read

Mut'a

Kwanza kabla ya yote lazima tujue Mut'a ni nini.

Sheikh Muhammad Sharif ameeleza hivi "Nikaha ya Mut'a ni:Mtu kukutana na mwanamke akamwambia: Mama! hebu nikuoe kiasi cha dakika kumi". Amuoe kwa dakika kumi, akisha ampe kama ni shilingi kumi an shilingi tano, khalas! mambo yamekwisha. Hiyo ndiyo nikaha ya mut'a, haina haja ya shahidi, haina haja ya Walii, hakuna habari ya chakula, hakuna kurithiana, na muda ukisha, khalas, hakuna nikaha tena mpaka uongezwe (baada ya kuieleza hivyo, akasema) Sallaaaaa La! Si upuuzi huo. (watu wakacheka) Mwisho wa kunukuu.

Sasa, tuyajadili maneno hayo:

A) Sheikh Muhammad kwanini hakutoa taarifa ya Mut'a ya ki Istilahi? Kwa faida ya wasomaji wetu, hapa tutatoa taarifa ya Mut'a:-

Mut'a ni: "Kukuoza mwanamke nafsi yake kwa kutaja mahari, na kwa muda maalumu".

B) Sheikh baada ya kutoa taarifa yake akasema:-

Sallaaaala! Si upuuzi huo, yaani Ndoa ya Mut'a ni upuuzi! TUNAULIZA:- Ikiwa anakubali ilikuwako kwa Mtume S.A.W. hiyo ni upunzi? Mtume S.A.W. anafanya upuuzi? Au wakati huo ilikuwa na Shahidi? au Waili? au mirathi? au chakula?

C) Pengine Sheikh anaona ajabu vipi mke wa Mut'a atakuwa Zawj hali ndoa yake haina: Shahidi, Walii, Chakula, mirathi. Hilo lisimshtue! Hata kwa ndoa ya daima huwezekana hilo.

Walii

Amesema Abu Hanifa na Zufar na Sha'aby na Zuhry:

"Atakapofunga ndoa mwanamke bila ya walii na akawa mume huyo ni kuf'u (anayefanana naye kwa akhlaq) ndoa hiyo ni sahihi".

TAZ: Bidayatul Mujtahid J. 2 uk. 10 Mughni ya Ibnu Quddama J. 7 uk. 337.

Shahidi

Amesema Ibn Mundhir:- "Haikuthibiti habari yoyote (sahihi) katika kushuhudia ndoa." Na hivi ndivyo walivyokuwa wakifanya (kuoa bila ya kuweka mashahidi) Abdullah bin Umar (mtoto wa Khalifa wa pili) na Alhasan bin Ali, Ibnuz Zubeir, Salim, na Hamza (watoto wa Ibnu Umar).

Taz

Mughni ya Ibnu Quddama J. 7 uk. 339

Nailul Awtar J. 6 uk. 260

Fiqhus Sunna J. 2 uk. 57

Bidayatul Mujtahid J. 2 uk. 19

Ikhtilaful Ulamaa uk. 123

Chakula

Amesema Muhammad Abdul Rahmani:- "Mwanamke Nashiz (anaegoma kuingiliwa na mumewe) ni haramu kwa Ijmai, kunaondoa haki ya kupewa chakula".

TAZ: Rahmatul Umma fyi Ikhtilafil aimma uk. 224.

Imepokewa kutoka kwa Nakh'i na Sha'aby wamesema:

"Chakula ni mukabala wa jimai (kumwingilia) atakapozuia kuingiliwa, atazuiliwa kupewa chakula".

TAZ: Fiqhus Sunna J. 2 uk. 151 na 149