read

Peshawar(Mikesha Ya Peshawar)

Sultanu’l-Wa’izin Shirazi, mwanachuo mkubwa wa Iran, alitembelea India mwaka wa 1927 (1345 A.H.) wakati akiwa na umri wa miaka 30. Alipata makaribisho makubwa popote alipokwenda. Watu walinufaika kutokana na ujuzi wake wa hadithi, historia, na tafsiri juu ya Qur’ani Tukufu.

Alishauriwa kuingia katika mjadala wa kidini tarehe 23 Rajab, 1345 A.H., na watu wa imani nyingine katika eneo la Peshawar, eneo ambalo lilikuwa ni katika India na ambalo leo ni eneo la Pakistan. Mjadala ulifanyika kwa muda wa mikesha kumi mfulululizo.

Washiriki wakubwa wawili kutoka upande mwingine walikuwa ni wanachuoni maarufu wa Kabul, Hafidh Muhammad Rashid na Sheikh Abdul’s-Salam. Waandishi wanne waliandika taarifa za mjadala huo mbele ya watu takirban 200 (Shia na Sunni).

Magazeti ya sehemu hiyo yaliandika taarifa za mjadala huo kila siku asubuhi iliyofuatia. Sultanu’l-Wa’idhin alikusanya maelezo ya magazeti kuhusu mjadala huo katika kitabu nchini Iran, na kuchapishwa Tehran kama Shabhaye-Peshawar, au Peshawar Nights ifuatayo ni tarjuma ya kitabu hicho: