read

Majadiliano Juu Ya Hadithi Ya Manzilat (Cheo)

Ma'mun: Ewe Is-haq, je, hadithi hii vile vile mnahadithia, kwamba Mtume (s.a.w.w) alisema, "Ya Ali Anta Minni Bimanzilati Haruuna Min Musa."
(Yaani, Ee, Ali wewe kwangu, una cheo na daraja kama alivyokuwa nayo Bw. Harun kwa H. Musa).

Allama: Bwana, mimi pia hadithi hiyo nimesikia, isitoshe haya nimewasikia wenye kuikubali na wenye kuipinga hiyo hadithi.

Ma'mun: Wewe, miongoni mwa hawa wanavyuoni kikundi kipi unakiamini na kukitegemea, katika wale wenye kuikubali hadithi hii au wale wenye kuipinga?

Allama: Nawasadiki na kuwaamini wale wanaoikubali hiyo.

Ma'mun: Inaaminika kwamba Mtume (s.a.w.w) amesema hadithi hiyo kwa mzaha na mchezo tu?

Allama: Ma'adhallah! Sivyo hivyo.

Ma'mun: Hujui kuwa Bwana Harun alikuwa ndugu halisi wa Mtume Musa?

Allama: Najua bila shaka.

Ma'mun: Je, hii sivyo kuwa Bwana Harun alikuwa Mtume na H. Ali hakuwa Mtume?

Allama: Hapana shaka ndivyo.

Ma'mun: Basi sasa, tumekwisha yakinisha kwamba H. Ali hakuwa ndugu halisi wa Mtume.

Allama: Hapana shaka ndivyo.

Ma'mun: Basi sasa, tumekwisha yakinisha kwamba H. Ali hakuwa ndugu halisi wa Mtume, wala hakuwa Mtume. Sifa zote hizo mbili hata moja hakuwa nayo. Sembuse Bwana Harun alikuwa nayo sifa zote mbili. (Yakini katika sifa hizi mbili H. Ali hakumshabih Bwana Harun kabisa). Kwa hivyo usemi wa Mtume, "Ya Ali, Anta Minni Bimanzilati Haruuna Min Musa," (Ee Ali wewe kwangu una daraja na cheo ambacho Bwana Harun alikuwa nacho kwa Mtume Musa), una maana gani? (Sasa H. Ali alikuwa na sifa na cheo kipi ambacho kamshabihi Bwana Harun hata Mtume akasema hadithi hiyo?).

Allama: Hadithi hiyo si kitu, kwa sababu Mtume kayasema maneno haya katika kumfurahisha H. Ali tu, hakuwa na shabaha zingine, na kwa sababu ya kufanya vile ni kuwa Wanafiki (Munafiqeen) walivumisha kwamba Mtume kwa vile moyoni alikwa hakuridhika naye ndipo akamwacha huko Madina.

Ma'mun: Kwa hivyo imethibiti kwamba Mtume juu ya jambo la upuuzi (uvumi) kataka kumfurahisha H. Ali tu.

Allama anasema "Kwa suala gumu hilo nikafadhaika na nikafikiri niseme nini? Lakini haikunijia akilini majibu yeyote, basi hapo Ma'mun akasema:

Ma'mun: Ewe Is-haq, kwa namna Mtume katika hadithi hiyo amemshabihisha H. Ali na H. Harun, namna hiyo hiyo maneno wazi wazi hapo katika Qur’ani.

Allama: (Kwa kuona ajabu sana) Bwana maneno gani?

Ma'mun: Kwa maneno ya Mtume Musa, Mwenyezi Mungu katika Qur’ani amesema, "Qala Musa li Akhi-hi Haruun ikhlufni fi Qawmi wa'aslih walaa tat-tabi Sabiylal ­muf-sideen." (Musa akamwambia ndugu yake, Harun: "Shika mahali pangu katika (kuwaendesha) watu wangu na usuluhishe wala usifuate njia ya Waharibifu." (7:142).

Allama: Bwana! haya vile vile angalia kuwa Mtume Musa alipokuwa anakwenda kuomba kwenye jabali ya Tuur ndipo akamfanya kiongozi nduguye H. Harun juu ya umma wake, na wakati ule H. Musa alikuwa hai, vile vile Mtume wetu akamfanya H. Ali kuwa kiongozi wa umma, wakati ule tu alipokuwa akienda kwenye vita vya Tabuuk, wakati wa uhai wake. (Vita vya Tabuuk vilikuwa katika mwaka wa tisa Hijria)

Ma'mun: Toba! Unasema nini? Sivyo hivyo kamwe, hebu sema wewe mwenyewe Mtume Musa alipomfanya H. Harun khalifa kushika mahala pake, alipokuwa akienda kwenye Tuur; je alimchukua mtu yeyote katika wafuasi wake kwenda naye huko?

Allama: Hakuna.

Ma'mun: Kwa hiyo, je, haioneshi; kwamba Mtume Musa kamfanya H. Harun kuwa ni Khalifa wa Umma wake wote?

Allama: Bila shaka, alikuwa khalifa juu ya umma wote.

Ma'mun: Lakini alipokwenda Mtume (s.a.w.w) kwenda kwenye vita vya Tabuuk; bila ya watoto, wanawake, na baadhi ya Waislamu dhaifu (wasio na afya) aliwawacha watu (wasio hao) wengine Madina? Basi vipi yaweza kusemekana kwamba tokeo hili ni kama la H. Musa? (Yaani ya Mtume Musa alikwenda kwenye jabali ya Tuur peke yake lakini Mtume wetu (s.a.w.w) alipokwenda Tabuuk, alikwenda na masahaba na wasaidizi wake; H. Musa kauacha Umma wote nyuma, lakini Mtume wetu isipokuwa Waislamu dhaifu, wanawake na watoto, waliobaki aliwachukuwa wote; kwa hivyo kuna faraka ya ardhi na mbingu, basi utalishabihisha vipi tukio la Mtume na H. Ali na tukio la nabii Musa na H. Harun?

Wazo moja linanijia akilini mwangu juu ya hadithi hii, na wazo hilo linatokana na Qur'ani, na ni uthibitisho wa nguvu juu ya jambo hili; nalo ni kuwa Mtume amemfanya H. Ali (Wakati wa uhai wake na baada ya kufa kwake) Khalifa halisi juu ya waislamu wote (yaani isiyo na kiasi wala mipaka). Mtu yeyote hawezi kuupinga uthibitisho huu wala kujibu dalili hii; wala hakuna mtu kabla ya mimi aliyeleta na kuonyesha dalili hiyo, bali na amini kwamba Mwenyezi Mungu kwa fadhili zake mahsusi juu yangu kaniwazisha uthibitisho huo.

Allama: Bwana, uthibitisho gani?

Ma'mun: Ni haya maneno ya nabi Musa ambaye Mwenyezi Mungu ameyataja katika Qur'ani hivi; "Waj-alliy Wazee-ran..." (mpaka mwisho wa aya; sura 20, Aya 29-35). "Na unijalie waziri (msaidizi) katika jamaa zangu, ndugu yangu Harun umfanye awe ndiye waziri kwangu) nitie nguvu kwa ndugu yangu huyu, na umshirikishe katika kazi (hii), ili tukutukuze sana na tukutaje kwa wingi. Hakika wewe unatuona." Vile vile Mtume wetu mtukufu (s.a.w.w) amesema kwamba, Ee, Ali wewe uko kwangu mwenye daraja na cheo kama alivyokuwa H. Harun kwa Mtume Musa, kuwa wewe ni Waziri wangu na vile vile ndugu yangu, ambao kwa wewe nimepata nguvu, na kukufanya kuwa mshiriki katika kazi zangu, ili tumtukuze sana, na tufanye atajwe sana kote. Je, sasa yuko mtu mwenye uwezo wa kueleza au kufasiri hadithi hii kwa vingine hata yasije maneno (hadithi) ya Mtume ya kubatilika au kuwa isiofaa ya upuuzi.

Allama anasema hivyo hivyo majadiliano ya nguvu kwa muda mkubwa yakaendelea kwa urefu hata ikafika alasiri, hapo Qadhi Qudhat (Qadhi mkuu) Yahya bin Aktham akasema:1

Qadhi Yahya bin Aktham: Bwana, hakika leo kwa wenye kutaka haki (ukweli) na kheri umewafungulia na kuthibitisha Siraatul Mustaqeem (Njia iliyonyooka ya kweli) na bila shaka umedhihirisha haki kwa dalili zenye nguvu hata hataweza mtu yeyote kuzijibu.

Allama Is-haq anasema, "Alipokwisha kuyasikia Ma'mun maneno ya Qadhi Yahya, basi akaelekea kwetu na akasema hivi: “Je, nyie mnasema nini? Sisi sote kwa pamoja tukasema, "Sisi vile vile tunawaafiki nyie bwana, na yote mliyoyasema ni ya haki na kweli."

Ma'mun: Naapa kwa jina la Mwenyezi Mungu isingekuwa Mtume (s.a.w.w) ametuamuru kukubali maneno ya watu na kuisadiki; basi kabisa kamwe nisingeyakubali maneno yenu haya (kwa sababu mpaka hivi sasa hamkubali moyoni kuwa H. Ali Khalifa (waziri) bila Fasli wa Mtume (bila kuwa kati mtu mwingine) kwani sasa mnafikiri mbele yangu tu).

Ee, Mola wangu mimi nimewanasihi na kufanya kutimiza wajibu wangu wa 'Amr Bil Maaruf’ kama inavyotakikana. Ewe Mola wangu, wajibu wa kudhihirisha na kufikisha haki na ukweli nimeshaufanya na mzigo huo nimeshautua, Ee Mola wangu, kwa ajili ya mapenzi ya H. Ali na ubashiri wake, unipe uwezo wa kukukaribia; na ninaifuata madhehebu hii.

 • 1. Ukitaka kujua zaidi vitazame vitabu vifuatavyo:
  Seeratun Nabi ya Ibn Hisham
  (b) Tabaqaat ibn Saad juzuu ya tatu, Uk 14
  Musnad ibn Hanbal, juzuu ya kwanza, Uk. 170 hadi 331, juzuu ya tatu, Uk. 32 na 338, juzuu ya sita, Uk. 369 na 438
  Saheeh Bukhari, Juzuu ya pili, Uk. 200 mlango wa sifi za Ali ibn Abi Talib
  Saheeh Muslim, juzuu ya saba, Uk. 120
  Sunan lbn Maajah, Juzuu ya kwanza Uk. 55
  Sunan Tirmidhi
  Khasis ya Ahmad bin Shueb nasai
  Tareekhul Umam ya Ibn Jareer Tabai, juzuu ya tatu Uk. 144
  Hakim katika Mustadrak, juzuu ya tatu, Uk. 109 na 133
  Ibn Abdul Bir katika Isteeb, juzuu ya pili, Uk. 473
  Ibnil Baghazili katika Kitabul Manaaquib
  Viko vitabu vingi vingine vya kuthibitisha hivyo lakini kwa muhtasari tumeandika hivyo tu