read

Lengo La Israa Na Miraji

Tukitaka kujuwa shabaha na hekima na muujiza wa Israa na Miiraji, lazima kusoma nassi zake na vipengele vyake kwa undani na makini. Na hapa tutaonyesha mambo yafuatayo:

Israa na Miiraji ni muujiza mkubwa wa kudumu, na leo katika karne hii ya ishirini tukio hili linakubaliwa na elimu ya sayansi na Teknolojia. Mwanadamu hashangai tena leo kusikia kuwa mtu amekwenda umbali wa maili nyingi zaidi katika upeo wa juu.

Mwenyezi Mungu ametaja wazi lengo la msafara huo aliposema:
"LINURIYAHU MIN AYAATINA", yaani, "Ili tumuonyeshe baadhi ya Aya (ishara) zetu" 17:1.

Kwahiyo, lengo ni kumuonyesha Mtume (s.a.w.) baadhi ya ishara za utukufu wa Mwenyeezi Mungu. Na kwakupelekwa Mtume Israa na Miiraji, kumefunguwa moyo wake na akili yake zaidi kwa kupata taaluma kubwa katika ulimengu huu anaouongoza.

(c) Mwanadamu (hasa Mwarabu) wakati huo aijishi katika ulimwengu finyu sana, na akili duni iliyofungwa katika tundu dogo. Kwa sabaha hii ikawa dharura kufunguliwa macho yake na moyo wake ili aujue ulimwengu anaoishi, ambao Mwenyeezi Mungu amemfanya awe khalifa wake.

Khadija Aliolewa Na Yeyote Kabla Ya Mtume?

Inasemekana kuwa: Mtume (s.a.w.) hakuoa mke yeyote aliye bikira isipokuwa Mwana Aisha tu. Wanasema kuwa: "Mwana Khadija kabla ya kuolewa na Mtume (s.a.w.) alikwisha olewa na waume wawili kabla ya Mtume Muhammad (s.a.w.) na amepata watoto wawili.

Tutataja kidogo hapa baadhi ya hoja zinazosemwa juu ya Mwana Khadija kuhusu watoto aliopata kwa waume wengine kabla ya Mtume Muhammad (s.a.w.) ni kama ifuatavyo:

Wanasema: Shahidi wa kwanza katika Uislamu ni mtoto wa Mwana Khadija aitwae Harithi bin Abi Hala, alipata shahada pale Mtume (s.a.w.) alipotangaza Uislamu hadharani.

Taz: Al' Isaba J. 1 Uk. 293

Al'Awaail J. 1 Uk. 311-312

Lakini, hoja hii inaangushwa na riwaya ya Qatada inayosema kuwa: Shahidi wa kwanza katika Uislamu ni Sumayya, mama yake Ammar bin Yasir.

Taz: Al' Isaba J. 4 Uk. 335

Imepokewa kuwa: Mwana Khadija (a.s) alikuwa na nduguye akiitwa Hala, aliolewa na mtu mmoja katika Koo ya Al'Makhzumi, akazaa mtoto wa kike jina lake Hala, Kisha aliachika akaolewa na mtu mmoja katika Koo ya At'Tamim aitwaye Abu Hindi, akamzalia mtoto jina lake Hind. Huyu Abu Hindi, alikuwa na mke mwingine ambaye alimzalia watoto wawili: Zaynab na Ruqayya.
Hatimae Abu Hindi na mkewe wa pili walikufa,akabakia Bi Hala ndugu ya Mwana Khadija, pamoja na watoto wawili: Zaynab na Ruqayya. Yule mtoto wake wa kuzaa: Hind, alikwenda kwa jamaa za mumewe. Ndipo Mwana Khadija alipowakusanya wote akawa nao, Bi Hala na watoto wawili walioachwa na mama yao: Zaynab na Ruqayya.
Mwana Khadija alipoolewa na Mtume (s.a.w.) Bi Hala alifishwa, wakabaki Zaynab na Ruqayya wakilelewa na Mtume (s.a.w.). Katika mila za Kiarabu, walikuwa wakiamini kuwa mtoto wa kufikia ni mtoto wako halisi, kwa hiyo, watoto hawa wakapewa ubinti wa Mtume (s.a.w.) (Zaynab binti Muhammad na Ruqayya binti Muhammad).

Taz: As' Sahihu Minsiiratin Nabi J. I Uk. 123

Majibu Yetu

Katika kitabu "Asha'shaafy" na "At Talkhis" inasema Mtume (s.a.w.) amemuoa Mwana Khadija akiwa bikira.

Amesema Abulqasim Alkufy: Mtume (s.a.w.) alipomuoa Mwana Khadija (a.s.) wanawake wa kikuraishi walimkasirikia sana Mwana Khadija wakisema: Wamekuposa mabwana wa kikuraishi wenye heshima, umekataa kuolewa na yeyote kati yao, umekubali kuolewa na Muhammad, yatima wa Abu Talib Lofa hana mali!!

Taz: Al' Istighatha J. 1 Uk. 70