read

Orodha Ya Vitabu Vilivyo Chapishwa Na Al-Itrah Foundation:

1. Qur'an Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanza mpaka kumi na tatu
2. Uharamisho wa Riba
3. Uharamisho wa uwongo Juzuu ya kwanza
4. Uharamisho wa uwongo Juzuu ya pili
5. Hekaya za Bahlul
6. Muhanga wa Imamu Husein (A.S.)
7. Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (A.S.)
8. Hijab vazi Bora
9. Ukweli wa Shia Ithnaashari
10. Madhambi Makuu
11. Mbingu imenikirimu
12. Abdallah Ibn Saba
13. Khadijatul Kubra
14. Utumwa
15. Umakini katika Swala
16. Misingi ya Maarifa
17. Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia
18. Bilal wa Afrika
19. Abudharr
20. Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu
21. Salman Farsi
22. Ammar Yasir
23. Qur'an na Hadithi
24. Elimu ya Nafsi
25. Yajue Madhehebu ya Shia
26. Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur'an Tukufu
27. Al-Wahda
28. Ponyo kutoka katika Qur'an.

Back Cover

Nafasi Ya Ahlul Bayt Katika Kuhifadhi Mafundisho Ya Uslamu

Madhehebu ya Ahlul-Bayt (a.s.) imetufundisha sisi kwamba Mwenyezi Mungu hana anachofanana nacho. Wake Yeye ni Upweke Kamili, na hakuna viungo au sehemu, hakuna nafasi au mipaka inayoweza kuhusishwa Kwake.
Kwa kufanya hivyo, Ahlul-Bayt (a.s.) wametupa sisi maana halisi ya Qur'ani Tukufu na hadithi za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na kuzing'oa zile fikra zote zisizo sahihi ambazo zilipata kupenyezwa kutoka kwenye kambi za Kiyahudi na Kikristo.

kinyume na Ahlul Bayt (A.S.), hata hivyo, kuna fikra zilizopo za kusiki- tisha za kikundi cha wanachuoni wa Kiislamu ambao wamekuwa mawindo ya dhana ya Tawhid isiyo ya Kiislamu. katika kitabu hiki kuna sura mbili zinazo husu Tawhid, kutokana na kazi kubwa iliyofanywa na Allamah Askari juu ya somo hili, dhana zote zile zenye kumfananisha Mwenyezi Mungu na mwanadamu kwa uzuri kabisa zimekanushwa.

Wanazuoni wa Madhehebu hii wamesimulia kutoka kwa Ahlul-Bayt (a.s.), katika vitabu vyao muhimu kama Tafsiir na Hadithi. Matokeo yake, ule muundo asili wa itikadi ya ya Kiislamu umebakia bila kuchafuliwa.

Sasa ni wazi kabisa kwamba, kama isingekuwa kwa juhudi kubwa na bila kuchoka za Maimamu wa Ahlul-Bayt (a.s.) na wafuasi wao, ile imani kuu ya Tawhid ndani ya Uislamu ingeweza kupotea kabisa moja kwa moja.

Kimetolewa na kuchapishwa na:
Alitrah Foundation
S.L.P. 19701 Dar es Salaam, Tanzania
Simu: +255 22 2110640 / 2127555
Barua Pepe: alitrah@raha.com
Tovuti: www.ibn-tv.com