read

Mkutano Wa Tatu – Jumamosi Usiku 25 – Rajab 1345 A.H.

Hafidh: Kwa msingi wa mazungumzo yako ya usiku wa jana naona kwamba Mashi’a wamegawanyika katika idadi ya matapo. Tafadhali tujulishe tujue ni lipi katika hayo matapo unalikubali, ili mipaka ya majadiliano yetu iwe katika tapo hilo.

Mashia Hawakugawanyika Katika Matapo

Muombezi: Mimi sikusema kwamba Mashi’a wamegawanyika katika matapo. Mashi’a wamejitoa kwa Allah (s.w.t.) na ni wafuasi wa Mtume na kizazi chake. Ni kweli baadhi ya matapo yamejichukulia jina la Shi’a ili kuwapotosha watu.

amechukua manufaa ya jina la Shi’a, wakahubiri imani potofu na kueneza mkanganyiko. Watu wasio na ujuzi wame- husisha majina yao miongoni mwa Mashi’a. Ziko faraka nne za namna hiyo, mbili katika hizo zimebakia: Zaidiyya, Kaysaniyya, Qaddahiyya na Ghullat.

Zaidiyya

Zaidiyya wanamfuata Zaid bin Ali bin Husein. Wanamchukulia mtoto wa Imam Zainu’l- Abidin, aitwaye Zaid kuwa ndiye Mrithi wake. Kwa wakati huu watu hawa wanapatikana kwa idadi kubwa nchini Yemen na majirani waizungukao. Wanaamini kwamba miongoni mwa Dhuria wa Ali na Fatima, Yeye ndiye “Imam ambaye ni mwanachuo, mcha Mungu, na shujaa.

Anachomoa upanga na kusimama dhidi ya maadui,” Katika wakati wa Khalifa dhalimu wa Kibani Umayya, Hisham ibn Abdul-Malik, Hadhrat Zaid alisimama dhidi ya wale waliokuwa katika mamlaka na akauwawa Shahidi na kwa ajili hiyo akakubaliwa na Zaidiyya kama Imam. Ukweli ni kwamba Zaid alikuwa na cheo cha juu zaidi kuliko hicho ambacho Zaidiyya wanakidai kwa ajili yake. Alikuwa ni Sayyid mashuhuri wa ukoo wa Bani Hashim, na alikuwa akijulikana kwa ucha Mungu wake, hekima, Sala, na ushujaa. Alipitisha mikesha mingi bila usingizi akikesha kusali na alifunga mara kwa mara. Mtume (s.a.w.w.) alitabiri Shahada yake (kifo cha kishahidi), kama ilivyosimuliwa na Imam Husein:

“Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akaweka mkono wake Mtakatifu kwenye mgongo wangu na akasema:
“Ewe Husein haitachukuwa muda mrefu atazaliwa mtu miongoni mwa Dhuria wako.

Atakuwa anaitwa Zaid; atauwawa kama Shahid. Katika siku ya ufufuo, yeye na Masahaba zake wataingia Peponi, wakiweka miguu yao juu ya shingo za watu.” Lakini Zaid mwenyewe hakudai kamwe kuwa yeye ni Imam. Ni masingizio yasiyo na msingi kwa watu kusema kwamba alidai. Kusema kweli, yeye alitambua Imam Muhammad Baqir kama Imam na alitoa utii wake kiukamilifu kwake.

Ilikuwa ni baada tu ya kufariki kwa Imam Muhammad Baqir ndipo watu wajinga wakatwaa itiqad ya kwamba: “Siye Imam yule akaaye nyumbani na kujificha machoni mwa watu; Imam ni yule ambaye ni Dhuria wa Hadharat Fatima, ambaye ni mwenye elimu, na ambaye anachomoa upanga na kusimama dhidi ya adui, na kulingania (kuwaita) watu upande wake. Zaidiyya wamegawanyika katika faraka Tano: Mughairiyya; Jarudiyya; Zakariyya; Khashbiyya; na Khaliqiyya.

Wa-Kaysaniyya Na Imani Yao.

Tapo la pili ni la Kaysaniyya. Hawa ni Masahaba wa Kaysan, Mtumwa wa Ali bin Abu Talib, ambaye alimuacha huru. Watu hawa wanaamini kwamba baada ya Imam Hassan na Imam Hussain, Muhammad Hanafiyya mtoto mwingine (wa kiume) anayefuatia kwa umri, wa Amir’l-Mu’minina, Ali (A.S.) alikuwa ndiye Imam. Lakini Muhammad Hanafiyya mwenyewe kamwe hajadai hivi.

Alikuwa akiitwa Muaminifu wa Watiifu. Alikuwa akijulikana sana kwa elimu yake, Ucha Mungu, Utiifu, Ibada, na mtiifu kwenye maamrisho ya Mwenyezi Mungu. Baadhi ya watu wajinga hutoa ushahidi ambao waliuita upinzani wake kwa Imam Zainul’l-Abidin. Walidai kwamba Muhammad Hanafiyya alidai kuwa ni Imam.
Ukweli ulikuwa vinginevyo. Hajadai kamwe kuwa ndiye Imam. Alitaka kuwaonyesha wafuasi wake wajinga cheo na hadhi ya Imam wa nne, Zaimul’l-Abidin. Matokeo yalikuwa kwamba, katika msikiti huohuo Mtukufu (wa Makka) wakati Hajaru’l-Aswad (jiwe jeusi) lilipothibitisha Uimamu wa Imam Zainul’l-Abidin, kama ilivyoandikwa kwa mpangilio katika vitabu vya Ta’rikh, Abu Khalid Kabuli, mkubwa wa wafuasi wa Muhammad Hanafiyya pamoja na wafuasi wengine, walimkubali Imam Zainu’l-Abidin kama Imam.

Lakini kundi la watu walaghai walipotosha watu wa kawaida na wajinga kwa kusema kwamba Muhammad Hanafiyya alionyesha tu adabu, kwamba mbele za Bani Umayya ilikuwa inapendeza mno kwa Muhammad Hanafiyya kufanya kama alivyofanya.

Baada ya kufariki Muhammad Hanafiyya, watu hawa walisema hakufa, na kwamba amejificha katika pango la Mlima Rizwi, na kwamba atakujatokea baadae kuujaza ulimwengu kwa haki na amani. Tapo hili lina matapo mengine madogodogo: Mukhtariyya; Karbiyya; Ishawiyya na Harabiyya.

Lakini leo hakuna lililopo hata moja kati ya hayo.

Qaddahiyya Na Imani Yao.

Tapo la tatu, Gaddahiyya, Wanajiita wenyewe Shia, lakini ni kundi la Makafiri.

Kitapo hiki kilianzishwa Misri na Ma’mum Ibn Salim (au Disan) ajulikanae kama Qada na Issa Chahar Lakhtan (Yesu wa sehemu nne.)

Walijitolea kutafsir Qur’ani Tukufu na kumbukumbu za Ta’rikh kwa kulingana na matakwa yao. Wanashikilia kwamba kuna kanuni mbili za dini: moja ya siri na nyingine ya wazi. Kanuni ya siri ilitolewa na Allah kumpa Mtume Muhammad. Mtume akaitao kwa Ali, naye akaitoa kwa dhuria wake na kwa Mashia halisi. Wanaamini kwamba, wale wanaoijua ile kanuni ya siri wamesamehewa katika Sala na kumuamudu Allah.

Wamesimamisha dini yao katika nguzo saba. Wanaamini Mitume saba, na Maimamu saba, Imam wa saba akiwa yuko Ghaibuni. Wanangojea kujitokeza kwake. Wamegawanyika katika vijikundi viwili.

1) Nasiriyya ambao walikuwa Masahaba wa Nasiri Khusru Alawi, ambaye kwa mashairi yake, hotuba na vitabu alivuta watu wengi kwenye ukafiri. Walienea katika Tabaristan yote kwa idadi kubwa.

2) Sabahiyya (wanaojulikana katika nchi za Magharibi kama ‘Assassins,’ yaani wauaji). Walikuwa ni Masahaba wa Hasan Sabba, mwenyeji wa Misri ambaye amekuja Iran, na ambaye alisababisha matukio ya misiba na huzuni ya Alamut, ambayo ilisababisha kuuwawa kwa idadi kubwa ya watu. Matapo haya yamehifadhiwa kwenye vitabu vya Ta’rikh.

Ghullat Na Imani Zao

Tapo jingine ni lile la Ghullat, ambalo ndio kundi potovu zaidi katika matapo yote. Wanajulikana kwa makosa kama ni Shi’a. Kwa kweli hawa wote ni makafiri. Wamegawanyika katika vijikundi Saba: Saba’iyya; Mansuriyya; Gharabiyya; Bazishiyya; Yaqubiyya; Isma’iliyya na Azdariyya.

Sio Shi’a Ithna Shariyya tu (wanoamini katika Maimam kumi na mbili), bali Waislamu wote ulimwenguni wanaikataa imani yao.

Shi’a Imamiyya Ithnashariyya Na Imani Yao.

Hili ndilo kundi Sahihi la Shi’a, ambalo linaamini Maimamu kumi na mbili baada ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Matapo haya mengine hayana kinachofanana na kundi letu; wamejichukulia tu jina la Shi’a.

Imani Katika Allah Na Mitume

Kundi la Shi’a Imamiyya wanamini kuwepo kwa Allah Mwenye Enzi zote daima Milele. Ni mmoja, kwa maana kamilifu ya upweke wa uhalisi wa kuwako kwake. Yeye ni mmoja, hana mfano wake. Yeye ni muumba wa vitu vyote vilivyopo. Hakuna chenye kulingana au kuwa sawa na Yeye katika hali yoyote. Manabii watukufu na Mitume walitumwa kuwaeleza watu kuhusu Allah, namna ya kumuabudu Yeye, na jinsi ya kumjua Yeye. Mitume wote walihubiri na kuongoza watu kwa mujibu wa Mafundisho yaliyowekwa mbele na Mitume wakubwa watano: Nuh, Ibrahim, Musa, Issa na mwisho wa wote, Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w.) ambaye dini yake itabakia mpaka Siku ya Kiyama.

Imani Katika Adhabu, Malipo, Jahannamu, Pepo, Na Siku Ya Kiyama.

Mwenyezi Mungu Mtukufu ameweka malipo kwa ajili ya matendo yetu, ambayo yatatole- wa kwetu katika Pepo au Jahanamu. Siku iliyowekwa kwa malipo ya matendo yetu inaitwa “Siku ya Malipo.” Wakati maisha ya Ulimwengu huu yatakapokoma, Allah (s.w.t.) atawafufua viumbe wa ulimwengu kuanzia wa mwanzo mpaka mwisho. Atawafanya wakusanyike katika Mashar; sehemu ya kukusanyikia Roho zote. Baada ya hesabu ya haki, kila mtu atapewa malipo au adhabu kwa kulingana na matendo yake.

Mambo haya yametabiriwa katika vitabu vyote vya Mwenyezi Mungu: Taurat, Zaburi, Injili na Qur’ani Tukufu. Kwetu sisi Kitabu cha Mwongozo kilicho sahihi zaidi ni Qur’ani Tukufu ambayo imefika kwetu kutoka wakati wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) bila mabadiliko yoyote. Tunatenda juu ya amri zilizomo ndani ya Qur’ani Tukufu, na tunataraji malipo kutoka kwa Allah. Tunaamini katika amri zote zile za wajib ambazo zimo katika Qur’ani, kama Sala, Saumu, Zaka, Hija na Jihad.

Imani Katika Kanuni Za Ibada:

Halikadhalika, tunaamini katika Kanuni za utendaji wa ibada, ikiwa ni pamoja na ibada za wajibu na za Suna na amri nyingine zote ambazo zimetufikia kupitia kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Tumejizatiti kushikamana nazo na kuzitekeleza kwa kadri ya uwezo wetu. Na tunajiepusha kutokana na madhambi yote, makubwa au madogo kama ulevi, kamari, uasherati, kulawiti, riba kuua, udhalimu ambavyo vimekatazwa katika Qur’ani Tukufu na Hadith.

Imani Katika Maimamu:

Sisi Shi’a vilevile tunaamini kwamba, kama ambavyo kuna mjumbe kutoka kwa Allah ambaye anazifikisha kwetu sisi kanuni na maamrisho, na ambaye ameteuliwa na kujulishwa kwetu na Allah (s.w.t.), vilevile kuna mrithi, Khalifa, au Mlinzi wa dini, ambaye anach- aguliwa na Allah na anatambulishwa kwetu kupitia kwa Mtume wa Allah. Kwa ajili hiyo Mitume wote wa Allah waliwajulisha warithi wao kwa Umma zao. Wa mwisho wa Mitume watukufu, ambaye alikuwa ndiye mkamilifu zaidi na aliye nyanyuliwa daraja ya juu zaidi kuliko Mitume wote wa Allah, aliacha kwa ajili ya wafuasi wake viongozi kusaidia watu kuepukana na matatizo.

Kwa mujibu wa hadith zilizothubutu, aliwajulisha kwa watu warithi wake kumi na mbili. Wa kwanza wao akiwa ni Ali bin Abu Talib (A.s.). Imam wa mwisho, ni Mahdi (A.f) ambaye yupo ulimwenguni, lakini yuko kwenye Ghaib (amefichwa kwenye macho ya watu), atatokeza katika muda usiojulikana baadae, wakati atakapoujaza ulimwengu uliovu- rugika kwa haki na amani.

Shi’a Imamiyya vilevile Wanaamini kwamba hawa Maimamu kumi na mbili wameteuliwa na Allah na wamejulishwa kwetu kupitia kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wa mwisho. Wa mwisho katika Maimam watukufu ametoweka katika macho ya watu (kwa amri ya Mwenyezi Mungu), kama vile Maimam wengine walivyotoweka katika wakati wa Mitume waliopita, kama ilivyoelezwa katika vitabu vingi vilivyoandikwa na Maulamaa wenu.

Kiumbe huyu Mtakatifu amehifadhiwa na Allah (s.w.t.) ili kwamba siku moja aweze kuujaza ulimwengu na haki. Kwa ufupi, Shi’a wanaamini katika yale yote ambayo yamo katika Qur’ani Tukufu na katika hadith Sahihi.
Ni mwenye kushukuru sana kwa Allah kwamba nimefuata imani hizi, sio kwa upofu tu wa kufuata wazazi wangu, bali kwa ukweli wenye mantiki na kuchunguza.

Hafidh: Mheshimiwa Maulana, hakika nina wiwa na wewe kwa kuweza kueleza imani za Shi’a, lakini kuna Hadith na Dua katika vitabu vyenu ambazo zinakwenda kinyume na maelezo yako na kuonyesha upotofu wa Mashi’a.

Muombezi: Tafadhali kuwa wazi zaidi.

Kanusho Juu Ya Hadith Ya Ma’rifa

Hafidh: Katika “Tafsir-e-Safi”, kilichoandikwa na mmoja wa Wanachuo wenu mwenye cheo cha juu, Faiz Kashi, mna hadith isemayo kwamba: “Siku moja Imam Husain; Shahid wa Karbala, akihutubia Masahaba wake alisema: “Enyi watu, Allah (s.w.t.) hakuumba waja Wake, bali kumjua Yeye.

Wakati wakimjua Yeye, wanamuabudu Yeye, wakati wakimwabudu Yeye, wanakuwa kinyume na kuabudu kitu kingine chochote.” Mmoja wa Masahaba akasema: “Maisha ya Baba yangu na Mama yangu na yawe mhanga kwa ajili yako! Ewe Mtoto wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)! Nini hasa maana ya kumjua Allah?” Mtukufu Imam akajibu, “Kwa kila mtu kumjua Allah ina maana kumjua Imam wake wa Zama, ambaye lazima atiiwe.”

Muombezi: Kwanza, lazima tuchunguze nyororo ya wasimuliaji ili kuthibitisha kama ni Sahihi. Hata kama ni sawa kwa kutegemeana na wasimuliaji, bado Aya za Qur’ani Tukufu na Hadith halisi za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) haziwezi kueleweka vibaya kwa sababu ya madai ya mtu mmoja.

Kwa nini usizichunguze hadith na simulizi za Maimam wetu Watukufu, na mijadala ya kidini kati ya viongozi wetu wa dini na makafiri, ambayo tayari imethibitisha Upweke wa Allah?

Kwa nini huangalii vitabu vikuu na Sharhe hasa za Shi’a kama vile Tawhid-e- Mufazzal. Tawhid-e-Saduq, Biharu’l-Anwar (Kitabu cha Tawhid) cha Allama Majlisi na vitabu vingine vilivyoandikwa na Maulamaa wa Kishi’a ambavyo vimejaa hadith za mfululizo (juu ya Tawhid) kutoka kwa Maimam wetu watukufu?

Kwa nini usiangalie katika An-Naktu’l-Itiqadiyya, cha Sheikh Mufid (Amefariki 413 A.H.) mmoja wa Maulamaa wa Kishi’a, na pia kitabu chake Awa’ilu’l-Maqalat fi’l-Madhahib wa’l-Mukhtarra au Ihtajaj cha Mwanachuo wetu mashuhuri, Abu Mansur Ahmad bin Ali bin Abu Talib Tabrasi? Kama ungefanya hivyo, ungepata kujua jinsi gani Mtukufu Imam wetu Ridha (A.S.) alivyothibitisha Umoja wa Allah.

Si haki kuchukua baadhi ya taarifa zenye mashaka kwa ajili ya kutaka tu kuwazulia uongo Mashi’a. Vitabu vyenu wenyewe vina mambo ya vichekesho na maoni yasioeleweka kiakili.

Kwa kweli hadith za ajabu ajabu zimo katika vitabu vyenu Sahihi zaidi - Sahihi Sitta (yaani vile vitabu sita vya hadith vinavyokubalika kwenu ninyi).

Hafidh: Kwa kweli, maneno yako ni ya kuchekesha sana maadam unaona makosa katika vitabu ambavyo umaarufu na usahihi wake si wa kutiliwa mashaka, hususan Sahihi Bukhar, na Sahih Muslim. Maulamaa wetu wanakubaliana kwamba hadith zote zilizomo humo ni za kweli. Kama mtu akivikataa vitabu hivi viwili, anaikataa Madhehebu halisi ya Sunni. Baada ya Qur’ani Tukufu, Sunni wanategemea juu ya usahihi wa vitabu hivi, viwili.

Pengine bila shaka umeona maelezo ya Ibn Hajar Makki mwanzoni mwa kitabu chake Sawa’iq al-Muhriqa, sura ya “Matukio” (Matukio ya ukhalifa wa Abu Bakar) kama ilivyoandikwa na Bukhar na Muslim katika Sahih zao mbili, ambavyo ndio vitabu sahihi zaidi na vya kutegemewa baada ya Qur’ani Tukufu kwa mujibu wa makubaliano ya pamoja ya wafuasi (yaani, Ummah).

Anasema kwamba maadam ummah wote uko pamoja kati- ka kuzikubali hadith za vitabu hivyo, chochote ummah wanachokubaliana kwa shauri moja hakiwezi kutiliwa mashaka. Juu ya msingi wa makubaliano haya, hadith zote zilizomo katika vitabu hivi zinakubalika bila kutiliwa mashaka.
Kwa hiyo, hakuna mtu anayeweza kujasiri kudai kwamba vitabu hivi vina mambo ya ajabu na ya kuchekesha.

Hadith Za Ajabu Katika Sahihain – Bukhari Na Muslim.

Muombezi: Kwanza, kwamba vitabu hivi vinakubaliwa na umma wote, kunapingwa kwa uwazi kabisa. Madai yako kuhusiana na rejea kutoka kwa Ibn Hajar, peke yake ni ya ajabu, kwa kuwa Waislamu milioni 100 hawaikubali nukta yake.

Kwa hiyo, makubaliano ya pamoja ya umma katika suala hili ni kama makubaliano ya pamoja yaliyodaiwa na watu wenu katika suala al ukhalifa. Pili, ninayosema yametegemezwa kwenye sababu zenye msingi thabiti. Kama utavichunguza vitabu hivyo bila kuwa na mawazo ya chuki, utashangaa sana.

Wengi wa maulamaa wenu wakubwa, kama vile Darqutni, Ibn Hazam, Allama Abu’l-Fazl Ja’far bin Tha’labi katika Kitabu’l-Imta’ fi Akhamus-Sama’, Sheikh Abdul’Qadir bin Muhammad Qarshi katika Jawahiru’l-Mazay’a fi Tabqatu’l-Hanafiyya, na wengineo, pamoja na maulamaa wote wa Kihanafia wamevilaumu vitabu hivi viwili (Sahihain) na wamekiri kwamba vina idadi kadhaa ya hadith dhaifu na zisizothibiti. Lengo la Bukhari na Muslim lilikuwa ni kukusanya hadith; sio kuhukumu usahihi wake.

Baadhi ya Wanachuo wenu watafiti kama vile Kamalu’d-Din, Ja’far bin Sa’lih wamechukuwa taabu kubwa katika kuonyesha kasoro na makosa ya hadithi na wameweka misingi yenye nguvu katika kuunga mkono matokeo ya utafiti wao.

Hafidh: Ningelilikaribisha suala la kama utazionyesha hoja hizo ili kwamba hadhara hii ipate kujua ukweli.

Muombezi: Nitaonyesha mifano michache tu.

Rejea Zinazoonyesha Kuhusu Kuonekana Kwa Allah

Kama mnataka kusoma Hadith za kupotosha kuhusu Allah kuchukua mwili wa kibinadamu (au kuingia katika mwili wa mwanadamu), ambazo zinatetea kwamba Yeye (Allah), kama kiumbe mwenye mwili, anaweza kuonekana katika ulimwengu huu, au ataonekana katika ulimwengu jao wa Akhera, (kama inavyoaminiwa na Tapo la Suni yaani Hanbaliyya na Ashariyya) mnaweza mkarejea kwenye vitabu vyenu wenyewe, hususan Sahih Bukhari, Juz. 1, uk. 100 katika Mlango wa Fadhla-s-Sujud Min Kitabu’l-Adhan, na katika Sahih Muslim Juz. 4, uk. 92 Babus-Sira Min Kitabu‘r-Riqaq na vilevile tena kwenye hiyo Sahih Muslim Juz. 1 uk. 86 Sura ya Isbatu’l-Ruyatu’l-Mu’Minin Rabbahum Fi’l-Akhira; na Musnad ya Imam Hanbal Juz. 2, uk. 275. Mtapata maelezo ya kutosha ya namna hii katika vitabu hivyo.

Kwa mfano, Abu Huraira anasema: “Makelele na kishindo cha ukali wa moto vitakithiri, hautatulia mpaka Allah aweke mguu Wake humo. Kisha Jahannam itasema: “Basi, basi! hiyo inanitosha; inanitosha.” Vilevile Abu Huraira anasimulia kwamba kikundi cha watu walimuuliza Mtukufu Mtume (s.a.w.w.); “Je, tutamuona Muumba wetu hiyo Siku ya Malipo?” Akajibu: “Bila shaka. Je, wakati wa mchana wakati anga inapokuwa haina mawingu, jua lina kuumizeni wakati mnapoliangalia?” Wakasema, “Hapana!” Yeye akase- ma tena: “Je, wakati wa usiku mnapoungalia mwezi mpevu wakati anga ni nyeupe, unakuumizeni?” Wakasema, “Hapana!”

Aliendelea: “Hivyo wakati mtakapomuona Allah Siku ya malipo hamtadhurika, kama vile tu ambavyo hamdhuriki muangaliapo hivi (jua na mwezi). Wakati Siku ya Hukumu itakapofika, itatamkwa na Allah kwamba kila umma wamfuate Mungu wao. Hivyo kila mtu ambaye alikuwa akiabudu masanamu au kitu kingine kisichokuwa Allah, Aliye Mmoja, ataingizwa katika moto wa Jahannamu. Kadhalika kila mmoja wa watu wema na wabaya watalipwa katika moto isipokuwa wale waliomuabudu Allah, Mmoja Mkamilifu. Watalala katika moto wa Jahannamu.

Katika muda huo Allah atatokeza katika umbo Makhususi mbele za watu ili kwamba wapate kumuona. Kisha Allah atawaambia kwamba Yeye ndiye Mola wao. Kisha Waumini watasema, “Tunajikinga na uungu wako. Sisi ni miongoni mwa wale ambao walikuwa hawaabudu kitu chochote isipokua Allah Mwenye mamlaka ya juu.”
Allah atasema katika kuwajibu, “Mnayo dalili yoyote kati yenu na Allah ambapo kwamba mnaweza kumuona Yeye na kumtambua?” Watasema, “ndio!” Kisha Allah atawonyesha mguu wake uliowazi (bila kiatu). Hapo waumini watanyanyua vichwa vyao kuelekea juu na watamuona katika hali ileile kama waliyomuona nayo kwa mara ya kwanza. Kisha Allah atasema kwamba, Yeye ndiye Muumba wao. Wote kwa pamoja watakubali kwamba Yeye ndiye Mola wao.”

Sasa ni juu yenu ninyi kuamua iwapo maelezo namna hii ni sawa na ukafiri au hapana, kwamba Allah atajitokeza kiumbo mbele za watu na atafunua mguu Wake!

Na nukta kubwa sana yenye kuunga mkono hoja yangu ni kwamba Muslim bin Hajjaj anaanza kuandika sura katika Sahih yake kuhusu uhakika wa kuonekana Allah (s.w.t.), na amenukuu simulizi za kubuni kutoka kwa Abu Huraira, Zaid bin Aslam; Suwaid bin Sa’id, na wengine. Na baadhi ya maulamaa wakubwa wa madhehebu yenu wenyewe kama Dhahabi katika ‘Mizanu’l-Itidal’ na Suyuti katika kitabu chake Kitabu‘l-Lu-ualia’l- Masnu’a fi haditha’l-Muzu’a, na Sibt ibn Jauzi katika Al-Muzu’a; wamethibitisha juu ya hoja za Msingi kwamba simulizi (Hadith) hizi ni za kubuni.

Qur’ani Tukufu Inakataa Dhana Ya Kuonekana Kwa Allah.

Hata kama kusingelikuwa na uthibitisho dhidi ya madai hayo hapo juu. Aya ya Qur’ani Tukufu inakataa waziwazi dhana ya kuonekana kwa Mwenyezi Mungu. Allah (s.w.t.) Anasema:

لَا تُدْرِكُهُ الْأَبْصَارُ وَهُوَ يُدْرِكُ الْأَبْصَارَ ۖ وَهُوَ اللَّطِيفُ الْخَبِيرُ {103}

“Macho hayamfikii, bali yeye anayafikia macho…” (6:103)

Tena, wakati Nabii Musa alipolazimishwa na wana Israel kwenda sehemu yake ya Sala na amuombe Allah “Ajidhihirishe kwake,” Qur’ani Tukufu inaandika tukio hili kama ifuatavyo:

قَالَ رَبِّ أَرِنِي أَنْظُرْ إِلَيْكَ ۚ قَالَ لَنْ تَرَانِي وَلَٰكِنِ انْظُرْ{143}

“…(Musa) akasema: “Mola wangu nionyehse (nafsi Yako) ili nikuone,” Akasema: “Huwezi (Ukathubutu) kuniona…” (7:143).

Seyyid Abdu’l-Hayy (Imam wa wa jama’at ya Ahli Sunna): Je! Hii sio kweli kwamba Ali Alisema: “Siwezi kumuabudu Mungu ambaye simuoni?” Wakati Ali anasema kitu cha namna hiyo, ina maana kwamba Allah anaweza kuonekana.

Hoja Na Hadith Kuhusu Kutokuonekana Kwa Allah

Muombezi: Rafiki Mheshimiwa, umeondoa sentensi moja nje ya fuo la maneno haya. Nitakusomea matini yote. Hadith hii imeandikwa na Sheikh mashuhuri, Muhammad Ibn Yaqub Kulain katika kitabu chake “Usul al-Kafi,” (juzuu juu ya tawhid), na hivyo hivyo Sheik Saduq katika kitabu chake juu ya Tawhid, Sura ya Ibtal Aqida Ruyatullah. Imam Ja’far as-Sadiq ananukuliwa akisema, mwanachuo mmoja wa Kiyahudi alimuuliza Amir’l-Mu’minin, Ali (A.S.) iwapo amemuona Allah katika wakati wa Sala. Imam akajibu: “Hawezi kuonekana kwa macho haya ya kiumbo.

Ni moyo ndio unaomuona Yeye, kwa mwanga wa uhalisi wa kuamini na kusadiki.” Kutokana na majibu ya Ali ni kwamba yeye anachomaanisha kwa kumuona Allah, sio kumuona kwa macho, bali kwa mwanga wa imani ya kweli. Kuna ushahidi mwingine mwingi uliotegemezwa juu ya hoja na mambo yaliyoandikwa ya kuthibitisha maoni yetu juu ya nukta hii.

Zaidi ya hayo, mbali na wanachuo wa Kishi’a, maulana wenu wenyewe, kama Qadhi Baidhawi na Jarullah Zamakhshari, wamethibitisha katika Sharhe zao kwamba haiwezekani kwa Allah kuonekana. Yeyote ambaye anaamini juu ya kuonekana kwa Allah, katika ulimwengu huu au ulimwengu ujao, anaamini kwamba ni kiumbe mwenye mwili. Kuamini hivyo ni ukafiri.

Rejea Zaidi Ya Hadith Za Ajabu Ajabu Katika Vitabu Viwili Vya Hadith

Mnafikiria vitabu vyenu sita vya Hadith, khususan vile vya Bukhari na Muslim, kama vitabu vya Ufunuo. Natamani kwamba mngeviangalia kwa busara na msivuke mipaka katika kuvisifu kwenu. Bukhari, katika Sura ya “Kitab-e-Ghusl,” na Muslim katika Sehemu ya 2 ya Sahih yake (Sura ya fadhil za Mtume Musa),
na Imam Ahmad bin Hanbal katika Musnad yake, Sehemu ya 2 uk. 315, na maulamaa wenu wengine wamemnukuu Abu Huraira akisema: “Miongoni mwa wana wa Israel ilikuwa ni desturi yao kuoga pamoja bila nguo, hivyo kwamba kila mmoja aliangalia utupu wa mwenziwe. Hawakufikiria kama kuna kizuizi katika hilo. Mtume Musa ndiye aliyekuwa akiingia kwenye maji peke yake, hivyo kwamba hakuna aliyeweza kuona sehemu zake za siri.

“Wana wa Israeli walizoea kusema kwamba Mtume Musa alikuwa na hitilafu katika sehe- mu zake za siri, hivyo alijiepusha kuoga nao. Siku moja Mtume Musa alikwenda mtoni kuoga. Alivua nguo zake, akaziweka juu ya jiwe na akaingia mtoni. Lile jiwe likakimbia na nguo zake. Musa akalikimbiza lile jiwe akiwa uchi, akipiga makelele: ‘Nguo zangu! Ewe jiwe nguo zangu.’ Wana wa Israel wakamuona Musa akiwa uchi na wakasema: ‘Kwa jina la Allah Musa hana hitilafu katika tupu zake.’

Kisha lile jiwe likasimama, na Musa akarudishiwa nguo zake. Kisha Musa akalipiga lile jiwe kwa nguvu sana kiasi kwamba lile jiwe likalia kwa sauti kubwa mara sita au mara saba kwa maumivu.”

Kweli mnaamini kitu kama hicho kinawezekana kwa Nabii Musa (A.S.), au kwamba jiwe, kitu kisicho na uhai, lingeweza kuchukua nguo zake? Kwa hakika itakuwa haiwezekani kwa Mtume kukimbia uchi mbele za watu.

Nitasimulia Hadith nyingine iliyoandikwa katika Sahih ambayo ni ya kichekesho zaidi. Bukhari anamnukuu Abu Huraira katika Sahih yake (Juz. 1, uk. 158 na Juz. 2, uk. 153), na tena katika Sura ya “Kifo cha Mtume Musa,” na Muslim vilevile anamnukuu huyo huyo (Abu Huraira) katika Sahih yake Juz. 2, uk. 309 katika Sura ya Fadhila za Musa akisema: “Malaika wa Mauti alikuja kwa Mtume Musa na akamtaka akubali mwito wa Mola wake. Aliposikia hivi, Musa alimchapa kofi kali la uso kiasi kwamba jicho lake moja liling’oka.

Hivyo alirudi kwa Allah na akalalamika kwamba amemtuma kwa mtu ambaye hataki kufa, na ambaye amemng’oa jicho lake moja. Allah akaponya jicho lake na akamuamuru arudi tena kwa Musa na amuambie kwamba, kama anataka maisha marefu, yapasa aweke mkono wake juu ya mgongo wa fahali wa ng’ombe. Ataishi miaka mingi kama idadi ya nywele zitakazofunikwa na mkono wake.”

Imam Ahmad bin Hanbal katika Musnad yake, Juz. 2 uk. 315, na Muhammad bin Jarir Tabari, katika kitabu chake chaTarikh, Juz. 1, chini ya kichwa cha habari, “Kifo cha Mtume Musa,” ametoa maelezo haya haya kutoka kwa Abu Hurira pamoja na nyongeza kwamba kufikia wakati wa Musa, Malaika wa mauti alikuwa akitoa roho (za watu) katika mwili kiwaziwazi. Lakini baada ya Musa kumchapa kofi la uso, alikuja bila kuonekana.”

Sasa ni juu yenu kuamua ni kichekesho gani hiki ambacho kimewekwa katika vitabu hivi viwili vya hadith, ambavyo mnaviita kuwa ni vya usahihi zaidi kuliko vitabu vyote baada ya Qur’ani Tukufu. Riwaya nilizoelezea hakika zinadhalilisha heshima za Mitume wa Allah.

Ama kwa Abu Huraira, sizishangai simulizi zake. Maulamaa wenu wenyewe wanakiri kwamba, ili apate kujaza tumbo lake kwa vyakula vyenye ladha vilivyotolewa na Mu’awiya, alibuni hadithi za uongo. Kwa sababu ya uzushi wake, Khalifa Umar alimpiga viboko. Ni jambo la kushangaza kwamba watu wenye akili wanaamini ngano kama hizi za kuchekesha.

Sasa ngoja turudi kwenye majadiliano yetu kuhusu hadith uliyonukuu. Ni dhahiri, mtu mkweli akiona hadith pekee (iliyosimuliwa na mtu mmoja) atailinganisha na hadith nyingine sahihi. Imma ataisahihisha au ataikataa moja kwa moja kuliko kuitumia kama msingi wa kuwashambulia ndugu zake wa madhehebu nyingine na kuwaita makafir.

Kwa vile kitabu Tafsiri-e-Safi hatunacho hapa, hatuwezi kusema chochote kuhusu usahihi wa hadith hii.

Hata kama ni kweli, yatupasa kutegemea juu ya kanuni kwamba, kama tunajua athari, tunaweza kujua sababu. Yaani, kama tunamjua Imam kama Imam, kwa hakika tunajua utambulisho wa Allah, katika njia ileile, ambayo kama mtu anamjua Waziri Mkuu, anamjua Mfalme. Ni kwa kuhusu kanuni hii kwamba Sura ya “Tawhid” na Aya nyingine za Qur’ani Tukufu zilishuka.

Zaidi ya hayo, kuna Hadith nyingi kuhusu upweke wa Allah zilizosimuliwa na Imam Husain mwenyewe na Maimamu wengine. Kumjua Imam wetu ni namna kubwa ya Ibada ya Allah. Maana hiyo hiyo imetolewa katika “Ziarat-e-Jami’a”, ambayo imefika kwetu kutoka kwa Mtukufu Imam. Tunaweza kuitafsiri pia kwa njia nyingine, kama wanachuo walivyofanya katika mambo kama haya. Mtekelezaji yoyote wa kitendo anaweza kuelewe- ka kwa asili ya kitendo chake.

Kwa vile Mtume na kizazi chake walifikia daraja ya juu kabisa katika uwezo wa kibinadamu, hakuna wengine wenye fadhila au ubora kama wao. Kwa kuwa hawa ndio njia dhahiri zaidi ya kumjua Allah, yeyote awajuaye hawa, anamjua Allah. Kama walivyosema wenyewe: “Ni kwa kupitia kwetu sisi, kwamba Allah anaweza kutumikiwa.” Tunaamini kwamba Ahlul Bait wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wametufundisha elimu kuhusu Allah na njia zinazostahili za kumuabudu Yeye. Wale ambao hawakuwafuata wamepotea njia.

Hadith Ya Thaqalain (Vizito Viwili).

Kusisitiza jambo hili hili, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema katika hadith inayokubali- wa na madhehebu zote. “Enyi watu (wafuasi) wangu! Mimi ninakuachieni kwa ajili yenu vitu viwili vizito (vya rejea): Kitabu cha Allah na Ahlul Bait wangu. Mtakapokuwa mumeshikamana na viwili hivi, kamwe, kamwe hamuwezi kupotea baada yangu, kwani kwa hakika viwili hivi kamwe havitatengana mpaka vinifikiea kwenye chemchem ya Kauthar.”

Hafidh: Hatutegemei juu ya hadith hii, ambayo unajaribu kuirudia. Kuna uzushi mwingi katika vitabu vyenu na mifano ya ushirikina, kama vile kutafuta kutekelezewa haja zetu kutoka kwa Maimamu zaidi kuliko kutoka kwa Allah. Ushirikina ni nini? Ushirikina una maana ya kumgeukia mtu mwingine yeyote au kitu zaidi kuliko kwa Allah kwa ajili ya kutekelezewa haja zetu. Imeonekana kwamba Mashi’a kamwe hawamuombi Allah. Wanawaomba Maimam. Hili si chochote, bali ni ushirikina.

Muombezi: Ninasikitika kwamba unapotosha ukweli. Labda ningeruhusiwa nikuelezeni ushirikina ni nini kwa mujibu wa maulamaa wakubwa wa Kiislamu na kwa mujibu wa aya za Qur’ani Tukufu.

Ushirikina Na Aina Zake:

Ushirikina ni wa aina mbili: Ushirikina wa wazi na ushirikina uliofichika. Ushirikina wa wazi una maana ya kumshirikisha mtu au kitu na Nafsi Kamili ya Allah au kumshirikisha na sifa Zake. Kumfanyia Allah washirika maana yake kushirikisha kitu na Upweke Wake na kuukiri ushirikishaji huu kwa ulimi, kama Sanamiyya (waabudu sanamu) au Mazorostania, ambao wanaamini katika kanuni mbili:

Nuru na giza. Wakristo pia wanafanya hivyo. Wanaamini katika utatu na kuugawanya uungu katika sehemu tatu - Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu. Wanaamini katika tabia tofauti za kila mmoja, na mpaka watatu hawa waungane, bila hivyo uungu wenyewe hautakuwa kamili. Qur’ani Tukufu inakataa imani hii, na Allah (s.w.t.) anaelezea upweke wake katika maneno haya:

لَقَدْ كَفَرَ الَّذِينَ قَالُوا إِنَّ اللَّهَ ثَالِثُ ثَلَاثَةٍ ۘ وَمَا مِنْ إِلَٰهٍ إِلَّا إِلَٰهٌ وَاحِدٌ ۚ{73}

“Kwa hakika wamekufuru wale waliosema: Hakika Allah ni Mmoja katika watatu; hali hakuna mungu ila Allah Mmoja….” (al-Maida; 5: 73).

Kushirikisha vitu na sifa za Uungu, maana yake ni kuamini kwamba sifa Zake, kama elimu Yake au nguvu ziko tofauti na, au ni nyongeza katika Nafsi Yake Kamilifu. Ashariyya wa Abu’l-Hasani Ali bin Ismail Ashari Basari, wanaelezewa na Maulamaa wenu wakubwa, kama Ali bin Ahmad katika kitabu chake Al-Kashf na Minhaju’l-Adilla fi Aqa’idi’l-Mila, Uk. 57 kuwa wanaamini kwamba Sifa za Allah ni nyongeza katika Nafsi Yake kamilifu, na kwamba ni za milele.
Hivyo yeyote mwenye kuamini kwa njia yeyote ile kwamba tabia au sifa yeyote ya Allah ni nyongeza katika Nafsi yake kamilifu, huyo ni mshirikina.

Kila sifa Yake ni yenye asili kwake. Ushirikina katika matendo ya mtu, ina maana kumshirikisha mtu mwingine katika Dhati Yake Yenye kujitosheleza Daima dumu. Mayahudi wanaamini kwamba Allah aliumba viumbe na kisha akajiweka mbali na viumbe Wake. Katika kuwalaumu watu hawa, aya ifuatayuo iliteremshwa:

وَقَالَتِ الْيَهُودُ يَدُ اللَّهِ مَغْلُولَةٌ ۚ غُلَّتْ أَيْدِيهِمْ وَلُعِنُوا بِمَا قَالُوا ۘ بَلْ يَدَاهُ مَبْسُوطَتَانِ يُنْفِقُ كَيْفَ يَشَاءُ ۚ{64}

“Na Mayahudi wanasema: Mkono wa Allah umefungwa! Mikono yao itafungwa (kwa pingu) na watalaaniwa kwa yale wanayoyasema. Bali, mikono yake yote iwazi; Hutoa apendavyo…” (5:64).

Ghullat wanaunda kundi lingine la washirikina. Pia wao wanaitwa Mufawwiza. Wanaamini kwamba, Allah ameweka au kuaminisha Mamlaka ya mambo yote kwa Maimam watukufu. Kwa mujibu wao, Maimam ni waumbaji na pia hutupatia sisi riziki. Kwa uwazi, wale wanaomuona mtu kuwa mshirika katika Mamlaka ya Uungu ni mshirikina.

Ushirikina Katika Swala:

Ushirikina katika Sala, ina maana ya mtu kugeuza mazingatio yake wakati wa swala kwa makusudi kuelekea kwa kiumbe aliyeumbwa badala ya kuelekea kwa Allah. Kama mtu akikusudia kuomba kwa kiumbe aliyeumbwa, huyo ni mshirikina. Qur’ani Tukufu inakataza haya katika maneno haya.

فَمَنْ كَانَ يَرْجُو لِقَاءَ رَبِّهِ فَلْيَعْمَلْ عَمَلًا صَالِحًا وَلَا يُشْرِكْ بِعِبَادَةِ رَبِّهِ أَحَدًا {110}

“…Anayetarajia kukutana na Mola Wake, naafanye vitendo vizuri, na asimshirik- ishe yeyote katika ibada ya Mola wake.” (18:110).

Aya hii inaonyesha kwamba sharti la msingi wa imani ni kwamba mtu lazima afanye lolote lile ambalo ni zuri na asije kumshirikisha yeyote pamoja na Allah katika kutoa utii na ibada Kwake. Kwa maneno mengine, yule ambaye anasali au kutekeleza Hija, au kufanya kitendo chochote kizuri kwa ajili tu ya kujionyesha kwa watu uzuri wake, ni mshirikina.

Amewashirikisha wengine pamoja na Allah katika jambo la kutekeleza vitendo vyake. Kuonyesha kujikinai kwa matendo mazuri ni ushirikina mdogo, ambao hutangua vitendo vyetu vizuri.

Imepata kuelezwa kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Jiepusheni na ushirikina mdogo.” Watu wakamuuliza, “Ewe, Mtume wa Allah, ni nini ushirikina mdogo? Akajibu: “Al-riya was-sama” (yaani, kuonyesha watu au kuwafanya wasikie juu ya ibada yako kwa Allah).

Vile vile Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Kitu kibaya mno ninachokuhofieni kwenu ni ushirikina uliofichika; hivyo kuweni na hadhi ya juu yake kwa kuwa miongoni mwa wafuasi wangu ushirikina ni wa siri mno kuliko kutambaa kwa mdudu chungu juu ya jiwe gumu katika usiku wa giza.”

Tena alisema: “Mtu ambaye anatekeleza ibada ya Sala kwa njia ya majivuno, ni mshirikina. Mtu ambaye anafunga au kutoa sadaka au kutekeleza Hija au kumuachia mtumwa huru ili kuonyesha kwa watu uadilifu wake au kujipatia jina zuri, ni mshirikina.”

Na kwa vile mistari hii ya mwisho inaelekeza kwenye mambo ya roho, umechanganywa katika ushirikina uliojificha.

Hafidh: Tunaona katika maelezo yako mwenyewe kwamba kama mtu atafanya maombi kwa kiumbe yeyote aliyeumbwa ni mshirikina. Hivyo Mashia nao ni washirikina, kwa vile wanafanya maombi kwa Maimamu watukufu na watoto wao.

Kuhusu Kuomba Au Ahadi:

Muombezi: Kama tunataka kuyakinisha imani ya jumuiya moja, hatupasi kutegemea juu ya watu wasio na ujuzi wa jumuiya hiyo. Yatupasa kusoma vitabu vyao vya kuaminika.

Kama unapenda kuuchunguza Ushi’a, usianze na Shi’a omba omba barabarani, wapigao makelele ya “Ya! Ali, Ya! Imam Ridha,” na kwa hoja hiyo, ukatangaza kwamba Mashi’a ni washirikina. Halikadhalika, kama mtu mjinga atafanya maombi au kiapo kwa jina la Maimamu au watoto wao, haipasi kuukashifu Ushi’a wote. Kama utasoma vitabu vya Sheria vya Shi’a, utaona kwamba hamna hata dalili moja ya ushirikina, au mambo ya upumbavu.

Msisitizo juu ya Upweke wa Allah uko wazi kila mahali. Vitabu mashuhuri zaidi, “Sharhe ya Lum’a, na Shara’i, vinapatikana kwa wingi na unaweza ukavichunguza. Katika Sura ya “Ahadi” (ya nadhiri) maelezo sahihi ya wanasheria wa Kishia yanatajwa katika vitabu vyote vilivyotajwa hapo juu na katika vitabu vingine vingi. Kwa kuwa nad- hir ni aina ya maombi, ni lazima kuwa na nia kwamba ni kwa ajili ya kujikurubisha kwa Allah (Kurbata ila llah).

Kuna Sharti mbili kwa nadhiri sahihi: Nia ya moyo na kutamka au kwa maelezo ya maneno ya lugha yoyote ile itakayokuwa. Kuhusu sharti la kwanza, nia ya moyo lazima iwe kwa ajili ya Allah. Sharti la Pili hukamilisha sharti la kwanza; mtu ambaye anafanya Nadhiri lazima aseme kwa maneno kwamba, ni kwa ajili ya Allah.

Kwa mfano, kama anaahidi kufunga au kuacha kunywa (ulevi), lazima aweke nia kwa kutumia maelezo ya maneno ambayo yana neno ‘lillah’ (kwa ajili ya Allah) bila ya hivyo nadhiri itakuwa batili.

Nadhiri Kwa Jina La Allah.

Kama tunafanya nadhiri isiyo kwa jina la Allah, bali kwa mtu mwingine, ikiwa amekufa au yuhai, au tukimchanganya pamoja na jina la Allah, hata kama ni Imam au mtoto wake, nadhir hiyo si sahihi. Kama hili likifanywa kwa makusudi na kwa kujua basi huo ni ushirikina wa dhahiri, kama ilivyo wazi kutoka kwenye Aya, “...Na usimshirikishe yoyote katika ibada ya Mola Wako. (18:110). Wanasheria (mafakihi) wa Kishi’a wanakubali kwamba, kufanya nadhiri kwa jina la mtu yoyote pamoja na Mitume au Maimam ni kosa. Kama ikifanywa kwa makusudi ni ushirikina.

Nadhiri yoyote lazima ifanywe katika jina la Allah, ingawa tumerehusiwa kufanya wakai wowote tunapopenda. Kwa mfano, kama mtu kwa jina la Allah atachukua mbuzi kumpeleka kwenye nyumba makhususi au sehemu ya ibada au kwenye kaburi la Imam au mtoto wa Imam na akamtoa dhabihu, hakuna madhara ndani yake.

Vilevile, kama akiahidi na kutoa fedha au nguo kwa jina la Allah kumpa Seyyid (mjukuu wa Mtume) maalum, au kutoa sadaka kumpa yatima, au muombaji, hakuna madhara ndani yake. Kwa kweli, kama mtu anaahidi kufanya nadhiri tu kwa ajili ya Mtume au Imam, au mtoto wa Imam au kwa ajili ya watu wengine, hiyo inakatazwa.

Ikifanywa kimakusudi, ni ushirikina. Ni wajibu wa kila Mtume au mwenye mamlaka ya kidini kuwaonya watu kama Qur’ani Tukufu inavyosema:

قُلْ أَطِيعُوا اللَّهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ ۖ فَإِنْ تَوَلَّوْا فَإِنَّمَا عَلَيْهِ مَا حُمِّلَ وَعَلَيْكُمْ مَا حُمِّلْتُمْ ۖ وَإِنْ تُطِيعُوهُ تَهْتَدُوا ۚ{54}

“Sema: Mtiini Allah na mtiini Mtume, na kama mkigueka basi juu yake kinabakia kile alichobebeshwa juu yake na juu yenu hubakia kile mlichobebeshwa juu yenu …” (24:54).

Ni wajibu wa watu kusikiliza kile anachokisema Mtume wa Allah na kukitekeleza. Walakini, kama mtu hajali kufuata mafundisho ya Kimungu na hayatekelezi, haiwezi kudhuru imani au kanuni ambazo ndani yake imani imesimamishwa.

Ushirikina Uliofichika: Kujionyesha Katika Sala.

Aina ya pili ya ushirikina ni ule ushirikina uliofichika, kama vile kufanya kujionyesha Sala zetu au namna zingine za utiii kwa Allah. Tofauti kati ya ushirikina huu na ule ushirikina wa katika Sala, ni kwamba kuhusu suala la ushirikina katika Sala tunashirikisha kitu kingine au kiumbe pamoja na Allah.

Kama mtu ataelekeza nia yake kwenye kitu kingine mbali na Allah, katika Ibada ya Sala, au kama kwa ushauri wa Shetani, akawa na picha bandia ya Mungu katika mawazo yake, au kama kiongozi wake ndio kiini cha nia yake, basi ni mshirikina.

Hakuna isipokuwa Allah Ndiye apasaye kuwa mlengwa wa nia katika ibada zetu. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema kwamba, kama mtu atafanya kitendo kizuri na akafanya mtu mwingine kuwa mshirika pamoja na Allah ndani yake, basi kitendo chake chote ni kwa ajili ya yule mshirika. Allah anachukia kitendo hicho na mtendaji wake pia. Vile vile imesimuliwa kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema kwamba,

“Kama mtu akifanya ibada ya Sala, au kufunga, au kutekeleza Hija na ana mawazo kwamba kufanya kwake hivyo watu watamsifu, “basi hakika, amefanya mshirika pamoja na Allah katika kitendo chake.”

Vilevile imesimuliwa kutoka kwa Imam Ja’far Sadiq kwamba kama mtu atafanya kitendo kwa kumuogopa Allah, au kwa ajili ya malipo ya Akhera na akachangaya ndani yake rid- haa ya binaadamu, basi mtendaji wa kitendo hicho ni mshirikina.

Ushirikina Kuhusiana Na Kisababisho

Aina moja ya ushirikina ni ile ambayo huhusishwa kwenye kisababisho, kwa kuwa watu wengi huweka matumaini yao na hofu juu ya kisababisho cha pili. Huu pia ni ushirikina, lakini unasameheka. Ushirikina una maana yakufikiri kwamba uwezo wote kiasili unatokana na kisababisho cha pili. Kwa mfano, jua hustawisha vitu vingi ulimwenguni, lakini kama mtu atafikiria uwezo huu ni wa msingi katika jua (yaani asili yake inatokana na jua lenyewe), basi huu ni ushirikina.

Walakini, kama tunaamini kwamba jua limepata uwezo huu kutoka kwa Allah, na kwamba jua ni kisababisho cha pili tu cha ukarimu wake, basi huu kamwe sio ushirikina. Bali hasa ni namna ya Ibada, kwa kuwa kutafakari juu ya ishara za Allah ni mwanzo wa kumwabudu Allah. Utajo umefanywa katika Aya za Qur’ani Tukufu kwenye ukweli huu kwamba yatupasa kutafakari juu ya ishara za Allah kwa kuwa hii huongozea kwenye mazingatio juu ya Allah.

Kwa njia hiyo hiyo, kutegemea juu ya kisababisho cha pili (nadhari ya mfanya biashara kwenye biashara, au nadhari ya mkulima kwenye shamba lake) humfanya mtu kuwa mshirikina kama kwa sababu hii atageuza mazingatio yake kunyume kutoka kwa Allah.

Kwa msingi wa maelezo ya ushirikina ya hapo juu, ni upi katika mifano iliyoelezwa hapo ambao unafikiri unatumika kwa Mashi’a? Ni kwa namna gani kutokana na mtazamo wa Sala, imani au hadithi za Shi’a ambayo umeiona, inayoweza kuwafanya washambuliwe kwa ushirikina?

Hafidh: Nakiri kwamba yote uliyosema ni sawasawa, lakini kama utachukua taabu ya kufikiri kidogo, utakubali kwamba kutegemea juu ya Maimam ni ushirikina. Kwa kuwa haitupasi kutafuta njia yoyote ya kibinadamu kumfikia Allah, yatupasa kumwomba Allah moja kwa moja kwa ajili ya kutaka msaada.

Kwanini Mitume Walitafuta Misaada Kutoka Kwa Watu?

Muombezi: Inashangaza kwamba unapuuza niliyokuwa nikisema hapa wakati wote huu. Je ni ushirikina kufanya maombi kwa watu wengine kwa ajili ya kutekelezewa haja zetu? Kama hii ingekuwa kweli, umma wote wa binadamu kwa ujumla basi ni wa kishirikina. Kama kuomba msaada kwa wengine ni ushirikina, kwa nini Mitume waliomba misaada kutoka kwa watu? Yakupasa uzichunguze aya za Qur’ani Tukufu ili upate kujua kipi ni kweli na sahihi. Aya zifuatazo zinafaa kuzingatiwa:

“Akasema: ‘Enyi wakuu! Ni nani atakayeniletea kiti chake cha enzi kabla hawajakuja kwangu, hali ya kuwa wamekwisha sslimu amri?Mjasiri mmoja miongoni mwa majini akasema: ‘Mimi nitakuletea kabla hujainuka mahali pako hapo na mimi bila shaka ninazo nguvu za hayo (na) ni muaminifu.’ ‘Akasema yule aliyekuwa na ilmu ya Kitabu: ‘Mimi nitakuletea kabla ya kupepesa jicho lako’ basi alipokiona kimewekwa mbele yake alisema: ‘Haya ni kwa fadhila za Mola wangu…..’” (28; 38-40)

Uletaji wa kiti cha Enzi cha Bilqis (Malikia wa Sheba) kwa Sulaiman ulikuwa hauwezekani kwa kila kiumbe. Kwa kukiri kabisa, ilikuwa sio kawaida, na Mtume Sulaiman, pamoja na kujua kwake kwamba ilihitaji uwezo wa Ki-Mungu, hakumuomba Allah kuleta kiti hicho cha enzi, bali aliomba viumbe wa kawaida tu kumsaidia. Ukweli huu unaonyesha kwamba kuomba msaada wa wengine sio ushirikina.

Allah, kisababisho cha kwanza, ndiye Muumba wa visababisho vya ulimwengu huu. Ushirikina ni jambo la moyo. Kama mtu anaomba msaada wa mwingine na hamfikirii yeye kuwa ni Allah au mshirika Wake, haikatazwi. Hali hii ni ya kawaida kila mahali. Watu huenda kwenye nyumba za wengine na kuomba msaada bila kuchukua jina la Allah.

Kama nikienda kwa Daktari na nikamuomba aniponyeshe, je, nitakuwa mshirikina? Tena kama mtu anakufa maji, na akapiga kelele za kuomba msaada hivi atakuwa ni mshirikina? Hivyo tafadhali kuwa muadilifu na usipoteze ukweli. Jumuiya yote ya Shi’a inaamini kwamba, kama mtu atafikiria kizazi cha Mtume kuwa ni Allah au washirika katika Dhati (Nafsi) Yake, hakika yeye ni mshirikina. Utakuwa umewasikia Mashi’a wakiwa katika shida wakilia, “Ya Ali, nisaidie!” Ya Husain, nisaidie!” Lakini ukweli ni kwamba, kwa kuwa ulimwengu ni nyumba ya visababisho vya pili, tunawafikiria wao kama njia ya kutolewa katika shida. Tunaomba msaada wa Allah kupitia kwao.

Hafidh: Badala ya kumuomba Allah moja kwa moja, kwa nini muombe visababisho?”

Muombezi: Matarajio yetu ya kudumu kuhusu haja zetu, dhiki, na hofu yamewekwa juu ya Allah, Mkamilifu. Lakini Qur’ani Tukufu inasema yatupasa kumfikia Allah, kupitia baadhi ya njia (visababisho) za kupelekea.

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّهَ وَابْتَغُوا إِلَيْهِ{35}

“Enyi ambao mmeamini! Mcheni Allah na tafuteni njia ya kumfikia Yeye…” (5:35).

Dhuria Watukufu Wa Muhammad Ni Njia (Wasyla – Visababisho)

Ya Neema Za Mungu.

Sisi Shi’a hatuwachukulii kizazi cha Mtume kama ufumbuzi wa matatizo yetu yote. Tunawaona wao kama wacha Mungu zaidi katika waja wa Allah na kama njia za neema za Mungu. Tunajiambatanisha wenyewe kwenye ile familia bora zaidi kwa mujibu wa maamrisho ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Hafidh: Kwa nini unasema kwamba, maneno: “Njia ya kumfikia (Wasyla)” katika Aya hiyo hapo juu yanawahusu kizazi cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)?”

Muombezi: Katika hadith nyingi, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), amependekeza kwetu, kwamba katika shida zetu tuwaombe watoto wake kama njia ya kumfikia Allah. Wengi wa Maulamaa wenu, kama Hafiz Abu Nu’aimi Isfahani katika kitabu chake “Nuzulu’l-Qur’ani fi Ali” (Ufunuo katika Qur’ani kuhusu Ali), Hafiz Abu Bakr Shiraz katika kitabu chake “Ma Nazala mina’l-Qur’ani fi Ali” na Imam Ahmad Tha’labi katika Tafsir (Sharhe) yake anasema kwamba Wasilat (njia ya kumfikia) katika aya hiyo hapo juu ina maana ya watoto wa Mtume (s.a.w.w.).

Maneno haya yamekuwa wazi kwenye hadith nyingi za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Ibn Abi’l-Hadid Mutazali, mmoja wa Mualamaa wenu maarufu, anase- ma katika “Sherhe Nahjul’l-Balagha” yake, Juz. 4, Uk, 79, kwamba Bibi Fatima Zahra, alitaja maana ya maneno ya Aya hii mbele ya Muhajirina na Ansari, wakati anatoa khutuba yake yenye kuhusu kunyang’anywa shamba lake la Fadak, katika maneno haya: “Namshukuru Allah Ambaye kwamba Ukuu Wake na Nuru Yake, Wakazi wa mbinguni na ardhini hutafuta njia ya kumfika Yeye. Miongoni mwa viumbe Wake sisi ni njia (Wasilat) ya kumfikia Yeye.”

Hadith Ath-Thaqalain (Hadith Ya Vizito Viwili).

Miongoni mwa hoja zetu nyingi zinazokubaliwa kuhusu uhalali wa kufuata kwetu kizazi cha Mtume ni “Hadith ath-Thaqalain” - vizito viwili, ambayo usahihi wake umekubaliwa na Madhehebu zote. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Kama mtashikamana na viwili hivi, kamwe, hamtapotea baada yangu.”

Hafidh: Nafikiri umekosea wakati unaposema kwamba hadith hii ni sahihi na kwamba inakubaliwa na wote kwa kuwa haijulikani kwa Maulamaa wetu mashuhuri. Kuthibitisha haya naweza kusema kwamba, msimuliaji mkubwa wa hadith wa madhehebu yetu, Muhammad bin Ismaili Bukhari, haisimulii katika Sahih yake, ambacho ndio kitabu sahi- hi zaidi baada ya Qur’ani.

Muombezi: Sikukosea kuhusu hadith hiyo. Usahihi wa hadith hii tukufu umekubaliwa na Maulamaa wenu wenyewe. Hata Ibn Hajar Makki, pamoja na uchungu wake na chuki, anakubali ukweli wake. Yakupasa uangalie katika “Sawai’q Muhriqah (Sehemu ya 2, Sura ya 2, Uk. 89-90, chini ya aya ya 4) ambamo ndani yake, baada ya kunukuu maelezo ya Tirmidhi, Imam Ahmad bin Hanbali, Tabrani, na Muslim, anasema:

“Elewa kwamba hadith inayohusu kujiambatanisha na Thaqalain - vizito viwili (Ahlul-Bait wa Mtume na Qur’ani) imesimuliwa katika njia nyingi. Wasimuliaji wa hadith hii idadi yao ni zaidi ya ishirini, wote ni Masahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).”

Kisha anasema kwamba kuna baadhi ya khitilafu ya namna ambayo kwayo hadith hii imesimuliwa. Wengine wanasema kwamba ilisimuliwa wakati Mtume yuko kwenye Hija yake ya mwisho huko Arafa; baadhi wanasema ilisimuliwa Madina, wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) yuko kwenye kitanda alichofia na chumba chake kilikuwa kimejaa Masahaba wake; wengine wanasema kwamba ilisimuliwa huko Ghadir-Khum; na wengine wanasema ilisimuliwa baada ya kurudi kwake kutoka Ta’if.

Baada ya kusema yote haya, yeye (Hajar Makki) mwenyewe anafafanua kwamba hakuna khitilafu ya wazi katika hadith yenyewe. Ama kwa tofauti ya sehemu, huenda ilikuwa kwamba Mtume amerudia kusimulia hadith hii katika nyakati tofauti na mara kwa mara (sehemu mbalimbali) kwa ajili ya kusisitiza ukubwa wa Qur’ani na kizazi chake kitukufu.

Umesema kwamba, kwa kuwa Bukhari hakuisimulia hadith hii katika Sahih yake, basi usahihi wake ni wa mashaka. Lakini hadith hii, ingawa haikuandikwa na Bukhari, imesimuliwa kiujumla na maulamaa wakubwa wa madhehebu yenu, pamoja na Muslim bin Hajjaj na waandishi wengine wa vitabu sita vya hadith, ambao wameziandika katika vitabu vyao kwa ukamilifu sana, na hawategemei ukusanyaji wa Bukhari tu peke yake.

Kama unakubali uadilifu wa Maulamaa wako wote mwenyewe, ambao wote walitambuliwa na Masunni waliopita, yapasa ukubali hadithi hii kwamba ni ya kweli, ambayo kwa sababu fulani haikuandikwa na Bukhari.

Hafidh: Hakuna sababu ya kuunga mkono kutokuiandika hadith hii. Bukhari alikuwa makini sana katika suala la kusimulia hadithi. Alikuwa ni mwanachuo mwangalifu sana, na kama aliona hadith, kwa mtazamo wa maudhui au chanzo chake, kuwa yenye madhara au kutokubalika na akili za kawaida, yeye hiyo hakuiandika.

Muombezi: Kama mithali inavyosema: “Kupenda sana kitu humfanya mtu kuwa kipofu na kiziwi.” Waheshimiwa Masuni wamekosea hapa, una shauku kubwa katika upendo wako kwa Imam Bukhari. Unasema alikuwa mchunguzi sana wa mambo, na kwamba simulizi zilizomo katika Sahih yake ni za kuaminika na kustahiki sifa ya Wahayi (Ufunuo). Lakini ukweli ni kinyume chake. Nyororo ya riwaya zilizotajwa na Bukhari zina watu ambao mara kwa mara wameshutumiwa kama waongo.

Hafidh: Madai yako sio ya kweli. Unashusha elimu na uwezo wa Bukhar, ambavyo ni tusi kwa madhehebu yote ya Sunni.

Muombezi: Kama uchunguzi ulioko juu ya msingi wa elimu ni matusi, basi wengi wa Maulamaa wenu maarufu ni watu ambao wamekebehi ile nafasi ya juu ya elimu na maarifa.
Ningependa kukushauri uvichunguze mwenyewe vitabu vilivyoandikwa na waandishi wakubwa na maulamaa wa madhehebu yenu ambao wameandika Sherhe juu ya Sahih Bukhari, k.m. “Al-Lu’ali’l- Masnu’a fi hadith’l-Mazu’a” ya Suyuti, “Mizanu’l-ibtidal” na Talkhisu’l-Mustadraka” ya Dhahabi; “Tandhkiratu’l-Mazu’a” ya Ibn Jauzi, “Tarikh Baghdad” kilichokusanywa na Abu Bakar Ahmad bin Ali Khatib Baghadad, na vitabu vingine vya “Ilm Rijal” (vinavyoitwa, makala juu ya sifa za wasimuliaji) vilivyoandikwa na maulamaa wenu wengi wakubwa. Kama utasoma vitabu hivi, hutathubutu kusema kwamba nimemkebehi Imam Bukhari.

Bukhari Na Muslim Wameandika Hadith Nyingi Zilizosimuliwa Na Wazushi.

Nilichosema ni hiki: Vitabu hivi viwili, Sahih Bukhari na Sahih Muslim, vina hadithi zili- zosimuliwa na waongo. Kama utavichunguza Sahih Muslim na Sahih Bukhari katika mwanga wa vitabu vya “Rijal” (yaani vitabu vyenye kuelezea maisha na tabia za wasimuliaji wa hadith), utaona kwamba wameandika hadith nyingi zilizosimuliwa kutoka kwa watu ambao walikuwa waongo wakubwa, kwa mfano Abu Huraira, muongo mwenye sifa mbaya, Ikrima Kharji, Sulaiman bin Amri, na wengine wa namna hiyo hiyo.

Bukhari hakuwa makini katika kuandika Hadith kama unavyofikiri. Hakuiandika “Hadith ya Thaqalain” ambayo wengine wameiandika, lakini hakusita kuandika ngano za kufedhehesha na matusi kuhusu Mtume Musa akimpiga kofi la uso Malaika wa Mauti, Mtume Musa akikimbia akiwa uchi mbele za watu akifukuza jiwe, na juu ya kuonekana kwa Allah (s.w.t.).

Fikiria ngano nyingine ya kudhihaki na matusi iliyoandikwa na Bukhari katika Sahih yake, Juz. 2, uk. 120, Sura ya “Al’Lahr Bi’l-Harb,” na Muslim katika Sahih yake Juz. 1, akimnukuu Abu Huraira akisema kwamba siku ya Idd baadhi ya mabedui kutoka Sudani walikusanyika katika Msikiti wa Mtume. Waliwaburudisha watazamaji kwa michezo na maonyesho yao.

Mtume akamuuliza Aisha (Mke wake - Mama wa Waumini) kama angependa kuona hayo maonyesho. Aisha, akasema anapenda kuyaona. Mtume akamfanya (Aisha) apande juu ya mgongo wake kwa hali ambayo kichwa chake kilikuwa juu ya mabega yake na uso wake juu ya kichwa cha Mtume.

Ili kumfurahisha Aisha, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akiwaomba wachezaji kuonyesha mchezo (dansa) nzuri zaidi. Mwishowe Aisha alichoka, na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akamuacha ateremke chini! Amua mwenyewe iwapo ngano kama hii haifedheheshi.

Kama Bukhari alikuwa makini kuhusu kusimulia mambo, je, ilikuwa inafaa kwa upande wake kuandika ngano za kipuuzi kama hizi katika Sahih yake? Lakini ni mpaka sasa unaviainisha vitabu hivi kuwa ndio sahihi zaidi baada ya Qur’ani Tukufu. Hakika Bukhari alichukua tahadhari maalum kuliacha jambo la Uimamu na Umakamu wa Ali (a.s.) na hivyo hivyo suala la Ahlul-Bait. Huenda aliogopa maelezo kama hayo yangeweza yakatu- mika siku moja kama silaha dhidi ya wapinzani wa Ahlul-Bait.

Hadith Nyingi Sahihi Zihusuzo Ahlul-Bait Ziliepukwa Kwa Makini Sana.

Hivyo wakati tukilinganisha Sahih Bukhari na Sahih nyinginezo, tunafikia kwenye uamuzi juu ya suala hili kwamba hadith yoyote yenye kuwahusu Ahli Bait, hata iwe sahihi vipi na kuungwa mkono kikamilifu na waandishi katika mwanga wa Qur’ani, Bukhari kwa makusudi alishindwa kuiandika.

Kwa mfano, kuna Aya nyingi za Qur’ani Tukufu, ambazo zina muelekeo wa moja kwa moja juu ya Ahadith (Hadhithu’l-Wilaya katika siku ya Ghadir; Hadith Inzar Yaumu’d-Dar; Hadithu’l-Muwakhat; Hadithus-Safina; Hadith Babu’l-Hitta n.k.) ambazo zinahusu, heshima juu yao, na umakamu wao dhuria wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Hizi Bukhari ameziacha kwa uangalifu na umakini sana.

Na kwa upande mwingine, zile zinazoitwa eti ni “Hadith” ambazo zinawatweza Mitume, hususan Mtume wetu na kizazi chake kilicho safi, zimeandikwa katika kitabu chake bila hata kufikiria kidogo kwamba zimesimuliwa na waongo.

Vyanzo Vya Hadith Ya Thaqalain.

Ama kwa hadith ya Thaqalain (Vizito viwili), ambayo Bukhari hakuiandika katika kitabu chake, vitabu vingine sahihi vya madhehebu yenu vimeisimulia. Kusema kweli, hata yule mwanahadith mkubwa, Muslim, ambaye anafikiriwa kuwa sawa na Bukhari, yeye pia ameisimulia.

Wanachuo wengine ambao wameisimulia hadith hii ni hawa wafuatao: Muslim bin Hajaji katika “Sahih” yake Juz. 7, uk. 122; Abu Dawud katika “Sahih” yake; Tirmidhi katika “Sunan” yake, sehemu ya 2, uk. 307; Nisa’i katika “Khasa’is” yake uk. 30; Imam Ahmad bin Hanbal katika “Musnad” yake Juz. 3, uk. 14-17, Juz. 4, uk. 26 na 59 na Juz. 5, uk. 182 na 189; Hakim katika “Mustadrak” Juz. 3, uk. 109 na 148; Hafidh Abu Nu’aim Isfahani katika Hilyatu’l-Auliya, Juz. 1, uk. 355; Sibt Ibn Jauzi katika Tadhkira yake, uk. 182; Ibn Athir Jazari katika “Usudu’l-Ghaiba”, Juz. 2, uk. 12 na Juz. 3, uk. 147; Hamidi katika “Jama’Baina-s-Sahihain” Razin katika “Jama’Baina-s-Siha-e-Sitta”; Tabran katika “Tarikh al-Kabir”; Dhahabi katika Talkh is-e-Mustadrak.

Ibn Abd Rabbih katika “Iqdu’l-Faridh” yake; Muhammad bin Talha Shafi’i katika “Matalibus-Su’ul”; Khatib Khawarizmi katika “Manaqib” Sulayman Balkhi Hanafi kati- ka “Yanabiu’l-Mawaddatu”, uk. 18, 25, 29, 30, 31, 32, 34, 95, 115, 126, 199 na 230, pamo- ja na tofauti ndogo katika maneno; Mir Seyyid Ali Hamadani katika “Mawadda” ya pili ya “Mawaddatu’l-Qurba;” Ibn Abi-l-Hadid katika “Sherh Nahju’l-Balaghah”; Shablanji katika “Nuru’l-Absar” uk. 99; Nuru’d-Din Sabbagh Maliki katika “Fusulu’l-Muhimma” uk. 25; Hamwaini katika “Fara’idus-Simtain”; Imam Tha’labi katika “Tafsir Kasfu’l-Bayan”; Sam’ani na Ibn Maghazili Shafi’i katika “Manaqib”; Muhammad bin Yusufu Ganji Shafi’i katika “Kifayatu’l-Talib”, Sura ya 1, katika maelezo ya usahihi wa Khutuba ya Ghadir Khum na vilevile katika Sura 62, uk. 130; Muhammad bin Sa’ad Khatib katika “Tabaqat”, Juz. 4, uk. 8; Fakhru’d-Din Razi katika “Tafsir Kabir” Juz. 3, chini ya Aya I’tisma (3:103), uk. 18; Ibn Kathir Damishqi katika “Tasfir” Juz. 4 chini ya aya ya Mawadda (42:23), uk. 113, Ibn Hajar Makki katika “Sawa’iq-e-Muhriqah” uk. 75, 87, 90, 99 na 136 pamoja na tofauti ya maneno.

Kuna wanachuo wengine kadhaa wa madhehebu yenu ambao majina yao siwezi kuyataja katika mkutano huu kutokana na uhaba wa muda. Wengi wa wanachuo wenu wameisimulia hadith hii muhimu kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa wingi sana na kwa mfu- atano usiokatika wa usimuliaji kutoka kwa mmoja hadi mwingine kiasi kwamba imepata hadhi ya hadith inayosimuliwa mara kwa mara.

Kwa mujibu wa hadith hii, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema yafuatayo: “Ninaacha kati yenu vitu viwili vizito; Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Ahlul-Bait wangu. Kama mtaambatana na viwili hivi, kamwe, kamwe hamtapotea. Viwili hivi havitatengana mpaka vije vinifikie kwenye Haudhi ya Kauthar.”

Kwa msingi wa hadith hii Sahihi, tunaona kwamba yatupasa kutafuta mshikamano kwenye Qur’ani Tukufu na Ahlul-Bait wa Muhammad (s.a.w.w.).

Sheikh: Hadith hii ya Mtume imesimuiliwa na Salih bin Musa bin Abdullah bin Ishaq, kupitia nyororo yake ya wasimuliaji waaminifu, akisema kwamba Abu Huraira ameisimulia katika njia hii: “Ninakuachieni vitu viwili vizito: Kitabu cha Allah (Qur’ani Tukufu) na Sunna zangu (Mwenendo)….”

Muombezi: Unanukuu tena hadith kutoka kwa mkorofi yule yule ambaye amepuuzwa na wakosoaji wa Shi’a (Kama Dhahabi, Yahaya, Imam Nisai, Bukhari na Ibn Adi, n.k.). Je, hutosheki na rejea za kuaminika ambazo nimezifanya kutoka Maulamaa wenu wenyewe wakubwa kuhusu hadith hii? Unanukuu maneno yasiyokubalika ya Hadith japokuwa Mashi’a na Masunni wote kwa pamoja wamekubali kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ametumia maneno, “Kitabu cha Allah na kizazi changu”, na sio “Sunna zangu.”

Kusema kweli “Kitabu” (Qur’ani) na “Sunna” (mwenendo) vyote vinahitaji tafsir. Kwa hiyo Sunna haiwezi kuelezea Qur’ani Tukufu.

Hivyo kizazi cha Mtume ambao ndio sawa na Qur’ani Tukufu ndio Wafasir halisi wa Qur’ani Tukufu na Sunna za Mtume (s.a.w.w.) vilevile.

Hadith Ya Safina.

Sababu nyingine inayotufanya tutafute kushikamana na kizazi cha Mtume ni hadith sahih, “Hadith ya Safina”, ambayo imesimuliwa na Maulamaa wenu wote wakubwa, takriban bila kuacha hata mmoja, na mlolongo usiovunjika.

Zaidi ya Wanachuo wenu mia moja wenyewe wameisimulia hadith hii: Muslim bin Hajjaj katika “Sahih” yake, Imam Ahmad bin Hanbal katika “Musnad”, Hafidh Abu Nu’aim kati- ka “Hilyatu’l-Auliya.” Ibn Abdi’l-Birr katika “Isti’ab.” Abu Bakar Khatib Baghdadi kati- ka “Ta’rikh Baghdad”; Mohammed bin Talha, Shafi’i katika “Matalibus-Suul;” Ibn Athir katika “Nihaya” Sibti Ibn Jauzi katika “Tadhkira”; Ibn Sabbagh Makki katika “Fusulu’l- Muhimma”; Allama Nuru’d-Din Samhudi katika “Ta’rikhu’l-Madina” Sayyid Mu’min Shablanji katika “Nuru’l-Absar;” Imam Fakhni’d-Din Razi katika “Tafsir Mafatihu’l- Ghaib”, Jalalu’d-Din Sayuti katika “Durru’l-Manthur”; Imam Tha’labi katika “Tafsir Kasfu’l-Bayan”, Tabrani katika “Ausat”; Hakim katika “Mustadrak” Juz. 3, uk, 151; Sulayman Balkhi Hanafi katika “Yanabiu’l-Mawadda”, Sura ya 4, Mir Seyyid Ali Hamadani katika “Mawaddatu’l-KurbaMawadda ya 2; Ibn Hajar Makki katika “Sawa’iqu’l-Muhrikah” chini ya Aya 8; Tabari katika “Tafsir” yake, na vilevile katika “Tarikh” yake; Muhammad bin Yusufu Ganji Shafi’i katika “Kifayatu’l-Talib.” Sura ya 100, uk. 233.

Maulamaa wengine wengi wa madhehebu yenu wamesimulia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Mfano wa Ahlul-Bait wangu ni ule wa Safina ya Nuh. Ambaye ataipanda ataokolewa; ambaye anaipa mgongo atazama na kuangamia.”

Imam Muhammad bin Idris Shafi’i amerejea kwenye Hadith hii Sahih katika beti zake za mashairi ambazo Allama Fazil Ajib ameziandika katika “Dhakhiratu’l-Ma’al.” Imam Shafi’i, ambaye anatambuliwa kama mmoja wa wanachuo maarufu wa madhehebu ya Suni, anakiri kwamba, kushikamana kwetu na familia iliyotoharishwa ya Mtume ni njia ya wokovu wetu kwa sababu, kati ya Madhehebu sabini za Uislam, ile madhehebu ambayo inafuata kizazi cha Mtume ndiyo peke yake itakayopata wokovu.

Kutafuta Njia Ya Kumfikia Allah Sio Ushirikina.

Umesema kwamba kutafuta njia ya kumfikia Allah ni ushirikina. Kama hii ilikuwa kweli, kwa nini Umar bin Khatib alitafuta msaada wa Allah (swt.) kupitia kwa kizazi cha Mtume?

Hafidh: Khalifa Umar kamwe hajafanya hivyo.

Muombezi: Katika nyakati za shida Umar alitafuta msaada wa kizazi cha Mtume, Alimwomba Allah kupitia kwao, na mahitaji yake yalitekelezwa. Ninarejea kwenye matukio mawili tu. Ibn Hajar Makki anaandika katika “Sawa’iq-e-Muhriqah,” baada ya Aya ya 14 (kutoka kwenye Tarikh Damascus) kwamba katika mwaka wa 17 Hijria watu waliswali kwa ajili ya kuomba mvua lakini hawakufanikiwa.

Khalifa Umar akasema kwamba angesali kwa ajili ya mvua siku ifuatayo kupitia njia ya kumfikia Allah. Asubuhui yake alikwenda kwa Abbas, ami yake Mtume na akasema: “Toka nje ili tuweze kumuomba Allah kupitia kwako kwa ajili ya mvua.”

Abbas alimuomba Umar akae kidogo ili kwamba hio njia ya kufikia kwa Allah ipatikane. Basi, Bani Hashim (Ahlul-Bait) walijulishwa. Kisha Abbas akatoka nje pamoja na Ali, Imam Hassan na Imam Husein. Bani Hashim wengine walikuwa nyuma yao. Abbas akamwambia Umar kwamba mtu yoyote mwingine asiongezwe kwenye kundi lao.

Kisha walikwenda sehemu ya kuombea ambapo Abbas alinyanyua mikono yake kwa ajili ya maombi na akasema: “Ya Allah! Wewe ndio umetuumba sisi, na unajua kuhusu vitendo vyetu. Ya Allah! Kama ulivyokuwa Mwema kwetu mwanzoni, hivyo kuwa Mwema kwetu mwishoni.” Jabir anasema kwamba du’a yao ilikuwa bado haijakwisha wakati mawingu yalipojitokeza na ikaanza kunyesha. Kabla hawajafika nyumbani kwao, walikwishalowa.

Bukhari pia anasimulia kwamba, siku moja wakati wa ukame Umar bin Khatib alimuom- ba Allah kupitia kwa Abbas bin Abdu’l-Muttalib na akasema:
“Tunatuma maombi sisi wenyewe kupitia kwa ami yake Mtume wetu; hivyo, Mwenyezi Mungu tunyeshee mvua.” Kisha ilianza kunyesha. Ibn Abi’l-Hadid Mutazili katika “Sherhe Nahju’l-Balaghah” (Chapa ya Misri), uk. 256, anaandika kwamba Khalifa Umar alikwenda pamoja na Abbas, ami yake Mtume, kumuomba Allah kwa ajili ya mvua.

Katika maombi yake kwa ajili ya mvua, Khalifa Umar alisema: “Ya Allah! Tunaleta maombi wenyewe kupitia kwa ami yake Mtume Wako, na kwa jadi yake na kwa watu wao maarufu waliobakia. Hivyo linda cheo cha Mtume wako kupitia kwa Ami yake. Tulikuwa tumeongozwa Kwako kupitia kwa Mtume, ili kwamba tutafute msaada wao na kufanya toba.”

Kama kuwatafuta kizazi cha Mtume na kuwaendea kwa ajili ya haja zetu katika njia ya Allah ni ushirikina, basi Khalifa Umar alikuwa mshirikina wa kwanza. Kizazi cha Muhammad (s.a.w.w.), kutoka wakati wa Mtume mpaka leo hii, wamekuwa ndio njia ya kupitia (Wasilat) katika du’a na maombi yetu kwa Allah. Tunawachukulia tu kama watu wacha-Mungu sana na walio karibu mno na Allah. Kwa hiyo tunawaona wao ni njia ya kutufikisha kwa Allah. Na uthibitisho mzuri wa hili ni vitabu vyetu vya Dua zilizoelezwa na Maimam wetu Ma’asum. Tunakubali maelekezo ya Maimam wetu.

Hapa ninavyo vitabu viwili: “Zadu’l-Ma’ad” cha Allama Majlisi na “Hidayatuz-Za’irin” cha Sheikh Abbas Qummi, ambavyo ninavitoa kwako ili uvichunguze. (Wote wawili Hafidh na Sheikh walichunguza vitabu vile). Waliisoma Du’a ya Tawassul, na waliona kwamba Ahlul-Bait wa Mtume walikuwa ni sehemu ya du’a. Kila mahali walikuwa wametajwa kama njia ya kufikia kwa Allah.

Katika muda ule Mulla Abdu’l-Hayy alisoma Du’a yote ya Tawassul, iliyoelezwa na Maimam watoharifu na kunukuliwa na Muhammad bin Babawayh Qummi.

Dua Ya Tawassul.

Haya ni maombi kwa Allah. Kama Ali ambavyo ametajwa hapa, na Maimam wote wametajwa kwa hali hiyo hiyo. Athari ya Ahlul-Bait wa Mtume inatafutwa kutufikisha kwa Allah. Wanatajwa namna hii: “Ewe Bwana wetu na kiongozi wetu! Tunatafuta msaada wako wa kutufikisha kwa Allah. Ewe unayeheshimika zaidi mbele ya Allah: Tuombee sisi Kwake.” Ahli Bait wote wa Mtume wametajwa katika hali hiyo hiyo.

Mashia Hawawasingizii Masunni.

Wakati du’a hii ilipokuwa ikisomwa, baadhi ya mabwana waungwana wa Kisuni waliguta kwa mshangao na butwaa na masikitiko juu ya kutoelewana kukubwa kulikosababiwa na watu. Muombezi akauliza: Je, kuna dalili yoyote ya ushirikina katika du’a hii? Je, jina tukufu la Allah halipatikani kila mahali? Ni watu wenu wangapi wasioelewa na wasio wavumilivu ambao wamewauwa Mashi’a wa watu masikini, wakiamini kwamba wameua mshirikina? Lawama juu ya mambo haya moja kwa moja ni juu ya maulamaa kama ninyi wenyewe.

Je, umewahi kusikia hata siku moja kwamba Shi’a mmoja amemuua Sunni? Ukweli ni kwamba maulamaa wa Kishi’a hawaenezi sumu.

Hawajengi chuki baina ya Shi’a na Sunni, na wanaona kuua kwamba ni dhambi kubwa. Katika mambo ya tofauti ya imani kati yao, wanafafanua misimamo kwa majadiliano yaliyojengeka juu ya msingi wa elimu na mantiki, na kufanya ijulikane kutokana na mazungumzo yao kwamba Sunni ni ndugu zao.

Maulamaa Wa Kisuni Wanawaita Mashi’a Makafiri.

Kwa upande mwingine, matendo ya maulamaa mashabiki wa Sunni wanafaa kuangaliwa. Wafuasi wa Abu Hanifa, Maliki bin Anas, Muhammad bin Idris Shafi’i na Ahmad bin Hanbal, ambao wanazo tofauti za wazi kabisa, wanawaita wafuasi wa Ali bin Abi Talib na Imam Ja’far bin Muhammad makafiri na washirikina.

Wanachuoni wengi wakubwa na wacha Mungu wa Kishi’a waliuwawa mashahidi kwa fat’wa zilizotolewa na Maulamaa wa Kisuni.
Kinyume chake hakuna mfano wa ukatili kama huo kwa upande wa Ulamaa wa Kishi’a. Maulamaaa wenu mara kwa mara hutoa maneno ya kuwalaani Mashia, lakini hutaona popote laana juu ya Masunni katika vitabu vilivyoandikwa na Maulamaa wa Kishi’a.

Hafidh: Hutendi haki. Unachochea chuki bure. Toa mfano mmoja tu wa mwanachuo wa Kishi’a aliyeuwawa kwa hukumu ya maulamaa wetu! Nani katika Mualamaa wetu aliyetoa maneno ya laana juu ya Shi’a?

Muombezi: Kama ingekuwa nielezee kirefu matendo ya Maulamaa wenu au ya watu wenu wa kawaida, mkutano mmoja usingekuwa mrefu wa kutosha. Nitarejea tu kwenye mifano michache yenye kuhusiana na matendo yao ili ujue kwamba mimi sichochei chuki, bali naonyesha ukweli.

Kama utavichunguza vitabu vya Maulamaa wenu mashabiki, utaona sehemu ambazo wamelaani Mashi’a. Kwa mfano, angalia vitabu vya Tafsiri vya Imam Fakhrud-Din Razi.

Wakati anapopata wasaa tu, kwa mfano kuhusiana na Aya za Wilayat, huandika kwa kurudia rudia: “Laana iwe juu ya Marafidhi, laana iwe juu ya Marafidhi,” lakini maulamaa wetu hata mara moja hawajaandika mambo kama hayo juu ya ndugu zetu Masunni.

Mfano wa vitendo vya kikatili vya maulamaa wenu kuhusu maulamaa wa Kishi’a ni zile hukumu ya Makadhi wakubwa wawili wa Syria (Burhanud-Din Maliki na Ibad bin Jama’at Shafi’i) dhidi ya mmoja wa Mwanasheria (Faqih) mkubwa, Abu Abdullah Muhammad bin Jamalu’d-bin Makki Amili.

Mwanachuo yule mkubwa alikuwa akijulikana katika wakati wake kwa ucha Mungu wake na elimu ya Sheria.

Mfano wa uwanachuo wake ni kitabu chake, “Lum’a,” ambacho alikiandika kwa muda wa siku saba bila kuwa na kitabu chochote mkononi mwake juu ya Sheria (Fiqih) isipokuwa “Mukhtasar Nafi’.” Zaidi ya hayo, wanachuo wa madhehebu haya manne (Hanafi, Maliki, Shafi’i na Hanbal) walikuwa miongoni mwa wanafunzi wake.

Kwa sababu ya maonevu ya Massuni, mara kwa mara alifanya Taqiyya (kujigeuza na kuficha mwelekeo wakati wa hatari), na hakutangaza Ushi’a wake waziwazi. Kadhi Mkuu wa Syria, Ibad bin Jama’at, ambaye ameweka uhusuda dhidi yake, alimzungumza vibaya kwa mtawala wa Syria (Baidmar) na akamshutumu kuwa yeye ni Rafidhi na Shi’a.

Mwanachuo huyu maarufu akatiwa nguvuni.Baada ya kutaabikia ufungwa na mateso ya mwaka mmoja, kwa fat’wa ya Makadhi hawa wawili (Ibnu’l-Jama’at na Burhanud-Din) yeye akauawa na mwili wake ukatundikwa kwenye kiunzi. Kwa vile walitangaza kwamba kuna Rafidh ni Kafiri yuko juu ya miti ya kunyongea, watu wa kawaida waliupiga mawe mwili ule. Baadae, mwili ule ulichomwa na jivu lake likasambazwa.

Miongoni mwa maulamaa na wanasheria wa Kishi’a wa kujivunia wa Syria katika karne ya 10 Hijriya, alikuwa Sheikh Zainu’d-Din bin Nuru’d-bin Ali bin Ahmad Amili. Alikuwa akijulikana sana miongoni mwa marafiki na maadui kwa elimu yake na uadilifu. Akiwa mtunzi wa vitabu vingi, alijiweka mbali na ulimwengu na akaandika vitabu 200 juu ya masuala mbalimbali.

Ingawa aliishi maisha ya kujitenga, bado maulamaa wa Kisunni walijenga chuki juu yake, na wivu juu ya umaarufu wake miongoni mwa watu. Mkubwa katika wapinzani wake alikuwa Kadhi Sa’ida, ambaye aliandika kwa Mfalme Sultan Salim malalamiko yafuatayo: “Hakika kuna mtu anaishi katika jimbo la Syria ambaye ni mzushi, mtu ambaye hahusiki na mojawapo ya madhehebu manne.”

Sultani Salim aliamrisha kwamba mwanasharia huyo aletwe mbele ya mahakama huko Istanbul (Uturuki). Alitiwa nguvuni ndani ya Msikiti Mtukufu wa Makka na alifanywa mfungwa siku arubaini mjini Makka.

Katika safari ya baharini kuelekea Istanbul, alikatwa kichwa na mwili wake ukatupwa baharini. Ni kichwa chake tu ndicho kilichopelekwa kwa mfalme

Waheshimiwa Mabwana! Nakuulizeni kwa shauku moyoni, kwa jina la Allah mseme iwapo mlipata kusikia tabia ya namna hiyo kwa upande wa Maulmaa wa Kishi’a dhidi ya Sunni kwa sababu ya kutofauta madhehebu ya Shi’a.

Ni hoja gani mtakayoleta kuthibitisha kwamba iwapo mtu akiacha kufuata yoyote katika madhehebu manne, yeye anakuwa ni kafiri na kwamba kuuawa kwake yeye ni wajib? Je, ni mantiki kufuata madhehebu ambayo yamekuja kuweko karne kadhaa baada ya Mtume, ambapo wale wanaofuata kanuni iliyokuwepo tangu wakati wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wanaamriwa wauawe?

Mashia Na Madhehebu Manne Ya Sunni.

Tafadhali hebu semeni kwa jina la Allah, iwapo hawa Maimam wanne Abu Hanafi, Malik, Shafi’i na Hanbal, walikuwa hai wakati wa uhai wa Mtume. Je, waliipata misingi ya dini kutoka kwa Mtume moja kwa moja?

Hafidh: Hakuna hata mmoja aliyedai hayo kuwa hivyo.

Muombezi: Je, Amir’l-Mu’minin Ali hakuwa mwenzi wa wakati wote wa Mtume, na je, hakutangaza kuwa Yeye ni lango la Jiji la Elimu?

Hafidh: Yeye kwa hakika alikuwa mmoja kati ya masahaba maarufu sana wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), na katika hali zingine yeye alikuwa ni mbora kuliko wao wote.

Muombezi: Je, hivi hatuna haki, kwa hiyo, ya kushikilia kwamba kumfuata Ali ni wajibu? Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mwenyewe alisema kwamba kumtii Ali ni sawa na kumtii yeye na kwamba yeye Ali alikuwa ni Lango la Elimu? Vile vile Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema kwamba yoyote yule anayetaka kupata elimu yapasa aende kwenye mlango wa Ali.

Vilevile, kwa mujibu wa “Hadith ath-Thaqalain” na “Hadith as-Safina,” ambazo zinatambuliwa na wote Sunni na Shi’a kugeuka kutoka kwenye njia iliyoonyeshwa na Ahlul-Bait wa Mtume itatuongozea kwenye maangamizi. Utovu wa utii, au uadui dhidi ya Ahlul-Bait wa Mtume ni sawa sawa na utovu wa utii kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mwenyewe.

Licha ya yote haya, Maulamaa wa Kishi’a hawajaonyesha ukosa subira wa namna hiyo kwa angalau hata Sunni wa kawaida, achilia mbali kwa maulamaa wao. Tulikuwa siku zote tukiwasihi Mashi’a kwamba Masunni ni ndugu zetu katika Uislamu na yatupasa kubakia tumeungana (yaani kulinda umoja wetu).

Kwa upande mwingine mara kwa mara maulamaa wa Kisunni wamekuwa wakiwachochea watu wao, wakisema kwamba Mashi’a ni wazushi, Marafidhi,Ghullat, au Mayahudi. Wanasema kwamba, kwa kuwa hawa Shi’a hawafuati mmoja katika Maimam wanne wa Kisunni (Abu Hanifa, Malikki, Shafi’i na Hanbali), basi ni makafiri. Ukweli ni kwamba wale wanaowafuata Ahlul-Bait wa Mtume (s.a.w.w.) wameongozwa sawasawa.

Mauaji Ya Mashi’a Huko Irani Na Afghanistan.

Waturuki, Bani Khawarizim, Wa-Uzbeg na wa-Afghan waliwateka nyara na kuwauwa Mashi’a wasio na hatia. Muhammad Amin Khan Uzbeg, ajulikanaye kwa jina la Khan Khawa, na Abdullah Khan Uzbeg waliwaua kikatili na kuwapora Mashi’a na wakakiri kuwa wamelifanya hilo.

Maulamaa wa Kisunni walitangaza kwamba Mashi’a ni makafiri na kwamba wanaweza kuuawa kwa mjibu wa Sharia ya dini. Ma-Amiri (viongozi) wa Afghanistani waliwatendea Mashi’a kwa namna hiyo hiyo.

Katika mwaka wa 1267 Hijiriyya siku ya Ashura (Mwezi 10 Muharam), Masunni walishambulia ukumbi katika Qandahar, ambako Mashi’a walikuwa wanaomboleza mauaji ya mjukuu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Waliwaua Mashi’a wengi kwa ukatili mkubwa, wakiwemo watoto, na wakapora mali zao. Kwa miaka mingi Mashi’a waliishi maisha ya dhiki na walikatazwa kuendesha ibada zao za kidini.

Katika siku ya Ashura wachache wao walikwenda kwenye kumbi za siri na waliombeleza mauaji ya Imam Husein (A.S) kisirisiri kabisa, na wale wengine walikuwa wakichinjwa kwenye nyanda za Karbala. Ilikuwa ni Mfalme Amanullah Khan aliyeondoa kikwazo hicho juu ya Shi’a na akawatendea upole.

Kuuwawa Shahidi Kwa Shahid Thalis.

Katika makaburi ya Akbarabad (Agra) India, pale amelala Mwanachuo Mchamungu mno wa Kishi’a, Qadhi Seyyid Nurullah Shustari. Aliuawa kishenzi sana akiwa na umri wa miaka 70 katika mwaka wa 1019 Hijiriya na Mfalme Jahangir, kufuatia fat’wa kutoka kwa wanachuo wa Kisunni kwamba Yeye alikuwa Rafidh.

Hafidh: Unatushambulia (kwa maneno) bila sababu yoyote. Mimi mwenyewe nimeshtushwa mno kusikia vitendo vya kuchukiza mno vya watu wajinga, lakini matendo ya Mashi’a pia yalikuwa yanahusika na matukio haya.

Muombezi: Unaweza kunieleza ni matendo gani ya Mashi’a ambayo yalifanya kuwa halali kwao kuuwawa?

Hafidh: Kila siku maelfu ya watu wanasimama mbele za makaburi ya waliokufa na kuwaomba msaada. Je, kitendo hiki sio mfano wa kuabudu wafu? Kwa nini Maulamaa wasikataze wakati mamilioni ya watu hao wakiweka mapaji yao ya nyuso zao kwenye ardhi wakisujudu katika kuwaabudu wafu? Nashangaa ni kwa vipi bado unayaita mambo haya kuwa sio shirki.

Wakati majadiliano na Mawalana Hafidh yakiendelea, faqihi wa Kihanafi, Agha Sheikh Abdus-Salam alikuwa anakichunguza Hidayatuz-Za’irin. Akasema kwa msisitizo mzito, “Tazama hapa! (akikionyesha kile kitabu).

Ulamaa wako anasema kwamba wakati mahujaji wanapomaliza Ziarat katika Makuba ya Maimam, wanapaswa kuswali rakaa mbili za Sala ya Ziarat.

Huenda hawaikusudii Sala hii kwa jina la Allah; vinginevyo, nini maana ya Sala ya Ziarat? Huu sio ushirikina kufanya ibada ya Sala kwa ajili ya Imam? Mahujaji wanaosimama na kuelekeza nyuso zao kwenye makaburi na kusali ni ushahidi mzuri wa ushirikina. Hiki ni kitabu chenu Sahihi. Unaweza ukatetea hali yenu hii?”

Muombezi: Mbona unajiingiza katika mazungumzo ya kitoto! Hivi umewahi kuwako kwenye Ziarat hizo na kuwaona Mahujaji hao ana kwa ana?

Sheikh: Hapana.

Muombezi: Sasa ni vipi ukaweza kusema kwamba mahujaji hao wanaswali wakiwa wameelekeza nyuso zao kwenye kaburi, na kusema kwamba swala hii ya Ziarat ni dalili ya ushirikina?

Sheikh: Kitabu hiki kinasema kwamba waswali Swala ya Ziarat kwa ajili ya Imam.

Muombezi: Hebu lete hicho kitabu nikiangalie. Ngoja nisome maelekezo kuhusu Ziarat, mpaka tufikie kipengele cha Sala ambacho ndio hoja ya kukataa kwako. Wakati wowote ukiona dalili ya ushirikina, tafadhali ionyeshe. Na iwapo utaona alama za kuamini na kuabudu Mungu Mmoja kuanzia juu mpaka chini usije ukajisikia vibaya kwa hilo, bali sema kwamba ulikuwa umeelewa vibaya. Kitabu kiko hapa mbele yenu.

Maelekezo Kuhusu Ziarat:

Maekelezo ni kama yafutayo: “Wakati mwenye kufanya Ziarat afikapo handaki la Kufa, anasimama pale na kusoma kisomo kifuatacho” Allah ni Mkubwa mno, Allah ni mkubwa mno Mwenye ukubwa, Utukufu, Sifa njema, na rehema. Allah ni Mkubwa Mno juu zaidi ya kile ambacho nakiogopa. Allah ni Mkubwa mno. Yeye ni msaada wangu; Kwake Yeye nategemea na Kwake Yeye yako matumaini yangu na Kwake Yeye naelekea.’

Wakati mwenye kufanya Ziarat akifika lango la Najaf, yampasa kusoma: ‘Sifa zote njema ni za Allah, ambaye ametuongoza katika hili, tusingekuwa ni wenye kuongoka kama Allah asingetuongoza.’
Wakati akifika lango la Uwanja wa Mtukufu yampasa asome, baada ya kumtukuza Allah:

‘Nashuhudia kwamba hakuna Mungu isipokuwa Allah, aliye Mmoja. Yeye hana mshirika. Na pia ninashuhudia kwamba, Muhammad ni mja na Mtume Wake.

Ametuletea kweli kutoka kwa Allah. Na pia nashuhudia kwamba Ali ni mja wa Allah na ndugu yake Mtume wa Allah. Allah ni mkubwa mno, Allah ni mkubwa mno, Allah ni Mkubwa mno. Hakuna Mungu isipokuwa Allah, na Allah ni Mkubwa mno. Shukrani zote ni Zake kwa mwongozo na msaada Wake kuitikia kile alichofunua juu ya njia kuelekea Kwake.’

Wakati Mwenye kufanya Ziarat akifika kwenye lango la Quba, yampasa asome: ‘Ninashuhudia kwamba hakuna Mungu isipokuwa Allah, aliye Mmoja. Yeye hana Mshirika pamoja Naye…’ mpaka mwisho.

Wakati, baada ya kwisha kuomba ruhusa ya Allah, ya Mtume, na ya Maimam, mwenye kufanya Ziarat hufika ndani ya Quba, husoma Ziarat mbalimbali ambazo zina maamkuzi kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na kwa Amir’l-Mu’minin. Baada ya Ziarat, husali rakaa sita (za Sunna), rakaa mbili kwa ajili ya Amir’l-Mu’minin na rakaa mbili kwa ajili ya Nabii Adam na mbili kwa ajili ya Nabii Nuh ambao wamezikwa katika eneo hilo hilo.”

Salat-Ziarat Na Dua Baada Ya Sala.

Je, utekelezaji wa ibada ya Sala kama sadaka kwa ajili ya roho za wazazi na waumini wengine, haikuamrishwa juu yetu? Je, maamrisho haya ni ushirikina? Vilevile ni kwa ajili ya ubinaadamu kwamba wakati mtu anapokwenda kumuona rafiki humpatia zawadi fulani. Kuna Sura katika vitabu vya Madhehebu zote ambamo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anatuamrisha kutoa zawadi kuwapa waumini.

Hivyo mwenye kufanya Ziara anapofika kwenye kaburi la mpendwa bwana wake na anajua kwamba kitu alichokuwa amekipenda zaidi ilikuwa ni Sala, anasali rakaa mbili katika njia yake ya kufikia kwa Allah na anaitoa Sala ile kama zawadi kwa ajili ya roho ya bwana wake huyo. Je, huo ni ushirikina? Baada ya kusoma kanuni za msingi wa Sala hii, pia soma du’a iliyoko baada ya Sala, ili kwamba mashaka yako yote yaondoke.

Du’a Baada Ya Sala:

Ibada ya Dua ni kwamba baada ya kumaliza Sala katika kichwa cha kaburi la Imam aliyezikwa pale, na nyuso zetu kuelekea Kibla (sio kuelekea kwenye kaburi), tunasoma du’a ifuatayo, “Ewe Allah! Sala hii nimeifanya zawadi kwa bwana na kiongozi wangu, Mtume Wako na ndugu yake Mtume Wako, Amir’l-Mu’minin Ali bin Abu Talib.

Ewe Allah, teremsha rehema na amani Yako juu ya Muhammad na kizazi chake. Zikubali rakaa mbili hizi za Sala kutoka kwangu na unijazi, kama ambavyo ungewajazi watendaji wa matendo mema.

Ewe Allah! Nimeitoa Sala hii (kama Sadaka) kwa ajili Yako, na nimerukuu na kusujudu mbele yako Wewe kwa kunyenyekea Kwako. Wewe ni Mmoja ambaye huna mshirika. Hairuhusiwi kusali, kurukuu au kusujudia chochote isipokuwa Wewe. Wewe ni Allah, uliye Mkuu na hakuna mungu isipokuwa Wewe.”

Mabwana waheshimiwa! Kwa jina la Allah, kuweni waadilifu. Kuanzia muda ule mwenye kuzuru anapoweka mguu wake juu ardhi ya Najaf, mpaka baada ya kusali sala yake ya Ziarat, yeye anajishugulisha katika kumkumbuka Allah swt.

Sheikh: Inashangaza kwamba huoni yalioandikwa hapa: “Busu kizingiti cha mlango na kisha ingia ndani ya haram ya Kuba.” Tumesikia kwamba wakati wenye kufanya Ziarat wakifika kwenye mlango wa kuba la Maimam wao, wanakwenda Sijida kwa heshima. Je kusujudu huku sio kwa ajili ya Ali? Je, sio ushirikina wakati tunasujudia mwingine asiyekuwa Allah?

Muombezi: Kama mimi ndio ningekuwa ni wewe, nisingelisema neno. Ningenyamaza kimya mpaka mkutano wa mwisho wa mjadala huu na kusikiliza mantiki ya majibu yangu. Lakini nitakuambia kwa ufupi mara nyingine tena kwamba, kubusu kizingiti au sakafu ya makuba ya Maimam sio ushirikina.
Umelitafsiri vibaya neno “kubusu” na kuliona kuwa ni sawa na kusujudu. Wakati unasoma kitabu hicho mbele yetu unadiriki kufanya mabadiliko ya ugeuzaji maana ya maneno kama huu, sijui ni jinsi gani utatusingizia wakati utakapokuwa peke yako ukiwahutubia watu wasio na elimu.

Maelekezo yaliyomo katika kitabu hiki na vitabu vinavyohusu Du’a na sehemu za Ziarat ni kwamba mwenye kufanya Ziarat, kama namna ya kuonyesha heshima, inampasa kubusu kizingiti sio kusujudu. Vipi unafikiria kubusu na kusujudu kuwa ni kitu kimoja?

a, ni wapi umeona ima katika Qur’ani tukufu au katika hadith yoyote kwamba kubusu kizingiti cha Kuba la Mtume au Imam kumekatazwa? Hivyo kama huna jibu la maana kwa swali hili, usipoteze wakati wetu.

Na, kama unavyosema “umesikia” kwamba wafanyao Ziarat husujudu kwa heshima. Kwa uhakika hukuwaona kwa macho yako wakifanya hivi. Qur’ani tukufu inasema, “Enyi ambao kwamba mmeamini! Akikujieni fasiki na habari, ichunguzeni, msije mkadhuru watu kwa ujinga, kisha mkawa ni wenye kusikitika kwa yale muliyoyafanya.” (49:6).

Kwa mujibu wa amri hii ya Qur’ani Tukufu, hatupasi kutegemea maelezo ya watu waovu. Yatupasa kufanya juhudi kubwa kujua ukweli, hata ikiwezekana kufanya safari ili kupata habari ya kweli moja kwa moja.

Wakati nilipokuwa Baghdadi, nilikwenda kwenye makaburi ya Abu Hanifa na Sheikh Abdul’Kadir Jilani na nikaona watu walivyofanya. Ilikuwa vibaya zaidi kuliko ulivyoelezea kuhusu Mashi’a wanavyofanya, lakini kamwe sijal- izungumza hili.

Nilipofika kwenye kaburi la Abu Hanifa hapo Mu’azza’m, niliona kundi la Masunni wakirudia rudia kubusu Sakafu, badala ya kizingiti, na kujigaragaza kwenye sakafu. Lakini kwa kuwa hawakuonekana kwa mahabithi, na kwa sababu sikuwa na sababu za kuwalaumu, kwamwe sikuitaja habari hii kwa mtu yoyote. Nilielewa kwamba walikuwa wakifanya hivyo kwa ajili ya mahaba sio kama ibada.

Ewe bwana mheshimiwa! Hakika hakuna Shi’a mcha-Mungu ambaye amediriki kusujudu kwa yeyote isipokuwa Allah. Kama, kwa vyovyote vile iwavyo, kama tunaanguka chini ya ardhi katika hali kama ya kusujudu na kusugua mabapa ya nyuso zetu juu yake (bila kuwa na nia ya kuabudu), hiki ni kitu kidogo sana. Kuinama mbele ya mtu mtukufu bila kumfikiria kuwa yeye ni Allah, au kuanguka chini juu ya ardhi na mtu kusugua uso wake juu yake, sio ushirikina. Ni matokeo ya mahaba makubwa.

Sheikh: Inakuwaje kwamba tunaposhuka chini juu ya ardhi na kuweka paji letu la uso juu yake, kwamba kitendo hiki kisiweze kuwa sawa na kusujudu?

Muombezi: Kusujudu kunategemea juu ya nia, na nia ni jambo la moyo. Ni Allah peke yake ndiye anayejua nia zetu za moyoni. Kwa mfano tunaweza kuona watu wamelala chini juu ya ardhi kwa hali kama ya kusujudu.

Ni kweli kwamba kusujudia yeyote asiyekuwa Allah sio sawasawa, hata ikiwa bila nia yoyote. Walakini, kwa kuwa hatujui nia za mioyo yao, hatuwezi kuiita hiyo kuwa ni Sijida ya Ibada.

Kusujudu Kwa Ndugu Zake Yusufu Mbele Yake.

Kwa hiyo, kusujudu katika hali iliyo sawa na Sijida ya ibada (lakini bila nia yake), kuonyesha heshima kwa mtu sio ushirikina. Kwa mfano nduguze Nabii Yusufu walisujudu mbele yake. Wakati huo Mitume wawili walikuwepo, Ya’qub na Yusufu, lakini hawakuwakataza kufanya hivyo. Allah (s.w.t.) Anasema katika Suratul-Yusufu ya Qur’ani Tukufu.

وَرَفَعَ أَبَوَيْهِ عَلَى الْعَرْشِ وَخَرُّوا لَهُ سُجَّدًا ۖ وَقَالَ يَا أَبَتِ هَٰذَا تَأْوِيلُ رُؤْيَايَ مِنْ قَبْلُ قَدْ جَعَلَهَا رَبِّي حَقًّا ۖ{100}

“Na aliwainua wazazi wake na kuwaweka katika kiti cha Ufalme, na wote wakaporomoka kumsujudia, na akasema; “Ewe Baba yangu, hii ndiyo hakika ya ndoto yangu ya zamani; bila shaka Mola wangu ameithibitisha …..” (12:100).

Aidha, Qur’ani Tukufu inasema katika sehemu nyingi kwamba Malaika walifanya Sajida mbele ya Mtume Adam. Hivyo kama kusujudu namna hiyo ni ushirikina, basi nduguze Mtume Yusufu na Malaika wa Allah walikuwa washirikina. Ni Iblis aliyelaaniwa peke yake ndiye ambaye hakuwa mshirikina!

Kuwaomba Maimamu Sio Kuwaabudu Wafu.

Sasa napenda kumjibu Mheshimiwa Hafidh, ambaye amesema kwamba maombi mbele ya makaburi ya Maimam ni sawa sawa na kuwaabudu wafu. Unauliza kwa nini Mashi’a wanaomba msaada kwenye makaburi ya Maimam. Pengine unaamini kwamba hakuna maisha baada ya kifo na unasema: “Kilicho kufa kimeangamia moja kwa moja.” Allah (s.w.t.) anaelezea katika Qur’ani Tukufu mawazo potovu haya,

Anasema:

إِنْ هِيَ إِلَّا حَيَاتُنَا الدُّنْيَا نَمُوتُ وَنَحْيَا وَمَا نَحْنُ بِمَبْعُوثِينَ {37}

“Hakuna ila maisha yetu haya ya dunia, tunakufa na kuishi, basi, wala sisi si wenye kufufuliwa.” (23:37).

Kama mjuavyo nyote, wale wanaoamini katika Allah wanajua kwamba kuna maisha baada ya kifo. Wakati mwanadamu akifa, mwili wake unakuwa hauna uhai, lakini, tofauti na wanyama, roho na hisia ya kusema hubakia katika viwiliwili vilivyo sawa na hivi, lakini halisi zaidi na watarehemiwa au kuadhibiwa katika hali ya mpito (barzakh) au mahali pa mateso.

Mashahidi na wale waliouawa katika njia ya Allah watafurahia neema maalum. Hii imesimuliwa katika Qur’ani Tukufu:

“Na usiwadhanie wale waliouawa katika njia ya Allah kuwa ni wafu; bali wahai na wanaruzukiwa kwa Mola wao, wanafurahia aliyowapa Allah kwa fadhila zake, na wanafurahia kwa hilo hilo wale ambao wameachwa nyuma yao, bado hajajiunga nao; ya kwamba haitakuwa hofu juu yao wala hawatahuzunika.” (3: 169-170).

Ninatafakari juu ya maneno haya: “Wahai (na) wanaruzukiwa kwa Mola wao……” (3: 169) Wao wanatujibu, lakini kwa vile kusikia kwetu kumefunga kwa mapazia ya ulimwengu wa kimaada hatusikii sauti zao. Kwa ajili hiyo katika salaam (ziarat) kwa Imam Husein, tunasema; “Ninashuhudia kwamba unasikia ninayosema na kwamba unajibu.” Je, umesoma Khutuba na 85 katika Nahju’l-Balagha? Kizazi cha Mtume wametambulishwa kama ifuatavyo: “Enyi watu huu ni usemi wa Mtume:

Yeyote anayekufa miongoni mwetu sio mfu, na yeyote ambaye anaoza (baada ya kufa) kutoka miongoni mwetu kwa hakika haozi.’” (Nahjul-Balaghah Tarjuma ya Kiingereza, Juz. 1, uk. 130 iliyochapishwa na Peer Muhammad Ebrahim Trust, Karachi.) Hivyo ni kwamba, katika uwanja wa mwanga na mambo ya Kiroho, Ahlul-Bait wanaishi na wanabakia wenye kudumu milele.

Kwa ajili hiyo, Ibn Abi’l-Hadid Mutazali na Sheikh Muhammad Abdul, Mufti mashuhuri wa Misri, wakisherehesha hadith hiyo hapo juu, wanasema kwamba, dhuria wa Mtume (s.a.w.w.) hawakufa kwa namna walivyokufa wengine. Hivyo tunaposimama mbele ya makaburi ya Maimam, hatusimami mbele za wafu, na hatuzugumzi wafu. Tunasimama mbele za walio hai na kuzungumza na wanaoishi. Kwa ajili hiyo sisi sio waabuduo wafu.

Tunamuabudu Allah. Je huamini kwamba Imam Ali, Imam Husain, na mashahidi wa Badr, Hunain, Uhud na Karbala walitoa muhanga maisha yao katika njia ya Allah kwa ajili ya haki? Je, hawakuwakabili madhalimu wa Kiquraishi, Bani Umayya, Yazid na wafuasi wake, ambao lengo lao lilikuwa ni kuifulitia mbali Dini.

Kama vile ule uimara wa masahaba wa Mtume na mihanga ya mashahidi wa Badri, Hunain, na Uhud ulivyopelekea kushindwa kwa ukafiri, kwa njia hiyo hiyo uamuzi imara wa Imam Husain kutoa mhanga maisha yake, uliimarisha Uislamu. Kama Imam asingesimama imara dhidi ya nguvu za uovu, mwana kulaaniwa Yazid angeuharibu Uislamu na angeweza kupenyeza ukafiri wake katika Umma wa Kiislamu.

Sheikh: Inashangaza kwamba, unamwita Khalifa wa Waislamu Yazid bin Mu’awiya kuwa ni kafir. Yakupasa uelewe kwamba Mu’awiya bin Abu Sufyan alimchagua yeye kuwa Khalifa. Khalifa wa Pili Umar bin Khattab na Khalifa wa tatu Uthman aliyedhulimiwa, walimchagua Mu’awiya kuwa Amir (Gavana) wa Syria. Kwa sababu ya uwezo na vipaji vyao, watu waliwakubali kuwa Makhalifa kwa uaminifu kabisa.

Hivyo uhusishaji wako wa makhalifa wa Uislamu kuwa ni makafiri una maana kwamba hukuwatukana tu Waislamu wote ambao wamewakubali kama makhalifa, bali vile vile umewatukana Makhalifa waliopita ambao wamewaidhinisha wao kuwa makhalifa au magavana. Kwa kweli walifanya makosa, ambayo yalitokea wakati wa ukhalifa wao.

Mjukuu wa Mtume, Imam Husain, aliuwawa, lakini hili lilisamehewa. Kwa vile walitubia, Allah Mwingi wa rehema, aliwasamehe. Imam Ghazali na Damiri wameshughulika na nukta hii kwa uan- galifu kabisa katika vitabu vyao na wamethibitisha usafi wa khalifa Yazid.

Muombezi: Kamwe sikutaraji kwamba ushabiki wako utakwenda mbali kiasi hicho mpaka kutetea kusudi la mlaaniwa Yazid. Unasema kwamba kwa vile wakubwa wao waliowatangulia waliona inafaa kuwafanya ma-Amir au watawala, basi Waislam wote ili- wapasa wawakubali.

Kauli hii haileti maana yoyote. Tunasema kwamba Khalifa yapasa awe safi (aliyeepukana kabisa na madhambi yote) na kuteuliwa ki-Ungu ili kwamba tusije tukadumu katika ukandamizwaji. Unasema kwamba Ghazali na Damiri wametetea nafasi ya Yazid. Lakini walikuwa mashabiki kama ulivyo wewe.

Hakuna mtu mwenye akili timamu ambaye atathubutu kamwe kujaribu kutetea matendo ya mlaaniwa Yazid. Unasema kwamba Yazid alifanya “kosa” katika kumuua Imam Husain.

Lakini kumuuwa mtoto kipenzi mno wa Mtume, kuchanganya pamoja na watu 72, wakiwemo watoto wadogo na wazee, na kuwachukua mateka mabinti wacha-Mungu wa Mtume vichwa wazi na nyuso wazi, haikuwa “kosa” la hivi hivi tu. Ulikuwa ni ukatili usiosemeka. Aidha, jinai zake hazikuishia kwenye chinja chinja hii ya kutisha peke yake. Kuna mifano mingi mingine ya ukafiri wake.

Ukafiri Wa Yazid.

Miongoni mwa mambo yanayothibitisha ukafir wa Yazid ni beti zake mwenyewe za kishairi. Kwa mfano anaandika hivi:

“Kama kunywa (pombe) kunakatazwa katika dini ya Muhammad, basi na iwe hivyo; mimi nitaukubali Ukristo.”

“Ni ulimwengu huu tu, kwa ajili yetu. Hakuna ulimwengu mwingine. Haipasi sisi kuzuiliwa starehe za ulimwengu huu.”

Beti hizi zinajitokeza katika mkusanyiko wa kazi zake za kishairi, na Abu’l-Faraj bin Jauzi ameyaandika katika kitabu chake “Radd Ala’l-Muta’asibu’l-Anid.” Anasema tena:

“Mwenye kututishia na hekaya za siku ya mwisho, muache afanye hivyo.
Haya ni mambo ya uongo, yanayotunyima sisi starehe zote za sauti na muziki.”

Sibt Ibn Jauzi anaandika katika kitabu chake “Tadhkira,” uk. 748 kwamba, wakati dhuria wa Mtume walipoletwa Syria kama mateka, Yazidi alikuwa amekaa katika ghorofa ya pili ya kasri yake. Yeye alisoma beti mbili zifuatazo:

Wakati machela za ngamia zilizobeba wafungwa zilipotokea, kunguru alilia (ndege mbaya katika Uarabu). Nilisema: “Ewe Kunguru, kama ulie au usilie, nimelipa kisasi juu ya Mtume.”

“Kisasi” huelekeza kwenye ukweli kwamba, wazee wake na jamaa zake wa karibu wali- uawa katika vita vya Badr, Uhud, na Hunain. Aliwachukulia kisasi cha vifo vyao kwa kuwaua watoto wa Mtume.

Ushahidi mwingine wa Ukafir wake ni kwamba alipofanya hafla ya kusherehekea Shahada ya Husain, alisoma beti za Kikafir za Abdullah bin Uzza Ba’ri. Sibt Ibn Jauzi, Abu Raihan, na wengine wameandika kwamba Yazid alitamani wazee wake wangekuwepo, ambao wote walikuwa makafir, na waliuawa katika vita vya Badr kwa amri ya Mtume.

Yazid alisema: “Natamani watu wa ukoo wangu ambao waliuawa huko Badr, na wale ambao wame- waona watu wa ukoo wa Khazraj wakilia

(katika vita ya Uhud) kwa ajili ya majeraha ya michomo mikali (ya panga, mikuki na mishale), wangekuwa hapa. Wangelinishangilia kwa sauti na kusema: ‘Ewe Yazid mikono yako kamwe isipooze,’ kwa sababu nimewauwa wakuu wa ukoo wake( yaani ukoo wa Mtume). Nimefanya hivyo kama kisasi cha Badr, ambacho sasa kimekamilika.

Bani Hashim walicheza mchezo tu na serikali. Hakukuja ujumbe kutoka kwa Allah, wala ufunuo wowote. Nisingekuwa wa familia ya Khandaq kama nisingechukua kisasi juu ya dhuria wa Mtume. Tumeyalipa kisasi mauaji yaliyofanywa na Ali kwa kumuuwa mtoto wake, mpanda farasi na simba mwerevu.

Ruhusa Ya Kumlaani Yazid Iliyotolewa Na Maulamaa Wa Kisunni.

Wengi wa Maulamaa wenu wanamuona Yazid kama kafiri. Hata Imam Ahmad bin Hanbal na Maulamaa wengine wengi wakubwa wa madhehebu yenu wameshauri kwamba laana juu yake zinapaswa kuelezwa. Abdur-Rahman Abul-Faraj bin Jauzi ameandika kitabu juu ya somo hili, Kitabul-Radd Ala’l-Muta’asibu’l-Anidul-Mani’an La’n-e-Yazid La’natullah. Ni Maulamaa mashabiki wachache tu wa madhehebu yenu, kama Ghazali, wameonyesha upendeleo kwa Yazid, na wamebuni makinzano yasiyo na maana kwa ajili ya kumtetea.

Hata hivyo, wengi wa Maulmaa wenu, wameiona tabia yake isiyo ya kidini na ya kidhal- imu. Muslim anasema kwamba, kama Khalifa; Yazid alidiriki kuiangamiza dini, Mas’udi katika kitabu chake “Muruju’z-Dhahab, “Juz. 2, anasema kwamba tabia ya Yazid ilikuwa sawa na ile ya Firauni, lakini ni kwamba Firauni alikuwa muadilifu zaidi kwa watu wake kuliko alivyokuwa Yazid.

Utawala wa Yazid ulileta fedheha juu ya jina zuri la Uislam. Uovu wake ulikuwa ni pamoja na kunywa pombe, kumuua mtoto wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), kumlaani mshika Makamu wa Mtume Ali, kubomoa nyumba ya Allah (Masjidu’l-Haram) na mauaji ya halaiki. Amefanya uhalifu usiohisabu dhidi ya Sheri ‘ah ya dini, na dhambi ambazo hazisameheki.

Nawab: Yazid alihusika vipi na mauwaji ya halaiki?

Muombezi: Wanahistoria wengi wamelisimulia jambo hili. Sibt Ibn Jauzi katika kitabu chake “Tadhkira” uk. 63, anasema kwamba baadhi ya watu wa Madina walikwenda Syria katika Mwaka wa 62 A.H. Walipoyagundua matendo maouvu ya Yazid walirudi Madina na kuvunja kiapo cha utiifu kwake, wakamlaani, wakamfukuza, gavana wake, Uthman bin Abi Sufyani. Abdullah bin Hanzala ( Ghusilu’l-Mala’ikat) alisema:

“Enyi watu, hatukuasi dhidi ya Yazidi mpaka tulipothibitisha kwamba si mtu mwenye kufuata dini. Aliua watoto wa Mtume, alnajihusisha kinyume na sheria na mama zake, binti zake, na dada zake, anakunywa pombe, na hajishughulishi na ibada ya Sala.”

Habari hizi zilipomfikia Yazid, alituma jeshi kubwa la watu wa Syria chini ya Mulsim bin Uqba dhidi ya watu wa Madina. Mauaji ya Waislamu yaliendelea kwa muda wa siku tatu. Jeshi la Yazidi liliua watu 700 waungwana wa Kikuraish, Muhajirina, na Ansar, na watu 10,000 wa kawaida.

Naona aibu kusema jinsi Waislamu walivyonyanyaswa. Nitanukuu kifungu kimoja tu katika ‘Tadhkira,’ ya Sibti Ibn Jauzi uk. 163, kilichosimuliwa na Abu’l- Hasan Mada’an:“Baada ya mauwaji ya halaiki ya watu wa Madina, wanawake 1000 wasiolewa walizaa watoto.”

Je, Yazid Anapaswa Kulaaniwa?

Sheikh: Madai haya yanaonyesha madhambi yake. Madhambi yanasameheka na yanaweza kufidiwa, na Yazid alionyesha hali ya kutubia. Allah ambaye ndiye Mwenye kusamehe madhambi amemsamehe. Basi kwa nini wakati wote unamlaani na kumuita muovu?

Muombezi: Baadhi ya mawakili hubishana juu ya kesi ya wateja wao mpaka dakika ya mwisho kwa sababu wamepokea malipo kutoka kwao, ingawaje wanaelewa vizuri ustahili wa kesi yenyewe. Lakini nashindwa kuelewa kwa nini unapendelea mno kumtetea Yazid, mbele ya mauaji yake ya watoto wa Mtume wa Allah na kuwaua kwake watu wa Madina. Aidha, maelezo yako kwamba alionyesha kutubia hayathibitiki.

Je kukataa kwake misingi muhimu ya Uislamu siku ya ufufuo, Wahyi na Utume hakustahili laana yetu kwake? Je, Allah hakuwalaani madhalimu? Kama hoja hizi hazitoshi kwa mawakili wa Yazid bin Mu’awiya, kwa ruhusa yako nitanukuu hadith kutoka kwa Maulamaa wenu maarufu.

Bukhari na Muslim katika “Sahih” zao, Allama Samhudi katika “Ta’rikhu’l-Madina,” Abu’l-Faraj bin Jauzi katika Kitabu‘r-Radd Ala’l-Muta’asibul-Anid,” Sibt Ibn Jauzi katika Tadhkira-e-Khawasul-Umma, Imam Ahmad bin Hanbali katika “Musnad” na wengine wanamnukuu Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akisema: “Kama mtu yeyote atawatishia na kuwaonea watu wa Madina, Allah atamtishia (yaani Siku ya Malipo). Atalaaniwa na Allah, Malaika, na wanadamu wote. Na katika Siku ya Malipo, Allah hatayakubali matedno yake yoyote.

Vilevile Mtume amesema: “Laana iwe juu ya yule mwenye kuutishia mji wangu (watu wa Madina).” Je, mauaji haya ya halaiki hayakuwatishia wale watu wa Madina? Kama yalifanya basi kubali pamoja na Mtume, Malaika na watu wote kwamba yule mfanya mauovu mbaya alilaaniwa na atakuwa akiendelea kulaaniwa mpaka Siku ya Kiyama.

Wengi wa ulamaa wenu wamemlaani Yazid. Abdullah bin Muhammad bin Amir Shabrawi Shafi’i katika “Kitabu’l-Ittihaf bi Hubbi’l Ashraf Raji’ba La’n-e-Yazid” uk. 20, anaandika kwamba wakati jina la Yazid lilipotajwa mbele ya Mulla Sa’d Taftazan, yeye alisema: “Laana iwe juu yake na wafuasi na wasaidizi wake.”

Allama Samhudi katika kitabu chake “Jawahirul-Iqdain” ananukuliwa akisema; “maulamaa kwa ujumla wamekubaliana kwamba, inaruhusiwa kumlaani aliyemuua Imam Husein, au aliyetoa amri ya yeye kuuliwa, au yule aliyeridhia mauaji yake, au yule aliyekubali kuuliwa kwake.”

Ibn Jauzi, Abu Ya’la na Salih bin Ahmad, wakihoji kutoka kwenye Aya za Qur’ani wanaandika kwamba: “Imethibitika kwamba imeruhusiwa kumlaani Yazid. Ni wajibu wa Waislamu wote kwamba yawapasa kujua haki alizonazo Imam Husein juu yao.

Na ni vipi, kwa nguvu ya kupatwa kwake na mateso ya udhalimu na uonevu, yeye alivyounyweshea mti wa Uislamu kwa damu yake mwenyewe na damu ya familia yake. Vinginevyo, mti ule uliobarikiwa ungekufa kwa sababu ya udhalimu wa Bani Umayyah. Alikuwa ni Husain ambaye aliupatia Uislamu uhai mpya.

Nasikitika kwamba badala ya kuitambua huduma hii ambayo watu hawa watukufu wameitoa kwa Uislamu, mnazua makinzano kuhusu wafanya ziara ambao wanazuru makaburi yao na kuwaita wenye kuabudu wafu. Mara nyingi tunasoma kwamba katika sehemu muhimu za nchi, kama Paris, London, Berlin, na Washington kuna makaburi ya kumheshimu “Askari asiyejulikana.”Inasemekana kwamba, kuteseka kwa uonevu wa adui na kwa kuihami nchi yake, alijitoa muhanga maisha yake.

Lakini hakukuwa na alama juu ya mwili wake au nguo kuonyesha utambulisho wa familia yake au mji anakotoka. Kwa sababu alitoa maisha yake kwa ajili ya kuitetea nchi yake, ingawaje alikuwa hajulikani, alistahiki heshima. Wakati mfalme au mtu yeyote mashuhuri anapotembelea miji hii, huzuru hilo kaburi la “Askari asiyejulikana” na kuweka mashada ya maua juu yake.

“Askari asiyejulikana” anapata heshima zaidi, lakini nasikitika kwamba, badala ya kuwa- heshimu wafanya Ziara wanaozuru makaburi ya wanachuoni Waislamu wacha-Mungu sisi tunawashutumu. Baadhi yao waliijua Qur’ani yote kwa moyo.

Walitoa mhanga maisha yao kuutetea Uislamu. Watu hawa ni pamoja na mawakala (wadhamini) wa Allah, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na dhuria wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) .

Kuvunjwa Heshima Ya Makaburi:

Baadhi ya Waislamu wameyabomoa kabisa makaburi kama hayo na wakapika chai juu ya masanduku yaliyopangwa juu ya makaburi hayo. Tukio kama hilo lilitokea mwaka wa 1216 A.H. katika Siku ya Iddi’l-Ghadir, wakati wengi wa wakazi wa Karbala huenda Najaf kwa ajili ya ziara.

Ma-Wahhabi wa Najaf waliishambulia Karbala na wakawauwa Mashi’a. Wakayabomoa makaburi ya wale waliotoa mhanga maisha yao kwa ajili ya Uislamu. Karibu wakazi 5,000 wa Karbala, ikiwa ni pamoja na Maulamaa, wazee, wanawake, watoto, waliuawa.

Hazina ya Imam Husain iliporwa na vito vya thamani, taa za dhahabu, na mazulia ya thamani yalichukuliwa. Sanduku la thamani lililokuwa juu ya kaburi hilo lilichomwa moto na chai ikapikwa juu yake. Watu wengi walichukuliwa kama wafungwa. Ole kwa Waislamu kama hao!

Masikitiko yalioje kwamba katika nchi zote zilizostarabika, makaburi ya wafalme, wanachuo, na hata askari wasiojulikana yanaheshimiwa, lakini Waislamu ambao wanategemewa kuonyesha hisia nzuri za umuhimu wa kuhifadhi makaburi, ya wale ambao ni fahari yao, huyapora na kuyabomoa kama washenzi.

Katika mji wa Makka na Madina, Wahhabi walibomoa makaburi ya mashahidi wa Uhud, pamoja na la Hamza, na jadi zake Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), kama Abdu’l-Muttalib, Abdullah, na wengineo.

Vile vile walibomoa makaburi ya familia ya Mtume, watoto wake, kama Imam Hasani, Imam Zainu’l- Abidin, Imam Muhammad Baqir, Imam Ja’far Sadiq, Bibi Fatima binti ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), na wengi wengine wa ukoo wa Bani Hashim na Maulamaa watukufu. Bado wanajiita wao ni waislamu.

Hakika wao wanajenga ma-Quba makubwa kwa ajili ya watu wao mashuhuri na wafalme. Ukweli ni kwamba, Maulmaa wa madhehebu zote wamenukuu hadithi nyingi zikitutaka tuzuru makaburi ya waumini ili kwamba yasalimike kutokana na kuharibika.

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mwenyewe alizuru makaburi ya waumini na akamuomba Allah kwa ajili ya wokovu wao.

Dhuria Wa Mtukufu Mtume (S.A.W.W.) Ni Mashahidi Katika Njia Ya

Allah Na Wako Hai

Je, Unafikiri familia ya Mtume iliyotukuka ambao walitoa maisha yao katika njia ya dini ni mashahidi? Kama utasema sio mashahidi, ni nini hoja yako? Kama ni mashahidi, vipi utawaita kuwa wao, ni “Wafu?” Qur’ani Tukufu inaeleza kwamba:

بَلْ أَحْيَاءٌ عِنْدَ رَبِّهِمْ يُرْزَقُونَ {169}

Wako hai ( na) wanaruzukiwa na Mola wao.” (3:169).

Hivyo kwa mujibu wa Qur’ani na hadith, watu wale watukufu wako hai, Hivyo, sisi sio waabudu wafu. Hatuwasalimii wafu, tunawatukuza walio hai.

Na hakuna Shia yoyote, msomi au asiye msomi, ambaye anawafanya wao kama waondoaji wa matatizo moja kwa moja. Huwachukulia kama waja wacha Mungu na njia ya kufikisha kwa Allah.

Tunaweka mahitaji yetu mbele za Maimam wanyofu ili kwamba wamuombe Allah atuhurumie waja wake. Wakati tukisema, “Ewe Ali, nisaidie, “Ewe Husain, nisaidie” ni kama tu, mtu ambaye anataka kumfikia Mfalme. Anaweza kwenda kwa waziri Mkuu na kuomba amsaidie.

Hakika hamfanyi waziri mkuu huyo wa kama kimbilio la mwisho kwa kuondoa matatizo yake.
Kusudio lake pekee ni kumfikia mfalme kupitia kwake, kwa vile kwa kutokana na cheo chake, anaweza kuonana na mfalme kwa urahisi sana. Shi’a hawawachukuli dhuria wa Mtume kama washirika katika vitendo vitukufu; wanawachukulia wao kama waja Wake wacha-Mungu.

Daraja Ya Maimamu Ma’sumin

Kwa vile ni wawakilishi wa Mwenyezi Mungu wanawakilisha mahitaji ya shida zao Kwake. Kama ombi linastahili, Yeye hulikubali. Vinginevyo, jazaa yake itatolewa kesho akhera. Nukta moja haipasi kuachwa bila maelezo: Mashi’a wanachukulia cheo cha Maimam Ma’sum kama cha juu kuliko mashahidi wengine wa Uislamu.

Hafidh: Taarifa hii inahitaji maelezo. Ni tofauti gani kati ya Maimam wenu na Maimam wengine wote isipokuwa tu kwamba wao wana uhusiano na Mtume?

Muombezi: Kama utaitazama nafasi ya Uimam, utoana tofauti iliyowazi kati ya dhana ya Uimam inavyochukuliwa na Mashi’a na ile ya Masunni.