read

Unayo Majibu Manne

Mifano aliyotoa haiwezi kukubalika katika mahakama yoyote adilifu. Mashahidi watatu wataje miaka mitatu tofauti ya kitendo kimoja?!

Ieleweke kuwa hapo inayohusika si miaka (wakati) peke yake, na mahala vilevile.

Tazama imetajwa, Khaybara na Makka Je! Mashahidi wako wakisema: Waliona ukimkopesha Mombasa shilingi elfu moja, wapili Dar es Salaam, watatu Kampala. Bado hapana Idhtirab??

Je ikiwa hiyo miaka mitatu yote ilitolewa na mtu moja, akasema: Aliona ukimkopesha mtu huyo mmoja mwaka 1981 Mombasa, mwaka 1982 Dar es Salaam, mwaka 1983 Kampala, bado haidhuru Idhtirab?/ Hivi ndivyo zilivyo hadithi nne zilizobaki, zote zimepokewa kwa mtu mmoja Ar'Rabii bin Sabura Al'Jahny.

Zaidi ya hvyo, mtu huyohuyo mmoja riwaya zake zina Idhtirab. Sheikh Muhammad Sharif anatuambia kuwa:- "Idhtirab hii ingekuwa mbaya, lau kama mtu angesema: Mtume S.A.W. ameharamisha Mut'a mwaka wa Khaybara, ikaja riwaya ya pili kasema: Mtume S.A.W. amehalalisha Mut'a mwaka ya Khaybara idhtirab ndiyo ingedhuru. Lakini hii haidhuru, hukumu ni ileile moja." Mwisho wa kunukuu.

Majibu Yetu

Anasema Ar'Rabii bin Sabura (kama ilivyo katika Sahihi Muslimu na Musnad Ahmad) ruhusa (ya Mut'a) ilikuwa baada ya siku kumi na tano kuingia Makka.

Anasema tena Ar'Rabii bin Sabura:- (kama ilivyo katika Sahihi Muslim na Musnad Ahmad) ruhusa (ya Mut'a) ilikuwa wakati wa kuingia Makka, (anasema) wakati tulipofika Makka, tukatufu, kisha tukaamrishwa kuowa Mut'a. Bila shaka Sheikh amefahamikiwa kuwa Idhtirab hii imedhuru.