read

Idhaa Ya Sauti Ya Ujerumani

Tarehe 18/9/1989, katika majira ya saa moja kasorobo asubuhi. Sauti ya Ujerumani ilitangaza kuwa "Katika nchi ya Morocco, ndoa ya Mut'a imeshika nguvu sana. Vijana wa kiume na wakike wanaowana Mut'a kwa idadi kubwa, na inasemekana kuwa Masaudi wengi wanakwenda Morocco kwa ajill ya kuowa Mut'a. Mwanamke wa Morocco hujulikana kuwa ameolewa Mut'a kwa kuonekana mapambo ya dhahabu aliyonayo ambayo huyapata kwa Masaudi."

Basi tunataraji nchi nyingine zitachukua mfano wa Morocco kwa kuimarisha ndoa ya Mut'a. Lakini jukumu hili zaidi linawakabili Waislamu wake kwa waume popote walipo kuisoma na kuitumia ndoa hii, kwa sababu ni Sharia ya Mwenyeezi Mngu na Mtume wake.

Mwenyeezi Mngu anasema:- Haiwi kwa mwanamume aliyeamini wala kwa mwanamke aliyeamini, Mwenyeezi Mngu na Mtume wake wanapokata shauri, wawe na khiyari katika shauri lao. Na mwenye kumuasi Mwenyeezi Mungu na Mtume wake, hakika amepotea upotovu uliowazi." 33:36.