Makala hii ni mazungumzo na majadiliano kati ya mtawala (wa ukoo wa Abbassid) Ma'mun al-Rashid na wanachuoni mashuhuri katika zama hizo juu ya "ubora wa Seyyidna Ali bin Abi Talib (a.s) ikilinganishwa na Masahaba wengine wa Mtume Mtukufu (s.a.w.w)." Msomaji atanufaika sana na maelezo haya.

[Pia kuna neno la lugha ya Kiurdu lililo tumika katika makala hii; neno hilo ni 'Hazrat'; imetumika wakati wa kuwataja watu wenye hadhi yaani kwa mfano, badala ya kusema 'Seyyidina Ali' au 'Nabi Musa' sehemu nyingi wametajwa kama Hazrat Ali (H. Ali) na H. Musa; imeelezwa hayo ili msomaji asighafilike].