read

Ndoa Ya Mut'a Katika Sunna

Imepokewa kwa Jaabir Bin Abdullah Al'Ansar amesema:-

"Sisi tulikuwa tukifanya Mut'a wakati wa Mtume S.A.W. na wakati wa Abubakar na nusu katika utawala wa Umar, kisha akaikataza Umar."

TAZAMA:

• Fat'hul Bari J. 11 uk. 76

• Umdatul Qary J. 8 uk. 310

• Sharhu Sahihi Muslim J. 8 uk. 233

• Musnadu Ahmad J. 3 uk. 380

• Bidayatul Mujtahid J. 2 uk. 58

• Zadul Maad J. 1 uk. 208 - 209.

Sheikh Muhammad Sharif yeye anasema"ILIKUWAKO" si sawa na "IKO MPAKA LEO" Basi jambo gani lililofanya Shia waamini iko mpaka leo? Ni sababu nne:

1. Ni mutawatir katika vitabu vyetu vya hadithi, hilo peke yake linatosha.

2. Haijathibiti kuwa imenasikhiwa, hata kwa hadithi za Sunni kama tulivyoona katika masomo yaliyopita.

3. Lililothibiti ni kuwa iliendelea baada ya Mtume S.A.W. kufariki.

4. Sayydna Umar ndiye aliyeiondoa na yeye hana uwezo huo. Ushahidi, aliyeiondoa ni Umar:- Amesema Umar bunul Khattab:- "Mut'a mbili zilikuwako wakati wa Mtume, na mimi nazikataza na natoa adhabu (kwa atakefanya) Tamauuu ya Hija na ndoa ya Mut'a.

TAZAMA:

Tafsirul Kabir 3.3 uk. 200

Musnad Ahmad J.1 uk. 52

AI'Mughuniya ya Ibnu Quddama J. 7 uk. 572

Sheikh Muhammad Sharif anashangaa, vipi sahaba walimwogopa Umar, wakanyamaza wasimpinge?

Jawabu:- Hakuogopewa. Wako waliompinga kwa vitendo, wakaendelea kuoa na kuolewa Mut'a bila kujali maneno yake. Katika waliompinga Umar ni:-

1. Imam Ali bin Talib A.S.

2. Abdullah bin Abbas A.S.

3. Imran bin Alhuswain Alkhuzai A.S.

4. Jaabir bin Abdullah Al'Ansar A.S.

5. Abdullahi bin Masuud. A.S.

6. Abu Said Alkhudry A.S.

7. Said bin Jubair A.S.

8. Abdallah bin Umar.

9. Rabia bin Ummi bin Kaab Al'Ansar.

10. Az'Zubeir bin Al'Awwam Al'qurash.

11. Salmata bin Umayya Al'jamhi.

12. Maabad bin Umayya Al'jamhi.

13. Muawia bin Abu Sufyan.

Haya utayapata katika vitabu hivi:-

1. Tafsirut Tabari J. 5 uk. 9

2. Bidayatul Mujtahid J. 2 uk. 63

3. Lisanul Arab J. 14 uk. 66

4. Taajul A'rus J. 10 uk. 200

5. Al'Faiq ya Az'Zamakhshary J. 1 uk. 331

6. Al'Muhalla J. 9 uk. 519

7. Sharhu Sahihi Muslim J.11 uk. 186

Kama ambavyo masunni wote wamempuuza Umar bunul Khattab, katika Tamattu'u ya Hija wanaendelea bila kujali kelele zake. Tazama vitabu vyao (Masunni) vya Fiq'h katika mlango:- AINA ZA KUHIRIMIA wamegawanya aina tatu:- QIRAN, TAMATU'U, (ambayo Umar bunul Khattab ameipiga marfuku) na IFRAD. Wanazuoni wote wa kisunni wamekubaliana waendelee nazo, licha ya kukataza Umar Tamattu'u ya Hija.

TAZAMA: Fiq'hus Sunna J.1 uk. 553

Na hata kama walinyamaza, ni aibu? Kwani hawakunyamaza?

Alipoonya kwamba Mtume hakufa? "Imesimuliwa na mwana Aisha kuwa:- Zilipotangazwa habari za kifo cha Mtume S.A.W. Umar bunul Khattab na Mughira bin Shuuba waliomba kuingia chumbani alikolazwa Mtume S.A.W. walipoingia, wakamfunua uso, Umar akasema: Oh msiba nizito! Kuondokewa Mtume S.A.W. kisha wa-katoka walipofika mlangoni, Mughira akasema: "Ewe Umar! Kwa kweli Mtume amekufa." Umar akajibu: "Wewe muongo, Mtume hajafa, isipokuwa wewe muongo, ni mtu unayesumbuliwa na fitina, mtume S.A.W. hatakufa mpaka wanafiki wamalizike wote."

TAZAMA: Albidayatu Wannihaya J.5 uk. 212 Umar akaanza kuonya kuwa:- Nitakae nisikia anasema Mtume amekufa nitakata kichwa chake, wako wanafiki wanadai kuwa Miume amekufa, na wala hakufa. Umar hakunyamaza mpaka alipomuona Abubakar kafika akakaa chini!!!

Alipofanya talaka tatu ni tatu? Imepokewa kwa Abdillahi bin Ali bin Assaib, kutoka kwa Nafii bin Ajiiz bin Abdi Yazid kwamba: "Rukana bin Abdi Yazid alimpa talaka tatu mkewe, Mtume akapewa habari hiyo, akaamuru mke arejeshwe kwa mumewe mara moja.

TAZAMA: Tafsirul Qurtubi J .3 uk. 131

Fiq'hus Sunna J. 2 uk. 231

Kwa hiyo katika zama za Mtume S.A.W. mtu akiacha talaka tatu mara moja huhesabiwa ni talaka moja tu, kwa mujibu wa hukumu ya Mtume S.A.W. Mwenyeezi Mngu anasema:- "Haiwi wa mwanamume aliyeamini wala mwanamke aliyeamini, Mwenyeezi Mngu na Mtume wake wanapokata shauri, wawe na hiari katika shauri lao." 33:36. Ulipofika utawala wa Umar bunul Khattab yeye akaamuru talaka tatu ni tatu kinyume na amri ya Mtume!!

Alipoleta jamaa ya taraweh?

Mtume hakuleta sala ya taraweh iia wala haikuwako katika zama za Abu Bakar. Katika sala za jamaa za sunna aIizofundisha Mtukufu Mtume S.A.W. taraweh haimo, bali huo ni uzushi wa Umar bunul Khattab.

TAZAMA: Al'Kamil fit Tarekh J. 3 uk. 31

At'Tabaqatul Kubra J. 3 uk. 281

AI'Milal Wannihal J. 1 uk. 78

Sheikh Muhammad Sharif anakataa kuwa Umar ndiye aliyekataza Mut'a yeye anasema:-

Ilivyo ni kwamba: Sayyidna Umar alipanda katika mimbari akasema:- "Kwa nini watu wanaowa hii Mut'a na hali Mtume amaeikataza; sikilizeni mimi sitaletewa yeyote aliyeowa ndoa hiyo isipokuwa nitampopoa mawe." Hivyo ndivyo anavyosema Sheikh Muhammad Sharif.

Jawabu:- Hilo halikubaliki, kwa sababu mategemeo ya hadithi hiyo ni mabovu kabisa.

TAZAMA: A'jarhu Wattaa'adil J. 4 uk. 171

Mizanul Itidali J. 4 uk. 184

Lisanul Mizani J. 6 uk. 95

Sasa, vipi utalinganisha hadithi hiyo na zile tulizokwisha zitaja?!!. Kwa hiyo riwaya hiyo haina mashiko tupa nje. Sasa, tuje kwa Ibnu Abbas:- Sheikh Muhammad amesema hivi:- Ibnu Abbas mwenyewe alipokwenda akaulizwa na masahaba kwamba: Ewe Ibnu Abbas Fat'wa yako imefika mbali, watu wametunga mashairi, akasema:- "LA ILAHA ILLALLAH, ASTAGH'FIRULLA INNAMA HIYA KAL'MAYTAT" Hivyo ndiyo alivyosema Sheikh Muhammad, na sisi tunamwambia kuwa maneno ya Ibnu Abbas yalikuwa hivi:- INNA LILLAHI WAINNA ILAYHI RAJIUN WALLAHI MA BIHADHA AFTAYTU WALA HADHA ARADTU WALA AH'LALTU MIN'HA ILLA MA AHALLALLAHU MINAL MAYTATI WADDAMI WALAHMIL KHINZIR".

Maana yake, "Sisi ni wa Mwenyeezi Mngu na sisi tutarejea kwake, Wallahi haya sikuyatolea fat'wa na wala sikuyataka. Na sikuihalalisha ila vile alivyohalalisha Mwenyeezi Mngu katika nyamafu na damu na nyama ya nguruwe."

TAZAMA: Majmauz' Zawaid J. 4 uk. 268.