read

Qur'an Imeumbwa

Ndugu zetu masunni wanaamini kuwa: Qur'an ni ya tangu na tangu (Qadim) Mashia Ithan Ashar wanaamini kuwa: Qur'an imeumbwa.

Kwahiyo, hapa tutachunguza kama ifuatavyo: Katika matumizi ya lugha ya kiarabu, tamko la "JAA'L".

Linapotegemezwa kwa Mwenyeezi Mungu huwa kwa maana ya "KHALQ" yaani, "KUUMBA". Na hapa tutataja baadhi ya mifano hiyo:

"Wajaa'la min'ha zawjaha" yaani, "Na ameumba mkewe".

"Huwalladhi jaa'la lakumul layla" yaani, "Yeye ndiye aliyewaumbia usiku".10:6

"Inna jaa'lna maa'l ardhi ziinatan laha" yaani, "Kwa hakika tumeviumba vyote vilivyoko juu ya ardhi viwe mapambo yake". 18:7

"Jaa'la laum min anfusikum az'wajan" yaani, "Amewaambieni wake katika jinsi yenu". 42:11

"Inna jaa'lnahu Qur'anan a'rabiyyan" yaani, hakika tumeifanya (tumeiumba) Qur'an (kwa lugha ya) Kiarabu". 43:3

"Khaaliqu kulli shay'in" yaani, "Muumba wa kila kitu". 6:102

Sasa, Qur'an ama iwe ni kitu au isiwe ni kitu. Kama itakuwa sikitu, basi yanini kujadili jambo ambalo halipo!! Na endapo itasemwa kuwa Qur'an ni kitu, jee! Ni kwa hoja gani Qur'an itatolewa katika umuun ya ibara hii: "Muumba wa kila kitu"? Na hapana shaka yoyote, Qur'an ni kitu, kwa hiyo: kwakuwa vitu vyote vimeumbwa (kama isemavyo Qur'an) Qur'an nayo pia imeumbwa.

Taqiyya

Maana ya Taqiyya, kama alivyo tafsiri Sahaba Abdullah ibn Abbas ni "Kusema kwa ulimi na hali moyo unatulia kwa imani". Kwa hiyo, Taqiyya ni kuficha imani ndani ya moyo, na kutamka kwa ulimi yaliyo kinyume na ya moyoni.

Taz: Tafsirul Qurtubi, J. 4, Uk. 57

Kwakupata ufafanuzi katika somo hili, tumsikilize Imam Bukhari anasema: "Imepokewa kutoka kwa Abu Dardai anasema: 'Hakika sisi wallahi tunawakenulia jamaa ili hali nyoyo zetu zinawalaani."

Taz: Tafsir ibn Kathir J.1, Uk. 365

Safwatut Tafasir J.1, Uk.196

Abu Dardai anatufahamisha hapa yakuwa: Wao wanapojumuika na baadhi ya watu wasioafikiana nao katika jambo fulani, huchanganyika nao kwa bashashi kubwa kwa kicheko na kukenua mena kama kwamba wanakubaliana na yao. Kumbe ndani ya mioyo yao wanawalaani!!!
Hii ndiyo Taqiyya tunayo izungumza hapa, na ndiyo Taqiyya aliyoisema Mwenyeezi Mungu:

"Waumini wasiwafanye makafiri kuwa viongozi badala ya waumini. Na atakaefanya hivyo, basi hatakuwa na chochote kwa Mwenyeezi Mungu, isipokuwa kwa kujilinda nao sana" 3:28.

Iliposemwa: "Na atakaefanya hivyo" maana yake: "Atakaewafanya makafiri kuwa viongozi wake" Mwenyeezi Mungu anamwambia: "Hatakuwa na chochote kwa Mwenyeezi Mungu". Kwa mantiq hii, Mwislamu yeyote anayeongozwa na kafiri, hana chochote kwa Mwenyeezi Mungu. Mpaka hapa hukumu hii itawagusa Waislamu wengi sana! Lakini Alhamdulillah hali haiko hivyo, kwa sababu ibara katika Aya inaendelea kusema: "Isipokuwa kwa kujilinda nao sanasana". Taqiyya imemuopoa Mwislamu katika hukumu aliyohukumiwa laiti isinge kuwapo Taqiyya.

Kwa ajili hii, sahaba Ammar bin Yasir alipoadhibiwa na makafiri, akauliwa mama yake, Sumayya, mbele ya macho yake baada ya kuteswa sana. Hilo halikutosha, akachukuliwa baba yake Yasir akawekwa mbele ya macho yake, akateswa sana hatimae akauliwa, kisha ndipo walipomgeukia naye Ammar, akapigwa na kuteswa, Ammari ndipo alipotamka neno la kufru.

Alipofika kwa Mtume (s.a.w.) Ammar aliliya sana na kusema: "Ewe Mjumbe wa Mwenyeezi Mungu, nitauweka wapi uso wangu ili hali mimi nimesema neno chafu (la kufru) baada ya kuteswa sana, na kuniulia mbele ya macho yangu wazazi wangu wawili baba na mama!! Kabla Mtume (s.a.w.) hajasema lolote Mwenyeezi Mungu akateremsha Aya:
"Anayemkataa Mwenyeezi Mungu baada ya imani yake (ataadhibiwa adhabu kali) isipokuwa yule aliyelazimishwa hali moyo wake unatulia kwa imani 16:106.

Mtume (s.a.w.) akamsomea Aya hii Ammar bin Yasir, kisha akamwambia: "Basi, kama watarudia (kukutesa) rudia (nawewekuwapa maneno ya kufru).

Taz: Tafsir Ibn Kathir J. 2 Uk. 609

Tafsirul Qurtubi J. 10 Uk. 180

Tafsirul Khaazin J. 4 Uk. 117

Tafsirul Maraghi J. 14 Uk. 146.

Hii ndiyo Taqiyya wanayoelekezwa waumini, kama ambavyo Taqiyya inamfikisha Mwislamu katika ngazi ya Uumini. Mwenyeezi Mungu anasema:

"Na akasema mtu muumini aliyekuwa mmoja wa watu wa Firauni anayeficha imani yake, jee! Mtamuua mtu kwa sababu anasema Mola wangu ni Mwenyeezi Mungu’ 40:28.

Huyu bwana alionyesha ukafiri, akasihi pamoja najamaa yake Firauni, lakini kwa ndani alikuwa muumini kweli kweli, akatumia Taqiyya ili Firauni asimjue.

Mpenzi msomaji! Bila shaka umeona nafazi ya Taqiyya iliyo nayo katika Uislamu, umefahamu kuwa Taqiyya ni kiungo muhimu sana kati ya Islam na Mwislamu. Umesoma Aya zilizozungumza kuhusu Taqiyya umemuona Sahaba Ammar bin Yasir alivyowakejeli makafir kwa kutamka neno Ia kufru, kisha Mtume (s.a.w.) akaongeza kusema: "KAMA WATARUDIA NAWE RUDIA".

Tahriful Qur'an

Takriban, kuna aina tano za Tahrif, nazo ni kama ifuatavyo:

Kupungua, au kuzidi, harfu au haraka, wakatihuo huo Qur'an isipotee kitu chochote.

Tahrif aina hii, inapatikana katika Qur'an, hili linashuhudiwa kama ifuatavyo:

Katika Surat Hud Aya 78 inasomwa: "HUNNA AT'HAARU LAKUM" katika silabi ya RAA kumetiwa dhamma, na katika qiraa kingine, inasomwa: "HUNNA AT'HARA" kwa nasbu.

Taz: Tafsirul Qurtubi J. 9 Uk. 76

Katika Surat Sabai Aya 19 inasomwa: "RABBANAA BAAI'D BAYNA ASFARINA" na katika qiraa kingine, inasomwa:- "RABBANAA BAA'DA" kwa madhi.

Taz: Tafsir Qurtubi J. 14 Uk. 290

Katika Suratul Baqara Aya 259 inasomwa: "KAYFA NUNSHIZUHA" na katika qiraa kingine, inasomwa: "KAYFA NUNSHIRUHA" kwa silabi ya RAA badala ya ZAA.

Katika Suratul Waqia'h Aya 29 inasomwa:"WATWAL'H'IN MANDHUD" na katika qiraa kingine inasomwa: "WATWAL'I'N MANDHUD" kwa A'YN badala ya H'AA.

Katika Surat Saad Aya 23 inasomwa: "LAHU TIS'U'N WATIS'U'NA NAA'JAH" na katika qiraa kingine inasomwa: "LAHU TAS'U'N WATAS'U'NA".

Kupungua, au kuzidi neno moja au zaidi. Pamoja na kuwa nafsi ya Qur'an itabaki salama bila ya kupungua au kuzidi kitu.

Katika zama za masahaba hali hii imetokea, ambapo Uthman bin Affan aliiunguza moto misahafu mingi. Na akatoa agizo kwa wawakilishi wake wote popote walipokuwa, waichome moto misahafu yote isipokuwa ile aliyoikusanya yeye.

Taz: Manahilul I'r fani J. 1 Uk. 253

Kuzidi au kupungua katika Aya au sura. Pamoja na kuwepo ukamilifu wa Qur'an, na wakaafikiiana Waislamu wote kuwa: Mtume (s.a.w.) aliisoma. Hali hii ipo, na mfano halisi ni kama ifuatavyo: "BISMILLAHIR RAHMANIR RAHIM" Waislamu wote wanakubaliana kuwa, Mtume (s.a.w.) alikuwa akiisoma kabla ya kila sura isipokuwa Suratut Tawba.

Kwa ndugu zetu Masunni imetokea hitilafu kati yao kuwa: "Bismillahi" si katika Qur'an, wengine wakasema: Ni katika Qur'an.

Taz: Tafsirul Alus J. 1 Uk 39

Tafsir lbn Kathir J. 1 Uk. 17

Tafsirul Khazin J. 1 Uk. 18

Tafsirush Shawkan J. 1 Uk. 7

Ama Shia Ithna Ashar, wao wanakubaliana kuwa "Bismillahi" ni sehemu ya kila sura isipokuwa Suratut Tawba.

Kuzidi baadhi ya Aya au sura yasiyokuwa Maneno ya Mwenyeezi Mungu. Tahrif aina hii haikubaliwi na Waislamu wote.

Kupungua, yaani, Msahafu huu uliopo mikononi mwa Waislamu haukukusanya Qur'an yote iliyoteremshwa na Mwenyeezi Mungu, na kwamba Qur'an nyingine imepotea, Tahrif ama hii ipo, wako wanaothibitisha hilo, na wengine wanakataa kuwa haiko.

Wanaothibitisha Kuwa Ipo

Amepokea Ibnu Abbas kwamba: "Umar bnul Khattab, siku moja alipokuwa juu ya Mimbar alisema: "Sisi tulikuwa tukisoma katika Qur'an: AN LAA TARGHABU A'N ABAAIKUM FAINNAHU KFRUN BIKUM AN TARGHABU A'N ABAAIKUM"...

Taz: Sahihi Bukhari J. 8 Uk. 26

Sahihi Muslim J. 5 Uk. 116

Umar bnul Khattab alileta Ayatur rajmi ili itiwe katika msahafu, lakini haikuandikwa, kwa sababu Umar alikuwa peke yake hakuwa na shahidi.

Taz: Al' It'qan J. 1 Uk. 101

Aya yenyewe aliyoileta Umar inasomeka hivi: ASH'SHAYKHU WASH'SHAYKHATU IDHA ZANAYAA FARTUMUHUMAA ALBATTATA NAKAALAN MINALLAHI WALLAHU A'ZIZUN HAKIMUN".

Taz: Tafsirul Qurtubi J. 14 Uk. 113

Al' It'qan J.2 Uk.32

Inasimuliwa kuwa: katika mbao za Mwana Aisha ilikuwako Qur'an ikisomeka hivi: "INNA LLAHA WAMALAIKA TAHU YUSWALLUNA A'LAN NABIYY YA AYYUHA LLADHINA AMANU SWALLU A'LAYHI WASALLIMU TASLIIMA WA A'LALLADHI NA YUSWALLUNA ASSUFUFAL AWWALA"

Mwana Aisha (mkewe Mtume) alikuwa nayo Qur'an hiyo kabla Uthman bin Affan hajabadilisha misahafu!!

Taz: Al' It'qan J. 2 Uk. 33

Anasema Mwana Aisha (mkewe Mtume) katika zama za Mtume (s.a.w.) Suratul Ahzabi ilikuwa inafikia Aya mia mbili, lakini, ulipoandikwa msahafu Aya zikawa hivi kama zilivyo sasa ambazo ni sabini na tatu tu!! Aya mia moja ishirini na saba zimepotea!!!

Taz: Tafsirul Qurtubi J. 14 Uk. 113

Waliosema Kuwa Haipo

Mizani ya kupima riwaya zilizo tajwa hapo juu kuonyesha kuwa kuna baadhi ya amma sura au aya zilizopotea, riwaya hizo na za mfano wa kama hizo ni batili, Mwenyeezi Mungu anasema:- (Qur'an)
"Haitaifikia batili mbele yake wala nyuma yake" 41:42
"Hakika sisi tumeiteremsha Qur'an, na hakika sisi ndio wenye kuilinda" 15:9. Hii ndio itikadi ya Shia Ithna Ashar.

Taz: Al'I'tigad J. 1 Uk. 16

Tafsir Aalair Rahman J. 1 Uk. 25

Albayan fit'tafsiril Qur'an Uk. 213

Tafsirul Qur'an, assayid shubbar Uk. 17