read

Mkutano Wa Tano; Jumanne Usiku 27 Rajab 1345, A.H.

Hafidh: Kutoka kwenye mazungumzo yako fasaha ya usiku uliopita ninahitimisha kwamba ulitaka kuthibitisha kwamba Ali alikuwa ndiye mrithi anayefuatia mara moja wa Mtume, ingawa ukweli ni kwamba hadith hii ina maana makhususi tu. Ilisimuliwa wakati wa safari ya Tabuk. Hakuna uthibitisho kwamba ina maana ya jumla.

Muombezi: Katika Hadith hii neno “Manzila” (Cheo) linatumika katika maana ya jumla. Neno hili kwa kuonyesha upekee, huthibitsha kwa uwazi kwamba maelekezo ni ya maana ya jumla. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimtaja Ali sambamba na neno “Mtume” na akaelezea Manzila yake (Yaani cheo chake) akitumia usemi, “isipokuwa kwamba haku- takuwa na Mtume baada yangu.”

Maulamaa wengi wakubwa na waandishi wamenukuu hadith hii hii kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), ambaye inasemekana alimuambia Ali: “Je, huridhiki kwamba kwangu wewe ni kama Harun alivyokuwa kwa Musa isipokuwa kwamba hakutakuwa na Mtume baada yangu?”

Muda wa kutokuepo kwake kwa siku arobaini, Musa hakuacha mambo katika uamuzi wa wafuasi wake. Alimchagua Harun, mtu bora miongoni mwa Bani-Israil kukaimu kama Khalifa wake na mrithi. Vivyo hivyo, Mtume wa mwisho, ambaye dini yake ni kamili zaidi, alikuwa na sababu kubwa zaidi za kuwalinda watu wake kutokana na machafuko ya dhamira zao huru.

Alihifadhi Sheria ya dini ili kwamba isije ikapitia katika mikono ya watu wasio na ujuzi, wale ambao wangeweza kuigeuza kwa mujibu wa matamanio yao. Watu wasio na ujuzi wangetegemea juu ya kukisia kwao na kusababisha migawanyiko katika mambo ya Sheria.

Hivyo, katika hadith hii tukufu Mtume anasema “Ali yuko kwangu mimi kama alivyokuwa Harun kwa Musa,” akithibitisha kwamba Ali alishikilia viwango vile vile vya daraja na mamlaka, sawa kama Harun alivyokuwa. Ali alikuwa bora kwa Umma wote na kwa ajili hiyo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akamchagua kuwa msaidizi wake na mrithi wake.

Hafidh: Uliyosema kuhusu Hadith hii hayana ubishani. Lakini kama utaangalia jambo hili kwa uangalifu, utakubali kwamba hadith hii haina maana ya jumla. Maana yake imekomea kwenye Vita vya Tabuk wakati Mtume alipomteua Ali kuwa Khalifa wake kwa muda maalum.

Hadith Ya Manzila Imesimuliwa Mara Nyingi:

Muombezi: Ungeweza kuwa ni mwenye haki katika maneno yako kama hadith hii inges- imuliwa wakati wa vita vya Tabuk tu. Lakini Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliirudia hadith hii katika sehemu tofauti. Ilisimuliwa wakati undugu miongoni mwa watu tofauti katika Muhajirina (wahamiaji) ulipoanzishwa katika mji wa Makka. Ilisimuliwa vilevile katika mji wa Madina wakati undugu ulipoanzishwa kati ya Muhajirina na Ansar.

Katika nyakati zote Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimchagua Ali kama ndugu yake, akisema, “Wewe kwangu mimi ni kama alivyokuwa Harun kwa Musa isipokuwa kwamba hakutakuwa na Mtume baada yangu.”

Hafidh: Kadiri nilivyochunguza mimi, hadith ya Manzila ilisimulwa wakati wa vita vya Tabuk tu. Mtume alimuacha Ali katika nafasi yake hali iliyofanya Ali kuhuzunika. Mtume akamliwaza kwa maneno haya. Nafikiri umepotoshwa.

Muombezi: Hapana, mimi sijakosea. Vitabu vyenu wenyewe vya Sahih vimeisimulia Hadith hii. Miongoni mwao ni Mas’ud (Mwandishi wa kutegemewa kwa mujibu wa mad- hehebu zote) ambaye ameandika katika “Muruju’dh-Dhahab”, Jz. 2, uk. 49; Halabi katika “Siratu’l-Halabiyya”, Jz. 2, uk. 26 na 120, Imam Abdu’r-Rahman Nisa’i katika “Khasa’isu’l-Alawiyya”, uk. 19, Sibt Ibn Jauzi katika “Tadhkira”, uk. 13-14, Sulaiman Balkhi Hanafi katika “Yanabiu’l-Mawadda, Sura ya 9 na 17, na vingine vingi vimesimulia hadith hii.

Wote wanasema kwamba, “Mbali na sehemu mbili za kuanzisha undugu (Makka na Madina kati ya Masahaba) imesimuliwa pia katika sehemu nyingine nyingi.

Kwa hiyo, hadith hii sio ya kutafsiriwa katika maana ya kukomea yenye mipaka au kwa tukio moja makhususi tu. Maana yake ya jumla ni jambo lililothubutu. Ni kupitia Hadithi hii ambapo Mtukufu Mtume alitangaza katika matukio yanayostahili umakamu wa Ali baada yake. Moja ya matukio hayo lilikuwa lile la vita ya Tabuk.

Hafidh: Inawezekana vipi Masahaba wa Mtume waliisikia Hadith hii katika maana yake ya jumla, wakijua kwamba ilikuwa na maana ya kwamba umakamu wa Ali uliridhiwa na Mtume na bado baada ya kifo cha Mtume, wakawa maadui na wakamkubali mtu mwingine kuwa Khalifa?

Muombezi: Nina marejeo mengi ya kuunga mkono jibu langu kwa swali lako, lakini majibu mazuri zaidi kwa wakati huu ni kuiangalia mitihani ya Harun katika hali inayqfanana kama hii hii. Qur’ani inaeleza kwamba, wakati Musa alipomteua Harun kuwa makamu wake, aliwakusanya mbele yake Bani-Israil (kwa mujibu wa baadhi ya taarifa watu 70,000 walikusanyika).

Musa alisisitiza kwamba, wakati wa kutokuwepo kwake yawapasa kumtii Harun, Khalifa na makamu wake. Kisha Musa alikwenda juu mlimani kuwa peke yake na Allah. Kabla ya mwezi kupita, Samiri alichochea fitna miongoni mwa Bani Isra’il.

Alitengeneza ndama (wa ng’ombe) wa dhahabu na Bani Israil wakiwa wamemuacha Harun, walikusanyika mbele ya msaliti Samiri katika idadi kubwa. Ilikuwa ni muda mfupi tu umepita kabla ya tukio hili, Bani Israil, hawa hawa walimsikia Musa akisema kwamba wakati wa kutokuwepo kwake Harun atakuwa Khalifa wake na kwamba yawapasa kumtii.”

Hata hivyo watu 70,000 walimfuata Samiri. Nabii Harun kwa nguvu sana alipinga kitendo hiki na kuwakataza wasijiingize katika matendo hayo ya dhambi, lakini hakuna hata mmoja aliyemsikiliza. Aya ya Sura ya A’raf inaeleza kwamba, wakati Musa aliporudi, Harun alimwambia: “Ewe mtoto wa mama yangu! Hakika watu hawa wameniona mimi mnyonge na walikuwa karibu waniuwe….” (7: 150)

Harun Alikuwa Ni Mrithi (Makamu) Wa Musa Aliyeteuliwa.

Bani Isra’il wenyewe waliyasikia maelekezo ya wazi kutoka kwa Musa, lakini Musa alipokwenda juu mlimani, Samiri akaitwaa fursa hiyo. Alitengeneza ndama wa dhahabu na kuwapoteza Bani Isra’il.

Kufanana Kwa Hali Ya Mambo Kati Ya Ali Na Harun.

Hali kadhalika, baada ya kifo cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), baadhi ya watu ambao walikuwa wamemsikia akisema kwamba Ali alikuwa ndiye mrithi wake, waligeuka dhidi ya Ali. Imam Ghazali ameelezea jambo hili katika mwanzo wa Makala yake ya nne kati- ka “Sirru’l-Alamin.” Anaeleza kwamba baadhi ya watu walirejea kwenye hali yao ya mwanzo ya ujinga.

Kwa hali hii, kuna kufanana kukubwa kati ya hali ya Harun na ile ya Ali. Kama wengi wa wanahistoria wenu wenyewe, Abu Muhammad Abdullah bin Muslim bin Qutayba Bahili Dinawari, Kadhi maarufu sana wa Dinawar, katika “Al-Imama wa Siyasa” Jz. 1, uk. 14 anasimulia kwa urefu matukio ya Saqifa.

Anasema kwamba, walitishia kuchoma nyumba ya Ali na wakamchukua mpaka Msikitini kwa mabavu na kutishia kumuua isipokuwa achukue kiapo cha utii kwao. Ali alikwenda kwenye kaburi tukufu la Mtume na akarudia maneno yale yale ya Qur’ani ambayo Harun alimwambia Musa:

قَالَ ابْنَ أُمَّ إِنَّ الْقَوْمَ اسْتَضْعَفُونِي وَكَادُوا يَقْتُلُونَنِي{150}

Yeye (Harun) akasema: Ewe Mtoto wa Mama yangu! Hakika watu hawa waliniona mimi mnyonge na walikuwa karibu waniuwe…” (7: 150).

Nawab: Wakati Umakamu wa Ali ulikuwa umethibitishwa, kwanini Mtume atumie maneno ambayo yalidokezea hiyo maana tu? Kwa nini hakutangaza wazi kwamba Ali alikuwa ndiye makamu wake, ili kwamba kusiweze kuja kutokea pingamizi lolote baada yake?

Muombezi: Nilikuambieni kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alielezea ukweli katika njia zote. Hili liko dhahiri kutoka vitabu vyenu, ambavyo vimeandika hadith nyingi mno kuhusiana na suala hili. Watu wasomi wanaelewa kwamba kidokezo ni chenye nguvu sana kuliko maelezo ya vivi hivi tu, hususan pale kidokezo hicho kikiwa chenye mzizi wa kina mno kiasi kwamba kina maana nyingi sana ndani yake”

Nawab: Umesema kwamba kuna Hadith nyingi za wazi zilizoandikwa na Maulamaa wenu zinazohusu umakamu wa Ali. Tafadhali, je unaweza kutuelezea zaidi kuhusu hili? Tunaambiwa kwamba hakuna hadith ambayo inathibitisha Umakamu wa Ali.

Muombezi: Ziko hadith nyingi zinazohusu Ukhalifa katika vitabu vyenu wenyewe vya uhakika.

Hadith Ya Karamu Ya Ndugu Na Mtume Kumchagua Ali Kama Khalifa Wake.

Kati ya hadith zote zinazohusu umakamu wa Ali, hadith ya Karamu ndiyo ya muhimu zaidi. Katika siku ambayo Mtume alitangaza Utume wake, alitangaza pia kwamba Ali alikuwa Mrithi wake. Maulamaa wa Madhehebu yenu, wakiwemo Imam Ahmad bin Hanbal, Muwaffaq bin Ahmad Khawarizmi, Abu Ja’far Muhammad bin Jarir Tabari, Ibn Abi’l-Hadid Mutazali na kundi la wengine wamesimulia kwamba wakati Aya ya 214 ya Sura ya Shu’ara: “Na waonye jamaa zako wa karibu”, (26:214) ilipoteremshwa, Mtume alikaribisha Makuraish arubaini (miongoni mwa ndugu zake), nyumbani kwa Abu Talib.

Aliweka mbele yao mguu wa mbuzi, mkate na kikombe cha maziwa.Walicheka na kusema: “Ewe Muhammad! Hukuandaa chakula chakutosha hata kwa mtu mmoja.” Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Anzeni kula kwa jina la Allah.” Wakati walipokula na wakawa wameshiba vya kutosha, waliambizana: “Muhammad amewarogeni na chakula hiki.”

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasimama katikati yao na kusema; “Enyi kizazi cha Abdu’l-Muttalib! Allah Mwenye uwezo wote amenituma mimi kama Mjumbe kwa viumbe wote kwa jumla na hususan kwenu ninyi. Nakutakeni ninyi mutamke kauli mbili ambazo ni nyepesi na rahisi kwa ulimi, lakini katika mizani ya matendo ni nzito. Kama mtatamka kauli hizo mbili, mutakuwa mabwana wa nchi za Waarabu na wasio kuwa Waarabu.

Kupitia kauli hizo mtakwenda Peponi na mtapata kinga kutokana na Moto wa Jahannam. Maelezo hayo mawili ni:

Kwanza, kutoa shahada kwa Upweke wa Allah, na Pili kutoa Shahada kwa Utume wangu. Wa kwanza ambaye ataukubali wito wangu na kunisaidia katika kazi yangu atakuwa ndugu yangu, msaidizi wangu, mrithi wangu, na Makamu wangu baada yangu.

Mtume alirudia maneno haya ya mwisho mara tatu, na mara zote tatu hakuna aliyejibu isipokuwa Ali, akisema, “Mimi nitakusaidia, Ewe Mtume wa Allah.” Hivyo Mtume akatangaza: “Huyu Ali ni ndugu yangu, na yeye ndiye mrithi wangu, na Khalifa miongoni mwenu.

Uthibitisho Kutoka Ulamaa Wa Kisunni Na Waandishi Wa Ulaya.

Mbali na Maulamaa wa Kiislamu wa Kishia na Kisunni, Wanahistoria wengi walio waadilifu wa mataifa mengine wameelezea kwa kirefu Karamu hii. Walikuwa hawana upendeleo wa kidini, wakiwa wao sio Shia wala Sunni.

Mmoja wa Waandishi hawa ni mwana-Historia na Mwanafilosophia wa Kiingereza wa Karne ya kumi na tisa, Thomas Carlyle katika kitabu chake “Heroes and Hero-worship” ametoa maelezo ya kina juu ya karamu iliyofanyika nyumbani kwa Abu Talib. Baada ya maelezo ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), Ali alisimama na akabainisha imani yake kwa Mtume.

Kwa ajili hiyo Ukhalifa uliwekwa juu yake. Waandishi wengine wa Ulaya wamethibitisha jambo hili, wakiwa ni pamoja na George Sale wa Uingereza na Hashim, Mkristo wa Syria katika kitabu chake “Maqalatu’l-Islam”, na Bw. John Davenport katika kitabu chake “Muhammad and the Qur’an.”

Wote wanakubali kwamba mara tu baada ya tangazo la Utume wake, alimuita Ali Ndugu yake, Msaidizi, Makamu na Khalifa wake. Aidha, Hadith nyingi zinathibitisha kwamba Mtume alisisitiza jambo hili katika matukio mengine mengi.

Hadith Za Wazi Na Dhahiri Kuhusu Ukhalifa Wa Ali.

(1) Imam Ahmad Ibn Hanbal katika “Musnad” yake na Mir Seyyed Ali Hamadani Shafi’i katika “Mawaddati’l-Qurba” kuelekea mwisho wa Mawadda ya nne, wameandika kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema; “Ewe Ali! Utatekeleza majukumu kwa niaba yangu, na wewe ni makamu wangu juu ya wafuasi wangu.”

(2) Imam Ahmad Ibn Hanbal katika “Musnad”, Ibn Maghazili Faqih Shafi’i katika “Manaqib” na Tha’labi katika “Tafsir” yake wamesimulia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema kumwambia Ali: “Ewe Ali! Wewe ni ndugu yangu, Makamu, Mrithi na Mlipa madeni wangu.”

(3) Abu Qasim Husain bin Muhammad (Raghib Ispahani) katika “Mahadhiratu’l Udaba wa Muhawaratu’Sh-Shu’ara wa’l-Balagha” (kilichochapishwa Amira-e-Shazafiyya, Seyyed Husain Afandi, 1326 A.H.), sehemu ya 2, uk. 213, ananukuu kutokea kwa Ibn Malik kwamba Mtume amesema: “Hakika rafiki yangu, msaidizi, makamu na mbora wa watu ambaye ninamuacha nyuma yangu, ambaye atalipa deni langu na kutimiza ahadi yangu ni Ali bin Abu Talib.”

(4) Mir Seyyed Ali Hamadani katika “Mawaddatu’l-Qurba.” Katika mwanzo wa Mawadda ya sita, anasimulia kutoka kwa Khalifa wa Pili, Umar bin Khattab, kwamba wakati Mtume alipoanzisha uhusiano wa Kindugu miongoni mwa Masahaba, alisema: “Huyu Ali ni ndugu yangu katika dunia hii na kesho Akhera; yeye ni mrithi wangu kutoka miongoni mwa jamaa zangu na makamu wangu miongoni mwa umma wangu; yeye ndiye mrithi wa elimu yangu na mlipaji wa deni langu, chochote anachoniwia mimi, nami nawiwa naye, faida yake ni faida yangu na hasara yake ni hasara yangu; yoyote aliye rafiki yake ni rafiki yangu,mtu ambaye ni adui yake ni adui yangu.”

(5) Katika Mawadda hiyo hiyo, ananukuu hadith kutoka kwa Anas bin Malik, ambayo nimeitaja mapema. Kuelekea mwisho wake anasema kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema; “Yeye (Ali) ni Makamu wangu na Msaidizi.”

(6) Muhammad bin Ganji Shafi’i ananukuu Hadith kutoka kwa Abu Dharr Ghifari katika Kitabu chake, “Kifayatut-Talib” kwamba Mtume amesema: “Bendera ya Ali, Kiongozi wa Waumini, Kiongozi wa watu wenye nyuso zenye kung’ara, na Makamu wangu, itakuja kwangu katika chemchem ya Kauthari.”

(7) Baihaqi, Khatib Khawarizmi, na Ibn Maghazili Shafi’i wanaandika katika “Manaqib” zao kwamba alisema kumuambia Ali: “Sio sawasawa kwamba mimi niondoke kuwaacha watu bila ya wewe kuwa Makamu wangu kwa vile wewe ndiye bora zaidi wa Waumini baada yangu.”

(8) Imam Abu Abdur-Rahman Nisa’i mmoja wa Maimam wa vitabu sita (Siha) vya hadith, anasimulia kwa urefu kutoka kwa Ibn Abbas fadhila za Ali kuhusiana na hadith Na. 23 katika “Khasa’isu’l-Alawi.” Baada ya kuelezea cheo cha Mtume Harun, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema kumwambia Ali: “Wewe ni Makamu wangu baada yangu kwa kila Muumini.” Hadith hii na nyingine ambazo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ametumia maneno “baada yangu” zinathibitisha wazi kwamba Ali alikuwa ndiye mrithi wa mara tu.

(9) Kuna “Hadith ya Uumbwaji,” ambayo imesimuliwa katika njia mbalimbali. Imam Ahmad Ibn Hanbal katika “Musnad” yake, Mir Seyyed Ali Hamadani katika “Mawadda-tul-Qurba”, Ibn Maghazili Shafi’i katika “Manaqib”, na Dailami katika “Firdaus” wamemnukuu Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akisema: “Mimi na Ali tumeumbwa kwa Nuru Takatifu moja miaka 14,000 kabla Nabii Adam hajaumbwa.

Kutoka kwenye mgongo wa Adam na kupitia kizazi chake kitukufu, Nuru hiyo ilirithiwa na Abdu’l-Muttalib, na kutoka kwake iligawanywa na kurithiwa na Abdullah (baba yake Mtume) na Abu Talib (baba yake Ali). Mimi nilipewa Utume, na Ali alipewa Ukhalifa.”

(10) Hafiz Abu Ja’far Muhammad bin Jarir Tabari (amekufa 310 A.H.) anaandika katika kitabu chake “Kitabu’l-Wilaya” kwamba Mtume amesema mwanzoni mwa khutuba yake maarufu pale Ghadir Khum; “Malaika Jibril amenifikishia amri ya Allah kunitaka kwamba nisimame sehemu hii na kuwajulisha watu kwamba Ali bin Abu Talib ni ndugu yangu, wasii wangu, na Khalifa wangu baada yangu. Enyi watu! Allah amem- fanya Ali kuwa Walii (mlezi) wenu, na Imam (kiongozi). Utii kwake ni wajibu juu ya kila mmoja wenu; amri yake ni yenye mamlaka ya juu; maneno yake ni kweli tupu; laana iwe juu yake yule ambaye anampinga, rehma ya Allah iwe juu ya yule ambaye amemfanya rafiki.”

(11) Sheikh Suleyman Balkhi katika “Yanabiu’l-Mawadda” anaelezea kutoka katika kitabu cha “Manaqib” cha Ahmad, na yeye kutoka kwa Ibn Abbas, hadith inayoelezea fadhila nyingi za Ali. Ninainukuu yote hapa. Ibn Abbas anasimulia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Ewe Ali! Wewe ni Mchukuzi wa Elimu yangu, Walii na rafiki yangu, Wasii wangu, Mrithi wa elimu yangu na khalifa wangu. Wewe ndiye mdhamini wa urithi wa Mitume wote waliotangulia. Wewe ni msiri wa Allah katika ardhi hii na hoja ya Allah kwa viumbe wote. Wewe ni nguzo ya Iman na mlezi wa Uislam. Wewe ni taa katika giza; nuru ya muongozo, na kwa ajili ya watu wa ulimwengu wewe ni bendera iliyonyanyuliwa juu kabisa.

Ewe Ali! Yeyote akufuatae wewe atakuwa ameokolewa; yule ambaye hakutii wewe ataangamia; wewe ni njia ing’aayo, na iliyonyooka; wewe ni Kiongozi wa watu wasafi, na Kiongozi wa Waumini; kwa yeyote yule ambaye mimi ni mwenye kutawaliwa mambo (Maula) wake wewe pia ni maula (bwana) kwake; na mimi ndiye Maula (Bwana) wa kila muumini; (Mwanaume na Mwanamke). Ni rafiki yako tu yule aliyezaliwa katika ndoa halali. Allah hakunipeleka mbinguni kuzungumza Naye bila kuniambia, ‘Ewe Muhammad! fikisha salamu zangu kwa Ali na muambie kwamba ni Imam wa rafiki zangu na nuru ya waabuduo!’ Hongera Ewe Ali, juu ya ubora huu wa ajabu.”

(12). Abu Mu’ayyid Muwafiqu’d-Din, msemaji mzuri wa Khawarizm, katika kitabu chake “Fadha’il’l-Amirul-Mu’minin,” kilichochapishwa mwaka 1313 A.H., Sura ya 19 uk. 240, ananukuu nyanzo ambavyo vimesimulia kwamba Mtume amesema: “Wakati nilipofika Sidratu’l-Muntaha (Kituo cha juu sana wakati wa Mir’raji) nilisemeshwa hivi: ‘Ewe Muhammad! Wakati ulipowajaribu watu, ni yupi uliyemuona mtiifu zaidi.’ Nikasema ‘Ali!’ Kisha Allah akasema: ‘Umesema kweli Muhammad!’ Tena akaendelea kusema:

“Umechagua Makamu ambaye atafikisha elimu yako kwa watu, na kuwafundisha waja wangu kutoka Kitabu Changu yale mambo ambayo hawayajui?’ Nikasema, ‘Ewe Allah! Yoyote utakayemchagua Wewe, nami nitamchagua.’ Yeye akasema: nimekuchagulia Ali juu yako. Ninamfanya yeye Makamu na Wasii wako.’ Na akampamba Ali na elimu Yake na uvumilivu. Yeye ni Kiongozi wa Waumini ambaye hakuna hata mmoja anayeweza kuwa sawa naye katika cheo miongoni mwa watangulizi wake au warithi wake.’” Kuna hadith nyingi kama hizi katika vitabu vyenu Sahih.

Baadhi ya Maulamaa wenu waadilifu, kama Nizzam Basri, wameukubali ukweli huu. Salahu’d-Din Safdi katika kitabu chake “Wafa-Bi’l-Wafiyya”, kuhusiana na maelezo ya Ibrahim bin Sayyar bin Hani Basri, ajulikanae kama Nizzam Mu’tazali, anasema: Mtukufu Mtume wa Allah (s.a.w.w.) alithibitisha Uimama wa Ali na akamchagua kuwa Imam. Masahaba wa Mtume walikuwa na habari kamili juu ya hili, lakini Umar kwa ajili ya Abu Bakr, aliufunika Uimamu wa Ali kwa pazia.”

Ni wazi kutoka katika vitabu vyenu, hadith na tafsiri za Qur’ani kwamba Ali alishika nafasi ya juu sana ya ubora. Khatib Khawarizmi anasimulia kutoka kwa Ibn Abbas katika “Manaqib”, Muhammad bin Yusufu Ganji Shafi’i katika kitabu chake “Kifayatut-Talib”, Sibt Ibn Jauzi katika “Tadhkira” yake, Ibn Sabbagh Maliki katika “Fusulu’l-Mawadda”, Suleiman Balkhi Hanafi katika Yanabiul-Mawadda’ na Mir Seyyed Ali Hamadani katika “Mawaddatu’l-Qurba”, Mawadda ya 5, nakala kutoka kwa Khalifa wa Pili, Umar bin Khattab – wote wakithibitisha pamoja na tofauti kidogo tu ya maneno kwamba Mtume alisema: “Kama miti yote ingelikuwa ni kalamu, kama bahari ingelikuwa ni wino, kama majini wote na watu wangekuwa waandishi - hata hivyo sifa za Ali bin Abu Talib zisingeweza kuorodheshwa zote.”

Tabia Za Masahaba.

Sheikh Abdus-Salam: (Akimgeukia Hafidh Muhammad Rashid Sahib). Niruhusu niseme kitu kwa ufupi. (Akigeuka kumwangalia Muombezi). Kamwe hatuzikatai sifa za hali ya juu za Ali, lakini kuweka mipaka ya utukufu kwake peke yake sio sawa, kwa vile Masahaba wakubwa wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) walikuwa kila mmoja, ni watu wa uadilifu. Unajiingiza katika mazungumzo ya upande mmoja, ambayo yanawapoteza watu. Niruhusu kunukuu hadith moja juu ya sifa zao ili ukweli juu ya jambo hili uweze kudhi- hirishwa.

Muombezi: Mimi sijishughulishi na mambo na watu, Aya za Qur’ani tukufu na hadith sahihi zinatuelekeza katika muelekeo mmoja. Ninaapa kwa Jina la Allah kwamba mimi simpendi au kumchukia yeyote kimbumbumbu. Ninawaomba wasikilizaji kunisimamisha kama wakati wowote nitakimbilia njia yoyote ambayo ni kinyume na hoja au busara. Hadithi zinazokubaliwa na madhehebu zote ziwe ndio za kutegemewa.

Sizikatai sifa nzuri za masahaba waadilifu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), lakini yatupasa kutafuta miongoni mwao mmoja ambaye ni bora juu ya umma wote. Mjadala wetu sio wa kuhusu watu wema kwa kuwa wema ni wengi. Yatupasa kutafuta ni yupi aliyekuwa na sifa bora zaidi baada ya Mtume ili kwamba tuweze kumfuata yeye.

Sheikh: Unaleta vikwazo visivyo muhimu. Katika vitabu vyenu hakuna hata hadith moja yenye kuwasifu makhalifa. Tutahojiana vipi juu ya msingi huo?

Muombezi: Katika usiku wa kwanza wa majadiliano yetu, utakumbuka kwamba Hafidh Sahib mwenyewe aliukubali mjadala juu ya masharti kwamba hoja zetu zitegemee juu ya Aya za Qur’ani na juu ya Hadith zinazokubaliwa na Madhehebu zote. Kwa vile ninavyo vitabu vyenu Sahih, mimi nilikubali sharti hili. Kama ambavyo nyote mtathibitisha, sijatoka katika msimamo huo. Katika kuunga mkono hoja zangu nimesoma Aya za Qur’ani tu na Hadith zilizoandikwa katika vitabu Sahih vya Maulamaa wenu mashuhuri.

Wakati mlipoweka sharti hili, hamkujua kwamba mtakuja kunaswa baadae. Hata hivyo, bado sitaki sharti hili lichukuliwe kikamilifu moja kwa moja. Niko tayari kusikiliza hadith zenu za upande mmoja kama ni Sahih. Kisha tutaweza kuyaamua mambo kwa haki. Mimi sina kusita katika kuukubali ukweli kwenye kulinganisha fadhail za Ali.

Sheikh: Umetaja hadith inayohusu umakamu wa Ali lakini ukasahau ukweli kwamba kuna hadith nyingi kuhusu Abu Bakr.

Muombezi: Kwa kuzingatia akilini kwamba Maulamaa wenu wakubwa, kama vile Dhahabi, Suyuti na Ibn Abi’l-Hadid wameelezea kwamba Amawi - wafuasi wa Mu’awiyya na wa Abu Bakr wamebuni hadith nyingi katika kumtukuza Abu Bakr, unaweza kutaja hadithi moja kutoka miongoni mwa nyingi ya hizo ili kwamba mtu muadilifu aweze kua- mua juu ya usahihi wake.

Hadith Katika Kumtukuza Abu Bakr.

Sheikh: Kuna Hadith Sahihi iliyosimuliwa na Umar bin Ibrahim bin Khalid, ambaye anasimulia kutoka kwa Isa bin Ali bin Abdullah bin Abbas, na yeye kutoka kwa baba yake, na yeye kutoka kwa babu yake, Abbas, kwamba Mtume wa Uislamu alimwambia bwana huyo, “Ewe Ami yangu! Allah amemfanya Abu Bakr kuwa khalifa wa dini yake. Hivyo msikilize na umtii ili kwamba uweze kupata wokovu.”
Muombezi: Hii ni Hadith iliyokataliwa.

Sheikh: Ni Hadith iliyokataliwa kwa vipi?

Muombezi: Maulamaa wenu mashuhuri wenyewe wameikataa. Kwa sababu wasimuliaji wa hadith hii walikuwa ni waongo wenye sifa mbaya na waghushaji, Maulamaa wenu hawaioni kama inastahili kukubalika. Dhahabi katika “Mizanul-Itidal”, akiandika kuhusu Ibrahim bin Khalid, na Khatib Baghdadi akiandika kuhusu Umar bin Ibrahim anasema: “Yeye ni muongo mkubwa.” Na Hadith iliyosimuliwa na muongo haikubaliki.

Sheikh: Imesimuliwa kutoka vyanzo vya kuaminika kwamba mmoja wa masahaba wachamungu wa Mtume, Abu Huraira, alisimulia kwamba, Jibril alijitokeza mbele ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na akasema: “Allah anakutolea salaam, Anasema, ‘Nimemridhia Abu Bakr; muulize kama na yeye pia ameniridhia Mimi au laa.’”

Muombezi: Yatupasa kuwa waangalifu sana kuhusu kutaja Hadith. Nataka usikilize Hadith ambayo Maulamaa wenu wenyewe, kama Ibn Hajar (ndani ya Isaba) na Ibn Abdu’l-Bar (katika Isti’ab) wananukuu kutoka kwa Abu Huraira kwamba Mtume amesema: “Kuna wengi ambao huninukuu vibaya, na mwenye kunitafsiri vibaya makazi yake ni motoni. Wakati hadithi inaposimuliwa kwenu kwa niaba yangu ni lazima muipime na Qur’ani.”

Hadith nyingine inayokubaliwa na Madhehebu zote, imesimuliwa na Imam Fakhru’d-Din Radhi katika “Tafsir Kabir” Jz. 2, uk. 271 anasimulia kwamba Mtume amesema: “Wakati hadith kutoka kwangu inapoelezewa kwenu, iwekeni mbele ya Kitabu cha Allah kama ikikubaliwa na Qur’ani Tukufu, ikubalini. Vinginevyo, ikataeni.” Vitabu vya maulamaa wenu wenyewe mashuhuri vinaeleza kwamba mmoja wa wale ambao walighushi hadith kwa jina la Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), alikuwa huyu mtu aliyekataliwa, Abu Huraira, ambaye umemuita mchamungu.

Sheikh: Sikutarajia mtu wa kiwango chako kusema maneno ya kuzua kuhusu masahaba wa Mtume.

Muombezi: Unataka mimi nitishwe na neno “Sahaba”, lakini umekosea kama unafikiri neno “Sahaba” lazima libebe heshima. Kweli usahaba na Mtume unaongezea fadhila za mtu, lakini hili hutegemea juu ya sharti kwamba Sahaba huyo ni mtiifu kwa Mtume. Kama anakwenda kinyume na maelekezo ya Mtume, basi kwa hakika atakataliwa. Je, Munafiqina (wanafiki) hawakuwa miongoni mwa Masahaba wa Mtume? Ndiyo, walikuwemo, na wote walilaaniwa.

Sheikh: Haikuthibishwa kwamba walikataliwa. Kama walikataliwa ni uthibitisho gani kwamba watakwenda motoni? Je, kila mtu aliyekataliwa au kulaaniwa atakwenda motoni? Mtu aliyelaaniwa ni yule ambaye kwa mujibu wa Sheria ya wazi ya Qur’ani Tukufu, au Hadith ya Mtume ametangazwa hivyo (kuwa atakwenda motoni).

Tabia Ya Abu Huraira Na Laana Yake:

Muombezi: Kuna sababu za wazi kuonyesha kwamba Abu Huraira alikuwa sio mtu wa kuaminika. Maulamaa wenu wenyewe wamethibitisha ukweli huu. Moja ya sababu ya kulaaniwa kwake ni kwamba, kwa mujibu wa maneno ya Mtume, alikuwa rafiki wa mwana kulaaniwa wa mlaaniwa Abu Sufyan. Abu Huraira alikuwa mmoja wa wanafiki. Katika baadhi ya nyakati huko Siffin alisali Sala iliyoongozwa na Amiru’l-Mu’minin Ali.

Wakati mwingine alikaa katika meza ya chakula ya Mu’awiya kula chakula chake cha ghali. Kama ilivyoelezwa na Zamakhashari katika “Rabiu’l-Abrar” na Ibn Abi’l-Hadid katika Sherhe ya “Nahju’l-Balagha, wakati Abu Huraira alipoulizwa sababu za sera yake hii ya udanganyifu, yeye alisema; “Chakula cha Mu’awiyya ni kitamu sana na chenye ladha, na Sala nyuma ya Ali ni bora zaidi.”

Maulamaa wenu wenyewe, kama vile Sheikhu’l-Islam Hamwaini katika “Fara’id” Sura ya 37, Khawarizmi katika “Manaqib” Tibrani katika “Ausar”, Ganji Shafi’i katika “Kifayatut-Talib” (na kundi la wengine), wananukuu kutoka kwa huyu huyu Abu Huraira na wengine kwamba Mtume amesema: “Ali yu pamoja na Haki na Haki iko pamoja na Ali.”
Wakati alipomuacha Ali na kwenda kubembeleza hisani za Mu’awiya, hakuwa wa kulaaniwa. Kama mtu si tu hanyamazi aonapo matendo maovu ya Mu’awiya, bali hushirikiana naye hasa na humsaidia ili kuendeleza nafasi yake mwenyewe ya kilimwengu na kujaza tumbo lake, hivi huyo sio mtu wa kulaaniwa?

Abu Huraira huyo huyo mwenyewe anasimulia (kama ilivyoandikwa na Maulamaa wenu mashuhuri, kama Hakim Nishapuri katika Mustadrak, Jz. 2, uk. 124, Imam Ahmad bin Hanbali, Tibrani, na wengine), kwamba Mtume amesema: “Ali yu pamoja na Qur’ani na Qur’ani iko pamoja na Ali. Viwili hivi havitatengana mpaka vinifikie katika Chemchem ya Kauthar. Ali anatokana na mimi na mimi ninatokana na Ali. Yule ambaye anamtweza Ali, hunitweza mimi. Yule ambaye hunitweza mimi, anamtweza Allah.” Mu’awiya katika hutuba zake za Sala ya Ijumaa alimlaani Ali, Hasan, na Husein. Aliagiza kwamba katika mikusanyiko yote, watu hawa watukufu sharti walaaniwe.

Hivyo kama mtu kiukamilifu amejishirikisha na watu walaanifu kama hawa na yu aridhia matendo yao, huyu si wa kulaaniwa? Na wakati anashirikiana na watu hawa, kama huwasaidia kwa kughushi hadith na kulazimisha watu watoe laana dhidi ya watu watukufu, huyu si wa kulaaniwa?

Sheikh: Je, ni busara kwetu sisi kukubali masingizio haya, kwamba masahaba waamini- fu wa Mtume, wanaghushi hadith na waweze kuwalazimisha watu wamlaani Ali?

Muombezi: Kwa kweli ni vigumu kuamini kwamba sahaba mwaminifu angeweza kufanya kitu kama hicho. Kama yeyote katika Masahaba amefanya kitu kama hicho, ina maana kwamba hakuwa muaminifu. Kuna Hadithi nyingi zilizosimuliwa na Maulamaa wenu wenyewe kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Yule ambaye anamtweza Ali, hunitweza mimi na Allah.”

Sheikh: Kwa kuwa mkweli, wakati unawasingizia masahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), kusema kwamba, walighushi hadith, vipi tunaweza kutumaini kwamba hutahusisha maarubu mabovu kwa Maulamaa wa vyeo vya juu wa Kisunni? Ninyi Mashi’a mna tabia inayofahamika ya kuwakashifu watu maarufu.

Muombezi: Huna haki katika kuhusisha vitu kama hivyo kwetu. Historia ya Uislamu ya miaka 1400 iliyopita inathibitisha kinyume chake. Kuanzia mwanzo wa karne ya kwanza ya Uislamu, Bani Umayya wamewatukana Maimam Maasum, dhuria wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), na wafuasi wao Mashi’a. Hata leo, maulamaa wenu mashuhuri wanasimulia hadith za kashfa dhidi ya Mashi’a katika vitabu vyao ili kuwapoteza watu.

Sheikh: Ni ulamaa gani wa Sunni aliyewakashifu Mashi’a?

Kashfa Za Ibn Abd Rabbih Dhidi Ya Mashi’a.

Muombezi: Mmoja wa Maulamaa waandishi wenu wakubwa, Shahabu’d-Bin Abu Umar Ahmad bin Muhammad bin Abd Rabbih Qartabi Andalusi Maliki (aliyefariki 48 A.H.), katika Indu’l-Farid yake Jz. 1, uk. 269, amewaita Mashi’a Mayahudi wa Umma huu.” Anasema kwamba, kama vile Mayahudi walivyokuwa maadui wa Wakristo, Mashi’a ni maadui wa Uislamu.

Anadai kwamba, Mashi’a kama walivyo Mayahudi, hawaukubali ukweli kwamba mke aweza kutalikiwa mara tatu kutoka kwa mtu huyo huyo, wala hawaikubali sheria ya Edda.

Wote hapa, Mashi’a na Masunni ambao wana uzoefu na rafiki zao Shi’a watayacheka madai haya. Utaona katika vitabu vyote vya fiqih ya Kishi’a mashariti kuhusu talaka tatu na Edda baada ya talaka.

Vilevile anatuhumu kwamba Mashi’a, kama walivyo Mayahudi, ni maadui wa Jibril, kwa sababu Jibril amewasilisha maagizo ya Allah (Wahyi) kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), badala ya Ali (kicheko miongoni mwa wasikilizaji Mashi’a). Sisi Mashi’a tunamwamini Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Tunaamini kwamba maagizo ya Allah yaliteremshwa kwake kupitia kwa Malaika Jibril, ambaye cheo chake ni cha juu zaidi kuliko kile kilichohusishwa kwake na mwandishi huyu asiye maana.

Kashfa Zilizotolewa Na Ibn Hazm.

Mwingine kati ya Maulamaa wenu wakubwa ni Abu Muhammad Ali bin Ahmad bin Said Ibn Hazm Andalusi (amekufa 456 A.H.), ambaye ameandika kimakhususi dhana potofu kuhusu Mashi’a katika kitabu chake mashuhuri “Kitabu’l-Fasil fi’l-Milal Wa’n-Nihal.” Kwa mfano anasema Shi’a sio Waislamu, ni waasi, wafuasi wa Mayahudi na Wakristo. Katika Juzuu ya 4, uk. 182, anaandika kwamba:

“Kwa mujibu wa Mashi’a, ni halali kuoa wanawake tisa.” Riwaya hii inaweza kukanushwa kwa urahisi sana kwa kuangalia vitabu vya Shi’a ambavyo kwa uwazi vimeeleza kwamba ni haramu kuwa na zaidi ya wanawake wanne katika ndoa ya kudumu, kwa wakati mmoja. Kuna tuhuma nyingi zinazofanana na hizi, zisizo na msingi wa mambo machafu yaliyohusishwa na Mashi’a katika kitabu chake hiki, ambayo ungeona aibu kuyasikia.

Kashfa Zilizotolewa Na Ibn Taimiyya

Mmoja wa Ulamaa wenu mtovu wa dini zaidi ni Ahmad bin Abdu’l-Halim Hanbali, ajulikanaye kama Ibn Taimiyyah (amekufa 728 A.H.). Alikuwa na dhamira mbaya kupita kiasi juu ya Mashi’a, Amru’l-Mu’minin Ali, na kizazi cha Mtume. Kitabu chake “Minhajus- Sunna” kimejaa uadui mkali dhidi ya Ali na kizazi cha Mtume.

Yeyote yule ambaye ana ufahamu wa ukweli japo kidogo angeshangazwa kusikia uongo wake. Kwa mfano anaandika kwamba: “Hakuna kundi kubwa la waongo kama madhehebu ya Shi’a, na ni kwa sababu hii kwamba waandishi wa vitabu vya Sahih (Sihah Sita) hawakuingiza katika vitabu vyao Hadith zilizosimuliwa na wao.”

Katika Juz. ya 10, uk. 23 anasema kwamba, Mashi’a wanaamini katika misingi minne ya dini - Tauhidi, Adili, Nubuwat na Uimam. Kwa kweli katika vitabu vya itiqad vya Shia, vinavyopatikana kila mahali, imeandikwa kwamba itiqad ya Shia ina misingi mitatu: Tauhid, Nubuwat, na Ma’ad (Siku ya malipo); Adil ni sehemu ya Tauhid na Uimam ni sehemu ya Nubuwat.

Katika juzuu ya 1, Uk. 131, anaeleza kwamba Mashi’a hawakusanyiki misikitini. Hawasali Sala ya Ijumaa au Sala za jamaa. Kama wakisali wanasali kila mtu peke yake. (kicheko miongoni mwa Mashi’a).

Lakini kwa hakika tunaweka mkazo mkubwa katika Sala za jamaa. Katika miji mingi ya Iraq na Iran, ambayo ni vituo vya Mashi’a, misikiti yetu inajaa watu wanaoabudu wakisali sala za Jamaa. Katika ukurasa huohuo, anaandika kwamba Mashi’a hawafanyi Hijja kwenye Al-Kaaba.

“Hija yao ni ya kuzuru makaburi tu, ambayo wanaiona ni bora kuliko kwenda kuhiji Makka. Wanawalaani wale ambao hawafanyi Ziara kwenye makaburi.” (kicheko). Vitabu vya du’a vya Shi’a vina Sura maalum kwa ajili ya dua za hijja unaoitwa Kitabu’l-Hajj.

Wanatheolojia wa Kishi’a, wameandika vitabu vingi wakielezea kanuni kwa ajili ya Hijja, ambamo maelekezo maalum yametolewa kutekeleza taratibu za Hijja.

Hadithi nyingi kutoka kwa Maimamu wetu zinasisitiza kwamba, kama Muislamu (Shi’a au Sunni) anao uwezo na bado akashindwa kutekeleza Hija anatengwa katika Uislamu. Wakati akifa anaambiwa: “Kufa kifo chochote unachoweza, kiwe kifo cha kiyahudi, Kikristo, au cha muabudu moto.”

Unaweza kuamini kwamba mbele ya maelekezo kama hayo Mashi’a wangejiepusha na kutekeleza Hija? Kwa nyongeza juu ya tafsiri hizi potovu, mtu huyu muovu amesema kwamba mwanachuo mkubwa wa Kishia, Muhammad bin Muhammad bin Nu’man (Sheikh Mufid) ameandika “Manasikhu’l-Hajj li’l-Mashahid.”

Jina sahihi la kitabu hicho ni “Mansikhu’z-Ziarat”, ambacho kinapatikana kila mahali na ambacho kina maelekezo kuhusu kuzuru sehemu za Ziarat, pamoja na Ma Kuba matukufu ya wastahiki Maimamu.

Kama utaviangalia vitabu hivi vya Ziarat, utaona kwamba kutembelea kwenye makaburi ya Mtukufu Mtume na Maimamu kunapendekezwa, sio wajibu.

Uthibitisho mzuri dhidi ya tuhuma za mtu huyu mtovu wa dini ni mwendo unaofuatwa na Mashi’a, ambao huenda kuhiji kwa maelfu kila mwaka. Shutuma nyingine bandia ya muongo huyu, yaweza kupatikana katika juzuu ya 1, uk. 11, ambako anasema kwamba Mashi’a wanaita mbwa wao kwa majina ya Abu Bakr na Umar na kila siku wanawalaani (hao Abu Bakr na Umar). (Kicheko miongoni mwa Mashi’a). Hiki ni kichekesho.

Kwa mujibu wa itiqad ya Shia, mbwa ni najisi kabisa. Nyumba ya Muislam yenye mbwa hukosa baraka za Allah. Kwa hiyo, Waislamu Mashi’a wanakatazwa kabisa kufuga mbwa isipokuwa kwa masharti makhususi (kuwinda, kuilinda nyumba, au kuchunga mbuzi). Moja ya sababu nyingi za kutopatana kati ya Yazid na mjukuu wa Mtume, Imam Husain, ilikuwa kwamba Yazid alikuwa mpenzi wa mbwa na akiwafuga bila kuwa na sababu nzuri.

Ibn Taimiyya vilevile anaandika kwamba, kwa vile Mashi’a wanangojea kutokeza kwa yule wa mwisho wa Maimam wao, katika sehemu nyingi, hususan katika Sardab (Sakafu chini ya nyumba) ya Samara (ambako Mtukufu Imam alitoweka), ameandaliwa farasi kwa ajili yake. Wanamuita Imam wao ajitokeze, wakisema kwamba wamejiandaa kikamilifu kumtumikia Yeye.

Vilevile anaandika kwamba Mashi’a hugeuka kuelekea upande wa mashariki wakati wa siku za mwisho wa Ramadhani na kumwita Imamu ajitokeze. Baadhi yao huacha hata Sala zao za faradhi; wakifikiri kwamba kama watajishughulisha na kusali Sala zao na Imam akajitokeza wangeweza kukosa kumtumikia kwao. (Kicheko kwa Sunni na Mashi’a).

Hatushangazwi sana na Hadith za kuchekesha za mtu huyu muovu. Bali tunashangazwa na tabia za maulamaa wa sasa wa Misri na Damaskas ambao, bila kuwauliza Mashi’a ambao wanaishi nao, wanafuata upumbavu wa mtu kama Ibn Taimiyya. Itakuwa inachosha sana kutoa orodha ndefu ya riwaya zisizo sahihi za Ibn Hajar Makki, Hafidh, na Kadhi Ruzbahan. Vitabu yao vinajulikana, ingawa katika mtazamo wa usahihi, hivyo havina thamani.

Kwa mfano “Milal Wa’n-Nihal” cha Muhamma Ibn Abdu’l-Karim Shahrastani (amekufa 548 A.H.), katika macho ya wanachuoni, hakina thamani hata kidogo. Mtu hataweza kuona chochote ndani yake isipokuwa itiqad bandia kabisa zilizohusishwa kwa Mashi’a, kama kumuabudu Ali na imani ya kuhama kwa roho (baada ya kufa kuingia katika mwili mwingine). Ni wazi hakuwa mtu mwenye elimu. Akiandika kuhusu Shi’a Ithnashariyya, yeye anasema kwamba, kaburi la Ali Ibn Hadi Muhamma Naqi, ambaye amekuja baada ya Imam Muhammad Taqi, liko Qum.

Lakini hata watoto wadogo wanajua kwamba Kuba Tukufu la Imam Ali Naqi liko ubavuni mwa kuba la Mtoto wake, Imam Hasan Askari huko Samarra. Sidhani kwamba rejea nyingine zaidi za namna hii ni muhimu kuthibitisha kwamba ulamaa wa Kisunni wamebuni riwaya za uongo kuhusu Mashi’a. Na siko peke yangu katika kulenga shutuma dhidi ya uaminifu wa Abu Huraira. Maulamaa wa Kisunni wamefichua tabia zake mbaya katika vitabu vyao wenyewe.

Tabia Za Abu Huraira Na Hadith Zinazotaka Alaaniwe.

Ibn Abi’l-Hadid Mu’tazali katika Sherhe yake ya “Nahaju’l-Balagha,” Jz. 1, uk. 358, na katika Jz. 4, anasimulia kutoka kwa Sheikh na mwalimu wake, Imam Abu Ja’far Asqalani, kwamba Mu’awiyya bin Abu Sufyani aliandaa kikundi cha masahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na watoto wa masahaba hao kwa lengo la kughushi hadith.

Miongoni mwa wale waliobuni hadith chafu dhidi ya Ali walikuwa Abu Huraira, Amr bin Aas, na Mughira Ibn Sha’ba. Akitoa maelezo juu ya ngano hizi, Ibn Abil-Hadid anasimulia kwamba, wakati mmoja Abu Huraira aliingia Msikiti wa Kufa na kuona kundi kubwa la watu ambao walikuja kumpokea Mu’awiya. Alipaza sauti yake kwenye lile kundi la watu: “Enyi watu wa Iraq. Mnafikiri kwamba nitasema uongo katika kumpinga Allah na Mtume Wake na kujinunulia moto wa Jahanam? Sikieni kutoka kwangu nilivyosikia kutoka kwa Mtume.

‘Kila Mtume ana Haram (Sehemu takatifu ya kuishi) na Haram yangu ni Madina.

Mtu ambaye anahusika na uzushi katika mji wa Madina analaaniwa na Allah, na Malaika Wake, na pamoja na wanadamu wote!’ Naapa kwa jina la Allah, kwamba Ali alihusika na uzushi.” (Yaani, Ali alichochea mfarakano miongoni mwa watu, hivyo, kwa mujibu wa Mtume, anapaswa kulaaniwa).

Wakati Mu’awiya alipolifahamu hili (kwamba Abu Huraira amefanya kitu kama hicho kwa ajili yake na amekifanya katika makao makuu ya Ali, Kufa), alimuita, akampa zawadi, na akamfanya Gavana wa Madina. Je, matendo yake mabaya hayatoshi kuthibitisha kwamba anastahili laana? Je, ni sahihi kwamba mtu ambaye amemfanyia ubaya mbora zaidi wa Makhalifa achukuliwe kama mchamungu kwa sababu tu amewahi kuwa sahaba wa Mtume?

Sheikh: Ni katika sababu zipi ambazo Mashi’a wanamuona kuwa kalaaniwa?

Muombezi: Kuna hoja nyingi katika kuunga mkono maoni yetu. Mojawapo ya hizo ni kwamba, mwenye kumtukana Mtume, kwa mujibu wa madhehebu zote amelaaniwa. Kwa mujibu wa Hadith ambayo nimeitaja mapema, Mtukufu Mtume amesema: “Mwenye kumtukana Ali, hunitukana mimi, Mwenye kunitukana mimi humtukana Allah.” Ni dhahiri kwamba Abu Huraira alikuwa mmoja wa wale ambao, sio tu amemtukana Ali bin Abu Talib, bali ambaye alighushi hadith kuwachochea wengine kumtukana yeye.

Njama Ya Abu Huraira Na Busr Bin Artat Katika Mauwaji Ya Waislamu.

Vilevile tunamlaani Abu Huraira kwa kula njama kwake na Busri Ibn Artat katika mauaji ya maelfu ya Waislamu. Imesimuliwa na wanahistoria wenu wenyewe, akiwemo Tabari, Ibn Athir, Ibn Abi’l-Hadid, Allama Samhudi, Ibn Khaldum, Ibn Khallikan, na wengine kwamba Mu’awiyya alimtuma yule katili Busri Ibn Artat pamoja na wanajeshi wa Syria

4,000 kwenda Yemen kupitia Madina kuwasaga watu wa Yemen na Mashi’a wa Ali. Washambuliaji hawa waliwaua maelfu ya Waislamu katika mji wa Madina, Makka, Ta’if, Jabala (Mji wa Tihama), Najran, Safa, na vitongoji vyake. Hawakuwaacha vijana au wazee wa Bani Hashim au Shi’a wa Ali.

Waliwaua hata watoto wadogo wawili wa binamu yake Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) Ubaidullah bin Abbas Gavana wa Yemen, ambaye alikuwa ameteuliwa na Ali. Inasemekana kwamba zaidi ya Waislamu 30,000 waliuwawa kwa amri ya dhalimu huyu.

Bani Umayya na wafuasi wao walitenda ukatili huu wa kiwendawazimu. Mpendwa wenu Abu Huraira alishuhudia unyama huu na hakuwa kimya tu, bali pia aliuunga mkono kikamilifu.

Watu wasio na hatia kama Jabir bin Abdulla Ansari, na Abu Ayyub Ansari walitafuta pa kukimbilia. Hata nyumba ya Abu Ayyub Ansari ambaye alikuwa mmoja wa masahaba wakubwa wa Mtume, ilichomwa moto. Wakati Jeshi hili lilipoelekea Makka, Abu Huraira alibakia Madina.

Sasa naomba mtueleze, kwa jina la Allah, iwapo mtu huyu mlaghai ambaye alikuwa katika usahibu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa miaka mitatu, na ambaye amesimulia zaidi ya Hadith 5,000 kutoka kwa Mtume, hakusikia hadithi zile mashuhuri zinazohusu mji wa Madina?

Maulamaa wa madhehebu zote (kama Allama Samhudi katika “Ta’rikhu’l-Madina,” Ahmad bin Hanbal katika “Musnad” Sibt Ibn Jauzi katika “Tadhkira” uk. 163) wamenukuu kutoka Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ambaye amesema mara kwa mara: “Yule ambaye atawatishia watu wa Madina na mateso, atatishwa na Allah na atalaaniwa na Allah, Malaika Wake, na wanadamu wote. Allah hatakubali kitu chochote kutoka kwake.

Na alaaniwe yule mwenye kuwatisha watu wa Madina. Kama mtu yeyote atawadhuru watu wa Madina, Allah atamyeyusha kama risasi katika moto.”

Sasa ni kwa nini Abu Huraira alijiunga na jeshi lile ambalo liliiangamiza Madina? Kwa nini alibuni hadith zenye upinzani kwa makamu sahihi wa Mtume? Na kwa nini aliwachochea watu kumtukana yule mtu ambaye kuhusu yeye Mtume amesema: “Kumtukana yeye ni kunitukana mimi?”

Wewe amua iwapo kama mtu ambaye amebuni hadith kwa jina la Mtume hakuwa mwenye kulaaniwa?
Sheikh: Umekosa huruma, sio vyema kwako kumwita Sahaba muaminifu mno wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mtovu wa dini na mzushi.

Laana Ya Abu Huraira Na Kupigwa Kwake Na Umar.

Muombezi: Siko peke yangu ambaye “sina huruma” kwa Abu Huraira. Mtu wa kwanza ambaye hakuwa na huruma naye alikuwa Khalifa wa Pili, Umar bin Khattab. Ibn Athir na Ibn Abi’l-Hadid katika Sherhe yake ya Nahjul’l-Balagha, Jz. 3, uk. 104 (iliyochapishwa Misri) na wengine wengi wameeleza kwamba Khalifa Umar alimchagua Abu Huraira kuwa gavana wa Bahrain katika mwaka wa 21 A.H., watu wakamjulisha Khalifa kwamba Abu Huraira amejikusanyia mali nyingi na amenunua farasi wengi.

Kwa ajili hiyo Umar akamuondoa madarakani katika mwaka wa 23 A.H. Mara tu Abu Huraira alipoingia kwenye baraza, Khalifa akasema: “Ewe adui wa Allah na adui wa Kitabu Chake! Umeiba mali ya Allah?

Alijibu: “Sikuiba, bali watu wamenipa zawadi.” Ibn Sa’ad katika “Tabaqat” Jz. 4, uk. 90, Ibn Hajar Asqalani katika “Isaba”, na Ibn Abdi-e-Rabbih katika “Iqdu’l-Farid” Jz. 1, wanaandika kwamba Khalifa alisema: “Wakati nilipokufanya Gavana wa Bahrain, ulikuwa huna hata kiatu katika miguu yako, lakini sasa nimesikia kwamba umenunua farasi kwa dinari 1,600. umeipataje mali hii.’ Alijibu, ‘Hizi ni zawadi za watu ambazo faida yake imekuwa marudufu zaidi.’

Uso wa Khalifa uligeuka kuwa mwekundu kwa hasira, na alimpiga viboko kwa nguvu sana kiasi kwamba mgongo wake ulivuja damu. Kisha akaamuru zile dinari 10,000 ambazo Abu Huraira alizikusanya huko Bahrain zichukuliwa kutoka kwake na ziwekwe kwenye mfuko wa Baitu’l-Mal.”

Hii haikuwa mara ya kwanza kwa Umar kumchapa Abu Huraira. Muslim anaandika katika Sahih yake Jz. 1, uk. 34, kwamba wakati wa uhai wa Mtume, Umar bin Khattab alimpiga Abu Huraira kwa nguvu sana mpaka akaanguka chini. Ibn Abi’l-Hadid anaandika katika Sherhe yake ya “Nahjul’l-Balagha” Jz. 1, uk. 360: “Abu Ja’far Asqalani amesema: Kwa mujibu wa watu wetu mashuhuri (Yaani Wanachuoni), Abu Huraira alikuwa mtu muovu.

Hadith zilizosimuliwa na yeye hazikukubaliwa. Umar alimchapa na kiboko na akamwambia kwamba alikuwa amebadilisha hadith na alihusisha maneno ya uongo kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).’” Ibn Asakir katika kitabu chake “Ta’rikh Kabir”, na Muttaqi katika “Kanzu’l-Umma” wanasimulia kwamba Khalifa Umar alimchapa viboko, alimkemea na akamkataza kusimulia hadith kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Umar alisema: “Kwa sababu unasimulia hadithi nyingi kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) una uwezo tu wa kuhusisha uongo kwake. - Yaani mtu anatazamia mtu muovu kama wewe kutoa uongo tu kuhusu Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Hivyo ni lazima uache kusimulia Hadith kutoka kwa Mtume; vinginevyo nitakupeleka katika nchi ya Dus.” (Kabila katika Yemen ambalo kwamba Abu Huraira anatokana nalo). Ibn Abi’l-Hadid, katika Sherhe yake ya “Nahju’l-Balagha”, Jz. 1, uk. 360 (iliyochapishwa Misri) anasimulia kutoka kwa mwalimu wake, Imam Abu Ja’far Asqalini, kwamba Ali alisema: Jihadharini na muongo mkubwa miongoni mwa watu, Abu Huraira Dusi.”

Ibn Qutayba, katika “Ta’wil-e-Mukhtalifu’l-Hadith,” na Hakim katika Mustadrak Jz. 3, na Dhahabi katika “Talkhisu’l-Mustadrak” na Muslim katika Sahih yake, Jz. 2, wakielezea kuhusu tabia za Abu Huraira, wote wanasema kwamba Aisha alikuwa alipingana naye mara kwa mara na kusema: “Abu Huraira ni muongo mkubwa ambaye hughushi hadith na kuzihusisha na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

“Kwa ufupi sio sisi peke yetu ambao tumemkataa Abu Huraira. Kwa mujibu wa Khalifa Umar, Amirul’l-Muuminiina Ali, Ummu’l-Muuminina Aisha, na Masahaba wengine na wafuasi wa Mtume, wamesema kwamba alikuwa sio muaminifu kabisa.

Kwa ajili hiyo, Masheikh wa madhehebu ya Mutazila na Maimam wao, na ulamaa wa Kihanafia kwa kawaida wanakataa hadith zilizosimuliwa na Abu Huraira.

Aidha, katika Sherhe yake ya Sahih Muslim, Jz. 4, Nadwi anasisitiza nukta hii: “Imam Abu Hanifa amesema: ‘Masahaba wa Mtukufu Mtume kwa ujumla walikuwa ni wacha-Mungu na wanyofu. Ninaikubali kila hadith yenye ushahidi iliyosimuliwa na wao, lakini sizikubali hadith ambazo chanzo chake ni Abu Huraira, Anas Ibn Malik, au Samara bin Jundab.”

Tunamkataa Abu Huraira yule yule, ambaye Khalifa Umar alimchapa viboko na kumuita mwizi na muongo. Alikataliwa na Ummu’l-Mu’minina Aisha, Imam Abu Hanifa, na masahaba wengi na wafuasi wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Tunamkataa Abu Huraira huyo huyo ambaye alikataliwa na kuitwa muongo na Bwana wetu, kiongozi wa wenye kuabudu Mungu mmoja, Ali, na akakataliwa na Maimamu watukufu na dhuria wa Mtume.

Tunamkataa Abu Huraira ambaye alikuwa muabudu tumbo, ambaye pamoja na kujua ubora wa Ali, alimpuuza. Alimpendelea mfadhili wake, mlaaniwa Mu’awiya, alikaa kwenye meza yake ya chakula na kula vyakula vitamu naye, na akatunga hadithi za kumpinga Ali.

Kwa mtazamo wa mjadala wetu mpaka sasa, ninyi na mimi tunawajibika kuangalia kwamba wakati hadithi kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ikiwa kwenye mjadala, yatupasa kwanza kuirejesha kwenye Qur’ani Tukufu. Kama hadith inakubaliana na Qur’ani, yatupasa kuikubali, vinginevyo la.

Majibu Kwa Hadith Idhaniwayo Kwamba Allah Alisema, “Nimeridhishwa Na Abu Bakr - Je Na Yeye Ameridhika Na Mimi?”

Hadithi ambayo umeisimulia mapema (ingawa ni ya upande mmoja) yaweza kurejeshwa kwenye Qur’ani Tukufu. Kama hakuna pingamizi, hapana shaka tutaikubalia. Hata hivyo, aya moja ya Qur’ani inasema: “Na hakika tumemuumba mwanadamu, nasi tunajua yanayopita katika nafsi yake; nasi tukaribu naye zaidi kuliko mshipa wake wa shingo.” (50:16)

Mnatambua kwamba Hablu’l-Warid (mshipa wa shingo) ni usemi wa kawaida utumiwao kuelezea ukaribu uliozidi mno. Maana ya Aya hii ni kwamba, Allah ni Mjuzi wa yote. Hakuna kinachofichika kwake, hata kiwe ndani kiasi gani katika moyo wa mtu. Allah anajua siri za nyoyo zetu.

Na katika Sura ya “Yunus” Anasema: “Na hushughuliki katika kazi yoyote, wala hasomi humo (kitu chochote) katika Qur’ani, wala hamfanyi kitendo chochote, isipokuwa sisi tunakuwa mashahidi juu yenu mnaposhughulika nayo. Hakifichikani kwa Mola wako kitu chochote (hata) kilicho sawa na uzito wa mdudu chungu, la katika ardhi wala katika mbingu. Wala (hapana) kidogo kuliko hicho wala kikubwa, isipokuwa kimo katika kitabu (cha Allah) kielezacho (kila kitu).” (10:61).

Kwa mujibu wa Aya hizi, na kwa mujibu wa akili ya kuzaliwa, hakuna kinachofichikana kwa Allah. Anajua mtu anachofanya au kufikiri. Sasa linganisha hadithi hii na Aya hizi mbili na uone kama zinaweza kupatanishwa. Itawezekana vipi kwamba Allah Mwenye Nguvu zote asijue furaha ya Abu Bakr, kiasi kwamba Yeye mwenyewe awajibike kumuuliza kama ameridhishwa Naye au la? Akili ya kuzaliwa na Qur’ani Tukufu vinaonyesha kwamba “Hadith” hii ni ya uwongo.

Hadith Zenye Kumsifu Abu Bakr Na Umar Na Kutostahili Kwao.

Sheikh: Hakuna shaka kwamba Mtume alisema: “Allah atajionyesha kwa watu wote kwa ujumla na makhususi kwa Abu Bakr.” Vilevile alisema: “Allah hakuweka kitu chochote kwenye kifua changu ambacho hakukiweka kwenye kifua cha Abu Bakr.” Vilevle alisema: “Mimi na Abu Bakr ni kama farasi wawili ambao wanalingana sawa katika mbio.” Alisema tena: “Katika anga kuna malaika 80,000 ambao huomba rehma kwa ajili ya yule ambaye ni rafiki wa Abu Bakr na Umar. Na katika usawa wa upande mwingine wa anga kuna Malaika 80,000 ambao humlaani yule ambaye ni adui wa Abu Bakr na Umar.”

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) vilevile alisema: “Abu Bakr na Umar ni wabora wa wanadamu wote kuanzia mwanzo mpaka mwisho.”

Cheo cha Abu Bakr na Umar kinaweza kupimwa kutokana na Hadithi ambayo kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Allah ameniumba mimi kutokana na nuru Yake, Abu Bakr kutokana na nuru yangu, na Umar kutokana na nuru ya Abu Bakr. Umar ni taa ya watu wa Peponi.”

Kuna hadithi nyingi kama hizo ambazo zimeandikwa katika vitabu vyetu Sahihi. Nimesimulia Hadithi chache tu ili kwamba ujue Cheo halisi cha makhalifa.

Muombezi: Maana ya hadhithi hizi huongozea kwenye uasi na ukafiri wa kidini, ambavyo inadhihirisha wazi kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) asingeweza kusema vitu kama hivyo. Hadithi ya kwanza inaonyesha kwamba Allah ana mwili na ni ukafiri kuamini kwamba Allah ana mwili. Hadithi ya pili inaonyesha kwamba Abu Bakr alishiriki katika yale yaliyoteremshwa kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Hadithi ya tatu inamaanisha kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa hali yoyote hakuwa mbora zaidi kwa Abu Bakr. Hadithi nyingine inapingana na hadithi nyingi, ambazo zinakubaliwa na madhehebu zote, kwamba watu wabora zaidi wa ulimwengu huu ni Mtume Muhammad na kizazi chake.

Mbali na ukweli huu wa wazi, Maulamaa wenu mashuhuri kama Muqaddas katika kitabu chake “Tadhkiratu’l-Muzu’a”, Firuzabadi Shafi’i katika kitabu chake “Safarus-Sa’adat”, Hasan bin Athir Dhahabi katika kitabu chake “Mizanul-ltidal”, Abu Bakr Ahmad bin Ali Khatib Baghdad katika kitabu chake cha “Ta’rikh”, Abu’l-Faraj Ibn Jauzi katika “Kitabu’l- Muzu’a”, na Jalalu’d-Din Suyuti katika “Al’Lu’ali’l-Masnu’a fi’l-Abadusi’l-Muzu’a” - wote wamehitimisha kwamba Hadithi hizi ni zakutungwa. Zinapingana na Qur’ani Tukufu na akili ya kuzaliwa.

Sheikh: Lakini hebu angalia hadithi nyingine, ambayo hakika ni sahihi, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Abu Bakr na Umar ni Mabwana wa wazee wa Peponi.”

Muombezi: Kama utaichunguza kwa karibu zaidi Hadith hii inayotarajiwa, unaweza ukaona kwamba, mbali na ukweli kwamba ulamaa wenu wenyewe wameikataa, hadithi hii haiwezekani kuwa inatoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Kila mtu anajua kwamba pepo haitaingiwa na wazee. Hakuna mabadiliko ya kidogo kidogo huko. Kuna riwaya nyingi zinazokubaliwa na madhehebu zote zinazohusiana na jambo hili. Moja ya hizo ni suala la Ashja’iyya, mwanamke mzee ambaye alikuja kwa Mtume.

Katika maongezi yake, Mtume alisema: “Wanawake wazee hawataingia Peponi.” Yule mwanamke alihuzunika sana na akasema, huku akilia: “Ewe Mtume wa Allah, hii ina maana mimi sitaingia Peponi.”

Alipokwisha kusema hivi, akaondoka. Mtume akasema: “Muambieni kwamba siku hiyo atakuwa kijana na ataingia Peponi.” Kisha akasoma Aya ifuatayo kutoka kwenye Qur’ani Tukufu:

إِنَّا أَنْشَأْنَاهُنَّ إِنْشَاءً {35}

فَجَعَلْنَاهُنَّ أَبْكَارًا {36}

عُرُبًا أَتْرَابًا {37}

لِأَصْحَابِ الْيَمِينِ {38}

“Hakika tumewafanya wakuwe katika umbo (jipya), na tumewafanya vijana kama kwamba ndiyo kwanza wanaolewa, wanapendana na waume zao (walio) hirimu moja na wao, kwa ajili ya watu wa kheri. (56: 35 38).

Katika Hadithi nyingine inayokubaliwa na wote ninyi na sisi, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Wakati wakazi wa Peponi watakapoingia Mbinguni, watakuwa vijana na nyuso safi halisi, nywele za kipilipili, macho ya haiba, umri wa miaka 33.”

Sheikh: Maelezo yako ni kweli kama yalivyo, lakini hii ni hadithi Makhususi (yaani maalumu kwa ajili ya Abu Bakr na Umar).

Muombezi: Sielewi. Una maana gani kwa kusema “Hadith Makhususi.” Una maana kwamba Allah atapeleka kikundi cha wazee Peponi ili kwamba Abu Bakr na Umar waweze kuwa mabwana zao? Isitoshe, ulamaa wenu mashuhuri wanaiona Hadith hii kuwa ni ya kutungwa. Mtume ametupa utaratibu kwa ajili ya kuthibitisha Hadithi.
Nilisema mapema kwamba Hadithi yoyote ambayo haipatani na Qur’ani ni ya kupuuzwa. Wanachuoni wetu sisi wanakataa Hadithi nyingi zinazodaiwa kutokana na Mtume na Maimamu Watukufu katika misingi ya kanuni iliyotamkwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.):

“Wakati wowote itakapoelezwa Hadith kwamba inatoka kwangu, irejesheni kwenye Qur’ani Tukufu; kama inakubaliana nayo, ikubalini, vinginevyo, ikataeni”.

Kwa ajili hiyo, wanachuoni wetu hawakubali hadith ambazo hazikubaliani na Qur’ani Tukufu. Nilieleza mapema kwamba Maulamaa wenu wameandika vitabu juu ya kukataa Hadithi za kutungwa.

Kwa mfano Sheikh Majdu’d-Din Muhammad bin Yaqub Firuzabadi katika “Safarus- Sa’ada” (uk. 142), Jalalu’d-Din Suyuti katika “Kitabu’l-Lu’ali”, Ibn Jauzi katika “Muzu’a”, Muqaddasi katika “Tadhkiratu’l-Muzu’a”, na Sheikh Muhammad bin Darwish (Mashuhuli kwa jina la Hul-e-Beiruti) katika “Asna’l-Talib” - wote wamesema kwamba nyororo ya wasimuliaji wa hadith isemayo kwamba Abu Bakr na Umar ni mabwana wa wazee wa peponi humchanganya Yahya bin ‘Anbasa. Dhahabi anasema kwamba, “huyu Yahya ni msimuliaji asiyeaminika, na Ibn Jan anashikilia kwamba Yahya alikuwa akitunga hadithi.”

Hivyo, mbali na hoja zangu zilizopita, hata Maulamaa wenu wanaiona kuwa ni hadithi ya uwongo. Kwa kweli, inawezekana kwamba ilitungwa na wafuasi wa Abu Bakr, familia ya Umayya. Ili kuwadhalilisha Bani Hashim na kizazi cha Mtume, walikuwa wakitunga Hadith sambamba na zile sahihi zilizosimuliwa kwa kuitukuza familia ya Mtume.

Mtu kama Abu Huraira, ili kupata mwanya wa kuingia kwenye kundi maalum la kiutawala la Bani Umayya, mara kwa mara alighushi hadithi.

Kwa sababu ya uadui wao kwa kizazi cha Mtume, walitunga hadithi sambamba na zile zinazokubaliwa na Maulamaa wote wa Shi’a na Sunni.

Nawab: Ni Hadithi ipi inayokubaliwa katika suala hili?

Hadith Ya Kwamba Hasan Na Husein Wote Ni Mabwana Wa Vijana Wa Peponi.

Muombezi: Hadith iliyo Sahihi ni kwamba Mtume alisema: “Hasan na Husein ni mabwana wa vijana wa peponi, na baba yao ni mbora zaidi yao.” Maulamaa wengi wamesimulia Hadith hii. Kwa mfano Khatib Khawarizmi katika “Manaqib”, Mir Seyyid Ali Abu Abdu’r-Rahman Nisai katika “Khasa’is-il-Alawi” (hadithi tatu), Ibn Sabbagh Maliki kati- ka “Fusulu’l-Muhimma”, uk. 159, Sulaiman Balki Hanafi katika “Yanabiu’l-Mawadda”, Sura ya 54, Sibt Ibn Jauzi katika “Tadhkira”, akinukuu kutoka kwa Tirmidhi, Ibn Maja na Imam Ahmad Hanbal, Sibt Ibn Jauzi katika uk. 133 wa “Tadhkiratul-Mawadda,” Imam Ahmad bin Hanbal katika Musnad, Tirmidhi katika “Sunan” na Muhammad bin Yusufu Ganji Shafi’i katika “Kifayatu’l-Talib” Sura ya 97, wameandika hadithi hii na huyu wa mwisho akaongeza kwamba, msimuliaji mkubwa wa hadith, Imam Abdu’l-Qasim Tibrani, vilevile ameiandika Hadith hii katika “Mu’ajamu’l-Kabir” na akaorodhesha wasimuliaji wake mbalimbali wote, kama vile Amir’l-Mu’minina Ali, Umar bin Khattab (Khalifa wa Pili), Hudhaifa Yamani, Abu Sa’id Khudri, Jabir bin Abduullah Ansari, Abu Huraira, Usama bin Zaid, na Abdullah bin Umar.

Baada ya hapo. Muhammad bin Yusufu amesema kwamba ni hadith sahihi isiyo na ubis- hani. Kutovunjika muala wa nyororo ya wasimuliaji wa hadith hii ni uthibitisho wa kuwa kwake Sahihi. Aidha, Hafidh Abu Nu’aim Isfahani katika “Hilyatu’l-Auliya” Ibn Asakir katika “Tarikh Kabir” Jz. 4, uk. 206, Hikam katika “Mustadrak”, Ibn Hajar Makki katika “Sawa’iq-Muhriqa” - kwa ufupi, Maulamaa wenu mashuhuri wote wamethibitisha usahihi wa hadith hii.

Sheikh: Lakini hebu angalia hadith hii, ambayo usahihi wake hakuna atakayeukataa. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Katika taifa lolote atakaloishi Abu Bakr, sio sahihi kwa mtu yoyote kufadhilishwa kuliko yeye.” Hadithi hii inathibitisha kwamba Abu Bakr ni bora kwa Umma wote.

Muombezi: Nasikitika kwamba unakubali hadith bila udadisi hata kidogo. Hadith hii ingelikuwa imesimuliwa na Mtume, yeye mwenyewe angetenda kwa mujibu wake.
Lakini alitoa kipaumbele kwa Ali mbele ya macho ya Abu Bakr. Je, Abu Bakr hakuwepo wakati wa Mubahila pale ambapo Ali alichaguliwa kama nafsi ya Mtume? Katika vita vya Tabuk, wakati Abu Bakr mtu mzima na mzoefu zaidi alikuwepo, kwa nini Mtume akamfanya Hadhrat Ali naibu na Khalifa wake?

Kwa nini Abu Bakr aliondolewa kwa amri ya Mungu na kupendelewa Ali, wakati mtu mzima huyu alipotumwa kwenda Makka kulingania Uislamu na kuzisoma Aya kutoka Sura ya tisa ya Qur’ani “Baraat (Tawba)?” Wakati Abu Bakr alikuwepo kwa nini Mtume alimchukua Ali kwenda pamoja naye Makka kuvunja Masanamu, akamfanya apande juu ya mabega yake, akimuamrisha avunje sanamu la Hubal? Kwa nini wakati Abu Bakr alikuwepo Mtume akamtuma Ali kwenda kuhubiri miongoni mwa watu wa Yemen? Mwisho, kwa nini Mtume akamfanya Ali kuwa Mrithi na Makamu wake badala ya Abu Bakr?

Sheikh: Kuna hadithi yenye nguvu sana kutoka kwa Mtume ambayo haiwezi kupingwa. Imesimuliwa na Amr bin Aas ambaye amesema: “Siku moja nilimuuliza Mtume. ‘Ewe Mtume wa Allah! Ni nani unayempenda sana miongoni mwa wanawake?’

Akajibu: ‘Aisha.’ Nikasema: ‘Nani unayempenda sana miongoni mwa wanaume?’ Akajibu, ‘Baba yake Aisha, Abu Bakr.’” Kwa vile Mtume amempendelea Abu Bakr juu ya watu wote, basi alikuwa mbora kwa umma wote. Ukweli huu wenyewe, peke yake ni uthibitisho wenye kuvutia zaidi wa kuonyesha uhalali wa ukhalifa wa Abu Bakr.

Majibu Kwa Hadith Inayodhaniwa Kwamba Abu Bakr Na Aisha Walipendelewa Zaidi Na Mtume.

Muombezi: Mbali na ukweli kwamba hadithi hii imetungwa na wafuasi wa Abu Bakr, haipatani na Hadith Sahihi ambazo zinakubaliwa na Madhehebu zote. Hadith hii inapasa kuangaliwa kwa mitazamo miwilii. Kutoka upande wa Ummu’l-Mu’minina Aisha na kutoka upande wa Abu Bakr. Mtume asingeweza kusema kwamba kati ya wanawake wote alimpenda Aisha zaidi. Nimekwisha sema tangu mwanzo kwamba hii inakinzana na Hadithi nyingi Sahihi zilizomo kwenye vitabu vyote vya Sunni na Shia.

Sheikh: Ni hadithi zipi zinazopingana na riwaya hii?

Muombezi: Kuna hadithi nyingi kuhusu Mama wa Maimamu; Fatima Zahra, zilizosimuli- wa na Maulamaa wenu wenyewe, ambazo zinapingana na maelezo yako. Hafidh Abu Bakr Baihaqi katika Kitabu chake cha “Ta’rikh”, Hafidh Ibn Abdu’l-Bar katika “Isti’ab”, Mir Seyyid Ali Hamadani katika “Mawaddatu’l-Qurba”, na wengine miongoni mwa Maulamaa wenu, wamesimulia kwamba Mtume mara kwa mara amesema: “Fatima ni mbora wa wanawake wote na wa umma wangu.”.

Imam Ahmad bin Hanbal katika “Musnad”, na Hafidh Abu Bakr Shirazi katika “Nuzulu’l- Qur’ani Fi Ali” anasimulia kutoka kwa Muhammad bin Hanafiyya, na yeye kutoka kwa Amirul-Mu’minina Ali, Ibn Abdu’l-Bar katika “Isti’ab”, katika maelezo juu ya Fatima, yaliyosimuliwa katoka kwa Ummu’l-Mu’minina Khadija, kutoka kwa Abdu’l-Warith Bin Sufyani na kutoka kwa Abu Dawud na Anas Bin Malik, Sheikh Sulaimani Balkhi Hanafi katika Sura ya 55 ya “Yanabiu’l-Mawadda”, Mir Seyyid Ali Hamadani katika “Mawaddatu’l-Qurba”, Mawadda ya 13 - hawa na wasimuliaji wengine wa Hadith wameelezea kutoka kwa Anas Bin Malik kwamba, Mtume alisema:

“Kuna wanawake wanne walioshinda wote wa ulimwengu: Mariam, bint wa Imran; Asiya, bint wa Mazahim; Khadija, bint wa Khalid; na Fatima, binti wa Muhammad”.

Khatib katika “Ta’rikh Baghdad;” anasimulia kwamba Mtume aliwatangaza wanawake hawa wanne kuwa ni wabora wa wanawake wote wa ulimwengu. Kisha akamtangaza Fatuma kuwa ni mbora wao wote ulimwenguni na Akhera.

Muhammad bin Ismaili Bukhari katika “Sahihi” yake, na Imam Ahmad bin Hanbal katika “Musnad” yake wanasimulia kutoka kwa Aisha bint Abu Bakr kwamba Mtume alisema kumwambia Fatima:

“Ewe Fatima, ninakupa habari njema kwamba Allah amekufanya mbora wa wanawake wote duniani na amekufanya wewe kuwa ndiye mtakatifu zaidi wanawake wote wa Uislamu.”.
Vilevile Bukhari katika “Sahihi” yake, sehemu ya 4, uk. 64 Muslim katika Sahih yake Jz. 2, katika Mlango wa “Fadhail za Fatima,” Hamidi katika “Jam’a Bainus-Sahihain” yake, Abdi katika “Jam’a Bainus-Sihahu-s-Sitta” hawa na wengine wengi wamesimulia kutoka kwa Ummu’l-Mu’miniina Aisha kwamba Mtume alisema: “Ewe Fatima! hufurahi kwam- ba wewe ni Bibi wa wanawake wote wa ulimwengu?”

Ibn Hajar Asqalani amenukuu maneno hayo hayo katika kitabu chake “Isaba” kuhusiana na maisha ya Fatima pamoja na maelezo: “Wewe ni mbora wa wanawake wote wa ulimwengu.”

Vilevile, Bukhari, Muslim, Imam Ahmad Bin Hanbal, Tibrani na Sulaiman Balkhi Hanafi - wote wameiandika hadith hii.

Aya Juu Ya Mapenzi Kwa Familia Ya Mtume.

Kwa nyongeza, Bukhari na Muslim; kila mmoja katika Sahih yake, Imam Tha’labi katika Tafsir yake, Imam Ahmad bin Hanbal katika “Musnad”, Tibrani katika Mu’jamu’l-Kabir, Sulaimani Balkh Hanafi katika “Yanabiu’l-Mawadda”, Sura ya 32 kutoka kwenye “Tafsir” ya Ibn Abi Hatim, “Manaqib” ya Hakim, Wasit na Wahidi, “Hilyatu’l-Auliya” cha Hafidh Abu Nu’aim Isfahani na Fara’id ya Hamwaini, Ibn Hajar Makki katika “Sawa’iq, Muhriqa” chini ya Aya ya 14 kwa idhini ya Ahmad, Muhammad bin Talha Shafi’i katika “Mutalibus-Su’ul” uk. 8, Tabari katika Tafsir, Wahidi katika Asbabun-Nuzul, Ibn Maghazil katika “Manaqib”, Muhibu’d-Din Tabari katika “Riyazu’n-Nuzra”, Mu’min Shablanji kati- ka “Nuru’l-Absar,” Zamakhshari katika “Tafsir”, Imam Fakhru’d-Din Razi katika “Tafsir Kabir”, Sayyid Abu Bakr Shahabu’d-Din Alawi katika “Rishfatus-Sadi min Bahr-e- Faza’il-e-Baniu’l-Nabi’i’l-Hadi” Sura ya 1 uk. 22 –23 kutoka “Tafsir” ya Baghawi, “Tafsir” ya Tha’labi, “Manaqib” ya Ahmad, “Tafsir Kabir” na “Ausat” vya Tibrani na Sadi, Sheikh Abdullah bin Muhammad bin Amir Shabrawi Shafi’i katika “Al-Ittihaf” uk.5 kutoka kwa Hakim, Tibrani na Ahmad, Jalalu’d-Din Suyuti katika “Ihya’u’-l-Mayyit” kutoka Tafsir za Ibn Mudhir, Ibn Abi Hatim, Ibn Mardawaih, na “Mu’jamu’l-Kabir” cha Tibrani; na Ibn Abi Hatim na Hakim - kwa ufupi, wengi wa maulamaa wenu mashuhuri (ukiondoa wafusi wachache wa Bani Umayya na maadui wa Ahlul Bait), wamesimulia kutoka kwa Abdullah bin Abbas na wengine, kwamba wakati Aya ifuatayo ya Qur’ani Tukufu ilipoteremshwa:

“Sema: Siombi malipo yoyote kwa haya bali mapenzi kwa jamaa zangu; na anayefanya wema tutamzidishia wema…” (42:23).

Kikundi cha Masahaba wakauliza, “Ewe Mtume wa Allah! ni nani hao jamaa zako ambao mapenzi kwao yamefanywa wajibu juu yetu na Allah?” Mtume Akajibu, “Ni Ali, Fatima, Hasan na Husein.” Baadhi ya Hadith zina maneno, “na watoto wao” yaani watoto wa Hasan na Husein.

Kukubali Kwa Shafi’i Kwamba Mapenzi Kwa Ahlu Bait Ni Wajibu.

Hata Ibn Hajar (mtu shupavu sana asiye mvumilivu) katika kitabu chake “Sawa’iq-Muhriqa” uk. 88, Hafidh Jamalu’d-Din Zarandi katika “Mi’raju’l-Rasul”, Sheikh Abdullah Shabrawi katika “Kitabu’l-Ittihaf”, uk. 29, Muhammad Bin Ali Sabban wa Misir katika “As’afu’r-Raghibin”, uk. 119, na wengine wamesimulia kutoka kwa Imam Muhammad Bin Idris Shafi’i, ambaye ni mmoja wa Maimamu wenu wanne na kiongozi wa kidini wa madhehebu ya Shafi’i, kwamba alikuwa akisema:

“Enyi Ahli Bait wa Mtume wa Allah! Mapenzi kwenu yamefanywa wajibu kwetu na Allah kama ilivyokuja katika Qur’ani Tukufu (akirejea aya iliyotajwa hapo juu).

Inatosha kwa hadhi yenu kwamba, kama mtu hatatoleeni salamu katika Sala, Sala yake haitakubaliwa.” Sasa ninakuuliza, inawezekana hadithi ya upande mmoja iliyoelezwa na wewe ikasimama dhidi ya Hadith zote hizi Sahihi ambazo zimekubaliwa na madhehebu yote ya Sunni na Shia?

Dhana Potofu Kuhusu Mapenzi Ya Mtukufu Mtume (S.A.W.W.) Kwa Aisha.

Kuhusu mapenzi ya Mtume kwa Aisha, unafikiri kwamba kwa sababu ya matamanio yake ya kimwili alimpenda Aisha zaidi kuliko Fatima?
Ni kweli kwamba Aisha alikuwa mke wake na kwa hiyo ni Ummu’l-Mu’minina (Mama wa Waumini) kama wake wengine wa Mtume. Lakini je, inakubalika kwamba alimpenda Aisha zaidi kuliko alivyompenda Fatima, ambaye mapenzi kwake yamefanywa wajibu katika Qur’ani Tukufu, ambaye kwa ajili yake iliteremshwa aya ya utakaso na ambaye alijumuishwa kwenye Mubahila? Hakika unajua kwamba Mtume na warithi wake hawakushawishiwa na matamanio ya kimwili, na kwamba walimgeukia Allah peke yake.

Kujifunga huku kulikuwa kwa makhususi kabisa ni halisi hasa kwa yeye mwisho wa Mitume. Aliwapenda wale ambao Allah aliwapenda. Je, yapasa sisi kuzikataa hadithi hizi sahihi ambazo zimekubaliwa na Maulamaa wa madhehebu zote, na ambazo zinakubaliana na Aya za Qur’ani Tukufu, au tuichukulie Hadith ambayo umesimulia hivi punde tu kuwa ni ya kutungwa? Unadai kwamba Mtume amesema alimpenda Abu Bakr zaidi kuliko mtu mwingine yoyote. Lakini dai hili vilevile liko mbali na hadithi Sahihi nyingine nyingi ambazo zimesimuliwa na Maulamaa wenu wenyewe, ambao wamesisitiza kwamba, kwa mujibu wa Mtume, mtu aliyependwa sana alikuwa ni Ali.

Mtukufu Mtume (S.A.W.W.) Alimpendelea Ali Kuliko Watu Wengine Wote.

Sheikh Suleiman Balkhi katika “Yanabiu’l-Mawadda”, Sura ya 55, anasimulia kutoka kwa Tirmidhi hadith ya Buraida kwamba, kwa mujibu wa Mtume, mwanamke aliyependwa zaidi alikuwa ni Fatima na mwanaume aliyependwa zaidi sana alikuwa ni Ali. Muhammad bin Yusuf Ganji Shafi’i katika “Kifayatut-Talib” Sura ya 91, anaandika kutoka kwa Ummu’l-Mu’minina Aisha kwamba alisema: “Allah hakuumba mtu yeyote ambaye Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimpenda zaidi kuliko Ali.”

Anaongeza kusema kwamba, hii ndio hadith ambayo Ibn Jarir katika Manaqib yake na Ibn Asakir Damishqi katika tarjuma yake wameisimulia kutoka kwa Ali.

Muhyi’d-Din na Imamu’l-Haramain Ahmad Bin Abdullah Shafi’i wanasimulia kutoka kwa Tirmidhi katika “Dhakha’iru’l-Uqba” kwamba watu walimuuliza Aisha ni mwanamke yupi aliyekuwa anapendwa zaidi na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), na yeye akajibu, “Fatima.” Kisha aliulizwa kuhusu mwanaume aliyependwa zaidi na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na akajibu, “Ni mume wake, Ali bin Abu Talib.” Tena alisimulia kutoka “Mukhalis” cha Dhahabi, na Hafidh Abu’l-Qasim Damishqi na yeye kutoka kwa Aisha kwamba alisema yeye Aisha: “Sijaona mwanaume aliyependwa zaidi na Mtume kuliko Ali, wala mwanamke aliyependwa zaidi kama Fatima.”

Kwa nyongeza, Sheikh huyu anasimulia kutoka kwa Hafidh Khajandi na yeye kutoka kwa Ma’azatu’l-Ghifariyya kwamba alisema: “Nilikwenda kuonana na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwenye nyumba ya Aisha ambapo Ali alikuwa nje ya nyumba hiyo. Mtume akamuambia Aisha, “Huyu (Ali) ndiye kipenzi mno kwangu na mwenye kuheshimika zaidi miongoni mwa wanaume wote, Tambua haki yake na mpe heshima kwa cheo chake.”

Sheikh Abdullah bin Muhammad bin Amir Shabrawi Shafi’i ambaye ni mmoja wa Maulamaa wenu mashuhuri, ameandika katika “Kitabu’l-Ittihaf bi Hubbi’l-Ashraf,” uk. 9, Sulaiman Balkhi katika “Yanabiu’l-Mawadda” na Muhammad bin Talha Shafi’i katika Matalibus-Su’ul, uk. 6, kutoka kwa Tirmidhi, na yeye kutoka kwa Jami bin Umar - wote wamesimulia ifuatavyo: “Nilikwenda kwa Ummu’l-Mu’minina Aisha pamoja na shangazi yangu (dada yake baba), na tulimuuliza, ni nani ambaye alikuwa akipendwa zaidi na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Yeye alijibu, ‘Miongoni mwa wanawake alikuwa ni Fatima na miongoni mwa wanaume, ni mumewe Ali bin Abi Talib.’” Hadithi hii hii imesimuliwa na Mir Sayyid Ali Hamadani Shafi’i katika “Mawaddatu’l-Kurba” Mawadda ya 2, pamoja na tofauti kidogo kwamba Jami bin Umar alisema kwamba alipokea jibu hili kutoka kwa shangazi yake.

Halikadhalika, Khatib Khawarizmi amesimulia hadithi hii kutoka kwa Jami bin Umar, na yeye kutoka kwa Aisha mwishoni mwa sura ya 4 ya Manaqib yake, Ibn Hajar Makki, kati- ka “Sawa’iq Muhriqa”, kuelekea mwishoni mwa sura ya 2, baada ya kuandika hadithi 40 juu ya fadhila za Ali, anasimulia hadith ifuatayo kutoka kwa Aisha: “Miongoni mwa wanawake, Fatima alikuwa ndiye mwanamke aliyependwa zaidi na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), na miongoni mwa wanaume ni mume wake.”

Muhammad bin Talha Shafi’i, katika “Matalib-us-Su’ul”, uk. 7, baada ya ya kuandika Hadith mahususi mbali mbali juu ya suala hili, anaelezea hitimisho lake mwenyewe katika maneno yafuatayo: “Hadith hizi sahihi na zisizokifani huthibitisha kwamba Fatima alikuwa mwenye kupendwa zaidi na Mtume kuliko wanawake wote.

Ni mwenye cheo cha juu zaidi ya wanawake wote wa Peponi na pia wa mbele zaidi juu ya wanawake wa Madina.” Hadithi hizi za kuaminika, kwa uwazi zinathibitisha kwamba katika viumbe wote, Ali na Fatima walikuwa ndio wenye kupendwa zaidi na Mtume. Uthibitisho mwingine wa Mtume kumpendekeza zaidi Ali kuliko wanaume wengine ni ile “Hadith ya Ndege” (Hadith-e-Ta’ir). Hadithi hii inajulikana sana na kukubaliwa sana kiasi kwamba hatuhitaji kutaja vyanzo vyake vyote. Nitataja tu baadhi ya hivyo.

Hadithi Ya Ndege Aliyebanikwa:

Wengi wa ulamaa wenu, kama Bukhari, Muslim, Tirmidhi, Nisa’i, na Sijistani katika “Sahih” zao, Imam Ahmad bin Hanbali katika “Musnad” yake, Ibn Abi’l-Hadid katika Sherhe yake ya “Nahju’l-Balagha”, Ibn Sabbagh Maliki katika “Fusulu’l-Muhimma,” na Sulaiman Balkhi Hanafi katika “Yanabiu’l-Mawadda,” Sura ya 8, na kundi la waandishi wengine waaminifu wameiandika “Hadith-e-Ta’ir” katika vitabu vyao. Wanathibitisha kwamba hadithi hii ilielezewa na wasimuliaji wa Hadith 24, kutoka kwa Anas bin Maliki. Ibn Sabbagh Maliki katika “Fusulu’l-Muhimma” anaandika kuhusu hadith hii katika maneno haya: “Katika vitabu vya Hadith Sahihi na riwaya za kuaminika, Hadith-e-Ta’ir, kutoka kwa Anas bin Malik ni haipingiki.” Sibt Ibn Jauzi, katika uk. wa 23 wa kitabu chake “Tadhkira” na “Sunan” ya Tirmidhi na Mas’udi katika uk. wa 49 juzuu ya 2 ya “Muruju’dh-Dhahab”, wameangalia hususan katika sehemu ya mwisho ya hadithi hii ambayo ina dua ya Mtume na kukubaliwa kwake na Allah.

Imam Abdu’r-Rahman Nisa’i katika hadith ya tisa katika kitabu chake “Khasa’isu’l-Alawi” na Hafidh Bin Iqda na Muhammad bin Jarir Tabari, wote wamerejea kwenye nyororo isiyokatika ya wasimuliaji na kwenye vyanzo sahihi vya hadith hii, wakisema kwamba ilisimuliwa na masahaba 35 wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kutoka kwa Anas bin Malik.

Kwa ufupi, Maulamaa wenu wote mashuhuri wamethibitisha usahihi wa hadith hii na wameijumuisha kwenye vitabu vyao. Allama Sayyid Hamid Husain ameweka juzuu nzima ya kitabu chake “Abaqatu’l-Anwar” kwa ajili ya Hadithi hii tu. Alikusanya vyanzo vyote vya kuaminika kutoka kwa Maulamaa wenu mashuhuri na kwa wazi kabisa akathibitisha usahihi wa hadith hii.

Kwa mujibu wa Hadith hii, siku moja mwanamke mmoja alileta zawadi ya ndege aliyebanikwa kwa Mtume. Kabla ya kumla, Mtume akiwa amenyoosha mikono yake juu, akamuomba Allah hivi: “Ee Allah! Kati ya viumbe wako wote, mlete mtu ambaye ni mpenzi zaidi kwako na kwangu, ili kwamba ale pamoja nami ndege huyu wa kubanikwa.” Ndipo Ali akaingia ndani akala ndege yule wa kubanikwa pamoja na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Baadhi ya vitabu vyenu, kama vile “Fusulu’l-Muhimma” cha Malik, “Ta’rikh” cha Hafidh Nishapuri, “Kifayatut-Talib” cha Ganji Shafi’i na “Musnad” ya Ahmad Bin Hanbal, n.k. ambamo Hadith hii imesimuliwa kutoka kwa Anas bin Malik, vimeandikwa kwamba Anas bin Malik alisema “Mtume alikuwa bado hajamaliza dua yake wakati Ali alipoingia nyum- bani pale, lakini nikamficha jambo lile. Wakati Ali alipoingiza mguu wake mara ya tatu, Mtume akiniamrisha nimuache aingie ndani. Wakati Ali alipoingia Mtume akasema: “Baraka za Allah ziwe juu yako; ni kitu gani kimekuleta kuja kwangu? Ali akamueleza kwamba alikuja kwake mara tatu lakini aliruhusiwa kuingia safari hii tu. Mtume akaniuliza ni kitu gani kimenifanya niwe hivyo, na nikajibu: “Ukweli ni kwamba, niliposikia dua yako, nilitamani kwamba heshima hii ingekwenda kwa mmoja wa kabila langu.” Sasa nakuulizeni enyi waungwana iwapo dua ya Mtukufu Mtume ilikubaliwa au kukataliwa na Allah.

Sheikh: Ni wazi Allah aliikubali kwa vile aliahidi katika Qur’ani tukufu kwamba angekubali dua ya Mtume. Aidha, Allah alijua kwamba Mtume asingeweza kuomba dua isiyofaa. Hivyo Allah aliyakubali maombi yake kila wakati.

Muombezi: Allah alimpeleka Ali, mtu anayestahiki zaidi katika viumbe Wake, kwa Mtume. Wanachuoni wenu wenyewe wamethibitisha tukio hili. Muhammad bin Talha Shafi’i katika Kitabu chake “Matalib-Us-Su’lu”, Sura ya 1, sehemu ya 5, uk. wa 15, amethibitisha cheo cha juu cha Ali kama mwenye kupendwa zaidi na Allah na Mtume juu ya msingi wa “Hadith ya Bendera (Riyat)” na “Hadith ya Ndege.”

Katika kuhusiana na hilo anasema: “Nia ya Mtume ilikuwa kwamba watu waelewe cheocha kipekee na cha hali ya juu cha Ali, ambaye alifikia upeo wa juu zaidi wa kuweza kufikiwa na wacha Mungu.”

Vilevile Hafidh na Muhammad bin Yusufu Ganji Shafi’i (aliyekufa 658 A.H.) anaandika katika kitabu chake, Kifayatut-Talib Sura ya 33, akizungumzia fadhila za Ali ibn Abi Talib, kwamba hadith hii kwa uwazi kabisa inathibitisha kwamba Ali alikuwa kipenzi sana katika viumbe kwa Allah.

Baadae anasema kwamba Hakim Abu Abdullah Hafidh Nishapuri ameisimulia hii “Hadith-e-Ta’ir” ya Anas kutoka wasimuliaji 86 na vile vile akaandika na majina ya wasimuliaji wote 86 (Tazama Kifayatut-Talib, Sura ya 32). Ile hadith ambayo umenukuu wewe, ukiilinganisha na Hadith zilizosimuliwa na Maulamaa wenu wa daraja za juu (isipokuwa washupavu wakorofi wachache), haiwezi kutegemewa na ingekataliwa na watu wenye elimu.

Sheikh: Nina wasiwasi kwamba umeamua kwa akili yako kutokubali tunayo yasema.

Muombezi: Unawezaje kuhusisha chuki kama hizo kwangu? Unaweza ukatoa mfano mmoja tu ambapo umetoa hoja yenye nguvu na mimi bila sababu nikaikataa? Ninaapa kwamba katika mijadala ya kidini na Mayahudi, Wakristo, Wahindu na Wabrahmin na Mabahai wasio na elimu wa Iran, Makadian wa India na wayakinifu (wenye kuamini vitu vyenye kuonekana, kugusika na kuhisiwa tu) – katika hali zote hizi mimi sijawahi kufanya ukaidi katika hoja zangu. Kamwe sijawahi kuwa mbishi kwa makafir hawa – vipi nitaweza kufanya hivyo kwenu ninyi, ndugu zangu katika Uislamu?

Sheikh: Tumesoma maelezo ya mjadala wako na Wahindu na Wabrahmin wa Lahore katika magazeti. Tulivutiwa mno na maelezo hayo. Ingawa tulikuwa hatujakutana na wewe, tulijisikia tumeungana na wewe kimaadili. Natumaini kwamba Allah atakuongoza wewe na sisi kwenye njia iliyonyooka. Tunaamini kwamba kama kuna wasiwasi wowote kuhusu Hadith fulani, inatupasa, kwa mujibu wa ushauri wako, kuirejesha kwenye Qur’ani Tukufu.

Hata hivyo, kama unahoji ubora wa khalifa Abu Bakr na muundo wa ukhalifa wa makhalifa wakubwa, na kama utaziona hadith kuwa ni zenye mashaka, je, utasita vilevile kuamini hoja ambayo imetegemea juu ya Qur’ani Tukufu?

Muombezi: Allah asitujaalie siku tutakayotilia shaka ukweli uliotegemea juu ya Qur’ani Tukufu au Hadith Sahihi. Walakini, wakati tutakapokuwa tumeingia kwenye mjadala wa kidini na Taifa lolote au Jumuiyya, wao vilevile wanahoji kutoka kwenye Aya za Qur’ani Tukufu kuthibitisha mtazamo wao. Kwa vile Aya za Qur’ani zina daraja mbalimbali za maana, Mtume wa mwisho, ili kuwalinda watu dhidi ya kutoelewana, hakuiacha Qur’ani kama chanzo pekee tu cha mwongozo.

Kama inavyokubaliwa na madhehebu zote (Shia na Sunni), yeye mwenyewe (Mtume) alisema: “Nawaachieni vitu viwili vizito: “Kitabu cha Allah (Qur’ani) na kizazi changu. Kama mtashikamana na viwili hivi, kamwe, hamtapotea baada yangu. Hakika viwili hivi kamwe havitatengana mpaka vinifikie kwenye chemchem ya Kauthar.”

Kwa sababu hii, maana ya ufunuo wa Qur’ani Tukufu yapasa itafutwe ama kutoka kwa Mtume, fasir mkuu wa Qur’ani Tukufu, au baada yake, kutoka kwa wale walio sawa na Qur’ani Tukufu, dhuria watukufu wa Mtume. Qur’ani Tukufu inasema: “Basi waulizeni wenye kumbukumbu ikiwa ninyi hamjui.” (21:7).

“Watu Wenye Kumbukumbu” Ni Ahli Muhammad Dhuria Wa

Mtukufu Mtume (S.A.W.W.).

Ahlu’dh-Dhikr maana yake watu wenye kumbukumbu, ambao ni Ali na Maimamu watukufu, kizazi chake, ambao wako sawa na Qur’ani. Sheikh Sulaiman Balkhi Hanafi katika kitabu chake “Yanabiu’l-Mawada”, Sura ya 39, akinukuu kutoka “Tafsir-e-Kasfu’l- Bayan” ya Imam Tha’labi, anasimulia kutoka kwa Jabir Ibn Abdullah Ansari, ambaye amesema:
“Ali amesema: ‘Sisi dhuria wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ni watu wa kumbukumbu.’” Kwa vile “Dhikr, Kumbukumbu”, ni moja ya majina ya Qur’ani Tukufu, familia hii inajumuisha na watu wa Qur’ani.

Kama ilivyoelezwa na Maulamaa wa kwenu na wa kwetu, Ali amesema: “Niulizeni kitu chochote mnachotaka kabla sijakuacheni. Niulizeni kuhusu Kitabu kitukufu (Qur’ani) kwa vile ninajua kuhusu kila Aya ndani yake – iwe imeteremshwa wakati wa usiku au wakati wa mchana, katika tambarare au katika milima. Kwa jina la Allah, hakuna Aya ya Qur’ani Tukufu iliyoteremshwa bali najua iliteremshwa kuhusu nini.

Allah (S.w.t.) amenijaalia mimi kuwa na ulimi fasaha na akili yenye busara.” Kwa hiyo, kutegemeza hoja juu ya Aya za Qur’ani tukufu, yapasa iwe kwa mujibu na maana yake sahihi na tafsir iliyotolewa na wale wenye uwezo wa kutoa tafsir ya kuaminika. Vinginevyo, kila mtu atatoa tafsir yake ya Aya za Qur’ani, kwa mujibu wa upeo wa elimu yake na imani, na hii itaishia tu kwenye hitilafu za maoni na mgongano wa mawazo. Pamoja na hoja hii katika akili, naomba usome hizo Aya zako.

Aya Za Qur’ani Tukufu Kuhusu Kuchaguliwa Kwa Makhalifa Wanne,

Na Majibu.

Sheikh: Allah anasema kwa uwazi katika Qur’ani Tukufu:

مُحَمَّدٌ رَسُولُ اللَّهِ ۚ وَالَّذِينَ مَعَهُ أَشِدَّاءُ عَلَى الْكُفَّارِ رُحَمَاءُ بَيْنَهُمْ ۖ تَرَاهُمْ رُكَّعًا سُجَّدًا يَبْتَغُونَ فَضْلًا مِنَ اللَّهِ وَرِضْوَانًا ۖ سِيمَاهُمْ فِي وُجُوهِهِمْ مِنْ أَثَرِ السُّجُودِ ۚ{29}

“Muhammad ni Mtume wa Allah, na walio pamoja naye ni wenye nyoyo thabiti mbele ya makafiri, na wenye kuhurumiana wao kwa wao, utawaona wakiinama kwa kurukuu na kusujudu (katika Sala), wakitafuta fadhila za Allah na radhi (yake). Alama zao ni katika nyuso zao kwa taathira (athari) ya kusujudu…” (48:29).

Kwanza Aya hii huthibitisha ubora wa Abu Bakr. Pili huonyesha nafasi za makhailfa wanne kinyume na inavyodaiwa na madhehebu ya Shi’a kwamba Ali alikuwa Khalifa wa kwanza. Aya hii bila ubishani inaelezea kwamba Ali alikuwa Khalifa wa nne.

Muombezi: Hakika Aya hii haitoi dalili yoyote ya wazi kuhusu namna ya kuchaguliwa makhalifa au kuhusu ubora wa Abu Bakr. Kwa hiyo, lazima uonyeshe ni sehemu ipi katika Aya hii ambapo maana hiyo imefichwa.

Sheikh: Mwanzoni mwa Aya hii, usemi (usemao) “na walio pamoja naye” huashiria kwa yule mtu maarufu ambaye alikuwa na Mtume ‘usiku wa pango.’

Utaratibu wa kupokezana nafasi ya ukhalifa pia iko wazi katika aya hii. “Walio pamoja naye” ina maana ya Abu Bakr, ambaye alifuatana na Mtume kwenye Pango la Thawr katika usiku wa Hijra. Usemi, “wenye nyoyo thabiti mbele ya makafir” maana yake ni Umar Bin Khattab, ambaye alikuwa mkali sana kwa makafir. Usemi, “wenye kuhurumiana wao kwa wao” huashiria kwa Uthman bin Affan, ambaye alikuwa mpole sana.” Usemi, “alama zao ni katika nyuso zao kwa athari ya kusujudu” huashiria kwa Ali. Ni wazi kwamba Ali ni Khalifa wa nne, sio wa kwanza, kwa vile Allah amemtaja katika sehemu ya nne.

Muombezi: Nashangaa vipi nitaweza kujibu ili kwamba nisije nikalaumiwa kwa kujipendelea mwenyewe. Hakuna tafsir za Qur’ani, ukichukua pamoja na zile za maulamaa wenu wakubwa, ambazo zimetafsiri maneno haya kama ulivyofasili wewe. Aya hii ingekuwa inahusu utaratibu wa Ukhalifa, siku ya kwanza baada ya kifo cha Mtume, wakati Ali, Bani Hashim, na masahaba mashuhuri wa Mtume walipoweka vipingamizi na wakakataa kula kiapo cha utii kwa Khalifa, basi hoja zisizo za msingi zisingetolewa pale.

Wangeweza kutoa jibu la kunyamazisha kwa kusoma aya hii tukufu pale pale. Kwa hiyo, ni wazi kwamba tafsiri yako ni mawazo yaliyokuja baadaye. Hakuna yeyote katika wafasiri wakubwa wa madhehebu yenu, kama Tabari, Imam Tha’labi, Fadhil Nishapuri, Jalalu’d- Din Suyuti, Qadhi Baihawi, Jarullah Zamakhshari, Imam Fakhru’d-Din Radhi, au wengine ambao wameitafsir hivyo.

Nashindwa kuelewa jinsi unavyoipata maana hii. Wapi na kutoka kwa nani maana hii ilitolewa? Aya hii, kielimu na mtazamo wa kifundi, vilevile vinakwenda kinyuma na unavyosema.

Sheikh: Sikutarajia kwamba utakuwa mpinzani hivyo kwenye aya iliyo na maana ya wazi kiasi hicho. Hakika kama una lolote la kusema dhidi ya hivi unaweza ukatueleza tujue ili kwamba ukweli halisi uweze kuthibitishwa.

Muombezi: Ukichukulia ujenzi wa kinahau wa aya hii, kama tutaitafsiri maana yake kama ulivyofanya wewe, itakuwa na maana kwamba ama Muhammad ni Abu Bakr, Umar, Uthman na Ali au kwamba Abu Bakr, Umar, Uthman na Ali ni Muhammad!

Hata wanafunzi wanaoanza wanajua kwamba aina hii ya tafsir ya kinahau sio sahihi. Mbali na hayo, kama aya hii inaashiria kwa Makhalifa wanne, kungekuwa na kiungo “na” kupatanisha maneno ili kupata hiyo maana yako, lakini haiko hivyo.

Wafasiri wote wa madhehebu yenu wenyewe wanasema kwamba aya hii inaashiria kwa waumini wote. Aidha, sifa zilizotajwa katika aya hii kwa wazi kabisa zinaashiria kwa mtu mmoja tu, ambaye alikaa na Mtume kuazia mwanzo kabisa na sio watu wanne. Na kama tukisema mtu huyu mmoja alikuwa Amir’l-Mu’minina Ali, itakuwa sawasawa zaidi kulingana na akili za kuzaliwa na hadith kuliko kutaja wengine wowote.

Hoja Kutokana Na “Aya Ya Pango” Na Majibu Yake.

Sheikh: Ina shangaza kwamba unadai ati hujiingizi katika hoja zenye kupotosha, ingawa maoni yako ni ya kupotosha hasa. Allah anasema katika Qur’ani tukufu: “Kama hamtam- nusuru, basi Allah alimnusuru walipomtoa wale waliokufuru, yeye akiwa wa pili wake walipokuwa wote katika pango alipomwambia Sahibu y ake. ‘Usihuzunike kwa hakika Allah yu pamoja nasi, Allah akamteremshia utulivu wake na akamnusuru kwa majeshi msiyoyaona…’” (9: 40).

Kwanza, Aya hii inaunga mkono aya iliyopita na huthibitisha kwamba usemi “na walio pamoja naye”, huashiria kwa Abu Bakr ambaye alikuwa na Mtume katika Pango katika usiku wa Hijra, Pili, ukweli kwamba alikuwa na Mtukufu Mtume, yenyewe ni uthibitisho mkubwa wa fadhila na ubora wa Abu Bakr kwa umma wote. Mtume aliweza kutabiri kwamba Abu Bakr alikuwa Mrithi wake, na kwamba kuwepo kwa Khalifa baada yake ni muhimu.

Kwa hiyo, alitambua kwamba ilimpasa kumhifadhi Abu Bakr kama ambavyo angejihifadhi yeye mwenyewe. Hivyo, alimchukua kuwa naye ili kwamba Abu Bakr asije akakamatwa na maadui. Huduma kama hii haijafanywa kwa Mwislamu mwingine yeyote. Hii inathibitisha wazi haki yake ya ukhalifa kuliko wengine.

Muombezi: Kama ungeangalia Aya hii kwa busara zaidi, ungeona kwamba uamuzi wako ni wa makosa.

Sheikh: Unaweza kutoa sababu dhidi ya hitimisho ambalo tumelitoa?

Mombezi: Ningekuomba uliache suala hili kwa muda huu kwa sababu maneno huzaa maneno. Baadhi ya watu wenye chuki wanaweza wakafasiri maoni yetu kwa nia mbaya. Sitaki kuchochea chuki. Mtu anaweza akasema tunataka kuwavunjia heshima makhalifa, ingawa cheo cha kila mmoja kimewekwa, na sio muhimu kufanya tafsir zisizo na maana.

Sheikh: Unakuwa mkwepaji. Elewa kwamba hoja yenye maana haizai chuki; huondoa kutokuelewana.

Muombezi: Kwa vile umetumia neno “Mkwepaji,” ninalazimika kujibu, ili uweze kujua kwamba silikwepi suala hili. Nilitaka kudumisha utaratibu wa mjadala wetu. Natumaini kwamba hutaona makosa kwa upande wangu. Umetoa utetezi wa kizembe sana kwamba Mtume alijua kwamba Abu Bakr atakuwa Khalifa wake baada yake. Kwahiyo, ilikuwa muhimu kwake kuokoa maisha yake, na hivyo akamchukuwa ili awe pamoja naye.

Ukweli Kuhusu Abu Bakr Kufuatana Na Mtukufu Mtume (S.A.W.W.).

Majibu kwa maelezo yako ni rahisi. Kama Abu Bakr angekuwa Khalifa pekee baada ya Mtume, maoni kama hayo yangewezekana, lakini mnaamini katika makhalifa wanne. Kama hoja yako hii ni sahihi, na kama ilikuwa muhimu kwa Mtume kulinda usalama wa Khalifa, basi Mtume angeondoka nao wote wanne kutoka mjini Makka. Kwa nini aliweza kuwaacha wale watatu, mmoja wao katika hali ya hatari ya kulala katika kitanda cha Mtume, ambavyo ilikuwa ni hatari katika usiku ule wakati maadui zake walikuwa wamekusanyika ili kumuua?

Kwa mujibu wa Tabari (Sehemu ya tatu ya “Tarikh”) Abu Bakr hakuwa na habari za harakati za Mtume za kuondoka Makka. Wakati alipokwenda kwa Ali na kumuuliza kuhusu Mtume, alimueleza kwamba Mtume amekwenda kule pangoni. Ali akamwambia kwamba kama alikuwa na shughuli yoyote naye, alipaswa amkimbilie. Abu Bakr alikimbia na akamkuta Mtume njiani. Na hivyo akafuatana naye. Mtiririko huu wa matukio unaonyesha kwamba Mtume hakukusudia kumchuka Abu Bakr kuwa naye. Aliungana naye katikati ya njia bila ruhusa ya Mtume.

Kwa mujibu wa taarifa nyingine, Abu Bakr alichukuliwa katika safari hiyo kwa kuhofia asije akasababisha matatizo na kutoa habari kwa maadui. Maulamaa wenu wenyewe wameukiri ukweli huu. Kwa mfano, Sheikh Abu’l-Qasim bin Sabbagh, ambaye ni mmoja katika maulamaa wenu anayejulikana sana wa madhehebu yenu, ankiandika katika kitabu chake Al-Nur-Wa’l-Burhan kuhusu maisha ya Mtume, anasimulia kutoka kwa Muhammad bin Ishaq, na yeye kutoka kwa Hasan bin Thabit Ansari, kwamba alikwenda Makka kufanya Umra kabla ya kuhama kwa Mtume.

Aliona kwamba Maquraishi makafiri walikuwa wamewaandama masahaba wa Mtume. Mtume akamuamrisha Ali kulala katika kitanda chake, na kwa kuogopa kwamba Abu Bakr angetoa siri hii kwa makafiri, Mtume akamchukua awe pamoja naye.

Mwisho, ingelikuwa vizuri kama ungeonyesha ni ushahidi gani uliopo katika Aya hii, unaoonyesha ubora wa Abu Bakr au iwapo kufuatana na Mtume katika safari ni uthibitisho kwamba mtu anayo sifa ya Ukhalifa.

Sheikh: Ushahidi upo. Kwanza, usuhuba wa Mtume na kwamba, Allah amemuita saha- ba wa Mtume, yenyewe ni sifa tosha. Pili, Mtume mwenyewe amesema: “Hakika Allah yu pamoja nasi.” Tatu, uteremshwaji wa utulivu juu yake kutoka kwa Allah, kama ilivyotajwa katika Aya hii, ni uthibitisho wa kuvutia zaidi wa ubora wa Abu Bakr. Kwa hiyo, nukta zote hizi zikiwekwa pamoja huonyesha ubora wake kwa wengine kuhusiana na ukhalifa.

Muombezi: Hakuna anayesita kuikubali nafasi ya Abu Bakr, Mwislam mtu mzima, mmoja wa masahaba mashuhuri na baba wa mke wa Mtume. Hata hivyo, sababu hizi hazithibitishi ubora wake katika ukhalifa. Kama utajaribu kuthibitisha nukta yako hii kwa maelezo haya mbele ya watu waadilifu wasio na upendeleo, utakuwa unavutia lawama nzito.

Watasema kwamba usuhuba na watu wema sio uthibitisho wa sifa au ubora. Kwa mfano, mara kwa mara tunaona kwamba watu wabaya hufuatana na watu wema, na kundi la makafiri hufuatana na Waislamu katika safari. Pengine umesahau Qur’ani Tukufu inavyosema kuhusu Mtume Yusufu ambaye amesema:

يَا صَاحِبَيِ السِّجْنِ أَأَرْبَابٌ مُتَفَرِّقُونَ خَيْرٌ أَمِ اللَّهُ الْوَاحِدُ الْقَهَّارُ {39}

“Enyi wafungwa sahibu wenzangu wawili! Je! waungu wengi wanaofarikiana ndio bora au Mwenyezi Mungu, Mmoja Mwenye nguvu?” (12:39).

Kuhusu Aya hii, wafasiri wamesema kwamba wakati Yusufu alipopelekwa jela, siku hiyo hiyo mpishi wa Mfalme na mtunza mvinyo ambao wote walikuwa makafiri, vilevile walitiwa jela pamoja naye. Kwa muda wa miaka mitano watu hawa watatu (waumini na makafiri kwa pamoja ) waliishi pamoja kama maswahiba. Wakati akiwahubiria, Yusufu aliwaita sahiba zangu.

Je, usuhuba huu wa Mtume Yusufu ulifanya hata mara moja hali ya kuwaona makafiri hawa wawili kama watu bora au wenye heshima? Je, usuhuba wao na Mtume Yusufu ulileta mabadiliko katika Iman zao? Maandishi ya Wafasiri na wanahistoria yanatuambia kwamba, baada ya miaka mitano ya usahaba, waliachana kila mmoja katika hali ile ile.Aya nyingine ya Qur’ani Tukufu inasema:

قَالَ لَهُ صَاحِبُهُ وَهُوَ يُحَاوِرُهُ أَكَفَرْتَ بِالَّذِي خَلَقَكَ مِنْ تُرَابٍ ثُمَّ مِنْ نُطْفَةٍ ثُمَّ سَوَّاكَ رَجُلًا {37}

“Sahiba wake akamuambia na hali ya kuwa anajibishana naye: Je! Unamkufuru, Yule aliyekuumba kwa udongo, kisha kwa tone la manii, kisha akakufanya mtu kamili?” (18:37)

Wafasiri wanakubaliana kwamba aya hii inazungumzia ndugu wawili, mmoja alikuwa muumini, ambaye jina lake lilikuwa Yahuda. Mwingine alikuwa kafir jina lake lilikuwa Bara’tus. Jambo hili limeelezewa vilevile katika “Tafsir-e-Kabir” na Imam Fakhru’d-Din Razi, ambaye ni mmoja katika Maulamaa wenu.

Ndugu hawa wawili walizungumza pamoja, maelezo ambayo hayataweza kutolewa hapa. Hata hivyo Allah amewaita wote wawili (Muumin na Kafiri). “Masahibu.” Je, yule kafiri alipata faida kutokana na usuhuba wake na Muumini? Kwa hakika hapana. Hivyo usuhuba peke yake sio msingi wa mtu kudaiwa kuwa ni bora. Kuna mifano mingi yenye kuunga mkono maoni haya.

Maneno Ya Mtukufu Mtume (S.A.W.W.) “Allah Yuko Pamoja Nasi” Sio Uthibitisho Wa Ubora Wa Abu Bakr.

Umesema pia kwamba kwa vile Mtume alimuambia Abu Bakr, “Allah yuko pamoja nasi.” kwamba huo ni uthibitisho wa ubora wa Abu Bakr na haki yake ya Ukhalifa! Waweza ukayafikiria tena maoni yako. Watu wanaweza wakakuuliza, kwa mfano, “Je, Allah anakuwa na waumini na mawalii tu, na sio na makafir?” Unajua sehemu yoyote ambayo Allah hayupo? Je, hivi Allah hayupo na kila mtu? Chukulia kwamba muumini na kafiri wako pamoja katika mkusanyiko. Qur’ani inasema:

أَلَمْ تَرَ أَنَّ اللَّهَ يَعْلَمُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۖ مَا يَكُونُ مِنْ نَجْوَىٰ ثَلَاثَةٍ إِلَّا هُوَ رَابِعُهُمْ وَلَا خَمْسَةٍ إِلَّا هُوَ سَادِسُهُمْ وَلَا أَدْنَىٰ مِنْ ذَٰلِكَ وَلَا أَكْثَرَ إِلَّا هُوَ مَعَهُمْ أَيْنَ مَا كَانُوا ۖ{7}

“Je! Huoni kwamba Allah anajua vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini? Haupatikani mnong’ono wa watu watatu ila yeye huwa ni wanne wao, wala watano ila yeye huwa ni wa Sita wao, wala wachache kuliko hao wala zaidi ila Yeye huwa pamoja nao, popote walipo…”(58:7).

Kwa mujibu aya hii na wa akili ya kawaida, Allah yupo na kila mtu.

Sheikh: Maelezo “Allah yupo pamoja nasi” Yana maana kwamba walikuwa wapenzi mno wa Allah kwa sababu wamesafiri katika njia ya Allah kwa madhumuni ya kuhifadhi dini yake. Baraka za Allah zilikuwa pamoja nao.

Muombezi: Lakini hakika maelezo haya hayathibitishi kwamba mtu anazo baraka za milele. Allah Mwenye nguvu hutizama matendo ya watu. Imetokea mara kwa mara kwamba wakati fulani, watu walifanya matendo mema na wakawa ni wenye kupokea rehema kutoka kwa Allah.

Baadae wakamuasi Allah na ikawapata adhabu ya Mungu. Ibilis kama unavyojua, alimuabudu Allah kwa maelfu ya miaka na akapata upole kutoka Kwake. Hata hivyo mara tu alipoasi amri yake, akalaaniwa. Qur’ani Tukufu inasema:

قَالَ فَاخْرُجْ مِنْهَا فَإِنَّكَ رَجِيمٌ {34}

وَإِنَّ عَلَيْكَ اللَّعْنَةَ إِلَىٰ يَوْمِ الدِّينِ {35}

“Akasema: Basi toka humo, na hali ya kuwa wewe ni mwenye kufukuzwa… Na kwa yakini itakuwa laana juu yako mpaka Siku ya Malipo.” (15:34-35).

Kumradhi, hakuna madhara katika kutoa mifano, madhumuni yangu ni kufafanua hii nukta. Historia imejaa mifano mingi ya wale ambao walikuwa karibu na Allah, lakini ambao baada ya kujaribiwa, walilaaniwa.

Bal’am Bin Ba’ur, kwa mfano, wa hirimu moja na Musa, alitokea kuwa karibu sana na Allah kiasi kwamba Allah alimfunulia lile Ism-e- A’dhim (jina tukufu la Allah, ambalo kupitia hilo chochote kinachoombwa kinakubaliwa upesi sana na Allah).

Alimuomba Allah kwa njia ya Ism-e-A’dhim na akasababisha shida ikampata Musa katika Bonde la Tia! Lakini wakati wa majaribio, Bal’am alizidiwa nguvu na mahaba ya vitu vya ulimwengu. Alimfuata Ibilis na akalaaniwa.

Wafasiri wametoa maelezo kamili ya tukio hili. Imam Fakhru’d-Din Razi katika Tafsir yake sehemu ya 4, uk. 463, ameelezea habari hii kutoka kwa Ibn Abbas, Ibn Mas’ud, na Mujahid. Allah katika Qur’ani Tukufu anatueleza hivi: “Na wasomee habari za yule tuliyempa Aya zetu kisha akajivuna nazo. Na shetani akamuandama na akawa miongoni mwa waliopotea.”

Barsisa Abid.

Au angalia la Barsisa Abid, ambaye mwanzoni alimwabudu Allah kiasi kwamba akakuwa Mustajabu’d-da’wa (mtu ambaye maombi yake hukubaliwa). Hata hivyo,wakati muda wa majaribio ulipofika, alishindwa.

Akipotezwa na Shetani, akafanya zinaa na msichana, akanyongwa, na akafa kafiri, Qur’ani inamzungumzia katika maneno haya:

كَمَثَلِ الشَّيْطَانِ إِذْ قَالَ لِلْإِنْسَانِ اكْفُرْ فَلَمَّا كَفَرَ قَالَ إِنِّي بَرِيءٌ مِنْكَ إِنِّي أَخَافُ اللَّهَ رَبَّ الْعَالَمِينَ {16}

فَكَانَ عَاقِبَتَهُمَا أَنَّهُمَا فِي النَّارِ خَالِدَيْنِ فِيهَا ۚ وَذَٰلِكَ جَزَاءُ الظَّالِمِينَ {17}

“Ni kama shetani, anapomwambia mtu: kufuru; na anapokufuru akamwambia: Mimi si pamoja na wewe, hakika namuogopa Allah, Mola wa walimwengu. Basi mwisho wa wote wawili hao ikawa waingie motoni wakae humo, na hiyo ndiyo jaza ya madhalimu.” (59:16-17).

Hivyo kama mtu aliwahi kufanya matendo mema wakati fulani, haina maana kwamba mwisho wake utakuwa mzuri. Ni kwa sababu hii kwamba tunaelekezwa kusema katika maombi yetu: “Matendo yetu na yawe na mwisho mwema.”

Sheikh: Kwa hakika sikutarajia mtu mwenye heshima kama wewe kutoa mfano wa shetani, Bal’am Ba’ur na Barsisa.

Muombezi: Samahani, nimekwishaeleza kwamba hakuna madhara katika kutoka mifano. Kwa kweli ni lazima tuitoe katika mijadala ya kielimu ili kuthibitisha ukweli. Allah awe shahidi yangu: Kamwe sikukusudia kumtweza yeyote kwa kutoa mifano hii. Madhumuni yangu ni kuthibitisha hoja yangu tu.

Sheikh: Aya hii kwa wazi kabisa huthibitisha ubora wa Abu Bakr kwa sababu inasema: “Hivyo Allah akamteremshia utulivu juu yake….” (9:40). Kijina hapa humuashiria Abu Bakr, ambacho huthibitisha ubora wake.

Muombezi: Umeielewa vibaya, kijina kilichotumiwa baada ya “Sakina” (utulivu) huashiria kwa Mtume. Utulivu uliteremshwa kwake na sio kwa Abu Bakr, kama ilivyo dhahiri katika sentensi inayofuatilia ambapo Allah anasema: “…na akamnusuru kwa majeshi msiyoyaona…” (9:40) ukweli ni kwamba majeshi ya Malaika wasioonekana yalikuwa kwa ajili ya kumsaidia Mtume, sio Abu Bakr.

Sheikh: Nakubali kwamba msaada wa Mungu ulikuwa kwa ajili ya Mtume, lakini Abu Bakr akiwa pamoja na Mtume, hakuwa bila rehma.

Kuteremshwa Kwa Utulivu Kulikuwa Kwa Ajili Ya Mtume Wa Allah.

Muombezi: Kama upewaji wa rehma za Mungu umeashiria kwa watu wawili, nahau ya Kiarabu ingehitaji kwamba vijina vilivyotumika vingehusisha watu wawili katika misemo yote ya Aya hii. Lakini vijina hivi vinaashiria kwa mtu mmoja, Mtume, na rehma za Allah zilikuwa kwa ajili yake.
Kama kupitia kwake yeye, upewaji wa rehma ungekusudiwa vilevile kwa ajili ya wengine, majina yao yangetajwa. Hivyo, uteremshaji wa utulivu katika aya hii ni kwa ajili ya Mtume peke yake.

Sheikh: Mtume wa Allah alikuwa hana haja ya kupewa utulivu wa Mungu. Alikuwa hauhi- taji kwa sababu alikuwa amehakikishiwa rahma za Mungu. Hivyo upewaji wa utulivu ulikuwa kwa ajili ya Abu Bakr.

Muombezi: Kwa misingi gani wewe unasema kwamba Mtume alikuwa hategemei upewa- ji wa rehma za Mungu? Hakuna mtu - awe Mtume Imam au Walii ambaye anajitegemea kwa (upewaji wa) rehma za Mungu. Pengine umesahau Qur’ani Tukufu inasema nini kuhusu tukio la Hunain.“Kisha Allah akateremsha utulivu wake juu ya Mtume wake na juu ya waliomini…” (9:26).

Kitu hicho hicho kimesemwa katika Sura ya 48 (Fat’h) aya ya 26, ya Qur’ani Tukufu. Waumini wamejumuishwa baada ya Mtume katika aya hii, kama vile katika “aya ya Pango.” Kama Abu Bakr angekuwa mwenye kustahiki kupewa utulivu, ima kijina kwa ajili ya watu wawili kingetumika, au jina lake lingetajwa mbalim- bali.

Jambo hili liko wazi kabisa kiasi kwamba Maulamaa wenu wenyewe wanakiri kwamba kijina kilichofungamanishwa na utulivu hakiashirii kwa Abu Bakr. Unaweza kuitazama “Naqzu’l-Uthmaniyya” kilichoandikwa na Sheikh Abu Ja’far Muhammad bin Abdullah Iskafi, ambaye ni mmoja wa Maulamaa mashuhuri na masheikh wa Mu’tazil. Mwanachuo huyu anaukana moja kwa moja uongo wa Abu Uthman Jahiz. Ibn Abi’l-Hadid vilevile ameandika baadhi ya majibu hayo katika Sharh yake ya Nahju’l-Balagha Jz. 3, uk. 253- 281. Kwa nyongeza, kuna usemi katika Aya hii, ambao maana yake halisi ni kinyume na hoja yako. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimuambia Abu Bakr: “Usihuzunike.” Usemi huu unaonyesha Abu Bakr alikuwa muoga.

Je, woga huu ulikuwa unafaa kusifiwa au hapana? Kama ingelikuwa hivyo, Mtume asingemzuia yeyote kufanya tendo jema. Mwakilishi wa Allah ana sifa makhususi. Muhimu zaidi ya hizo, kama ilivyotajwa katika Qur’ani Tukufu, ni kwamba haogopi kubadilika kwa maisha. Anafanya uvumilivu na ushujaa. Qur’ani Tukufu inasema: “Sikilizeni (eleweni)! Hakika vipenzi vya Allah hawatakuwa na khofu wala hawatahuzunika.” (10:62).