read

Neno La Mchapishaji

Kitabu kilichoko mikononi mwako, ni tarjuma ya kitabu cha Kiingereza, kwa jina la: "The role of Ahlul Bait (as) in Preserving the teaching of Islam" Tarjuma ya Mulla Asghaar M. M. Jaffer kutoka lugha ya Kiarabu. Sisi tumekiita: "Nafasi ya Ahlul Bayt katika kuhifadhi mafub- disho ya Kiislamu."

Mwandishi wa kitabu hiki amelishughulikia sana suala la ‘tawhid’. Suala hili limezua mjadala mkali sana miongoni mwa wanachuoni wa Kiislamu, wengine wakimhusisha Mwenyezi Mungu na viungo na makazi na wengine wakiwa wanaikataa dhana hiyo, kila upande ukitoa hoja na dalili zake. upande mmoja ni wa wanachuoni wa Madhehebu ya Sunni ambao wanaunga mkono dhana hii, na upande mwingine ni wa wanachuoni wa Kishia ambao wanapinga dhana hiyo.

Mwandishi wa kitabu hiki (Allamah Syed Murtadha Askari, mwanazuoni wa Kishia’h) amelishughulikia suala hili kwa kulinganisha hoja za pande zote mbili kwa kutumia vitabu vyao vya tawhid na vya hadith, na akahitimisha kwa kuonesha pasina shaka yoyote kwamba Mwenyezi Mungu yu mbali na hayo wanayo mhusisha nayo.

Sisi tunamuachia msomaji asome kwa makini na utulivu, na uwamuzi utakuwa ni wake; bali matumaini yetu ni kwamba ataelekea kule kwenye haki, bila ya kujali haki hiyo iko kwa nani.

Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote. Kutokana na ukweli huu, Taasisi yetu ya 'Al-Itrah Foundation' imeona ikitoe kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili, kwa madhumuni yake yale yale ya kuwahudumia

Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili.

Tunamshukuru ndugu yetu, Ramadhani Kanju Shemahimbo kwa kukubali jukumu hili la kukifanyia tarjuma kitabu hiki. Vilevile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwa kitabu hiki.

Mchapishaji:
Al-Itrah Foundation
S. L. P. 19071 Dar-es-Salaam.

Marhum Mulla Asghar ameacha alama isiyosahaulika katika Jumuiya nzima ya Shi’a katika zama hizi. Mtu mwenye kipaji cha ubora huu, na athari kama hii, anachipukia mara moja tu katika maisha. Kama mubaligh adhimu, aliwasilisha kwa ufasaha kabisa mafundisho ya Ahlul Bayt (a.s.) kwa watu kwa jumla.
Akithibitishwa na wanazuoni wa wakati wake, umaizi wake wa kina katika masuala ya Fiqh, theolojia, falsafa, teosofia (imani kwamba wanadamu wanaweza kumfahamu Mungu na kuwasiliana Naye kwa kutulia na elimu ya kina) na vile vile masuala ya nyakati hizi, yeye alikuwa maarufu. Kama muelimishaji kwa kiwango cha hali ya juu kabisa, uwezo wake wa kujulisha na kuelimisha wanafunzi wake juu ya fikra za Kiislamu kwa kweli ulikuwa unataalimisha sana. Kwa kupitia fikra zake, maandishi yenye kuchochea na hotuba zenye msukumo, vichwa au akili nyingi zimefanywa zianzishe tafakari, na maisha ya watu wengi yamebadilishwa. Athari zake juu ya jamii yetu ilikuwa kama ya ajabu sana na ambayo imekuwa ya kusaidia sana katika kubadilisha mifano (ya maisha).

Ninatumaini kwamba mfululiza huu wa vitabu wenye ukumbusho, vinavyozingatia maadhimisho ya miaka 25 ya Jumuiya yetu ya Kimataifa - World Federation – utaendelea kunururisha mafundisho ya Ahlul-Bayt (A.S.) kwa ulimwengu kwa jumla kupitia maneno ya mwanazuoni huyu mashuhuri. Kwa kuunga mkono Mfuko wa Kumbukumbu wa Mulla Asghar (Mulla Asghar Memorial Fund), ambao, miongoni mwa miradi ya kielimu, umefanya mfululizo huu wa machapisho kuwezekana, utasaidia kuhakikisha kwamba mapenzi yake juu ya kueneza mafundisho ya Ahlul- Bayt (A.S.) yanaendelea baada yake. Kwa pamoja, tunaweza kuleta ukweli kwenye zile ndoto nyingi alizokuwa nazo na kusaidia World Federation kuendelea katika njia ya huduma ambayo aliieneza chini ya uongozi wake wenye haiba kubwa. Ninawaombeni kumkumbuka Mulla Saheb kwa kumsomea Suratul-Fatihah

Hasnain Walji
Raisi, World Federation, KSI Muslim Communities.