read

Kurithi

a) Mwanamke Ahlulkitabi aliyeolewa na Mwislamu, hawezi kumrithi mumewe.

TAZ: Bidayatul Mujtahid J. 2 uk. 381 Sublus salam J. 3 uk. 954

b) Mwanamke aliyemuua mumewe. Amesema Mtume S.A.W. "Muuwaji hana kitu."

TAZ: Fiqhus Sunna J. 3 uk. 427.

Kwa hiyo majibu yetu hapa ni:-

Ndoa ya Mut'a inatimia bila ya Waiji, wala shahidi, wala chakula, wala kurithiana.

Zaidi ya hayo, tunayaona ya Umar bunul Khattab:- Imepokewa kwa:- Abu Salamata bin Sufyani kuwa:- Mwanamke mmoja alikuja kwa Umar bunul Khattab akamwambia:- "Ewe Amierul Muuminina! Nilikwenda kwenye soko la mbuzi wangu, akanikuta mtu mmoja. Akanikusanyia mafungu matatu ya tende, kisha amenichukua. Umar akamuuliza, unasemaje? Yule mwanamke akarudia kama alivyosema kwanza. Umar akamwambia, (hayo ni) Mahari, mahari, mahari, kisha akamwacha (akaenda zake).

TAZ: AL'MUHALLA J.11 uk. 250.

Je! Palikuwa na walii hapo?

Palikuwa na Shahidi?

Sheikh Muhammad vilevile amesema:- "Sisi hatusemi kwamba mut'a haikuwako katika Uislamu, mut'a ilikuwako: Wahaswalatil mut'a fyi dhurufin qasin (Imepatikana mut'a katika mazingira magumu) Wakati wana shida, masahaba wametoka wamekwenda vitani, wameketi muda mrefu, wenda mshitakia Mtume Alaa Nastakhswi Ya Rasulallah? (Je! tujivunje maume?) Shida! Waenda kwa Mtume S.A.W. kwamba afadhali tujikhasi. Mtume S.A.W. akawaambia:- La, la, la, la, ila hilo! haiwezekani! Wakapatiwa nafasi ya mut'a kwa dharura. Wakati wa vita nje ya Mji! Hawako Mjini kwao." Mwisho wa kunukuu.

TUNAULIZA:- Je! Dharura hiyo sasa haipatikani? Watu hawasafiri nje ya miji yao?

Masheikh wa kisunii wanakubali kuwa: Dharura hiyo iko, isipokuwa hawapendelei kuiondoa kwa Mut'a badala yake baadhi yao wanapendelea Ponyeto (kujipuli) maana yake kuchezea utupu kwa mkono au na kitu kingine kwa kuwezesha kutoa manii. Wengine wanapendelea Khadaa. Baadhi ya masheikh wa Kihanafi na baadhi ya masheikh wa Kihanbali.

Taz

Sublus Salami J. 3 uk. 974

Fiqhus Sunna J. 2 uk. 368

Alhalalu Walharamu uk. 161

Kwa upande wa pili wa wanaopendelea Khadaa:-

Amesema Ahmad bin Taymiyya:- "Mtu akisafiri nje ya Mji wake

(basi anayo haki ya) kuoa, atatia nia moyoni mwake kuwa, 'Ninamuoa mwanamke huyu kwa muda fulani, na nikisha rejea Mjini kwangu nitamwacha.'"

TAZ: Fatawa ya Ahmad bin Taymiyya J. 32 uk. 147.

Maana yake, Mwanamke aliyeolewa kwa ndoa namna hii yeye huwa hajui kuwa ufikapo muda fulani (alionuia mume) ataachika. Bali yeye mwanamke analolijua ni kwamba: Ameolewa na wataishi na mumewe daima!! Kumbe amehadaiwa!!! Je! lipi bora:-

Mut'a au kupoteza watoto kwa kujipuli?

Mut'a au kumhadaa mwanamke na ukawa utamwacha ghafla?

Khulasa

a) Mut'a ilikuwako wakati wa Mtume.

b) Ndoa hiyo si upuuzi, hasha Mtume S.A.W. kuruhusu upuuzi.

c) Si kosa kuwa haina shahid, Walii, chakula wala kurithi.

d) Hata ndoa za daima, kwa Sunni huwa hivyo.

e) Dharura iliyowekewa Mut'a mpaka leo iko, kwa hivyo lazima iendelee.

f) Baadhi ya masheikh wa kisunni wanakubali kuwa dharura iko, lakini wao wanapendelea kujipuli na kuhadaa. LIPI BORA!!