read

Mkutano Wa Sita Jumanne Usiku 28 Rajab 1345 A.H.

Bwana Ghulam Imamain, mfanyabiashara wa Kisunni mwenye kuheshimika, alikuja katika sehemu ya mkutano kabla ya jua kuzama. Alitaja sababu yake ya kuja. Alisema kwamba yeye na watu wengine walivutiwa sana na maelezo ya Muombezi. Akasema kwamba amesikia ukweli ambao hajapata kuusikia kabla yake.

Yeye na baadhi ya Sunni wengine walikuwa na majadiliano yasiyopendeza na Maulamaa wao, ambao hawakuweza kukanusha hoja za Muombezi lakini ambao kwa ukaidi wameng’angania msimamo wao. Wakati wa Sala ya Magharibi ulipowadia, Bw.Ghulam Imamain alisali Sala zote Magharibi na Isha nyuma ya Muombezi. Wakati wengine walipowasili, mjadala ulianza na ushauri wa Nawab Sahib.

Nawab: Tafadhali endelea na mazungumzo ya usiku wa jana. Tafsir ya ile aya ilikuwa haikukamilika.

Muombezi: (Akiangalia upande wa Maulamaa wa Kisunni). Mradi na nyie mliruhusu hilo.

Hafidh: (Kwa hasira kidogo). Hakuna madhara. Kama kuna kitu kimebakia kusemwa, tuko tayari kukisikiliza.

Muombezi: Usiku uliopita nilithibitisha kwa mtazamo wa kinahau kwamba maelezo ya baadhi ya wafasiri wanaosema kwamba aya hii huonyesha namna ya kuamua ukhalifa yalikuwa hayakubaliki. Sasa nitaelezea kutokana na mtazamo mwingine.

Sheikh Abdu’s-Salam Sahib alisema usiku uliopita kwamba kuna sifa nne zilizotajwa katika aya hii. Sifa hizi, alisema, zinaonyesha kwamba aya hii iliteremshwa kwa habari ya Makhalifa wanne wa kwanza na kwamba aya hii inaonyesha mpango wa ukhalifa.
Majibu yangu kwa hoja hii ni: kwanza, wafasir wenye kuaminika hawajawahi kutoa maelezo kama hayo kuhusu maana halisi ya aya hii.

Pili, nyote mnajua kwamba wakati sifa inapohusish- wa na mtu inaenda sawasawa na tabia yake, hapo ndipo (sifa hiyo) itakuwa na maana. Kama tutayaangalia mambo kwa busara zaidi, tunaona kwamba ni Ali tu ambaye alikuwa na sifa hizo zilizoelezewa katika aya hii. Sifa hizi kwa njia yoyote haziafikiani na hizo zilizotajwa na Sheikh Sahib.

Hafidh: Aya zote hizo ulizokwishasimulia kuhusu Ali hazikutosha? Unataka sasa kwa ujanja wako wa ufasaha wa kusema kuthibitisha kwamba aya hii tukufu vilevile iliteremshwa kwa kumtukuza Ali? Kama ni hivyo, hebu tujulishe ni vipi haikubaliani na ukhalifa wa makhalfa wanne wa kwanza.

Aya Mia Tatu Zenye Kumtukuza Ali.

Muombezi: Sijahusisha Aya ya Qur’ani Tukufu kwa kumtukuza Ali kwa uongo. Umechanganya mambo. Unaweza ukapuuza ukweli kwamba tafsiri zenye kujulikana vizuri na vitabu vyenye kuaminika vilivyoandikwa na Maulamaa wenu wenyewe vimeta- ja aya nyingi za Qur’ani Tukufu zikiwa ni za kumtukuza Ali? Unawezaje kuona kuwa ni kitu cha pekee kwangu? Je, Hafidh Abu Nua’im Isfahani, muandishi wa “Ma-Nazala nina’l-Qur’ani Fi Ali”, na Hafidh Abu Bakr Shirazi, muandishi wa “Nuzulu’l-Qur’ani Fi Ali”, walikuwa Mashi’a? Je, wafasiri wakubwa, kama Imam Tha’labi, Jalalu’d-Din Suyuti, Tabari, Imam Fakhru’d-Din Radhi, na Maulamaa wengine wenye sifa kubwa, kama Ibn Kathir, Muslim, Hakim, Tirmidhi, Nisa’i, Ibn Maja, Abu Dawdi, Ahmad Bin Hanbal, na hata Ibn Hajar asiye mvumilivu, ambaye amekusanya katika kitabu chake “Sawa’iq” Aya za Qur’ani zilizoteremshwa kumsifia Ali pia walikuwa Shi’a? Baadhi ya ulamaa kama,Tabari, na Muhammad bin Yusufu Ganji Shafi’i mwanzoni mwa kitabu chake sehemu ya 62, anasimulia kutoka kwa Ibn Abbas, na Muhadith wa Syria katika kitabu chake “Tarikh-e-Kabir”, na wengine wameandika Aya nyingi kiasi kama mia tatu za Qur’ani Tukufu zenye kumtukuza Ali. Je, watu hawa walikuwa Mashi’a au wanatokana na maula- maa wenu wakubwa?

Hatuhitaji kuhusisha kwa uongo aya ya Qur’ani tukufu kwa ajili ya kuthibitisha cheo cha Amir’l-Mu’minina Ali. Maadui zake (Bani Umayya, Nawasib na Khawarij) wamezuia fadhila zake zisitajwe na marafiki zake wakasita kusimulia ubora wake kwa kuogopa matokeo yake. Bado, vitabu vimejaa fadhila zake na vinatoa mwanga juu ya mambo yote ya kufanikiwa kwake.

Kwa vyovyote inavyohusika aya hii, sikujitia katika “ujanja wa ufanisi wa kusema.” Nimefichua ukweli, nikitoa hoja kutoka katika vitabu vyenu. Mmeona mpaka hapo kwamba sikutoa hoja kutoka kwenye riwaya za waandishi wa Kishi’a. Hata kama vitabu vya Shi’a viwekwe kando, bado nitathibitisha ubora wa kipekee wa Ali. Niliyosema kuhusu Aya hii yanakubaliana na maoni ya Maulamaa wenu wenyewe.

Muhammad bin Yusufu Ganji Shafi’i amenukuu “Hadith ya kufanana” katika kitabu chake “Kifayatut-Talib” Sura ya 23, kutoka kwa Mtume yenye maana kwamba Ali alikuwa anafanana na Mitume. Anasema kwamba sababu ya Ali kuitwa kwamba anafanana na Mtume Nuh katika hekima ni kwamba Ali alikuwa mkali dhidi ya makafiri na mpole kwa waumini. Allah amezitaja sifa hizi katika Qur’ani Tukufu.

Ali ambaye siku zote alikuwa pamoja na Mtume, alikuwa “mkali dhidi ya makafiri na mwenye huruma kwa waumini.” Na ukichukulia, kama Sheikh Sahib anavyosema: kwamba usemi “Na wale ambao wako pamoja naye” unamuashiria Abu Bakr kwa sababu kwa muda wa siku chache alikuwa na Mtume ndani ya Pango, Hivi mtu kama huyo anaweza kuwa sawa na yule aliyekuwa na Mtume tangu utotoni na kupata maelekezo kutoka kwake?

Ali Ni Wa Kwanza Kutangaza Imani Juu Ya Mtume Wa Allah.

Aidha, katika tukio muhimu la kutangaza Utume wake, hakuna aliyemuunga mkono Muhammad isipokuwa Ali. Maulamaa wenu mashuhuli, kama Bukhari na Muslim, kati- ka “Sahih” zao, Imam Ahmad bin Hanbal katika “Musnad” yake, na wengine wengi, kama vile Ibn Abdi’l-Birr katika “Isti’abi”, Jz. 3, uk. 32, Imam Abu Abdu’r-Rahman Nisa’i katika “Khasa’isu’l-Alawi”, Sibt Ibn Jauzifi katika Tadhkira, uk. 63, Sheikh Suleimam Balkhi Hanafi ndani ya “Yanabiu’l-Mawadda”, Sura ya 12, kwa kunukuu kutoka kwa Tirmidhi na Muslim, Muhammad bin Talha Shafi’i katika “Matalibus-Su’ul” Sura ndogo - 1, Ibn Abi’l-Hadid katika “Sharh Nahju’l-Balagha”, Jz. 3, uk. 258, Tirmidhi katika “Jam’e- Tirmidhi”, Jz. 2, uk. 314, Hamwaini katika “Fara’id”, Mir Seyyed Ali Hamadani katika “Mawaddatu’l-Qurba”, na hata yulu shabiki Ibn Hajar katika “Sawa’iq-e-Muhriqa”, na wanachuoni wengine mashuhuri, wameandika pamoja na tofauti kidogo ya maneno, kutoka kwa Anas bin Malik na wengine kwamba:

“Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipewa Utume wa Allah siku ya Jumatatu, na Ali akatangaza imani yake kwake siku ya Jumanne.” Vilevile imesimuliwa tena kwamba: “Utume wa Allah ulitangazwa siku ya Jumatatu na Ali akasali na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) siku ya Jumanne.” Na halafu tena, “Ali alikuwa mtu wa kwanza kutangaza imani yake kwa Mtume.” Vilevile Tabari, Ibn Abi-Hadid, Tirmidhi, na wengine wanasimulia kutoka kwa Ibn Abbas kwamba “Ali alikuwa wa kwanza kusali.”

Kufundishwa Kwa Ali Tangu Utotoni Na Mtume.

Ninakuombeni muangalie wanachuoni wenu, Nuru’d-Din Bin Sabbagh Malik, katika “Fusulu’l-Muhimma.” Sura ya “Tarbiatu’n-Nabi”, uk, 16, na Muhammad Bin Talha Shafi’i, katika “Matalibus-Su’ul”, Sura ya 1, uk. 11, na wengine walichosimulia. Katika wakati mmoja wa ukame hapo Makka, Mtume alimwambia ami yake, Abbas, kwamba, kaka yake, Abu Talib, ana watoto wengi na kwamba uwezo wake wa kujikimu kimaisha ulikuwa ni mdogo. Mtume Muhammad alipendekeza kwamba kila mmoja wao amuombe Abu Talib ampe mtoto mmoja ili kusaidia kupunguza mzigo mzito alionao. Abbas alikubali. Walikwenda kwa Abu Talib na pendekezo lao, na akakubali. Abbas akamchukuwa Ja’far-e-Tayyar kuwa chini ya malezi yake na Mtume akamchukuwa Ali. Malik akaendelea, “Ali alibakia moja kwa moja na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mpaka alipotangazwa kuwa Mtume wa Allah.”

Ali alitangaza Imani yake kwake, na akamfuata kama Mtume wa Allah, wakati huo Ali akiwa na umri wa miaka kumi na tatu tu. Alikuwa mwanaume wa kwanza kuukubali Uislamu.

Mke wa Mtume Khadija alikuwa mtu wa pekee aliyemkubali Mtume kabla ya Ali. Katika Sura hiyo hiyo, Malik anaelezea kwam- ba Ibn Abbas, Jabir Ibn Abdullah Ansari, Zaid ibn Arqam, Muhammad ibn Munkadar, na Rabi’atu’l-Marai wamesema kwamba mtu wa kwanza kumuamini Mtume baada ya Khadija alikuwa ni Ali. Anasema Ali aliutaja ukweli huu, ambao umesimuliwa na Maulamaa wenu.

Alisema: Muhammad, Mtume wa Allah ni ndugu yangu na mtoto wa Ami yangu; Hamza Bwana wa mashahidi, ni Ami yangu; Fatima binti ya Mtume ni mke wangu; na watoto wawili (wanaume) wa binti yake ni watoto wangu kwa Fatima. Nani kati yenu amechangia sifa kama hizi nilivyo mimi? Nilikuwa wa kwanza kabisa katika kuukubali Uislamu wakati nilikuwa bado mtoto tu. Mtume alitangaza katika siku ya Ghadir-e-Khum kwamba ilikuwa ni wajibu kunikubali mimi kama kiongozi wenu. (Kisha akasema mara tatu) “Ole kwa yule ambaye atamkabili Allah kesho (Siku ya Kiyama), kama akiwa amenifanyia mimi ukatili wowote ule.”

Muhammad Bin Talha Shafi’i katika “Matalibus-Su’ul”, sehemu ya 1, Sura ya 1, uk. 11, na wengine wengi katika Maulamaa wenu, wamesimulia kwamba maelezo haya yalikuwa ni majibu ya barua ya Mu’awiya aliyomuandikia Ali ambayo kwayo alijigamba kwamba baba yake alikuwa kiongozi wa kabila lake wakati wa “zama za ujinga” na kwamba kati- ka Uislamu Yeye (Mu’amiya) alikuwa ni Mfalme.

Mu’awiya vilevile alisema kwamba yeye alikuwa “mjomba wa waumini” mwandishi wa wahayi (ufunuo), na mtu sifa njema.” Baada ya kusoma barua hii, Ali akasema: “Mtu wa tabia hii – mtoto wa mwanamke ambaye alitafuna maini - anajigamba mbele yangu! (kuhusu mama yake Mu’awiyya - Hindi ambaye baada ya Vita vya Uhud akiwa na hasira kali alichana maiti ya Hamza, akakata ini lake, na akalitafuna). Hata hivyo, Mu’awiyya ingawa alikuwa mpinzani mkali wa Ali, hakuweza kuzikataa sifa hizi.

Aidha, Hakim Abu’l-Qasim Haskani, mmoja wa Maulamaa wenu, anasimulia kutoka kwa Abdu’r-Rahman Bin Auf, kuhusu aya hiyo hapo juu ya Makuraishi kumi waliokubali Uislamu, kwamba Ali alikuwa wa mbele zaidi miongoni mwao. Ahmad Bin Hanbal, Khatib Khawarizmi, na Sulayman Balkhi Hanafi, wanasimulia kutoka Anas bin Malik kwamba Mtume alisema: “Malaika walinitakia rehma mimi na Ali kwa muda wa miaka saba, kwani kwa muda huo hakuna sauti iliyotamka Upweke wa Allah isipokuwa yangu na ya Ali.”

Ibn Abi’l-Hadid Mu’tazali katika “Sherh-e-Nahjul-Balagha”, Jz. 1, uk. 373-5, ameandika Hadith nyingi mbalimbali zilizosimuliwa kupitia wanachuoni wenu zenye maana kwamba Ali alikuwa wa mbele zaidi katika jambo la Uislamu.

Baada ya kuandika vifungu mbalimbali vya maneno na simulizi anahitimisha kwa kusema: “Hivyo mukhtasari wa yote tuliyoeleza ni kwamba Ali ni wa kwanza miongoni mwa watu kuhusu Uislamu. Maoni kinyume na haya ni mara chache kuyasikia, na hayana maana kwetu kuyazingatia.”

Imam Abdu’r-Rahman Nisa’i, mwandishi wa moja ya vitabu sita Sahih vya hadith, ameandika katika “Khasa’isu’l-Alawi” hadith sita za mwanzo juu ya suala hili na amethibitisha kwamba mtu wa mbele zaidi katika Uislamu na wa kwanza kusali na Mtume alikuwa Ali. Kwa nyongeza, Sheikh Sulayman Balkh Hanafi katika “Yanabiu’l-Mawadda.” Sura 12, ameandika hadith 31 kutoka kwa Tirmidhi, Hamwaini, Ibn Maja, Ahmad Bin Hanbal, Hafidh Abu Nu’ami, Imam Tha’labi, Ibn Maghazili, Abu’l-Muwayyid Khawarizmi, na Dailami, ambayo hitimisho lake ni kwamba Ali alikuwa wa kwanza katika umma wote wa Kiislamu kukubali Uislamu.

Hata shupavu mchungu Ibn Hajar Makki ameandika katika “Sawa’iq-Muhirika”, Sura ya 2 Hadith juu ya Suala hili hili, ambazo baadhi ya hizo zimekubaliwa na Sulayman Balkhi Hanaf katika kitabu chake “Yanabiu’l-Mawadda” kuelekea mwisho wa kufunga Sura ya 2, amesimuluia hadith juu ya suala hilo hilo, baadhi yake ambazo zimekubaliwa na Suleiman Balkhi Hanafi ndani ya Yanabiul’Mawadda yake.

Zaidi ya hayo, ndani ya Yanabiul’Mawadda, kuelekea mwisho wa Sura ya 12, amesimulia kutoka Ibn Zubair, Makki na yeye kutoka kwa Jabir Ibn Abdullah Ansari, Hadith kuhusu sifa za Ali, ambayo ningependa kuitoa hapa kwa ruhusa yenu ili kuhitimisha hoja yangu.

Mtume alisema: “Mwenyezi Mungu alinichagua mimi kuwa Mtume na akanifunulia maandiko matakatifu. Mimi nikamwambia, ‘Ee Allah, Mola Wangu, ulimtuma Musa kwa Firauni, Musa akakuomba umfanye ndugu yake, Harun, Waziri wake ambaye angeweza kuimarisha mkono wake, ili maneno yake yapate kushuhudiwa.

Sasa nakuomba, Ee Allah, uchague kwa ajili yangu kutoka miongoni mwa familia yangu Waziri ambaye ataimarisha mkono wangu. Mfanye Ali kuwa Waziri wangu na ndugu yangu, ingiza ushujaa kwenye moyo wake, na mpe nguvu juu ya maadui. Ali alikuwa mtu wa kwanza kuniamini na kushuhudia Utume wangu na mtu wa kwanza kutamka Upweke wa Allah sambamba pamoja na mimi.’

Baadae niliendelea kumuomba Allah. Kwa hiyo Ali ni kiongozi wa warithi (wangu). Kumfuata yeye ni rehma; kufa ukiwa na utii kwake ni Shahada. Jina lake huonekana katika Taurat pamoja na jina langu; mke wake, mwaminifu zaidi, ni binti yangu; watoto wake wawili wa kiume, ambao ni mabwana wa vijana wa Peponi, ni watoto wangu.

Baada yao, Maimam wote ni wawakilishi wa Allah juu ya viumbe baada ya Mitume; na ni milango ya elimu miongoni mwa watu wangu. Yeyote ambaye atawafuata ameokolewa kutokana na moto wa Jahanam; yeyote ambaye atawafuata ameongozwa katika njia iliyonyooka; yeyote ambaye amejaaliwa na Allah kuwa na mapenzi kwao hakika atapelekwa Peponi. Hivyo, watu wenye akili, chukueni tahadhari.’”

Ningeweza kunukuu hadith za namna hiyo usiku wote, ambazo zote zimeandikwa na Maulamaa wenu. Lakini nafikiri hii inatosha. Ni Ali peke yake aliyefuatana na Mtume tangu utotoni, na kwa hiyo ni sawa kwamba tunamuona ni mtu aliyeashiriwa katika maneno, “Wale ambao wako pamoja naye”, na sio mtu ambaye alifuatana na Mtume kwa safari ya siku chache tu.

Imani Ya Ali Akiwa Bado Mtoto Tu.

Hafidh: Umethibitisha Nukta yako, na kamwe hakuna hata mtu mmoja ambaye amekataa kwamba Ali alikuwa mbele zaidi katika kuukubali Uislamu. Lakini ukweli huu haumfad- hilishi yeye kuwa mwenye sifa zaidi kwa kumlinganisha na Masahaba wengine. Kweli, Makhalifa wakubwa walikubali imani katika Uislamu miaka kadhaa baada ya Ali, lakini imani yao ilikuwa tofauti na bora zaidi kuliko yake. Sababu yenyewe ni kwamba Ali alikuwa mtoto tu, na hawa walikuwa watu wazima.
Ni dhahiri kwamba, imani ya watu wazima, wenye busara ilikuwa bora zaidi kuliko ile ya mtoto. Kwa nyongeza, imani ya Ali ilikuwa ya ufuataji wa kibubusa na imani ya watu hawa ilijengwa juu ya akili. Imani inayopatikana kwa akili ni bora kuliko imani ya upofu. Kwa vile mtoto ambaye hayuko chini ya wajibu wa kidini wa kutekeleza ibada, haikiri imani isipokuwa kwa kufuata kwa upofu, hivyo Ali, ambaye alikuwa mtoto tu wa miaka kumi na tatu, alikiri imani yake kwa upofu tu wa kufuata.

Muombezi: Mazungumzo kama hayo kutoka kwa mtu msomi kama wewe kwa hakika yanashangaza. Nashangaa jinsi gani nitaivunja hoja kama hiyo. Kama ningekuwa niseme kwamba umechukuwa msimamo kama huo kwa ukorofi tu, ingekuwa dhidi ya tabia yangu kuhusisha sababu kama hiyo kwa mtu msomi. Ngoja nikuulize Swali: je, kuukubali Uislamu kwa Ali kulitegemea juu ya kupenda kwake mwenyewe binafsi au kwa kulinganiwa ya Mtume?

Hafidhi: Kwa nini unachukuwa mtizamo mkali kama huu juu ya namna tunavyoongea, kwani tunapokuwa na mashaka ni lazima tuyajadili. Kwa kujibu swali lako, nakiri kwamba Ali aliukubali Uislamu kwa ulinganio wa Mtume.

Muombezi: Wakati Mtume alipomlingania Ali akubali Uislamu, yeye hakujua kwamba mtoto hafungwi na majukumu ya kidini? Kama ukisema kwamba alikuwa hajui utakuwa unahusisha na ujinga na kama alijua na akamhubiria Ali hata hivyo, basi kitendo chake kilikuwa cha upuuzi. Ni dhahiri kwamba, kuhusiha upuuzi kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ni ukafir kwa vile Mtume ni Ma’sum (hakosei wala hatendi dhambi). Allah anasema kuhusu yeye katika Qur’ani Tukufu: Wala hasemi kwa matamanio (ya nafsi yake). Hayakuwa haya ila ni Wahyi uliofunuliwa (kwake)” (53:3-4).

Mtume alimuona Ali ni mtu wa kufaa kulinganiwa kuukubali Uislamu. Mbali na hili, ujana si lazima kutanguliwa na hekima. Utu uzima huchukuliwa maanani kuhusiana na utekelezaji wa wajbat za kidi- ni, lakini sio mambo yanayohusiana na hekima. Imani inahusiana na mambo yanayo endana na hekima na sio sheria za kidini. Hivyo Imani ya Ali wakati wa utoto ni sifa kwa ajili yake kama vile Allah anavyotuambia katika Qur’ani Tukufu kuhusu Isa katika maneno haya: “Hakika mimi ni Mtumishi wa Allah: Allah amenipa kitabu na amenifanya Nabii.” (19:30).

Vilevile katika Sura hiyo anasema kuhusu Mtume Yahaya: “Na tulimpa hekima angali mtoto.” (19:12).
Seyyed Ali Humairi Yamani, (alikufa 179 A.H.) anaonyesha ukweli huu katika mashairi yake. Ansema: “Kama vile Yahaya alivyofikia cheo cha Utume katika utoto wake, Ali ambaye alikuwa mrithi wa Mtume na baba wa watoto wake, vilevile alifanywa mwakilishi wa Allah na mlezi wa watu akingali mtoto.”

Sifa na heshima inayotolewa na Allah haitegemei juu ya umri. Hekima na akili hutegemea juu ya hali ya kuzaliwa. Nashangazwa na maelezo yako kwa vile hoja kama hizo zilitole- wa na Manasibi na Makhariji kwa kuchochewa na Bani Umayya. Waliishusha imani ya Ali kwamba ilikuwa ya utii wa kibubusa kwa yale aliyofundishwa.

Hata wanachuo wenu wameikubali sifa ya Ali kwa namna hii. Muhammad bin Talha Shafi’i, Ibn Sabbagh Maliki, Ibn Abi’l-Hadid na wengine wamenukuu mashairi ya Ali. Katika moja ya mashari yake anasema: “Nilikuwa wa kwanza na wa mbele zaidi miongoni mwenu katika kuukubali Uislamu wakati nilipokuwa mtoto mdogo tu.”

Kama imani ya Ali katika umri mdogo kama huo haikua bora, Mtume asingeielezea namna hiyo. Sulayman Balkhi Hanafi katika “Yanabiu’l-Mawadda”, Sura ya 55, uk. 202, anasimulia kutoka kwa Ahman Bin Abdullah Shafi’i akinukuu kutoka kwa Khalifa wa pili, Umar Bin Khattab, ambaye alisema:

“ Abu Bakr, Abu Ubaida Jarra na Kundi la watu waliokuwepo pamoja na Mtume wa Allah aliposhika bega la Ali na kusema: “Ewe Ali! Wewe ni wa kwanza na wa mbele zaidi miongoni mwa waumini wote na Waislamu katika kuukubali Uislamu, Wewe kwangu mimi ni kama alivyokuwa Harun kwa Musa.”

Vilevile Imam Ahmad Bin Hanbal anasimulia kutoka kwa Ibn Abbas, ambaye amesema yeye, Abu Bakr, Abu Ubaida Bin Jarra, na wengine walikuwa pamoja na Mtume wakati alipoweka mkono wake katika bega la Ali na akasema: “Wewe uko mbele zaidi katika imani ya Uislamu miongoni mwa Waislamu wote, na uko kwangu Mimi kama Harun alivyokuwa kwa Musa, Ewe Ali! Anayefikiria kwamba mimi ni rafiki yake ambapo ni adui yako, huyo ni muongo.”
Ibn Sabbagh Maliki ameandika hadith kama hiyo katika “Fusulu’l-Muhimma”, uk. 125, kutoka “Khasa-isu’l-Alawi” kama simulizi ya Abdullah bin Abbas, na Imam Abu Abdu’r-Rahman Nisa’i anaeleza katika “Khasa’isu’l-Alawi” kwamba alisema: “Nimemsikia Umar bin Khattab akisema, ‘Litajeni jina la Ali kwa heshima kwa sababu nimemsikia Mtume akisema kwamba Ali anazo sifa tatu. Mimi (Umar) natamani kwamba ningelikuwa na moja tu kati ya hizo kwa sababu kila moja ya sifa hizo ni yenye thamani kubwa sana kwan- gu kuliko kitu chochote katika ulimwengu huu.”

Ibn Sabbagh amesimulia kama ifuatavyo kwa nyongeza ya walivyoandika wengine. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema kuhusu Ali, “Yeye ambaye anakupenda wewe hunipenda mimi, na ambaye ananipenda mimi, Allah Humpenda, na yeyote apendwaye na Allah, humuingiza Peponi. Lakini yule ambaye ni adui kwako ni adui kwangu, na ambaye ni adui kwangu, Allah ni adui kwake na humhukumu kwenda Motoni.”

Kujitangaza kwa Ali kuwa Mwislamu hata ambapo alikuwa bado mdogo huthibitisha ubora wa hekima na sifa yake, ambayo hakuna Mwislamu mwingine anayeweza kuipata. Tabari katika kitabu chake cha Ta’rikh ananukuu kutoka Muhammad Bin Sa’ad Bin Abi Waqqas, ambaye alisema: Nilimuuliza Baba yangu iwapo Abu Bakr alikuwa wa kwanza wa Waislamu. Yeye akasema, ‘Hapana, zaidi ya watu hamsini waliingia Uislam kabla ya Abu Bakr; bali alikuwa mbora kwetu kama Mwislam.’” Vilevile anaandika kwamba Umar Bin Khattab aliingia Uislamu baada ya wanaume arobaini na tano na wanawake ishirini na moja. “Ama kwa aliyekuwa mbele zaidi katika Uislamu na Imani, alikuwa ni Ali Bin Abi Talib.”

Imani Ya Ali Ilikuwa Ni Sehemu Ya Asili Yake Hasa:

Mbali na ukweli kwamba, Ali alikuwa wa mbele katika kuingia Uislamu, alikuwa na sifa nyingine, ya kipekee kwake, na ya muhimu zaidi kuliko sifa zake nyingine.

Uislamu wa Ali ulitokana na asili yake, ambapo ule wa wengine umetokea tu baada ya kuwa makafir huko nyuma. Tofauti na Waislamu wengine na masahaba wa Mtume, Ali hajawahi kamwe kuwa Kafir. Hafidh Abu Nu’aim Ispahani katika “Ma-Nazalu’l-Qur’ani fi Ali”, na Mir Seyyed Ali Hamadani katika “Mawaddatu’l-Qurba” wanasimulia kwamba Ibn Abbas amesema: “Naapa kwa jina la Allah kwamba hakuna mtu hata mmoja ambaye alikuwa hakuabudu masanamu kabla ya kuingia Uislamu isipokuwa Ali. Ali, alikubali Uislamu akiwa kamwe hajapata kuabudu masanamu.”

Muhammad Bin Yusuph Ganji Shafi’i katika “Kifayatut-Talib”, Sura ya 24 anamnukuu Mtume akisema: “Wale ambao walitangulia kuikubali imani katika upweke wa Allah miongoni mwa wafuasi wa Mitume walikuwa ni watu watatu ambao hawajawahi kamwe kuwa washirikina:

Ali bin Abi Talib, mtu aliyetajwa katika Suratu Yaa-Sin, na Muumini katika watu wa Firauni. Wale wakweli (ma-Sidiq) ni Habib-e-Najjar, miongoni mwa kizazi cha Yaa Sin, Hizqil (Sawaiq al-Muhriqah, hadith ya 30 kati ya zile 40 kuhusu sifa za Ali, Yanabiu’l-Mawadda, Jz. 42, Nahjul-Balaghah, Jz. 2, uk. 451) miongoni mwa kizazi cha Firauni, na Ali bin Abi Talib, ambaye amewapita wote.” Mir Seyyed Ali Hamadani katika “Mawadda-tu’l-Qubra”, Mawadda ya 7, Khatib Khawarizmi katika “Manaqib” na Imam Tha’labi katika “Tafsir” yake anasimulia kutoka kwa Khalifa wa pili, Umar Bin Khattab: “Nashuhudia kwamba nimemsikia Mtume akisema, ‘Kama Mbingu Saba zingewekwa pamoja katika mizani moja na imani ya Ali katika nyingine, hakika imani ya Ali ingezidi uzito ile nyingine.’”

Nukta hiyo hiyo iliwekwa katika mashairi yaliyotungwa na Sufyani bin Mus’ab bin Kufi kama ifuatavyo: “Kwa jina la Allah, nashuhudia kwamba Mtume alituambia: ‘Haipasi kubakia bila kutojulikana na kwa mtu yeyote kwamba kama imani za wale wote wanaishi juu ya ardhi ingewekwa katika kipimio kimoja cha mizani na ile ya Ali katika kingine, imani ya Ali ingezidi uzito ile ya wengine.”

Ali Aliwapita Masahaba Wengine Wote Na Umma Wote Katika Ubora.

Mir Seyyed Ali Hamadani Shafi’i amendika hadith nyingi katika Mawaddatu’l-Qurba yake, ambazo zinaunga mkoni ubora wa Ali. Katika Mawadda ya Saba ananukuu kutoka kwa Ibn Abbas kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Mbora wa watu wa ulimwengu wote katika kipindi changu ni Ali.”

Wengi wa Maulamaa waadilifu wameukubali ubora wa Ali. Ibn Abi’l-Hadid katika Sharh yake ya “Nahju’l-Balagha” Jz. 3, uk. 40, anasema kwamba Abu Ja’far Iskafi, kiongozi wa madhehebu ya Mu’tazil, alitangaza kwamba Bashir bin Mu’amar, Abu Musa, Ja’far Bin Mubashir, na maulamaa wengine wa Baghdad wanaamini kwamba, “Mtu bora zaidi miongoni mwa Waislamu wote alikuwa Ali bin Abu Talib, na baada yake mtoto wake Hasan, kisha mtoto wake Husain, baada yake ni Hamza na baada yake ni Jafar Bin Abi Talib.” Anaendelea kusema kwamba kiongozi wake Abu Abdullah Basri, Sheikh Abu’l-Qasim Balkhi, na Sheikh Abu’l-Hasan Khayya wanayo imani hiyo hiyo kama Abu Ja’far Iskafi kuhusiana na ubora wa Ali. Anaelezea imani ya madhehebu ya Mu’tazil ikisema.

“Mtu bora baada ya Mtume wa Allah ni mrithi (makamu) wa Mtume, mume wa Fatima, Ali; baada yake, ni watoto wake wawili Hassan na Husain; baada yao, Hamza, na baada yake Ja’far (Tayyar).”

Sheikh: Kama ungejua maelezo ya maulamaa yenye kuunga mkono ubora wa Abu Bakr, usingesema maneno haya.

Imani Ya Ali Ni Bora Kuliko Ya Abu Bakr.

Muombezi: Maulamaa wote wa kutegemewa, wa Kisuni wameukubali ubora wa Ali. Kwa mfano, unaweza ukarejea “Sharh Nahju’l-Balagha” ya Ibn Abi’l-Hadid, Jz. 3, uk. 264, ambamo maelezo hayohayo yamenukuliwa kutoka kwa Jahiz kwamba imani ya Abu Bakr ilikuwa bora kuliko ile ya Ali. Walakini, Abu Ja’far Askafi, mmoja wa maulamaa wakubwa wa madhehebu ya Mu’tazil alikataa madai haya, akisema kwamba imani ya Ali ilikuwa bora kwa ile ya Abu Bakr na masahaba wengine wote. Abu Ja’far amesema: “Hatukatai ubora wa masahaba, lakini kwa hakika hatumchukulii yeyote kati yao kuwa mbora kuliko Ali.” Ali alikuwa wa cheo cha juu sana kiasi kwamba kutaja jina lake sambamba na masahaba wengine haifai.

Kwa kweli sifa za masahaba haziwezi kulinganishwa na sifa tukufu mno za Ali. Mir Seyyed Ali Hamadani anasimulia katika “Mawadda” yake ya 7 kutoka kwa Ahmad Bin Muhammadu’l-Karzi Baghdadi, ambaye amesema kwamba alisikia kutoka kwa Abdullah bin Ahmad Hanbal, ambaye alimuuliza baba yake Ahmadi Bin Hanbal kuhusu cheo cha Masahaba wa Mtume. Yeye akamtaja Abu Bakr, Umar na Uthman na akasimama. Kisha Abdallah akamuuliza baba yake. “Liko wapi jina la Ali bin Abu Talib?” Baba yake akajibu, “Yeye ni katika dhuria watukufu wa Mtume. Hatuwezi kutaja jina lake (kwa jinsi alivyo maarufu) sambamba pamoja na watu wale.”

Tunaona katika Qur’ani Tukufu kwamba katika aya ya Mubahila, Ali anatajwa kama nafsi ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Kuna hadithi yenye kuunga mkono habari hii, ambayo imeandikwa katika “Mawadda” ya 7 hiyohiyo, iliyosimuliwa kutoka kwa Abdullah Bin Umar Bin Khattab.

Alisema kwamba siku moja walipokuwa wakihesabu majina ya masahaba, yeye alimtaja Abu Bakr, Umar, na Uthman. Mtu mmoja akasema, “Ee Abdu’r-Abdur- Rahman! Kwa nini umeliacha jina la Ali? Yeye alijibu “Ali ni mmoja wa dhuria wa Mtume. Hawezi kuchanganywa na mtu yoyote yule. Yuko katika kundi namna moja na Mtume wa Allah.”

Ngoja nisimulie hadith nyingine kutoka katika “Mawadda” hiyo hiyo. Imesimuliwa kuto- ka kwa Jabir Bin Abdullah Ansari kwamba siku moja wakiwepo mbele ya Muhajirina na Ansari, Mtume alimwambia Ali:

“Ewe Ali! Kama mtu atatekeleza Sala zake kamili kwa Allah, na kisha akatia shaka kwamba wewe na familia yako ni bora kwa viumbe wengine wote, makazi yake yatakuwa Jahanam.” (Baada ya kusikia hadith hii, wale wote waliokuwepo pale, hususan Bw. Hafidhi, walionyesha kutubu, isije wakawa miongoni mwa wenye kutia mashaka).

Nimerejea hadith chache tu. Chaguo lenu linaelekea kuwa ni kuzikataa hadith zote hizi sahihi, ambazo zimeandikwa kwenye vitabu vyenu, au kukubali kwamba imani ya Ali ilikuwa bora kuliko ile ya masahaba wote, pamoja na ya Abu Bakr na Umar. Vilevile naomba muiangalie hadith hii (inayokubaliwa na madhehebu zote) ambamo Mtume alisema wakati wa Ghazawa-e-Ahzab (hujulikana vilevile kama vita vya Handaq), wakati Ali alipomuua Amru Ibn Abdu-e-Wudd kwa pigo moja la upanga wake:

“Pigo moja la Ali katika vita vya Khandaq limempatia fadhila zaidi kuliko malipo ya matendo mema ya umma wote (majini na watu) mpaka Siku ya Hukumu.”
Kama pigo moja la upanga wake lilikuwa bora katika fadhila kuliko Sala za majini na watu zikichanganywa zote pamoja hakika ubora wake hauwezi kuhojiwa na yeyote isipokuwa na mashupavu waovu.

Ali Kama Nafsi Ya Mtukufu Mtume (S.A.W.W.).

Ingekuwa hakuna uthibitisho mwingine wa ubora wa Ali kwa Masahaba wote na Wanadamu wote kwa ujumla, Aya ya Mubahila inatosha kuthibitisha ubora wake. Inamtaja Ali kama “nafsi” ya Mtume. Mtukufu Mtume alikuwa kwa kukubalika kabisa ni mbora zaidi kwa wanadamu wote kuanzia mwanzo mpaka mwisho.

Kwa hiyo, neno “anfusana” (nafsi zetu) katika aya hiyo linaloashiria kwa Ali huthibitisha kwamba pia alikuwa bora kwa wanadamu wote kuanzia mwanzo mpaka mwisho. Huenda sasa mtakubali kwamba ule usemi, “Na wale ambao wapo pamoja naye”, utajo wake ni kwa Ali. Yeye alikuwa pamoja na Mtume kabla ya mtu yeyote yule kuanzia mwanzo wa Uislamu.

Ama kwa nini Ali hakufuatana na Mtume katika usiku wa kuhama kutoka Makka, ni wazi kwamba Mtume alimkabidhi Ali majukumu muhimu zaidi. Hakuna aliyekuwa muaminifu kama Ali. Aliachwa nyuma kurudisha kwa wenyewe mali zilizowekwa amana kwa Mtume.

(Jukumu la pili la Ali lilikuwa ni kuipeleka familia ya Mtume na Waislamu wengine Madina. Na hata ingawa Ali hakuwa pamoja na Mtume katika pango usiku ule, alitekeleza jukumu muhimu zaidi kwa vile alilala katika kitanda cha Mtume).

Aya Ya Qur’ani Yenye Kumsifu Ali Kwa Kulala Kwake Katika Kitanda Cha Mtume Katika Usiku Wa Hijra.

Wanachuoni wenu wenyewe wametaja sifa za Ali katika tafsir zao (za Qur’ani). Kwa mfano, Ibn Sab’i Maghribi katika Shifa’us-Sudur, Tibrani katika “Ausat” na “Kabir”, Ibn Athir katika “Usudu’l-Ghaiba”, Jz. 4, uk. 25, Nuru’d-Din Sabbagh Maliki katika “Fusuli’l- Muhimma Fi Ma’rifati’l-’aimma”, uk. 33, Abu Ishaq Tha’labi, Fazil Nishapuri, Fakhru’d-Din Radhi na Jalalu’d-Dini Suyuti, kila mmoja katika Tafsir yake, Hafidh Abu Nu’aim Isphahani, muhadithina maarufu wa Ki-Shafi’i katika “Ma-Nazala’l-Qur’an fi Ali”, Khatib Khawarizmi katika “Manaqib” Sheikhul-Islam Ibrahim bin Muhammad Hamwaini katika “Fara’id”, Muhammad bin Yusuf Ganji Shafi’i katika “Kifayatut-Talib”, Sura ya 62, Imam Ahmad bin Hanbal katika “Musnad”, Muhammad bin Jarir kupitia vyanzo mbalimbali, Ibn Hisham katika “Siratu’n-Nabi”, Hafidh Muhadith wa Damascus katika “Arba’in Tiwal”, Imam Ghazali, katika “Ihya’u’l-Ulum”, Jz. 3, uk. 223, Abu’s-Sa’adat katika “Fadha’ilu’l-Iratit-Tahira”, Ibn Abi’l-Hadid katika Sharhe “Nahju’l-Balagha”, Sibt Ibn Jauzi katika “Tadhikira” na wengine katika maulamaa wenu mashuhuri, wanasimulia kwamba wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipokusudia, kwa amri ya Allah, kuondoka Makka na kwenda Madina, alimtaka Ali ajifunike shuka lake la kijani na alale katika kitanda chake.

Kwa hiyo, Ali akalala pahali pa Mtume kisha Mwenyezi Mungu akawaambia Malaika Jibril na Mikael kwamba amewafanya wao kuwa ndugu, na kwamba mmoja wao ataishi muda mrefu kuliko mwingine. Aliwauliza ni nani alikuwa tayari kumpa ndugu yake maisha yake ya ziada, ambayo kadiri yake hakuna mmoja wao aliyejua. Walimuuliza (Allah) iwapo chaguo hilo ni wajibu. Walielezwa kwamba sio wajibu. Hakuna hata mmoja wao aliyechagua kuachana na maisha yake ya ziada. Kisha yakafuata maneno haya matukufu: “Mimi nimeumba undugu kati ya mwakilishi wangu Ali na Mtume wangu Muhammad. Ali amejitolea kutoa mhanga maisha yake kwa ajili ya maisha ya Mtume. Kwa kulala katika kitanda cha Mtume, anayalinda maisha ya Mtume. Sasa ninyi wote mnaagizwa kwenda duniani kumuokoa kutokana na mbinu za uovu wa maadui.”

Kwa hiyo, wote wakaja duniani. Jibril akakaa kichwani kwa Ali na Mikaeli miguuni kwake. Jibril akasema, “Hongera, Ewe mwana wa Abu Talib! ambaye kwako Mwenyezi Mungu anajivunia mbele ya Malaika Zake.” Baada ya haya, Aya ifuatayo ikateremshwa kwa Mtume. “Na kuna aina ya watu ambao hutoa maisha yao kuzitafuta radhi ya Allah; na Allah ni mwingi wa upole kwa waja (wake).” (2:207).

Sasa nakusihini waheshimiwa, kuingalia aya hii kwa uangalifu wakati mtakaporudi nyumbani usiku na kutoa uamuzi wenu wenyewe.
Je, ubora kwa haki ni wa yule ambaye alibakia pamoja na Mtume katika safari ya siku chache, akionyesha woga na huzuni, au kwa yule ambaye alihatarisha maisha yake usiku ule kishujaa na kwa furaha, kwa ajili ya usalama wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Imam Ja’far Askafi, mmoja wa maulamaa wakub- wa na viongozi wa Mu’tazil, anathibitisha, (kama ilivyosimuliwa katika Sharhe ya “Nahaju’l-Balagha” na Abi’l-Hadid Jz. 3, uk. 269-281), kwamba kulala kwa Ali katika kitanda cha Mtume kulikuwa bora zaidi kuliko muda mfupi wa Abu Bakr aliokaa pamoja na Mtume.

Anasema: “Maulamaa wa Kiislamu kwa pamoja wanashikilia kwamba, kwa ukweli halisi, ubora wa Ali katika usiku ule ulitukuka mno kiasi kwamba hakuna mtu angeweza kuufikia isipokuwa Ishaka na Ibrahimu wakati walipokuwa tayari kutoa maisha yao mhanga katika kutii mapenzi ya Allah.” (Wafasiri wengi, maulamaa na wanahistoria wanaamini kwamba alikuwa ni Ismail ambaye alijitoa mhanga na sio Ishaka).

Katika ukurasa wa 271 wa Sharhe ya Nahaju’l-Balagha, maelezo ya Abu Ja’far Askafi katika kumjibu Abu Athman Jahiz Nasib yameandikwa. Anasema: “Nilikwisha kuthibitisha mapema kwamba kulala kwa Ali katika kitanda cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) katika usiku wa kuhama kulikuwa bora zaidi kuliko kule kwa Abu Bakr kubakia pamoja na Mtume katika Pango. Ili kusisitiza hoja yangu, nitaithibitisha katika mitazamo mingine miwili: Kwanza, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wa Allah akiwa na mkuruba wa karibu na wa siku nyingi na Ali, alimpenda mno. Kwa hiyo alihisi kupotea kwa upendo wakati walipotengana.

Kwa upande mwingine, Abu Bakr alipata fursa ya kwenda pamoja na Mtume. Kwa vili Ali alikuwa na uchungu wa kutengana kwao, malipo yake yaliongezeka kwa sababu jinsi maumivu yanavyokuwa makali zaidi katika utumushi, ndivyo yanavyopata malipo makubwa zaidi.

Pili, kwa vile Ali alikusudia kuondoka Makka na hata aliwahi mara moja kuondoka peke yake, hali yake kama raia kule iliongezeka kuwa ngumu. Hivyo wakati akiondoka Makka pamoja na Mtume, hamu yake ya kuondoka ilitimia. Kwa ajili hiyo hakuna ubora wa kimaadili kama huo kwa ajili yake kama ulivyo kwa Ali, ambaye alivumilia machungu makali katika kuhatarisha maisha yake mbele ya panga zilizochomolewa za maadui.

Ibn Sab’a Maghrib anasema katika kitabu chake “Shifa’us-Sudur” kuhusu ushujaa wa Ali: “Kuna umoja kamili (wa makubaliano) miongoni mwa maulamaa wa Kiarabu kwamba katika usiku wa Hijra, kulala kwa Ali katika kitanda cha Mtume kulikuwa bora zaidi ya kutoka pamoja naye. Ali alijifanya mwenyewe mwakilishi wa Mtume na akahatarisha maisha yake kwa ajili ya Mtume. Hoja hii ni wazi mno kiasi kwamba kamwe hakuna hata mtu mmoja aliyeikataa isipokuwa wale waliopatwa na uwenda wazimu au ushabiki.” Nitakomeshea hapa na kurudi kwenye nukta yangu muhimu. Umesema kwamba, maneno ya Qur’ani “Wakali dhidi ya makafir” (48:29) yanamuashiria Khalifa wa pili, Umar Bin Khattab.

Lakini dai hili haliwezi kukubaliwa kwa sababu tu kwamba umesema hivyo. Ni lazima tuamue iwapo sifa hii ni katika tabia yake au laa. Kama ndivyo, niko radhi kuikubali. Kwa hakika ukali unaweza kuonyeshwa katika njia mbili: Katika majadiliano ya kidini ambayo kwayo kwa nguvu ya hoja, maulamaa wa upande mwingine wananya- mazishwa. Pili, unaweza kuonyeshwa katika uwanja wa vita.

Kwa kadiri mijadala ya kielmu ihusikanavyo, hakuna mfano hata mmoja katika historia ambapo Umar ameonyesha ukali wowote. Katika kiwango chochote, sijaona taarifa yoyote ya kihistoria yenye kuonyesha kwamba Umar alionyesha ukali katika majadiliano ya kielimu. Nitawashukuruni kama mtanionyesha mfano wowote.

Kwa kweli, maulamaa wenu, wamekubali kwamba alikuwa ni Ali ambaye aliyatatua yale matatizo ngumu ya kisheria na kufutu mas’ala ya kidini wakati wa kipindi cha Makhalifa watatu. Ingawaje Bani Umayya na wafuasi mbumbumbu wa Abu Bakr walibuni hadithi zisizo na idadi kwa niaba yao, hawakuweza kuficha ukweli kwamba wakati watu wa imani nyingine walipokuja kwa Abu Bakar, Umar, au Uthman, kutatua matatizo magumu, makhalifa hawa waliyapeleka matatizo hayo kwa Ali.

Ali aliwapa majibu ya kuvutia kiasi kwamba watu wengi wasiokuwa Waislamu waliingia Uislamu. Ukweli kwamba Abu Bakr, Umar na Uthman walikubali ubora wa Ali unatosha kuthibitisha hoja yangu.

Wanachuoni wenu wameandika kwamba Khalifa Abu Bakr alisema: “Niondoeni, niondoeni, kwa vile mimi sio bora kuliko ninyi alimuradi Ali yuko kati yenu.”
Kwa uchache kabisa, takriban mara sabini, khalifa Umar alikiri: “Kama Ali asingekuepo Umar angeangamia.” Mazingira mengi yenye hatari yametajwa kwenye vitabu, lakini mimi sitaki kueleza sana juu ya nukta hii. Kunaweza kuwa na mambo mengi muhimu ya kujadili.

Nawab: Ni habari gani zaweza kuwa za muhimu zaidi kuliko hii? Je, mambo haya yametajwa katika vitabu vyetu? Kama yametajwa tafadhali tueleze tupate kujua.

Muombezi: Maulamaa waadilifu wa madhehebu yenu wanakubali kwamba, mara kwa mara Umar alikiri kwamba Ali alikuja kumuokoa.

Ushahidi Kuhusu Maneno Ya Umar:

“Kama Ali Asingekuwepo, Umar Angeangamia.”

Qadhi Fadhlullah Bin Ruzbahan, yule shabiki shupavu, katika kitabu chake “Ibtalu’l- Batil;” Ibn Majar Asqalani katika “Tihdhibu’l-Tahdid”, kilichochapishwa Hyderabad Daccan, uk. 337; Ibn Hajar katika Isaba, Jz. 2, iliyochapishwa Misir uk. 509; Ibn Qutayba Dinawari katika “Ta’wil-e-Mukhtalafu’l-Hadith” uk. 201-202, Ibn Hajar Makki katika Sawa’iq-e-Muhriqa uk. 78; Hajj Ahmad Afindi katika “Hidayatu’l-Murtab” uk. 146 na 152, Ibn Athir Jazari katika “Usudu’l-Ghaiba”, Jz. 4, uk. 22; Jalalu’d-Din Suyuti katika “Ta’rikhu’l-Khulafa”, uk. 66; Ibn Abdu’l-Birr Qartabi katika “Isti’ab” Jz. 2, uk. 474; Seyyed Mu’min Shablanji katika “Nuru’l-Absar” uk.73; Shahabu’d-Din Ahmad bin Abdu’l-Qadir A’jili katika “Dhakhiratu’l-Ma’al”; Muhammad bin Ali As-Subban katika Is’afu’r-Raghibin, uk.152; Nuru’d-Din bin Sabbagh Maliki katika “Fusulu’l-Muhimma”, uk. 18; Nuru’d-Din Ali bin Abdullah Samhudi katika “Jawahiru’l-Iqdani”; Ibn Abi’l- Hadid Mu’tazil katika “Sharhe Nahaju’l-Balagha”, Jz. 1, uk. 6. Allama Qushachi katika Sharhe-e-Tarid, uk. 407, Khatib Khawarizmi katika “Manaqib”, uk. 46 & 60 Muhammad bin Talha Shafi’i katika “Matalibus-Su’ul” Sura ndogo ya 6, uk. 29, Imam Ahmad bin Hanbal katika “Fadha’il” halikadhalia na “Musnad”; Sibt Ibn Jauzi katika “Fadhkira” uk. 85 na 87 Imam Tha’labi katika “Tafsir Kafshu’l-Bayan”, Allama Ibn Qayyim Jauzi katika “Turuqi’l-Hakim”, akiandika hukumu za Ali kuanzia uk. 41 mpaka uk. 53; Muhammd bin Yusufu Ganji Shafi’i katika “Kifayatut-Talib”, Sura ya 57; Ibn Maja Qazwini katika “Sunan” yake; Ibn Maghazili Shafi’i katika “Manaqib”; Ibrahim bin Muhammad Hamwaini katika “Fara’id”; Muhammad bin Ali bin Hasani’l-Hakim katika “Sharh-e- Fat’hil-Mubin”; Dailami katika “Firdaus” Sheikh Sulayman Balkhi Hanafi katika “Yanabiu’l-Mawadda”, Sura ya 14, Hafidh Abu Nu’aim Ispahani katika “Hilyatu’l- Auliya”, halikadhalika katika “Ma-Naza-la’l-Qur’an fi Ali”, na kundi la maulamaa wakub- wa wa madhehebu yenu, pamoja na tofauti ndogo katika maneno, wamesimulia usemi wa Umar, “Kama Ali asingekuwepo, Umar angeangamia.”

Mwanachuoni mkubwa, Ganji Shafi’i, katika sura ya 57, ya “Kifayatut-Talib Fi Manaqib Ali Bin Abu Talib”, baada ya kusimulia baadhi ya hadith sahihi anaelezea kutoka kwa Hudhaifa bin Yaman kwamba, “Siku moja yeye Hudhaifa alikutana na Umar, akamwuliza (yeye Hudhaifa): Ulijisikiaje hali yako wakati ulivyoamka asubuhi?” Hudhaifa akasema, “Niliamka asubuhi nikiichukia haki, nikipenda fitina, kushuhudia kitu kisichoonekana; kujifunza kwa moyo kitu kisichoumbwa, kusali bila kuwa na wudhuu, na kujua kwamba, kilichokuwa changu hapa duniani, sio kwa ajili ya Allah katika Mbingu.’

Umar alikasirishwa sana na maneno haya na alikusudia kumuadhibu Hudhaifa wakati Ali alipoingia ndani. Aliona dalili za hasira kwenye uso wa Umar na akauliza kwa nini alikuwa amekasirika hivyo. Umar akamueleza (maneno ya Hudhaifa) na Ali akasema: “Hakuna ubaya wowote kuhusu maneno haya.

Alichosema Hudhaifa ni sawa sawa: Haki maana yake kifo, ambacho anakichukia; fitna maana yake mali na watoto ambavyo anavitaka; na anaposema kwamba anashuhudia ambavyo hakuviona, hii ina maana kwamba anashuhudia upweke wa Allah, kifo, siku ya malipo, Pepo, Moto, daraja juu yake inayoitwa Sirat, ambavyo hakuna hata kimoja kati ya hivyo alichokiona.

Anaposema anajifundisha kwa moyo ambacho hakikuumbwa, hii huashiria kwenye Qur’ani. Anaposema kwamba anasali bila wuudhu, hii huashiria katika kumswalia Mtume wa Allah (kumtakia rehema na amani) ambako kuna ruhusiwa bila wuudhu; wakati akisema anacho kitu duniani ambacho si kwa ajili ya Allah Mbinguni, hii huashiria kwa mke wake, kwa vile Allah hana mke au watoto. Kisha Umar akasema: “Umar angepotea kama Ali asingetokea.’”

Ganji Shafi’i anasema kwamba maelezo ya Umar yanathibitika kwa mujibu wa riwaya za wasimuliaji wengi wa hadith. Mwandishi wa “Manaqib” anasema kwamba Khalifa Umar, mara kwa mara alisema: “Ewe Abu’l-Hasan! (Ali). Sitakuwa sehemu ya jamii bila wewe.” Vilevile alisema: “Wanawake hawana uwezo wa kuzaa mtoto kama Ali.”

Muhammad bin Talha Shafi’i katika “Matalibus-Su’-ul” na Sheikh Sulayman Balkh Hanafi katika “Yanabiu’l-Mawadda”, Sura ya 14, akisimulia kutoka kwa Tirmidhi, ameandika riwaya yenye kinaganaga kutoka kwa Ibn Abbas ambapo mwisho wa riwaya hiyo anasema: “Masahaba wa Mtume walikuwa wakitafuta hukumu za kidini kutoka kwa Ali, na walikubali maamuzi yake. Hivyo, Umar Bin Khattab alisema katika nyakati mbalimbali, “Kama isingekuwa ni Ali, Umar angeangamia.”

Katika mambo ya kidini na mijadala ya kielimu Umar hakuonyesha ukali wowote. Kinyume chake, alikiri udhaifu wake mwenyewe na kumkubali Ali kama kimbilio lake. Hata Ibn Hajar Makki katika sura ya 3 ya “Sawa’iq-Muhriqa”, akielezea kutoka kwa Ibn Sa’d anamnukuu Umar akisema: “Naomba msaada wa Allah katika kuamua yale matati- zo magumu ambayo kwamba Abu’l-Hasan (Ali) hayupo.”

Ushujaa Wa Khalifa Umar Haujaonekana Kamwe Katika Uwanja Wowote Wa Vita.

Amma kuhusu ukali wa Umar katika uwanja wa vita, historia haikuandika mfano wowote juu ya hilo. Kinyume chake, wanahistoria wa madhehebu zote wanasimulia kwamba wakati wowote Umar alipokabiliana na adui mwenye nguvu, yeye alikimbia. Matokeo yake, Waislamu wengine pia walikimbia na mara kwa mara jeshi la Kiislamu lilishindwa.

Hafidh: Umezidisha pole pole ukosefu wa uungwana. Umemtukana Khalifa Umar ambaye alikuwa ni fahari ya Waislamu na ambaye katika zama zake Waislamu walipataushindi mkubwa. Kwa sababu ya Umar, jeshi la Waislamu lilishinda vita vyao. Unamuita muoga na kusema kwamba alikimbia kutoka uwanja wa vita na kwamba kushindwa kwa jeshi la Kiislamu kulikuwa ni kwa sababu yake! Je, ni sahihi mtu wa hadhi kama yako kumsingizia Khalifa Umar?

Muombezi: Nina wasiwasi kwamba umekosea. Ingawa umekuwa na mimi kwa mikesha mingi, hujanielewa bado. Pengine unafikiria ni kwa sababu ya chuki kwamba ndio ninalau- mu au kusifu watu. Sio hivyo. Kuna kuwiwa kukubwa katika mijadala ya kidini, ambako kumekuwa ni chanzo cha upinzani miongoni mwa Waislamu kwa karne nyingi. Mijadala kama hiyo mara kwa mara uchochea hali ya uovu, ambayo haipatani na maamrisho ya Qur’ani. Qur’ani kwa uwazi inasema:

“Enyi ambao mmeamini! Jiepusheni sana na dhana (kama iwezekanavyo) kwani baadhi ya dhana katika hali nyingine ni dhambi.” (49:12). Unafikiria kwamba maelezo yangu yamechochewa na uovu.Ukweli ni kinyume chake. Sijatamka neno kinyume cha ambavyo maulamaa wenu wameandika. Umesema hivi punde tu kwamba nimemtukana Khalifa Umar.

Lakini kulikuwa hakuna hata chembe ya dalili ya matusi. Niliyosema yanaoana na kumbukumbu za Historia. Sasa nalazimika kutoa mtazamo ulio wazi ili kunyamazisha upinzani huu.

Ushindi Haukuwa Kwa Sababu Ya Sifa Binafsi Za Umar.

Umesema Khalifa Umar alikuwa anahusika na ushindi wa Waislamu. Hakuna mtu anayekataa kwamba Waislamu walipata ushindi mkubwa wakati wa Ukhalifa wa Umar. Lakini kumbuka kwamba kwa mujibu wa maulamaa wenu mashuhuri, kama Qadhi Abu Bakr Khatib, katika kitabu chake, Ta’rikh Baghdad, Imam Ahmad Bin Hanbal katika “Musnad”, Ibn Abi’l-Hadid katika “Sharhe Nahju’l-Balagha” na waandishi wengine wengi, Khalifa Umar alitafuta mwongozo kutoka kwa Ali katika mambo yote ya kiutawala na kijeshi.

Na alikuwa akitenda kwa kufuata ushauri wa Ali. Kwa nyongeza, kulikuwa na tofauti katika ushindi wa Kiislamu kwa vipindi tofauti. Namna ya kwanza inarejea kwenye ushindi wakati wa kipindi cha Mtume mwenyewe, ambao ulikuwa kimsingi kwa sababu ya Ushujaa wa Ali. Kila mtu anakubali kwamba Ali alikuwa shujaa zaidi wa mashujaa. Kama hakupigana katika vita, ushindi haukupatikana.

Kwa mfano katika vita vya Khaibar, alipata maradhi ya macho, na ilikuwa haiwezikani kwa yeye kwenda kwenye mapigano.Waislamu walirudia rudia kushindwa kila walipokwenda kwenye uwanja wa mapambano, mpaka alipotibiwa na Mtume, Ali aliwaendea maadui mpaka akaziteka ngome za Khabar. Katika vita vya Uhud, wakati Waislamu wakivunja safu na kukimbia, alikuwa ni Ali aliyesimama imara.

Bila woga, alimkinga Mtume kutokana na maadui mpaka sauti iliyojificha ikatangaza, “Hakuna upanga kama Dhu’l-fiqah, na hakuna kijana shujaa kuliko Ali.”

Namna ya pili ya ushindi inahusiana na vile vita ambavyo vilipiganwa baada ya kifo cha Mtume. Ushindi huu ulikuwa ni kutokana na ushujaa wa maaskari mashuhuri wa Kiislamu na ubingwa wao wa kupanga. Lakini hapa hatuhusiki na ushindi wa Kiislamu wa wakati wa Ukhalifa wa Umar. Maudhui yetu ni kuhusu ujasiri wa Umar mwenyewe. Hauthibitishwi na ushahidi wowote wa kihistoria.

Hafidh: Ni matusi kudai kwamba Umar alikimbia kutoka uwanja wa mapambano, na kwamba hii ilipelekea kushindwa kwa Waislamu.

Muombezi: Kama kuonyesha ukweli wa kihistoria kuhusu mtu ni matusi, basi matusi haya yameandikwa na maulamaa wenu.

Hafidh: Ni wapi maulamaa wetu walipoandika kwamba Khalifa Umar alikimbia kutoka Uwanja wa mapambano? Ni wakati gani alisababisha kushindwa kwa Waislamu?

Kushindwa Kwa Abu Bakr Na Umar Katika Vita Vya Khaibar.

Muombezi: Kwa vile Ali alikuwa akiumwa macho katika siku ya kwanza ya vita vya Khaibar, Mtume alimpa Abu Bakr bendera ya Waislamu, ambaye aliongoza jeshi la Waislamu dhidi ya Mayahudi. Alirudi akiwa ameshindwa baada ya muda mfupi wa mapambano. Siku iliyofuata bendera ya Waislamu ilitolewa kwa Umar, lakini kabla hajafika sehemu ya mapambano, alikimbia kwa woga.

Hafidh: Maelezo haya ni uzushi wa Shi’a.

Muombezi: Vita vya Khaibar vilikuwa ni tukio muhimu la maisha ya Mtukufu Mtume, lililosimuliwa kwa kinaganaga na wanahistoria wa madhehebu zote. Hafidh Abu Nu’aim Ispahani katika “Hilyatu’l-Auliya” Jz. 1, uk. 62, Muhammad Bin Talha Shafi’i katika “Matalibus-Su’ul”, uk. 40, kutoka katika “Sira” cha Ibn Hisham, Muhammad bin Yusuf Ganji Shafi’i katika “Kifayatut-Talib”, Sura ya 14, na maulamaa wenu wengi wengine wameandika tukio hili.

Lakini simulizi iliyo sahihi zaidi ni ile ya wanachuoni wawili wakubwa. Muhammad bin Ismail Bukhari, ambaye ameandika katika Sahih yake Jz. 2 iliy- ochapishwa Misir 1320 A.H., uk. 100, na Muslim Bin Hujjaj, ambaye anaandika katika Sahih yake, Jz. 2, iliyochapishwa Misir 1320 A.H., uk. 324, kwamba, “Khalifa Umar alikimbia kutoka Uwanja wa mapambano katika safari mbili.”

Miongoni mwa thibitisho nyingi zilizo wazi juu ya nukta hii ni beti zilizo za wazi za Ibn Abi’l-Hadid wa madhehebu ya Mu’tazila zijulikanazo kama “Alawiyyat-e-Sab’a” katika

kumsifu Ali. Kuhusu “lango la Khaibar”, anasema: “Je, umesikia hadithi ya ushindi wa Khaibar? Miujiza mingi imefunganishwa pamoja ambayo huchanganya hata akili zenyes busara! Hawa wawili (Abu Bakr na Umar) walikuwa hawana mapenzi kwayo, au maarifa, ya kubeba bendera (kuongoza jeshi). Hawakujua siri za kutunza heshima ya bendera, waliifunika na twezo na wakakimbia ingawa walijua kwamba kukimbia kutoka kwenye uwanja wa mapambano ni sawa sawa na ukafiri.

Walifanya hivyo kwa sababu ya mmoja wa wanajeshi shujaa wa Kiyahudi, kijana mrefu na upanga wa wazi mkononi, akiwa amepanda juu ya farasi mwenye umbo refu, akiwashambulia kama mbuni dume aliyesisimuliwa, ambaye amepata nguvu kutokana na hewa ya msimu wa kuchipua na uoto wake wa mimea. Alikuwa kama ndege mkubwa ambaye amejipamba kwa rangi za kupendeza na aliyekuwa akienda kuelekea kwa mpenzi wake. Mng’aro wa moto wa kifo kutoka kwenye upanga wake na mkuki uliangaza na kuwatishia watu wawili hawa.”
Ibn Abi’l-Hadid akizungumza nao (Abu Bakr na Umar) anaendelea kusema: “Nakuombeeni msamaha juu yenu, kwa kule kushindwa na kukimbia kwenu, kwa vile kila mtu anachukia kifo na kupenda uhai. Kama wengine wote, ninyi pia hamkukipenda kifo ingawa hakuna kinga kutokana na kifo. Lakini hamkuweza kujihatarisha na kifo.” Lengo langu sio kumkashifu mtu yeyote, ninasimulia ukweli wa kihistoria kuonyesha kwamba Khalifa hakuwa na ushujaa kama huo ambao angestahiki sifa ya “Mkali dhidi ya Makafir.” Ukweli ni kwamba yeye alikimbia kutoka uwanja wa mapambano.

Sifa hii katika mjadala inamhusu Ali peke yake, ambaye katika kila vita alikuwa mkali dhidi ya makafiri. Ukweli huu umethibitishwa na Allah kwenye Qur’ani Tukufu. Yeye Anasema:

“Enyi mlioamini! atakayeiacha dini yake miongoni mwenu, basi hivi karibuni Mwenyezi Mungu ataleta watu wengine ambao atawapenda, nao watampenda, wanyenyekevu kwa waumini, na wenye nguvu kwa makafiri. Watapiganaia dini ya Mwenyezi Mungu, wala hawataogopa lawama ya wenye kulaumu. Hiyo ndiyo fadhila ya Mwenyezi Mungu, humpa amtakaye, na Mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa, Mwenye kujua.” (5:54-56).

Hafidh: Inashangaza kwamba unajaribu kuhusisha aya hii na Ali. Hii inazungumzia wau- mini ambao wanazo sifa hizi na vipenzi wa Allah.

Muombezi: Ingekuwa vizuri kama ungeniuliza ni hoja gani ningeweza kutoa kuunga mkono maneno yangu. Jibu langu ni kwamba kama aya hii ingeteremshwa katika kuwasifu waumini, wasingekimbia kamwe kutoka uwanja wa mapambano.

Hafidh: Je, ni haki kuwalaumu waumini na masahaba wa Mtume (lawama) ya kukimbia kutoka kwenye hatari? Watu hawa walipigana kishujaa katika vita.

Muombezi: Sio mimi niliyewaita “Wakimbiaji.” Historia inawaonyesha kama hivyo. Pengine umesahau kwamba katika vita vya Uhud na Hunain waumini wote na masahaba kwa ujumla, pamoja na masahaba wakubwa wa Mtume, walitafuta usalama kwa kukimbia.

Kama ilivyosimuliwa na Tabrini na wengine, wao walimuacha Mtume peke yake kati ya makafiri. Je, inawezekana kwamba wale waliogeuka na kuwapa maadui migongo wakimuacha Mtume peke yake kuwakabili maadui walikuwa wapenzi wa Allah na Mtume Wake?

Siko peke yangu katika kudai kwamba Aya hii iko katika kumsifu Ali. Abu Ishaq Imam Ahmad Tha’labi, ambaye mnamchukulia kama mkubwa wa wasimuliaji wenu wa Hadith, anaandika katika kitabu chake “Kashfu’l-Bayan” kwamba aya hii imeteremshwa katika kumsifu Ali kwa sababu hakuna mtu mwingine aliyekuwa na sifa zilizotajwa ndani yake.

Hakuna mwanahistoria - wa kwetu au wa nje - ambaye ameandika kwamba katika vita 36 vilivyopiganwa na Mtume, Ali hakuserereka kamwe hata katika moja. Katika vita vya Uhud, wakati masahaba wengine wote walipokimbia, na jeshi la adui lenye askari 5000 likawashambulia Waislamu, mtu pekee aliyebakia kwenye sehemu yake mpaka ushindi ulipopatikana alikuwa ni Ali.

Ingawa alijeruhiwa sehemu mbalimbali na kuvuja damu kwa wingi, aliwakusanya wale ambao walikuwa wamekimbia na kuendelea kupigana mpaka ushindi ulipopatikana.

Hafidh: Huna aibu kuhusisha “kukimbia” kwa masahaba wakubwa? Masahaba wote kwa ujumla na hasa Abu Bakr na Umar kwa ushujaa walimzunguuka Mtume na kumlinda.

Muombezi: Hukujifunza historia kwa uangalifu. Kwa ujumla, wanahistoria wameandika kwamba, katika vita vya Uhud Hunain na Khaibar masahaba wote walikimbia. Nimekueleza kuhusu Khaibar.

Amma kuhusu Hunain, Hamid katika “Jam-e-Banus- Sahihain” na Halabi katika “Siratu’l-Halabiyya”, Jz. 3, uk. 123, anasema kwamba masahaba wote walikimbia isipokuwa wanne: Ali na Abbas walikuwa mbele ya Mtume, Abu Sufyan Bin Harith alishika hatamu za farasi wa Mtume, na Abdullah Bin Mas’ud alisimama upande wake wa kushoto. Kukimbia kwa Waislamu huko Uhud hakukukataliwa na mtu yeyote.

Muhammad bin Yusuf Ganji Shafi’i katika “Kifayatut-Talib” Sura ya 27, kwa vyanzo vyake mwenyewe, anamnukuu Abdullah Bin Mas’ud akisema kwamba Mtume amesema: “Wakati wowote Ali anapopelekwa peke yake katika pambano, nilimuona Jibril upande wake wa kulia, Mikael upande wake wa kushoto, na wingu likimfunika kutoka juu mpaka Allah Alipomfanya mshindi.”

Imam Abu Abdu’r-Rahman Nisa’i anasimulia hadith 202 katika kitabu chake “Khasa’is-e- Alawi” kwamba Imam Hasan, akiwa amevaa kilemba cheusi alikuja kwa watu na akasimulia sifa za baba yake, akisema kwamba katika vita vya Khaibar, wakati Ali alipokwenda kuelekea ile ngome, “Jibril alikuwa akipigana upande wake wa kulia na Mikael upande wake wa kushoto.

Alimkabili adui kwa ushujaa mkubwa mpaka alipopata ushindi na akawa anastahiki mapenzi ya Allah.”

Ali Alikuwa Mwenye Kupendwa Na Allah Na Mtukufu Mtume (S.A.W.W.).

Katika Aya hii Allah anasema kwamba Yeye anawapenda wale ambao wana sifa hizi na kwamba wao pia wanampenda Yeye. Sifa hii ya kupendwa na Allah ni ya kipekee kwa Ali. Kuna ushahidi mwingi sana wenye kuunga mkono mtazamo huu. Miongoni mwa hadithi nyingi zinazohusiana na jambo hili ni ile inayosimuliwa na Muhammad Bin Yusuf Ganji Shafi’i katika “Kifayatut-Talib”, Sura ya 7.

Anasimulia kupitia vyanzo vyake mwenyewe, kutoka kwa Abdullah ibn Abbas, ambaye amesema kwamba, siku moja alikuwa amekaa na baba yake, Abbas mbele ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wakati Ali alipoingia hapo na kumsalimia. Mtume akasimama, akamchukua mikononi mwake, akambusu katikati ya macho yake na akamfanya akae upande wake wa kulia. Kisha Abbas akamuuliza Mtume kama anampenda Ali. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akajibu, “Ewe ami yangu mheshimika! Wallahi, Allah anampenda zaidi kuliko ninavyompenda mimi.”

Hadith Ya Bendera Katika Ushindi Wa Khaibar.

Uthibitisho wenye nguvu wa Ali kupendwa na Allah, na wa ushujaa wake katika uwanja wa vita, ni “Hadith-e-Rayat” (Hadith ya Bendera) ambayo ni sehemu ya mkusanyiko wenu wa Hadith. Hakuna hata mmoja wa Maulamaa wenu mashuhuri aliyeikataa.

Nawab: Ni nini Hadith-e-Rayat? Tafadhali kama ikiwezekana inukuu pamoja na vyanzo vyake.

Muombezi: Maulamaa na wanahistoria mashuhuri wa madhehebu hizi mbili (Shia na Sunni) wamesimulia “Hadith-e-Rayat.” Kwa mfano, Muhammad Bin Isma’il Bukhari katika Sahih yake Jz. 2 ‘Kitabu’l-Jihad Wa’s-Siyar,’ Sura Du’au’n-Nabi, vilevile katika Jz.

3 ‘Kitabu’l-Maghazi’, Sura ya Ghazawa-e-Khaibar. Muslim Bin Hajjaj katika Sahih yake, Jz. 2, uk. 324; Imam Abdu’r-Rahman Nisa’i katika “Khasa’isu’l-Alawi” Tirmidh katika “Sunan” yake; Ibn Hajar Asqalani katika “Isaba”, Jz. 2, uk. 508; Muhaddith-e-Sham kati- ka “Ta’rikh”; Ahmad bin Hanbal katika “Musnad”; Ibn Maja Qazwini katika “Sunan” yake; Sheikh Sulayman Balkh Hanafi katika “Yanabiu’l-Mawadda” Sura ya 6; Sibt Ibn Jauzi katika “Tadhkira”; Muhammad Bin Yusuf Ganji Shafi’i katika “Matalibus-Su’ul”; Hafidh Abu Nu’aim Isfani katika “Hilyatu’l-Auliya”; Abu Qasim Tibran katika “Ausat” na Abu Qasim Husain bin Muhammad (Raghib Isfahani) katika “Muhadhiratu’l-Uda-ba” Jz. 2, uk. 212. Kwa ufupi, kwa hakika karibu wanahistoria wenu wote na Muhadathina wameandika hadith hii, hivyo kwamba Hakim anasema: “Hadith hii imefikia hatua ya makubaliano ya pamoja.” Tabrini anasema: “Ushindi wa Ali katika Khaibar unathibitish- wa na umoja wake.”

Wakati jeshi la Waislamu lilipoizingira ngome ya Khaibar, lilishindwa mara tatu chini ya uongozi wa Abu Bakr na Umar, na wakakimbia. Masahaba walivunjika moyo sana. Ili kuwatia moyo masahaba Mtume alitamka kwamba Khaibar itatekwa. Alisema: “Kwa jina la Allah, kesho nitampa bendera mtu ambaye atarudi na ushindi. Ni mtu ambaye husham- bulia kwa kurudia rudia na kamwe haondoki kwenye uwanja wa mapambano na kamwe harudi nyuma mpaka apate ushindi. Yeye anampenda Allah na Mtume Wake, na Allah na Mtume Wake, wanampenda yeye.” Usiku ule masahaba hawakuweza kulala, wakifikiria ni nani angepewa upendeleo huu maalum.
Asubuhi, kila mmoja alivaa nguo za kijeshi na wakajitokeza mbele ya Mtume. Mtume akauliza: “Yuko wapi ndugu yangu na mtoto wa ami yangu, Ali Bin Abu Talib?” Walimwambia: “Ewe Mtume wa Allah, yeye anaumwa na macho sana kiasi kwamba hawezi hata kusogea.” Mtume akamtuma Salman amuite Ali. Salman akamshika Ali mkono akampeleka kwa Mtume.

Alimsalimia Mtume na baada ya kumrudishia salaam, Mtume akamuuliza, “una hali gani Ewe Abu’l-Hasan?” Akajibu, “Yote ni kheri kwa baraka za Allah. Naumwa kichwa na maumivu makali katika macho kiasi kwamba siwezi kuona chochote.” Mtume alimuomba aje karibu. Wakati Ali aliposogea karibu, Mtume aliweka mate ya kinywa chake mwenyewe kwenye macho ya Ali na akamuombea. Punde tu macho yake yakawa meupe na maumivu yake yakatoweka kabisa. Akampa Ali bendera ya ushindi.

Ali alielekea kwenye ngome za Khaibar, akapigana dhidi ya Mayahudi, akauwa wanajeshi wao mashujaa kama vile Marhab, Harith, Hisham na Alqama, na akazishinda ngome za Khaibar zilizokuwa hazishindiki.

Ibn Sabbagh Malik katika “Fusulu’l-Muhimma” uk. 21, amenukuu taarifa hii kutoka vitabu sita vya hadith, ambapo Muhammad bin Yusufu Ganji Shafi’i katika “Kifayatu’l-Talib” Sura ya 14, baada ya kuisimulia hadithi hii anasema kwamba mtunga mashairi mkuu wa Mtume, Hassan bin Thabit, alikuwepo wakati wa tukio hili. Alitunga mashairi kumsifu Ali:

“Ali alikuwa akiumwa macho. Kwa sababu kulikuwa hakuna tabibu, Mtume alimtibia kwa mate yake mwenyewe. Hivyo wote muuguzi na mgonjwa walibarikiwa. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema:‘Leo nitampa Bendera mpanda farasi aliye hodari mno, shujaa na muungwana, mwenzi wangu katika mapambano. Anampenda Allah na Allah anampenda; hivyo kupitia kwake Yeye Allah atatufanya tuzishinde ngome.’ Baada ya hili, akiwaacha wote pembeni, alimchagua Ali na akamfanya mrithi wake.”

Ibn Sabbagh Maliki anasimulia kutoka “Sahih Muslim” kwamba Umar bin Khattab amesema: “Kamwe sijatamani kuishika bendera lakini siku ile nilikuwa na hamu kubwa nayo.

Nilirudia rudia kujifanya nionekane mbele ya Mtume, nikitamani kwamba huenda pengine akaniita na kwamba nikaweza kubarikiwa heshima hii. Lakini alikuwa ni Ali ambaye ali- itwa na Mtume na utukufu ukaenda kwake.” Sibt Ibn Jauzi ameandika riwaya hii katika kitabu chake “Tadhkira”, uk. 15, na Imam Abdur-Rahman Ahmad Bin Ali Nisa’i katika “Khasa’isu’l-Alawi”, baada ya kusimulia hadithi kumi na mbili juu ya habari ya Ali kushika bendera kule Khaibar, ananukuu riwaya hiyo katika hadith ya kumi na nane kuhusu matumaini ya Umar kuipata bendera.

Vilevile Jalalu’d-Din Suyuti katika kitabu chake “Ta’rikhu’l-Khulafa”, Ibn Hajar Makki, katika “Sawa’iq” na Ibn Shirwaini katika kitabu chake “Firdausu’l-Akbar” anasimulia kwamba Umar Bin Khattab amesema: “Ali amejaaliwa mambo matatu na kama ninge- likuwa na moja tu ningelipendelea kuliko ngamia wote walioko katika miliki yangu:- Ndoa ya Ali na Fatima; kukaa kwake msikitini katika hali yoyote na hii haikuruhusiwa kwa yeyote isipokuwa Ali, na kushika kwake bendera katika vita vya Khaibar.”

Hoja yangu, kutegemea juu ya riwaya za Muhadithina wenu, inathibitisha kwamba maneno katika Aya - “Yeye (Allah) anawapenda na wao vilevile wanampenda Yeye” - yanahumhusu Ali. Muhammad Bin Yusufu Ganji Shafi’i katika “Kifayatut-Talib”, Sura ya 13, anasimulia kwamba Mtume amesema: “Kama mtu anataka kumtazama Adam, Nuh na Ibrahim, na amtazame Ali.” Anasema kwamba, Ali ndiye yule anayesemwa na Allah kati- ka Qur’ani Tukufu: “Na wale ambao wako pamoja naye ni wakali dhidi ya makafiri, (na) wenye kuhurumiana wenyewe kwa wenyewe.” (48:29).

Ama kwa kauli yako kwamba kifungu cha maneno katika aya hii “kuhurumiana wenyewe kwa wenyewe” kinamhusu Uthman na huonyesha nafasi yake kama Khalifa wa tatu, hii haiungwi mkono na ushahidi wa kihistoria. Kwa kweli, tabia yake ilikuwa ni kinyume chake kabisa. Kuna hoja nyingi zenye kuthibitisha jambo hili, lakini nitasimama hapa. Mambo ambayo yangesemwa yanaweza kuchochea uhasama.

Hafidh: Kama utaishia kwenye rejea sahihi tu, hakuna sababu kwa nini tuchukizwe.
Muombezi: Nitataja tu baadhi ya hizo.

Tabia Ya Uthman Na Namna Ya Maisha Ikilingan- Ishwa Na Ile Ya Abu Bakr

Na Umar.

Ibn Khaldun, Ibn Khallikan, Ibn A’sam Kufi (imeandikwa vilevile katika Siha-e-Sitta), Mas’ud katika “Muruju’dh-Dhahab” Jz. 1, uk. 435, Ibn Hadid katika “Sharhe Nahju’l- Balagha Jz. 1, na wengine katika Maulamaa wenu wanathibitisha kwamba wakati Uthman Bin Affan alipokuwa Khalifa, alikkwenda kinyume na mifano iliyowekwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na vilevile dhidi ya mwendo wa Abu Bakr na Umar. Madhehebu zote zinakubaliana kwamba katika Kamati ya Ushauri (Shura) ambayo kwayo alichaguliwa kuwa Khalifa, Abdur-Rahman Bin Auf alimlisha kiapo cha kutegemea juu ya kitabu cha Allah, Suna ya Mtume, na mwendo wa Abu Bakr na Umar.

Moja ya masharti ya kiapo chake ilikuwa kwamba Uthman hatawaacha Bani Umayya kuingilia (mambo ya uongozi) wala hangewapa mamlaka yoyote. Lakini nafasi yake (ya uongozi) ilipoimarika aliyavunja masharti haya. Kwa mujibu wa Qur’ani Tukufu na hadith za kuaminika, kuvunja makubaliano (Mkataba) ni dhambi kubwa.

Maulamaa wenu wenyewe wanasema kwamba Khalifa Uthman alivunja ahadi yake. Katika Ukhalifa wake wote alitenda kinyume na mwendo wa Abu Bakr na Umar. Aliwapa Bani Ummaya Mamlaka kamili juu ya maisha ya watu na mali zao.

Utajiri Wa Khalifa Uthman.

Hafidh: Ni katika njia gani alitenda dhidi ya mafunzo na matendo ya Mtume na mwendo wa Abu Bakr na Umar?

Muombezi: Muhadith mashuhuri, Mas’ud katika kitabu chake “Muruju’dh-Dhahab” Jz. 1, uk. 433, na wanahistoria wengine wameandika kwamba Uthman alijenga nyumba ya kipekee ya mawe yenye milango iliyotengenezwa kwa mti wa msandali. Alijikusanyia utajiri mkubwa, ambao aliutoa kiufujaji kwa Bani Umayya na wengine. Kwa mfano kodi ya kidini (Khums) kutoka Armania, ambayo ilitekwa katika kipindi chake ilitolewa kwa mlaaniwa Marwan bila idhini yoyote ya kidini.

Vile vile alimpa dirham 100,000 kutoka Baitul-mal (hazina ya Umma). Alimpa Abdullah Bin Khalid dirham 400,000, dirham 100,000 kwa Hakam Bin Abi’l-Aas, ambaye alilaaniwa na kuhamishwa na Mtume, na dirham 200,000 kwa Abu Sufyani (kama ilivyoandikwa na Ibn Abi’l-Hadid katika “Sherhe Nahju’l-Balagha.”, Jz. 1, uk. 68).

Katika siku aliyouawa, mali yake binafsi ilifikia dinari 150,000 na dirham milioni 20 taslimu. Alimiliki mali huko Wadiu’l-Qura na Hunain yenye thamani ya dinari 100,000 na kundi kubwa la ng’ombe, kondoo na ngamia. Kama matokeo ya matendo yake, Bani Umayya walio mbele walilimbikiza utajiri mkubwa utokanao na juhudi za watu.

Kwa Khalifa wa Uislam kujikusanyia utajiri kama huo wakati watu wengi wanateseka kwa njaa kwa hakika ilikuwa ni kosa. Aidha tabia hii ilikuwa inapingana kabisa na mwenendo wa masahaba wenzake, Abu Bakr na Umar. Uthman aliahidi katika Kamati ya Ushauri (Shura) kwamba angefuata nyayo zao. Mas’ud katika kitabu chake “Muruju’dh-Dhahab” anasema kuhusu Khalifa Uthman kwamba, wakati Khalifa Umar alipokwenda na mwanae Abdullah kuhiji, matumizi yao katika safari yao ya kwenda na kurudi yalikuwa dinari 16.

Alimwambia mwanae kwamba wamekuwa wafujaji. Kama utalinganisha mwendo wa ulaji mdogo wa Umar na matumizi ya kifujaji ya Uthman, utakubali kwamba mwendo wa maisha ya Uthman ulikuwa kinyume na kiapo chake katika ile Kamati ya Ushauri.

Khalifa Uthuman Aliwapa Moyo Watenda Maovu Miongoni Mwa Bani Umayya.

Uthmani vilevile aliwapa Bani Umayya mamlaka juu ya maisha na heshima za watu. Hatimaye, machafuko yalijitokeza katika ardhi za Waislamu. Aliwachagua watu wake anao wapendelea katika nafasi za juu kinyume na matakwa ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), Abu Bakr na Umar.
Kwa mfano alimpa nafasi za juu ami yake, Hakam Bin Aas, mtoto wake, Marwan ambao wote walihamishwa na kulaaniwa na Mtume.

Hafidh: Unaweza ukathibitisha kwamba walilaaniwa?

Muombezi: Kuna njia mbili za kuthibitisha kwamba walilaaniwa. Allah aliwaita Bani Umayya “Mti uliolaaniwa” katika Qur’ani Tukufu (17:60). Imam Fakhuru’d-Din Razi, Tabari, Qartabi, Nishapuri, Suyuti, Shawkani, Alusi, Ibn Abi Hatim, Khatib Baghdad, Ibn Mardawaih, Hakim, Maqrizi, Baihaqi na wengine katika maulamaa wenu wanasimulia kutoka Ibn Abbas kwamba “Mti uliolaaniwa” katika Qu’an unahusu kabila la Umayya. Katika ndoto, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliona nyani wakipanda na kushuka katika mimbari yake (na kufukuza watu kutoka Msikitini).

Alipoamka, Malaika Jibril akateremsha Aya hii na kumueleza Mtume kwamba nyani wale walikuwa Bani Umayya, ambao watanyang’anya Ukhalifa wake baada yake. Sehemu yake ya kusalia na mimbari vitabakia katika mamlaka yao kwa miezi elfu. Imam Fakhni’d-Din Razi anasimulia kutoka Ibn Abbas kwamba Mtume alitaja jina la Hakam Bin Aas. Kwa hiyo amelaaniwa kwa vile ana- tokana na “Mti uliolaaniwa.”

Kuna Hadith nyingi kutoka vyanzo vya Sunni kuhusu kulaaniwa kwao.Hakim Nishapuri, katika “Mustadrak” Jz. 4, Uk. 437 na Ibn Hajar Makki katika “Sawa’iq-e-Muhriqa”, ananukuu kutoka kwa Hakim hadith ifuatayo kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). “Hakika muda mfupi tu familiya yangu itatawanyishwa na kuuawa na Umma wangu. Bani Umayya, Bani Mughira, na Bani Makhzum ni makatili zaidi katika maadui zetu.” Mtume Akasema kuhusu Marwan, akiwa mtoto wakati huo, “Huyu ni mjusi, mtoto wa mjusi, mwenye kulaaniwa, mtoto wa aliyelaaniwa.”

Ibn Hajar anaelezea kutoka kwa Umar bin Murratu’l-Jihni, Halabi katika “Siratu’l- Halabiyya”, Jz. 1, uk. 337; Baladhuri katika “Ansab”, Jz. 5, uk. 126; Sulayman Balkhi katika “Yanabiu’l-Mawadda”; Hakim katika “Mustadrak”, Jz. 4, uk. 481; Damiri katika “Hayatu’l-Haiwan”, J. 2, uk. 291; Ibn Asakir katika kitabu chake cha “Ta’rikh”; Imamu’l- Haram Muhyi’d-Din Tabari katika “Dhakha’iru’l-Uqba” na wengine wamesimulia kutoka kwa Umar bin Murratul-Jihni kwamba Hakam Bin Aas alitaka mazungumzo na Mtume. Mtume alipoitambua sauti yake, akasema: “Muacheni aingie ndani. Laana iwe juu yake na juu ya kizazi chake, isipokuwa wale ambao wanaamini, na watakuwa wachache.”

Imam Fakhri’d-Din Razi, katika kitabu chake “Tafsir-e-Kabir”, Jz. 5, akiandika kuhusu Aya ya “Mti uliolaaniwa.......” na namna yake, anarejea kwenye kauli ya Aisha ambaye alisema kumuambia Marwan: “Allah alimlaani baba yako wakati upo kwenye mbegu zake za uzazi; hivyo na wewe vilevile ni sehemu yake yule ambaye amelaaniwa na Allah.”

Allama Mas’ud, anasema katika kitabu chake “Muruju’dh-Dhahab”, Jz. 1, uk. 435, kwamba Marwan bin Hakam alilaaniwa na kuhamishwa na Mtume. Alihamishwa kutoka Madina. Hakuruhusiwa kuingia Madina wakati wa Ukhalifa wa Abu Bakr na Umar, lakini Uthman alipokuwa Khalifa, alitenda kinyume cha mafundisho ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), Abu Bakr, na Umar na akamruhusu kuingia Madina. Alimuweka karibu sana naye mwenyewe pamoja na Bani Umayya wote na akawafanyia upendeleo.

Nawab: Hakam Bin Abil-Aas alikuwa ni nani, na kwanini alihamishwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)?

Muombezi: Hakam Bin Aas alikuwa ni ami yake Khalifa Uthman. Kwa mujibu wa Tabari, Ibn Athir, na Baladhuri, ambaye anaandika katika “Ansab”, Jz. 5, uk. 17, yeye alikuwa ni jirani yake Mtume Zama za Jahiliyya. Alimtukana Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), hususan baada ya tangazo lake la Utume. Alitembea nyuma ya Mtume na kumdhihaki kwa kumuigiza miondoko ya utembeaji wake.

Hata wakati wa Sala, alikuwa akimyooshea kidole kwa dharau. Baada ya kulaaniwa na Mtume, alibakia katika hali ya kupooza wakati wote na hatimaye akapoteza hali ya utimamu akili. Baada ya kutekwa Makka, alikuja Madina na inavyoonekana aliingia Uislamu, lakini mara kwa mara alimtukana Mtume.

Wakati alipokwenda nyumbani kwa Mtume, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mara moja alitoka nje ya nyumba yake na akasema “Mtu yeyote asiombe msamaha kwa niaba yake. Sasa yeye na watoto wake, Marwan na wengine wanapaswa waondoke Madina.” Kwa hiyo, mara moja Waislamu wakamtoa na kumfukuzia Ta’if. Wakati wa kipindi cha Abu Bakr na Umar, Uthman alimsaidia, akisema kwamba alikuwa ni ami yake na kwamba inapaswa aruhusiwe kurudi Madina. Lakini hawa wengine hawakulikubali shauri hili, wakisema kwamba kwa vile alilaaniwa na kuhamishwa na Mtume hawatamruhusu kurudi.

Wakati Uthman alipokuwa Khalifa, aliwarudisha wote. Ingawa watu wengi walilipinga shauri hili; Uthman alionyesha upendeleo maalum kwa jamaa zake na wengine anaowapenda. Alimfanya Marwan kuwa msaidizi wake na Afisa Mkuu wa Baraza lake. Alijikusanyia karibu yake waovu wengi wa kabila la Umayya na akawateua kushika nafasi za juu (katika serikali). Matokea yake ni kwamba, kwa mujibu wa utabiri wa Umar, wao ndio walihusika na janga lililompata Uthman.

Miongoni mwa watu walioteuliwa na Uthman alikuwa Walid bin Aqaba bin Abi Mu’ith ambaye alipelekwa Kufa kuwa Gavana. Kwa mujibu wa riwaya ya Mas’ud katika “Muruju’dh-Dhahab”, Jz. 1, Mtume alisema kuhusu Walid: “Hakika yeye ni mmoja wa wale watakaokwenda motoni.” Alijitumbukiza waziwazi kabisa katika matendo maovu. Kwa mujibu wa maelezo ya Mas’ud katika “Muruju’dh- Dhahab”, Abdu’l-Fida katika “Ta’rikh” yake, Suyuti katika “Ta’rikhu’l-Khulafa”, uk. 104, Abu’l-Faraj katika “Aghani” Jz. 4, uk. 128, Imam Ahmad bin Hanbal katika “Musnad”, Jz. 1, uk. 42 Yaqubi katika “Ta’rikh” yake Jz. 2, uk. 142; Ibn Athir vilevile katika Usudul- Uqba, Jz. 5, uk. 91 na wengine walisema kwamba, wakati wa ugavana wake huko Kufa, Walid alipitisha usiku mzima akifanya ufuska. Alikuja msikitini kwa ajili ya Sala ya Alfajiri akiwa amelewa na akasalisha rakaa nne za Sala ya asubuhi (badala ya mbili) kisha akawageukia watu na kusema “Uzuri ulioje wa asubuhi hii! Ningetaka kuendeleza Sala hii kama mutaridhia”.

Baadhi wanasema kwamba alitapika kwenye kibla ya msikiti kitendo ambacho kilileta maudhi makubwa kwa watu ambao walilalamika kwa Khalifa Uthman. Mmoja wa watu hawa wanaojulikana sana ni Mu’awiya, ambaye alifanywa kuwa Gavana wa Syria. Walid aliondolewa na badala yake akateuliwa Sa’id Bin Aas kama Gavana wa Kufa.

Wakati watu walizipogundua sera za Uthman, sera zilizo kinyume na mafunzo ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), walighadhibika. Walichukuwa hatua ambazo hatimae zilisabisha matokeo yake mabaya kama hayo. Uthman alihusika na kifo chake mwenyewe kwa sababu hakufikiria athari za matendo yake. Alipuuza ushauri wa Ali na akawa amepotezwa na wadanganyifu wenye kujipendekeza. Ibn Abi’l-Hadid ananukuu mazungumzo kati ya Umar na Ibn Abbas katika Sherhe ya “Nah’ju’l-Balagha”, Jz. 3, uk. 106. Khalifa Umar alisema kitu kuhusu kila mmoja wa wajumbe sita wa Kamati ya Ushauri na akaonyesha udhaifu wao.

Wakati jina la Uthmani lilipotajwa, baada ya kushusha pumzi mara tatu, Umar akasema kwamba, “Kama Ukhalifa utamfikia Uthman atawaweka watoto wa Abi Mu’it (Bani Umayya) juu ya watu. Kisha Waarabu watasimama na kuasi dhidi yake na kumuua.’

Ibn Abi’l-Hadid anakubaliana na uchambuzi wa Umar. Wakati Uthman alipokuwa Khalifa aliwakusanya karibu yake Bani Umayya. Aliwateuwa kuwa magavana na wakati walipoyachezea vibaya mamlaka yao, alifumba macho. Khalifa Uthman hakutaka hata kujinasua mwenyewe kutokana na Marwan.Watu wakichemka kwa kutoridhika, waliasi dhidi yake na mwishowe wakamuua.

Mtukufu Mtume (S.A.W.W.) Aliwalaani Abu Sufyan, Mu’awiya Na Mtoto

Wake Yazid.

Itasaidia sana kama utasoma kitabu maarufu cha Historia cha Jarir Tabari, mmoja wa maulamaa wenu wakubwa, ambaye ameandika: “Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimuona Abu Sufyani akiwa amepanda punda. Mu’awiya alikuwa anaivuta kwa mbele, na mtoto wake Yazid, alikuwa anaisukuma kwa nyuma. Mtume akasema: “Laana iwe juu ya mpan- daji, mvutaji na msukumaji.” Maulamaa wenu mashuhuri, kama Tabari na Ibn A’sam Kufi wamemuona Khalifa Uthman kuwa ni mwenye makosa kwa kutomuua Abu Sufyan wakati alipoukana Uislamu, Wahyi (ufunuo), na kuwepo kwa Jibril.

Baada ya kumkemea Abu Sufyan kidogo, Uthman akalitupa kando suala hili. Nitawaomba vilevile muangalie Khutba ya 163 ya “Nahju’l-Balagha” na simulizi ambayo Ibn Abi’l-Hadid katika Sherhe yake ya “Nahju’l-Balagha” Jz. 2, (iliyochapishwa Misr) uk. 582, ananukuu kutoka “Tar’rikh-e-Kabir”, ya Tabari kwamba baadhi ya masahaba katika majimbo mbalimbali waliandika barua wakishawishi watu kutangaza vita vya Jihad, ili kujilinda kutokana na uonevu wa kikatili wa Uthman.
Katika mwaka 34 A.H. watu wenye malalamiko dhidi ya maofisa walioteuliwa na Uthman walikuja Madina kwa Ali na wakamuomba aingilie kati.

Uthman Hakukubali Ushauri Wa Ali.

Ali alikwenda kwa Uthman na akamuonya kuhusu matokeo ya kutisha ya kuendelea na sera zake hizo. Ali alisema, “Nakuambia kwa ajili ya Allah, usije ukajifanya wewe mwenyewe kuwa ni kiongozi wa umma huu aliyeuawa. Imesemekana kwamba kiongozi mmoja wa umma huu atauwawa, ambapo baada yake milango ya umwagaji damu na mauaji itabakia wazi mpaka Siku ya Kufufuliwa.”

Lakini Marwan na masahaba wa ki-Bani Umayya walipuuza ushauri wa Ali. Baada ya Ali kuondoka, Uthman aliamuru watu kukusanyika Msikitini. Alikwenda kwenye mimbari na badala ya kuwatuliza watu, aliwachokoza zaidi. Matokeo yakawa kama Khalifa Umar alivyotabiri. Uthman akauawa na waasi. Tofauti na Abu Bakr na Umar ambao walifuata ushauri wa Ali, Uthman alipuuza onyo lake na matokeo yake yakampata yaliyompata.

Uthman Aliwapiga Masahaba Wa Mtukufu Mtume (S.A.W.W.) Bila Huruma

Aidha, Uthman aliwapiga Masahaba ambao walipinga uonevu wake. Miongoni mwao alikuwa ni Abdulla Bin Mas’ud, ambaye alikuwa Hafidhi, Qari (msomaji Qur’ani) Mtunza Hazina ya Umma, Mwaandishi ambaye aliandika Aya zilizoteremshwa, na mmoja wa masahaba wakubwa wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Aliheshimiwa sana na Abu Bakr na Umar, ambao wote walichukuwa ushauri kutoka kwake. Ibn Khaldun katika Ta’rikh yake ameeleza kwamba, Khalifa Umar alisisitiza kwamba Abdullah abakie naye kwa sababu alikuwa na elimu kamili ya Qur’ani Tukufu na kwa sababu Mtume alimsifia sana. Ibn Abi’l-Hadid na wengine wameandika jambo hilo hilo.

Maulamaa wenu wanakubali kwamba wakati Uthman alipokusudia kukusanya Qur’ani Tukufu, alichukuwa nakala zote kutoka kwa waandishi. Alidai vilevile nakala ya Qur’ani Tukufu kutoka kwa Abdullah bin Mas’ud. Abdullah hakumpa nakala yake hiyo. Uthman alikwenda mwenyewe nyumbani kwake na akaichukuwa hiyo nakala ya Qur’ani Tukufu kutoka kwake kwa nguvu.

Baadae wakati Abdullah alipogudua kwamba, kama ilivyofanywa kwa nakala nyingine za Qur’ani Tukufu, na nakala yake pia imechomwa moto, alihuzunika mno. Katika mikusanyiko ya kijamii na kidini alisimulia hadith za shutuma ambazo alizijua kuhusu Uthman. Wakati habari hizi zilipomfikia Uthman, aliamrisha watumwa wake, wakampiga sana kiasi kwamba meno yake yalivunjika na alibakia kitandani. Baada ya siku tatu alikufa kwa majeraha yake. Ibn Abi’l-Hadid anaandika kwa kina kuhusu ukweli huu kutoka Jz. 1, uk. 67 na 226 wa Sharh “Nahju’l-Balagha” (iliyochapishwa Misir) chini ya “Ta’n VI” na akaendelea kusema kwamba Uthman alikwenda kumuangalia Abdullah aliyekuwa anaumwa.

Walizungumza pamoja kwa muda. Uthman akasema, “Ewe Abdu’r-Rahman! Niombee msamaha kwa Allah.” Abdullah akasema, “Namuomba Allah achukue haki yangu kutoka kwako.” (yaani haki ifanyike). Wakati Abu Dharr, sahaba wa karibu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), alipohamishiwa Rabza, Abdullah alikwenda kumuaga.

Kwa sababu hii, Abdullah alipigwa viboko arubaini. Hivyo Abdullah akamsisitizia Ammar Yasir kwamba Uthman asikubaliwe kumsalia Abdulla Sala ya jeneza. Ammar Yasir alikubali, na baada ya kifo cha Abdullah, alisali Sala ya jeneza pamoja na kikundi cha masahaba. Uthman alipogundua mpango huu wa mazishi, alikuja kwenye kaburi la Abdullah na aka- muuliza Ammar kwanini alisali Sala ya jeneza. Akajibu kwamba alilazimika kufanya hivyo kwa sababu Abdullah aliusia hivyo.

Ammar Alipigwa Kwa Amri Ya Uthman.

Mfano mwingine wa ukatili wa Uthman ulikuwa ni kumpiga kwake Ammar Yasir. Maulamaa wa madhehebu zote wanasimulia kwamba wakati uonevu wa Bani Umayya ulipozidi, baadhi ya masahaba wa Mtume walimuandikia Uthman, wakimtaka awe na huruma.

Walisema kwamba, kama ataendelea kuwasaidia magavana wake hao makatili wa ki-Bani Umayya hatakuwa anaudhuru Uislamu tu, bali yeye mwenyewe pia atajitia katika matokeo mabaya sana. Walimtaka Ammar Yasir kufikisha kwa Uthman ile barua ya malalamiko kwa vile Uthman mwenyewe alikubali uadilifu wa Ammar. Walikuwa wamemsikia Uthman mara kwa mara akisema kwamba, Mtume amesema kwamba imani ilikuwa imechanganyika na nyama na damu ya Ammar. Hivyo Ammar aliichukua barua ile na kuipeleka kwa Uthman.

Wakati alipowasili, Uthman alimuuliza, “Je, una shughuli na mimi?” Akajibu , “Sina shughuli ya namna ya kibinafsi. Bali kikundi cha masahaba wa Mtume wameandika katika barua hii mapendekezo fulani na ushauri kwa ajili ya ustawi wako. Wameyatuma kwako kupitia kwangu.”

Baada ya kusoma misitari michache, Uthman akaitupa ile barua chini. Ammar akasema: “Ilikuwa sio vizuri kwako wewe kufanya hivyo. Barua kutoka kwa masahaba wa Mtukufu Mtume wa Allah (s.a.w.w.) inastahiki heshima. Kwa nini umeitupa chini? Ingelikuwa vizuri kwako wewe kuisoma na kuijibu.”

“Unaongopa” Uthman alisema kwa sauti kali. Kisha akaamuru watumwa wake kumpiga, na Uthman mwenyewe akampiga teke la tumbo. Alianguka chini, akazimia; jamaa zake wakaja wakamchukua, wakampeleka kwenye nyumba ya Ummu’l-Mu’Minin Umm Salma (mmoja wa wake za Mtume). Kuanzia adhuhuri mpaka usiku wa manane alikuwa bado amezimia. Makabila ya Hudhail na Bani Makhzun waligeuka dhidi ya Uthman kwa sababu ya ukatili wake kwa Abdullah Bin Mas’ud na Ammar Yasir.

Uthman alikuwa katili vilevile kwa Jandab Bin Junada, anayejulikana kama Abu Dhar Ghifari, mmoja wa masahaba karibu mno wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na mtu mwenye elimu. Muhadithina wakubwa na wanahistoria wa madhehebu zote wamesimulia kwamba mzee huyu wa miaka tisini alihamishwa isivyo halali kutoka sehemu hii kwenda sehemu nyingine kwa fedheha kubwa - kutoka Madina kwenda Syria, kutoka Syria kwenda Madina tena, kisha kutoka Madina kwenda kwenye Jangwa la Rabza. Alipanda ngamia asiye na matandiko akifuatana na binti yake tu. Alikufa katika (jangwa) la Rabza katika hali ya umasikini na ya kutelekezwa.

sMaulamaa na wanahistoria wenu wakubwa, pamoja na Ibn Sa’d katika “Tabaqat”, Jz. 4, uk. 168, Bukhari katika “Sahih” yake, mlango wa “Kitab-e-Zaka”; Ibn Abi’l-Hadid kati- ka Sherhe yake ya “Nahju’l-Balagha”, Jz. 1, uk. 240 na Jz. 2, uk. 375 – 87, Yaqubi katika kitabu chake cha Ta’rikh Jz. 2, uk. 148; Abu’l-Hasan Ali Bin Husain Mas’ud, muhadithi- na na mwanahistoria mashuhuri wa Karne ya Nne katika kitabu chake “Muruju’dh- Dhahab”, 1, uk. 438; na wengine wengi wamesimulia ukatili wa Uthman.

Imeelezwa kwa mapana jinsi gani alivyomfanyia ubaya Abu Dharr mtu mwenye moyo safi, mtu aliyepend- wa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), na vilevile jinsi gani Abdullah Bin Mas’ud, Hafidh na mwandishi wa Wahyi, alivyopigwa viboko arobaini kwa sababu alikwenda kumuaga Abu Dharr Ghifari. Hali ya ufidhuli wa aina hiyo hiyo ulionyeshwa kwa Ali kwa sababu hizo hizo.

Hafidh: Kama Abu Dharr alipatishwa mateso, ni kwa sababu ya maofisa wakorofi. Khalifa Uthman, ambaye alikuwa mpole sana na mwenye moyo laini, alikuwa hana habari na matukio haya.

Muombezi: Utetezi wako kwa Khalifa Uthman ni kinyume na ukweli. Mateso aliyopata Abu Dharr ilikuwa ni kwa ajili ya amri za wazi za Uthman mwenyewe. Kuthibitisha ukweli huu, anachohitaji mtu ni kurejea kwa Maulamaa wenu tu.

Kwa mfano unaweza ukaangalia “Nihaya” kitabu cha Ibn Athir, Jz.1, na kitabu chake, “Ta’rikh-e-Yaqubi” na hususan uk. 241 wa Jz. 1, ya “Sharhe Nahju’l-Balagha” cha Ibn Abi’l-Hadid. Wanachuoni hawa wameinakili barua ya Uthman iendayo kwa Mu’awiyya. Wakati Mu’awiyya alipopeleka taarida yenye uovu dhidi ya Abu Dharr kutoka Syria, Uthman alimuandikia hivi:

“Mlete Jundab (Abu Dharr) kwangu juu ya ngamia asiye na matandiko, peke yake, na mtu katili atakayemswaga ngamia huyo mchana na usiku.”

Wakati alipofika Madina, miguu yake Abu Dharr ilikuwa imechubuka na kutoa damu. Na bado Maulamaa wenu wamesimulia hadith isemayo kwamba Abu Dharr alitajwa makhususi kabisa na Mtume kama mtu ambaye kila mwanadamu lazima ampende.
Hafidh Abu Nu’aim Isfahani katika “Hilyatu’l-Auliya”, Jz. 1, uk. 172; Ibn Maja Qazwini katika “Sunan” yake Jz. 1, uk. 66; Sheikh Sulayman Balkhi Shafi’i katika “Yanabiu’l- Mawadda”, Sura ya 59, akisimulia hadithi ya tano kati ya hadith arobaini zilizoandikwa katika “Sawa’iq-Muhriqa” na Ibn Hajar Makki kama sahihi, zikiwa zimechukuliwa kutoka kwa Tirmidhi na Hakim, kama ilivyosimuliwa na Buraida, na yeye kutoka kwa baba yake; Ibn Hajar Asqalani katika “Isaba”, Jz. 3, uk. 455; Tirmidh katika “Sahihi” yake, Jz. 2, uk. 213; Ibn Abdi’l-Birr katika “Isti’ab”, Jz. 2, uk. 557; Hakim katika “Mustadrak”, Jz. 3 uk. 130; na Suyuti, katika “Jam’us-Saghir” wamesimulia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema:“Allah ameniamrisha mimi kuwapenda watu wanne; na amenijulisha kwamba Yeye pia anawapenda.” Watu wakasema “Ewe Mtume wa Allah tueleze majina yao.”

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema “Ni Ali, Abu Dharr, Miqdad, na Salman.” Je, haki itaruhusu kwamba watu kama hao wapendwao na Allah kutendewa ukatili hivyo na kuyaita matendo hayo kuwa ni huruma?

Hafidh: Historia imesimulia kwamba Abu Dharr alikuwa mtu mvurugaji. Aliendesha propaganda kali huko Syria yenye kumpendelea Ali, akawatanabahisha watu wa Syria juu ya cheo cha Ali, na akasema kwamba alikuwa amemsikia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akisema kwamba Ali alikuwa ndiye mrithi wake.

Kwa sababu aliwaita wengine wanyang’anyi na akasema kwamba Ali alikuwa Khalifa wa haki aliyeteuliwa na Allah, Khalifa Uthman, ili kulinda umoja na kuepusha matatizo, alilazimika kumuita kutoka Syria (arudi Madina). Kama mtu anajaribu kusababisha fitna miongoni mwa watu, ni jukumu la Khalifa kumuondoa kutoka sehemu hiyo.

Muombezi: Kama mtu anasema kweli, ni haki kumhamisha na kumtesa kwa sababu anafanya hivyo? Je, Uislamu unaturuhusu kumlazimisha mtu mzee kupanda ngamia aliyekonda, asiye na matandiko, ikiswagwa kwa nguvu na mtumwa mwenye harara, bila kusimama kwa ajili ya kupumzika, hivyo kwamba anawasili mashukio yake akiwa amechubuka na kuvuja damu?

Je, hii inaonyesha upole na moyo wa wema? Mbali na hilo kama Uthman alitaka kudumisha umoja na kuepusha matatizo kwa nini asiwaondoe Bani Umayya wahalifu, kama Marwan, ambaye alilaaniwa na kuhamishwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na Walid mpotovu na fuska wa dhahiri (afanyaye maovu bila kuficha) ambaye alisalisha akiwa amelewa na ambaye alitapika kwenye kibla ya msikiti? Kwa nini asiwaondoe wanasiasa madhalimu kutoka kwenye serikali yake, watu ambao wamewaonea watu, ambao mwishowe wakaasi na kumuuwa Uthman.

Hafidh: Unawezaje kusema kwamba Abu Dharr alisema kweli? Unajuaje kwamba aliyosema yako katika misingi ya elimu iliyo sawa na kwamba hakubuni hadithi kwa jina la Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)?

Muombezi: Tunasema hivyo kwa sababu Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mwenyewe alithibitisha ukweli wa Abu Dharr. Maulamaa wenu wenyewe wameandika kwamba Mtume alisema: “Abu Dharr miongoni mwa watu wangu ni kama Isa miongoni mwa Bani Isra’il katika ukweli, utii na Ucha Mungu.” Muhammad Bin Sa’d mmoja wa Maulamaa wa cheo cha juu na muhadithina wa madhehebu yenu, ndani ya “Tabaqat”, Jz. 4, uk. 167- 168; Ibn Abdu’l-Birr katika “Isti’ab”, Jz. 1, Sura ya Jundab, uk. 84; Tirmidh katika “Sahih” yake Jz. 2, uk. 221; Hakim katika “Mustadrak”, Jz. 3, uk. 342; Ibn Hajar katika “Isaba” Jz. 3, uk. 662; Muttaqi Hindi katika “Kanzu’l-Ummal”, Jz. 6, uk. 169; Imam Ahmad Bin Hanbal katika “Musnad” Jz. 2 uk.163 na 175; Ibn Abil’-Hadid katika “Sherhe Nahju’l- Balagha” Jz. 1, uk. 241; kutoka kwa Mahidi; Hafidh Abu Nu’aim Isfahani katika “Hilyatu’l-Auliya” na mwandishi wa “Lisanu’l-Arab”, juu ya vyanzo mbali mbali vya kutegemewa wamesimulia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Ardhi haikuzaa wala mbingu haikufunika mtu muaminifu zaidi kuliko Abu Dharr.”

Kama Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anathibitisha uaminifu wa mtu, tunaweza kuwa na uhakika kwamba mtu yule alisema kweli. Wala Allah hamuiti mtu mpenzi wake, yule ambaye ni muongo. Kama kungalikuwa na mfano mdogo tu wa Abu Dharr kusema uwongo, Maulamaa wa mwanzo wa madhehebu yenu wangeuandika kama walivyoandika kuhusu Abu Huraira na wengine. Mtume alithibitisha uaminifu wake na vilevile akatabiri mateso yake. Hafidh Abu Nu’aim Isfahani katika “Hilyatu’l Auliya”, Jz. 1 uk. 162, anasimulia kutoka vyanzo vyake mwenyewe kwamba Abu Dharr alisema kwamba alikuwa amesima- ma mbele ya Mtume wakati alipomuambia: “Wewe ni mcha-Mungu, mara tu baada yangu utapatwa na shida.”

Nikauliza:“Katika njia ya Allah? Akasema: “Ndio, katika njia ya Allah! Nikasema: “naikaribisha (naikubali) amri ya Allah!” Hakika shida aliyopata sahaba mtukufu Abu Dharr katika jangwa kwa amri ya Mu’awiyya, Uthman na jamaa zao Bani Umayya ilikuwa ni shida ile ile aliyotabiri Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Hadith: “Masahaba Wote Ni Kama Nyota” Inamhusu Na Abu Dharr Vilevile.

Kwa kweli nashangaa kauli zako zenye kupingana zenyewe. Kwa upande mmoja unasimulia hadith kutoka kwa Mtume kwamba, “Masahaba wangu wote ni kama nyota, kama mkimfuata yeyote miongoni mwao mtaokolewa.”

Kwa upande mwingine, wakati mmoja wa Masahaba watukufu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anateswa na kufa katika huzuni, wewe unamtetea mkosaji! Yakupasa ama upuuze maelezo ya maulamaa wenu, au ukubali sifa zilizotajwa katika aya iliyo katika mjadala kwamba hazihusiani na wale waliowatesa masahaba watukufu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Hafidh: Abu Dharr alichagua kwenda Rebza kwa hiari yake mwenyewe.

Muombezi: Maelezo kama hayo yanaakisi majaribio ya maulamaa wenu mashabiki kuficha matendo mabaya ya viongozi wao. Kuhamishwa Abu Dharr kwa nguvu kwenda Rabza kunajulikana wazi sana. Kama mfano, nitaishia kunukuu riwaya moja, ambayo imesimuliwa na Imam Ahmad Bin Hanbal katika “Musnad” Jz. 5, uk. 156, Ibn Abi’l-Hadid katika “Sharhe Nahju’l-Balagha” Jz. 1, uk. 241, na Waqid katika kitabu chake cha Ta’rikh kutoka kwa Abu’l-Aswad Du’ili.

Abu Dharr aliulizwa kuhusu Safari yake ya Rabza. Abu Dharr akasema kwamba, “ali- hamishwa kwa nguvu na kupelekwa kuishi porini”. Akaendelea: “Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alinijulisha kuhusu hili. Siku moja nililala Msikitini. Mtume akaja na akaniuliza kwa nini nimelala msikitini. Nikasema kwamba usinginzi umenipitia tu.

Akaniuliza nitafanya nini kama nitahamishwa kutoka Madina. Nikasema ningekwenda kwenye nchi takatifu ya Syria. Akaniuliza nitafanya nini kama nitahamishwa huko pia. Nikasema nitarudi msikitini.

Aliniuliza tena ningefanya nini kama ningefukuzwa kutoka hapa pia. Nikasema: Nitachomoa upanga na kupigana. Aliniuliza kama ningependa aniambie kitu ambacho kingekuwa kwa manufaa kwangu. Niliposema ‘Ndio’ yeye akaniambia: ‘Nenda sehemu yoyote watakayokupeleka!’ Hivyo nikasikiliza alivyoniambia na nikamtii.

Baada ya hivi Abu Dharr akasema, kwa Jina la Allah, wakati Uthman atakapokwenda mbele ya Allah atasimama akiwa ni mwenye dhambi kuhusiana na suala langu.’”

Upole Na Ukarimu Wa Ali Bin Abu Talib:

Kama utayachunguza mambo kwa akili huru iliyo wazi, utakubali kwamba Ali alikuwanazo sifa za huruma na upole kwa kiwango cha hali ya juu sana. Wanahistoria wote, pamo- ja na Ibn Abi’l-Hadid, wameeleza kwamba wakati Ali alipochukua Ukhalifa, aliondoa mambo mabaya na mazushi ambayo yaliingizwa ndani (ya Uislamu).

Aliwaondoa maofisa wasiomjua Mungu wa Ki-Bani Umayya, ambao waliyakandamiza majimbo wakati wa kipindi cha Ukhalifa wa Uthman.

Wanasiasa wachoyo walimshauri aahirishe uamuzi wake huo wa kuwondoa maofisa hao mpaka Ali atakapojiimarisha zaidi katika mamlaka. Mtukufu Imam akasema: “Naapa kwa Jina la Allah kwamba sitaruhusu hila za kijanja kama hizo.

Mnasisitiza kwamba nitumie njia za upatanisho, lakini hamjui kwamba jinsi wanavyoendelea kubakia katika mamlaka wakiniwakilisha mimi, wataendelea kutenda mabaya yale yale ya kidhalimu na ukatili ambao nitawajibika kwenye Mahakama ya haki ya Mungu. Siwezi kuruhusu udhalimu huu.”
Uondoaji wa maofisa uliofanywa na Ali ulipelekea uhasama kwa watu wenye uchu wa madaraka, kama Mu’awiyya, na wakaitayarisha njia ya vita vya Jamal na Siffin. Kama Talha na Zubair wangechaguliwa kama magavana, wasingelichochea ghasia kule Basra na kuacha vita vya Jamal kutokea.

Upole na ukarimu wake ulienea sawasawa kwa marafiki na maadui. Uthman alikuwa katili sana kwake (zaidi kuliko alivyokuwa Abu Bakr na Umar), lakini waasi walipolazimisha kizuizi kwenye Ikulu ya Uthman, wakizuia maji na chakula, aliomba msaada kwa Ali. Ali aliwatuma watoto wake, Hasan na Husein, wakiwa na mikate na maji.

Ibn Abi’l-Hadid anaelezea tukio hili kwa kina katika Sharhe “Nahju’l- Balagha.” Khalifa Uthman alikuwa na sifa ya kutoa Sadaka na kusaidia wengine, lakini ilikuwa kwa jamaa zake tu, kama Abu Sufyani, Hakam Bin Abi’l-As na Murwan Bin Hakam. Aliwamwagia pesa na zawadi kutoka hazina ya Umma bila kibali cha kidini.

Lakini Amirul-Mu’minina Ali kamwe hakutoa zaidi ya kilichostahiki, hata kwa jamaa zake wa karibu. Kaka yake mkubwa, Aqil, alikuja kwake na kutaka pesa zaidi kuliko kawaida ya alivyokuwa akipewa.

Ali hakusikiliza ombi lake. Aqil alisisitiza na akasema kwamba kwa vile Ali alikuwa Khalifa na alikuwa na mamlaka kamiki juu ya mambo inapasa haja zake zitekelezwe. Kama onyo kwa kaka yake, Ali akapasha moto kipande cha chuma kwa siri na akakiweka karibu na mwili wa Aqil. Alipiga kelele kama mtu aliye katika maumivu makali, akiogopa kuwa ataungua.

Ali akasema: “Wacha waombolezaji waomboleze kifo chako, ewe Aqil! Ulinywea wakati chuma kilichopashwa moto na mwanadamu kiliposogazwa karibu yako, na bado unanisogeza mimi kunielekeza kwenye moto ambao Allah ameumba kwa ghadhabu yake. Je, ni sawa wewe utafute hifadhi kutokana na maumivu haya ya kawaida, na kwamba mimi nisijihifadhi mwenyewe na
Moto wa Jehanamu?”

Upole Wa Ali Kwa Marwan Na Abdullah Bin Zubair:

Hata baada ya kuwashinda maadui zake, Ali bado alikuwa mpole kwao. Mlaaniwa Marwan, mtoto wa mlaaniwa Hakum alikuwa ni adui muovu wa Ali. Lakini Ali alipomshinda Marwan katika vita ya Jamal, alimsamehe. Abdullah Bin Zubair alikuwa ni adui mwingine muovu.

Alimtukana Ali wazi wazi, na Abdullah aliposoma Khutuba yake kule Basra mbele za watu, alisema: “Hakika Ali Bin Abu Talib ni fisadi, duni, na bahili.” (Allah atuepushie mbali). Lakini Mtukufu Imam aliposhinda vita vya Jamal na mtu huyu muovu alipoletwa kama mateka mbele yake, Ali hakusema hata neno kali dhidi yake. Ali alimgeuzia kando uso wake na akamsamehe.

Upole Wa Ali Kwa Aisha

Mfano mzuri wa huruma ya Ali ulikuwa ni mwenendo wake kwa Aisha. Jinsi alivyokuja uso kwa uso kupigana naye na kumshutumu kungemkasirisha mtu duni. Lakini Ali alipomshinda, alimshughulikia kwa heshima. Alimpa Muhammad bin Abu Bakr, kaka yake Aisha, jukumu la kuangalia ustawi wake. Kwa maagizo yake, wanawake ishirini wenye nguvu waliovaa kama wanaume walimsindikiza Aisha mpaka Madina. Alipofika Madina, alielezea shukurani zake kwa wanawake hao na wake za Mtume.

Alisema kwamba siku zote atabakia mwenye shukurani kwake. Alikiri kwamba, ingawa alikuwa katili kwake na alikuwa amehusika na ghasia kiasi hicho, hakusema neno lolote baya dhidi yake.

Alisema alikuwa na lalamiko moja tu dhidi yake. Alishangaa kwa nini alimsafirisha kwenda Madina huku akisindikizwa na wanaume. Wanawake wale vijakazi mara moja walivua mavazi yao ya kiume. Ikajulikana wazi kwamba mpango huu ulifanywa kwa madhumuni ya kulinda mali zao kutokana na majambazi.

Mfano mwingine wa huruma za Ali ni jinsi alivyomshughulikia Mu’awiyah katika vita vya Siffin. Jeshi la askari 12,000 la Mu’awiyah liliufunga mto wa Euphrate.
Wakati jeshi la Ali lilipoona kwamba njia waliyokuwa wanaitegemea ya kupatia maji ilikuwa imeshikwa, Ali alituma ujumbe kwa Mu’awiyah akisema kwamba Mu’awiyah hapaswi kufunga njia ya kufikia maji. Mu’awiyah alijibu kwamba atawanyima kutumia maji.

Ali akamtuma Malik Ashtar na kikosi cha askari. Alisukuma nyuma jeshi la Mu’awiyah na kuifungua njia ya kuufikia mto Euphrate. Masahaba wakasema: “Ewe Ali! Na sisi tulipize na tuwanyime maji, ili kwamba maadui wafe kwa kiu na vita vitakuwa vimekwisha.” Ali akasema: “Hapana! Kwa jina la Allah, sitalipiza kwa kufuata mfano wao. Waacheni askari wao wapate njia ya kufikia mto Euphrate.”

Maulamaa wenu wenyewe, kama Tabari katika kitabu chake “Ta’rikh”, Ibn Abi‘l-Hadid katika “Sharhe Nahju‘l-Blagha”, Suleimani Balkhi katika “Yanabiu‘l-Mawadda”, Sura ya 15, Mas‘udi katika “Murju‘dh-Dhahab”, na wanahistoria wengine wameandika kwa urefu kuhusu uugwana wa Ali. Unaweza ukachunguza maelezo haya na kisha ukaamua ni nani anayeelekea kulengwa na aya hii: “Na wakahurumiana wenyewe kwa wenyewe…” Katika aya iliyoko kwenye mjadala, Muhammad, Mtume wa Allah, ndiye mlengwa na kinacho fuatilia ni arifu yake.

Sifa zote zile ni kwa ajili ya mtu huyo huyo. Kuwa pamoja na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), kuwa mkali dhidi ya makafiri katika medani ya vita na katika mijadala ya kielimu, kuwa na huruma kwa marafiki na maadui – sifa zote hizi hurejea kwa mtu ambaye kamwe hajamuacha Mtume au hata kufikiria kumuacha.

Mtu huyo ni Ali Bin Abi Talib. Nilikwisha sema mapema kwamba, mwanachuo mkubwa, Muhammad bin Yusuf Ganji Shafi‘i ameandika katika kitabu chake “Kifayatu‘t-Talib” kwamba katika ayah ii Allah anamsifia ‘Ali.

Sheikh: Kuna majibu mengi kwa maelezo yako, lakini umetafsri tu visivyo aya hii. Usemi “na wale ambao wako pamoja naye” ni wa wingi na hauwezi kuonyesha mtu mmoja tu. Kama sifa zilizotajwa katika aya zinamuonyesha mtu mmoja tu, kwanini vijina vikawa kwa wingi?

Muombezi: Kwanza, unasema kwamba kuna majibu mengi kwa maelezo yangu. Kama hiyo ilikuwa kweli, basi kwa nini usiyataje? Kunyamaza kwako ni uthibitisho kwamba hakuna “mjibu mengi” kwa maelezo yangu. Pili, ulichosema hivi punde tu ni hoja potofu.

Unajua kwamba katika luhga zote ikiwemo Kiarabu utumiaji wa wingi kwa ajili ya mmoja ni kitu cha kawaida kama dalili ya heshima. Kuna mifano mingi ya utumiaji huu katika Qur’ani Tukufu kama aya hii: “Hakika walii wenu ni Allah na Mtume wake na walio amini ambao husimamisha Salat na hutoa zaka na huku wamerukuu.” (5:55) Inakubaliwa na wote kwamba aya hii imeshuka kwa ajili ya Ali.

Wafasiri na muhadithina, kam vile Imamu Fakhru‘d-Din Razi katika “Tafsir Kabir”, juzuu ya 3, uk. 431; Imamu Abu Ishaq Tha‘labi katika kitabu chake “Kashfu ‘l-Bayan”; Jarullah Zamakhshari katika “Tafsir Kashshaf”, juzuu ya 1, uk. 422; Tabari katika “Tafsir” yake, juzuu 6, uk. 186; Abu‘l-Hasan Rammani katika “Tafsir” yake; Ibn Hawazin Nishapuri katika “Tafsir” yake; Ibn Sa‘dun Qartabi kati- ka “Tafsir” yake, juzuu ya 6, uk. 221; Nasafi Hafiz katika “Tafsir” yake, uk.496 (kwa njia ya ufafanuzi kwenye Tafsir ya Khazin Bahgdadi); Fazil Nishapuri katika “Gharibu‘l-Qur’ani”, juzuu ya 1, uk.461; Abu‘l-Hasan Wahidi katika “Asbabu’n-Nuzul”, uk. 148; Hafiz Jassas katika “Tafsir Ahkamu’l-Qur’ani,” uk. 542; Hafiz Abu Bakr Shirazi katika “Fima Nazala Mina’l-Qur’ani Fi Amiru’l-mu’minin”; Abu Yusuf Abdu’s-Salam Qazwini katika “Tafsir Kabir”; Kadhi Baidhawi katika “Anwart-Tanzil”, juzuu ya 1, uk. 345; Jalalu’d-Din Suyiti katika “Durr’l-Mansur”, juzuu ya 2, uk. 239; Kadhi Shukani San’a’i katika “Tafsir Fathu’l-Qadir”; Sayyid Muhammad Alusi katika “Tafsir” yake, juzuu ya 2, uk. 329; Hafiz Ibn Abi Shaiba Kufi katika “Tafsir” yake; Abu’l-Baraka katika “Tafsir” yake, juzuu ya 1, uk. 496; Hafiz Baghawi katika katika “Ma’alimut-Tanzil”; Imamu Abu Abdu’r-Rahman Nisa’i katika “Sahih” yake.

Muhammad bin Talha Shafi’i katika “Matalibus-Su’ul”, uk. 31; Ibn Abi’l-Hadid katika “Sharhe Nahju’l-Balagha”, juzuu ya 3, uk. 375; Khazin Ala’u’d-Din Baghdadi katika “Tafsir” yake, juzuu ya 1, uk. 496; Suleimani Hanafi katika “Yanabiu’l-Mawadda”, uk. 212; Hafiz Abu Bakr Baihaqi katika “Kitab Musnnaf”;

Razin Abdari katika “Jam’Bainus- Siha Sitta”; Ibn Asakir Damishiq katika “Ta’rikh Sham”; Sibt Ibn Jauzi katika “Tadhkira”, uk. 9; Kadhi Azuda’ili katika “Mawaqif”; uk.276; Sayyid Sharif Jurjani katika “Sharhe Mawaqif”; Ibn Sabbagh Malik katika “Fusu’l-Muhimma”, uk. 123; Hafiz Abu Sa’d Sam’ani katika “Fadha’ils-Sahaba”; Abu Ja’far Askafi katika “Nagzi’l-Uthmaniyya”; Tibrani katika “Ausat”; Ibn Maghazili Faqih Shafi’i katika “Manaqib”; Muhammad bin Yusuf Ganji Shafi’i katika “Kifayatut-Talib”; Mulla Ali Qushachi katika “Sharhe Tajrid”; Sayyid Muhammad Mu’min Shablanji katika “Nuru’l-Absar”, uk. 77; Muhibu’d-Din Tabari katika “Riyazu’n-Nuzra”, juzuu ya 2, uk. 247, halikadhalika na wengine wengi miongoni mwa wanachuoni wenu maarufu, wote wamesimesimulia kutoka kwa Said, Mujahid Hasan Basri, A’mash, Atba Bin Hakim, Ghalib Ibn Abdullah, Qais Bin Rabi’a, Abaya Bin Rab’i , Abdullah Ibn Abbas, Abu Dharr Ghifari, Jabir Ibn Abdullah Ansari, Ammar, Abu Rafi, na Abdullah Bin Salam, na wengine wanakiri kwamba aya hii iliteremshwa katika kumsifia Ali.

Aya hii inaashiria kwenye wakati ambao Ali alitoa pete yake kumpa muombaji wakati akiwa kwenye rukuu. Hapa vile vile maneno yapo katika wingi kwa staha na heshima juu ya cheo cha Wilaya (walii), na kuthibitisha kwamba Ali alikuwa Imamu na mrithi wa Mtume (s.a.a.w.).

Msisitizo wa neno “In’nama”, hutoa maana ya – uamuzi wa Allah – wa mwisho na uliopangwa, yaani, uamuzi wa Allah kwamba Walii wa waumini lazima awe ni Allah, Mtume Wake (Muhammad), na waumini ambao hutoa sadaka huku wakiwa wanasali, huyu wa mwisho akiashiriwa bayana kuwa ni Ali.

Sheihk: Hakika utakubali kwamba tafsiri yako haikuthubutu kwa vile kuna maoni tofauti kuhusu hilo. Baadhi wanasema huashiria kwa Ansar, baadhi wanasema ni katika kumsifia Ibadat Bin Samit, na baadhi wanasema kwamba inaashiria kwa Abdullah Bin Salam.

Muombezi: Kwa hakika inashangaza kwamba mwanachuo kama wewe unaweza kupingana na ulamaa wako mwenyewe. Unachukua maoni ya wajinga wachache na wasioaminika ambao riwaya zao zinakataliwa. Wanachuoni wenu wakubwa kwa pamoja wametamka kwa dhati kuthibitisha juu ya nukta hii, watu kama Fazil Taftazani na Mulla Ali Qushachi, ambaye anasema katika kitabu chake, Sharhe Tajrid:

“Kwa mujibu wa maoni ya pamoja ya wafasiri, aya hii iliteremshwa katika kumsifia Ali, ambaye wakati akiwa kwenye rukuu katika Sala, alitoa pete yake kumpa muombaji.”

Mashaka Na Utata Kuhusu “Aya Ya Walii” Na Ufafanuzi Wake

Sheikh: Katika mlolongo wa mazungumzo yako kuhusiana na aya hii, umejaribu kuthibisha kwamba Ali alikuwa ndiye mrithi wa mara moja wa Mtume (s.a.w.w.), ingawa neno “Wali” katika aya hii lina maana ya “rafiki” au “mwenye kupendwa sana”, na sio “Imamu” au “Mrithi.” Kama maoni yako ni yenye kukubalika kwamba “Wali” maana yake ni “mrithi” na “Imamu”, basi kwa mujibu wa kanuni iliyokubaliwa, haikomei kwa mtu mmoja, bali wengine wanakuwemo pia, Ali akiwa mmoja mionmgoni mwao.

Vile vile katika aya, “Hakika walii wenu ni Allah, na Mtume Wake, na wale ambao wameamini…” utumiaji wa (sarufi) wingi huonyesha watu kwa ujumla. Kusema kwamba muundo wa wengi ni kuonyesha heshima, haina maana bila hoja yenye nguvu, mfano wa ki-Qur’ani, au chanzo kingine.

Muombezi: Umeulewa vibaya msemo “…Walii wenu…” “Wali” ni (sarufi ya) umoja, “kum” (wenu) ni wingi ambao huashiria kwa watu na haioneshi umoja. Naam hakika, “Wali” ni kwa ajili ya mtu ambaye ni mlezi kwa jamii nzima katika zama zote. Pili, katika aya ambayo iko kwenye mjadala, pale ambapo wingi umetumika, baadhi ya mashabiki wamesema kwamba haiwezi kutafsiriwa kama umoja kama katika aya “…wale ambao wanasimamisha Sala…” pingamizi hili nililijibu mapema.

Nilisema kwamba, waandishi wakubwa mara nyingi wametumia umoja kumaanisha wingi. Vile vile umedai kwamba muundo wa (sarufi ya) umoja katika aya hii huashiria watu kwa ujumla. Tunasema kwamba, kwa mujibu wa msisitizo wa neno “hakika”, anayeashiriwa ni Ali, lakini hatukusema kwamba kuhusika huko ni kwa aina ya pekee tu kwake.

Wengine kutoka nyumba ya Mtume wanakuwemo pia. Kwa mujibu wa hadithi zilizo sahihi, Maimamu wote wa kizazi cha Mtume wamejumuishwa katika aya hii. Jarullah Zamakhshari anaandika katika “Kashshaf” kwamba aya hii iliteremshwa makhususi katika kumsifia Ali, lakini ule wingi uliotumika ndani yake, unamaanisha kwamba wengine lazima wamfuate.

Sheikh: Katika aya hii neno “Wali” haswa lina maana ya “msaidizi.” Kama lingekuwa na maana ya “mlezi” ambayo hujumuisha na cheo cha mrithi, basi angeliteuliwa wakati wa uhai wa Mtume (s.a.w.w.).

Muombezi: Cheo cha Ali ni cha kudumu. Ujengaji wa sentensi kisarufi na neno “Wali” uliotumika kama sifa, huthibitisha cheo cha kudumu cha Ali. Ukweli huu unaungwa mkono zaidi na Mtume kwa kumtangaza Ali kama makamu wake wakati wa safari ya Tabuk na kamwe hakulifuta tangazo hilo.

Mtazamo wetu unaimarishwa zaidi na Hadith-e-Manzila (Hadithi ya cheo) ambayo Mtukufu Mtume amerudia mara nyingi kuisimulia: “Ali kwangu mimi ni kama Harun alivyokuwa kwa Musa,” ambayo nimeilezea katika mikesha iliyopita. Hii yenyewe ni uthibitisho mwingine kwa Ali wa kuwa kwake Walii au Makamu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wakati wa uhai wa Mtume na baada ya kufa kwake.

Sheikh: Kama ingekuwa tulipe suala hili mazingatio yanayostahili, tungelikiri kwamba aya hii haimzungumzii Ali. Cheo chake ni kikubwa kuliko kile tunavyotaka kukithibitsha kutoka kwenye aya hii. Haithibitishi ubora wowote juu yake, bali hukiangusha chini cheo chake.

Muombezi: Sio wewe wala mimi – si yeyote katika Umma – pamoja na wale masahaba wakubwa wa Mtume, ambaye ana haki yoyote ya kuingilia tafsiri halisi za aya hizi. Aya za Qur’ani hazikuteremshwa kwa mujibu wa matakwa yetu. Kama baadhi ya watu wakitafsiri maana zao kwa kuegemeza juu ya maoni yao au wakataja tukio au habari ambayo imeteremshiwa, basi kwa hakika hao sio watu wa dini.

Kwa mfano, wafuasi wa Abu Bakr wanasema kwamba kwa mujibu wa hadithi iliyosimuliwa na mghushaji mkorofi Akrama, aya hii iliteremshwa kwa ajili ya Abu Bakr. Unaweza ukatueleza ni jinsi gani aya hii inavyoangusha cheo cha Ali?

Sheikh: Moja ya tabia za murwa wa cheo cha Ali ni kwamba, wakati anaposali kamwe hageuzi hadhari yake kwenye kitu kingine. Wakati fulani Ali alijeruhiwa katika vita. Kiwembe cha mshale kilibakia mwilini, na ilikuwa haiwezikani kukiondoa bila kusababisha maumivu makali. Lakini aliposimama kwa ajili sala, kiwembe cha mshale kiliondolewa, na kwa sababu ya kuzama katika ibada yake kwa Allah, hakusikia maumivu. Kama wakati wa kusali alitoa pete yake kumpa muombaji, kulikuwa na dosari kubwa kati- ka Sala yake.

Itaezakana vipi mtu ambaye amezama katika rehema ya Allah na wakati huo huo andoe hadhari yake kutoka kwa Allah kwa ajili ya kuitikia sauti ya omba omba? Aidha, katika kutenda kila jambo jema na kutoa sadaka kuweka nia ni kitu cha lazima. Wakati wa kusali hadhari ya mtu lazima iwe imeelekea kwa Allah peke Yake.

Inawezekana vipi kwamba nia yake imegeuka kutoka kwenye Sala na kugeuka kumuelekea kiumbe? Kwa vile tunakiona cheo cha Ali kuwa ni cha juu sana, hatukubali tafsiri yako.

Na kama alitoa chochote kwa omba omba, basi kwa hakika haikuwa wakati wa Sala, kwa vile rukuu maana yake ni kunyenyekea mbele ya Allah.

Muombezi: Umejifunza vizuri jinsi ya kusoma, lakini umeikosa njia ya kuendea kwenye maombi. Pingamizi hili ni dhaifu kuliko hata utando wa buibui. Kwanza, kitendo cha Ali kwa njia yoyote hakiangushi chini cheo chake. Kwa hakika kumsikiliza omba omba ili kumpa sadaka, ni chanzo cha ubora.

Katika hali hii, alikusanya sala yake ya kimwili na ya kiroho pamoja na sala ya kiyakinifu. Sala zote zilikuwa katika njia ya Allah. Ndugu wapenzi! Uharibifu ambao unanyongesha Sala ni ule ambao unatokana na fikra binafsi.

Kuzingatia sala nyingine, wakati ambapo unasali Sala mahususi, ni dalili ya ubora. Kwa mfano, kama wakati wa ibada ya Sala, mtu akalia kwa mapenzi makubwa ya jamaa zake, Sala yake itakuwa batili. Lakini kama akilia kwa mapenzi makubwa ya Allah, au kwa kumuogopa Yeye, basi hiyo ni dalili ya ubora. Umesema kurukuu maana yake ni kunyenyekea kwa unyofu kwa Allah. Maana hii inaweza ikatumika kwa matukio mengine.

Lakini kama ukisema kwamba kurukuu katika Sala, ambako ni hakika na lazima, kunabeba maana hiyo hiyo ya kilugha, watu wasomi watakudharau. Vile vile umejaribu kuondoa au kupuuza maana ya wazi ya aya. Umeitolea maana ya kistiari, ingawa unajua kwamba neno hilo huelezea kitendo kinachohitajika cha ibada ya Sala, ambacho ni kuinama mpaka viganja kufikia magoti. Na ukweli huu umekubaliwa na maulamaa wenu wakubwa, kama nilivyoelezea mapema.

Fadhil Qushachi, katika Sharhe Tjrid, anaelezea maoni ya wafasiri kwa ujumla kwamba Ali, wakati anarukuu katika Sala, alitoa pete yake kumpa omba omba. Tukiweka kila kitu pem- beni, tafadhali tueleze iwapo aya hii ilitaremshwa kwa kusifu au kwa kulaumu?

Sheikh: Ni wazi ilikuwa kwa kusifia.

Muombezi: Hivyo wakati maulamaa wa madhehebu zote wamesema kwamba aya hii iliteremshwa kwa kumsifia Ali, na kwamba ina ridhaa ya Allah (swt), kwa nini ulete ukinzani usio na maana, ukubaliane na Makhawariji washabiki, ambao maoni yao yameduk- izwa kwenye akili yako safi tangu utotoni? Kwa nini hukubali ukweli huu?

Sheikh: Samahani! Kwa vile wewe ni mzungumzaji fasaha, mara nyingi unatumia vidokezo na rejea ambazo zinaweza kujenga mawazo ambayo yanaweza kuleta matokeo yasiyofurahisha katika akili za watu ambao hawana elimu ya kutosha juu ya masuala haya. Ingekuwa vyema kama ungejizuia kutokana na lugha kama hizo.

Muombezi: Katika mazungumzo yangu hakuna chochote ila ukweli. Allah awe shahidi wangu, kamwe sijakusudia kutumia madokezo au rejea zisizo za moja kwa moja. Hakuna haja ya kufanya hilo. Chochote ninachotaka kusema, nakisema kwa wazi. Tafadhali nieleze ni vidokezo gani unavyomaanisha.

Sheikh: Muda mfupi uliopita wakati wa mazungumzo yako kuhusiana na aya iliyoko kwenye mjadala, ulisema kwamba sifa zilizotajwa ndani yake ni za kipekee kwa Ali Bin Abu Talib ambaye kuanzia mwanzo mpaka mwisho wa uhai wake, kamwe hajawa na shaka katika imani yake. Kwa namna hii unaonesha kwamba wengine walikuwa na hatia ya ukana mungu.

Je, wale makhalifa wakubwa au masahaba kuna yeyote aliyekuwa na shaka katika imani zao? Bila shaka hao masahaba, kama alivyokuwa Ali, kamwe hawajautilia shaka ukweli wa Uislamu. Hata mara moja hawajakengeuka katika mafindisho ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Muombezi: Kwanza, kamwe sijatumia maneno ambayo wewe umeyatumia sasa hivi. Pili, unaelewa kwamba kuthibitisha kitu kwa mtu fulani haina maana ya kutothibitisha kitu hicho kwa watu wengine. Tatu, ingawa unajaribu kunikosoa, nafikiri wengine hawana kitu kama hicho katika akili zao.

Allah awe shahidi wangu, sikufanya rejea yoyote isiyo ya moja kwa moja kwa kitu chochote, wala sijafikiria kufanya hivyo. Na kama kitu chochote kilitokea kwenye akili yako, ungeweza kuniuliza kuhusu kitu hicho kwa faragha.

Sheikh: Namna ya uzungumzaji wako huonyesha kwamba kuna nukta fulani ambazo unazinyamazia. Nakuomba utufahamishe kilichoko akilini mwako na kutupa rejea sahihi kwa unachosema.

Muombezi: Ni wewe uliyejenga kitu hicho akilini mwetu; unasisitiza kwamba suala hili lijadiliwe. Nakuomba tena, liache suala hili na uache kusisitiza juu yake.

Sheikh: Kama kulikuwa na kitu chochote cha usafihi, imekwisha. Sasa huna jinsi ila kujibu. Kama hutatoa jibu la wazi, ima la kukubali au kukataa, basi nitawajibika kuamua kwamba uliyoyasema yalikuwa hayana msingi wowote.

Muombezi: Hakuna chochote cha usafihi katika maelezo yangu, lakini kwa vile unasisitiza, sina jinsi isipokuwa kuufichua ukweli. Ulamaa wenu wakubwa wanakubali kwamba masahaba wa Mtume ambao imani yao ilikuwa bado haijakamilika, mara kwa mara walionyesha kuwa na mashaka. Baadhi yao walilea shaka hiyo na uasi wa kidini. Baadhi ya aya ziliteremshwa kwa ajili ya kuwalaumu.

Kwa mfano, walikuwepo munafiqin (wanafiki) ambao katika kulaumiwa kwao Sura nzima ya Qur’ani Tukufu iliteremshwa. Lakini masuala kama hayo hayapaswi kujadiliwa waziwazi. Nakuomba tena ujizuiye kuindama nukta hii.
Sheikh: Una maana kwamba wale makhalifa wakubwa walikuwa ni miongoni mwa wale waliokuwa na mashaka.

Muombezi: Kama majibu yangu yatasababisha hisia mbaya miogoni mwa watu wasio na elimu, wewe ndiye utakayebeba lawama. Umesema sasa hivi, “Useme hivi au umesema kwamba.” Lakini tena, ni maulamaa wenu wenyewe ndio ambao wamesimulia mambo haya.

Sheikh: Wameandika kuhusu suala gani, na ni katika tukio gani makhalifa wameonesha shaka yao, na ni watu gani ambao walitia shaka? Tafadhali tujulishe.

Muombezi: Watu wengi walikuwa na shaka kubwa sana, lakini wakarudi kwenye imani yao ya asili. Baadhi yao wakang’ang’ania katika shaka zao. Ibn Maghazili Shafi’i, katika kitabu chake “Manaqib,” na Hafidh Abu Abdullah Muhammad Bin Abi Nasir Hamidi katika “Jam’Bainus-Sahihain-e-Bukhari”, na Muslim wanaandika: “Umar Bin Khattab alisema,‘Sijapata kuutilia mashaka utume wa Muhammad kama nilivyofanya siku ya Hudaibiyya.’” Maelezo haya yanaonyesha kwamba aliutilia shaka utume wa Muhammad zaidi ya mara moja.

Nawab: Samahani. Ni tukio gani katika Hudaibiyya ambalo lilimfanya awe na shaka kuhusu Mtume?

Muombezi: Mtume aliona usiku mmoja kwenye ndoto kwamba alikwenda Makka pamoja na mashaba zake kufanya Umra. Asubuhi yake, aliposimulia ndoto hii kwa masahaba zake, walimuomba aitafsiri ndoto hiyo. Mtume akasema, “Mwenyezi Mungu akipenda tutakwenda Makka kuitekeleza ibada hii Insha’allah.” Lakini hakuainisha ni wakati gani itafanyika.

Akiwa na nia ya kuizuru Nyumba ya Allah, Mtume aliondoka na masahaba zake kuelekea Makka katika mwaka ule ule.

Wakati walipofika Hudaibiyya (kisima kilicho karibu na Makka), Maquraishi walikuja pale na kuwazuia wasiendelee mbele. Kwa vile Mtume hakuenda kule akiwa amejiandaa kupigana, alijitolea kufanya amani nao.

Mkataba ulisainiwa na Mtume akarudi Madina. Katika tukio hili, Umar alikuwa na mashaka. Alikwedna kwa Mtume na akasema: “Je, wewe sio Mtume wa Allah na mtu mkweli? Je, wewe hukutuambia kwamba utakwenda Makka na kufanya Umra kisha unyoe kichwa chako na upunguza ndevu zako? Kwa nini sasa umeshindwa kufanya hivi?”

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimuuliza iwapo yeye aliweka muda kwa ajili ya hilo au kama aliwaambia kwamba atakwenda kule katika mwaka ule ule. Umar akakiri kwamba Mtume hakuainisha wakati. Mtume akasema kwamba alichowaambia ni sahihi, na Mungu akipenda watakwenda Makka siku zijazo na ndoto yake itatimizwa.

Hakika wakati kwa ajili ya utekelezaji wa tafsiri ya ndoto, uwe mapema au baadae utetagemea juu ya utashi wa Allah (swt). Kisha kwa uthibitisho wa maelezo ya Mtume, Jibril alijitokeza na kuteremsha aya ifuatayo ya Qur’n Tukufu:

“Hakika Allah amemtimizia Mtume Wake ndoto kwa haki. Bila shaka ninyi mtauingia Msikiti Mtukufu, insha-Allah kwa amani, na hali mmenyoa vichwa vyenu na (baadhi) mmepunguza nywele. Hamtakuwa na hofu. Yeye anajua msiyoyajua. Basi atakupeni kabla ya haya ushindi karibuni.” 48:27.

Ushindi hapa una maana ya ushindi wa Khaibar. Hii ilikuwa kwa ufupi tukio la Hudaibiyya ambalo kwa kweli lilikuwa ni mtihani kwa waumini na kwa watu wanaoyumba.

Kufikia hapa ulifuatia mjadala wa iwapo tuendelee na mjadala au la, kwa ajili ya ratiba ya wageni wa ki-Sunni kutoka Afghanistan na halikadhalika na Muombezi, matokeo yake ambayo ilikuwa ni uamuzi wa kuendelea.