisa…” (Qur’ani; 33:33).

Maulamaa wenu wengi, kama Muslim, Tirmidhi, Tha’labi, Sijistani, Abu Nu’aim Isfahani, Abu Bakr Shirazi, Suyuti, Hamwani, Ahmad Bin Hanbal, Zamakhshari, Baidhawi, Ibn Athir, na wengine wameshikilia kwamba aya hii iliteremshwa kwa kuwatukuza wale watukufu watano, Ahlu’l-Bayt (watu wa Nyumba): Muhammad, Ali, Fatima, Hasan na Husein. Aya hii ndio uthibitisho mkubwa wa kutokukosea (Ma’sum) na usafi wa watu hawa watukufu. Uchafu mkubwa sana ni mapenzi ya mamlaka ya kidunia. Kuna hadithi nyingi kutoka kwa Mtume na Maimamu zinazolaumu hamu ya mamalaka ya kidunia na utekelezaji wa matamanio yetu maovu.

Mtume alisema: “Mapenzi na urafiki na dunia ni mzizi wa maovu yote.” Abu Abdillah Husein hakuwa na mapenzi na mamlaka ya kidunia. Kwa kweli hakuhatarisha maisha yake na maisha ya familia yake kwa ajili ya kupata utawala wa mpito katika dunia hii.

Kama kusimama kwa Husein dhidi ya Yazid kulikuwa kwa ajili ya mamlaka ya kilimwengu tu, Mtume asingeamuru watu kumsaidia. Maulamaa wenu wenyewe wanathibitisha nukta hii. Sheikh Suleimani Balkhi Hanafi katika “Yanabiu’l-Mawadda” kutoka katika vitabu vya historia vya Bukhari, Baghawi, na Ibnu’s-Sikkin kutoka Dhakha’iru’l-Uqba ya Imamu’l-Haram Shafi’i, na Sirat-e-Mulla wanasimulia kutoka kwa Anas Bin Harith Bin Bayya, ambaye amesema kwamba alimsikia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akisema: “Hakika, mtoto wangu Husein atauawa katika ardhi ya Karbala. Kila mtu kati yenu ambaye atakuwepo wakati huo lazima amsaidie.”

Taarifa inaendelea: “Anas Bin Harith alifika Karbala na kwa kutii amri ya Mtume, aliuawa shahidi pamoja na Imamu Husein.” Kwa hiyo ina maana kwamba kule Karbala Imamu Husein alisimama kwa ajili ya haki na sio kwa mapenzi ya dunia hii. Kuandaa safari kwa Imamu Husein akiwa na kundi dogo, wakiwemo wanawake na watoto wadogo, ni ishara nyingine kuonesha kwamba alitoka nyumbani kwake sio kwa madhumuni ya kupata mamlaka.

Kama hiyo ingekuwa ndio nia yake, angelikwenda Yemen, ambako anaungwa mkono na wengi. Yemen ingelikuwa ni kituo cha kimantiki cha kuanzishia shughuli za kijeshi. Kwa hakika rafiki zake mara nyingi wamemshawishi kwenda Yemen, lakini walikuwa hawatambui madhumuni yake.
Lakini Imamu Husein alijua kwamba hakuna njia ya kupa- ta mafanikio ya dhahiri. Safari yake ilianza na watu 84, wakiwemo wanawake na watoto, akilenga kwenye msingi mzuri. Ule mti mtukufu – la ilaha ill’allah (hakuna mungu isipokuwa Allah) – ulipandwa na babu yake, ukarutubishwa na damu yake na damu ya mashahidi wa Badir, Uhud, na Hunain. Mti huo uliaminishwa kwa mtunza bustani mzuri, Ali Bin Abu Talib, ambaye alizuiwa kwa vitisho vya mauaji na uchomaji moto mali wa makusudi.

Matokeo yake ilikuwa kwamba ile chemchem ya Tawhid (upweke wa Mungu) na utume ukakumbwa na mbadiliko ya kipupwe. Taratibu utawala wa bustani ukaangukia mikononi mwa Bani Umayya waovu.

Kuanzia ukhalifa wa Uthman Bin Affan, Bani Umayya wakahodhi utawala wa dola. Abu Sufyan, mzee na kipofu, lakini daima hamu yake ya mamlaka ilikuwa kali, alipiga kelele kwenye baraza ya Bani Umayya: “Enyi Bani Umayya! Uzuieni ukhalifa kwenye familia yenu wenyewe.

Pepo na moto ni ngano za watu wa kale. Enyi Bani Umayya! Ukamateni ukhalifa kama mpira. Naapa kwa kile ambacho nakiapia, kwamba kila siku nimetamani utawala huu kwa ajili yenu. Uchungeni ili kwamba uwe ni urithi wa vizazi vyenu.”

Makafiri hawa waliwaondoa watunza bustani sahihi kutoka kwenye bustani. Maji ya uhai yalisimamishwa na mti mtukufu ulisinyaa mpaka wakati wa utawala wa Yazid, wakati ulipoonekana kuelekea kufa.

Imamu Huseini akasafiri kwenda Karbala kuinyweshea ile bustani ya utume na kuimarisha ule mti mtukufu wa la ilha ill’Allah. Baadhi ya watu wanahoji kwa nini Imamu Husein asipandishe bendera ya upinzani mjini Madina. Hawajui kwamba angebakia Madina malengo yake yangelibakia bila kueleweka. Imamu Husein alikwenda Makka katika mwezi wa Rajabu alihutubia maelfu ya watu, akiwambia kwam- ba Yazid alikuwa anaung’oa mti wa Tawhid.

Alisema kwamba Yazid ambaye alidai kuwa Khalifa wa Waslamu, alikuwa anauharibu msngi wa Uislamu. Akiwa ametawaliwa na ulevi wa pombe na kamari, Yazid alijiburudisha kwa kucheza na mbwa na manyani. Imamu Husein aliona kutoa mhanga maisha yake ni muhimu kwa ajili ya kuuhifadhi Uislamu.

Imamu Husein Alikataa Ushauri Wa Kuuacha Ujumbe Wake

Marafiki wa Imamu Husein na jamaa zake wamshawishi asiende Kufa, wakisema kwam- ba watu wa Kufa waliomtaka aende kule wana sifa mbaya wasioaminika. Watu wengi walikusanyika kwa Bani Umayya na kupokea pesa na upendeleo wa kisiasa kwa malipo ya kuwaunga mkono kwao. Kwa hiyo, kwa mujibu wa wengi wa wafuasi wake, Imamu Husein hakuwa na nafasi ya kuweza kuwashinda.

Walimuomba aache safari yake hiyo. Walimhimiza aende Yemen ambako alikuwa na wafuasi wengi, na ambako angeweza kuishi kwa amani. Lakini Huseini hakuweza kuelezea ukweli wa hali yake. Hata hivyo, alimtosheleza kila mmoja kwa jibu fupi.

Aliwaambia marafiki wa karibu na jamaa zake, kama ndugu yake, Muhammad Bin Hanafiyya: Unasema jambo sahihi. Mimi vile vile najua kwamba sitapata umiliki wa dhahiri, lakini siendi kwa ajili ya ushindi wa kidunia. Ninakwenda ili nikauawe. Natamani kwamba kwa kupitia nguvu yangu ya kuteseka kwa uonevu, ningeweza kuung’oa msingi wa udhalimu na ukatili. Nimemuona babu yangu, Mtume, katika ndoto akiniambia: ‘Fanya safari ya kwenda Iraq. Allah (swt) anataka kukuona wewe ukiuliwa.’”

Muhammad Bin Hanafiyya na Ibn Abbas wakasema: “Kama hivyo ndivyo, kwa nini unakwenda na wanawake?” Akajibu: “Babu yangu amesema kwamba Allah anataka kuwaona wao wakiwa mateka. Hivyo, kutokana na amri ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), ninawachukuwa na kwenda nao.” Kutekwa kwa wanawake kutakuwa ndio sehemu ya maamuzi ya kuuliwa kwake shahidi.

Watauonesha ulimwengu ukatili wa Bani Umayya kwa kizazi cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Bibi Zainabu binti wa Ali na Fatima, alitoa hotuba fasaha ya malalamiko katika baraza ya Yazid iliyojaa watu, ambapo mamia ya watu, wakiwemo watu maarufu, watu wakubwa kutoka Bani Umayya, na mabalozi wa nje, walisheherekea ushindi wao.

Imamu wa nne, Zainu’l-Abidin Ali Ibn Husein, naye vile vile alitoa hotuba ya madai fasa- ha juu ya haki na uadilifu katika mimbari ya Msikiti wa Bani Umayya, mbele ya Yazid. Baada ya kumtukuza Allah (swt) Zainu’l-Abidin alisema: “Enye watu! Sisi kizazi cha Mtume Muhammad, tumejaaliwa na Allah sifa sita na tumefanywa wabora kwa viumbe wote kwa kupewa fadhila saba.

Tumepewa elimu, uvumilivu, ujasiri, haiba yenye kupendeza, ufasaha, ushujaa, na tunapendwa na waumini. Sisi ni bora juu ya kila mtu kwa sababu Mtume Muhammad anatokana na sisi; Siddiq Ali Bin Abu Talib anatoka kwetu; Ja’far-e-Tayyar anatoka kwetu; Hamza anatoka kwetu, wajukuu wawili wa Mtume, Hasan na Husein, wanatoka kwetu; na Mahdi wa uma huu (Imam-e-Hujjat Bin Hasan) anatokana na sisi. Mtu ambaye hanijui mimi anapaswa ajue kuhusu familia yangu na hadhi yake; mimi ni mtoto wa Mtume wa Allah aliyetukuka mno na mbora, Muhammad Mustafa!”

Kisha kutoka kwenye mimbari ileile ambayo Mu’awiya na Yazid waliitumia kumtukana Ali, Imamu alimtukuza babu yake mashuhuri wa kupigiwa mfano, Ali Bin Abu Talib, mbele ya Yazid na wakuu wa Bani Umayya.

Watu wengi wa Syria hawajawahi kusikia sifa za Ali na fadhila zake. Imamu akasema: “Mimi ni mtoto wa mtu yule ambaye alipigana mbele ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.); ambaye awalipiga makafiri kule Badir na Hunain; ambaye katu hakupoteza imani yake kwa Allah japo kwa sekunde.

Mimi ni mtoto wa mtu mchamungu mno zaidi wa waumini wote, mrithi wa mitume, muuaji wa makafir, mtawala wa Waislamu, rehema ya waabuduo, mfalme wa wale ambao wanalia kwa hofu juu ya Allah, mvumilivu mno wa wavumilivu, mbora wa wanaotekeleza Salat.

Mimi ni mtoto wa mtu ambaye alisaidiwa na Jibril na Mikail. Mimi ni mtoto wa mtu yule ambaye alikuwa mlinzi wa heshima ya Waislamu na mkataji vichwa vya makafir. Ni mtoto wa mtu yule ambaye alipigana vita takatifu dhidi ya maadui, ayelikuwa fahari ya Makuraishi, mtangulizi wa wale walioukubali ujumbe wa Allah na Mtume Wake, wa kwanza kati ya wale walioukubali Uislamu, ulimi wa hekima ya Allah, msaidizi wa dini ya Allah, mlinzi wa amri za Allah, bustani ya hekima ya Allah, hazina ya elimu Yake.

Mimi ni mtoto wa mkuu wa wenye subira, mvunjaji wa vizuizi, ambaye moyo wake ulikuwa imara zaidi, ambaye maamuzi yake yalikuwa imara zaidi, ambaye tabia yake ilikuwa imara sana kuliko mtu yeyote. Alikuwa simba mkali kwenye uwanja wa vita, ambaye aliwakata maadui na kuwaangusha chini kwa upanga wake na kuwatawanya kama upepo mkali unavyotawanya majani makavu.

Alikuwa ndiye shujaa zaidi miongoni mwa watu wa Hijaz, jasiri zaidi miongoni mwa watu wa Iraq, Mwislamu safi zaidi, yeye ambaye alikula kiapo cha utii kule Aqaba, shujaa wa Badir na Hunain, mtu jasiri zaidi wakati wa kiapo cha utii chini ya mti, mtoa kafara wa aina yake, ya kipekee wakati wa kuhama kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), mkuu wa ulimwengu wa ki-Arabu, mlinzi wa Ka’ba Tukufu, baba wa wajukuu wawili wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Hizi ni sifa za babu yangu, Ali Bin Abu Talib.

Mimi vile vile ni mtoto wa Khadijatul-Kubra; mimi ni mtoto wa Fatima Zahra; mimi ni mtoto wa yule ambaye ameuawa kwa dharuba nyuma ya shingo; mimi ni mtoto wa yule ambaye aliutoka ulimwengu huu akiwa na kiu; mimi ni mtoto wa yule ambaye alinyimwa maji wakati ambapo maji yaliruhusiwa kwa viumbe waliobakia. Mimi ni mtoto wa yule ambaye mwili wake haukuoshwa wala kuvishwa sanda; mimi ni mtoto wa yule ambaye kichwa chake kitukufu kilinyanyuliwa katika ncha ya upanga; mimi ni mtoto wa yule ambaye wanawake wake walikashifiwa na kunyanyaswa waziwazi katika ardhi ya Karbala na kuchukuliwa mateka. Mimi ni mtoto wa yule ambaye wanawake wake waliletwa Syria kama mateka.”

Kisha Imamu alilia kwa sauti kubwa, na kuendelea: “Mimi ni…Mimi ni…” yaani, aliendelea kueleza fadhila za wahenga zake waliomtangulia na mateso ya mtukufu baba yake na Ahlu’l-Bayt. Kama matokeo ya hotuba yake hii, watu walilia sana. Baada ya kuliwa shahidi kwa Imamu Husein, majlis ya kwanza (kikao cha maombolezo) kwa ajili ya mateso ya kikatili aliyoyapata Imamu Husein ilifanyika katika Msikiti huu mkuu wa Bani Umayya.

Imamu Zainu’l-Abidin, baada ya kusimulia sifa za Ali mbele ya maadui, alitoa maelezo yenye kugusa nyoyo juu ya mateso aliyopata mtukufu baba yake ambayo yalisababisha kilio kikubwa cha kuumiza kutoka kwa watu wa Syria mbele ya Yazid. Alitishika sana na kuondoka Msikitini pale.
Ilikuwa ni kutoka Msikitini hapa, kutokana na hotuba ya Imamu, ndipo watu wakasimama dhidi ya Yazid. Kwa sababu ya kelele za upinzani mkubwa wa watu, Yazid alilazimika kumlaani Ubaidullah Bin Marjana kwa kitendo chake kiovu. Hatimaye, ngome ya dhulma ya Bani Umayya iliteketezwa. Leo hatuoni katika Syria yote kaburi hata moja la Bani Umayya.

Tukirudi kwenye swali lako, Imamu Husein mara kwa mara alitabiri kuuawa kwake shahi- di. Wakati mmoja aliwahi kusimulia mjini Makka, mnamo siku ya Tarwia (siku ya 8 ya Dhu’l-Hijja 60 A.H.), akisema: “Kifo kimeambatanishwa kwa kila mmoja wa kizazi cha Adamu kama mkufu ulivyoambatanishwa kwenye shingo ya msichana. Nina shauku ya kukutana na wahenga wangu kama vile Yaqub alivyokuwa kwa ajili ya kukutana na Yusuf. Sehemu ambayo nitafia imekwishateuliwa kwa ajili yangu, na lazima niende kwenye sehemu hiyo. Ninawaona chui mwitu wakiniuwa, wakichana vipande vipande mwili wangu kati ya Nawawi’s na Karbala.”

Imamu Husein alijua kwamba hatafika Kufa, makao makuu ya Iraqi (zama hizo). Alijua kwamba atauawa na watu ambao walikuwa kama wanyama wakali, wakikata mwili wake vipande vipande. Alifanya safari hiyo kwa madhumuni ya kufa shahidi na sio kwa sababu za kisiasa.

Njiani humo aliwambia watu juu ya kifo chake kinachomngojea. Aliwaeleza marafiki zake na jamaa zake kwamba mfano mmoja ulikuwa unatosha kuthibitihsa jinsi ulimwengu huu usivyokuwa na thamani. Alisema kwamba baada ya Nabii Yahya kukatwa kichwa chake, kichwa hicho kiliwasishwa kwa mzinifu. Alisema kwamba kichwa chake yeye hivi punde kitachukuliwa kupelekwa kwa mlevi, Yazid.

Fikiria suala hili kwa muda. Hur Bin Riyahi pamoja na kikosi cha farasi cha askari 1000 waliizuia njia ya Husein. Kufa ilikuwa umbali wa maili thalathini tu. Hurr alikuwa ameteuliwa na Ubaidullah Ibn Ziyad kumzuia Imamu Husein. Hurr alikuwa asimuachie andelee kwenda Kufa wala kuachana naye bila kupata maelekezo zaidi. Kwa nini Imamu alijisalimisha kwa Hurr? Kama Husein alikuwa akitafuta mamlaka ya kisiasa, kwa hakika asingeweza kuzuiwa na Hurr, ambaye alikuwa hana zaidi ya askari 1000. Imamu alikuwa na askari 1300.

Hali ya kuwa angewashinda, Imamu angelifika Kufa, ambako ana watu wengi wanaomuunga mkono. Kutoka huko hali ya kuwa jeshi limeongezeka nguvu, angeweza kukabiliana na adui na kupata umiliki. Lakini alikubali amri ya Hurr, alisimama pale katika jangwa akizunguukwa na adui. Baada ya siku nne majeshi ya nyongeza ya adui yaliwasili pale, na mtoto wa Mtume akalazimika kustahamili mateso ya ukatili.

Ushahidi mzuri katika kuunga mkono maoni yangu ni hotuba ya Imamu katika usiku wa kuamkia Siku ya Ashura. Mpaka usiku ule askari 1300 walikuwa wako tayari kupigana kwa ajili yake.

Husein aliwakusanya watu hao pamoja na akawaambia: “Wale ambao wamekuja kwa ajili ya kupata faida ya kidunia, basi wajue kwamba yeyote atakayebakia hapa kesho katika ardhi hii atauawa. Adui ana haja na mimi peke yangu; naondoa nguvu ya kifungo cha utii kutoka katika shingo zenu. Huu sasa ni usiku, na mnaweza kuondoka katika giza hili la usiku.” Wengi walikubali pendekezo lake na wakaondoka. Watu 42 tu walibakia, 18 Bani Hashim na 24 Masahaba.

Baada ya usiku wa manane, askari 30 wa adui walielekea kwenye kambi ya Imamu kwa ajili ya mashambulizi ya usiku, lakini walipom- sikia Husein akisoma Qur’ani Tukufu, walijawa na jazba na wakaungana na Imamu. Hawa ndio wale watu 72 waliojitolea mhanga maisha yao Siku ya Ashura. Wengi wao walikuwa wachamungu, na wengi walikuwa ni wasomaji wa Qur’ani Tukufu.

Leo mhanga mtukufu wa Husein unakubaliwa na marafiki na maadui kwa pamoja. Hata wale ambao ni wageni katika dini yetu wamevutia na ushujaa wake. Katika Da’iratu’l- Ma’rif ya Kifaransa, kuna makala ndefu yenye anwani ya “Mashahidi watatu” iliyoandikwa na mwanachuo mwanamke wa Kiingereza. Dhamira yake ni kwamba katika historia yote kumekuwa na mashahidi watatu, ambao kwa kujitolea kwao mhanga maisha yao, wamekuwa kivutio kikubwa katika kuendeleza njia ya haki. Wa kwanza alikuwa ni Socrates, na wa pili alikuwa ni Yesu - Isa Masihi (mwandishi alikuwa ni Mkristo). Sisi Waislamu, kwa hakika tunaamini kwamba Isa hakusulubiwa. Qur’ani Tukufu kwa uwazi inasema:

وَقَوْلِهِمْ إِنَّا قَتَلْنَا الْمَسِيحَ عِيسَى ابْنَ مَرْيَمَ رَسُولَ اللَّهِ وَمَا قَتَلُوهُ وَمَا صَلَبُوهُ وَلَٰكِنْ شُبِّهَ لَهُمْ ۚ وَإِنَّ الَّذِينَ اخْتَلَفُوا فِيهِ لَفِي شَكٍّ مِنْهُ ۚ مَا لَهُمْ بِهِ مِنْ عِلْمٍ إِلَّا اتِّبَاعَ الظَّنِّ ۚ وَمَا قَتَلُوهُ يَقِينًا {157}

بَلْ رَفَعَهُ اللَّهُ إِلَيْهِ ۚ وَكَانَ اللَّهُ عَزِيزًا حَكِيمًا {158}

“Na hawakumuuwa wala hawakumsulubisha, bali walifananishwa kwao (mtu mwingine, kama Isa), na kwa hakika wale ambao wanatofautiana kwalo wana shaka juu ya hilo. Hawana elimu kuhusiana nalo, bali hufuata dhana tu. Kwa yakini hawakumuuawa. Hasha! Allah alimchukuwa juu Kwake.” (Qur’ani 4:157-158)

Shahidi wa tatu, anaandika mwanamke huyu, alikuwa ni Husein, mjukuu wa Muhammad. Anaandika: “Wakati tunapokusanya matukio ya kihistoria na kuyaangalia yale mazingira ambamo watu hawa watatu walitoa maisha yao, tunakubali kwamba mhanga wa Husein uliipita ile mingine miwili. Ukweli ulikuwa kwamba, Socrates na Yesu walitoa tu maisha yao wenyewe kwa kafara katika njia ya Mungu, lakini Husein alitoka nyumbani kwake kwenda nchi ya mbali ya jangwa kwenda kuzunguukwa na adui.

Yeye na familia yake yote waliuawa mashahidi kwa ajili ya kutetea njia ya haki. Aliwapeleka rafiki na jamaa zake kumkabili adui na kutoa mhanga maisha yao kwa ajili ya dini ya Allah. Hii kwa hakika ilikuwa ni ngumu mno kuliko kutoa maisha yake mwenyewe.”

Mfano wa dhahiri zaidi wa mateso ya udhalimu aliyopata Husein ulikuwa ni yale mauaji ya kikatili ya mtoto wake mdogo wa miezi sita. Alimbeba mtoto mikononi mwake akiomba maji kwa ajili yake (ambayo yalikuwa mengi), lakini maadui wakatili wale, badala ya kumpa maji, walimuuwa mtoto yule kwa mshale. Ushenzi huu wa maadui unathibitisha kwamba Imamu Husein alikuwa ni muathiriwa wa udhalimu.

Uvumilivu wake wa kushangaza ulivunjilia mbali kabisa nguvu za Bani Umayya na uliwashutumumbele ya ulimwengu. Ilikuwa ni kwa ajili ya mihanga yake na Ahlu’l-Bayt wake watukufu ambapo dini ya Muhammad ilipata uhai mpya.

Nawab: Kwa hakika tunawiwa mno na wewe. Tumevutiwa sana na maelezo yako ya mambo yanayomhusu Imamu Husein. Mpaka sasa tulikuwa tunafuata watu wengine na tulikuwa tunazikosa fadhila za ziarat (kuzuru kaburi tukufu la Imamu). Tumeambiwa kwamba kuzuru kaburi la Imamu Husein ni bida’a “uzushi.” Ama kwa hakika ni bida’a nzuri iliyoje hiyo, kwa vile humfanya mtu awe na ari na kumsaidia aelewe ukweli kuhusu kizazi cha Mtume.

Maana Halisi Ya Bida’a (Uzushi)

Muombezi: Neno “bidat,” lina asili yake katika madhehebu ya maulamaa wa ki-Sunni na ya Nasib na Khawarij, ambao walikuwa ni maadui waliothibitika wa Ali. Wameiita ziarat “bida’a” bila kufikiria ukweli kwamba bida’a inahusian na jambo linalohusu Mtume au Ahlul’Bayt wake, ambalo halikuamriwa na Allah.

Hata hivyo, kuhusu suala la kuzuru kaburi la Husein, kuna hadithi nyingi katika vitabu vya maulamaa wenu wenyewe. Nitakomea kwenye hadithi moja mashuhuri iliyoandikwa katika vitabu vyote vya maqatil na hadith mukhtar.

“Siku moja Mtume alikuwa nyumbani kwa Aisha wakati Husein alipoingia ndani. Mtume alimchukuwa mikononi mwake, akambusu na kumnusa. Aisha akasema: ‘Maisha ya baba yangu na mama yangu yawe mhanga kwa ajili yako! Kiasi gani unampenda Husein!’

Mtume akasema: ‘Hujui kwamba mtoto huyu ni sehemu ya ini langu na ua langu?’ Baada ya hapo Mtume akaanza kulia.

Aisha akauliza sababu ya kulia kwake. Mtume akajibu kwamba alibusu mahali ambako Bani Umayya watakuja kumjeruhi Husein. Aisha akauliza kama watamuuwa.

Akasema, ‘Ndio atauawa. Hawatapata usaidizi wangu (kesho akhera). Aliyebarikiwa ni yule anayekwenda kuzuru kaburi lake baada ya shahada yake.’ Aisha akamuuliza Mtume, ni malipo gani yatakuwa kwa ajili ya ziarat hiyo. Mtume akasema:
‘Itakuwa ni sawa na hijja yangu moja.’ Aisha akasema, ‘Hijja moja ya kwako!’ Akasema, ‘Hapana, mbili,’ Aisha alipoonesha mshangao tena, akasema, ‘Hapana, Hijja nne.’

Jinsi alivyozidi kuonesha mshangao ndivyo malipo yalivyozidi kuongezeka, mpaka mwishowe akasema, ‘Aisha! Kama mtu atakwenda kuzuru kabutri la Husein, Allah atampa malipo sawa na Hijja 90 na Umra 90 zilizofanywa na mimi.’ Kisha Aisha akanyamaza.’” Sasa nakuulizeni, Ziarat kama hiyo ni uzushi (bida’a)?

Faida Za Kuzuru Makaburi Ya Maimamu Watukufu

Kuna faida nyingine ambazo hupatikana kwa kuzuru makuburi ya Maimamu. Sehemu za ndani kabisa za eneo la kaburi, zinazoitwa haram, hubakia wazi kwa ajili ya wangeni usiku na mchana. Haram hizo na misikiti karibu yake kwa kawaida huwa zinakutwa zimejaa mahujaji na wafanyao ibada.

Wale ambao wamezoea kusali si zaidi ya Salat za wajibu mara nyingi hufanya jitihada maalumu za kiibada wakati wa kuzuru makaburi matukufu. Wanamuomba Allah kwa unyofu na kusoma Qur’ani. Je, ibada kama hiyo ni bida’a?

Nawab: Kwa hakika hatuna wa kumlaumu isipokuwa sisi wenyewe kama hatukuyaangalia mambo haya kwa ukaribu zaidi. Miaka michache iliyopita nilikwenda Baghdad kuzuru kaburi la Imam A’Dham Abu Hanifa na Abdu’l-Qadir Jilani. Siku moja nilikwenda kutembea karibu ya Kadhmain (sehemu aliyozikwa Imamu wa saba, Musa Ibn Ja’far Al-Kadhim na Imamu wa tisa, Muhammad Ibn Ali at-Taqi).

Wakati niliporudi, wenzangu walinilaumu vikali sana. Nashangaa kwamba kuzuru makuburi ya Imam A’dham huko Mu’dham, Sheikh Abdu’l-Qadir huko Baghdad, la Khwaja Nidhamu’d-Din huko India, la Sheikh Akbar Muhyi-d-Din Ibn Arabi huko Misr kunaweza kuchukuliwa kwamba kunastahili

malipo ya thawabu. Kila mwaka watu wengi miongoni mwa madhehebu ya Sunni huzuru sehemu hizi ingawa Mtume kamwe hajalipendekeza hilo. Inawezekana vipi kwamba ziarat kwenye kaburi la Shahidi mkuu, mjukuu wa Mtume, ambayo Mtume ameipendekeza, iambiwe kuwa ni bida’a?

Naamua kwa dhati kabisa kwamba, Allah akipenda, mwaka huu nitakwenda kuzuru kaburi la mjukuu kipenzi cha Mtume, Husein. Nitamuomba Allah anisamehe makosa yangu yaliyopita.