read

Mkutano Wa Tisa, Usiku Wa Ijumaa 2 Sha’ban 1345 A.H.

Sheikh: Siku zote unakosoa matendo ya Masunni, lakini hujali mwenendo wa Mashi’a. Unawatetea pasi na haki ingawa matendo yao yamepotoka.

Muombezi: Nimezoea kutetea haki. Imamu wetu Amiru’l-Mu’minin, aliwanasihi watoto wake, hususan Hasan na Husein kwa maneno haya: “Siku zote semeni kweli na fanyeni matendo yenu kwa kuzingatia kesho akhera. Kuweni wakali kwa madhalimu na wasaidieni wanaodhulumiwa.”

Kama nimewakosoa wapinzani au kuwatetea Mashi’a, nimefanya hivyo kwa kuunga mkono ukweli. Kile nilicholalamikia kilikuwa katika misingi ya hoja ya kimantiki. Nitasikiliza madai yako kuhusiana na matendo mabaya ya Mashi’a.

Mashi’a Kumshutumu Aisha Kwa Uzinifu Na Majibu Yake

Sheikh: Kitu kiovu kabisa ambacho Mashi’a wana hatia nacho ni kwamba wanamshutumu Ummu’l-Mu’minin Aisha na uzinifu. Ni ukweli unaokubalika kwamba alipata heshi- ma ya unyumba na Mtukufu Mtume wa Allah (s.a.w.w.), na kwamba alikuwa mkewe kipenzi. Hawatambui shutuma hizi za masingizio zinaelekeza kwenye kitu gani. Hawakusoma Sura ya an-Nur ya Qur’ani Tukufu? Allah anasema: Wanawake wabaya ni kwa wanaume wabaya, na wanaume wabaya ni kwa wanawake wabaya, na wanawake wema ni kwa wanaume wema, na wanaume wema ni kwa wanawake wema.” (24:26)

Muombezi: Kwanza madai ya kwamba Mashi’a wanamshutumu Ummu’l-Mu’minin Aisha kwa matendo ya kifisadi na uzinifu ni ya uwongo kabisa. Kamwe kitu kama hicho hakijasemwa na Mashi’a.

Madai haya ni uzushi wa dhahiri uliosambazwa na Nawasib na Khawarij karne nyingi zilizopita ili kuchochea ghasia. Waliyahusisha kwa Mashi’a yale ambayo wameyasema wao wenyewe. Matokeo yake wengine bila kufanya utafiti, wakawashambulia Mashi’a kama unavyofanya wewe sasa. Kama ungelisoma vitabu vya Mashi’a, usingeona mahali popote ambapo Ummu’l-Mu’minin Aisha ameshutumiwa kwa uzinzi.

Kumtoa Aisha Kwenye Shutuma Ya Uzinifu

Kama utosoma vitabu vya historia na vya tafsir vya Shi’a, utaona jinsi gani walivyomtetea Ummu’l-Mu’minin Aisha kutokana na shutuma za uzinzi. Ukweli ni kwamba riwaya kama hizi zilifanywa na kikundi cha wanafiki wakati wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Baadhi ya waliohusika ni Mista Bin Uthatha, Hasan Bin Thabit na Abdullah Bin Ubayy. Kuhusu Aisha kutolewa katika shutuma za uwongo za wanafiki, aya saba ziliteremshwa katika Qur’ani Tukufu. Mashi’a wanaamini kwamba kutoa shutuma za uwongo za uzinzi au tendo la kifisadi dhidi ya Mwislamu ni haramu, sikuambii kumtaja mke wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), awe yeye ni Aisha au Hafsa.

Mume Na Mke Sio Lazima Washiriki Kiwango Kimoja Cha Mafanikio

Pili, Aya Tukufu ambayo umeisoma haina maana ya kile ulichokisema. Sio lazima hivyo kwamba kama mume ni muumini mwema na anayestahiki Pepo kwamba na mkewe naye atakuwa ni hivyo hivyo. Kuna mifano mingi ambayo inathibitisha kwamba wenza wanaweza kuwa viwango tofauti vya ubora.

Allah anasema katika Surat-Tahrim: “Allah anapiga mfano wa waliokufuru, kwa mke wa Nuhu na mke wa Luti, hawa wawili walikuwa chini ya waja wetu wema wawili, basi (wanawake hao) wakawafanyia khiyana, (lakini waume zao) hawakuwasidia chochote mbele ya Allah na ikasemwa: Ingieni motoni pamoja na waingiao. Na Allah anapiga mfano wa walioamini kwa mke wa Firauni aliposema: ‘Ee Mola Wangu! Nijengee nyumba peponi karibu Yako na uniokoe na Firauni na matendo yake, na uniokoe kutoka kwa watu madhalimu.” (66:10-11)

Sheikh: Inashangaza kwamba kwa kipindi kifupi hiki kunajitokeza mabadiliko katika maelezo yako.
Muombezi: Tafadhali nieleze hicho unachoona kama mabadiliko.

Sheikh: Katika sehemu moja unasema kwamba kumshtumu mtu yeyote kwa uzinzi ni haramu, lakini katika sehemu nyingine unasema kwamba mke wa Nuhu na mke wa Luti hawakuwa waaminifu kwa waume zao. Je, kauli hizi mbili sio mbali mbali kwa kila moja? Je, si makosa kwako wewe kuwashutumu wake za mitume kwa uzinzi na kutokuwa waaminifu?

Muombezi: Nina hakika unajua kwamba unatumia njia ya hila. Unajua vizuri sana “kutoaminika” inamaanisha nini katika aya tukufu ya Qur’ani tuliyoirejea mwanzo.

Maana Ya Kutoaminika Kwa Mke Wa Nuhu Na Mke Wa Luti

Ni ajabu juu yako kwamba unalikosea neno kutokuaminika kuwa lina maana ya uzinzi ingawa kuna tofauti kubwa kati ya maneno mawili haya. Wake wa Mitume walikuwa wameepukana kabisa na uzinzi. Hapa mjadala ni kuhusu kutokuaminika kwao. Kwanza, mke wa Mtume akitenda kinyume na maelekezo ya mumewe, basi hakika sio muaminifu. Pili, sio mimi ninayesema kwamba wameonesha kutoaminika. Qur’ani yenyewe inalielezea hilo: “Walikuwa sio waaminifu kwa waume zao,” na kutoaminika hakukuwa uzinzi. Kama nilivyosema mwanzo, wake za mitume wameepushwa kabisa na aina hii ya udanganyifu.

Hivyo maana ya kutoaminika kwao kulikuwa ni utovu wa utii (uasi). Mke wa nabii Nuhu alikuwa akipingana na mume wake na alikuwa akimfedhehi hadharani. Alisema: “Mume wangu ni mwenda wazimu. Kwa vile niko naye mchana kutwa na usiku, naijua hali yake halisi. Asikudanganyeni.” Mke wa Luti alikuwa akiwajulisha watu juu ya kila mgeni aliyekuja nyumbani kwake. Alikuwa akisababisha matatizo kwa kufichua siri za nyumbani kwa maadui zake.

Kutokuaminika Kwa Wake Hakumaanishi Kuwa Wachafu

Kwa mujibu wa mufasirina wa Qur’ani na vile vile kwa mujibu wa maelezo ya Ma’sumin, maana ya ya aya ya an-Nur, ambayo kwayo unatoa maoni yako, ni kwamba wanamke wachafu wanastahili wanaume wachafu na wanaume wachafu wanavutiwa nawo. Wanamke safi wanastahiki wanaume safi, na wanaume safi wanavutiwa nawo.

Katika sura hiyo hiyo katika aya iliyotangulia Allah anasema: “Mwanaume fasiki hataoa ila mwanamke fasiki au mwanamke mshirikina, na mwanamke fuska haolewi ila na mwanaume fuska au mshirikina .....” (24:3) Kwa ufupi, aya tukufu “wanawake wachafu kwa wanaume wachafu…” kwa njia yoyote haithibitishi hoja yako.

Kuhusiana Na Tabia Ya Aisha

Kukosolewa kwa Aisha sio kwa sababu ya chuki. Ni kwa sababu ya tabia yake mbaya. Aisha amefanya maovu ambayo hakuna mke mwingine wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), pamoja na Hafsa bint wa Umar aliyeyafanya. Aidha, ukosoaji wa Mashi’a uko hasa hasa ndani ya mipaka ya maelezo yaliyotolewa na maulamaa wenu wenyewe, ambao wanasimulia kwamba mwanamke huyu mwenye dukuduku alifanya maovu mabaya mno.

Sheikh: Je, ni sahihi kwa mtu mtukufu kama wewe kutoa shutuma kama hizo dhidi ya Ummu’l-Mu’minin?

Muombezi: Wake wote wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wako sawa kwa daraja isipokuwa Ummu’l-Mu’muminin Khadija (yeye daraja yake ni kubwa). Ummu Salama, Suda, Aisha, Hafsa, Maimuna, na wengine kwa mtazamo wetu sisi, wote ni Ummu’l-Mu’minin. Lakini tabia ya Aisha na maneno yake kwa hakika yalikuwa tofauti na yale ya wanawake wengine. Tena, haya sio maneno yangu tu, lakini maulamaa wenu wameandika kwamba maisha yake yalikuwa na dosari. Matendo mazuri na mabaya ya watu hayawezi kufichika daima. Hatimaye ukweli hujitokeza wenyewe.

Sheikh: Bila shaka, kwa sababu alimpinga Ali, unamkosoa kuhusiana na mambo yasiyo na maana.

Muombezi: Hatumkosoi kuhusiana na mambo yasiyo na maana. Upinzani wa Aisha kwa Amiru’l-Mu’minin, Imam Hasan, Imam Husein, na Ahlu’l-Bayt ni suala tofauti. Lakini msingi wa historia mbaya wa maisha yake uliwekwa wakati wa kipindi cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mwenyewe. Alikuwa akimuudhi na kumsumbua sana.

Sheikh: Inashangaza kwamba unamuona Ummu’l-Mu’minin Aisha, mke kipenzi wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), kuwa asiye na thamani kimaadili kiasi hicho na unathubutu kusema kwamba alimuudhi Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Tutaamini vipi madai yako wakati Ummu’l-Mu’minin kwa hakika alisoma Qur’ani Tukufu na aya ifuatayo: “Kwa hakika wale ambao wanamuudhi Allah na Mtume Wake, Allah amewalaani duniani na akhera, na amewaandalia adhabu ya kufedhehesha. (33:57).

Hivyo inawezekana kwa yeye kumuudhi Mtukufu Mtume ili aweze kulaaniwa na Allah? Hii kwa hakika ni moja ya kashfa za Mashi’a.

Muombezi: La hasha, huu sio uongo! Kuhusiana na aya hizi tukufu, ninakiri kwamba Ummul-Mu’minin Aisha atakuwa lazima amezisoma, bali baba yake na masahaba wengine mashuhuri watakuwa lazima wamezisoma. Kwa kuzingatia zile riwaya na hadith ambazo nimezitaja katika mikesha iliyopita, ukweli mwingi utafichuka kwetu alimuradi tu kwam- ba tunakuwa waadilifu.

Aisha Alimhuzunisha Mtukufu Mtume

Ukweli kwamba Aisha alimhuzunisha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) haukusimuliwa na Ulamaa wa ki-Shi’a tu, bali na ulamaa wenu mashuhuri pia. Imam Ghazali katika kitabu chake, Ihya’ul-Ulum, Jz. 2, mlango wa 3, Kitab-e-Adabun-Nika, uk. 135, amesimulia hadithi nyingi kuhusiana na tabia ya Aisha. Miongoni mwa hizo ni kugombana kwake na Mtukufu Mtume na Abu Bakr kuingilia kati.
Tukio hili pia limesimuliwa na Mulla Ali Muttaqi ndani ya Kanzul-Ummal, Jz. 7, uk. 116; Abu Yala katika Musnad yake na Abu’sh-Sheikh katika Kitab-e-Amthal. Wanaandika kwamba Abu Bakr alikwenda kumuona binti yake, akakuta kwamba palikuwa na manung’unika kati ya Aisha na Mtukufu Mtume.

Uamuzi ya hilo uliachwa mikononi mwa Abu Bakr. Aisha akatumia lugha na kauli za matusi. Katika kuongea kwake, alimtaka Mtume kufanya haki katika tabia yake.

Kauli hii ya kifidhuli ilimfanya Abu Bakr akasirike kiasi kwamba akampiga kofi kwa nguvu sana usoni mwake mpaka damu ikachirizika hadi kwenye nguo zake.

Vile vile Imam Ghazali katika huohuo Mlango wa Ndoa na wengineo, pia wamesimulia kwamba safari moja, wakati Abu Bakr alipofika nyumbani kwa binti yake, alimkuta Mtume akiwa amemkasirikia Aisha. Yeye akawaomba wamueleze kuhusu kile kilichosababisha huzuni yao ili aweze kuleta suluhu baina yao.

Mtukufu Mtume alimuomba Aisha kama ataanza yeye kuelezea mkasa huo. Yeye akajibu, “Unaweza kuanza wewe lakini useme kweli.” Katika kauli yake iliyofuata akaongeza, “Wewe ni mtu anayejifikiria yeye mwenyewe kwamba ni Mtume!”

Maneno haya yanaonyesha kwamba isha hakuwa akiamini kwamba Mtukufu Mtume alikuwa ni Mtume aliyeteuliwa na Mungu. Kauli za dharau kama hizo zimesimuliwa katika vitabu vyenu kwa idadi kubwa. Zilikuwa ni chanzo cha maumivu makali sana kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)

Hakuna Riwaya Kama Hizo Kuhusu Wake Wengine Wa Mtukufu Mtume

Utaona kwamba ulamaa na wanahistoria wa madhehebu zote hawakusimulia mambo kama hayo kuhusu wake wengine wa Mtukufu Mtume. Hawakuhusisha mambo kama hayo hata kwa Hafsa binti ya Umar. Ilikuwa ni tabia tu ya Aisha iliyomsababishia aibu. Tumesimulia kiasi kile tu ulamaa wenu mashuhuri walichokisema kumhusu yeye.

Je, hukuvisoma vitabu vya Imam Ghazali, historia za Tabari, Mas’ud na ibn Atham Kufi na kadhalika, ambazo zinasimulia kwamba ulamaa wenu wakubwa wote wamemuelezea yeye kama asiyekuwa mtiifu kwa Mtukufu Mtume.

Bado unalalamika kwa sababu nimeishutumu tabia ya Ummul-Mu’minin. Kunaweza kuwa na doa la dhahiri katika tabia ya mtu kuliko kupituka dhidi ya amri ya Allah na Mtume Wake na kuasi dhidi ya khalifa wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)?

Katika Surat al-Ahzab, Allah swt. ameongea na wake za Mtukufu Mtume: “Na kaeni majumbani mwenu wala msijishauwe kwa majishauwo ya kijahilia ya zamani .....” (Al-Ahzab; 33: 33).

Kwa kweli wake wengine wa Mtukufu Mtume walikubaliana na amri hii na kamwe hawakuziacha nyumba zao bila ya sababu ya dharura muhimu. Hata A’mash amelisimulia jambo hili.

Ummul-Mu’minin Suda Hakutoka Japo Kwenda Hijja Au Umra

Imesimuliwa katika Sahih na vitabu vingine vya wanahistoria na wanahadithi wenu kwamba watu walimuuliza Suda, mke wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), kwa nini hakwenda Hijja wala Umra.

Yeye alijibu akasema: “Ni wajibu juu yangu mimi kufanya Hijja moja na Umra na wala sio zaidi. Na Yeye anasema: “Na bakieni majumbani mwenu.”

Hivyo kwa kuitii amri hii, mimi sitatoka nje ya nyumba yangu; bali nia yangu ni kwamba sitatoka, kwa kiasi inavyowezekana, nje ya chumba ambamo Mtukufu Mtume wa Allah ameniweka mpaka nitakapofariki.” Kwa kweli alifanya hivyo na ilikuwa ni mwili wake mfu ndio uliotolewa kutoka kwenye chumba hicho.

Suda, Aisha na Ummu Salma wote walikuwa ni wake za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na walikuwa ni Mama wa Waumini. Kwa hakika wanatofautiana kila mmoja wao kutokana na tabia zao.
Kwa mujibu wa umma, Aisha na Hafsa walikuwa wanastahiki heshima, sio kwa sababu walikuwa mabinti wa Abu Bakr na Umar, ingawa mnawaheshimu kwa matokeo ya hoja hiyo, bali ni kwa sababu walikuwa ni wake za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Lakini wake za Mtume wanastahiki heshima kama wakiwa watiifu, kama ilivyoelezwa wazi ndani ya Qur’ani tukufu: “Enyi wake za Mtume! Ninyi sio sawasawa na wanawake wengine wowote.” (33: 32)

Aisha Atoka Kwenda Kupigana Dhidi Ya Ali

Hivyo Suda alikuwa mchamungu, mke mtiifu wa Mtume wa Allah. Aisha alikuwa mke mkaidi ambaye alikula njama na Talha na Zubair dhidi ya Ali na akaenda Basra. Kule Uthman Bin Hunaif, sahaba mkubwa wa Mtume na gavana wa Basra aliyeteuliwa na Ali, alikamatwa. Nywele zake na ndevu vilivutwa; aliteswa na akafukuzwa nje ya mji. Zaidi ya watu 100 wasio na hatia na wasiojiweza waliuawa. Ibn Athir, Mas’udi, Muhammad Bin Jarir Tabari, Ibn Abi’l-Hadid, na wengine wameandika kwa urefu kuhusu kadhia hii.

Baada ya kitendo hiki cha jeuri na ufisadi, alipanda ngamia aitwaye Askar, akiwa amevaa vazi lililotengenezwa kwa ngozi ya simba, akiwa amekingwa na jeshi aliingia kwenye uwanja wa mapambano kama mwana jeshi. Kwa sababu ya uasi wake, maelfu ya Waislamu walipoteza maisha yao. Je, uamuzi huu kwa upande wake haukuwa wa kuvuka mipaka dhidi ya amri ya Allah na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)?

Maadili Ya Ali Yamevuka Kiwango Kwa Idadi

Na kinachoshsngaza zaidi ni kwamba alichukuwa msimamo wa aibu dhidi ya Ali Bin Abi Talib, ambaye maadili yake na wema wake vimeandikwa kwa wingi sana na maulamaa wenu wenyewe mashuhuri kiasi kwamba sio rahisi kuyasimulia yote.

Imamu Ahmad Bin Hanbal katika “Musnad” yake, Ibn Abi’l-Hadid katika kitabu chake “Sharh-e-Nahju’l-Balagha”, Imam Fakhrud-Din Razi katika kitabu chake “Tafsir-e- Kabir”, Khatib Khawarizmi katika kitabu chake “Manaqib”, Sheikh Suleimani Balkhi Hanafi katika kitabu chake “Yanabiu’l-Mawadda”, Muhammad Yusuf Ganji Shafi’i katika “Kifayatut-Talib” Sura ya 62, na Mir Seyyid Ali Hamadani Shafi’i katika kitabu chake “Mawaddatu’l-Qurba”, Mawadda ya 5, anasimulia kutoka kwa Khalifa wa pili, Umar Bin Khattab na Abdullah Ibn Abbas kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimuambia Ali: “Kama bahari zote zingekuwa ni wino, miti yote ingelikuwa kalamu, na wanadamu wote wangelikuwa ni waandishi na majini wote wakatunza kumbukumbu, hata hivyo, Ewe Abu’l-Hasan! Maadili yako yasingeweza kuhesabiwa.”

Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anasema kwamba ‘binadamu na majini wote kwa pamoja hawawezi kuhesabu maadili yake, je, sisi tutaweza vipi, na akili zetu zenye ukomo kutoa hesabu kamili ya sifa zake?
Mbali na ulamaa wa ki-Shia, maulamaa wenu wenyewe pamoja na ushupavu wao mkubwa wote, wamejaza vitabu vyao na sehemu tu ya maadili yake mengi.

Hadithi Katika Kusifia Maadili Ya Ali

Inakupaseni kuchunguza vitabu vyenu vya “Siha-e-Sitta” (vile vitabu sita maarufu vya hadithi). Mbali na hivi imeelezwa katika “Mawaddatu’l-Qurba” cha Mir Sayyid Ali Hamadani; “Mu’ajam Kabir” cha Tabrani “Matalibus-Su’ul” cha Muhammad Bin Talha Shafi’i; “Musnad” na “Fadha’il” vya Imam Ahmad Bin Hanbal; “Bainus-Sahihain” cha Hamid; “Manaqib” ya Khawarizmi; “Sharh-e-Nahju’l-Balagha” Jz. 2, uk. 449, cha Ibn Abi’l-Hadid; “Fusulu’l-Muhimma”, cha Ibn Sabbagh Maliki, hususan uk. 124, kutoka kwa Hafiz Abdu’l-Aziz Bin Al-Akhzaru’l-Janabiz, ambaye anaandika katika kitabu chake “Ma’alimu’l-Atratu’n-Nabawiyya” kwamba Fatima Zahra alisema kwamba katika usiku wa Arafa baba yake, Mtukufu Mtume wa Allah (s.a.w.w.), alikuja kwake na akasema, “Allah (swt) huwa na fahari kwenu watu ninyi mbele za malaika na amekusameheni ninyi wote na hususan Ali.

Mimi, Mtume wa Allah ninasema bila kuzingatia upendo kwa ndugu kwamba hakika mtu mwenye bahati sana na mwenye kufuzu ni yule ambaye ni rafiki wa Ali wakati wa uhai wake na baada ya kifo chake. Mtu aliyelaaniwa zaidi miongoni mwa waliolaaniwa, ni yule ambaye ni adui wa Ali wakati wa uhai wake au baada ya kifo chake.”

Vile vile katika vitabu hivyo hapo juu kuna hadithi ndefu ambayo nafikiri niliitaja katika mikesha ya mwanzo, kutoka kwa Khalifa Umar Bin Khattab, ambaye alisema kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimuambia Ali: “Mtu mwongo ni yule ambaye anafikiri kwamba ananipenda mimi ambapo ni adui wako. Ewe Ali! Yule ambaye ni rafiki yako ni rafiki yangu.

Kama mtu yeyote ni rafiki yangu, Allah ni rafiki yake pia. Kama Allah ni rafiki kwa mtu yeyote, basi humuingiza Peponi. Yule ambaye ni adui yako, ni adui yangu. Kama mtu yoyote ni adui yangu, Allah vile vile ni adui yake na humtupa Motoni.”

Urafiki Na Ali Ni Imani Na Upinzani Kwake Ni Ukafiri Na Unafiki

Vile vile imesimuliwa katika “Kitabu’l-Al” cha Ibn Khalawayh, akisimulia kutoka kwa Abu Sa’id Khadiri, kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimuambia Ali: “Ewe Ali! Urafiki na wewe ni imani na upinzani kwako ni unafiki. Mtu wa kwanza kuingia Peponi atakuwa ni rafiki yako, na mtu wa kwanza kutupwa motoni atakuwa ni adui yako.”

Mir Sayyid Hamadani Shafi’i katika kitabu chake “Mawaddatu’l-Qurba”, Mawadda ya 3, na Hamwaini katika kitabu chake “Fara’id” wanaandika kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema wakati akiwa miongoni mwa Sahaba wake: “Hakuna anayempenda Ali isipokuwa mtu muumini, na hakuna aliye na uadui kwake isipokuwa yule ambaye ni kafiri.”

Na katika tukio lingine anasema: “Ewe Ali! Akupendaye wewe ni yule tu ambaye ni muumin, na mnafiki ni yule tu ambaye hukuchukia wewe.”

Ali Ni “Mbora Wa Viumbe” Amesema Mtukufu Mtume – Imesimuliwa Na Aisha

Muhammad Bin Yusuf Ganji Shafi’i katika Kifayatut-Talib, ukurasa wa 119, Sura ya 62, ananukuu kutoka kwenye Ta’rikh-e-Damishiq, Muhadith-e-Sham na Muhadth-e-Iraq, wakisimulia kutoka kwa Hudhaifa na Jabir kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Ali ni mbora wa viumbe; mtu ambaye anakataa kulikubali hili, huyo ni kafiri.”

Vile vile imesimuliwa kutoka kwa Ata kwamba watu walimuuliza Aisha kuhusu Ali na akasema: “Ni mbora wa viumbe. Hakuna yeyote mwenye shaka ya aina yoyote ile isipokuwa kafir.”

Anasema kwamba Hafidh Ibn Asakir katika kitabu chake cha Ta’rikh, kitabu chenye juzuu 100, juzuu tatu kati hizo zimeandikwa kwa kumsifia Ali, ameisimulia hadith hii kutoka kwa Aisha.

Muhammad Bin Talha Shafi’i katika Matalibus-Su’ul, ukurasa wa 17, Ibn Sabbagh Makki katika kitabu chake Fusulu’l-Muhimma, wanasimulia kutoka kwa Tirmidhi na Nisa’i kwamba Abu Sa’id Khudri alisema: “Wakati wa uhai wa Mtume tulizoea kuwatambua wanafiki kwa uadui wao kwa Ali.”

Inasimuliwa katia Fusulu’l-Muhimma kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema kumuambia Amiru’l-Mu’minin Ali: “Ewe Ali! Kupigana dhidi yako wewe ni kupigana dhidi yangu; damu yako ni damu yangu.

Napigana dhidi ya yule ambaye anapigana dhidi yako wewe; ni yule tu aliyezaliwa ndani ya ndoa ndiye mwenye kukupenda wewe, na ni aliyezaliwa nje ya ndoa tu ndiye mwenye uadui na wewe. Ni mu’uminin tu ndiye ambaye anakupenda wewe, na ni mnafiki tu ndiye ambaye ana uadui na wewe.”

Sheikh: Hadith kama hizo sio za kipekee kwa Ali tu; zimesimuliwa vile vile kuhusu makhalifa wengine.

Muombezi: Tafadhali taja hadthi hizo kwa njia ya mfano.

Sheikh: Abdu’r-Rahman Ibn Malik Maghul anasimulia kutoka kwenye vyanzo vyake kwamba Jabir alisema kwamba Mtukufu Mtume wa Allah (s.a.w.w.) alisema: “Mu’umin hana uadui kwa Abu Bakr na Umar, na mnafiki hana upendo kwao.”

Muombezi: Nimeshangazwa tena kusikia kitu kama hicho kutoka kwako. Umesahau makubaliano yetu ya pamoja tuliyoyafanya usiku wa kwanza kwamba hatutategemea juu ya hadithi zenye mashaka. Hupaswi kunukuu hadithi za kubuni, ambazo wasimuliaji wake ni waongo na waghushaji. Nukuu hadith sahihi.

Sheikh: Majibu yako yanaonesha kwamba kama ukisikia hadithi yoyote kutoka kwetu utaikataa.

Muombezi: Kamwe sifanyi hivyo, sio mimi peke yangu niliyeikataa hadithi hiyo. Hata maulamaa wako mwenyewe wameikataa. Rejea kwenye Mizanu’l-Itidal cha Dhahabi na Ta’rikh ya Khatib-e-Baghdadi, juzuu ya 10, uk. 236. Utaona kwamba wengi wa wafasir wakubwa wameandika kuhusu tabia ya Abdu’r-Rahman Bin Malik wakisema:

“Hakika, huyu alikuwa ni muongo, mwenye kufuru na mghushaji wa hadithi kiasi kwamba hakuna yeyote mwenye shaka kuhusu hilo. Tafadhali tueleze kama hadithi hiyo ya upande mmoja iliyosimuliwa na muongo na mghushaji, inaweza kulinganishwa na hadithi zile ambazo maulamaa wako mashuhuri wamezisimulia, na ambazo baadhi yake nimezitaja.

Ningekushauri kuitazama Jami’u’l-Kabir, cha Suyuti, juzuu ya 6, uk. 390, Riyazu’n- Nazara, juzuu ya 9, uk. 215, cha Muhibu’d-Din; Jami’i Tirmidhi, juzuu 2, uk. 299; Isti’ab, juzuu ya 3, uk. 46, cha Ibn Abdu’l-Birr; Hilyatu’l-Auliya, juzuu 6, uk. 295, cha Hafidh Abu Nu’aim, Matalibus-Su’ul, uk. 17, cha Muhammad Bin Talha Shafi’i; Fusulu’l-Muhimma, uk. 126, cha Ibn Sabbagh Malik. Utaona kila mmoja wao amesimulia kwa hitilafu kidogo ya maneno kutoka Abu Dharr Ghifari ambaye alisema: “Wakati wa uhai wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) tulizoea kuwatambua wanafiki kwa alama tatu: kumkataa Allah na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), kushindwa kuswali, na uadui kwa Ali Bin Abi Talib.” Imesimuliwa kutoka kwa Abi Sa’id Khudri kwamba Abu Dharr Ghifari alisema: “Tumezoea kuwatambua wanafiki kwa uadui wao dhidi ya Ali na wakati wa uhai wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) tulikuwa hatuna alama nyingine ya kuwatambua wanafiki isipokuwa kwamba walikuwa maadui kwa Ali.”

Waandishi Wanaosimulia Hadithi Ya Mtukufu Mtume Kuhusu Chuki

Za Wanafiki Juu Ya Ali

Kwa nyongeza, waandishi wafuatao wanasimulia hadithi kuhusu chuki za wanafiki juu ya Ali: Imam Ahmad Hanbal katika Musnad, juz. 1, uk. uk. 95, 138; Ibn Abdul’l-Birr katika Isti’ab, juz. 3, uk. 37; Ahmad Khatib Baghdadi katika Ta’rikh-e-Baghdad, juz. 14, uk. 426; Ibn Abi’l-Hadid, katika Sharh-e-Nahju’l-Balagha, juz. 4, uk. 264; Imam Nisa’i katika Sunan yake, juz. 8, uk. 117 na Khasa’isu’l-Alawi, uk 27; Hamwaini katika Fara’id, Sura ya 22; Ibn Hajar katika Isaba, juz. 2, uk. 509; Hafidh Abu Nu’aim katika Hilyatu’l-Auliya, juz. 4, uk. 185; Sibt Ibn Jauzi katika Tadhkira, uk. 15; Suyuti katika Jami’u’l-Kabir, uk. 152 na 408; Muhammad Ibn Talha Shafi’i katika Matalibus-Su’ul, uk. 17; Tirmidhi katika Jami’i, juz. 2, uk. 13, wote hawa wameandika katika vitabu vyao kwa tofauti kidogo ya maneno kutoka kwa Ummu Salma au Ibn Abbas kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Ewe Ali! Mnafiki sio rafiki yako na mu’umini sio adui yako. Ni mu’min tu yule ambaye anakupenda wewe, na ni mnafiki tu ndiye ambaye hukuchukia wewe. Mnafiki hampendi Ali na mu’umin hamchukii Ali.”

Ibn Abi’l-Hadid katika Sharh-e-Nahju’l-Balagha, juz. 1, uk. 367, anasimulia kutoka kwa Sheikh Abu’l-Qasim Balkhi, mkuu wa madhhebu ya Mu’tazili, kwamba amesema, “Hadithi zote kwa pamoja zinasimulia zile hadithi sahihi na hakuna shaka juu ya usahihi wa zile ambazo zinasema kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema kumuambia Ali, “Hakuna mtu yeyote ambaye ni adui kwako isipokuwa yule ambaye ni mnafiki. Hakuna mtu yeyote ambaye ni rafiki yako isipokuwa ni mtu ambaye ni mu’umin.”

Vile vile, kati- ka juzuu ya 4 ya kitabu chake (Ibn Abi’l-Hadid), ukurasa wa 264, ananukuu hotuba ya Amirru’l-Mu’minin, ambayo kwayo Mtukufu Imam anasema:

“Kama ninampiga dharuba mu’umin na upanga huu katika uso wake ili kwamba awe na uadui juu yangu mimi, kamwe hawezi kuwa na uadui na mimi; lakini kama ninautoa ulimwengu mzima kumpa mnafiki ili anipende, kamwe hatanipenda.

Na hili ni kulingana na kauli ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ambaye alisema: ‘Ni waumin tu wanaokupenda wewe, na ni wanafiki tu ndio wenye uadui na wewe.
Kuna hadith nyingi za aina hii katika vitabu vyenu vya kuaminika. Nimevitaja tu baadhi ya hivyo. Je, uasi wa Aisha dhidi ya mamlaka ya Ali haukuwa ni uasi dhidi ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mwenyewe? Je, kupigana au kushawishi kwake watu kupigana dhidi ya Ali kulikuwa ni kwa sababu ya urafiki wake au ilikuwa ni kwa sababu ya uadui wake? Ni dhahiri, ilikuwa ni kwa sababu ya uadui.

Katika hadithi zote ambazo nimezisimulia hivi punde tu, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema kwamba moja ya alama za unafiki ni kupi- gana dhidi ya Ali. Utaupatanisha vipi msimamo uliochukuliwa na Ummu’l-Mu’minin Aisha katika kupigana na Ali pamoja na hadithi hizi?

Imekuja kwenye akili yangu hivi punde kwamba Mir Sayyid Ali Hamadani Shafi’i katika Mawaddatu’l-Qurba, mawdda ya 3, amesimulia kutoka kwa Aisha mwenyewe kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Allah ameahidi neno Lake kwangu kwamba yeyote yule ambaye anaasi dhidi ya Ali ni kafiri na makazi yake ni Motoni.”

Inashangaza kwam- ba wakati watu walipomuuliza kwa nini aliasi dhidi ya Ali hali ya kuwa amesikia hadithi kama hiyo kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), alijibu tu: “Niliisahau hadithi hii siku ya Vita vya Jamal (vita vya Ngamia). Sikuikumbuka mpaka nilipofika Basra.”

Sheikh: Lakini vipi unamuona Ummu’l-M’uminin kuwa na makosa wakati ni dhahiri kwamba kusahau ni ubinadamu.

Muombezi: Hata kama nitakiri kwamba alisahau hadithi ile siku ya Vita vya Jamal, je, hakuikumbuka wakati anarudi kutoka Makka na marafiki zake wote pamoja na wake wachamungu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) walipomuonya kwamba asifanye kitendo kama hicho, kwa vile upinzani kwa Ali ulikuwa ni upinzani kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)?

Wanahistoria wenu wenyewe ambao wameandika kuhusu Vita vya Jamal wamevuta nadhari kwenye ukweli kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Ewe Aisha! Ogopa ile njia ambayo mbwa wa Haw’ab watakubwakia.” Hata hivyo wakati akiwa njiani kuelekea Basra, alifikia kijito kidogo cha Bani Kilab, mbwa wakamzunguka na kuanza kubweka. Aliwauliza watu hiyo ilikuwa ni sehemu gani. Aliambiwa kwamba hapo ni Haw’ab.

Kisha alikumbuka kile alichoambiwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Kwanini basi aliingia kwenye mtego wa Talha na Zubair? Kwa nini aliendelea mpaka akafika Basra ambako alis- ababisha fujo na ghasia kama ile? Je, utasema kwamba alikuwa amesahau na hili pia, au alipita njia ile kwa makusudi? Aliivunja amri ya Allah na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa makusudi, na huku akiwa amekula njama na Talha na Zubair, alikwenda kupigana dhidi ya Khalifa na mwandamizi wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), ingawa yeye mwenyewe amesimu- lia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Mtu anayepigana dhidi ya Ali ni kafiri.”

Je, hiyo haikuwa sababu ya kuhuzunisha kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwamba mara tu baada ya Amiru’l-Mu’uminin kuchuka hatamu za ukhalifa, vurugu zilianzshwa na wahai- ni walitayarisha vita dhidi yake. Niliwaambieni mapema kwa vyanzo sahihi kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Ambaye anamhuzunisha Ali, hakika ananihuzunisha mimi. Yule ambaye ananihuzunisha mimi, hakika anamhuzunisha Allah, Enyi watu! Yule ambaye atamhuzunisha Ali atafufuliwa kama Myahudi au Mkiristo hiyo Siku ya Hesabu.”

Mauaji Ya Masahaba Na Waumini Wasio Na Hatia Huko Basra Kwa Amri

Ya Aisha

Riwaya hizi zinaweza kupatikana katika vitabu vyenu sahihi. Kwa nini basi muwaone Mashi’a kuwa na makosa? Uwajibikaji kwa ajili ya damu ya waumini wasio na hatia, mateso na kufukuzwa kwa Uthman Bin Hunaif, na mauaji ya zaidi ya watu 100 pamoja na walinzi wa Hazina wasio na silaha ambao hawakuwa na habari na vita hivyo - 40 miongoni mwao ambao waliuawa msikitini - umeangukia sawasawa juu ya wachochezi wa vita hivyo.

Allama Mas’udi katika kitabu chake Muruju’z-Dhahib, juz. 2, uk. 7, ameandika kuhusu hili katika maneno haya: “Mbali na wale waliojeruhiwa, walinzi sabini wasio na silaha wa Hazina ya Umma waliuawa.
Kati ya hawa sabini, hamsini walikatwa vichwa vyao ndani ya jela. Watu hawa walikuwa wa kwanza miongoni mwa Waislamu waliokuwa wameteswa mpaka kufa.” Miongoni mwa maulamaa wenu na wanahistoria, Ibn Jarir na Ibn Athir wametoa maelezo ya kinaganaga kuhusu matukio haya.

Mashi’a Wanasema Kuhusu Aisha Kile Haswa Kinachooneshwa Na Wanahistoria

Pengine itakulazimu kufuta riwaya hizi kutoka kwenye vitabu vyenu vya sahihi. Kwa kweli, katika machapisho ya marudio ya vitabu hivi, baadhi ya maulamaa wenu wamebadilisha baadhi ya maelezo haya wasiokubaliana nayo na katika hali nyingine wameyaondoa kabisa.

Itakupasa imma kukataa kile walichokiandika maulamaa na wanahistoria wenu mashuhuri, au itakupaseni kuacha kuwalaumu Mashi’a. Wanasema tu yale ambayo yame- andikwa kwenye vitabu vyenu wenyewe vya kuaminika.

Hakuna Ushahidi Kwamba Aisha Alitubia

Sheikh: Unachosema kwa hakika ni kweli, lakini Ummu’l-Mu’uminin Aisha alikuwa ni mwadamu tu; hakuwa ma’asum (asiyekosea). Akiwa katika hali ya kupotoshwa alifanya kosa. Ilikuwa kwa sababu ya wepesi wake wa kudanganyika kwamba alinasa kwenye mtego wa masahaba wawili mashuhuri, lakini baadae alitubia kwa ajili ya uasi wake. Allah alimsamehe kwa hilo.

Muombezi: Kwanza, umekiri kwamba baadhi ya masahaba mashuhuri walikuwa waovu, ingawa walikuwa miongoni mwa wale ambao walikuwa “chini ya mti” na katika Bai’atu’l- Ridhwan. Usiku mmoja uliopita ulitoa hoja kwamba masahaba walikuwa kama nyota, na tutakapomfuata yeyote miongoni mwao, tutaongozwa kwa haki. Sasa unakiri kwamba hii sio kweli.

Pili, umesema kwamba Ummu’l-Mu’minin Aisha alitubia kitendo chake hicho. Ni dai lililo tupu tu. Wakati ambapo uasi, vita na mauaji ya Waislamu yanakubaliwa na wote kwa pamoja, hakuna ushahidi wa kutubia kwake.

Aisha Anazuia Kuzikwa Kwa Imam Hasan Karibu Na Mtukufu Mtume

Kama mambo yalivyo, ni ukweli kwamba Ummu’l-Mu’minin Aisha hakutulizana. Alitenda makosa mengi ya kipumbavu. Lakini unadai kwamba alitubia kosa lake na kwa kusikia aibu, alijifungia nyumbani kwake. Lakini kama hii lingekuwa kweli kwa nini aufanyie vitendo vya aibu mwili wa mjukuu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)?

Tumejadili jinsi alivyomhuzunisha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na hatimaye jinsi alivyok- enda kwenye vita akiwa amepanda ngamia kwenda kupigana dhidi ya mwandamizi wa Mtume. Lakini baadae, safari hii akiwa amepanda juu ya nyumbu, alizuia mwili wa mjukuu mkubwa wa Mtukufu Mtume usizikwe karibu na (kaburi la) Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Maulamaa wenu mashuhuri na wanahistoria, pamoja na Yusuf Sibt ibn Jauzi katika kitabu chake Tadhkira Khawasu’l-Umma, uk. 122; Allama Mas’ud, mwandishi wa Muruju’z-Dhahab, katika Isbatu’l-Wasiyya, uk. 136; Ibn Abi’l-Hadid katika Sharh-e- Nahju’l-Balagha, juz. 4, uk. 18, akisimulia kutoka kwa Abu’l-Faraj na Yahya Bin Hasan, mwandishi wa Kitabu’n-Nasab; Muhammad Khwawind Shah katika kitabu chake Raudhatus-Safa, na wengine wengi wameandika kwamba wakati mwili wa Imam Hasan ulipokuwa unapekwa Madina, Aisha, alipanda nyumbu na akifuatwa na kundi la Bani Umayyah na watumwa wao, walilisimamisha kundi lililokuwa na mwili wa Imam Hasan.

Walisema kwamba hawataruhusu mwili wa Imam Hasan kuzikwa kando ya (kaburi la) Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). kwa mujibu wa riwaya ya Mas’udi, Ibn Abbas alisema: “Ni ajabu juu yako ewe Aisha! Je, haikukutosha ile siku ya Jamal, yaani siku ile ambayo uliingia kwenye uwanja wa mapambano ukiwa umepanda juu ya ngamia?

Je, sasa vile vile watu waweke kwenye kumbukumbu Siku ya Baghi (nyumbu)? Ukiwa umepanda nyumbu umelizuia jeneza la mtoto wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).
Siku moja umepanda ngamia, siku nyingine umepanda nyumbu, umeivunja staha ya Mtukufu Mtume wa Allah (s.a.w.w.). Je, umedhamiria kuingamiza nuru ya Allah? Lakini kwa hakika Allah anaikamilisha Nuru Yake lau washirikina wachukie; hakika, sisi ni wa Allah na Kwake Yeye tutarejea.”

Baadhi ya watu wameandika kwamba Ibn Abbas alimuambia: “Wakati mmoja ulipanda ngamia na wakati mwingine nyumbu. Kama utaishi zaidi, utapanda tembo vile vile (yaani utapigana dhidi ya Mungu)! Ingawa katika moja ya nane una mgao wa moja ya tisa, bado umechukuwa miliki ya kitu kizima.”

Bani Hashim walichomoa panga zao na wakadhamiria kuwafukuzilia mbali. Lakini Imam Husein akaingilia kati na akasema kwamba kaka yake alimuambia kwamba hakutaka hata tone la damu limwagwe kwa sababu ya mazishi yake. Kwa hiyo, jeneza lilirudishwa kutoka pale na mwili wake ukazikwa Baqi (eneo la makuburi mjini Madina ambalo bado linatembelewa na mahujaji mpaka leo).

Kusujudu Kwa Aisha Wakati Wa Kuuliwa Kishahidi Kwa Amirul-Mu’minin

Kama Aisha alitubia kwa uasi wake dhidi ya Amirul-Mu’minin, kwa nini alifanya sijda ya shukurani wakati aliposikia habari za kuuliwa kishahidi kwa mtukufu Imam? Abu’l-Faraj Ispahani, mwaandishi wa Aghani, akiandika kuhusu mtukufu Imam katika kitabu chake Maqatilut-Talibin, anasema: “Wakati Aisha aliposikia habari za shahada ya Amirul- Mu’minin Ali, alifanya sijda (ya shukurani).” Baadae, hata hivyo, alimuuliza mtoa habari juu ya ni nani aliyemuua Ali. Aliambiwa kwamba alikuwa ni Abdur-Rahman Ibn Muljim wa ukoo wa Bani Murad. Mara moja alisoma ubeti wa shairi, ambao maana yake ni: “Kama Ali yuko mbali na mimi, habari za kifo chake zililetwa na mtumwa, ambaye anaweza kuwa hana vumbi katika mdomo wake.”

Zainab, bint ya Ummu Salma alikuwepo wakati ule. Alimuuliza Aisha kama ilikuwa ni sahihi kwake yeye kuonyesha furaha yake na kutoa maneno kama hayo kuhusu Ali. Kilikuwa ni kitu kibaya sana. Aisha akajibu kwamba alirukwa na akili na kwamba alitoa maneno yale kwa kusahau. “Kama kitu kama hicho kikitokea tena kwangu na nikarudia maneno hayo, unaweza ukanikumbusha, ili nijizuie kufanya kitu kama hicho tena.” Mambo haya yanaonesha kwamba Aisha hakutubia baadae katika maisha yake kama unavyodai.

Kauli Za Aisha Zinazokinzana Kuhusu Uthman

Wakati huo huo nakumbuka akilini mwangu kitu kingine. Watu wenu wanawapinga Mashi’a kwa sababu wanamkosoa Khalifa Uthman kwa ajili ya makosa yake, makosa ambayo maulamaa wenu wenyewe wameyaandika katika vitabu vyao.

Kwa hiyo, pia hampaswi kumuangalia kwa upendeleo Ummu’l-Mu’minin Aisha vilevile, kwa sababu ulamaa na wanahistoria, kama vile Ibn Abi’l-Hadid katika Sharh-e-Nahju’l- Balagha, juz. 2, uk. 77; Mas’ud katika Kitab-e-Akhiru’z-Zaman na Ausat; Sibt Ibn Jauzi katka Tadhkira Khawasu’l-Umma, uk. 36; Ibn Jarir, Ibn Asakir, na wengine wameandika kwamba Ummul-Mu’minin Aisha siku zote alikuwa akimsema vibaya Uthman, kiasi kwamba alikemea:

“Muuweni Na’thal (mzee mpumbavu) Allah naamuuwe huyo, kwani amekuwa kafir.” Lakini punde tu Uthman alipouawa, yeye kwa sababu ya upinzani wake kwa Ali, alianza kusema: “Uthman ameuawa kama mtu aliyeonewa. Kwa jina la Allah nitalipiza kifo chake. Hivyo simameni na munisaidie.”

Ibn Abi’l-Hadid anaandika: “Hakika Aisha alikuwa adui mkubwa wa Uthman. Kiasi kwamba alitundika nguo ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) katika nyumba yake na alizoea kuwaambia watu ambao walikuja pale: ‘Hii ni nguo ya Mtukufu Mtume wa Allah (s.a.w.w.). Bado haijachakaa, lakini Uthman ameizeesha na kuichakaza sunna ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).’”

Ibn Abi’l-Hadid anaandika kwamba, wakati Aisha yuko Makka aliposikia habari za kuuli- wa kwa Uthman, alisema: “Allah amkatae kwenye rehema Yake. Alitenda matendo mabaya. Na Allah hawaonei viumbe wake, yaani, kama akimuadhibu yeyote, ni kwa sababu ya dhambi zake mwenyewe.

Mnazisikia kauli hizi kutoka kwa Aisha kuhusu Uthman bila ushahidi wowote na bado hamzitilii maanani. Lakini kama maneno kama hayohayo yanapotumiwa na Mashi’a, hara- ka sana mnawaita makafir.

Lazima tuchukue msimamo wa uadilifu wa mambo. Ni ukweli uliothibitika kwamba Ummul-Mu’minin Aisha alimpinga Imam Amirul-Mu’minin vikali sana.

Wakati aliposikia kwamba Waislamu wamekula kiapo cha utii kwa mtukufu Imam alisema: “Kuanguka kwa mbingu juu ya ardhi ni bora kuliko kusimamishwa kwa ukhalifa wa Ali. Uthman ameuawa kama mtu aliyeonewa.” Kwa hakika kauli hizi zisizopatana zinaashiria akili isiyotulia.

Allah Ni Mwingi Wa Huruma Lakini Damu Ya Waislamu Wasio Na Hatia Haiwezi Kupita Bila Kuhojiwa

Sheikh: Kutokupatana huku kwa kauli hizi za Ummul-Mu’minin kwa hakika kwa ujumla kumesimuliwa sana, lakini mambo mawili yanakubalika na kuthibitika. Kwanza, kwamba alidanganywa na kwa muda mfupi alikuwa hakuzingatia uandamizi wa Ali.

Yeye mwenyewe alisema kwamba aliusahau na aliukumbuka tu wakati alipokuwa Basra. Pili, alitubia kwa ajili ya kitendo chake. Hakika Allah, akiwa amekwishamsamehe, atampa nafasi ya juu katika Pepo.

Muombezi: Sitarudia niliyokwisha sema kuhusu suala la kutubia. Damu ya Waislamu wale ambao waliuawa bila kosa lolote, fedheha na aibu waliyofanyiwa, na kuporwa kwa mali zao hakuwezi kupita bila kupingwa. Ni kweli kwamba katika mahali pa msamaha, Allah ni Mwenye huruma mno, lakini katika mahali pa adhabu, Allah ni mkali sana. Mbali na hili, yeye mwenyewe alikiri mpaka wakati wa kifo chake kwamba alihusika na matukio yote yale ya kuchukiza.

Kama maulamaa wenu wenyewe walivyosimulia, aliigiza katika wosia wake kwamba hawezi akazikwa kando ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Alijua kwamba alisaidia katika vurugu nyingi baada yake.

Hakim katika kitabu chake, Mustadrak; Ibn Qutayba katika kitabu chake, Ma’arif; Muhammad Bin Yusuf Zarandi katika kitabu chake, Kitab-e-A’lam bi siratu’n-Nabi na Ibnu’l-Bayya Nishapuri na wengine wamesimulia kwamba Aisha alimsihi Abdullah bin Zubair katika maneno haya: “Nizike kando ya dada zangu katika makaburi ya Baqi. Nilizua mengi na mapya baada ya Mtukufu Mtume wa Allah (s.a.w.w.).”

Aisha Hawezi Kudai Kupoteza Kumbukumbu Kwa Sababu Alikumbushwa

Na Ummu Salamah

Unasema kwamba alikumbuka nemsi za Ali wakati akiwa Basra na alisahau kile ambacho Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimkataza kufanya. Hii sio kweli. Inapaswa uangalie vitabu sahihi vya maulamaa wenu mashuhuri. Kwa mfano, rejea kwenye Sharhe-e-Nahju’l- Balagha, juz. 2, uk. 77 ya Ibn Abi’l-Hadid.

Ibn Abi’l-Hadid anaandika kutoka kwenye Ta’rikh ya Abi Makhnaf Lut Bin Yahya Azadi kwamba Ummu Salma naye vile vile alikuwa Makka, wakati aliposikia kwamba Aisha anakusudia kulipa kisasi kwa ajili ya mauaji ya Uthman na alikuwa anakwenda Basra.

Hili lilimshitua sana na akaanza kutangaza ubora wa Ali katika mikutano yote. Aisha alikwenda kwa Ummu Salamah ili kumshawishi juu ya msimamo wake huo kabla ya kuondoka kwenda Basra.

Ummu Salamah akamuambia Aisha: “Mpaka jana ulikuwa unamtukana Uthman na kumuita mzee mjinga, na sasa umemgeukia Ali kutaka kulipa kisasi cha kuuawa kwa Uthman. Je, wewe hujui maadilifu ya Ali? Kama umesahau basi mimi nitakukumbusha.”

“Kumbuka siku ile, wakati nilipokuja chumbani kwako pamoja na Mtukufu Mtume wa Allah (s.a.w.w.)? Kisha Ali akaingia ndani na akaanza kuongea faragha na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Wakati mazungumzo ya faragha yalipoendelea kwa muda kiasi, uliamka na kumkaripia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Nilikusihi usifanye kitu kama hicho, lakini hukujali ushauri wangu. Ukamuambia Ali huku ukiwa umekasirika: ‘Katika siku tisa, moja ni kwa ajili yangu, na bado katika siku hiyo unakuja ndani kwangu na kumshughulisha na mazungumzo.’
Kwa sababu ya kitendo chako hicho Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikasirika sana kiasi kwamba uso wake uligeuka kuwa mwekundu na akasema: ‘Rudi! Naapa kwa jina na Allah kwamba yeyote yule ambaye ana uadui wa aina yoyote ule na Ali, awe anatokana na nyumba yangu au vinginevyo, anaondolewa katika imani.’ Kisha ukiwa umeabika, ulirudi nyuma.” Aisha akasema: “Ndio nakumbuka.”

Ummu Salamah akaendelea kusema: “Utakumbuka kwamba siku moja ulikuwa unaosha kichwa cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), nami nilikuwa natayarisha ‘hais’ (aina ya chakula). Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alinyanyua kichwa chake na akasema:

‘Ni nani miongoni mwenu ambaye ni yule muovu ambaye atapanda Ngamia, na ambaye atabwakiwa na mbwa wa Haw’ab, na ambaye ataanguka kichwa chini kutoka kwenye Daraja ya Sirat.’ Kisha niliicha ile ‘hais’ na nikasema:

Ewe Mtukufu Mtume wa Allah (s.a.w.w.)! Najikinga kwa Allah na Mtume Wake kutokana na kitendo kama hicho.’ Baada ya hili, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akikupiga mgongoni kwako alisema: ‘Liepuke hili; ni wewe utakayefanya kitendo hiki.’” Aisha akasema: “Ndio nakumbuka.”

Ummu Salamah akaendelea: “Nakukumbusha kwamba katika moja ya safari wewe na mimi tulikuwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Siku moja Ali alikuwa anashona viatu vya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), na sisi wawili tulikuwa tumekaa kwenye kivuli cha mti.

Ilitokea kwamba baba yako, Abu Bakr na Umar walikuja na kutaka ruhusa. Wewe na mimi tukaenda nyuma ya pazia. Walikaa chini na baada ya kuzungumza kwa muda, walisema:

‘Ewe Mtukufu Mtume wa Allah (s.a.w.w.)! Hatujui ubora wa usuhuba wako. Hivyo tunakuomba utujulishe ni nani atayekuwa mwandamizii na Khalifa wako ili baada yako apate kuwa ndio kiongozi wetu.’”

Mtukufu Mtume akawaambia: “Ninaijua nafasi yake, cheo chake na hadhi yake, lakini kama nitamtambulisha moja kwa moja ninyi mtamkataa kama Bani Israil walivyomkataa Haruni.’

Wote walinyamaza kimya na mara wakaondoka. Baada ya kuwa wamekwisha kuondoka sisi tukatoka nje. Mimi nikamuuliza Mtukufu Mtume, ‘Ni nani atakayekuwa khalifa wako kwa ajili yao?’ Mtume akajibu, ‘Anatengeneza viatu vyangu.’ Tukaona kwamba hakuna mwingine isipokuwa Ali. Kisha nikasema, ‘Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! sikumuona yeyote isipokuwa Ali.’Yeye akasema, ‘Ali huyohuyo ndiye khalifa wangu.’”

Aisha akasema: “‘Nakumbuka.’ Kisha Ummu Salamah akasema: ‘Ikiwa unajua hadithi zote hizi, sasa unakwenda wapi?” Akajibu: “Nakwenda kufanya amani miongoni mwa watu.”

Kwa hiyo, ni wazi kwamba Ummul-Mu’minin Aisha alikuwa hakudanganywa na wengine tu. Yeye mwenyewe alisababisha matatizo makubwa, na akiwa anajua mambo yote haya, kwa makusudi alisimama katika uasi ingawa Ummu Salamah alimkumbusha hadithi za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Hata baada ya kukiri cheo na nafasi ya Amirul-Mu’minin, aliondoka na kuelekea Basra na kusababisha vurugu kubwa, ambayo yaliishia katika kuuawa kwa Waislamu wengi.

Hadithi Ya Kushona Viatu Ndio Ushahidi Mkubwa Wa Uimam Na

Ukhalifa Wa Ali

Hadithi ya kushona viatu ndio ushahidi mkubwa wa Uimam na ukhalifa wa Ali. Mashi’a wanafanya udadisi wa kitafiti kwenye mambo ya miaka 1400 iliyopita. Pamoja na ujuzi wa aya za Qur’ani Tukufu na vitabu sahihi vya maulamaa wa madhehebu zote, wanafikia mahitimisho ya haki.

Kwa hiyo, tunaamini kwamba, igawa kihistoria, Ali alipewa nafasi ya nne, nafasi hii ya chini kidhahiri kabisa, haiathiri ubora wake wala kudogesha umuhimu wa hadithi ambayo inathibitisha nafasi yake sahihi kama mrithi wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Vile vile tunakubali kwamba ni ukweli uliohifadhiwa katika vitabu vya historia kwamba Abu Bakr (kwa hila za kisiasa) aliteuliwa kuwa Khalifa katika ukumbi wa Saqifa bila ya kuwepo Ali, Bani Hashim na masahaba wengine mashuhuri, pamoja na kuwepo upinzani wa ukoo wa Khazraj wa Ansari wa Madina. Baada ya hapo ikawa ni kwa udikiteta wa mtu mwenyewe binafsi, ambapo Umar na Uthmani walikalia kiti cha ukhalifa.

Lakini kuna tofauti. Watu hawa walikuwa makhalifa wa jumuiya; washirika wao ndio waliowafanya makhalifa. Kwa upande mwingine Amirul-Mu’minin Ali alikuwa ndiye Khalifa wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na aliteuliwa na Allah na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kuwa mwandamizi wa Mtukufu Mtume.

Sheikh: Huku ni kutokuwa kwako na huruma. Kulikuwa hakuna tofauti kati yao. Watu wale wale ambao wote kwa pamoja waliamua kuukabidhi ukhalifa huo kwa makhalifa watatu, Abu Bakr, Umar na Uthman vile vile waliukabidhi kwa Ali.

Tofauti Katika Mtindo Wa Uteuzi Wa Makhalifa Watatu Wa Mwanzo Ni Ushahidi Tosha Wa Kutosi- Hi Kwa Ukhalifa Wao

Muombezi: Kulikuwepo na tofauti nyingi za wazi katika namna ya uteuzi wa makhalifa. Kwanza, umetaja Ijma (uamuzi wa makubaliano ya pamoja). Hakuna ulazima wa kurudia hoja yangu. Nimethibitisha kutokuwepo kwa msingi wowote katika suala la Ijma katika mikesha iliyopita. Kwa hakika kulikuwa hakuna uamuzi wa pamoja kuhusu ukhalifa wa yeyote kati yao.

Ushahidi Mwingine Wa Ubatilifu Wa Ijmai

Pili, kama unategemea Ijmai (makubaliano ya wote pamoja) kama msingi wa ukhalifa na kuchukulia kwamba unakubalika kwa upande wa Allah na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), basi wakati wowote anapokufa Khalifa, umma wote ungelikusanyika pamoja kuteua Khalifa. Yeyote ambaye angechaguliwa angekuwa Khalifa wa watu [kwa kweli sio wa Mtukufu Mtume wa Allah (s.a.w.w.)]. Na utaratibu huu ungelifuatwa katika zama zote.

Hata hivyo, lazima ukiri kwamba Ijmai kama hiyo au makubaliano ya wote kama hayo hayajawahi kufanyika kamwe. Hata Ijmai ile ambayo haikukamilika ambayo kwayo Bani Hashim na Answar (watu wa Madina) hawakuwepo pia haikufanyika kwa yeyote isipokuwa kwa Abu Bakr Bin Qahafa.

Ukhalifa wa Umar, kwa mujibu wa maoni ya wanahistoria wote na wanahadthi wa Uislamu, ulitegemea juu ya uamuzi wa pekee wa Abu Bakr Bin Qahafa. Kama Ijma ilikuwa ni kihitajio kwa ajili kuteuliwa kwa Khalifa, kwa nini isifanyike kwa ajili ya kuukabidhisha ukhalifa kwa Umar na kwa nini maoni ya wote pamoja yasitafutwe juu ya hilo?

Sheikh: Ni dhahiri kwamba wakati ambapo Abu Bakr alifanywa kuwa Khalifa kwa makubaliano ya wote pamoja (Ijmai), uamuzi wa Khalifa wa kumteuwa mrithi wake ulikwa halali kabisa. Kulikuwa hakuna haja ya kufanyika Ijma nyingine. Bali, uamuzi wa kila Khalifa wa uteuzi wa Khalifa baada yake kimsingi ulikuwa sahihi na wa kutosha.

Haki hii imewekwa kwa Khalifa ili kwamba aweze kumteua Khalifa baada yake ili kwamba watu wasije wakaachwa kwenye mchafuko na mkanganyiko. Kwa hiyo, wakati Khalifa aliyekubaliwa, Abu Bakr, aliyeteuliwa kwa makubaliano ya jumla, alimteuwa Umar kama Khalifa, na hivyo yeye (Umar) akawa ni Khalifa wa haki wa MtukufuMtume (s.a.w.w.).

Uteuzi Wa Mtukufu Mtume Juu Ya Ali Ulipuuzwa, Na Uteuzi Wa Abu Bakr

Juu Ya Umar Ukahalalishwa

Muombezi: Unaamini kwamba Khalifa aliyekubaliwa ana haki ya kuteuwa mrithi. Ni jukumu lake kwamba asiuache umma kwenye mchafuko na bila kuongozwa, na uamuzi wake unatosha kwa ajili ya uteuzi wa Khalifa.

Lakini kama unaamini hivyo, kwa nini mnanyima Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) haki hii? Na kwa nini mnazipuuza dalili zote zile za wazi ambazo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa dhahiri kwa kurudia rudia alizozitoa katika nyakati tofauti na sehemu tofauti, akimtaja

Ali kama mrithi wake, na dalili ambazo zimo zote katika vitabu vyenu sahihi. Unalikwepa kirahisi tu suala hili na kutetea tafsiri zisizo sahihi kama Ibn Abi’l-Hadid alivyoipuuza hadithi ya Umma Salma katika misingi ya ajabu isiyo na maana yoyote.

Aidha ni kwa msingi gani unaweza kudai kwamba Khalifa wa kwanza, ambaye aliteuliwa kwa njia ya Ijmai, alikuwa na haki ya kuteua mrithi wake. Je, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alitoa maelekezo kama hayo? Hapana. Vile vile unadai kwamba wakati Khalifa wa kwanza aliupata wadhifa wake kwa Ijma, kulikuwa hakuna haja ya uteuzi wa makhalifa wengine kwa njia ya Ijmai. Makhalifa hao hao walikuwa na mamlaka kutoka kwenye umma kuteua Khalifa kwa ajili yao.

Pingamizi Juu Ya Majlis-E-Shura(Kamati Ya Ushauri)

Kama hali ilikuwa hivyo, kwa nini kanuni hiyo ilitwaliwa kwa ajili ya ukhalifa wa Umar peke yake? Kwa ukhalifa wa Uthman kanuni hii haikufuatwa. Badala ya kuteuwa Khalifa baada yake, Umar aliliacha suala hili kuamuliwa na kamati ya ushauri ya watu sita. Sijui ni nini unachofikiria kama ndio kanuni ambamo kwamba uteuzi wa Khalifa umetegemea. Unajua kwamba kama kuna tofauti za msingi katika mabishano ya hoja, hilo suala halisi huwa batili.

Kama msimamo wako ni kwamba msingi wa ukhalifa ni Ijmai na umma wote kwa pamoja lazima ufanye uamuzi (bila kutaja ukweli kwamba Ijma kama hiyo haikufanyika kwa ajili ya ukhalifa wa Abu Bakr), basi kwa nini Ijmai kama hiyo isifanyike kwa ajili ya ukhalifa wa Umar?

Kama unachukulia kwamba Ijmai hiyo ilikuwa lazima tu kwa ukhalifa wa kwanza, na kwa ajili ya uteuzi wa makhalifa wa baadae uamuzi wa Khalifa aliyechaguliwa ulikuwa unatosha, basi kwa nini kanuni hii isifuatwe katika suala la ukhalifa wa Uthman? Kwa nini Khalifa Umar aliiacha kanuni iliyotangazwa wazi na Abu Bakr? Kwa nini aliacha uteuzi wa Khalifa kwenye Majlis-e-Shura (kamati ya ushauri)?

Khalifa Umar aliiteua kidikteta kamati hiyo ingawa ingepaswa kuwa kamati ya uwakilishi wa umma (kusudi kuweze kuwa na uwakilishi fulani kidogo wa maoni ya wengi).

Pingamizi Kwa Abdu’r-Rahman Bin Auf Kuwa Ndio Msuluhishi

Kitu cha kushangaza zaidi ni kwamba haki za wajumbe wote wa kamati zilifanywa zinyenyekee kwa Abdu’r-Rahman bin Auf. Hatuelewi uteuzi wa Abdu’r-Rahman Auf umefanywa kwa misingi ipi. Je, ilikuwa dini, heshima, elimu au utendaji? Tunaweza tu kuona kwamba alikuwa jamaa wa karibu wa Uthman na hatamsaidia yeyote yule isikokuwa yeye. Iliamuliwa kwamba atakachosema Abdu’r-Rahman kitakuwa sahihi, na wakati akila kiapo cha utii kwa yeyote (katika wale watu watanoukimuondoa yeye mwenyewe), wengine wote lazima wamfuate.

Kwa Mujibu Wa Mtukufu Mtume, Ali Anapaswa Kufuatwa Kuliko Wengine Wote

Wakati tunapoliangalia suala hili kwa makini zaidi tunaona kwamba ilikuwa ni maagizo ya kidikiteta yaliyotolewa chini ya kisingizio cha Shura (kamati ya ushauri). Hata leo hii tunaona kwamba kanuni za demokrasia ziko kinyume kabisa na demokrasia yenyewe. Lakini Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa kurudia rudia alisema: “Ali anaiznguka haki na haki inamzunguka Ali.”

Vile vile alisema: “Ali ni ‘Faruq’ (Mbainishaji - wa haki na batili) wa umma huu na anavuta upambanuzi kati ya haki na batili.” Hakim katika kitabu chake Mustadrak, Hafidh Abu Nu’aim katika Hilya; Tabrani katika Ausat; Ibn Asakir katika Ta’rikh; Muhammad Bin Yusuf Ganji Shafi’i katika Kifayatut-Talib; Muhibu’d-Din Tabari katika Riyazu’n-Nuzra; Hamwaini katika Fara’id; Ibn Abi’l-Hadid katika Sharh-e- Nahju’l-Balagha na Suyuti katika Durru’l-Mansur wanasimulia kutoka kwa Ibn Abbas, Salman, Abu Dharr na Hudhaifa kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Mara tu baada yangu mimi vurugu zitaanza.
Katika wakati huo itakuwa lazima kwenu ninyi kuji- ambatanisha wenyewe na Ali Bin Abi Talib kwa vile ni mtu wa kwanza ambaye atapeana mikono pamoja na mimi katika Siku ya Hukumu. Yeye ndiye mtu muaminifu mno zaidi na ndiye Faruq wa umma huu; yeye anaonesha kipambanuzii kati ya haki na batili, na ndiye kiongozi wa waumini.”

Kwa mujibu wa hadithi kutoka kwa Ammar Yasir (ambayo kwayo nimeitaja mapema pamoja na maelezo kamili ya vyanzo vyake), Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Kama watu wote wanakwenda njia moja na Ali anakwenda njia nyingine, lazima umfuate Ali na kuwaacha wengine wote. Ewe Ammar! Ali hatakupotosha na hatakuelekeza kwenye maangamizi. Ewe Ammar! Utii kwa Ali ni utii kwangu mimi, na utii kwangu ni utii kwa Allah swt.”

Dhulma Mbaya Iliyofanywa Na Umar Kwenye Nafasi Ya Amirul-Mu’minin

Pamoja na hayo, Khalifa Umar, akiyadharau maelekezo ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), anamfanya Ali kuwa ni mdogo kwa Abdu’r-Rahman katika Shura. Je, mamlaka hayo ni halali, ambayo yanawakana masahaba mashuhuri? Waheshimiwa mabwana! Kuweni wenye haki! Chunguzeni maelezo ya kihistoria ya wakati huo, kama vile Isti’ab, Isaba na Hilyatu’l-Auliya.

77Kisha mlinganisheni Ali na Abdu’r-Rahman, na muone iwapo kama yeye alistahiki kupata haki ya kura ya turufu (veto) au Amirul-Mu’minin. Mtaona kwamba ni kutokana tu na hila za kisiasa kwamba haki ya Ali iliporwa.

Aidha, kama njia ya uteuzi iliyofuatwa na Umar Bin Khattab ilikuwa inafaa kufuatwa, yaani kama Majlis -e- Shura ilikuwa lazima kwa ajili ya uteuzi wa Khalifa, kwa nini basi isifanywe wakati Amirul-Mu’minin alipofanywa Khalifa?

Inashangaza kwamba katika ukhalifa wa makhalifa wanne (Abu Bakr, Umar, Uthman na Ali) njia nne tofauti zilifuatwa. Sasa ni ipi katika njia hizo kimsingi ilikuwa haki na ipi ambayo ilikuwa batili? Kama unasema kwamba njia zote nne zilikuwa za halali, basi laz- ima ukubali kwamba ninyi hamna kanuni ya msingi kwa ajili usimikaji wa Khalifa.

Sheikh: Huenda maelezo yako ni sahihi. Umesema lazima tutafakari sana suala hili. Tunaona kwamba ukhalifa wa Ali vile vile ni wa hali ya kuleta wasiwasi, kwani aina ya Ijmai ambayo ilimteuwa Abu Bakr, Umar na Uthman vile vile imemteuwa Ali kama Khalifa.

Muombezi: Unachosema kingeweza kuwa chenye kuweza kutetewa lau isingekuwa kwa kauli ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Kwa hakika ukhalifa wa Ali haukutegemea juu ya Ijmai ya umma. Uliamriwa na Allah.

Ukhalifa Wa Ali Uliamriwa Na Allah

Mtukufu Imam alitwaa ukhalifa kwa njia ya kuirudisha haki yake kwake. Kama haki ya mtu imeporwa, anaweza kuichukua wakati wowote anapopata fursa ya kufanya hivyo. Kwa hiyo, wakati ilipokuwa hakuna vikwazo na hali ya hewa ilihitaji hivyo, mtukufu Imam alijipatia haki yake.

Kama umesahau hoja tulizosema huko nyuma, unaweza kuangalia magazeti, ambayo yameandika taarifa tulizowasilisha kuhusiana na suala hili. Tumethibitisha kwamba Ali kukalia kiti cha ukhalifa msingi wake ulikuwa juu ya aya za Qur’ani Tukufu na juu ya hadithi za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Huwezi kutaja hadithi hata moja inayokubaliwa na madhehebu zote ambayo kwayo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema kwamba Abu Bakr, Umar, au Uthman walikuwa warithi wake.

Kwa hakika kama mambo yalivyo, mbali na hadithi katika vitabu vya Shi’a, kuna idadi kubwa ya hadithi kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) zilizoandikwa kwenye vitabu sahihi vyenu wenyewe, ambazo zinaonesha kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa dhahiri alimteuwa Ali kama mrithi wake.

Sheikh: Vile vile kuna hadithi ambazo zinaonesha kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema kwamba Abu Bakr alikwa ni Khalifa wake.
Muombezi: Kwa dhahiri umesahau hoja yangu ya mikesha iliyopita ambayo inakanusha kukubalika kwa hadithi hizo. Hata hivyo, nitajibu tena usiku huu. Sheikh Mujaddidu’din Firuzabadi, mtunzi wa Qamusu’l-Lughat anasema katika Kitab-e-Safarus-Sa’adat: “Chochote ambacho kimesemwa katika kumtukuza Abu Bakr kimetegemea juu ya visa vya kubuni kiasi kwamba akili ya kawaida haivikubali kuwa ni vya kweli.”

Kama utachunguza vizuri zaidi tatizo la ukhalifa, utaona kwamba kwa hakika kulikuwa hakuna Ijma kwa yeyote kati ya makhalifa wakubwa wanne (Abu Bakr, Umar, Uthman na Ali) au kwa yeyote kati ya makhalifa wa Banu Umayya na Banu Abbas. Umma wote kamwe haukukusanywa wala wawakilishi wa umma kukusanya pamoja kupiga kura zao.

Lakini, tukizungumza kwa ulinganishi, tunaona kwamba ukhalifa wa Ali uliungwa mkono na kile ambacho kilikuwa karibu sana na Ijmai. Wanahistoria na maulamaa wenu wenyewe wanaandika kwamba kwa ukhalifa wa Abu Bakr kwanza kabisa walikuwa ni Umar na Abu Ubaida Jarra, yule mchimba makaburi, ndio waliokuwepo tu.

Baadae baadhi ya ukoo wa Aus ulikula kiapo cha utii kwake kwa sababu walikuwa wanapingana na ukoo wa Khazraj ambao walikuwa wamemteuwa Sa’d Bin Ubaida kama mgombea. Baadae zaidi wengine kwa kupitia vitisho, (kama nilivyoelezea mapema kwa urefu) na kundi jingine likichochewa na fikra za kisiasa walikula kiapo cha utii kwa Abu Bakr. Ma-Answari (watu wa Madina) ambao walimfuata Sa’d Bin Ubaida, hawakuukubali ukhalifa mpaka dakika ya mwisho.

Kisha ukhalifa wa Umar uliasisiwa tu kwa pendekezo la Abu Bakr, ambalo halikuhusika na chochote na Ijmai. Hatimaye Uthman alikuwa Khalifa kwa uamuzi wa Majlis-e-Shura (kamati ya ushauri) ambayo iliundwa kidikteta na Khalifa Umar.

Wakati wa ukhalifa wa Ali wawakilishi wengi wa nchi nyingi za Kiislamu, ambao kwa bahati walikuja Madina kutafuta marekibisho ya manun’guniko yao, walisisitiza juu ya Ali kuwa Khalifa.

Nawab: Je, wawakilishi hao wa nchi za Kiislamu walikusanyika Madina kwa ajili ya kumchagua Khalifa wao?

Muombezi: Hapana. Khalifa Uthman alikuwa bado ni Khalifa. Wawakilishi wa mengi ya makabila na koo kubwa za Kiislamu walikusanyika mjini Madina kulalamika juu ya ukatili wa magavana wa Banu Umayya, maofisa wao na watu wengine mashuhuri wa baraza lao, kama Marwan. Matokeo ya Ijma hii ilkuwa kwamba Uthman, ambaye aling’ang’ania katika sera zake za ukandamizaji, aliuawa.

Ilikuwa ni baada ya kadhia hii kwamba watu wa Madina walimfuata Ali na kwa msisitizo wa maombi na kumsihi kwingi walimleta msikitini, ambako watu wote walikula kiapo cha utii kwake. Makubaliano ya pamoja, ya hadharani kama hayo, hayajawahi kufanyika kwenye ukhalifa wowote katika makhalifa watatu wa kwanza. Watu wa Madina na viongozi wa nchi mbalimbali walikula kiapo cha utii kwa mtu makhususi na wakamkubali kama Khalifa wao.

Msingi Halisi Wa Ukhalifa Wa Ali Sio Ijmai Bali Ni Matangazo Ya

Mtukufu Mtume

Lakini licha ya Ijmai hii iliyofanywa kwa ajili Amirul-Mu’minin, hatuifikirii kama msingi wa Ukhalifa wake. Kuhalalisha ukhalifa wake tunategemea tu juu ya Qur’ani Tukufu na maamrisho ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Ilikuwa ni kawaida ya mitume kwamba wao wenyewe, kulingana na amri ya Allah, waliwateua warithi na makhalifa.

Umesema kwamba hakuna tofauti kati ya Amirul-Mu’minin na makhalifa wengine. Na bado kuna dalili nyingi kwamba kulikuwa na tofauti kubwa kati ya Ali na makhalifa wengine.

Ali Alikuwa Mbora Kuliko Wale Makhalifa Wengine Wote

Sifa ya kwanza ya Amirul-Mu’minin ambayo imemfanya dhahiri kuwa yeye ni mbora zaidi kuliko makhalifa wengine wote ilikuwa kwamba yeye aliteuliwa na Allah na Mtume Wake kuwa mrithi wa Mtume.
Mwengine wote wamechaguliwa na vikundi vidogo vya watu. Ni dhahiri kwamba Khalifa aliyeteuliwa na Allah na Mtume Wake lazima awe bora kuliko wale ambao wamechaguliwa na watu.

Kama mambo yalivyo, sifa mashuhuri zaidi ya Amirul-Mu’minin ilikuwa ni ubora wake wa elmu, maadili, na uchamumgu. Maulamaa wote wa umma (isipokuwa wafuasi wachache tu wa Abu Bakr wa ki-Khawarij na Nasibi) wanakubaliana wote kwa pamoja katika maoni yao kwamba, baada ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), Ali anawapita wengine wote katika ilmu, uadilifu, haki, utukufu, na uchamungu. Katika kuunga mkono jambo hili huko nyuma nilinukuu idadi ya hadithi na aya kutoka kwenye Qur’ani Tukufu. Sasa nimekumbuka tena hadithi nyingine tena bado, kuhusiana na nukta hii.

Hadithi Ya Mtukufu Mtume (S.A.W.W.) Kuhusu Ubora Wa Ali

Imam Ahmad Bin Hanbal katika Musnad, Abu’l-Mu’ayyid Muwaffaq Ibn Ahmad Khawarizmi katika sura ya nne ya Manaqib, Mir Seyyid Ali Hamadani Shafi’i katika Mawaddatu’l-Qurba, Hafidh Abu Bakr Baihaqi Shafi’i katika Sunan, na wengine wengi wamesimulia kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa tofauti kidogo ya maneno na tafsiri kwamba alisema: “Ali miongoni mwenu ndiye mwanachuoni msomi zaidi, muadilifu zaidi, na hakimu bora zaidi.

Yule ambaye anakataa kauli zake, kitendo chake au maoni yake, kwa kweli ananikataa mimi. Yule ambaye atanikataa mimi, anamkataa Allah, na yuko ndani ya mipaka ya ushirikina.”

Aidha, Ibn Abi’l-Hadid Mu’tazali, ambaye ni mmoja wa maulamaa wenu mashuhuri, ameandika kwenye sehemu nyingi katika Sharh-e- Nahju’l-Balagha kwamba ubora wa Amirul-Mu’minin Ali ilikuwa ni imani ya masahaba wengi na wafuasi. Masheikh (Machifu) wa Baghdad vile vile walilikubali hilo.

Muombezi: Je, unaweza kunifahamisha tafadhali, unachochukulia kuwa ni nemsi katika mtu ambazo humfanya kuwa bora kuliko wote?

Sheikh: Kwa kweli kuna nemsi na tabia nzuri nyingi ambazo zaweza kustahili ubora kuloko nyingine, lakini katika maoni yangu sifa zenye kustahiki zaidi baada ya kuamini katika Allah na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ni hizi:

(1) Ukoo safi
(2) Ilmu
(3) Uchamungu.

Muombezi: Allah akubariki! Nitafungia mjadala wangu kwenye nukta hizi tatu.

Bila shaka kila sahaba, iwe alikuwa ni Khalifa au la, alikuwa na sifa fulani bainifu. Lakini wale ambao walikuwa na nemsi hizi walikuwa ndio haswa wabora kuliko wengine.

Kama nitathibitisha kwamba katika sifa hizi tatu ni Amirul-Mu’minin Ali ambaye anawazidi wengine wote, basi lazima ukubali kwamba mtu huyu mtakatifu alikuwa ni mdai mstahiki wa ukhalifa. Na kama alikoseshwa ukhalifa ni kwa sababu ya hila za kisiasa.

Kizazi Safi Halisi Cha Ali

Katika suala la kizazi ukimuondoa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), hakuna mtu anayeweza kulinganishwa na Ali. Hata baadhi ya maulamaa washupavu wa madhehebu yenu, kama Ala’u’d-Din Mulla Ali Bin Muhammad Ushji, Abu Uthman Amr Bin Bahr Jahiz Nasibi, na Sa’idu’d-din Mas’ud Bin Umar Taftazani wamesema: “Tunayastahi sana maneno ya Ali ambaye amsema: ‘Sisi ni Ahlul’l-Bayt wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). hakuna anayeweza kulingana na sisi.’”

Vile vile, katika khutba ya pili ya Nahju’l-Balagha, mtukufu Imam baada ya kukubali ukhalifa alisema: “Hakuna mtu katika umma huu anayeweza kulingana na familia ya Muhammad. Inawezekanaje wale ambao wamepokea rehema, ilmu, na upole kutoka kwao walingane nao? Wao ni msingi wa dini na nguzo za imani.

Wale ambao wanapotoka kutoka kwenye njia ya haki hugeukia kwao, na wale ambao wanakawia nyuma, hupiga hatua mbele kujiambatanisha kwao. Wao peke yao wana haki ya pekee ya uandamizi na Uimam.

Ilikuwa ni kwa ajili yao peke yao kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alifanya wosia wake. Walikuwa ni warithi wake wa haki. Sasa haki imerudi kwa mdai wake halali na tena ime- fikia sehemu ambayo kwamba ilikuwa imeondolewa.”

Maelezo haya ya Amirul-Mu’minin kuhusu madai yake la ukhalifa ni uthibitisho mzuri juu ya haki yake kwenye ukhalifa.

Lakini maneno haya hayakutamkwa na Amirul-Mu’minin peke yake. Hata wapinzani wake wamekiri kitu hicho hicho. Nilionesha katika usiku uliopita kwamba Mir Seyyid Ali Hamadani anasimulia katika Mawaddatu’l-Qurba, Mawadda ya 7, kutoka kwa Abi Wa’il, ambaye anasimulia kwamba Abdullah Bin Umar alisema: “Katika kuwaonesha masahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), tulitaja majina ya Abu Bakr, Umar na Uthman.

Mtu mmoja akauliza liko wapi jina la Ali? Sisi tukasema, ‘Ali anatoka na Ahlu’l-Bayt ya Mtume, na hakuna mtu yeyote anayeweza kulinganishwa na yeye. Yuko pamoja na Mtukufu Mtume wa Allah (s.a.w.w.) katika daraja mmoja (isipokuwa utume).’”

Vile vile yeye anasimulia kutoka kwa Ahmad Bin Muhammad Kurgi Baghdadi, ambaye alisema kwamba Abdullah Bin Ahmad Hanbal (mtoto wa Imam wa madhehebu ya Hanbali) alimuuliza baba yake kuhusu ubora wa masahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), ailimtaja Abu Bakr, Umar na Uthman.

Kisha akamuuliza ni nini anachofikiria kuhusu Ali Bin Abi Talib. Ahmad Bin Hanbal akasema, “Anatokana na Ahlu’l-Bayt. Watu wengine hawawezi kulinganishwa naye.”

Amma kwa ukoo wa Ali, una vipengele viwili: kimoja cha nuru na kimoja cha mwili. Hivyo kulingana na hili Ali alikuwa na daraja ya pekee baada ya Mtukufu Mtume wa Allah (s.a.w.w.).

Kuumbwa Kwa Ali Kutokana Na Nuru, Na Uhusiano Wake Na Mtukufu Mtume

Kutokana na mtazamo wa nuru, Amirul-Mu’minin alichukua nafasi ya juu kabisa, kama ambavyo maulamaa wenu wengi mashuhuri wanavyoonesha. Imam Ahmad Bin Hanbal katika Musnad yake, Mir Seyyid Ali Hamdani Faqih Shafi’i katika Mawaddatu’l-Qurba; Ibn Maghazili Shafi’i katika Manaqib yake na Muhammad Bin Talha Shafi’i katika Matalibus-Su’ul fi Manaqib-e-alu’r-Rasul wanasimulia kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwamba alisema: “Mimi na Ali Bin Abi Talib wote tulikuwa nuru moja mbele ya Allah miaka 14,000 kabla ya kuumbwa Adam. Wakati alipomuumba Adam, aliiweka nuru ile kwenye kiuno cha Adam.

Tulibakia pamoja kama nuru mmoja mpaka pale tulipotengana katika kiuno cha Abu’l-Muttalib. Kisha nilipewa Utume na Ali akapewa Ukhalifa.”

Mir Seyyid Ahmad Ali Hamdani Faqih Shafi’i katika Mawaddatu’l-Qurba, Mawadda ya 7, anaitaja nukta hii: “Ali na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wanatokana na nuru moja. Ali alijaaliwa na sifa kama vile ambavyo hakupewa mtu yeyote mwingine katika ulimwengu wote.”

Miongoni mwa hadithi ambazo zimeandikwa katika Mawadda hii kuna riwaya kutoka kwa Khalifa wa tatu, Uthman Bin Affan, ambaye alisema kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Mimi na Ali tuliumbwa kutokana na nuru mmoja miaka 14,000 kabla ya kuumbwa kwa Adam. Wakati Allah alipomuumbwa Adam, aliiweka nuru ile katika kiuno cha Adam.

Tulibakia kama nuru mmoja mpaka tulipotenganishwa katika kiuno cha Abdu’l- Muttalib. Kisha nilipewa Utume na Ali akapewa uandamizi.”

Katika hadithi nyingine anaandika kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), wakati akimzunguzisha Ali, alisema: “Hivyo Utume na Unabii ukaja kwangu. Uandamizi (ushikamakamu) na Uimam ukaja kwako wewe Ali.”
Hadithi hiyo hiyo ilisimuliwa na Ibn Abi’l-Hadid Mu’tazali katika Sharh-e-Nahju’l- Balagha, Jz. 2, uk. 450 (chapa ya Misir) kutoka kwa mwandshi wa Kita-e-Firdaus. Vile vile Sheikh Sulayma Balkhi katika Yanabiu’l-Mawadda, sehemu ya 1, anasimulia kutoka Jam’u’l-Fawa’id, Manaqib ya Ibn Maghazili Shafi’i, Firdaus ya Dailami, Fara’idus- Simtain ya Hamwaini na Manaqib ya Khawarizmi, pamoja na tofauti kidogo katika maneno lakini sio katika madhumuni, kwamba Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w.) na Ali waliumbwa kutokana na nuru maelfu ya miaka kabla ya kuumbwa kwa ulimwengu na kwamba wote kwa pamoja walikuwa nuru moja mpaka walipotengenishwa katiki kiuno cha Abdu’l-Muttalib. Sehemu moja iliwekwa katika kiuno cha Abdullah na kutokana nayo alizaliwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Sehemu nyingine iliwekwa kwenye kiuno cha Abu Talib na kutokana nayo alizaliwa Ali. Muhammad aliteuliwa kuwa Mtume na Ali kuwa mwandamizi, kama ilivyoelezwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mwenyewe.

Abu’l-Mu’ayyid Mu’affaq Bin Ahmad Khawarizmi na wengine wengi wamesimulia kutoka vyanzo vya kuaminika kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Mimi na Ali tumezaliwa kutokana na nuru moja. Tulibakia pamoja mpaka tukafikia kwenye kiuno cha Abdu’l-Muttalib ambamo tulitenganishwa.”

Kizazi Cha Kimaumbile Cha Ali

Kwa kadiri ambavyo uumbaji wa kimwili wa Ali unavyohusika, ni dhahiri ulikuwa ni wa daraja ya juu kwa pande zote, kikeni na kiumeni. Wahenga wake wote waliotangulia mpaka kufikia kwa Adam mwenyewe walikuwa ni wenye kumuabudu Allah.

Kamwe nuru hii haijatua katika kiuno au tumbo chafu la uzazi. Hakuna yeyote miongoni mwa masahaba anayeweza kutoa madai kama haya. Nasaba ya Ali ni kama ifuatavyo:

(1) Ali Bin (2) Abu Talib Bin (3) Abdu’l-Muttalib (4) Hashim (5) Abd-e-Manaf (6) Qusai (7) Kilab (8) Murra (9) Ka’b (10) Luwai (11) Ghalib (12) Fihr (13) Malik (14) Nazir (15)Kinana (16) Khazima (17) Mudrika (18) Ilyas (19) Muzar (20) Nizar (21) Ma’d (22) Adnan (23) Awwad (24) Al-Yasa (25) Al-Hamis (26) Bunt (27) Sulayman (28) Haml (29) Qidar (30) Isma’il (31) Ibrahim Khalil-Ullah (32) Ta’rikh (33) Tahur (34) Sharu (35) Abraghu (36) Taligh (37) Abir (38) Shale’ (39) Arfakhad (40) Sam (41) Nuh (42) Lumuk (43) Mutu Shalkh (44) Akhnukh (45) Yarad (46) Mahla’il (47) Qinan (48) Anush (49) Seth (50) Adam Abu’l-Bashir.

Isipokuwa kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) tu, hakuna mwingine yeyote aliyekuwa na ukoo safi kama huu.

Baba Yake Ibrahim Alikuwa Ni Azar!!

Sheikh: Umesema kwamba wahenga wote wa Ali walikuwa wanaamini Mungu Mmoja. Nadhani umekosea. Baadhi ya wahenga wake walikuwa ni waabudu masanamu. Kwa mfano baba yake Ibrahim Khalilullah, Azar, aliabudu masanamu. Qur’ani Tukufu kwa uwazi inasema: “Na wakati Ibrahim alioposema kumuambia baba yake, Azar: je, mnayafanya masanamu kama miungu? Hakika nakuona wewe na watu wako katika upotofu ulio dhahiri.”

Muombezi: Unarudia yale waliyoyasema wakubwa zako, ingawa unajua kwamba wanachuoni wa nasaba kwa pamoja wote wanakubaliana kwamba baba yake Ibrahim alikuwa ni Ta’rukh, na sio Azar.

Sheikh: Lakini hii ni Ijtihad (hoja inayotegemea juu ya uamuzi wako mweyewe) mbele ya amri ya kimungu.
Unaweka mbele mitazamo ya wanachuo wa nasaba katika kupingana na Qur’ani Tukufu, ambayo kwa uwazi inasema baba yake Ibrahim ni Azar, ambaye alikuwa muabudu sanamu.

Muombezi: Kamwe sibishani kwa kupingana na sheria ya ki-Mungu. Nia yangu ni kuta- ka kujua tafsiri halisi ya Qur’ani. Ili kufanikisha hili natafuta mwongozo kutoka kwa wale ambao wako sawa na Qur’ani Tukufu kama vyanzo vya mwongozo, nao ni Ahlu’l-Bayt wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Neno hili katika aya hii tukufu limetumika katika maana ya jumla, kwa sababu katika maana ya jumla hata ami na mume wa mama vile vile huitwa ‘baba.’
Kuna mitazamo miwili katika suala la Azar. Moja ni kwamba alikuwa ni ami yake Ibrahim na wa pili ni kwamba zaidi ya kuwa ami yake, baada ya kufa baba yake Ibrahim (Tarukh), Azar alimuoa mama yake Ibrahim. Kwa hiyo Ibrahim alikuwa akimwita yeye ni baba yake kwa vile alikuwa ni ami yake na halikadhalika ni mume wa mama yake.

Sheikh: Hatuwezi kupuuza maana ya wazi ya Qur’ani Tukufu, mpaka tuone maana yake nyingine katika Qur’ani yenyewe, ikionesha kwa uwazi kwamba ami au mume wa mama vile vile huitwa ‘baba’. Kama ukishindwa kuonesha ushahadi kama huo (na kwa hakika utashindwa), hoja yako haitakubaliwa.

Muombezi: Kuna mifano katika Qur’ani ambako maneno yametumika katika maana yao ya jumla. Kwa mfano, Aya ya 133 Sura ya 2, Al-Baqarah, Qur’ani Tukufu inaunga mkono nukta yangu. Inaandika maswali na majibu ya Mtume Ya’akub na wanawe wakati wa kifo chake. Inasema:

أَمْ كُنْتُمْ شُهَدَاءَ إِذْ حَضَرَ يَعْقُوبَ الْمَوْتُ إِذْ قَالَ لِبَنِيهِ مَا تَعْبُدُونَ مِنْ بَعْدِي قَالُوا نَعْبُدُ إِلَٰهَكَ وَإِلَٰهَ آبَائِكَ إِبْرَاهِيمَ وَإِسْمَاعِيلَ وَإِسْحَاقَ إِلَٰهًا وَاحِدًا وَنَحْنُ لَهُ مُسْلِمُونَ {133}

“Aliposema kuwaambia watoto wake: mtaabudu nini baada yangu? Wakasema: tutamuabudu Mungu wako na Mungu wa baba zako, Ibrahim na Isma’il na Is’haq, Mungu Mmoja tu, na kwake tunajisalimisha.” (2:133)

Katika Aya hii uthibitisho wa dai langu ni neno Isma’il. Kwa mujibu wa Qur’ani, baba yake Ya’kub alikuwa ni Is’haq na Isma’il alikuwa ni ami yake, lakini, kwa mujibu wa matumizi ya kawaida, alizoea kumuita baba yake. Kwa vile watoto wa Ya’kub vile vile kwa mujibu wa matumizi ya kawaida, walimuita ami yao baba yao, walitumia neno hilo hilo katika kumjibu baba yao.

Mungu alijulisha swali na jibu lao kama ilivyokuwa. Halikadhalika, Ibrahim vile vile alizoea kumuita ami yake na mume wa mama yake ‘baba’, ingawa kwa mujibu wa ushahidi wenye nguvu wa kihistoria na maelezo ya kinasaba, ni jambo linalokubalika kwamba baba yake Ibrahim hakuwa ni Azar, bali ni Tar’ukh.

Baba Na Mama Zake Mtukufu Mtume Hawakuwa Washirikina Bali

Walikuwa Wote Ni Waumini

Ushahidi wa pili wa ukweli kwamba wahenga wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hawakuwa washirikina na makafiri ni Aya ya 219 Sura ya 26; Surat Shu’ara:“Na mageuko yako (ya kuinama na kuinuka na kusimama katika Sala) katika wale wanaosujudu.” (26:219)

Kuhusu maana ya Aya hii tukufu Sheikh Sulayman Balkhi Hanafi katika Yanabiu’l- Mawadda, Jz. 2, na wengine wengi katika maulamaa wenu wamesimulia kutoka Ibn Abbas, ambaye alisema:

“Allah alihamisha chembe chembe za uhai wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kutoka kwenye kiuno cha Adam kwenda kwa mitume waliofuatia mmoja baada ya mwingine, ambao wote walikuwa wanaamini Mungu Mmoja, mpaka alipomfanya atokeze kutoka kwenye kiuno cha baba yake kupitia kwenye ndoa na sio kupitia njia ya haramu.”

Vile vile kuna hadithi mashuhuri sana ambayo maulamaa wenu wote wameisimulia. Hata Imam Tha’labi, ambaye anaitwa Imam wa hadithi, anaandika katika kitabu chake cha tafsiri na Sulaman Balkhi Hanafi katika kitabu chake Yanabiu’l-Mawadda, Jz. 2, anasimulia kutoka kwa Ibn Abbas, kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Allah alinipele- ka duniani katika kiuno cha Adam na akanihamishia kwenye kiuno cha Ibrahim.

Aliendelea kunihamisha kutoka kwenye viuno mashuhuri na vitukufu kwenda matumbo (ya kina mama) safi mpaka aliponiumba kutoka kwa baba yangu na mama yangu, ambao kamwe hajakutana kiharamu.”

Katika hadithi nyingine inasimuliwa kwamba alisema: “Kamwe Allah hakunichanganya mimi na elementi yoyote ya ujinga.”

Katika sura hiyo hiyo, Sulayman Balkhi anasimulia kutoka Ibkaru’l-Afkar kitabu cha Sheikh Salahu’d-din Bin Zainu’d-din Bin Ahmad ajulikanaye kama Ibnus-Sala Halbi na kutoka kwenye Sharh-e-Kibrit-e-Ahmar ya Sheikh Abdu’l-Qadir akisimulia kutoka kwa Ala’u’d-Dowlat Semnani hadithi yenye maelezo ya kinaganaga kutoka kwa Jabir Ibn Abdullah kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliulizwa kuhusu Allah alichoumba kwanza. Alijibu swali hilo kwa maelezo marefu ambayo siwezi kuyasimulia kwa wakati huu.

Kuelekea mwishoni mwa hadithi hiyo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Halikadhalika, Allah aliendelea kuhamisha nuru yangu kutoka upande safi kwenda upande safi, mpaka aliponiweka kwa baba yangu, Abdullah Bin Abdu’l-Muttalib. Kutoka hapo Alinipeleka kwenye tumbo la mama yangu, Amina. Kisha alinifanya nitokeze katika ulimwengu huu, na akanipa cheo cha Sayidu’l-Mursalin (bwana wa Mitume) na Khatamu’n-Nabiyyin (Muhuri au Mwisho wa Mitume).”

Maelezo ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwamba aliendelea kuhamishwa kutoka mtu safi kwenda mtu safi yanathibitisha kwamba hakuna yeyote katika wahenga wake aliyekuwa kafiri. Kwa mujibu wa Qur’ani Tukufu: “…Hakika washirikina ni najisi…” (9:28) kila kafiri na mshirikina ni najisi.

Alisema kwamba alihamishwa kutoka matumbo safi kwenda matumbo safi - ya uzazi. Kwa vile waabudu masanamu ni najisi, hivyo hii ina maana kwamba hakuna yeyote katika wahenga wake aliyekuwa muabudu sanamu.
Katika sura hiyo hiyo ya Yanabiu’l-Mawadda moja hadithi kutoka Ibn Abbas inasimuliwa kupitia Kabir kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Sikuzaliwa kupitia ndoa ya haramu ya siku za ujahiliya. Nilizaliwa kupitia njia za Kiislamu za Nikah (ndoa).”

Je, hukusoma khutba ya 105 katika Nahju’l-Balagha? Amirul-Mu’minin anasema kuhusu wahenga wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). “Allah aliwapa (yaani mitume) sehemu bora (viuno vya wahenga wao) na matumbo safi ya uzazi ya mama zao. Aliwahamisha kutoka kwenye viuno maarufu na vyenye kuheshimiwa kwenda kwenye matumbo safi ya uzazi.

Wakati baba wa yeyote kati yao alipofariki, mtoto wake alimrithi yeye pamoja na dini ya Allah, mpaka Allah Mwenye nguvu zote alipomfanya Muhammad kuwa Mtume na Mjumbe Wake, hivyo alifanya chanzo cha uumbwaji wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kuwa kilichotukuka mno zaidi. Nasaba ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ilijumuisha Mitume Wake swt. ambao walikuwa wa daraja za juu kabisa.”

Kwa ufupi, wahenga wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kurudi nyuma mpaka kwa Nabii Adamu walikuwa waumini na wenye kuabudu Mungu Mmoja. Hivyo, ni dhahiri kabisa kwamba watu wa Ahlu’l-Bayt ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) walijua zaidi kuhusu hadhi ya wahenga wao kuliko wengine.

Wahenga Wa Ali Vivyo Hivyo Waliepukana Na Ushirikina

Wakati imethibitika kwamba wahenga wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) walikuwa waumini na waabubu Mungu mmoja, bila shaka kabisa ina maana kwamba wahenga wa Ali vile vile walikuwa ni wenye kumuabudu Allah. Nimekwisha thibitisha kupitia kwenye vitabu vyenu wenyewe kwamba Muhammad na Ali wanatokana na nuru moja na wakati wote walibakia pamoja kwenye viuno na matumbo safi ya uzazi mpaka walipotenganishwa katika kiuno cha Abdu’l-Muttalib. Kila mtu mwenye busara atakiri kwamba mtu mashuhuri kama huyo alikuwa ni mdai wa haki wa ukhalifa.

Kutoeleweka Kuhusu Imani Ya Abu Talib Kwafafanuliwa

Sheikh: Naukubali ukweli kwamba Tarukh alikuwa baba yake Ibrahim, na umethibitisha utohara wa wahenga wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). lakini haiwezekani kupata ushahidi kama huo katika suala la Ali. Hata kama tukikubali kwamba wahenga wake wote kuanzia juu mpaka kwa Abdu’l-Muttalib walikuwa ni waabudu Mungu Mmoja, baba yake, Abu Talib, kwa hakika aliutoka ulimwengu huu akiwa ni kafiri.

Muombezi: Nakubali kwamba kuna tofauti ya maoni miongoni mwa umma kuhusu imani ya Abu Talib. Lakini tunapaswa kusema: Ewe Allah! Mlaani dhalimu wa kwanza ambaye alionesha udhalimu kwa Muhammad na ulaani na kizazi chake.

Laana ya Allah iwe juu ya yule ambaye alibuni hadithi ambazo matokeo yake ni kwamba Nasib na Khawariji walianza kudai kwamba Abu Talib alifariki dunia akiwa kafiri. Maulamaa wa Shi’a kwa ujumla na watu wote wa familia ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wanaamini katika imani ya Abu Talib. Ve vile, wengi wa wanachuo wenu na maulamaa wasiopendelea upande wowote, kama vile Abi’l-Hadid, Jalalu’d-Din Sututi, Abu’l-Qasim Balkhi, Abu Ja’far Askafi, walimu wao kutoka madhehebu ya Mu’tazali, na Mir Seyyid Ali Hamadani Faqih Shafi’i - wote wanakubaliana kwamba Abu Talib alikuwa ni Mwislamu.

Ijmai Ya Shia Kuhusiana Na Imani Ya Abu Talib

Shia wanaamini kwamba, kuanzia mwanzo kabisa Abu Talib alimwamini Mtukufu Mtume. Shia wanaowafuata Ahlu’l-Bayti wanakiri kwa kauli moja “Abu Talib kamwe hajaabudu masanamu; alikuwa ni mmoja kati ya warithi wa Ibrahim.” Mtazamo huo huo umeoneshwa pia katika vitabu sahihi vya maulamaa wenu wenyewe. Kwa mfano, Ibn Athir anasema katika kitabu chake Jam’u’l-usul: “Kwa mujibu wa Ahlu’l-Bayti tukufu, miongoni mwa ami zake wote Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), ni Hamza, Abbas, na Abu Talib tu walioukubali Uislamu.

Makubaliano ya pamoja ya watukufu Ahlu’l-Bayti kuhusiana na nukta yoyote, lazima ichukuliwe kama yenye maamuzi. Hadithi ya Thaqalain na hadithi nyingine ambazo nimezitaja kakita mikesha iliyopita zinathibitisha wazi kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alitoa maelezo ya wazi kuhusiana na uma’asum wa familia yake.

Walikuwa sambamba na Qur’ani Tukufu na moja ya Thaqalain (vizito viwili) ambavyo Mtume aliviacha kama vyanzo vya mwongozo usio na dosari kwa ajili ya watu wake. Ni muhimu kwamba Waislamu wote wavifuate ili kwamba wasipotoshwe.

Pili, kwa mujibu wa msemo “Watu wa nyumba wanajua vizuri kuhusu masuala ya familia”, familia hii iliyotukuka walijua zaidi kuhusu imani ya wahenga wao kuliko Mughira Bin Sha’ba, Banu Umayya, Khawarij na Nasib au watu wengine wasio na ujuzi.

Kwa hakika inashangaza kwamba maulamaa wenu hawakubali maelezo ya Ahlu’l-Bayti wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), pamoja na Amir wa waumini, ambaye kwamba unyofu na uaminifu wake umethibitishwa na Allah na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Wote wanasema kwamba Abu Talib alikufa akiwa muumini. Hamuamini hilo, lakini mnakubali maneno ya Mughira, muongo na muovu aliyethibitishwa, na baadhi ya Amawi, Khawarij na Nasib.

Ibn Abi’l-Hadid Mu’tazali, ambaye ni mmoja wa maulamaa wenu mwenye sifa, anasema katika Sharh-e-Nahju’l-Balagha, Jz. 3, uk. 310: “Kuna tofauti ya maoni kuhusu Uislamu wa Abu Talib. Madhehebu ya Imamiyya (Shi’a) na wengi katika Zaidiyya wanasema kwamba aliutoka ulimwengu huu akiwa Mwislamu. Mbali na maulamaa wote wa Shia, baadhi ya maulamaa wetu wakubwa kama Abu’l-Qasim Balkhi na Abu Ja’far Askafi mtazamo wao ni kwamba Abu Talib aliukubali Uislamu, lakini hakuonesha imani yake ili kwamba aweze kumpa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) msaada kamili, na kwa sababu ya ushawishi wake (Abu Talib), wapinzani wasiweze kuzuia njia ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Kuelewa Vibaya Kuhusu Hadithi Ya Kubuni Ya Zuhzah Kwafafanuliwa

Sheikh: Kwa dhahiri wewe huijui ile “hadithi ya Zuhzah” ambayo inasema: “Abu Talib yuko kwenye moto wa Jahannam.”

Muombezi: Hii ni hadithi ya kughushi iliyozushwa wakati wa kipindi cha Mu’awiyya Bin Abu Sufian na baadhi ya maadui wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Baadae Bani Umayya na wafuasi wao waliendeleza juhudi zao za kughushi hadithi dhidi ya Ali Bin Abi Talib na kuzisambaza miongoni mwa watu. Hawakuruhusu imani ya Abu Talib kujulikana kama ile ya Hamza na Abbas. Mghushaji wa hadithi ya Zuhzah alikuwa ni Mughira, ambaye alikuwa muovu na adui wa Amir wa waumini, Ali Bin Abi Talib. Ibn Abi’l-Hadid katika Sharhe-e-Nahju’l-Balagha, Jz. 3, uk. 159-163; Mas’ud katika Muruju’z-Dhahab na maulamaa wengine wanaadika kwamba Mughira alifanya uzinifu huko Basra.

Wakati mashahidi wake walipoletwa mbele ya Khalifa Umar, watatu walitoa ushahidi dhidi yake, lakini wa nne alifundishwa kusema vitu ambavyo vilifanya ushahidi wake usikubalike. Kwa hiyo, mashahidi wale watatu walipewa adhabu, na Mughira aliachiwa huru.

Mtunzi wa hadithi hii hata hivyo, alikuwa mzinifu na mlevi ambaye adhabu iliyowekwa na dini ilikuwa karibu itekelezwe juu yake. Alibuni hadithi kwa sababu ya upinzani wake kwa Amir wa waumini, Ali Bin Abi Talib na kumfurahisha Mu’awiya. Mu’awiya na wafuasi wake na Bani Umayya wengine waliimarisha hadithi hii ya uwongo na wakaanza kushuhudia kwamba “Abu Talib yuko katika moto wa Jahannam.” Aidha, wale ambao wameunganishwa na hadithi hii kama Adu’l-Malik Bin Umar, Abdu’l-Aziz Rawandi na Sufyan Thawri, ni wasimuliaji dhaifu na wasio kubalika.

Ukweli huu ulifafanuliwa na mfasir na mwanachuoni wenu mashuhuri Zahri, ambaye amelezea mtazamo huu katika kitabu chake Mizanu’l-Itidali, Jz. 2. Hivyo basi, ni vipi mtu atategemea juu ya hadithi kama hii, ambayo alisimuliwa na watu waongo na wasimuliaji wenye sifa mbaya kama hawa?

Ushahidi Juu Ya Imani Ya Abu Talib

Kuna ushahidi mwingi wa kuthibitisha imani ya Abu Talib:

(1) Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anasema katika hadithi moja: (akiunganisha vidole vyake viwili) “Mimi na mwenye kumsaidia yatima wako pamoja katika Pepo kama vidole hivi viwili.” Ibn Abi’l-Hadid vile vile ameisimulia hadithi hii katika Sharh-e-Nahju’l-Balagha yake, Jz. 4, uk. 312, anaandika kwamba, ni wazi kwamba katika kauli hii ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) haimaanishi wenye kuwasidia mayatima wote, kwa vile wengi wa wanao wasaidia mayatima ni wenye dhambi.

Hivyo, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa hadithi hii alimaanisha Abu Talib na babu yake maarufu, Abdu’l-Muttalib, ambao walimlea Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) huko Makka alikuwa akijulikana kama yatima wa Abu Talib kwa sababu baada ya kufariki kwa Abdu’l-Muttalib, Mtume, kuanzia umri wa miaka nane alikuwa katika uangalizi wa Abu Talib.

(2) Kuna hadithi mashuhuri sana ambayo Shia na Sunni wameisimulia katika njia tofauti. Baadhi yao wanasema kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Jibrail alikuja kwangu na akanipa habari njema katika maneno haya: ‘Allah ameviepusha na moto viuno ambavyo kwavyo umetokea, tumbo lililokubeba, matiti yaliyokunyonyesha, na mapaja yaliyokusaidia wewe.’”

Mir Seyyid Ali Hamadani katika Mawaddatu’l-Qurba yake, Sheikh Sulaiman Balkhi Hanafi katika Yanabiu’l-Mawadda, na Qadhi Shukani katika Hadith Quds yake wamesimulia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Jibrail alikuja kwangu na akasema: ‘Allah anakutolea salamu na anasema, hakika Ameviepusha na moto viuno ambavyo vimekupa wewe hifadhi, tumbo ambalo lilihimili uzito wako, na mapaja ambayo yamkusaidia wewe.’”

Riwaya na hadithi hizi kwa uwazi zinathibitisha imani za watu ambao waliomsaidia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), yaani, Abdu’l-Muttalib, Abu Talib na mkewe Fatima Bint Asad, na vile vile baba yake baba yake Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), Abdallah, na mama yake Amina Bint Wahhab, na mama yake aliyemnyonyesha, Halima.

Beti Za Abil-Hadid Katika Kumtukuza Abu Talib

(3) Mwanachuoni wenu mkubwa, Izzu’d-din Abdu’l-Hamid Ibn Abi’l-Hadid Mu’tazali, alitunga beti zifuatazo katika kumsifia Abu Talib. Zimeandikwa katika Sharh-e-Nahju’l- Balagha, Jz. 3, uk. 318: “Bila ya Abu Talib na mwanawe (Ali Bin Abu Talib) Uislamu usingelikuwa na heshima au nguvu. Abu Talib alimlinda Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) huko Makka na akamsaidia na Ali huko Madina.

“Abd’al-Manaf (Abu Talib) kwa amri ya baba yake Abdu’l-Muttalib, aliendelea kumlea Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na Ali, na akakamilisha juhudi hizo. Wakati Abu Talib alipok- ufa kwa utashi wa Allah, haikuleta hasara yoyote kwa sababu aliacha manukato yake (Ali) kama kumbukumbu yake. Abu Talib alianzisha huduma muhimu sana katika njia ya Allah na Ali akazikamilisha kwa ajili ya Allah.
“Utukufu wa Abu Talib hauwezi kudhuriwa na kauli za kipumbavu za watu, au kwa ukandamizaji wa makusudi wa nemsi zake (unaofanywa na maadui zake), ni kama vile mtu anapouita mwanga wa mchana kuwa ni giza la usiku, mwanga huo hautadhurika chochote.”

Beti Za Abu Talib Huthibitisha Uislamu Wake

(4) Halikadhalika, beti za mashairi alizozilitunga Abu Talib mwenyewe katika kumsifia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), ni uthibitisho wa wazi wa imani yake. Baadhi ya beti hizi zimeandikwa na Abi’l-Hadid katika Sharh-e-Nahju’l-Balagha yake, Jz. 3, uk. 316. Aidha, maulamaa wenu mashuhuri kama Abu’l-Qasim Balkhi na Abu Ja’far Askafi, wamezitoa beti hizi kama ushahidi juu ya imani ya Abu Talib.

Abu Talib aliandika: “Naomba hifadhi kwa Allah kutokana na wale ambao hutushutumu sisi au kutuhusisha sisi na mwendo mbaya, kutokana na muovu anayetusema vibaya, na kutokana na mtu ambao hushirikisha vitu katika dini ambavyo tuko mbali navyo.

“Naapa kwa Nyumba ya Allah (Ka’aba),
kwamba anadanganya yule anayesema kwamba tutamuacha Muhammad,
ingawa bado hatujapigana dhidi ya maadui zake kwa panga na mikuki.
“Kwa hakika sisi tutamsaidia yeye,
mpaka tutakapo msaga adui yake. Tutajitoa mhanga kiasi kwamba,
sisi tutasahau wake zetu na watoto wetu.

“Nuru yake ni ya namna ya kiasi kwamba,
kupitia mwanga wa uso wake,
sisi tunaomba rehema za Allah kutushukia.

“Yeye anakuja kwenye kuwasaidia mayatima;
na yeye ni kimbilio la wajane.

Watu wa Bani Hashim wasiojiweza,
hukimbilia kwake kwa ajili ya kutaka msaada,
na wanabarikiwa kwa aina zote za neema.

“Naapa kwa uhai wangu kwamba,
mimi nina mapenzi makali kwa Ahmad.
Ninampenda yeye kwa mapenzi ya rafiki mkweli halisi.

“Niliiona nafsi yangu inafaa kujitoa mhanga kwa ajili yake,
hivyo nilimsaidia kwa vile ni pambo kwa watu wa dunia hii,
na ni laana kwa maadui na rehema kwa jamii.

“Namuomba Muumba wa ulimwengu amuimarishe kwa msaada Wake,
na aidhihirishe dini Yake, ambayo ni njia ya kuelekea kwa Allah,
na ambayo kwayo ndani yake hamna hata chembe ya kosa.”

Kuna baadhi ya beti maalumu za mashairi ya Abu Talib ambayo Ibn Abi’l-Hadid katika Sharh-e-Nahju’l-Balagha, Jz. 3, uk. 312, na wengine wameyanukuu mashairi hayo kwa ushahidi wa imani yake. Katika maandishi ya wasifu wake, anasema:

“Watu hawa wanatutegemea sisi tupigane dhidi ya Uislamu kwa panga na mikuki; wanafikiri tutamuuwa Muhammad. Lakini nyuso zetu bado hazijapakwa damu katika kumsaidia yeye. Naapa kwa Nyumba ya Allah (Ka’aba) kwamba mumeniambia uwongo; mnaweza kuangukia kwenye janga.

Hatim na Zamzam vyaweza kujaa mpaka kwenye midomo yao kwa vichwa vilivyokatwa. Dhulma inafanywa kwa Mtume, ambaye ametumwa na Allah kuwaongoza watu. Amepewa Kitabu, ambacho kiliteremshwa na Mola wa Mbingu.”

Mbali na ushahidi huu wa wazi, ambao unathibitisha imani ya Abu Talib, Ibn Abi’l-Hadid katika Sharh-e-Nahju’l-Balagha yake, Jz. 3, uk. 315, ananukuu beti zifuatazo: “Mnashuhudia kuwepo kwa Allah!

Shuhudieni kwamba hakika nafuata dini ya Mtume wa Allah, yaani, Ahmad. Wengine wanaweza kupotoshwa katika dini yao, lakini mimi ni mmoja wa wale ambao wameongoka.” Mabwana! Kuwenu waadilifu na mtuambie kama muandishi wa mashairi kama haya anaweza kuitwa kafiri.

Sheikh: Mashairi haya hayakubaliki kwa sababu mbili. Kwanza, hakuna mwendelezo wa hadithi kuhusu mashairi haya. Pili, hakuna popote palipoonesha kwamba Abu Talib aliukubali Uislamu. Kusimulia baadhi ya mashairi yake hakuthibitishi kwa uhakika kwamba alikuwa Mwislamu.

Muombezi: Pingamizi lako kuhusu kukosekana kwa mwendelezo wa hadithi ni la ajabu. Wakati unapotaka, unakubali riwaya ya pekee na wakati ukiwa hutaki, unatumia silaha ya ukosefu wa mwendelezo. Kama utatafakari kwa muda kwamba kama mashairi haya hayakusimuliwa kwa mwendelezo na watu, hata hivyo, yakichukiliwa kwa ujumla, yanathibitisha kwamba Abu Talib aliamini utume wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Kuna vitu vingi kama hivyo ambavyo mwendelezo wake wa hadithi huamuliwa kwa njia hii hii. Kwa mfano, vita alivyopigana Amir wa Waumini (Ali) na mifano ya ushujaa wake vile vile hutegemea juu ya riwaya za pekee. Lakini zikichukuliwa kwa ujumla taarifa hizi hujenga maana ya mwendelezo, ambao hutupa sisi elimu muhimu ya ushujaa wake. Ukarimu wa Hatim na uadilifu wa Nushirwan hujulikana kwa njia hiyo hiyo. Kwa vile wewe ni mpenzi sana wa mwendelezo, tafadhali tufahamishe ni vipi utathibitisha kwamba Hadithi ya Zuhza imewasilishwa kwa mfuatano.

Kukubali Kwa Abu Talib Imani Yake Juu Ya Allah Wakati Wa Kifo Chake

Ama kwa pingamizi lako la pili, jibu langu ni rahisi sana. Ni muhimu kuonyesha kukubali kwa mtu upweke wa Allah, utume, Siku ya Ufufuo, nk., katika nathari (lugha ya moja kwa moja isiyo ya kishairi). Lakini kama mtu akitunga mashairi ambayo kwayo anaelezea imani yake, huwa inatosha kabisa. Wakati Abu Talib aliposema: “Enyi ambao mnamumini Allah!

Shahudieni kwamba hakika mimi ninafuata dini ya Mtume wa Allah, Ahmad,” ilikuwa na athari ile ile kana kwamba ameisema katika nathari.

Mbali na hili, halikadhalika alikiri imani yake wakati wa kifo chake katika nathari vilevile. Seyyid Muhammad Rasuli Bazranji, Hafidh Abu Nu’aim, na Baihaqi wamesimulia kwam- ba kikundi cha wakuu wa Makureishi, pamoja na Abu Jahl na Abdullah Ibn Abi Umayya, walikuja kwa Abu Talib wakati alipokuwa anafariki.

Wakati huo Mtume alisema kumuambia ami yake Abu Talib: “Sema kwamba ‘hakuna mungu ila Allah,’ ili niwze kulishuhudia hilo mbele ya Allah.” Mara moja Abu Jahl na Abi Umayya walisema: “Abu Talib! Utaipa mgongo imani ya Abdu’l-Muttalib?”

Walirudia maneno haya tena na tena mpaka aliposema, “lazima muelewe kwamba Abu Talib anafuata imani ya Abdu’l-Muttalib.” Matokeo yake watu wale waliondoka pale wakiwa wamefurahi. Wakati alama za kifo zilipojitokeza juu ya Abu Talib, ndugu yake Abbas, ambaye alikuwa amekaa kwenye ukingo wa kitanda chake, aliona kwamba midomo yake ilikuwa inatikisika.

Wakati aliposikiliza alichokuwa anasema, alimsikia akisema: “Hakuna mungu ila Allah.” Abbas akamuambia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): “Ewe mpwa wangu! Naapa kwa jina la Allah kwamba ndugu yangu (Abu Talib) amesema kile ulichomuamuru kusema.” Kwa vile Abbas alikuwa bado hajaingia Uislamu wakati ule, hakuyatamka maneno hayo.

Tulithibitisha mapema kwamba wahenga wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wote walikuwa wanaamini katika upweke wa Allah (tawhid). Lazima uelewe kwamba ilikuwa ni kauli yenye kufaa kwa Abu Talib kusema kwamba anafuata imani ya Abdu’l-Muttalib. aliwaridhisha watu wale, na katika ukweli alikiri imani yake katika upweke wa Allah kwa sababu Abdu’l-Muttalib alifuata imani ya Mtume Ibrahim.

Aidha, aliyatamka haya maneno “Hakuna mungu ila Allah.” Kama unachunguza taarifa za kihistoria kuhusu Abu Talib, kwa hakika utakiri kwamba alikuwa muumini.

Mazungumzo Ya Mtukufu Mtume Na Abu Talib Wakati Wa Tangazo La

Utume Wake

Katika siku ya bi’that (kutangazwa kwa utume) Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), pamoja na ami yake Abbas, walikwenda kwa Abu Talib na akamuambia: “Hakika Allah ameniamuru mimi kutangaza amri Yake; hakika, amenifanya mimi Mtume Wake; basi wewe utanitendea vipi?”

Abu Talib alikuwa ni mkuu wa Makureishi, Kiongozi wa Bani Hashim na mtu mnyofu zaidi katika macho ya watu wa Makka. Alimlea Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Lau angekuwa kafiri mara moja angelimpinga. Na ikiwa hilo halikuthibitisha vya kutosha, kwa vile Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuja kwake kutaka msaada wa kutangaza utume wake, Abu Talib kwa kuona kwamba hiyo ilikuwa ni kinyume na dini yake, angemzuia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) au angalau angemfukuza kutoka kwenye eneo lake.

Kukataa kwa namna hiyo kungemkwaza Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kutokana na azima yake kubwa. Domo ya Abu Talib (tukichukulia kwamba ilikuwa ni ushirikina) ingeweza kuokolewa, na angeweza kupokea shukurani kutoka kwa washirika wake. Abu Talib angemkemea Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kama Azar alivyofanya kwa mpwa wake Mtume Ibrahim.

Tangazo La Ibrahim La Utume Na Mazungumzo Yake Na Azar

Katika Qur’ani Tukufu, Allah swt. anazungumzia kunyanyuliwa kwa Ibrahim Khalilu’r- Rahman kama Mtume wa Allah. Anasema kumuambia ami yake Azar: “Ewe baba yangu! Kwa yakini imenijia ilmu isiyokujia. Basi nifuate nikuongoze njia iliyo sawa. …Akasema: je! Unaichukia miungu yangu, ewe Ibrahim? Kama huachi lazima nitakupiga mawe. Na niondokee mbali, kwa muda mchache (huu)” (Qur’ani 19: 46)

Abu Talib Amhakikishia Mtukufu Mtume Msaada Kamili Na Pia Asoma Mashairi Katika Kuusifu Uislamu

Lakini kinyume chake, wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipotaka msaada wake, Abu Talib alisema: “Ewe mpwa wangu endelea na kazi ujumbe. Hakika, wewe uko juu kwa cheo, mwenye nguvu katika ukoo wako na uliye tukuka zaidi katika nasaba ya familia. Naapa kwa jina la Allah kwamba ulimi utakaozungumza vibaya juu yako utajibiwa na mimi kwa upanga mkali. Kwa jina la Allah, dunia yote ya Arabia itapiga magoti mbele yako, kama mnyama anayenyenyekea mbele ya bwana wake.”

Aidha, alitunga beti zifuatazo, akitaja ujumbe wa Mtume. beti hizi zimeandikwa na Ibn Abi’l-Hadid katika Sharh-e-Nahju’l-Balagha yake, juz. 3, uk. 306, na Sibt Jauz katika Tadhkira yake, uk. 5:

“Wallahi naapa kwamba watu wale pamoja na wafuasi wao,
kamwe hawatakufikia wewe, mpaka niwapeleke kwenye makaburi yao.

“Hivyo unaweza kuendelea kufanya kazi yako.
Mimi nakupa habari njema za mafanikio yako.
Yafanye macho yako yatulie kwayo.

“Umenilingania mimi kwenye dini yako.
Naamini umeniongoza kwenye njia iliyonyooka; hakika wewe ndiye mkweli
na wakati wote umekuwa mwaminifu.

“Umetuletea dini ambayo najua ni bora juu ya dini zote.
Kama nisingekuwa na hofu ya dhihaka na lawama,
ungeniona mimi nikikusaidia wewe kwa dhahiri kabisa.”

Mashairi haya yanaonesha kwamba Abu Talib alitambua Muhammad kwamba ni mjumbe wa Allah. Hata hivyo kuna mashairi mengine mengi kama haya ambayo Ibn Abi’l-Hadid katika Sharh-e-Nahju’l-Balagha yake na maulamaa wengi wameyaandika kwenye vitabu vyao.

Je, mtu anayesoma mashairi kama haya ni kafiri au ni muumini wa kweli?

Abu Talib Alikuwa Msaidizi Na Mlezi Wa Mtukufu Mtume

Wengi wa maulamaa wenu maarufu wamealisimulia jambo hili. Unaweza kuangalia kitabu Yanabiu’l-Mawadda cha Sheikh Sulaiman Balkhi Hanafi Sura ya 52, ambamo ndani yake imesimuliwa kutoka kwa Abu Uthman Amr Bin Bahr Jahiz kwamba, akiandika kuhusu Abu Talib alisema: “Abu Talib alikuwa ni muunga mkono wa utume na unabii wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Aliandika mashairi mengi katika kumtukuza Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Alikuwa ndiye kiongozi wa Makureishi.”

Ushahidi huu wa wazi unathibitisha unyofu wa imani ya Abu Talib. Kwa jinsi ilivyo, Bani Umayya waliwashawishi watu kumlaani kiongozi wa waaminio Mungu mmoja, Amir wa waumini, na baba wa wajukuu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), Hasan na Husein. Vile vile walibuni hadith kulaani mtukufu Imam na wakaghushi riwaya kwamba baba yake (Abu Talib), alikufa akiwa kafiri.

Msimuliaji wa riwaya hiyo alikuwa mlaaniwa Mughira Bin Sha’ba, adui wa Ali na rafiki wa Mu’awiya. Makhawarij na Manasib walieneza maoni ya kwamba Abi Talib alikuwa kafiri.

Watu wa kawaida walipotoshwa wakafanywa waamini kwamba huo ulikuwa ni mtazamo sahihi. Inashangaza kwamba walimuona Abu Sufyan, Mu’awiya na Yazid (Laana ya Allah iwe juu yao) kuwa ni waumini na Waislamu, ingawaje kuna dalili zisizo na idadi za kinyume chake. Na bado wanahusisha ukafiri kwa Abu Talib pamoja na uthibitisho wa wazi ambao unaonesha kwamba alikuwa muumini thabiti.

Sio Sahihi Kumwita Mu’awiya ‘Khalu’l-Mu’minin’

Sheikh: Je, ni sahihi kweli kwako wewe kumuita Khalu’l-Mu’minin (mjomba wa waumini), Mu’awiya Bin Abu Sufyan “kafiri” na kumlaani wakati wote? Je, utatufahamisha sisi tujue ni ushahidi gani ulionao kwamba Mu’awiya Bin Abu Sufyan na Yazid walikuwa makifiri na kustahili kulaaniwa? Watu hawa wawili maarufu walikuwa miongoni mwa makhalifa. Kusema kweli Mu’awiya alikuwa Khalu’l-Mu’minin na vile vile Khatib-e- Wahyi (mwandishi wa Wahyi).

Muombezi: Tafadhali, unaweza kunieleza ni vipi Mu’awiya amestahiki cheo cha Khalu’l-Mu’minin (mjomba wa waumini)?
Sheikh: Kwa vile dada yake Mu’wiya Ummu Habiba, alikuwa mke wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na Ummul-Mu’minin (mama wa waumini), hivyo kaka yake Mu’awiya alikuwa Khalu’l-Mu’minin.
Muombezi: Kwa maoni yako wewe, je! cheo cha Ummul-Mu’minin Aisha kilikuwa ndio kikubwa au kile cha Ummu Habiba, dada yake Mu’awiya?
Sheikh: Ingawa wote ni Ummul-Mu’minin, Aisha kwa hakika alikuwa juu kuliko Ummu Habiba.

Muombezi: Kwa mujibu wa kigezo chako, makaka wote wa wake za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ni Khalu’l-Mu’minin. Basi kwa nini humwiti Muhammad Bin Abi Bakr Khalu’l- Mu’minin? Kulingana na ninyi, baba yake alikuwa mbora zaidi kwa cheo kuliko Muawiya, na dada yake vile vile alikuwa ni mbora zaidi kwa dada yake Mu’awiya. Hapana, kuwa kwake Mu’awiya Khalu’l-Mu’minin hakuna ukweli.

Mu’awiya Alitamka Takbir Wakati Wa Kifo Cha Kishahidi Cha Imam Hasan

Abu’l-Faraj Ispahani katika Maqatilut-Talib, Ibn Abdu’l-Birr katika Isti’ab. Mas’ud kati- ka Isbatu’l-Wasiyya, na maulamaa wengine wengi wamesimulia kwamba Asma Ju’da, kwa amri na ahadi ya Mu’awiya, alimpa sumu Abu Muhammad Hasan Ibn Ali Bin Abi Talib. Ibn Abdu’l-Birr na Muhammad Bin Jarir Tabari vilevile wamesimulia kwamba wakati Mu’awiya alipojulishwa kifo cha mtukufu Imam, alipiga kelele ya takbira. Bila shaka, mtu mwenye laana kama huyo anaweza kuitwa Khalu’l-Mu’minin kwa maoni yako!

Muhammad Bin Abi Bakr Aliuawa Akiwa Na Kiu Na Kuchomwa Hadi Majivu Kwa Ajili Ya Mapenzi Ya Ahlu’l-Bayti

Lakini hebu mtazame Muhammad Ibn Abu Bakr, ambaye alilelewa na Amir wa waumini Ali Ibn Abi Talib, na alikuwa moja katika wale marafiki waaminifu wa watukufu Ahlu’l- Bayti!

Akiizungumza na familia hii maarufu anasema: “Enyi kizazi cha Fatima! Ninyi ni sehemu yangu ya usalama na ni walezi wangu. Ni kwa kupitia kwenu ninyi kwamba katika Siku ya Hukumu, umuhimu wa matendo yangu mazuri utakuwa mkubwa. Kwa vile mapenzi yangu kwenu ni ya kweli, sitajali kama mtu atabweka karibu yangu.”

Ingawa alikuwa mtoto wa Khalifa wa kwanza, Abu Bakr na kaka wa Ummul-Mu’minin, Aisha, hajaitwa Khalu’l-Mu’minin. Alitendewa vibaya na kunyimwa urithi wa baba yake!

Wakati Amr Bin Aas na Mu’awiya Bin Khadij walipoishinda Misri, walimkatia mgao wa maji Muhammad Bin Abu Bakr. Wakati alipokuwa yuko karibu kufa kwa kiu, aliuawa. Kisha alifungashwa kwenye ngozi ya punda na kutupwa kwenye moto. Wakati Mu’awiya alipofahamishwa hili alifurahi sana.

Ukisikia habari hizi, huhoji ni kwa nini watu hawa waliolaaniwa walimtendea ukatili wa namna hii mtoto wa Abu Bakr, Khalu’l-Mu’minin Muhammad Bin Abu Bakr. Lakini wakati Mu’awiya anapolaaniwa haraka sana unakasirika.

Hivyo unaona upinzani kwa kizazi cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na unaendelea mpaka leo!! Kwa vile Muhammad Bin Abu Bakr alikuwa mmoja wa marafiki wa kizazi cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), wewe hukumuita Khalu’l-Mu’minin wala kusikitia mauaji yake. Kwa vile Mu’awiya alikuwa adui mbaya kabisa wa Ahlu’l-Bayt wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) unamuita Khalu’l-Mu’minin. Allah atuokoe na upotofu huu wa kishabiki!!!

Mu’awiya Hakuwa Mwandishi Wa Wahyi Bali Wa Barua Tu

Pili, Mu’awiya hakuwa mwandishi wa Wahyi. Aliingia Uislamu katika mwaka wa kumi Hijiriyya wakati wahyi ulikuwa umekamilika. Kwa kweli yeye alikuwa mwandishi ambaye aliandika barua. Alisababisha matatizo makubwa kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). katika mwaka wa nane Hijiriyya wakati Makka iliposhindwa na Abu Sufyan akaingia Uislamu, Mu’awiya aliandika barua nyingi kwa baba yake akimlaumu kwa sababu alikuwa ameukubali Uislamu.

Hata hivyo, wakati rasi yote ya Arabia na nje ya mipaka yake ilipokuja chini ya athari za Uislamu, Mu’awiya mwenyewe alilazimika kuingia Uislamu. Kwa kufanya hivyo alipoteza hadhi yake yote.

Kisha Abbas akamuomba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ampe Mu’awiya cheo chochote ili kwamba asiweze kujisikia amadhalilika. Kwa kuzingatia pendekezo la ami yake, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimteuwa kama mwandishi kwa ajili ya kuandika barua.

Ushahidi Wa Ukafiri Wa Mu’awiya

Tatu, kuna sura nyingi za Qur’ani na hadithi ambazo zinathibitisha kwamba alikuwa kafiri anayestahili kulaaniwa.

Sheikh: Ningependa sana kusikia Sura na hadithi hizo.

Muombezi: Chache tu ya hizo zitaoneshwa. Kama nitasimulia zote, zitafanya kitabu kamili. Muslim katika Sahih yake anasimulia: Mu’awiya alikuwa mwandishi wa Mtukufu Mtume.

Mada’ini anasema: “Sa’id Bin Thabit alikuwa ndiye mwandishi wa Wahyi na Mu’awiya alikuwa akiandika barua za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa makabila mengine ya Kiarabu.”

Ushahidi Kutoka Sura Za Qur’ani Tukufu Na Hadithi Kuwa Mu’awiya Na Yazid Wamelaaniwa

(1) Tafadhali rejea aya ya 60 ya Sura ya 17 (Bani Israil). Wafasiri kutoka kwa maulmaa wenu wenyewe, kama Tha’labi, Imam Fakhru’d-din Razi, na wengine wanasema kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliona katika ndoto kwamba Bani Umayya, kama manyani walipanda na kushuka mimbari yake. Baada ya hapo Jibrail alileta aya hii: “Na tulipokuambia: Hakika Mola wako amewazunguka watu. Na hatukuifanya ndoto ile tuliyo kuonesh ila kuwajaribu watu na katikaQur’ani mti uliolaaniwa. Na tunawahadharisha lakini haiwzidishii ila uasi mkubwa tu.” (7:60)

Allah swt., Amewaita Banu Umayya, ambao viongozi wao walikuwa ni Abu Sufyan na Mu’awiya, “Mti uliolaaniwa” ndani ya Qur’ani tukufu. Mu’awiya ambaye alikuwa tawi imara la mti huu, alikuwa kwa hakika amelaaniwa.

(2) Tena Allah swt., Anasema:

فَهَلْ عَسَيْتُمْ إِنْ تَوَلَّيْتُمْ أَنْ تُفْسِدُوا فِي الْأَرْضِ وَتُقَطِّعُوا أَرْحَامَكُمْ {22}

أُولَٰئِكَ الَّذِينَ لَعَنَهُمُ اللَّهُ فَأَصَمَّهُمْ وَأَعْمَىٰ أَبْصَارَهُمْ {23}

“Na kama ninyi mkipata utawala ni karibu mtaiharibu nchi na mtaukata ujamaa wenu. Na hao ndio ambao Allah amewalaani na amewatia uziwi na amewapofusha macho yao.” (47:22-23)

Katika aya hii wale ambao wanafanya uharibifu katika nchi na kuvunja mfungamano wa undugu wanalaaniwa na Allah.

Ni nani aliyekuwa mharibifu mkubwa kuliko Mu’awiya, ambaye ukhalifa wake ulikuwa wenye sifa mbaya kwa matendo yake ya kiovu. Mbali na hili alivunja mfungamano wa undugu.

(3) Vile vile Allah Ansema katika Qur’ani Tukufu:

إِنَّ الَّذِينَ يُؤْذُونَ اللَّهَ وَرَسُولَهُ لَعَنَهُمُ اللَّهُ فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ وَأَعَدَّ لَهُمْ عَذَابًا مُهِينًا {57}

“Kwa hakika wale wanaomuudhi Allah na Mtume Wake, Allah amewalaani katika dunia na akhera, na amewaandalia adhabu yenye kufedhehesha.” (33:57)

Kwa hakika kumtesa Amir wa waumini na wajukuu wawili wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) Hasan na Husein halikadhalika na Ammar Yasir na masahaba wengine maarufu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ilikuwa ni sawa sawa na kumtesa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mwenyewe.

Kwa vile Mu’awiya aliwatesa watu hawa wachamungu, kwa mujibu wa maneno ya wazi ya aya hii alikuwa kwa hakika aliye laaniwa katika dunia hii na katika akhera.

(4) Katika sura Mu’min, Anasema:

يَوْمَ لَا يَنْفَعُ الظَّالِمِينَ مَعْذِرَتُهُمْ ۖ وَلَهُمُ اللَّعْنَةُ وَلَهُمْ سُوءُ الدَّارِ {52}

“Siku ambayo hautawafaa madhalimu udhuru wao, na watapata laana na makazi yao yatakuwa mabaya.” (40:52)

(5) Katika sura Hud, Anasema:

أَلَا لَعْنَةُ اللَّهِ عَلَى الظَّالِمِينَ {18}

“…Sasa kwa hakika laana ya Allah iko juu ya madhalimu.” (11:18)

(6) Katika sura Al-A’raf, Allah anasema:

فَأَذَّنَ مُؤَذِّنٌ بَيْنَهُمْ أَنْ لَعْنَةُ اللَّهِ عَلَى الظَّالِمِينَ {44}

“…Mara mtangazaji atatangaza baina yao kwamba laana ya Allah iko juu ya mad- halimu.” (7:44)

Halikadhalika, katika aya nyingine nyingi zilizoteremshwa kuhusu watu madhaalimu, ni wazi kwamba kila dhaalimu amelaaniwa. Sidhani yeyote katika ninyi atakataa dhuluma za wazi zilizofanywa na Mu’awiya.

Hivyo kwa ukweli wenyewe kwamba alikuwa dhaalimu, huthibitisha kwamba alistahili laana ya Allah kwa mtazamo wa dalili hizi za wazi, sisi pia tunaweza kumlaani mtu ambaye anastahili laana ya Allah.

(7) Katika sur ya Nisa Allah Anasema:

وَمَنْ يَقْتُلْ مُؤْمِنًا مُتَعَمِّدًا فَجَزَاؤُهُ جَهَنَّمُ خَالِدًا فِيهَا وَغَضِبَ اللَّهُ عَلَيْهِ وَلَعَنَهُ وَأَعَدَّ لَهُ عَذَابًا عَظِيمًا {93}

“Na mwenye kumuuwa Muumini kwa kukusudia, basi malipo yake ni Jahannam, humo atakaa milele na Mwenyezi Mungu amemghadhibikia na amemlaani, na amemuandilia adhabu kubwa.” (4:93)

Mauaji Ya Waumini Mashuhuri Kama Imam Hasan, Ammar, Hajar Bin Adi, Malik Ashtar, Muhammad Bin Abi Bakr, Nk. Kwa Amri Ya Mu’awiya.

Aya hii tukufu kwa uwazi inasema kwamba kama mtu anamuua muumini mmoja kwa makusudi, anastashili laana ya Allah na makazi yake ni Jahannam. Je, Mu’awiya hakujihusisha na mauaji ya waumini? Je, hakuamuru mauaji ya Hajar Bin Adi na masahaba wake saba? Je hakuamuru kwamba Abdu’r-Rahman Bin Hasan Al-Ghanzi azikwe akiwa hai?

Ibn Asakir na Yaqub Bin Sufyan katika vitabu vyao vya Ta’rikh; Baihaqi katika kitabu chake Dala’il; Ibn Abdu’l-Birr katika Isti’ab; na Ibn Athir katika Kamil wamesimulia kwamba Hajar Bin Adi alikuwa mmoja wa masahaba maarufu ambaye, pamoja na masahaba wengine saba aliuawa kikatili na Mu’awiya. Kosa lao lilikuwa kukataa kumlaani Ali.

Imam Hasan alikuwa ni mjukuu mkubwa wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Je, yeye hakujumuishwa katika As’hab-e-Kisa (Watu wa shuka/kishamia)? Je, yeye siye mmoja wa viongozi wawili wa vijana wa Peponi na Mu’mini wa daraja la juu? Kwa mujibu wa riwaya ya Mas’ud, Ibn Abdu’l-Birr, Abu’l-Faraj Ispahani, Tabaqa cha Muhammad Bin Sa’d, Tadhkira cha Sibt Ibn Jauzi, na maulamaa wengine maarufu wa Sunni, wanaandika kwamba, Mu’awiya alimpelekea sumu Asma Ju’da na kumuahidi kwamba kama akimuua Hasan Ibn Ali, atampa Dirham 100,000 na atamuozesha kwa mwanawe Yazid.

Baada ya kifo cha Imam Hasan, alimpa dirham 100,000 lakini akakataa kumuozesha kwa Yazid. Utasita kumita Mu’awiya mlaaniwa? Je, sio ukweli kwamba katika vita vya Siffin sahaba mkubwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), Ammar Yasir, aliuawa kwa amri ya Mu’awiya? Maulamaa wenu wote mashuhuri wanasema kwa muafaka mmoja kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimuambia Ammar Yasir: Haitachukuwa muda kabla wewe hujauawa na kikundi cha kiuasi na kipotofu.”

Je, una mashaka yoyote kwamba maelfu ya waumini waaminifu waliuawa na wafuasi wa Mu’awiya? Je, askari safi na shujaa, Malik Ashtar hakulishwa sumu kwa amri ya Mu’awiya? Je, unaweza kukataa kwamba maofisa wakuu wa Mu’awiya, Amr Bin Aas na Mu’awiya Bin Khadij, walimuuwa kikatili gavana wa Amir wa waumini, mchamungu Muhammad Bin Abi Bakr? Bado hawakutosheka na hilo, wakauweka mwili wake kwenye mzoga wa punda na kuuchoma moto.

Kama nikisema niwape maelezo kuhusu waumini waliouawa na Mu’awiya na maofisa wake, itahitaji si usiku mmoja, bali zaidi.

Mauaji Ya Waumini 30,000 Waliouawa Na Busr Bin Artat Kwa Amri Ya Mu’awiya

Ukatili mkubwa kabisa ulikuwa ni ule wa Busr Bin Artat ambaye aliwauwa maelfu ya wau- mini kwa amri ya Mu’awiya.
Abu’l-Faraj Ispahani na Allama Samhudi katika Ta’rikhu’l-Madina, Ibn Khallikan, Ibn Asakir na Tabari katika vitabu vyao vya Ta’rikh; Ibn Abi’l-Hadid katika Sharh-e-Nahju’l- Balagha, Jz. 1, na wengine wengi wa katika maulamaa wenu maarufu wameandika kwamba Mu’awiya alimuamuru Busr kushambulia San’a na Yemen kutokea Madina na Makka. Alitoa amri kama hiyo hiyo kwa kwa Zuhak Bin Qais Al-Fahri na wengine.

Abu’l-Faraj anaisimulia katika maneno haya: “Yeyote katika masahaba na Shia wa Ali akionekana laz- ima auawe; hata wanawake na watoto wasiachwe.” Kwa amri hizi kali, walitoka na watu 3000 na akashambulia Madina, San’a, Yeman, Ta’if, na Najran.

Walipofika Yemen, gavana, Ubaidullah Ibn Abbas, alikuwa nje ya mji. Waliingia ndani ya nyumba yake na kuuwa watoto wake wawili Sulaiman na Daudi katika mapaja ya mama yao.

Ibn Abi’l-Hadid anaandika katika Sharh-e-Nahju’l-Balagha, Jz. 1, uk. 121, kwamba katika shambulio hili watu 30,000 waliuawa, ukiondoa wale waliochomwa moto wakiwa hai. Je, mabwana nyie bado mna mashaka kwamba Mu’awiya anastahili kulaaniwa?

Mu’awiya Alitoa Amri Kwamba Ali Alaaniwe

Miongoni mwa ushahidi mwingi uliowazi kwamba Mu’awiya alikuwa kafiri na kustahili laana ilikuwa kumkataa kwake hadharani Amir wa Waumini na kuwaamuru watu wasome visomo vya malaanifu dhidi ya mtukufu Imam katika Qunuti zao. Jambo hili linakubaliwa na wote, ninyi na sisi.

Hata wanahistoria wa mataifa mengine wameandika kwamba matendo maovu yalikuwa yakifanywa wazi na kwamba watu wengi waliuawa kwa sababu hawakutoa maneno yale ya laana dhidi ya Imam Ali. Uovu huu ulisitishwa na Khalifa wa Banu Umayya, Umar Ibn Abdu’l-Aziz.

Ni dhahiri, mtu ambaye humlaani ndugu yake Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), mume wa Fatima, Amir wa Waumini, Ali Bin Abi Talib na ambaye anawaamrisha wengine kufanya hivyo kwa hakika ni mlaaniwa. Jambo hili limeandikwa na ulamaa wenu wote maarufu katika vitabu vyao sahihi. Kwa mfano, Imam Ahamad Bin Hanbal katika Musnad yake, Abu Abdu’r-Rahman Nisa’i katika Khasa’isu’l-Alawi, Imam Tha’labi na Imam Fakhru’d- din Razi katika Tafsir zao, Ibn Abi’l-Hadid katika Sharh-e-Nahju’l-Balagha, Muhammad Bin Yusuf Ganji Shafi’i katika Kifayatut-Talib, Sibt Ibn Jauzi katika Tadhkira, Sulayman Balkhi Hanafi katika Yanabiu’l-Mawadda, Mir Seyyid Ali Hamadani katika Mawaddatu’l-Qurba, Dailami katika kitabu chake Firdaus, Muslim Bin Hajjaj katika Sahih yake, Muhammad Bin Talha Shafi’i katika Matalabus-Su’ul, Ibn Sabbagh Maliki katika katika Fusulu’l-Muhimma, Hakim katika Mustadrak, Khatib Khawarizzmi katika Manaqib yake, Abraham Hamwaini katika Fara’id, Ibn Maghazili Shafi’i katika Manaqib yake, Imam’l- haram kati Dhakha’iru’l-Uqba, Ibn Hajar katika Saw’iq, na maulamaa wenu mashuhuri wamwesimulia katika tofauti kidogo ya maneno kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alise- ma: “Mtu ambaye anamtukana Ali, ananitukana mimi; na mwenye kunitukana mimi, haki- ka anamtukana Allah.”

Dailami katika katika Firdaus, Sulayman Hanafi katika Yanabiu’l-Mawadda wamesimulia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Mtu ambaye anamchukiza Ali, hakika ananichukiza mimi, na laana ya Allah iko juu ya yule ambaye ananichukiza mimi.”

Ibn Hajar Makki katika kitabu chake Saw’iq anasimulia hadithi inayohusu matokeo kwa mtu ambaye hulaani dhidi ya yeyote katika kizazi cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Anasimulia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Kama mtu yeyote atamlaani Ahlu’l-Bayti wangu, hakuna cho chote kwake bali kuondolewa katika Uislamu. Kama mtu yeyote atanichukiza mimi kuhusiana na Ahlul’l-Bayti wangu, laana ya Allah iwe juu yake.”

Kwa hiyo, kwa hakika Mu’awiya alikuwa amelaaniwa. Kama inavyosimuliwa na ibn Athir katika kitabu chake Kamil, Mu’awiya alizoea kumalaani Ali, wajukuu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) Hasan na Husein na vile vile Abbas na Malik Ashtar katika Qunut ya sala zake za kila siku.

Imam Ahmad Hanbal anasimulia katika Musnad yake kutoka vyanzo mbali mbali kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema:
“Kama mtu yeyote anamchukiza Ali atatendewa kama Yahudi au Mkirsto katika Siku ya Hukumu.” Kwa hakika lazima uelewe kwamba ni moja ya mafundisho ya Uislamu kwamba kumuita Allah na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa majina mabaya humpeleka mtu kwenye ukafiri.

Muhammad Bin Ganji Shafi’i katika Kifayatut-Talib sehemu ya 10, anasimulia kwamba siku moja Abdullah Ibn Abbas na Sa’id Ibn Jabir waliona katika ukingo wa Zamzam kikundi wa watu wa Syria wakimshutumu Ali. Walikwenda pale walipo na wakasema:

“Ni nani miongoni mwenu aliyekuwa anamtukana Mtukufu Mtume wa Allah (s.a.w.w.)?” wakajibu: “Hakuna kati yetu aliyekuwa anamtukana Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).” Kisha wakasema: “Vema, nani miongoni mwenu aliyekuwa anamtukana Ali?” Wakasema: “Ndio tulikuwa tukimtukana Ali.”

Kisha Abdullah na Sa’id wakasema: “Yawapasa mshuhudie kwamba tulimsikia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akimuambia Ali, ‘Mtu anayekutukana wewe kwa hakika hunitukana mimi; mtu ambaye hunitukana mimi, kwa hakika humtukana Allah. Kama mtu akimtukana Allah, Atamtumpa kichwa chini kwenye moto wa Jahannam.’”

Masahaba Wa Mtume Walikuwa Katika Viwango Tofauti Vya Uwelewa

Sheikh: Je, ni sahihi kwa mtu wa hadhi yako kumlaani sahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mwenye uwezo na hadhi kama huyu? Je, sio ukweli kwamba Allah swt., ameteremsha idadi ya aya katika kuwatukuza masahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na akawapa habari njema za kuokolewa kwao. Khalu’l-Mu’munin Mu’awiya, ambaye kwa hakika alikuwa sahaba mashuhuri, alistahiki sifa iliyomo katika aya hii tukufu. Je, kutukana sahaba sio sawa na kumtukana Allah na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)?

Muombezi: Huenda umesahau kile ambacho tayari nimekuambia katika mikesha iliyopita. Hakuna anayekataa kwamba aya zimeteremshwa katika kuwasifu masahaba. Lakini kama unaelewa maana ya sahaba, utakubali kwamba aya zilizoteremshwa katika kuwasifu masahaba kwa ujumla haziwahusishi masahaba wote. Hatuwezi kuwachukuliwa wote kuwa ni wasafi kabisa. Bwana mheshimiwa! Unajua vizuri sana kwamba sahaba kilugha ina maana ya kuunganika kwa watu pamoja.

Hivyo inaweza kuwa na maana ya kuishi pamoja au kama kwa kawaida inavyoeleweka, kusaidia au kutoa msaada kwa wengine.

Kwa mujibu wa leksikografia (usawidi kamusi) ya Kiarabu, Qur’ani, na hadithi, sahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) maana yake ni mtu ambaye ametumia uhai wake katika kuwa pamoja na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), imma awe alikuwa Mwislamu au kafiri.

Hivyo tafsiri yako kwamba masahaba wote wanastahiki Pepo sio sahihi. Hii inakinzana na akili ya kawaida na halikadhalika hukinzana na hadithi.

Katika Maneno Ya Qur’ani Tukufu Sahab Na Swahaba, Kwa Maana Ya “Wenzi” Hayana Maani Ya Kiheshima

Nitawasilisha aya za Qur’ani za nyogeza na hadithi sahihi kutoka wanachuoni wa Sunni ili kwamba usije ukakosea kuhusu neno sahaba.

Neno hili lilikuwa linatumika kwa sahaba wote, iwe walikuwa Waislamu au la:

(1) Katika Suratun Najm, Allah anawaambia washirikina:

مَا ضَلَّ صَاحِبُكُمْ وَمَا غَوَىٰ {2}

“Kwamba swahibu wenu hakupotea wala hakukosea.” (53:2)

(2) Katika Surat Saba, Allaha anasema:

قُلْ إِنَّمَا أَعِظُكُمْ بِوَاحِدَةٍ ۖ أَنْ تَقُومُوا لِلَّهِ مَثْنَىٰ وَفُرَادَىٰ ثُمَّ تَتَفَكَّرُوا ۚ مَا بِصَاحِبِكُمْ مِنْ جِنَّةٍ ۚ{46}

“Sema: mimi ninakunasihini tu kwa jambo moja kuwa; msimame kwa ajili ya Allah, wawili wawili na mmoja mmoja, kisha mtafakari: swahiba wenu hana wazimu…”(34:46)

(3) Katika Surat Kahf, Allah anasema:

ثَمَرٌ فَقَالَ لِصَاحِبِهِ وَهُوَ يُحَاوِرُهُ أَنَا أَكْثَرُ مِنْكَ مَالًا وَأَعَزُّ نَفَرًا {34}

“…Na akamwambia swahiba wake hali akibishana naye: mimi nina mali nyingi kuliko wewe na (nina) nguvu zaidi kwa wafuasi.” (18:34)

(4) Katika Sura hiyo hiyo, Allah anasema:

قَالَ لَهُ صَاحِبُهُ وَهُوَ يُحَاوِرُهُ أَكَفَرْتَ بِالَّذِي خَلَقَكَ مِنْ تُرَابٍ ثُمَّ مِنْ نُطْفَةٍ ثُمَّ سَوَّاكَ رَجُلًا {37}

“Swahiba wake akamwambia hali ya kubishana naye: je, umemkufuru yule aliyekuumba kwa udongo, tena kwa tone la manii, kisha akakufanya mtu kamili.” (18:37)

(5) Katika Sura ya A’raf, Allah anasema:

أَوَلَمْ يَتَفَكَّرُوا ۗ مَا بِصَاحِبِهِمْ مِنْ جِنَّةٍ ۚ إِنْ هُوَ إِلَّا نَذِيرٌ مُبِينٌ {184}

“Je, hawatafakari? Swahiba wao hana wazimu, hakuwa yeye ila ni muonyaji dhahiri.” (7:184)

(6) Katika Sura ya An’am, Allah anasema:

قُلْ أَنَدْعُو مِنْ دُونِ اللَّهِ مَا لَا يَنْفَعُنَا وَلَا يَضُرُّنَا وَنُرَدُّ عَلَىٰ أَعْقَابِنَا بَعْدَ إِذْ هَدَانَا اللَّهُ كَالَّذِي اسْتَهْوَتْهُ الشَّيَاطِينُ فِي الْأَرْضِ حَيْرَانَ لَهُ أَصْحَابٌ يَدْعُونَهُ إِلَى الْهُدَى ائْتِنَا ۗ قُلْ إِنَّ هُدَى اللَّهِ هُوَ الْهُدَىٰ ۖ وَأُمِرْنَا لِنُسْلِمَ لِرَبِّ الْعَالَمِينَ {71}

“Sema: Je, tumuombe asiyekuwa Allah ambaye hatupi faida wala hawezi kutudhuru, na turudishwe nyuma baada ya Allah kutuongoza, sawa na yule ambaye mashetani yamempoteza akiwayawaya katika ardhi? Anao maswahiba wanaomwita kwenye mwongozo hasa ni mwongozo wa Allah, na tumeamrishwa tumnyenyekee Mola wa walimwengu wote.” (6:71)

(7) Katika sura ya Yusuf, Allah anasema: (Yusuf akiwaambia wafungwa wenzake wawili)

يَا صَاحِبَيِ السِّجْنِ أَأَرْبَابٌ مُتَفَرِّقُونَ خَيْرٌ أَمِ اللَّهُ الْوَاحِدُ الْقَهَّارُ {39}

“Enyi maswahiba wangu wawili, je, waungu wawili wanaofarikiana ni bora au Allah Mmoja, Mwenye nguvu?” (12:39)

Hizi ni aya chache, ambazo nimezinukuu kwa njia ya mfano. Ni wazi kwamba maneno sahaba, sahib, musahib na ashab hayana uhusiano maalum kwa Waislamu. Hutumika katika kuwahusu Waislamu na washirikina halikadhalika.

Kama nilivyosema, mtu ambaye ana shughuli ya kijamaa na mtu mwingine anaitwa musahib au ashab. Masaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) huashiria wale ambao wana shughuli za kijamii pamoja na yeye.

Kwa hakika miongoni mwa sahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na miongoni mwa wale ambao walikaa pamoja naye, walikuwa ni aina zote za watu, wazuri na wabaya, waumini na halikadhalika wanafiki.

Aya zilizoteremshwa katika kuwasifu masaba haziwezi kuhusishwa kwao wote. Zinaashiria tu kwa wale masahaba wazuri. Vile vile ni kweli kwamba hakuna katika mitume wakubwa wa zamani ambao walikuwa na masahaba maarufu mno kama wale wa Mtukufu Mtume wetu (s.a.w.w.).

Kwa mfano, masahaba wa Badr, Uhud, na Hunain walikuwa kiasi kwamba walitimiza kipimo cha wakati ule. Walimsaidia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na walikuwa imara katika uthabiti wao.

Lakini miongoni mwa masahaba wake vile vile ilikuwako idadi ya watu wenye tabia duni, maadui wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na Ahlul’l-Bayti wake, watu kama Abdullah Bin Ubayy, Abu Sufyan, Hakam Bin Aas, Abu Huraira, Tha’labi, Yazid Bin Sufyan, Walid Bin Aqaba, Habib Bin Musailima, Samra Bin Jundab, Amr Bin Aas, Busr Bin Artat (mtawala dhalimu mwenye kiu ya damu), Mughira Bin Shu’ba, Mu’awiya Bin Abi Sufyan, na Dhu’s-Sadiyya.

Watu hawa, kwa nyakati zote, katika uhai wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na hata baada ya kufa kwake, walisababisha ghasia kubwa miongni mwa watu. Mmoja wa watu kama hawa ni Mu’awiya, ambaye Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimlaani katika wakati wa uhai wake mwenyewe.

Baada ya kifo cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), wakati Mu’awiya alipopata fursa, alifanya uasi kwa jina la kulipa kisasi kwa ajili ya kifo cha Uthman na akasababisha umwagaji damu ya Waislamu wengi.

Katika mauaji haya masahaba wengi wenye kuheshimiwa wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), kama Amar Bin Yasir, waliuawa kishahidi. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mwenyewe alitabiri kifo chke hicho cha shahada. Nimekwishataja baadhi ya hadithi zinazohusiana na tukio hili.

Qur’ani Tukufu Inawasifia Masahaba Wema Lakini Pia Inawalaani

Masahaba Waovu

Kuna aya nyingi katika Qur’ani Tukufu na hadithi zenye kuwasifia masahaba mashuhuri na waumini wachamungu. Na vile vile kuna aya nyingi na hadithi zenye kuwalaani wale masahaba waliokuwa ni watenda maovu.

Sheikh: Vipi utadai kwamba masahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) walisababisha vurugu za kijamii?

Muombezi: Hili sio tu dai langu. Allah swt., katika Sura ya Aali Imran anasema:

وَمَا مُحَمَّدٌ إِلَّا رَسُولٌ قَدْ خَلَتْ مِنْ قَبْلِهِ الرُّسُلُ ۚ أَفَإِنْ مَاتَ أَوْ قُتِلَ انْقَلَبْتُمْ عَلَىٰ أَعْقَابِكُمْ ۚ{144}

“Na hakuwa Muhammad ila ni Mtume aliyepitiwa na mitume kabla yake. Basi je, akifa au akiuliwa mtarudi nyuma kwa visigino vyenu?...” (3:144)

Mbali ya hii na aya nyingine za Qur’ani, maulamaa wenu wenyewe, pamoja na Bukhari, Muslim, Ibn Asakir, Yaqub Bin Sufyan, Ahmad Bin Hanbal, Abdu’l-Birr, na wengine wamesmulia idadi ya riwaya na hadithi kuhusiana na kulaaniwa kwa baadhi ya masahaba. Nitafanya rejea kwenye hadithi mbili tu. Bukhari anasimulia kutoka kwa Sahl Ibn Sa’d na Abdullah Ibn Mas’ud kwamba Mtukufu Mtume wa Allah (s.a.w.w.) alisema: “Nitakuwa nawangojea kwenye chemchemu ya Kauthar.

Wakati kundi kati yenu litakapotoka kutoka kwenye njia yangu, nitasema, ‘Ewe Allah! Hawa walikuwa ni masahaba wangu!’

Kisha jibu kutoka Kwake litakuja kwangu: ‘Wewe hujui ni mangapi waliyoyazua baada yako.’”

Tena Imam Ahmad Bin Hanbal katika Musnad yake, Tabrani katika Kabir, na Abu Nasr Sakhri katika Ibana wanasimuliwa kutoka kwa ibn Abbas kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Nataka kuwaokoeni ninyi kutoka kwenye adhabu ya Jahannam. Nawatakeni ninyi muogope moto wa Jahannam na kufanya mabadiliko kwenye dini ya Allah. Wakati nitakapofariki na kutenganishwa na ninyi, nitakuwepo kwenye chemchemu ya Kauthar.

Yeyote yule atakayenifikia mimi hapo atakuwa ameokolewa. Wakati wa mwisho nintakapoona idadi kubwa ya watu wameshikwa katika adhabu ya kimungu, nitasema: ‘Ewe Allah! Hawa ni watu wa umma wangu.’ Jibu litakuja: ‘Hakika, watu hawa walirudi kwenye imani yao ya zamani (waliritadi) baada yako.’

Kwa mujibu wa riwaya ya Tabrani katika Kabir, jibu litakuwa: “Hujui ni uzushi gani waliuanzisha baada yako. Walifuata dini yao ya zamani ya ujinga.”

Abu Talib Alikuwa Muumini Imara

Unasisitiza kwamba Mu’awiya na Yazid ni Waislamu ingawa ukatili wao mwingi umeandikwa katika kwenye vitabu vyenu wenywewe.

Baadhi ya maulamaa wa Sunni wameandika vitabu kamili katika kuwalaani, lakini kwa ukaidi unasisitiza kwamba walikuwa wanastahiki sifa na Abu Talib muumini mwaminifu alikuwa kafir! Ni dhahiri kabisa kwamba mazungumzo haya ya kipuuzi ni matokeo ya chuki dhidi ya Amir wa Waumini Ali.

Unajaribu kukataa hoja ambazo zinathibitisha ukafiri na unafiki wa Mu’awiya na Yazid. Na bado unakataa matamko ya wazi ya Abu Talib yanayohusiana na imani yake juu ya Allah na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Ushahidi Wa Nyongeza Juu Ya Imani Ya Abu Talib

Je, sio kweli kwamba Ahlu’l-Bayt wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wamesema kwamba Abu Talib alikuwa mu’mini na kwamba alikufa akiwa mu’mini? Je, Asbagh Bin Nabuta, mtu mwenye kuaminiwa sana, hakusimulia kutoka kwa Amir wa Wauimini kwamba alisema:

“Naapa kwa jina la Allah kwamba baba yangu, Abu Talib, babu yangu, Abdu’l-Muttalib Hashim, na Abdu’l-Manaf kamwe hawakuabudia masanamu.” Je, ni sahihi kwamba ukatae maelezo ya Ali na Ahlu’l-Bayti na kuamini maelezo ya mlaaniwa Mughira, ma-Awami, Makhawarij, Manasibi, na maadui wengine wa Amir wa Waumini?

Ja’far Tayyar Amekubali Uislamu Kwa Amri Ya Baba Yake

Aidha, wengi wa maulamaa wenu pamoja na Ibn Abi’l-Hadid katika Sharh-e-Nahju’l-Balagha, wameandika kwamba siku moja Abu Talib alikuja msikitini na akaona kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa anaswali. Ali naye alikuwa anaswali upande wake wa kulia. Abu Talib akamuamrisha mtoto wake Ja’far ambaye alikuwa pamoja naye na alikuwa bado hajaingia katika Uislamu, akamuambia ‘Simama pembeni kwa binamu yako na uswali pamoja naye.’

Ja’far alisogea mbele na akasimama upande wa kushoto wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), akaanza kuswali swala zake. Wakati huo Abu Talib akasoma beti hizi za shairi:

“Hakika Ali na Ja’far ni nguvu na faraja yangu katika huzuni na masikitiko. Ewe Ali na Ja’far! Kamwe msiachane na binamu yenu na mpwa wangu, bali msaidieni. Naapa kwamba kamwe sitamuacha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Je, yawezekana mtu akaacha kufuatana na Mtume wa familia tukufu kama hii?” Hivyo ni mtazamo wa wote pamoja wa maulamaa wenu kwamba kuingia Uislamu kwa Ja’far na kuswali pamoja na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ilikuwa ni kwa amri ya Abu Talib.

Mtukufu Mtume Alilia Sana Wakati Wa Kifo Cha Abu Talib Na Akaomba

Baraka Za Allah Ziwe Juu Yake

Ibn Abi’l-Hadid katika Sharh-e-Nahju’l-Balagha na Ibn Jauzi katika Tadhkirat-e-Khawasu’l-Umma wanasimulia kutoka Tabaqat-e-Muhammad, Ibn Sa’d, ambaye anasimulia kutoka kwa Waqidi na Allama Seyyid Muhammad Bin Seyyid Rasul Barzanji katika Kitabu’l-Islam Fi’l-‘am-u-Aba’-e-Sayyidul’l-An’am, riwaya kutoka kwa Ibn Sa’d na Ibn Asakir, ambao wanasimulia kutoka kwenye vyanzo sahihi kutoka kwa Muhammad Bin Ishaq kwamba Ali alisema: “Wakati Abu Talib alipokufa na nilipomjulisha Mtukufu Mtume wa Allah (s.a.w.w.) kuhusu kifo hicho, alilia sana. Kisha akaniambia, ‘Nenda ukaoshe mwili wake kwa ajili ya matayarisho ya mazishi, uuvishe mwili wake sanda, na umzike. Allah ambariki na awe na huruma juu yake!”

Je, inaruhusiwa na Uislam kufanya ibada za mazishi kwa mshirikina? Je, ni sawa kwetu kusema kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliomba baraka za Allah juu ya kafiri na mshirikina? Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hakutoka Nyumbani mwake kwa muda wa siku kadhaa na kuendelea kuomba kwa Allah kwa ajili amani ya milele ya Abu Talib.

Nauha Za Ali Kwa Ajili Ya Baba Yake, Abu Talib

Nauha za ali kwa ajili ya baba yake, Abu Talib- Nauha ni nyimbo za maombolezo.

Kama utaangalia kitabu Tadhkira cha Sibt Ibn Jauzi, uk. 6 utaona nini alichosema Amir wa Waumini katika nauha zake kwa ajili ya baba yake: “Ewe Abu Talib! Ulikuwa ni mbingu ya wenye kutafuta hifadhi, mvua ya neema kwa ardhi kavu, na mwanga ulio penyeza kati- ka giza. Kifo chako kimeporomosha nguzo za usalama. Sasa Mfadhili halisi ameweka rehema juu yako. Allah swt., amekuambatanisha na baraza Yake. Hakika ulikuwa ndiwe ami mbora wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).”

Je, yaweza kuaminika kwamba mtu ambaye alikuwa mfano halisi wa tawhid angeweza kuandika nauha kama hii kwa ajili ya mtu aliyekufa kafiri?

Abu Talib Alificha Imani Yake Ambapo Abbas Na Hamza Walitangaza Zakwao

Sheikh: Kama Abu Talib alikuwa muumini, kwa nini asidhihirishe imani yake kama walivyofanya ndugu zake, Hamza na Abbas?

Muombezi: Kulikuwepo na tofauti kubwa sana kati ya Abbas na Hamza na Abu Talib. Hamza alikuwa haogopi kabisa na mtu mwenye kutisha sana kiasi kwamba watu wa Makka walimuogopa sana. Kuingia kwake Uislamu kulidhihirisha msaada mkubwa mno kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Hata hivyo, Abbas hakutangaza Uislamu wake mara moja. Ibn Abdu’l-Birr anaandika katika kitabu chake, Isti’ab kwamba Abbas aliingia Uislamu wakati akiwa Makka, lakini aliificha imani yake kwa watu. Wakati Mtume alipohama kutoka Makka, Abbas vile vile alikusudia kuwa pamoja naye.

Lakini Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimuandikia kwamba kubakia kwake Makka kutakuwa na manufaa kwake (yeye Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)). Kwa hiyo, alibakia Makka na akawa anampelekea habari Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kutoka pale. Waabudu masanamu walikuja naye kwenye vita vya Badr. Wakati makafiri waliposhindwa, alichukuliwa mateka. Katika siku ya kuishinda Khaibar aliruhusiwa mwishowe kudhihirisha imani yake.

Sheikh Sulayman Balkhi Hanafi katika Yanabiu’l-Mawadda, sura ya 56, uk. 226, anasimulia kutoka kwenye Dhakha’iru’l-Uquba cha Imam’l-Haram Abu Ja’far Ahmad Bin Abdullah Tabari Shafi’i, ambaye anasimulia kutoka kwenye Fadha’il cha Abu’l-Qasim Ilahi kwamba wanachuoni wanajua kwamba Abbas aliingia Uislamu mwanzoni lakini ali- ificha imani yake.

Katika vita vya Badr wakati alipokuja na makafiri, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliwaeleza watu wake: “Yeyote atakayemuona Abbas asimuuwe kwa sababu ali- fuatana na makafiri bila hiyari yake. Alikuwa tayari kuhama, lakini nilimuandikia barua kwamba abakie kule awe ananipa habari kuhusu makafiri.” Siku ambayo Abu Rafi’i alimjulisha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwamba Abbas ametangaza kukubali kwake Uislamu, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimuacha Abu Rafi’i huru.

Kwa Nini Abu Talib Afiche Imani Yake

Kama Abu Talib angeonesha imani yake Kureishi wote na taifa lote la Arabia lingeungana dhidi ya Bani Hashim. Abu Talib alifahamu faida ya kuficha Uislamu wake. Alijifanya kuwa mtiifu kwa Makureishi ili azuiye shughuli za adui.

Alimuradi Abu Talib anabakia hai, hali hiyo iliendelea, na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa katika ulinzi. Lakini wakati wa kifo cha Abu Talib, Malaika Jibrail alitokeza mbele ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na akasema: “Sasa yakupasa kuondoka Makka. Baada ya Abu Talib huna msaidizi hapa.”
Sheikh: Je, Uislamu wa Abu Talib ulijulikana wakati wa uhai wa Mtukufu Mtume wa Allah (s.a.w.w.)? Na je, umma uliamini hivyo?

Muombezi: Ndiyo, ulijulikana sana kwa watu na walilitamka jina lake kwa heshima kamili kabisa.

Imani Ya Abu Talib Ilikuwa Ikijulikana Kwa Kawaida Wakati Wa Uhai

Wa Mtukufu Mtume

Sheikh: Inawezekanaje kwamba wakati wa uhai wa Mtume kitu kilikuwa kinazungumzwa sana na kwa kawaida kikajulikana kwa watu wote, lakini baada ya muda wa miaka thelathini, mtazamo wa kinyume ukapata nguvu kwa sababu ya hadithi za uwongo?

Muombezi: Huu haukuwa mfano wa kipekee. Mara nyingi kile ambacho kilikubaliwa wakati wa uhai wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kilibadilika kabisa muundo wake baada ya miaka michache kwa sababu ya hadithi za kughushi.

Amri nyingine za kidini na matendo ya ibada yaliyokuwepo wakati wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) yaliachwa baada ya miaka kadhaa kwa sababu ya ushawishi wa watu.

Ndoa Ya Mut’a Na Hajj Nisa Zilikuwa Halali Mpaka Wakati Wa Abu Bakr

Lakini Zikaja Kuharamishwa Na Umar

Sheikh: Tafadhali hebu taja mfano mmoja wa mabadiliko kama hayo.

Muombezi: Kuna mifano mingi; miwili itatosha kuelezea nukta yangu. Nitajadili mut’a (ndoa ya muda) na Hajj Nisa. Madhehebu zote zinakubali kwamba matendo haya mawili ya kiibada yalikuwa ya kawaida wakati wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Aidha, yalikuwa yakitekelezwa wakati wa ukhalifa wa Abu Bakr na vile vile sehemu ya kipindi cha ukhalifa wa Umar. Lakini Khalifa Umar alisababisha ugeuzaji kabisa wa amri ya Qur’ani.

Alisema: “Mut’a mbili zilikuwa zinafanyika wakati wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Sasa natamka kwamba zote ni haramu na nitawaadhibu wale ambao wanajishughulisha katika matendo haya.”

Kilichokuwa kumehalalishwa na Allah ghafla kilifutwa. Hukumu ya Umar ilitangazwa kwa mapana sana na ikafuatwa kibubusa sana kiasi kwamba ile sheria ya asili mara moja ikasahauliwa. Hata leo hii, wengi wa ndugu zetu Masunni wanaiona Mut’a kama uzushi wa Mashi’a.

Kama wazo la ajabu ajabu la Umar limeweza kugeuza amri ya wazi ya Allah na ukweli wa kihistoria kwamba mut’a ilikuwa ikifanyika, je, unaweza kuwa na shaka kwamba imani ijulikayo vizuri ya Abu Talib inaweza vile vile kukatiliwa?

Sheikh: Je, unataka kusema kwamba mamilion ya Waislamu wamevunja amri ya Qur’ani na sunna ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)? Kumbuka, ulimwengu wote unatuita sisi Sunni, yaani, wafuasi wa Sunna. Mashi’a wanaitwa Rafidh, yaani, wale waliopotoka kutoka kwenye sunna ya Mtume.

Sunni Kwa Kweli Ndio Marafidhi Na Mashi’a Ndio Sunni Hasa

Muombezi: Kiukweli hasa Mashi’a ndio Masnni, yaani, wao wanafuata Qur’ani Tukufu na sunna ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Ninyi watu nyie ni Marafidhi kwa sababu mnavun- ja amri za Qur’ani Tukufu na maamrisho ya Mtume.

Sheikh: Hii ni ajabu kweli! Umewageuza mamiloni ya Waislamu safi kuwa marafidhi! Unaweza kuleta hoja yoyote ya kuunga mkono hili?

Muombezi: Nimekwisha kukuambia katika mikesha iliyopita kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ilituagiza kwamba baada yake lazima tufuate Qur’ani Tukufu na kizazi chake.

Lakini ninyi watu kwa makusudi mkakitelekeza kizazi cha Mtume na kufuata wengine. Mmeutupa mwenendo wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Mliwaacha watu wale (Ahlu’l- Bayti) kwa amri ya masheikh wenu wawili na kisha mkawaita wafuasi halisi wa sunna ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) Marafidhi.

Miongoni mwa maagizo hayo kuna amri nyingine ya wazi katika Qur’ani Tukufu ambayo inasema:

“Na jueni kwamba chochote mlichokiteka, basi sehemu yake ya tano ni ya Allah na Mtume na (jamaa zake Mtume) na yatima na masikini na msafiri (aliyeharibikiwa)…” (8:41)

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliitekeleza amri hii na akatoa khums (1/5) ya mali iliyopatikana kutoka kwa adui na kuwapa jamaa na ndugu zake. Lakini ninyi watu mnaupinga mwendo huu.

Kufanya mut’a ni mfano mwingine mzuri. Ilikuwa ni kwa mujibu wa amri ya Allah. Ilithibitishwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na masahaba zake.

Utekelezaji wake uliendelea wakati wa ukhalifa wa Abu Bakr na vile vile kwa kipindi katika wakati wa ukhalifa wa Umar.

Lakini kwa amri yake Umar ninyi watu mmekifanya haramu kile Allah alichoki- fanya halali.

Aidha, mmeiuuza sunna ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Na bado mnajiita wenyewe Sunni na kutuita sisi Rafidh.

Khalifa Umar mwenyewe hakutoa sababu yoyote ya kuifuta amri ya Mungu. Maulamaa wa Sunni wamejaribu bila mafanikio kuthibitisha kwamba uamuzi wa Khalifa Umar ulikuwa wa haki.

Hoja Za Uhalali Wa Mut’a

Sheikh: Unaweza ukathibitisha uhalali wa mut’a? unaweza ukathibitisha kwamba Khalifa Umar alivunja amri ya Qur’ani na sunna ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)?

Muombezi: Uthibitisho wenye nguvu sana unatolewa na Qur’ani Tukufu. Katika Sura ya Nisa
Allah anasema:

فَمَا اسْتَمْتَعْتُمْ بِهِ مِنْهُنَّ فَآتُوهُنَّ أُجُورَهُنَّ فَرِيضَةً ۚ{24}

“…Na kwa wale ambao mmestarehe nao katika wao, basi wapeni mahari yao yaliyolazimu…” (4:24)

Kwa dhahiri amri ya Qur’ani Tukufu daima ni ya wajibu isipokuwa iwe imefutwa na Qur’ani yenyewe. Kwa vile haikufutwa, amri hii hubakia ya wajibu daima.

Sheikh: Vipi aya hii isihusike na ndoa ya kudumu? Ni aya hii hii ambayo hutoa maeleke zo kuhusu kulipa mahari.

Muombezi: Umeichanganya nukta yenyewe. Maulamaa wenu wenyewe, kama Tabari katika Tafsir-e-Kabir, Jz. 5 na Imam Fakhru’d-din Razi katika tafsiri yake Tafsir-e-Mafatihu’l-Ghaib, Jz. 3, wamethibitisha kwamba aya hii inazungumzia mut’a.

Mbali na tafsiri ya wazi ya maulamaa wenu na wafasir, vile vile una habari kwamba kati- ka Sura yote ya Nisa, aina mbali mbali za ndoa zimetajwa: ndoa ya kudumu, mut’a, (ndoa ya muda) na ndoa ya mulk-e-Yamin (watumwa).

Kwa ndoa ya kudumu Qur’ani Tukufu inasema:

فَانْكِحُوا مَا طَابَ لَكُمْ مِنَ النِّسَاءِ مَثْنَىٰ وَثُلَاثَ وَرُبَاعَ ۖ فَإِنْ خِفْتُمْ أَلَّا تَعْدِلُوا فَوَاحِدَةً أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُكُمْ ۚ{3}

“…Basi oweni mnaowapenda katika wanawake, wawili au watatu au wanne; lakini kama mkiogopa kuwa hamuwezi kufanya uadilifu basi (oweni) mmoja au waliom likiwa na mikono yenu…” (4:3)

Kuhusu Mulk-e-Yamin (watumwa), Allah anasema:

وَمَنْ لَمْ يَسْتَطِعْ مِنْكُمْ طَوْلًا أَنْ يَنْكِحَ الْمُحْصَنَاتِ الْمُؤْمِنَاتِ فَمِنْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُكُمْ مِنْ فَتَيَاتِكُمُ الْمُؤْمِنَاتِ ۚ وَاللَّهُ أَعْلَمُ بِإِيمَانِكُمْ ۚ بَعْضُكُمْ مِنْ بَعْضٍ ۚ فَانْكِحُوهُنَّ بِإِذْنِ أَهْلِهِنَّ وَآتُوهُنَّ أُجُورَهُنَّ بِالْمَعْرُوفِ مُحْصَنَاتٍ{25}

“Na miongni mwenu asiyeweza kupata mali ya kuoa wanawake waungana wa Kiislamu, basi aowe katika wajakazi wenu wa Kiislamu mliowamiliki; na Allah anajua sana imani yenu. Baadhi yenu mnatokana na baadhi, basi waoeni kwa idhini ya watu wao na muwape mahari yao kwa haki…” (4:25)

Ile amri katika aya ya 24 ya sura Nisa inayosema: “…Na kwa wale ambao mmestarehe nao katika wao, basi wapeni mahari yao yaliyolazimu…”

ilikuwa kwa ajili ya mut’a, au ndoa ya muda. Isingeweza kuwa kwa ajili ya ndoa ya kudumu, kwani vinginevyo, ingemaanisha kwamba katika sura hiyo hiyo amri inayohusu ndoa ya kudumu imerudiwa mara mbili, ambayo ni kinyume cha kanuni, na kama ni kwa ajili ya mut’a, basi kwa dhahiri ni amri ya kudumu na iliyo tofauti (na ndoa nyingine).

Pili, sio Mashi’a tu bali Waislamu wote wanakubali kwamba mut’a ilikuwa ikifanyika wakati wa siku za mwanzo za Uislamu. Masahaba mashuhuri waliifanya wakati wa uhai wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Kama aya hii inaashiria ndoa ya kudumu, basi ni ipi aya kwa ajili ya mut’a? kwa dhahiri hii ndio aya inayohusu mut’a, ambayo wafasir wenu wenyewe wameikubali. Hakuna aya katika Qur’ani Tukufu ambayo inaifuta amri hii.

Ahli-Sunna Wazingatia Uhalali Wa Mut’a

Imesimuliwa katika Sahih Bukhari na Musnad ya Imam Ahmad Ibn Hanbal, kutoka kwa Abu Raja kutoka kwa Imran Ibn Hasin, kwamba aya ya mut’a iliteremshwa katika Kitabu cha Allah.

Hivyo tulifanya (mut’a) kwa mujibu wake wakati wa uhai wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). hakuna aya iliyoteremshwa kuifanya haramu, wala kamwe Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hajaikataza. Mtu mmoja aliamua kuibadilisha amri hii. Bukhari anasema kwam- ba mtu huyo alikuwa ni Umar.”

Muslim katika Sahih yake Jz. 1, katika sura ya Nikatu’l-Mut’a, anasema: “Hasan Halwa’i alitusimulia kwamba, aliambiwa na Abdu’r-Razzaq, ambaye alijulishwa na Ibn Jarih, ambaye alielezwa na ‘Ata kwamba Jabir Ibn Abdullah Ansari alikuja Makka kwa ajili ya Umra na walikwenda nyumbani kwake alikofikia. Watu walimuuliza maswali mengi.

Wakati walipokuja kwenye suala la mut’a, yeye alisema: ‘Ndio, tulizoea kufanya mut’a wakati wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na wakati wa ukhalifa wa Abu Abkr na Umar.’”

Vile vile katika kitabu hicho hicho Jz. 1, katika sura ya al-Mut’a Bi’l-Hajj wa’l-Umra, inasimuliwa kutoka kwa Abu Nazara kwamba alisema: “Nilikuwa pamoja na Jabir Ibn Abdullah Ansari wakati mtu mmoja alipokuja na kusema: ‘kuna tofauti ya maoni kati ya Ibn Abbas na ibn Zubair kuhusu hizi mut’a mbili, Mut’atu’n-Nisa na Mut’atu’l-Hajj.’ Kisha Jabir akesema: ‘Tumezifanya zote hizo wakati wa uhai wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Baada ya hapo, wakati Umar alipozikataza, hatukuweza kuzifanya.’”

Imam Ahmad Bin Hanbal katika Musnad yake, Jz. 1, uk. 25, anasimulia riwaya ya Abu Nazara katika njia nyingine. Vile vile wote wanasimulia riwaya nyingine kutoka kwa Jabir kwamba yeye alisema:

“Katika siku za uhai wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na Abu Bakr, tulizoea kufanya mut’a kwa makubaliano ya kiganja cha tende na unga mpaka Umar alipoikataza katika suala la Amr Bin Harith.”

Hamid, katika Jam’-e-Bainus-Sahihain, anasimulia kutoka kwa Abdullah Ibn Abbas kwamba alisema: “Tulizoea kufanya mut’a wakati wa uhai wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Wakati Umar alipokuwa Khalifa akasema: ‘Allah swt., alifanya chochote alichokitaka kwa ajili ya Mtume Wake. Sasa amekufa, na Qur’ani inachukuwa mahala pake. Hivyo wakati ukianza Hajj au Umra, lazima uzimalize kama Allah alivyokuamuruni. Lazima mtubie na mjiepushe kufanya mut’a, nileteeni yule aliyefanya mut’a ili niweze kumpiga mawe.’”

Kuna riwaya nyingi kama hizo katika vitabu vyenu wenyewe vya kuaminika zikionesha kwamba mut’a iliruhusiwa wakati wa uhai wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Masahaba waliifanya mpaka Umar alipoiharamisha. Mbali na riwaya hizi, baadhi ya masahaba, kama Ubayy ibn Ka’b, ibn Abbas, Abdullah ibn Mas’ud, Sa’id ibn Jabir na Sa’d wamesoma aya ya mu’ta katika njia hii: “…na kwa wale ambao mmefanya nao mut’a mpaka muda uliowekwa…”

Jarullah Zamakhshari anasimulia katika Kashshaf kutoka kwa kwa Ibn Abbas na vile vile Muhammad Bin Jarir Tabari katika Tafsir-e-Kabir na Imam Fakhru’d- din Razi katika Tafsir-e-Mafatihu’l-Ghaib, Jz. 3, wakiandika kuhusu aya hii tukufu na Imam Nuwi katika Sharh-e-Muslim, Sura ya 1, Nikatu’l-Mut’a anasimulia kutoka kwa Nazari kwamba Qadhi Ayaz alieleza kwamba “Abdullah Bin Mas’ud, yule mwandishi wa Wahyi, alizoea kusoma aya hii katika njia hiyo hiyo, yaani, ‘mpaka muda uliowekwa.’”

Imam Fakhru’d-din Razi, baada ya kunukuu maelezo ya Ubayy Ibn Ka’b na Ibn Abbas, alisema: “Umma haukukataa usomaji wao wa aya katika njia hii, hivyo tulichokisema kimekubaliwa kwa ijma (makubaliano ya wote pamoja).”

Tena katika ukurasa ufuatao anajadili kwa namna hii: “Usomaji huu kwa dhahiri huthibitisha kwamba mut’a inayo idhini ya kidini. Hatuna tofauti ya maoni kwamba mut’a iliruhusiwa katika wakati wa uhai wa Mtukufu Mtume.”

Amri Inayoruhusu Mut’a Haikufutwa

Sheikh: Unaweza kuthibitisha kwamba ilikuwa halali wakati wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na kwamba haikufutwa baadae?

Muombezi: Kuna ushahidi mwingi kwamba amri hii haikufutwa. Hoja yenye kuvutia sana ni kwamba mut’a iliruhusiwa kuanzia wakati wa uhai wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mpaka katikati ya ukhalifa wa Umar.

Maelezo ya Khalifa Umar mwenyewe yamesimuliwa kwa jumla na maulamaa wenu. Wameandika kwamba alipanda kwenye mimbari na akasema:

“Katika wakati wa Mtume mut’a mbili ziliruhusiwa. Mimi ninazifanya zote mbili hizi kuwa ni haramu, na kama mtu yeyote atazifanya, nitamuadhibu.”

Sheikh: Unachosema ni sahihi, lakini nukta yangu ni kwamba kuna amri nyingi ambazo zilikuwa zikitumika mwanzo katika wakati wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), lakini baadae zikafutwa. Mut’a vile vile iliruhusiwa wakati wa mwanzo, lakini baadae ikapigwa marufuku.

Muombezi: Kwa vile asili na msingi wa dini ni Qur’ani Tukufu, kama amri yoyote inakuwemo ndani ya Qur’ani ufutaji wake lazima vile vile uwe ndani yake. Sasa tafadhali nifahamishe ni wapi katika Qur’ani ambapo amri hii imefutwa.

Sheikh: Katika Sura ya 23, Mu’minin, aya ya 6 inafuta amri hii. Inasema: “Isipokuwa kwa wake zao au kwa (wanawake) wale waliomilikiwa na mikono yao, basi hao si wenye kulaumiwa.” (23:6) Aya hii inaweka masharti mawili kwa ajili ya uhusiano wa kinyumba: ndoa au kuingiliana (kijamiiana) na mtumwa. Hivyo aya hii inathibitisha kwamba amri ya mut’a ilifutwa.

Muombezi: Aya hii kwa njia yoyote haithibitishi kwamba mut’a ilifutwa; bali inaithibitisha. Mwanamke aliyeunganishwa na mut’a ni mke halisi wa mwanaume huyo. Lau asingekuwa mke wake halisi, Allah asingeamrisha mahari yake ilipwe.

Aidha, sura ya al-Mu’minin iliteremshwa wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) yuko Makka, Sura ya Nisa iliteremshwa wakati akiwa Madina. Ni dhahiri kwamba Sura za Makka zilitangulia zile za Madina. Je, inawezekana aya A kufuta aya B, ikiwa aya A ilikuja kabla ya B?

Masahaba Maarufu Na Imam Malik Wanasisitiza Kwamba Amri Ya

Mut’a Haijafutwa

Abdullah Ibn Abbas, Abdullah Ibn Mas’ud, Jabir Bin Abdullah Ansari, Salama Ibn Akwa, Abu Dharr Ghifari, Subra Bin Ma’bad, Akwa Bin Abdallah al-Aslami na Imran Bin Hasin wameeleza kwamba amri ya mut’a haijafutwa. Aidha, maulamaa wenu maarufu wamethibitisha kwamba haijafutwa.

Kwa mfano, Jarullah Zamakhshari, katika Tafsir-e-Kashshaf kuhusiana na maelezo ya Abdullah Ibn Abbas kwamba aya ya mut’a ilikuwa ni moja ya amri za wazi za Qur’ani Tukufu, anasema kwamba aya hii haijafutwa. Imam Malik Bin Anas vile vile alisema kwamba uruhusiwaji ya mut’a haukufutwa.

Mulla Sa’idu’d-din Taftazani katika Sharh-e-Maqasid, Burhanu’d-din Hanafi katika kitabu chake, Hidaya, Ibn Hajar Asqalani katika Fathu’l-Bari na wengine vile vile wamesimulia ile kauli na hukumu ya Malik ambaye anasema: “Mut’a ni halali. Imeruhusiwa na dini.

Uhalali wake, kwa ilivyothibitishwa na Ibn Abbas, hujulikana sana na wengi wa masahaba wake kutoka Yeman na Makka walikuwa wakiifanya.” Katika sehemu nyingine anase- ma: “Mut’a ni halali kwa vile imeruhusiwa, na uhalali wake na ruhusa yake imethibiti mpaka iwe imefutwa.” Utaona kwamba mpaka Malik alipokufa kulikuwa hakuna ushahidi kwamba amri ya mut’a imefutwa.

Aidha, wafasiri wenu maarufu, kama Zamakhshari, Baghawi, na Imam Tha’labi wamefuata msimamo wa Ibn Abbas na masahaba wengine maarufu na wameamini katika uhalali wa mut’a.

Masharti Yote Ya Ndoa Yanatimizwa Katika Ndoa Ya Mut’a

Sheikh: Kwa vile hakuna masharti kwa mwanamke aliyeunganishwa katika mut’a, kama vile urithi, talaka baada ya muda kwisha na kumkimu, kama ilivyo muhimu kwa mke, hawezi kuwa mke halisi.

Muombezi: Mwanamke aliyeunganishwa na mwanaume kwa mut’a, analindwa na masharti yote ya mke yeyote isipokuwa yale ambayo kimantiki yameondolewa. Mut’a ni aina ya ndoa, ambayo kwayo mwanamke anastahiki kuwa mke halisi. Kama mambo yalivyo kwa ajili ya ustawi wa umma na kuwaokoa kutokana na uvunjaji wa sheria, baadhi ya masharti na taratibu zimeondolewa.

Ama kuhusu masharti yake, kwanza, haikuthibishwa kwamba urithi ni sharti la muhimu katika ndoa. Wanawake wengi, pamoja na kuwa wake, hawapati urithi kutoka kwa waume zao. Kwa mfano, wake wasio watiifu au wale wanaouwa wananyimwa urithi.

Pili, haikuthibitishwa kwa uhakika iwapo mwanamke aliyeunganishwa katika mut’a ananyimwa haki yake ya urithi. Wanachuo wa sheria wanahitalifiana katika maoni juu ya hili, na tofauti kama hizi zipo pia miongoni mwenu.

Tatu, maulamaa wa Imamiyya kwa kauli moja wanashikilia mtazamo wa kwamba mwanamke aliyeunganishwa katika mut’a vile vile lazima akae edda. Ufupi wake umewekwa kwamba ni siku 45.

Kama mume akifariki itambidi huyo mke akae edda ya kawaida ya miezi mine na siku kumi, awe amewahi kujamiana na mume wake au la, au iwapo amevuka umri wa kupata haidhi au la.

Nne, haki ya kumkimu sio sharti la muhimu liloambatanishwa kwenye ndoa. Kuna idadi ya wake ambao hawastahili matumizi ya kukimiwa, kama vile wale ambao sio watiifu au ambao wamewauwa waume zao.

Tano, kwisha kwa muda uliokubaliwa kwenyewe ni talaka. Halikadhalika, kwa ridhaa ya mume wake, anaweza kuachika kabla ya muda kwisha.
Kwa hiyo, hakuna katika masharti uliyotaja aambalo lina nguvu yoyote ya kisheria. Mwanachuoni maarufu wa Shia, Allama Jamalu’d-Din Hilli (Hasan bin Yusuf Bin Ali Bin Mutahhari), alitoa katika maelezo marefu hoja hiyo hiyo kwa majibu ya mitazamo ya ulamaa wenu maarufu.

Nimeyataja kwa ufupi. Anayetaka kusoma kwa urefu, anaweza kuan- galia kitabu cha Allama Hilli, Mabahithat-e-Sunniyya wa Ma’rifat-e-Nussariyya.

Je, Amri Ya Qur’ani Juu Ya Mut’a Ilifutwa Na Mtukufu Mtume?

Sheikh: Mbali na aya hii tukufu vile vile kuna idadi kubwa ya hadithi ambazo zinazsema kwamba amri inayohusiana na mut’a imefutwa wakati wa uhai wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Muombezi: Tafadhali tufahamishe amri hiyo ya kufuta.

Sheikh: Imesimuliwa pamoja na tofauti fulani. Baadhi ya wasimuliaji wanasema kwamba ilifutwa siku ya kutekwa kwa Khaibar, baadhi wanasema ilitokea katika siku ya kutekwa Makka, baadhi wanasema kwamba ilikuwa wakati wa hija ya mwisho, na baadhi wanasema kwamba ilikuwa katika siku ya Tabuk. Wengine, hata hivyo, maoni yao ni kwamba amri hiyo ya kufuta ilitolewa siku ya Umratu’l-Qadhwa (Hija ya mwago).

Hoja Zinazohusu Kufutwa Kwake Wakati Wa Uhai Wa Mtume

Muombezi: Hizo riwaya zinakinzana zenyewe zinathibitisha wazi kwamba kulikuwa hakuna amri ya kufutwa. Na vipi riwaya hizo zitaaminika wakati kinyume chake kuna hadithi nyingi zilizosimuliwa katika Sahih-e-Sitta: Jam-e-Bainus-Sahihain, Jam-e- Bainus-Sahih-e-Sitta, Musnad, nk., kutoka kwa masahaba maarufu ambazo zinathibitisha kwamba aya hii haikufutwa mpaka wakati wa ukhalifa wa Umar.

Hoja ya kuvutia sana ambayo maulama wenu wenyewe wameinukuu ni ile kauli ya Khalifa Umar, ambaye alisema: “Naziharamisha zile mut’a mbili ambazo zilikuwa zikitumika wakati wa uhai wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).”

Lau kungelikuwa na aya, au amri ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), Khalifa angelisema: “Kwa mujibu wa maelekezo ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), ambayo yanaungwa mkono na aya ya Qur’ani, kama mtu atafanya kitendo cha haramu kwa kuvunja amri iliyofutwa, mimi nitamuadhibu.”

Maelezo kama haya yangekuwa zaidi sana yenye kuvutia kwa watu. Lakini alisema tu: Mut’a mbili zilikuwa zimeruhusiwa wakati wa uhai wa Mtume, mimi naziharamisha.”

Hata hivyo, kama madai yako ni sahihi na aya ya mut’a ilifutwa, kwanini wanafunzi wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), kama Abdullah Ibn Abbas, Imran Bin Hashim na masahaba wengine waliifanya? Muhadithina na wanahistoria wenu wakubwa, ikiwa ni pamoja na Bukhari na Muslim, wameandika habari hii.

Taarifa zote hizi zinathibitisha kwa uwazi kwamba kutoka wakati wa uhai wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mpaka wakati wa ukhalifa wa Umar masahaba walifuata sheria hii.

Je, Khalifa Umar Angeweza Kuifuta Mut’a?

Hivyo, ni wazi kwamba mut’a itaendelea kuwa halali daima. Abu Isa Muhammad Bin Sawratu’t-Tirmidhi katika Sunan yake, ambayo inachukuliwa na ninyi kama moja ya Sahih sita, Imam Ahmad Bin Hanbal katika Musnad yake, sehemu ya 2, uk. 95, na Ibn Athir katika Jam’u’l-Usul wamesimulia kwamba mtu mmoja wa Syria alimuuliza Abdullah Bin Umar Bin Khattab anachofikiria kuhusu Mut’a-e-Nisa. Yeye akasema: “Bila shaka, ilivyo hiyo ni halali.”

Yule mtu akasema tena: “Lakini baba yako, Khalifa, alikataza watu kuifanya.” Akasema: “Iliamriwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.); hivyo, kama imekatazwa na baba yangu amri hiyo haiwezi kuizidi amri ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Mimi ni mfuasi wa amri ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).”

Ama kwa riwaya ambazo zimesimuliwa, huenda watu walighushi hadithi baadae ili kuunga mkono kauli ya Umar. Suala hili liko wazi kiasi kwamba halihitaji ufafanuzi wa zaidi. Ukweli ni kwamba huna ushahidi wa kweli juu ya uharamu wa mut’a isipokuwa ile kauli ya Khalifa Umar.

Sheikh: Kauli ya Khalifa Umar yenyewe ni ushahidi wenye nguvu sana kwa ajili ya Waislamu, na lazima waifuate. Kama alikuwa hakuisikia kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) asingeweza kuisema.

Muombezi: Je, kauli ya Khalifa Umar ni ya kushurutisha kiasi hicho kwamba Waislamu lazima waifuate? Sijaona hadithi hata moja kwenye vitabu vyenu, ambayo kwayo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema kwamba kauli ya Umar Bin Khattab ilikuwa ni chanzo kilichothibitishwa au kwamba Waislamu lazima waifuate.

Kwa upande mwingine vitabu vyenu vimejazwa hadithi za kuaminika zinazosema kwamba lazima tufuate kizazi cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), hususan Ali. Nimzitaja baadhi ya hadithi hizi katika mikesha iliyopita. Hao Ahlul’l-Bayti wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wamesema kwamba amri ya mut’a haikufutwa.

Umesema kwamba lau kama Khalifa Umar asingesikia amri hiyo ya kufuta mut’a kutoka Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), asingesema aliyoyasema. Lakini hili ni rahisi kulikanusha. Kwanza, kama Khalifa Umar alikuwa amesikia juu ya ufutwaji wa amri ya mut’a kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), angeisimulia wakati wa uhai wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mpaka wakati wa ukhalifa wake mwenyewe.

Hii ingekuwa na umuhimu maalum kwa vile aliwaona masahaba mashuhuri walikuwa wakiifanya, na ilikuwa ni wajibu wake kuwaeleza watu kwamba matumizi ya mut’a yalikuwa yamefutwa. Kwanini hakutekeleza jukumu la kuzuiya uovu?

Pili, matumizi ambayo yalikuwepo miongoni mwa umma kwa amri ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), yangeweza tu kufutwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Kusingekuwa na ucheleweshaji katika suala hili. Je, inaingia akilini kwamba kama amri kwa ajili ya umma ilikuwa imekwisha kusambazwa na baadae ikafutwa, je, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) asingezungumza kwa mtu yeyote isipokuwa kwa Umar?

Na je, ingeleta maana yoyote kwamba Umar asingemuambia mtu yeyote mpaka baadae katika ukhalifa wake mwenyewe? Katika kipindi chote hiki wakati umma ukiendelea kufuata amri hii (inayodai- wa) iliyofutwa, je, hakukuwa na uwajibikaji kwa upande wa Umar?

Unasema kwamba ukatazaji wa matumizi “yaliyofutwa na yasiyo ya kidini” usingeweza kufanywa ujulikane kwa watu wengine na kwa hiyo umma uliendelea kuyafuata. Je, mtu mwingine yeyote yule mbali na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anaweza kuwajibishwa kwa sababu ya kutokutangaza amri iliyofutwa, akiwa yeye kamuambia Umar peke yake tu? Je, sio ukafiri kusema kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amepuuza kutekeleza kazi yake na kwamba umma kwa sababu ya kutokujua kwao, waliendelea kutenda amri iliyofutwa kwa muda mrefu?

Tatu, kama amri ya mut’a ilikuwa imefutwa wakati wa uhai wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na Umar alikuwa amelisikia hili kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), Umar angelisema wakati alipokuwa analikataza hili kwamba yeye mwenyewe amemsikia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akisema kwamba matumizi ya mut’a yamepigwa marufuku. Ni dhahari, kama angekuwa anarejea kauli ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), umma ungevutiwa mno na hilo.

Lakini alisema: “Wakati wa uhai wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), mut’a mbili zilikuwa zimeruhusiwa, lakini mimi ninaziharamisha. Sasa nitawapiga mawe wale wanaoifanya.”

Je, sio jukumu la Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kutangaza vitu kuwa ni halali au haramu? Au, inaweza kuwa haki ya Khalifa ambaye alichaguliwa na watu?

Sielewi ni kwa misingi ipi Umar alitangaza kuharamisha kile alichohalalisha Allah swt. Ajabu iliyoje Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mwenyewe kamwe hajasema kwamba amekifanya kitu fulani kuwa halali au haramu. Wakati wowote alipotangaza amri yeyote, alisema kwamba Allah alimuamrisha kuifikisha kwa watu. Ujasiri ulioje alikuwa nao Umar aliposema: “Mut’a mbili zilikuwa zimeruhusiwa wakati wa uhai wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Mimi nazifanya zote hizo kuwa haramu. Nitawaadhibu wale ambao wanatenda matendo hayo.”

Amri Ya Allah Au Ya Mtukufu Mtume Haiwezi Kufutwa Na Khalifa

Sheikh: Kwa hakika unafahamu kwamba baadhi ya wanachuoni wetu wenye ilmu ya juu wanaamini kwamba kwa vile Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa mujtahid katika masuala ya amri za kidini, mujtahid mwingine kwa mujibu wa utafiti wake mwenyewe, anaweza kuweka kando amri iliyotangulia. Ni kwa msingi huu kwamba Umar alisema: “Naviharamisha vitu viwili hivyo.”

Muombezi: Katika kujaribu kuweka sawa kosa moja unafanya makosa mengine mengi. Je, ijtihad ina maana yoyote katika kukanganya amri yoyote ya Qur’ani Tukufu. Je, kauli yako hiyo sio ya kichekesho kabisa na inayopingana na aya za Qur’ani? Allah swt., anasema katika Sura ya Yunus:

قُلْ مَا يَكُونُ لِي أَنْ أُبَدِّلَهُ مِنْ تِلْقَاءِ نَفْسِي ۖ إِنْ أَتَّبِعُ إِلَّا مَا يُوحَىٰ إِلَيَّ ۖ{15}

“…Sema: siwezi kuibadilisha kwa hiari ya nafsi yangu. Sifuati ila ninayofunuliwa kwa wahyi…”
(10:15)

Ni kweli kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hawezi akafanya mabadiliko yoyte katika amri za dini isipokuwa mpaka aamrishwe na Allah kufanya hivyo. Vipi, amewezaje Umar, ambaye hana ujuzi wa Wahyi, kuwa na mamlaka ya kufanya haramu kile ambacho Allah amekifanya halali?

Katika Suratun-Najm Allah anasema:

وَمَا يَنْطِقُ عَنِ الْهَوَىٰ {3}

إِنْ هُوَ إِلَّا وَحْيٌ يُوحَىٰ {4}

Wala hazungumzi kwa matamanio ya nafsi yake. Hayakuwa haya ila ni wahyi ulioteremshwa. (53:3-4)

Katika Surat Ahqaf, Allah anasema:

قُلْ مَا كُنْتُ بِدْعًا مِنَ الرُّسُلِ وَمَا أَدْرِي مَا يُفْعَلُ بِي وَلَا بِكُمْ ۖ إِنْ أَتَّبِعُ إِلَّا مَا يُوحَىٰ إِلَيَّ وَمَا أَنَا إِلَّا نَذِيرٌ مُبِينٌ {9}

“Sema: mimi sio wa kwanza katika mitume, wala sijui nitakayofanywa mimi wala mtakayofanywa ninyi. Sifuati ila niliyoteremshiwa kwangu, na mimi siye ila ni muonyaji dhahiri. (46:9)

Utii kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ni wajibu. Hakuna yeyote, awe Umar au mtu mwingine yeyote, aliye na haki ya kuingilia amri za Mungu na kufanya haramu alichokifanya Allah halali.

Manufaa Hayawi Msingi Kwa Ajili Ya Ufutaji

Sheikh: Kwa hakika Umar aliona inafaa na akaichukulia katika masilahi bora ya watu kuifuta amri ile. Tunaona siku hizi kwamba baadhi ya watu wanamchukua mwanamke katika mut’a kwa ajili ya kustarehe tu kwa muda wa saa moja, mwezi mmoja, au mwaka mmoja. Baadae bila kujali kama mwanamke ni mjamzito au la, wanamtelekeza.

Muombezi: Huu ni mzaha mkubwa! Uhalali huu wa amri ya Kiislamu unahusiana nini na watu wanaojiingiza katika uhusiano wa kujamiiana kuliko haramu? Kama tukifuata hiyo mantiki yako, huenda hata ndoa ya kudumu itafanywa kuwa haramu.

Kwani kuna watu wanawaoa wasichana wazuri wenye heshima zao kwa ajili ya pesa zao au urembo wao na baadae huwaacha bila kuwapa msaada wowote wa kifedha. Kwa vile baadhi ya watu wanafanya hivi, unafikiri ndoa ya kudumu lazima ifutwe?

Hapana. Lazima tuwahimize watu kuwa wanyofu na kuwapa mafunzo sahihi ya duni. Kama mtu mnyofu atajikuta hana uwezo wa kubeba jukumu la kuwa na mke wa kudumu, na kama anataka kuepuka kitendo
cha haramu, atakuwa kwa kuafikiana na sheria ya dini, anataka kuchukua mwanamke katika mut’a au ndoa
ya muda.

Kwa hiyo, atataka kujua masharti ya mut’a kwa sababu anajua kwamba kwa kila amri kuna masharti fulani. Wakati wa makubaliano ya wote wawili, atatoa kile kiasi cha mahari kwa ajili ya mwanamke ambacho kitatosha kwa matumizi ya kumkimu wakati wa edda, ambao ni siku 45, baada ya muda wa kipindi cha mut’a kwisha.

Pili, baada ya kutengana, atamuangalia mwanamke wakati wa kipindi chote cha edda. Kama atakuwa mjamzito, atamtunza mama huyo sawa sawa ili aweze kumchukua mtoto wake atakapo zaliwa. Kama baadhi ya watu wanashindwa kufuata masharti haya, haina maana kwamba amri ya halali ya kisheria imefutwa.

Ustawi wa umma ulikuwa unajulikana vizuri kwa Allah na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kuliko Umar. Na hawakukataza mut’a. Kama wao hawakuikataza, hakuna Khalifa au Imam, au mtu yoyote yule, hata aliyeteuliwa na Mungu, anayeweza kwa hiyari yake mwenyewe kukifanya haramu kile Allah alichokifanya halali. Hivyo madai yako kwamba ilikuwa ni kwa masilahi ya umma kwamba watu waache mut’a, hayathibitiki.

Mut’a haikuwa ndio sababu ya kuenea kwa uvunjaji wa sheria; bali ilikuwa ni kupigwa marufuku kwake ndiko ambako kumeeneza uzinifu.

Wale vijana wa kiume na wa kike ambao hawakumudu kuungana katika ndoa ya kudumu kama hawawezi kujidhibiti na kuzuia hamu zao za kujamiiana, watajiingiza katika ngono haramu. Na kama mambo yalivyo kuenea kwa zinaa na uasherati huharibu maadili mema ya mataifa yote kabisa.

Imam Tha’labi na Tabari katika Tafsir zao na Imam Ahmad Bin Hanbal katika Musnad yake, wakiandika kuhusiana na aya ya mut’a, wanasimulia kutoka kwa Amiru’l-Mu’minin Ali kwamba alisema: “Kama Umar asingezuia mut’a hakuna mtu yeyote, isipokuwa mwanaume mwenye bahati mbaya, angefanya uzinifu.”

Vile vile Ibn Jarih na Amr Bin Dinar wanasimulia kutoka kwa Abdullah Ibn Abbas ambaye alisema: “Kwa hakika mut’a ni rehema ya Allah, ambayo ameitoa kwa umma wa Muhammad. Kama Umar asingeipiga marufuku, hakuna mtu yeyote isipokuwa mtu mwenye bahati mbaya angefanya uzinifu.”

Hivyo, kwa mujibu wa maoni ya masahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), sababu hasa ya kuenea kwa uzinifu ilikuwa ni kukatazwa kwa mut’a, na si kwa ajili ya kuifanya. Kwa hakika amri zote za Mungu zinazohusu halali na matendo ya halali ambazo zimewasilishwa kwa umma kupitia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) zilikusudiwa kwa ajili ya ustawi wa watu. Bado zinaendelea kuwanufaisha watu hadi hii leo.

Imani Ya Abu Talib Ilikuwa Inajulikana Sana Wakati Wa Mtukufu Mtume

Mada yetu ya kujadali haikuwa hii, lakini nilitaka kuondoa shaka yenu kwa vile umesema kwamba kile kilichokuwa kinajulikana wakati wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kinawezakikafanywa kuwa bure kabisa kupitia hadithi za kughushi. Halikadhalika hakuna uhalali katika kukataa kwako kuhusiana na imani ya Abu Talib.

Imani yake wakati wa uhai wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ilikuwa vile vile inajulikana sana na kuchukuliwa kwa heshi- ma. Lakini kwa kubuni hadithi ya Zahza, baadhi ya watu wakaeneza riwaya za kinyume kabisa. Watu wasio na ujuzi, wakiwafuata wakubwa zao kibubusa, wakazikubali riwaya hii ya uwongo.

Kwa ufupi, nilichosema kinathibitisha vya kutosha na zaidi kwamba Ali alitokana na familia bora kiasi kwamba hakuna yeyote katika masahaba maarufu anayeweza kulingana naye.

Mahali Alipozaliwa Ali Ilikuwa Ni Ndani Ya Ka’aba

Dalili nyingine ya hadhi maalum ya Ali ilikuwa ni mahali alipozaliwa. Hakuna mtu mwingine yeyote, kuanzia kwa Adam kuja chini kupitia mitume wote, aliyekuwa na sifa hii.

Kati ya wanadamu wote, ni yeye peke yake aliyezaliwa katika eneo takatifu la Ka’aba. Wakati wa kuzaliwa kwa Nabii Isa, mama yake mashuhuri alilazimika kutoka kwenye nyumba takatifu. Sauti ilimuambia: “Ewe Maiamu! Toka humo Baitu’l-Muqaddas, kwa vile ni sehemu ya kufanyia ibada na sio ya kuzalia watoto.”

Lakini wakati wa kuzaliwa Ali ulipokaribia, mama yake, Fatima Bint Asad, aliambiwa kuingia ndani ya Kaaba. Na hii haikuwa jambo la bahati kana kwamba mwanamke alikuwa ndani msikiti na ghafla akajifungua mtoto. Yeye aliitwa makhsusi kabisa kuingia ndani ya Kaaba, ambayo mlango wake ulikuwa umefungwa. Baadhi ya watu wasio na ujuzi wanafikiri kwamba Fatima Bint Asad alikuwa ndani ya Msikiti Mtukufu wakati aliposikia uchungu wa kuzaa, hakuweza kutoka nje, na akajifungua mtoto.

Ukweli ulikuwa ni kinyume cha hivyo. Ulikuwa ni mwezi wa Fatima Bint Asad wa kujifungua. Alikwenda Masjidu’l-Haram, ambako alisikia uchungu wa uzazi. Alimuomba Allah katika eneo takat- ifu la Kaaba akisema: “Ewe Allah! Nakuomba kwa jina la heshima Yako na kwa unyenyekevu, kunipunguzia uchungu huu wa uzazi.” Ghafla ukuta wa Kaaba, ambao ulikuwa mzima kabisa, ulitoa mwanya.

Riwaya nyingine inasema kwamba sauti ilisikika ikisema: “Ewe Fatima! Ingia ndani ya Nyumba (al-Ka’aba).” Fatima akaiingia ndani ya Nyumba ya Allah, mbele ya kundi la watu ambao walikuwa wamekaa pembeni mwa sehemu hiyo, ukuta wa Kaaba ulipasuka na Fatuma Bint Asad aliingia ndani kisha ukuta ule ukarudia hali yake ya kawaida. Watu wal- ishangazwa sana.

Abbas vile vile alikuwepo pale. Wakati alipoona kilichotokea, mara moja akamuambia Abu Talib kwa sababu alikuwa nazo funguo za mlango. Mara moja alikuja pale na akajaribu kwa bidii zake zote kufungua mlango, lakini mlango haukufunguka. Kwa muda wa siku tatu Fatima Bint Asad alibakia ndani ya Kaaba, inavyoonekana bila chakula cha aina yoyote.

Tukio hili lisilokuwa la kawaida likawa ni gumzo la mjini hapo. Hatimaye, katika siku tatu, sehemu aliyopitia ilifunguka tena, na Fatima akatoka nje. Watu wakaona kwamba alikuwa amepakata mtoto mzuri mikononi mwake. Madhehebu zote (Shia na Sunni) wanakubali kwamba hakuna mtu mwingine yeyote ambaye amewahi kupewa sifa kama hiyo kamwe.

Hakim katika Mustadrak yake na Nuru’d-din Bin Sabbagh Malik katika Fusulu’l-Muhimma, Fasl ya 1, uk. 14, anasema: “Hakuna yeyote kabla ya Ali aliyezaliwa ndani ya Kaaba. Hii ilikuwa ni sifa aliyopewa Ali ili kuzidisha ubora wa hes- hima, cheo, na hadhi yake.”

Asili Ya Jina La Ali Ilikuwa Ni Ulimwengu Usioonekana

Dalili nyingine ya hadhi maalumu ya Ali ni kwamba jina lake lilikuwa na asili katika ulimwengu usioonekana.

Sheikh: Umesema kitu kigeni. Hii ina maana Abu Talib alikuwa Mtume ambaye alimpa jina Ali kupitia msukumo wa ki-Mungu. Kauli yako ni moja kati ya ule uwongo ambao Mashi’a wameutunga katika mapenzi yao yaliyovuka mpaka (ghulu) kwa Ali.

Lakini ni kichekesho kusema kwamba Allah aliamuru kwamba mtoto huyo aitwe Ali. Ali lilikuwa ni jia la kawaida ambalo wazazi hao kwa utashi wao, walipanga kumpa mtoto wao. Halikuwa na cho chote cha kuhusiana na ulimwengu wa ghaibu.

Muombezi: Kitu nilichosema hakina ugeni ndani yake. Kustaajabu kwako kunatokana na kukosa ujuzi kwako kuhusu ustahili na sifa ya wilaya (uandamizi).

Kwanza, wewe unafikiri kwamba mtoto huyo alipewa jina baada ya kuzaliwa kwake, ingawaje haikuwa hivyo. Katika vitabu vyote vitakatifu, majina ya Muhammad na Ali yametajwa.

Allah swt., aliwapa majina miaka elfu kadhaa kabla ya uumbaji wa ulimwengu. Majina haya yaliandikwa mbinguni, kwenye milango ya mbingu na kwenye Arsh. Hayahusiani cho chote na wakati wa Abu Talib.

Sheikh: Hakika kauli hii ni mfano wa mapenzi yaliyovuka mpaka juu ya Ali. Umempandisha juu mno kiasi kwamba unadai kwamba jina lake liliandikwa zamani mno kabla ya kuumbwa ulimwengu. Matokeo ya kauli kama hizi ni kwamba wanachuo wenu wanachukulia kulitaja jina la Ali baada ya jina la Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) katika adhana.

Muombezi: Hapana, bwana, kauli yangu haihusiani na mapenzi ya kuvuka mpaka. Na sio mimi niliyeandika jina lake mbinguni. Allah aliamrisha jina la Ali liandikwe pamoja na Jina Lake na jina la Mtume Wake.

Sheikh: Tafadhali taja yoyote katika hadithi hizo.

Baada Ya Majina Ya Allah Na Mtukufu Mtume Jina La Ali Limeandikwa Juu Ya Arsh

Muombezi: Muhammad Bin Jarir Tabari katika Tafsiir yake, Ibn Asakir katika Ta’rikh yake, Muhammad Bin Yusuf Ganji Shafi’i, katika Kifayatut-Talib, sura ya 62, Hafidh Abu Nu’aim, katika Hilyatu’l-Auliya, na Sheikh Sulaiman Balkhi Hanafi katika Yanabiu’l- Mawadda, uk. 238, sura ya 56, hadithi ya 52, wanasimulia kutoka kwenye Dhakha’iru’l- Uqba ya Imam’l-Haram Ahmad Bin Abdullah Tabari Shafi’i kutoka kwa Abu Huraira (pamoja na tofauti kidogo maneno) kwamba Mtukufu Mtukufu alisema: “Imeandika juu ya Arsh kwamba, ‘Hakuna mungu ila Allah, Mmoja Ambaye hana mshirika; na Muhammad ni Mjumbe na Mtume Wangu, ambaye nimemuimarisha kupitia kwa Ali Bin Abi Talib.’”

Vile vile katika Khasa’isu’l-Kubra ya Jalalu’d-Din Suyuti, Jz. 10, na Tafsir-e-Durr-e- Mansur, mwanzoni mwa sura ya Isra’il, inasimuliwa kutoka Ibn Adi na Ibn Asakir, ambao wanasimulia kutoka kwa Anas Ibn Malik, kwamba Mtukufu Mtume wa Allah alisema kwamba aliona maandishi kwenye Arsh: “Hakuna mungu ila Allah; Muhammad ni Mtume wa Allah; nimempa msaada kupitia kwa Ali.”

Katika Yanabiu’l-Mawadda inasimuliwa kutoka kwenye Dhakha’iru’l-Uqba ya Imam’l-Haram Tabari, kwa mujibu wa riwaya ya Sirat-e-Mullah, kwamba Mtukufu Mtume wa Allah (s.a.w.w.) alisema: “Katika ule usiku wa Mi’raj, nilipochukuliwa mpaka kwenye mbingu ya juu kabisa, huko niliona maandishi upande wa kulia wa Arsh: ‘Muhammad ni Mtume wa Allah. Nimempa msaada kupitia kwa Ali.’”

Imesimuliwa katika Yanabiu’l-Mawadda, Hadith 19, kutoka kwenye Kitabus-Sabi’in cha Imamu’l-Haram Tabari, akinukuu kutoka Manaqib ya Faqih Wasti Ibn Maghazili Shafi’i, na vile vile Mir Seyyid Ali Hamadani Shafi’i anaandika katika Mawadda 6 kutoka Mawaddatu’l-Qurba hadithi mbili; Khatib Khawarizmi katika Manqib, Ibn Shirwaih katika Firdaus, na Ibn Maghazili Shafi’i katika Manaqib, akisimulia kutoka kwa Jabir Bin Abdulla Ansari kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Imeandikwa katika mlango wa Pepo kwamba ‘hakuna mungu ila Allah, Muhammad ni mtume wa Allah, na Ali ni Wali (mwandamizi) wa Allah na ndugu wa Mtukufu wa Mtume wa Allah.’ Hiyo iliandikwa miaka 2,000 kabla ya kuumbwa kwa mbingu na ardhi.”

Nakumbuka hadithi nyingine. Mir Seyyid Ali Faqih Shafi’i anaandika katika Mawadda 8 ya Mawaddatu’l-Qurba kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimuambia Ali: “Nimeliona jina lako likiwa limeunganishwa na la kwangu katika sehemu nne:

(1) Katika usiku wa Miraji wakati nilipofika Baitu’l-Maqaddas (Kuba ya Jiwe), niliona maandishi juu ya jiwe: “Hakuna mungu ila Allah, na Muhammad ni Mtume wa Allah ambaye nimempa msaada kupitia kwa waziri wake Ali.”

(2) Wakati nilipofika Sidratu’l-Muntaha, niliona maneno: “Hakika Mimi ni Allah; haku- na mungu ila Mimi, Mmoja, na Muhammad miongoni mwa viumbe wangu wote ndiye mpendwa Wangu. Nimempa msaada kupitia kwa waziri wake, Ali.”

(3) Wakati nilipofikia Arsh ya Allah swt, niliona kuna maandshi kwenye nguzo zake: “Hakika, Mimi ni Allah, na hakuna mungu isipokuwa Mimi. Katika viumbe Wangu wote Muhammad ni mpendwa Wangu. Nimemsaidia kupitia kwa waziri wake, Ali.”

(4) Wakati nilipofika Peponi, niliona maandishi kwenye lango lake: “Hakuna mungu, ila Mimi. Katika viumbe Wangu wote Muhammad ndiye mpendwa Wangu. Nimemsaidia kupitia kwa waziri wake, Ali.”

Imam Tha’labi katika Tafsir Kashfu’l-Bayan na Sheikh Sulaiman Balkhi katika Yanabiu’l- Mawadda, sura 24, akisimulia kutoka kwa Hafidh Abu Nu’aim Ispahani, Muhammad Bin Jariri Tabari katika Tafsir na Ibn Asakir katika Ta’rikh yake, anasimulia kutoka kwa Ibn Abbas na Abu Huraira kwamba aya 62 ya Sura ya Anfal:

هُوَ الَّذِي أَيَّدَكَ بِنَصْرِهِ وَبِالْمُؤْمِنِينَ {62}

“…Yeye ndiye aliyekusaidia kwa ushindi wake na kwa waumini.” (8:62)

kisha wanasema kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Niliona maandishi juu ya Arsh kwamba: ‘Hakuna mungu ila Allah, Mmoja, ambaye hana mshirika, na Muhammad ni mtumishi na Mtume Wangu; nimemtia nguvu kwa Ali Bin Abi Talib.”

Kisha wanasimulia hadithi nyingine za aina hii kutoka kwenye Kitab-e-Sifa na Manaqib. Chanzo cha majina ya Muhammad na Ali ni Allah Mwenyewe.

Maneno Yaliyotumiwa Na Adam Kwa Ajili Ya Kukubaliwa Kwa Toba Yake Yalikuwa Ni Majina Ya Watoharifu Watano

Vile vile Imam Tha’labi katika Tafsiir Kashfu’l-Bayan na Sheikh Sulaiman Balkhi Hanafi katika Yanabi sura ya 24, wakisimulia kutoa kwa Faqih Wasti Ibn Maghazili Shafi’i ni maelezo juu ya aya 37 ya Sura ya 2 ya Qur’ani Tukufu:

Kisha Adam akapokea maneno kutoka kwa Mola wake, akamkubalia toba yake; hakika Yeye ndiye apokeaye toba, Mwenye kurehemu.” (2:37)

Sa’id ibn Jabir alisimulia kutoka kwa Ibn Abbas, ambaye amesema: “Mtukufu Mtume aliulizwa kuhusu maneno ambayo Nabii Adam alikuwa amejifunza na ambayo yalisababisha kukubaliwa kwa toba yake. Mtukufu Mtume akasema: “Alimuomba Allah kwa majina ya Muhammad, Ali, Fatima, Hasan na Husein. Hivyo Allah swt. aliikubali toba yake na akamsamehe.”

Wahyi Na Ilham Vilitolewa Kwa Watu Wengine Mbali Na Mitume,

Hata Kwa Wanyama

Kuhusu Abu Talib kupewa wahyi na utume, hapa tena umekosea. Wahyi na Ilham vina hatua ambazo sio za kipekee kwenye cheo cha utume tu. Istilahi hizi zinaashiria kwenye uwezo wa mtu wa kuelewa moja kwa moja ilmu iliyofichwa. Ilmu hii inatolewa kwa watu maalum na halikadhalika kwa wanyama.

Je, na nyuki alikuwa mtume ambaye kwaye Allah alitumia wahyi? Aya ya Qur’ani Tukufu katika Sura ya Nahl kwa uwazi inasema:

Na Mola wako akamteremshia wahyi nyuki kwamba tengeneza majumba katika milima na katika miti na katika yale wanayojenga.” (16:68)

Je, unafikiri kwamba Nukhabuz (au, kwa mujibu wa wafasir wengine Yukhabuz), mama yake Nabii Musa alikuwa Mtume? Katika Surat al-Qasas imeelezwa wazi kwamba alipewa amri mbili, sheria mbili za kukataza, vipande viwili vya habari na bishara njema mbili kwa njia ya Wahyi, Allah alisema:

وَأَوْحَيْنَا إِلَىٰ أُمِّ مُوسَىٰ أَنْ أَرْضِعِيهِ ۖ فَإِذَا خِفْتِ عَلَيْهِ فَأَلْقِيهِ فِي الْيَمِّ وَلَا تَخَافِي وَلَا تَحْزَنِي ۖ إِنَّا رَادُّوهُ إِلَيْكِ وَجَاعِلُوهُ مِنَ الْمُرْسَلِينَ {7}

“Na tulimpelekea wahyi mama yake Musa kwamba mnyonyeshe, na utakapomhofia basi mtie mtoni na usiogope wala usihuzunike, kwa hakika sisi tutamrudiasha kwako, na tutamfanya miongoni mwa mitume.” (28:7)

Mbali na ukweli huu, sio muhimu kwa mwongozo wa watu kwamba maelekezo yote na amri za Allah ziwasilishwe kwa Wahyi.

Wakati mwingine huwaongoza watu kwa sauti. Imetokea mara kwa mara na Qur’ani Tukufu inatoa ushahidi wa habari hii katika Sura ya Mariamu, anasema jinsi alivyomuongoza Mariamu:

فَنَادَاهَا مِنْ تَحْتِهَا أَلَّا تَحْزَنِي قَدْ جَعَلَ رَبُّكِ تَحْتَكِ سَرِيًّا {24}

“Kisha (sauti) (19:24-26) ikaita kutoka chini yake: Hakika Mola wako ameweka kijito chini yako.” (19:24)

Abu Talib Aliongozwa Na Allah Kumpa Mtoto Wake Jina La Ali

Katika njia hiyo hiyo ambayo nyuki, mama yake Musa na mama yake Isa walivyoelekezwa na Allah, ingawa hakuna hata mmoja kati yao aliyekuwa mtume, Abu Talib vile vile alielekezwa kumpa mtoto wake jina.

Aidha, hakuna mtu hata mmoja ambaye amewahi kusema kwamba Abu Talib ni mtume au kwamba Wahayi uliteremshwa kwake. Sauti ya ki-ungu na ubao ndio vilikuwa na maelekezo hayo ya kumpa mtoto jina. Maulamaa wenu wenyewe wameandika kuhusu habari hii katika vitabu vyao.

Sheikh: Ni wapi maulamaa walipoelezea hili?
Muombezi: Kuna vitabu vingi kama hivyo.

Ufunuo Wa Lawh (Ubao) Kwa Abu Talib

Mir Seyyid Ali Hamadani Faqih Shafi’i, katika Mawaddatu’l-Qurba yake, Mawadda ya 8, kutoka kwenye riwaya ya Abbas Bin Abdu’l-Muttalib, ambayo Sulayman Balkhi Hanafi vile vile ameinukuu katika Yanabiu’l-Mawada yake sura ya 56, na Muhamaad Bin Yusuf Ganji Shafi’i katika kitabu chake Kifayatut-Talib wanasimulia pamoja na tofauti kidogo ya maneno kwamba wakati Ali alipozaliwa mama yake Fatima Bint Asad alimpa jina la baba yake Asad.

Abu Talib hakukubaliana naye na akasema: “Ewe Fatima! Twende kwenye vilima vya Qubais, na tumuombe Allah (baadhi ya wasimuliaji wanasema kwamba, alisema twende kwenye Masjidu’l-Haram).

Huenda akatueleza jina la mtoto huyu.” Ilikuwa usiku wakati walipowasili kwenye vilima vya Abu Qubais (au Masjidu’l-Haram) na wakaanza maombi yao. Abu Talib aliomba: “Ewe Muumba wa usiku huu wa giza na mwezi unaong’ara, tufahamishe tujue utashi Wako kuhusiana na jina la mtoto huyu?”

Katika wakati huo sauti ilisikika kutoka angani. Wakati Abu Talib aliponyanyua kichwa chake aliona ubao kama kito cha kijani, wenye misitari mine iliyoandikwa juu yake.

Aliuchukuwa ule ubao akaukumbatia kifuani kwake. Wakati alipousoma aliona maneno haya: “Nimewapa heshima maalum juu yenu nyote kwa kuwapeni mtoto twahir, maarufu. Amepewa jina la Ali kutoka upande wa Allah. Linatokana na ‘Aliy’ (Aliyetukuka).”

Ganji Shafi’i anaandika katika Kifayatut-Talib kwamba sauti ilikuja katika kujibu ushairi wa Abu Talib akisoma beti hizi mbili: “Enyi watu wa nyumba tukufu ya Mtume! nimewatukuza ninyi kwa kuwapa mtoto aliye twahara. Hakika, ameitwa Ali kutoka upande wa Allah swt. Jina hili linatokana na jina la Allah Mwenyewe la Al-Aliiyu.”

Abu Talib alifurahishwa mno na akaporomoka chini na akamsujudia Allah swt. Kama ishara ya shukurani kwa ajili ya tukio hili kubwa, alitoa dhabihu ngamia kumi. Alitundika ule ubao ndani ya Masjidu’l-Haram.

Bani Hashim walikuwa wakijifaharisha na ubao huo mbele za Makureishi. Ubao huo ulibakia umening’inia pale mpaka ulipotoweka wakati wa vita kati ya Abdullah Ibn Zubair na Hajjaj.

Riwaya hii vile vile inaunga mkono hadithi iliyotajwa huko nyuma ambayo inasema kwamba kuanzia mwanzoni hasa Abu Talib alikuwa ni muumin.

Alimuomba Allah kumtajia jina la mtoto. Alipoona neema ya ukarimu wa Allah, aliporomoka chini katika hali ya kusujudu mbele Yake. Je, hii ni tabia ya kafiri?

Jina La Ali Sio Sehemu Ya Adhana Au Iqama

Umedai kwamba wanachuoni wa Shia wanasisitiza kwamba jina la Ali huchukuliwa kama wajibu katika Adhana na Iqama. Kwa kweli hakuna mwanachuoni hata mmoja aliyeeleza kwamba jina la Ali ni sehemu muhimu ya Adhana au Iqama. Katika vitabu vyote vya fiqih mafaqih wote wa Shia bila kuhitilafiana wanasema kwamba kushuhudia wilayat ya Amirru’l-Muminin sio sehemu ya Adhana au Iqama.

Kuitamka katika adhana au iqama kwa nia hiyo ni haram. Kama wakati wa kuanza kwa Swala nia ni kwamba jina la mtukufu Imam ni sehemu ya lazima ya Swala, basi utekelezaji wa swala hiyo unakuwa Batili.

Lakini bila shaka, baada ya kutaja jina la Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), ukataja na jina la Ali bila kulichukulia ulazima kwa madhumuni hayo, bali kwa ajili ya heshima na kubarakiwa inafaa. Allah amelitaja jina lake kila mahali baada ya kutaja jina la Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kama nilivyokwisha kutaja huko nyuma. Sasa tunakuja kwenye hoja yetu kubwa: hakuna yeyote miongoni mwa sahaba mashuhuri aliyekuwa na nasaba tukufu kama alivyokuwa Ali.

Uchamungu Wa Ali

Ama kwa uchamungu wa Ali, hakuna mwingine yeyote anayelingana naye. Wote marafiki na maadui zake wanakubali kwamba baada ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), hakuna mwingine aliyekuwa mchamungu kama alivyokuwa Ali. Ibn Abi’l-Hadid katika Sharh-e- Nahnu’l-Balagha na Muhammad Ibn Talha Shafi’i katika Matalibus-Su’ul, wanasimulia kutoka kwa Umar Ibn Abdul’l-Aziz kwamba mtukufu Imam alikuwa mbora zaidi katika uchamungu kuliko wanadamu wote.

Yeye anasema: “Hatumjui mtu yeyote katika umma baada ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ambaye alikuwa mtiifu zaidi na mchamungu kuliko Ali Bin Abi Talib.” Mullah Ali Qushachi, pamoja na chuki yake kubwa, anaandika kwamba wanadamu hawawezi kutambua fadhila za Ali. Katika kitabu chake Sharh-e-Tajrid anasema: “Watu wanashangazwa wanaposikia matendo ya maisha ya Ali.”

Riwaya Ya Abdullah Bin Rafi’i

Abdullah Ibn Rafi’i anasema kwamba katika mwisho wa siku ya funga, alikwenda kwa Amiru’l-Mu’minin. Aliona kwamba mfuko uliofungwa kwa lakiri uliletwa kwake. Wakati Ali alipoufungua, ulionekana kuwa unga ambao haukuchekechwa. Imam alichota mafumba matatu ya unga, akayala, akanywa maji kidogo, na akatoa shukurani kwa Allah. Abdullah Bin Rafi’i akasema: “Ewe Abu’l-Hasan! Kwanini umeufunga kwa lakiri mdomo huo wa mfuko?” Imam akajibu: “Ni kwa sababu watoto wangu ambao wananipenda sana wasije wakachanganya mafuta ya zeituni au sukari pamoja na unga huu, ambao utafanya nafsi ya Ali kuonja utamu wake.”

Hivyo alikuwa na tabia ya kujiweka mbali na vyakula vitamu ili asije akalainishwa navyo. Sulaiman Balkhi Hanafi vile vile ameitaja hadithi hii katika Yanibiu’l-Mawadda, sura ya 51, kutoka kwa Ahnaf Bin Qais.

Riwaya Ya Suwaid Bin Ghafla

Aidha,Sheikh katika Yanabiu’l-Mawadda, Muhammad Bin Talha Shafi’i katika Matalabus-Su’ul, Khatib Khawarizmi katika Manqib, na Tabari katika Ta’rikh yake wamesimulia kutoka kwa Suwaid Bin Ghafla kwamba alisema: “Siku moja nilipa bahati ya kumtembelea Amiru’l-Mu’minin.

Niliona mbele yake kikombe cha maziwa ambayo yalikuwa chachu mno kiasi kwamba niliweza kusikia harufu yake. Imam alikuwa na mkate mkavu katika mkono wake. Ulikuwa mkavu sana kiasi kwamba haikuwezakana kuuvunja. Imam aliuvunja kwa kuuweka chini ya goti lake na baada ya kuulainisha katika maziwa yale chachu, aliula.

Alinikaribisha na mimi nile pamoja naye. Nilimuambia kwamba nimefunga. Imam akasema: “Nimesikia kutoka kwa swahiba yangu, Mtume wa Allah, kwamba kama mtu amefunga na anapenda chakula fulani, lakini hakili kwa ajili ya Allah, basi Allah atampa vyakula vya kimbinguni.”
Suwaid aliendelea: “Nilipoona hali ya Ali, nilishangazwa sana. Nilimuuliza mtumishi wa Imam, Fizza, ambaye alikuwa amesimama karibu yangu, kwa nini hamuogopi Allah, yaani, kwa nini alipika ule mkate wa shayiri bila kuondoa mapumba.

Fizza alisema kwa kuapa kwamba Ali mwenyewe alimuagiza kwamba asiondoe mapumba. Imam akaniuliza nilichokuwa nazungumza na Fizza. Nilimuambia kwamba nilikuwa nikimuuliza ni kwa nini hakuuchekecha huounga. Ali akasema: ‘Baba yangu na mama yangu watolewe kafara kwa ajili ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)! Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kamwe hakuwahi kuondoa mapumba; kamwe hajazima njaa yake kwa mkate wa ngano kwa muda wa siku tatu mfulilizo. Mimi ninafuata mwenendo wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.),’”

Ali Alijizuia Kula Halwa

Muwaffaq Bin Ahmad Khawarizmi na Ibn Maghazili Faqih Shafi’i wanaandika katika Manaqib zao kwamba siku moja wakati wa ukhalifa wa Ali, kiasi fulani cha halwa (aina ya chakula kitamu) kililetwa mbele yake. Alichukua kidogo akakinusa, na akasema: “Kuvutia kulikoje na harufu nzuri iliyoje!

Lakini Ali hajui ladha yake. Kamwe sijawahi kula halwa.” Msimuliaji akasema kumuambia: “Ewe Ali! Je, kwani halwa ni haramu kwako?” Imam akajibu: “Kile ambacho Allah amekifanya kuwa halali hakiwezi kamwe kuwa haramu.

Lakini je! naweza kuridhika kulijaza tumbo langu ambapo kuna watu wenye njaa katika nchi? Je, naweza kulala, na tumbo langu likiwa limejaa wakati watu katika Hijazi yote wanakufa kwa njaa? Vipi nitaridhika mimi mwenyewe na jina langu likiwa ni Amiru’l-Mu’minin? Kwanini nisijishirikishe na watu katika ufukara na shida zao.” Vile vile Khawarizmi anasimulia kutoka kwa Abi Bin Thabit kwamba siku moja ‘faluda’ (kinwaji kitamu) kililetwa mbele ya Ali, lakini alizuia hamu yake na hakuinywa.

Hii ni baadhi ya mifano ya mwenendo wake kuhusiana na kula na kunywa. Alikula mkate mkavu wa shayiri wakati mwingine pamoja na siki au chumvi na wakati mwingine pamoja na mboga kidogo na maziwa. Kamwe kulikuwa hakuna aina mbili ya chakula katika kitambaa cha meza ya chakula.

Katika mwaka wa 40 A.H. katika usiku wa mwezi 19 Ramadhani, wakati Abdu’r-Rahman Muljim Muradi (L.A) alipomtia lile jeraha baya, yeye alikuwa mgeni nyumbani kwa bint yake,Ummu’l-Kulthum, kwa ajili ya kufuturu.

Wakati mkate, maziwa na chumvi vilipowekwa kwenye kitambaa cha chakula, Ali ambaye alikuwa na mapenzi makubwa na bint yake Ummu’l-Kulthum, kwa hasira akasema: “Sijaona msichana kuwa katili hivi kwa baba yake.” Ummu’l-Kulthum akasema: “Baba! Nimefanya kosa gani?” Ali akasema: “Ulisha wahi kumuona baba yako akiwa na vyakula vya aina mbili katika kitambaa chake cha chakula?”

Kisha aliamuru kwamba maziwa yaondolewe. Hata hivyo, alikula vipande vichache vya mkate na chumvi na kisha akasema: “Itatubidi kuja kutoa hesabu kwa ajili ya vitu vyote vya halali; kuna adhabu kwa ajili ya matendo haramu.”

Mavazi Ya Ali

Mavazi ya Ali yalikuwa duni sana. Ibn Abi’l-Hadid katika Sharh-e-Nahju’l-Balagha, Ibn Maghazili Shafi’i katika Manaqib, Imam Ahmad Ibn Hanbal katika Musnad yake, Sibt Ibn Jauzi katika Tadhkira, na wengine katika maulamaa wenu wameandika kwamba: “Mavazi yake yalikuwa ni nguo yenye mikwaruzo, gwanda (lisilo laini), iliyonunuliwa kwa dirham tano.”

Aliweka viraka kwenye nguo zake. Viraka vilikuwa vya ngozi au majani ya mtende, viatu vyake vile vile vilikuwa vimetengenezwa kwa majani ya mtende.

Muhammad Bin Talha Shafi’i katika Matalibus-Su’ul, Sulaiman Balkhi Hanafi katika Yanabiu’l-Mawadda, na Ibn Abi’l-Hadid Mut’azali katika Sharh-e-Nahju’l-Balagha wameandika kwamba Ali alikuwa na viraka vingi sana katika nguo zake kiasi kwamba wakati wa ukhalifa wake, binamu yake Abdullah Ibn Abbas aliviona na akahuzunika.
Ali akasema: “Nina viraka vingi katika nguo zangu kiasi kwamba sasa namuonea haya huyo mshona viraka. Kwani Ali anahusika nini na mapambo ya kidunia? Vipi nitatosheka na starehe ambazo ni za kutoweka na neema ambayo sio ya kudumu?” Mtu mwingine alipinga jinsi Ali anavyoonekana akisema: “Kwa nini unaweka viraka kwenye nguo zako hata wakati wa ukhalifa wako na ukubwa?”

Hali hii hufanya maadui wakudharau.” Ali akasema: “Hili ni aina ya vazi ambalo huzuia majivuno yetu, huondoa hisia za kiburi ndani ya mtu, na hukubaliwa na muumini.”

Muhammad Bin Talha katika Matalibus-Su’ul, Khawarizmi katika Manaqib yake, Ibn Athir katika kitabu chake Kamil, na Sulaiman Balkhi katika Yanabiu’l-Mawadda wamesimulia kwamba Ali na mtumishi wake walikuwa na nguo zinazofanana. Alinunua nguo mbili za aina moja na bei moja, moja alivaa mwenyewe na moja alimpa mtumishi wake, Qanbar.

Hizi zilikuwa ndio desturi za Ali kuhusiana na chakula na mavazi. Yeye mwenyewe alikula mkate mkavu wa shayiri na kuwapa masikini na yatima mikate iliyotengenezwa kwa ngano, sukari, asali na tende. Alivaa nguo zenye viraka yeye mwenyewe, lakini aliwapa mayatima na wajane nguo nzuri.

Mazungumzo Ya Zurar Na Mu’awiya Kuhusu Ali

Kuna mifano mingi ya Ali kuipa nyogo dunia, Ibn Abi’l-Hadid katika Sharh-e-Nahju’l- Balagha, Hafidh Abu Nu’aim Isfahani katika Hilyatu’l-Auliya, Jz. 1, uk. 84, Sheikh Abdullah Bin Amir Shabrawi Shafi’i katika Kitabu’l-Ittihad Bil Hubbi’l-Ashraf, uk. 8; Muhammad Bin Talha katika Matalibus-Su’ul, uk 33; Nuru’d-din Bin Sabbagh Malik kati- ka Fusulu’l-Muhimma, uk. 128; Sheikh Sulaiman Balkhi Hanafi katika Yanabiu’l- Mawadda, sura 51; Sibt Bin Jauzi katika Tadhkira Khawasu’l-Umma mwishoni mwa sura ya 5, na wengine wengi katika maulamaa na wanahistoria wenu maarufu wameandika kwa urefu mazungumzo kati ya Mu’awiya na Zurar Bin Zumra.

Mwishoni mwa mazungumzo yake na Mu’awiya, Zurar alimtukuza Ali katika maneno haya: “Katika nyakati fulani nimemuona Ali wakati wa usiku, nyota zikiwa zimezagaa mbinguni, akiwa ameshika ndevu zake na kutapatapa kama mtu aliyeumwa na nyoka, akilia kama vile yuko kwenye maumivu makali, akisema: ‘Ewe dunia! Mdanganye mwingine badala yangu mimi.

Je, unanikumbatia mikononi mwako na una mapenzi makubwa na mimi? Hili haliwezekani. Nimekupa talaka tatu, ambazo kwazo baada yake kuungana tena ni muhali. Muda wako ni mfupi, hofu unayoleta ni kubwa, na starehe yako ni yenye kufedhehesha sana.

Allah atuokoe na uhaba wa njia za kusafiria, umbali wa mashukio, na hatari za njiani!’ Kisha Mu’awiya akaanza kulia na kusema: ‘Allah amhurumie Abu’l-Hasan. Wallahi alikuwa kama hivyo.’ Vile vile alisema: ‘Wanawake hawana uwezo wa kuzaa mtu kama Ali Bin Abi Talib.’”

Utambuzi Wa Mtume Juu Ya Uchamungu Wa Ali

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mwenyewe alitambua uchamungu wa dhahiri wa Ali, Muhammad Bin Yusuf Ganji Shafi’i katika Kifayayut-Talib, sura ya 46, anasimulia kutoka kwa Ammar Yasir, ambaye alisema kwamba alisikia kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwamba alimwambia: “Hakika Allah amekupa wewe pambo ambalo mfano wake hakumpa yeyote yule ambaye Alimpenda. Na (pambo) hilo ni uchamungu wako katika ulimwengu huu.

Amekufanya hivyo kiasi kwamba hunufaiki kutokana na ulimwengu huu, wala hauwezi kukufanya wewe kuuelekea. Amejaalia juu yako wewe upendo kwa masikini na mafukara. Hivyo walifurahishwa na Uimam wako na mimi vile vile nimefurahishwa nao kwa sababu ya kukufuata wewe. Aliyebarikiwa ni yule anayefanya urafki na wewe na kukukubali; na laana iwe kwa yule ambaye ni adui kwako. Wale wanaokupenda na kukubali wewe watakuwa majirani zako katika Pepo na maswahiba wako katika kasir yako. Wale ambao walikuwa wakikupinga wewe watahesabiwa kama waongo na Allah Siku ya Hukumu wapewa adhabu yao inastahili.”

Allah Na Mtukufu Mtume Walimuita Ali ‘Imamu’l-Muttaqin’

(Kiongozi Wa Wachamungu)

Alifikia hatua ya hali ya juu ya uchamungu kiasi kwamba marafiki na maudui wanamuita Imam’l-Muttaqin (kiongozi wa wachamungu). Kwa hakika mtu wa kwanza kumuita kwa sifa hii ni Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mwenyewe. Ibn Abi’l-Hadid katika Sharh-e-Nahju’l- Balagha, Jz. 2, uk. 450; Hafidh Abu Nua’aim Ispahani katika Hilyatu’l-Auliya; Mir Seyyid Ali Hamadani katika Mawaddatu’l-Qurba na Muhammad Bin Yusuf Ganji Shafi’i katika Kifayatut-Talib, sura ya 54, wanasimulia kutoka kwa Anas Bin Malik kwamba siku moja Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimuambia amletee maji kwa ajili ya kuchukulia wudhu.

Wakati alipoleta maji Mtumkufu Mtume alichukuwa wudhu na kisha akasali Sala ya rakaa mbili. kisha akasema: “Ewe Anas! Mtu atakayefuatia kuingia mlango huu ni mkuu wa wachamungu, kiongozi wa Waislamu, mtawala wa waumini, na mwisho wa mawasii (warithi) ambaye atawaongoza watu wenye nyuso na mikono angavu mpaka Peponi.”

Anas anasema: “Nilimuomba Allah moyoni mwangu mwenyewe kwamba aweze kumleta Ansar (mtu wa Madina) mmoja kwenye mlango huo, lakini nililifanya ombi langu kuwa siri. Ghafla, nilimuona Ali akiingia mlangoni. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akauliza huyo alikuwa ni nani. Nikajibu kwamba alikuwa ni Ali Bin Abi Talib. Kisha Mtufufu Mtume kwa furaha akaamka kumuamkia Ali.

Alimkumbatia kwenye mikono yake na kumfuta jasho katika uso wake. Ali akasema, ‘Ewe Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)! Unanifanyia mimi leo kiasi ambacho hujanifanyia kabla!’ Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema: ‘Kwa nini nisifanye hivyo wakati ambapo wewe utawasilisha utume wangu kwa umma, utafanya wasikie sauti yangu, na utawaelezea yale mambo ambayo kwayo wamehitalifiana kimaoni.’”

Vile vile Ibn Abi’l-Hadid katika Shahr-e-Nanju’l-Balagha, Jz. 2, na Hafidh Abu Nu’aim katika Hilyatu’l-Auliya wanaandika kwamba siku moja Ali alikuja kwa Mtume. Mtume akamuambia: “Karibu, kiongozi wa Waislamu na Mkuu wa wachamungu.” Ali akasema: “Namtukuza Allah kwa neema ambayo ameiweka juu yangu, na naomba ukarimu Wake kwangu.” Muhammad Bin Talha Shafi’i vile vile anasimulia hadithi hii mwishoni mwa juzu ya 4, sehemu ya 1, ya Matalibus-Su’ul na kwayo inathibitisha kwamba Ali alikuwa Imam wa wachamungu wote.

Hakim, katika Mustadrak, sehemu ya 3, uk. 38 na Bukhari na Muslim, kila mmoja katika Sahih yake, wanasimulia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Allah amenitumia wahyi kuhusu Ali unaohusiana na mambo matatu: (1) ni maula na mkuu wa Waislamu; (2) ni mkuu wa wachamungu; na (3) ni kiongozi ambaye atawaongoza watu wenye nyuso na mikono angavu (kwenda Peponi).”

Muhammad Bin Yusuf Ganji Shafi’i anasimulia katika Kifayatu’l-Talib sura ya 45, kutoka kwa Abdullah Bin Asad bi Zurara kwamba Mtume alisema: “Katika usiku wa Miraji, wakati nilipochukuliwa kwenda mbinguni, niliruhusiwa kuingia kasir ya lulu, ambayo sakafu yake ni ya dhahabu inayomeremereta.

Kisha wahyi ulitumwa kwangu, na nilielezwa vitu vitatu kuhusu Ali: (1) kwamba kwa hakika yeye ni maula na mkuu wa Waislamu; (2) kwamba yeye ni Imam na mkuu wa wachamungu; na (3) kwamba yeye ni kiongozi ambaye atawaongoza watu wenye nyuso na mikono angavu (kwenda Peponi).”

Imam Ahmad Bin Hanbal anaandika katika Musnad yake kwamba siku moja Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimuambia Ali hivi: “Ewe Ali! Kuutazama uso wako ni ibada; hakika wewe ni mkuu wa wachamungu na kiongozi wa waumini. Yule aliye rafiki yako ni rafiki yangu, na aliye rafiki yangu kwa hakika ni rafiki wa Allah. Yeye ambaye ana nia mbaya dhidi yako ana nia mbaya dhidi yangu, na yule ambaye ana nia mbaya dhidi yangu hakika ana nia mbaya dhidi ya Allah.”

Hivyo inatosha kwa cheo kitukufu cha Ali kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisisitiza kwamba Ali anawapita masahaba katika uchamungu. Yeye peke yake ndiye aliyekuwa amepewa cheo cha ‘Imam’l-Muttaqin,’ na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mara kwa mara alimtaja kama hivyo.

Kamwe Imam’l-Muttaqin Ali Hakuwa Na Mapenzi Ya Kujiingiza Kwenye

Anasa Au Mamlaka

Sheikh: Mtu hawezi kusema sana katika kumtukuza Ali, bila shaka Mu’awiya alisema kitu sahihi: wanawake wa ulimwenguni hawana uwezo wa kuzaa mtu kama Ali.

Muombezi: Sasa ni wazi kwamba miongoni mwa masahaba wenye kuheshimika Ali alikuwa mkuu wa wachamungu. Kuna wazo limenijia sasa hivi. Kama mtaniruhusu nitawaomba kitu kimoja.

Sheikh: Ndio tafadhali fanya hivyo.

Muombezi: Baada ya kukiri kwamba miongoni mwa masahaba maarufu Ali alikuwa na hadhi ya kipekee ya kuwa mkuu wa wachamungu, je, utaweza kufikiria kwamba alikuwa na mwelekeo wowote wa kujiingiza kwenye anasa au mamlaka?

Sheikh: Haiwezekani kufikiria kitu kama hicho kuhusu yeye. Umeonesha jambo linalojulikana sana kwamba Ali aliipa dunia talaka tatu. Tukiwa tumethibitisha kujitenga kwake na dunia vipi ataiinamia. Mbali na hili, cheo chake ni kitukufu mno kiasi kwamba haiwezekani kuhusisha ndani yake dhana ya uwongo kama hiyo kwake.

Muombezi: Hivyo ina maana kwamba matendo yote ya mtu mfano wa uchamungu kama huyo yalikuwa ni kwa ajili ya Allah. Kamwe hakugeuka hata inchi moja kutoka kwenye ile njia ya haki.

Sheikh: Ni dhahiri kwamba sisi hatukatai mambo haya kuhusu Ali.

Kukataa Kwa Ali Kutoa Kiapo Cha Utii Kwa Abu Bakr Kunathibitisha Mbinu Ya Kuchaguliwa Kwake Kama Khalifa Haikuwa Sahihi

Muombezi: Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipofariki, kwa mujibu wa wosia wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), Ali alifanya taratibu zote za mazishi. Baadhi ya watu, wakiwa wamekutana huko Saqifa-e-bani Sa’ida, walikula kiapo cha utii kwa Abu Bakr.

Baadae, wakati Ali alipoitwa, kwanini alikataa kula kiapo cha utii?

Kama namna ambayo kwamba Abu Bakr alichaguliwa kuwa Khalifa ilikuwa sahihi na suala la Ijma lilithibitika kuwa la haki, basi Ali, akiwa mchamungu kiasi kikubwa mno asingepotoka kutoka kwenye haki.

Utakumbuka hadithi ambayo niliitaja katika mikesha iliyopita, ambayo kwayo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Ali yuko pamoja na haki na haki iko pamoja na Ali.”

Kama mkutano kule Saqifa ulikuwa umetegemezwa juu ya uadilifu na uchaguzi wa Abu Bakr kama Khalifa ulikuwa halali, Imam (Ali) angewakaribisha na kumkubali Abu Bakr kama Khalifa wa haki. Lakini kwa kweli alipinga uchaguzi ule kwa nguvu zote.

Upinzani wa Ali lazima utakuwa uliegemea juu ya moja ya mambo mawili. Amma Ali alikuwa anakwenda kinyume na njia ya haki, na alivunja amri ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), au alichukulia hiyo Ijma kuwa ni kichekesho.

Amma kwa uwezekano huu wa kwanza, hiyo haiwezekani kufikiria kwamba Ali angeweza kuikataa haki. Kwa mujibu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) “Ali yuko pamoja na haki na haki iko pamoja na Ali.” Aidha, hakuna hata mtu mmoja ambaye amewahi kudai kwamba yeye (Ali) alikuwa anapenda mamlaka ya kidunia. Aliupa ulimwengu talaka tatu.

Hakuwa na haja ya kupata umaarufu wa kisiasa. Ilikuwa ni ile hali ya pili ambayo ilimchochea yeye kukataa kuukubali ukhalifa wa Abu Bakr. Alijua unapingana na utashi wa Allah na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).
Sheikh: Ni ajabu kwako wewe kusema kwamba Ali hakula kiapo cha utii kwa Abu Bakr. Rejea katika vitabu vyenu na vyetu vya historia vithibitisha kwamba Ali alikula kiapo cha utii kwa Khalifa Abu Bakr na hakupinga Ijma.

Muombezi: Je, umesahau mijadala yetu yote iliyopita ambayo kwayo nilitoa maelezo kamili ya kauli za maulamaa wenu mashuhuri? Hata Bukhari na Muslim wameandika kila mmoja kwenye Sahih yake kwamba Ali hakutoa kiapo cha utii katika wakati ule.

Maulamaa wenu kwa ujumla wamekiri kwamba katika siku ya kwanza, wakati mtukufu Imam alipoburuzwa kwa nguvu na kwa matusi kutoka nyumbani kwake kwenda msikitini (kama ilivyoelezwa mapema) yeye hakutoa kiapo bali alirudi nyumbani. Ibrahim Bin Sa’d Saqafi (kafa 283 A.H.), Ibn Abi’l-Hadid, Tabari na wengine wameandika kwamba Ali alitoa kiapo cha utii baada ya miezi sita (yaani, baada ya kifo cha Fatima). Hata kama tukubali, kwa njia ya kukisia, kwamba Imam alitoa kiapo cha utii, kwa nini alingojea mpaka baada ya miezi sita kabla ya kufanya hivyo?

Sheikh: Kwa hakika lazima kulikuwa na sababu fulani kwa hilo. Yeye peke yake ndiye alilijua hilo. Lakini kwa nini tuwe na wasi wasi kuhusu kutoafikiana kwa wakubwa zetu? Kwa nini tudasisasi tofauti zao baada ya miaka 1300? (kicheko kikubwa kutoka kwa wasikilizaji).

Muombezi: Wakati unapokuwa huwezi kupata jibu kuthibitisha hoja yako, unategemea juu ya jibu kama hilo. Lakini mbele za watu wapenda haki suala hilo liko wazi mno kuhitaji ufafanuzi wowote au uthibitisho.

Amma kwa maelezo yako kwamba hatuhitaji kuingilia katika tofauti za watangulizi wetu, bila shaka uko sawa, kwa kadiri kwamba mambo yao sio mzigo juu yetu. Lakini katika suala lililopo sasa umekosea kwa sababu ni wajibu wa kila Mwislamu mwadilifu kuwa na imani iliyoegemea juu ya mantiki, sio kwa kufuata kibubusa bila kuelewa. Kwa kufanya utafiti kuhusiana na dini, tunasoma historia inayofahamika ya Waislamu.

Tunaona kwamba baada ya kufariki Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) madhehebu mbili zilijitokeza. Kwa hiyo, tunapaswa kufanya utafiti wa kina ili tujue ni madhehbu ipi ambayo imeongozwa kwa sawa sawa. Ni dhahiri hatupaswi kuwafuata kibubusa watangulizi wetu bila kuelewa.

Sheikh: Hakika hoja yako ni kwamba ukhalifa wa Abu Bakr haukuwa wa haki.

Lakini kama Abu Bakr hakuwa ndiye Khalifa wa haki, na kama ilikuwa ni haki ya Ali kuijaza nafasi hiyo, kwa nini asitumie nguvu zake na ujasiri maalumu kusimamisha haki? Alikuwa akihudhuria katika Sala vile vile, na mara kwa mara alikuwa akitoa ushauri wa kufaa kwa makhalifa mashuhuri katika masuala muhimu.

Ukimya Wa Mitume Watukufu

Muombezi: Kwanza, Mitume na warithi wao walitenda kwa mujibu wa utashi wa Allah. Kwa hiyo, hatuwezi kuleta pingamizi lolote la kwa nini hawakupigana vita, au kwa nini walitwaa kunyamaza kimya mbele ya adui, au kwa nini walishindwa.

Kama utachunguza taarifa za kihistoria kuhusiana na maisha ya mitume watukufu na warithi wao, utaona mifano mingi kama hii ya kunyamaza kimya. Qur’ani Tukufu imesimulia baadhi ya matukio hayo.

Katika Surat al-Qamar, Qur’ani Tukufu inasimulia kile alichosema Nabii Nuh pale watu wake walipompuuza:

فَدَعَا رَبَّهُ أَنِّي مَغْلُوبٌ فَانْتَصِرْ {10}

“…Kwa hakika nimeshindwa, kwa hiyo nisaidie.” (54:10)

Katika Surat Mariam, Qur’ani inatusimulia ukimya wa Nabii Ibrahim wakati alipotaka msaada kutoka kwa ami yake Azar na akapokea jibu la kuvunja moyo:

وَأَعْتَزِلُكُمْ وَمَا تَدْعُونَ مِنْ دُونِ اللَّهِ{48}

“Na mimi najitenga nanyi na mnayoyaabudu kinyume cha Allah…”(19:48)

Hivyo kama vile ambavyo Nabii Ibrahim alivyojitenga kutoka kwa watu wakati alipokosa msaada kutoka kwa ami yake Azar, Ali vile vile lazima atakuwa alijitoa kwa watu na akajitenga nao.

Sheikh: Nafikiri kujitenga huku kunaonesha kujitoa kwa moyo. Yaani, alijitoa na akakaa mbali nao lakini hakuchukua kujitenga kwa kimwili.

Muombezi: Kama utachunguza maelezo ya wafasiri wa madhehebu zote, utaona kwamba kujitoa kwake huku kutoka kwa watu kulikuwa ni kwa kimwili, sio tu kwa kisaikolojia. Nakumbuka kwamba Imam Fakhru’d-din Razi anasema katika tafsiri yake Tafsir-e-Kabir, jalada la 5, uk. 809: “Kujitenga kutokana na kitu maana yake ni kukaa mbali nacho.

Alichomaanisha Ibrahim ilikuwa kwamba alitaka kukaa mbali nao, kimwili na kwa msimamo wa kidini.” Taarikh zinasimulia kwamba baada ya kukataa huku Ibrahim alihama kutoka Babylon kwenda Kuhistan iliyoko Fars (Iran ya sasa) na akaishi maisha ya kujitenga katika mazingira yale ya milima kwa muda wa miaka saba. Kisha baadae akarudi Babylon na tena akatangaza hadharani ujunbe wa Allah na akavunja masanamu ya watu.

Katika hili watu wakamtupa kwenye moto. Allah akaufanya moto kuwa baridi na salama kwa ajili yake, na hivyo utume wake ukasimama imara. Katika Surat al-Qasas, kisa kinachohusu Mtume Musa kukimbia kwa kuhofia maisha yake kimesimuliwa katika njia hii:

فَخَرَجَ مِنْهَا خَائِفًا يَتَرَقَّبُ ۖ قَالَ رَبِّ نَجِّنِي مِنَ الْقَوْمِ الظَّالِمِينَ {21}

“Basi (Musa) akatoka akiogopa, akiangilia huku na huku, akasema: Mola wangu! niokoe katika watu madhalimu.” (28:21)

Katika Surat al-A’raf, Qur’ani Tukufu inatuelezea masaibu ya Harun wakati Musa alipomucha katika uongozi wa Bani Israil. Punde watu wakaanza kuabudu ndama wa dhahabu, kwa sababu Harun hakuwa na mtu wa kumsaida, aliamua kunyamaza kimya. Qur’ani inasema:

قَالَ ابْنَ أُمَّ إِنَّ الْقَوْمَ اسْتَضْعَفُونِي وَكَادُوا يَقْتُلُونَنِي{150}

“…Na akakamata kichwa cha nduguye akamvuta kwake akasema: Ewe mwana wa mama yangu! Hakika (watu) hawa wamenidharau, na hata walikaribia kuniuwa…” (7:150)

Hali Ya Ali Inafanana Na Ya Harun

Hivyo, kwa mujibu wa Qur’ani Tukufu Harun hakuchomoa upanga dhidi ya watu. Alijichukulia njia ya ukimya wakati wao walipofuata ndama wa dhahabu wa Samiri kama kitu cha kuabudu kwa sababu yeye (Harun) alitambua kwamba alikuwa amezidiwa kwa wingi wao.

Halikadhalika, Ali, ambaye Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimtangaza kuwa ana cheo sawa na Harun (kama tulivyoeleza kwa urefu huko nyuma), vile vile alikuwa sawa sawa kabisa katika kuchukua njia ya kunyamaza kimya na uvumilivu wakati alipoachwa peke yake.

Mtukufu Imam aliletwa msikitini kwa nguvu na upanga wa wazi uliwekwa kichwani mwake ili kumlazimisha kula kiapo cha utii. Baadae alikwenda kwenye kaburi la Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na akayarudia maneno yale yale ambayo Allah ameyasimulia kwa ulimi wa Harun.

Harun alisema kumuambia Musa: “…Hakika (watu) hawa wamenidharau, na hata walikaribia kuniuwa…”

Kunyamaza Kwa Mitume

Mfano wa Mtume Muhammad kuhusiana na nukta hii kwa hakika zaidi ni mwongozo. Lazima tufikirie ni kwa nini alikaa kimya kwa muda wa miaka kumi na tatu mbele ya harakati mbaya za maadui huko Makka mpaka mwishowe akalazimika kuuacha mji wake wa nyumbani wakati wa giza la usiku. Sababu ilikuwa ni kwamba alikuwa hana wasaidizi.Kwa kweli, hata wakati wa mamlaka yake, hakuweza kuachana na baadhi ya mambo yaliyozushwa.

Sheikh: Inakuwaje wewe unasema Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alishindwa kuangamiza mambo ya uzushi?

Mtukufu Mtume Hakuweza Kufanya Mabadiliko Makali Kwa Kuhofia Watu

Muombezi: Imesimuliwa na Hamidi katika Jam’i bainus-Sahihain na Imam Ahmad Bin Hanbal katika Musnad kutoka kwa Ummu’l-Mu’minin Aisha kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimwambia: “Lau kama watu hawa wasingekuwa karibu na zama za ukafiri na ujinga, na kama nisingeogopa kwamba ingeharibu imani zao, ningeamuru Nyumba ya Ka’ba ibomolewe na chochote kilichokuwa kimechukuliwa kutoka humo kirudishwe.

Baada nikiwa nimeisawazisha, ningelisimamisha milango miwili kuelekea upande wake mashariki na magharibi kama ilivyokuwa wakati wa Nabii Ibrahim, na ningeijenga tena juu ya misingi iliyowekwa na Ibrahim.”

Bila shaka kama Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mwenyewe alikuwa hakuweza kupinga mageuzi makubwa yaliyokwisha kuanzishwa, Ali alikuwa na haki ya kutekeleza kanuni hiyo hiyo wakati alipokabiliana na changamoto kama hiyo. Faqihi mkubwa, Wasti Ibn Maghazili Shafi’i, na Khatib Khawarizmi wanasimulia katika Manaqib zao kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimuambia Ali: “Umma una kinyongo kikubwa dhidi yako.

Punde tu baada ya kifo changu watakulaghai na kufichua kile walichokuwa nacho katika nyoyo zao. Nakuagiza kuwa mvumilivu na ujizuiye mwenyewe kwa wakati huo ili kwam- ba Allah aweze kukupa malipo yake na fidia nzuri.

Baada Ya Kifo Cha Mtukufu Mtume Uvumilivu Wa Ali Ulikuwa Ni Kwa

Ajili Ya Allah

Pili, Amiru’l-Mu’minin kamwe hakujiangalia yeye mwenyewe bali alikuwa siku zote mwenye kumkumbuka Allah. Alikuwa amezama kabisa kwa Allah. Alijitolea yeye mwenyewe na watu wake kwenye utashi wa Allah. Kwa hiyo, subira na uvumilivu wake katika kupata haki yake ilikuwa kwa ajili ya Allah ili kwamba kusije kukawepo na kutokuelewana miongoni mwa Waislamu, na kwamba watu wasije wakarudia kwenye ukafiri wao wa zamani.

Wakati Fatima aliponyang’anywa mali yake, alirudi nyumbani akiwa amehuzunika na kuvunjika moyo. Alimuambia Ali: “Umerudi nyuma kama kilengwa. Umejitenga na ulimwengu kama mtu aliye shutumiwa na umevunja mbawa zako zifananazo na mwewe. Sasa mbawa hizo dhaifu za ndege hazikusaidii wewe.

Huyu Ibn Qahafa (Abu Bakr) ananinyang’anya kwa nguvu zawadi ya baba yangu na uwezo wa kujikimu wa watoto wangu. Kwa hakika watu hawa wamenitukana kwa nia mbaya ya wazi na kunikaripia.” Alizungumza kwa muda mrefu.

Mtukufu Imam alimsikiliza Fatima mpaka aliponyamaza. Kisha akampa jibu fupi ambalo lilimridhisha. Alisema: “Ewe Fatima! Katika suala la dini na kulingania haki, kamwe mimi sijawa mnyonge. Je, unataka kwamba hii dini takatifu ibakie imara na kwamba jina la baba yako mtukufu liwa linatajwa msikitini (katika adhana) hadi milele na miliele?” Akasema: “Ndio. Hiyo ndio hamu yangu kubwa.”

Ali akasema: “Basi lazima uwe na subira. Baba yako amenipa maelekezo kuhusu hali hii, na najua kwamba lazima niwe mvumilivu.
Vinginevyo, ninazo nguvu kiasi kwamba naweza kumshinda adui na kuirudisha haki yako kutoka kwao. Lakini lazima uelewe kwamba katika hali hiyo dini itaharibika. Hivyo, kwa ajili ya Allah na kwa ajili ya usalama wa dini ya Allah, kuwa mvumilivu. Malipo ya akhera kwa ajili yako ni bora kuliko haki ambayo imeporwa.”

Ni kwa aliji hii kwamba Amiru’l-Mu’minin aliifanya subira kuwa ni tabia yake. Alitwaa uvumilivu na kukaa kimya kwa ajili ya usalama wa Uislmu. Katika khutba zake nyingi amelirejea suala hili.

Maelezo Ya Ali Juu Ya Kufaa Kwa Kimya Chake Baada Ya Kifo Cha

Mtukufu Mtume

Ibrahim Bin Muhammad Saqafi, ambaye ni mmoja wa maulamaa wa kuaminika wa Sunni, Ibn Abi’l-Hadid, na Ali Ibn Muhammad Hamadani wanasimulia kwamba Talha na Zubair walivunja kiapo chao na wakaenda Basra, Ali aliamuru watu kukusanyika msikitini. Kisha baada ya kumshukuru Allah swt., alisema: “Baada ya kifo cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) tulisema kwamba sisi ni Ahlu’l-Bayti, warithi wake, na watu wenye haki kupokea mirathi yake. Hakuna mtu yeyote isipokuwa sisi tu anayeweza kudai utawala baada yake.

Lakini kikundi cha wanafiki kimepora utawala wa Mtukufu Mtume wetu (s.a.w.w.) kutoka kwetu na kuuweka kwa wale ambao walikuwa ni wapinzani wetu. Wallahi, nyoyo zetu na macho yetu yalilia kwa ajili hilo. Wallahi, tulijawa na huzuni kubwa na simanzi.

Naapa kwa jina la Allah kwamba kama kusingekuwa na hofu kwamba umma wa Kiislamu utaangamia, tungeweza kuupindua ukhalifa. Walikalia kiti cha utawala mpaka wakafikia mwisho wao. Sasa Allah amerudisha ukhalifa kwangu. Na watu hawa wawili (Talha na Zubair) vile vile walikula kiapo cha utii kwangu. Sasa wameelekea Basra wakidhamiria kusababisha gha- sia miongoni mwa watu.”

Miongoni mwa wanachuoni wenu wakubwa, Ibn Abi”l-Hadid na Kalbi, wamesimulia kwamba wakati wa kutoka kwake kwenda Basra, Ali aliwahutubia watu.

Yeye alisema: “Wakati Mtukufu Mtume wa Allah (s.a.w.w.) alipofariki, Makureishi walitushtukiza na wakatunyang’anya haki ambayo tuliistahiki zaidi kuliko yeyote yule. Hivyo niliona kwamba ni bora kuchukua subira wakati ule, kuliko kuwaacha Waislamu watetengane na damu yao kumwagwa, kwani walikuwa ndio wameingia kwenye Uislamu hivi karibuni tu.”

Ukimya wa Ali na kuacha kuupa changamoto ukhalifa wa Abu Bakr na Umar hakukuwa kwa ajili kupatana nao. Ilikuwa ni kwa sababu alitaka kuepusha kusababisha mgogoro mkali miongoni mwa watu na kwa sababu alitaka kuikoa dini kutokana na kuangamia.

Hivyo, baada ya miezi sita ya ukimya na kutokubali, basi, kama ilivyoelezwa na maulamaa wenu, alitoa kiapo cha utii na akashirikiana nao. Katika barua aliyoipeleka kwa watu wa Misri kupitia kwa Malik Ashtar, yeye anaandika wazi kwamba kimya chake kilikuwa ni kwa ajili ya kuhifadhi Uislamu.

Maandishi ya asili ya barua ya Ali ambayo Ibn Abi’l-Hadid ameyaandika katika Sharh-e- Nahju’l-Balagha, jalida ya 4, uk. 164, ni kama ifuatavyo:

Barua Ya Amiru’l-Mu’minin Kwa Watu Wa Misr Kuelezea Ukimya Wake Wakati Aliponyimwa Ukhalifa

Allah swt., alimtuma Muhammad kama shahidi wa mitume ili kuwaonya watu. Hivyo wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipokufa Waislamu wakabishana wenyewe kwa wenyewe kuhusu ni nani atakayemrithi.

Naapa kwa Allah kwamba kamwe sikufikiria au kuamini, wala hakukuwa na dalili japo kidogo juu ya hilo, kwamba watu wa Arabuni wataichukua haki ya urithi kutoka kwa Ahlu’l-Bayt na kuwapa wengine baada yao.

Ilikuwa haiwaziki kwamba baada ya kifo cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), pamoja na amri yake ya wazi, wao wangeninyima mimi haki hiyo.
“Nilihuzunishwa sana kwamba watu walikimbia kuelekea kwa mtu fulani (Abu Bakr) na kula kiapo cha utii kwake. Hivyo, nilijitenga mpaka nilipoona kwamba kundi la watu walikengeuka kutoka kwenye Uislamu na kukusudia kuuangamiza.

Kisha nikahofia kwamba kama sikuusaidia Uislamu na Waislamu, Uislamu ungepatwa na uharibifu kiasi kwamba ungezidisha maumivu kwangu kuliko ilivyokuwa kwa kuporwa ukhalifa. Bila shaka nguvu za kisiasa haziwezi kudumu kwa muda mrefu. Lazima zitatoweka kama mawingu. Ilikuwa ni kwa hali kama hizi kwamba ilinilazimu kusimama, ili kwamba upagani uweze kuwa mnyonge na Uislamu kuwa imara.”

Khutba Ya Amirul-Mu’minin Baada Ya Kuuawa Shahidi Kwa Muhammad

Bin Abu Bakr

Ibn Abi’l-Hadid katika Sharh-e-Nahju’l-Balagha, jalada la 2, uk. 35, anasimulia kutoka Kitabu’l-Gharat cha Ibrahim Ibn Sa’d Bin Hilal Saqafi, ambaye anasimulia kutoka kwa Abdru’r-Rahman Bin Jundab, ambaye anasimulia kutoka kwa baba yake kwamba wakati maadui walipoikalia Misr na Muhammad Bin Abu Bakr alipokuwa ameuawa, Amiru’l-Mu’minin alitoa khutba ambayo ndani yake alionesha hisia zake za uchungu dhidi ya msimamo waliouchukua Waislamu baada ya kifo cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Aliandika maelezo yake kwa watu wa Misri. Mtukufu Imam alisema: “Mtu mmoja aliniambia; ‘Ewe mwana wa Abu Talib! Uchu ulioje ulionao kwa ajili ya ukhalifa.’

Nikamuambia: ‘Wewe ni mwenye uchu zaidi kuliko mimi na uko mbali mno na kwenye nafasi hiyo. Nani mwenye uchu zaidi kati yetu? Je, ni mimi ambaye nadai haki yangu, ambayo kwamba Allah na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wamenifanya mimi mdai mwenye haki zaidi, au ninyi, ambao Mmenizuia haki hiyo na umeweka vikwazo kati yangu na haki yangu.?’“Wote walifungwa midomo na hawakuweza kusema hata neno moja. Hakika, Allah hawasaidii watu waovu.”

Maelezo haya na khutba nyingine za Imam Ali huonesha kwamba sababu ya Imam kutokumkabili adui, bali akachukua njia ya ukimya na (kama inavyosemwa na maulamaa wenu) akatoa kiapo cha utii baada ya miezi sita, haikuwa kwamba alikubaliana nao katika uamuzi wao kuhusiana na ukhalifa. Ilikuwa ni kwa sababu alihofia kwamba

Uislamu ungetoweka na kwamba Waislamu wangegawanyika. Kama Ali angesimama kuichukuwa haki yake, bila shaka baadhi ya watu wangemuunga mkono (wengi walimuomba kufanya hivyo) na vita ya wenyewe kwa wenyewe ingeanza.

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amekufa tu hivi punde. Waislamu walikuwa karibu sana na zama za ukafiri, na mizizi ya imani ilikuwa bado haijaimarika. Mayahudi, Wakirsto, waabudu masanamu, na wanafiki, ambao walikuwa maadui wakubwa, wangepata fursa ya kuharibu heshima ya Waislamu. Hatimaye Uislamu ungeanguka.

Amirul-Mu’minin aliyaelewa mambo haya. Aidha, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimuambia kwamba msingi wa Uislamu hautaharibiwa na kwamba dini ilikuwa kama jua, ambayo inaweza kufichwa wakati mwingine kwenye mawingu ya ujinga na uadui lakini mwishowe itajitokeza ikiangaza mwanga wake kila sehemu.

Kwa ufupi, alidai haki yake kwa muda wa miezi sita na akathibitisha usahihi wa haki yake katika idadi ya mikutano na mikusanyiko, lakini hakula kiapo cha utii. Ingawa hakukim- bilia kwenye kupigana, aliendelea kudai haki yake kwa hoja na malalamiko.

Khutba Ya Shaqshiqayya Vile Vile Inaelezea Ukimya Wa Ali

Mtukufu Imam alianza khutba yake ya Shaqishaqiyya kwa nukta ile ile.

“Wallahi! mwana wa Abu Qahafa (Abu Bakr) amejivisha nao (ukhalifa) ingawa kwa hakika alijua kwamba uhusiano wangu nao ulikuwa kama nafasi ya mhimili katika mashine ya kusaga, maji ya mafuriko yanatiririka kutoka kwangu, na hakuna anayeweza kufikia kiwango cha ujuzi wangu.

Nilijitenga na ukhalifa. Kisha nikaanza kutafakari iwapo niichukuwe haki yangu kwa nguvu au nivumilie giza hili kwa ukimya, ambalo kwalo aliye komaa anyongeshwa, mdogo anakua na kuwa mzee, na muumini wa kweli kwa anashughulika kwa mashaka mpaka akutanane na Allah (wakati wakufariki). Niliona kwamba subira ndio njia nzuri ya kufuata.

Hivyo, nilikuwa mvumilivu ingawa kulikuwa na muwasho kwenye macho na kusongwa kwenye koo. Nilitazama uporaji wa urithi wangu mpaka wa kwanza akaondoka. Lakini akaukabidhi ukhalifa kwa Ibn Khattab (Umar) baada yake.”

Khutba hii imejaa mihemuko mizito ya Ali. Lakini kiasi hiki kinatosha kuthibitisha nukta yetu.

Mashaka Kuhusu Khutba Ya Shaqshaqiyya

Sheikh: Kwanza kabisa khutba hii haithibitishi kutokuridhika kwa Imam. Pili, khutba hii haihusiani na Ali. Kwa kweli, ni kazi ya Seyyid Sharif Razi, ambaye aliijumuisha katika khutba za Ali. Kwa kweli Ali hana malalamiko dhidi ya makhalifa. Bali yeye alikuwa ameridhika kabisa nao.

Muombezi: Kauli yako hii imeegemea juu ya chuki ya hali ya juu kabisa. Kile ambacho Ali ameelezea na kulalamikia kimekwisha simuliwa mapema. Huzuni za Imam hazikuishia kwenye khutba hii. Tuhuma yako kwamba mtunzi wa khutba hii alikuwa ni yule mwanachuoni mashuhuri mchamungu, Seyyid Raziu’d-din, sio sahihi.

Wanachuoni wenu mashuhuri, kama Izzu’d-din Abdu’l-Hamid Ibn Abi’l-Hadid, Sheikh Muhammad Abduh, Mufti wa Misri, na Sheikh Muhammad Khizari katika Muhadhirat-e-Ta’rikhu’l- Uma’imu’l-Islamiyya, uk. 127, wametamka kwamba khutba hii ni ya Ali.

Wanachuoni wenu wenyewe wameandika sharhe juu ya khutba hii. Baadhi ya maulamaa wenu washupavu wa zama za baadae kidogo walifanya juhudi kubwa kusababisha mashaka kuhusu usahihi wake, lakini hakuna yeyote katika zaidi ya wale maulamaa mashuhuri arobaini wa Sunni na Shia, ambao wameandika sharhe juu ya Nahju’l-Balagha, aliyesema kitu cha ajabu kama hicho.

Seyyid Razi

Bila shaka, mwanachuoni mchamungu mkubwa, Seyyid Raziu’d-din, angezuia kuhusisha moja ya khutba zake kwa Ali. Aidha, wataalamu katika lugha ya Kiarabu na fasihi yake ambao wamechunguza khutba za Nahju’l-Balagha wameamua kwamba, kwa mtazamo wa mtindo bora na fikra za kina, kazi hii (khutba) haiwezekani kuigwa na mtu yeyote.

Maulamaa wenu mashuhuri, kama Izza’d-di Abdu’l-Hamid Bin Abi’l-Hadid Mut’azali na Sheikh Muhammad Abduh, wamekiri kwamba uzuri na ujuzi wa kina wa khutba za Ali huthibitisha kwamba kazi hii iko chini katika ubora tu kwa maneno ya Allah na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Ibn Abi’l-Hadid anamsimulia Musaddiq Bin Shabbib akisema kwamba mwanachuo mashuhuri Ibn Khashshab alisema: “Haiwezekani kwa Razi au kwa yeyote yule kutoa mtungo kama huu. Tumezipitia kazi za Razi; haziwezi kulinganishwa na maandiko haya na khutba hizi tukufu.”

Khutba Ya Shaqshaqiyya Iliandikwa Zamani Kabla Ya Kuzaliwa Kwa Seyyid Razi

Wakipuuza vipengele vingine vyote vya suala hili, wanachuo wengi, muhadithina, na wanahistoria (wote Shia na Sunni) wamesimulia juu ya kuwepo kwa khutba hii kabla ya kuzaliwa kwa mwanachuoni huyu mkubwa Seyyid Razi na baba yake Abu Ahmad Naqibu’t-Talibin.

Ibn Abi’l-Hadid katika Sharh-e-Nahju’l-Balagha anaandika kwamba aliiona khutba hii katika vitabu vya Sheikh wake, Abu’l-Qasim Balkhi Imam-e-Mut’azila, ambaye aliishi katika wakati wa Muqtadir B’illah Abbasi. Ni dhahiri, Seyyid Razi alizaliwa muda mrefu baada yake.

Vile vile anaandika kwamba aliiona khutba hii katika Kitabu’l-Insaf, cha mubalighin mashuhuri, Abu Ja’far Bin Qubba, ambaye alikuwa mmoja wa wanafunzi wa Sheikh Abu’l-Qasim Balkhi na ambaye amekufa kabla ya kuzaliwa Seyyid Razi.

Vile vile Sheikh Abu Abdullah Bin Ahmad, anayejulikana sana kwa jina la Ibn Khashshab, anasimuliwa kwamba alisema: “Niliiona kutba hii katika vitabu vilivyoandikwa miaka 200 kabla Seyyid Razi hajazaliwa. Vile vile nimeiona khutba hii katika vitabu vya wanachuo wa fasihi ambao wameviandika kabla ya kuzaliwa baba yake Seyyid Razi, Ahmad Naqibu’t-Talibin.”

Amma kwa madai yako kwamba Ali alikuwa ameridhika na wapinzani wake. Haya bila shaka yanapuuza kauli zisizoidadi za kinyume chake zilizotolewa na maulamaa wenu, ambazo nimezionesha huko nyuma. Nitaonesha mfano mwingine tena bado. Ibn Abi’l- Hadid katika Sharh-e-Nahju’l-Balagha, jalada la 2, uk. 561, anamsimulia Ali akisema: “Nilibakia na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kuanzia mwanzo mpaka kifo chake.

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipumua pumzi yake ya mwisho juu ya kifua changu. Alikuwa ni mimi niliyeuosha mwili wake pamoja na msaada wa malaika, niliendesha sala ya mazishi yake, na nikamzika. Hivyo, hakuna mtu yeyote aliye karibu zaidi naye, au mrithi wa haki zaidi kwake kuliko mimi.”

Kuelekea mwisho wa khutba yake anawataja wapinzani wake katika maneno haya: “Naapa kwa jina la Allah, aliye Mmoja, kwamba niko kwenye njia iliyo sahihi na kwamba hao wapinzani wangu wako kwenye njia ya upotofu.”

Lakini wewe unadai kwamba Ali aliwachukulia wapinzani wake kuwa katika njia sahihi. Natamani ungeiangalia kwa makini ile aya ya Qur’ani Tukufu inayosema:

يُرِيدُونَ أَنْ يُطْفِئُوا نُورَ اللَّهِ بِأَفْوَاهِهِمْ وَيَأْبَى اللَّهُ إِلَّا أَنْ يُتِمَّ نُورَهُ وَلَوْ كَرِهَ الْكَافِرُونَ {32}

Wanataka kuzima nuru ya Allah kwa vinywa vyao, lakini Allah amekataa isipokuwa kutimiza nuru Yake, ijapokuwa makafiri wanachukia.” (9:32)