read

Sehemu Ya Tatu: Macho Ya Mwenyezi Mungu

1. “Macho” Ya Mwenyezi Mungu Kama Yanavyoeleweka Kwa Madhehebu Ya Makhalifa

Katika vitabu vya Tafsir na hadith, wanazuoni wa madhehebu hiyo hapo juu wamesimulia kutoka kwa Abu Huraira ambaye amesema, wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipozisoma Ayah zifuatazo:

إِنَّ اللَّهَ يَأْمُرُكُمْ أَنْ تُؤَدُّوا الْأَمَانَاتِ إِلَىٰ أَهْلِهَا وَإِذَا حَكَمْتُمْ بَيْنَ النَّاسِ أَنْ تَحْكُمُوا بِالْعَدْلِ ۚ إِنَّ اللَّهَ نِعِمَّا يَعِظُكُمْ بِهِ ۗ إِنَّ اللَّهَ كَانَ سَمِيعًا بَصِيرًا {58}

“Hakika Mwenyezi Mungu anawaamuruni kurejesha amana kwa wenyewe, na mtakapohukumu baina ya watu mhukumu kwa uadilifu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kuona.” (An- Nisaa; 4: 58)

“Niliona kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akionyesha wazi kusikia na kuona kwa Mwenyezi Mungu kwa kuweka dole gumba lake juu ya masikio yake na kidole chake cha shahada juu ya jicho lake.”

Wakati Abu Huraira aliposimulia hadithi hiyo hapo juu, aliurudia ule udhihirishaji kwa kuweka vidole vyake mwenyewe juu ya sikio na jicho lake. Alifanya hivyo kusisitiza kwamba Mwenyezi Mungu anasikia kwa msaa- da wa masikio na anaona kwa kusaidiwa na macho yake.

Jahmiyyah ilikuwa ni madhehebu, ambayo ilizishutumu na kuzikataa dhana kama hizi. Katika ukanushaji kwa madhehebu ya Jahmiyyah, Abu Dawuud anaandika katika Sunan yake maarufu kama ifuatavyo:

“Hadithi hii ya Abu Huraira inazikanusha imani za Jahmiyyah (ambao wanaamini kwamba Mwenyezi Mungu hana viungo, wala hana mwili)”
Ubunifu wa maneno ya uwongo wa Abu Huraira umeipelekea madhehebu ya Makhalifa katika kuamini kwamba popote pale hili neno Ayn linapotokeza kwenye Qur’ani Tukufu kuhusiana na Mwenyezi Mungu, ni lazima lieleweke kama jicho lenyewe hasa – sehemu ya mwili ambayo hutazama na kuona. Kwa hiyo tunakuta Ibn Khuzaimah, Imam wa Maimamu kama anavyotukuzwa na madhehebu yao, akisimamisha mlango wa pekee katika kitabu chake cha Tawhiid, kuthibitisha kwamba Mwenyezi Mungu, Aliye juu kabisa, anayo macho. Yeye anaandika hivi:

“Tunarudia kusema kile Mwenyezi Mungu Mwenyewe alichokisema kwenye Kitabu Chake na kile Mtume Wake (s.a.w.w.) wa kuheshimika alichokithibitisha juu ya Mwenyezi Mungu kuwa na macho.”

Baada ya hapo, anaendelea kunukuu Ayah zifuatazo:

i) Mwenyezi Mungu alimwambia Nabii Nuh (a.s.):

وَاصْنَعِ الْفُلْكَ بِأَعْيُنِنَا {37}

“Na tengeneza jahazi mbele ya macho Yetu (Huud; 11:37)

ii) Akizungumzia Jahazi la Nabii Nuh:

تَجْرِي بِأَعْيُنِنَا {14}

“Ikaenda mbele ya macho Yetu (Al-Qamar; 54: 14)

iii) Aliyoyazungumza kwa Nabii Musa (a.s.):

ۚ وَأَلْقَيْتُ عَلَيْكَ مَحَبَّةً مِنِّي وَلِتُصْنَعَ عَلَىٰ عَيْنِي {39}

“Na nimekirimu mapenzi yangu juu yako ili upate kulelewa machoni Mwangu.”
(At-Twaha; 20: 39)

iv) Aliyoyazungumza na Mtume wetu (s.a.w.w.)

وَاصْبِرْ لِحُكْمِ رَبِّكَ فَإِنَّكَ بِأَعْيُنِنَا ۖ {48}

“Na ingoje hukumu ya Mola Wako, hakika wewe uko mbele ya macho yetu …” (At-Tuur; 52: 48)

Ibn Khuzaimah anasema:

“Kwa kuzingatia Ayah hizi kutoka ndani ya Qur’ani Tukufu, ni wajibu juu ya kila Mu’min kuthibitisha imani ya kwamba Mwenyezi Mungu anayo macho, na hayo ameyathibitisha Yeye Mwenyewe. Na yoyote yule ambaye haamini yale Mwenyezi Mungu aliyoyadhihirisha ndani ya Kitabu Chake, na kile alichojihusisha Kwake Mwenyewe, kwa kweli huyo sio Mwislamu. Maana Qur’ani imedhihirishwa vya kutosha na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mwenyewe, kwani Mwenyezi Mungu amemuamrisha yeye ndani ya Qur’ani Tukufu hivi:

وَأَنْزَلْنَا إِلَيْكَ الذِّكْرَ لِتُبَيِّنَ لِلنَّاسِ مَا نُزِّلَ إِلَيْهِمْ {44}

“…Tumekuteremshia Qur’ani ili uwabainishie watu yaliyoteremshwa kwa ajili yao …”
(An-Nahl; 16: 44)

“Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) katika tafsiri yake ameeleza wazi wazi kwamba Mwenyezi Mungu anayo macho maw- ili! Tafsiri yake inakubaliana na maneno ya Qur’ani Tukufu,

Qur’ani hii hii ambayo iko katika muundo wa kitabu baina ya majalada mawili, na inasomwa ndani ya Misikiti na vyuo.”

Akiwa hakutosheka na hoja hiyo, anakimbilia kwenye hadithi, miongoni mwazo ni ile moja kutoka kwa Abu Huraira. Mwishowe, anatoa simulizi ifuatayo kutoka kwa Abdullah ibn Umar:

“Mtume (s.a.w.w.) amesema: Mwenyezi Mungu sio kipofu katika jicho moja, kama Dajjal ambaye jicho lake la kulia halioni. Linaning’inia kama mbegu ya zabibu.”

2. Hilo “Jicho” Kama Lilivyoelezwa Na Ahlul-Bayt (A.S.)

Maimamu wa Ahlul-Bayt (a.s.) wametoa maana halisi ya Ayah hizi. Hata hivyo, ni lazima tushughulike na somo hili kwa maelezo kiasi juu ya mistari ile.

Ibn Khuzaimah amelichukulia neno Ayn au A’yunina kwa maana halisi, kuthibitisha madai yake kwamba yanaashiria macho ya Mwenyezi Mungu. Ukweli ni kwamba neno Ayn na yatokanayo nalo yana maana kadhaa katika lugha ya Kiarabu. Kwa maelezo zaidi mtu anaweza kurejea kwenye kamusi maarufu, Lisanul Arab. Katika Mu’jamul Udaba Juz. 2, uk. 11, tunakuta taabini (maneno ya kusifu) ya Ibn Faris Ahmad bin Zakariyya (aliyefariki mwaka wa 369 Hijiria) ambamo ndani yake kila ubeti unaishia na neno Ayn, kila moja likiwa na maana tofauti. Syed Muhsin al-Amiin anayo taabini kama hiyo yenye beti sitini.

Qur’ani Tukufu imelitumia neno hilo katika maana zote mbili, maana halisi na ile ya kiistiari vile vile. Katika sehemu ishirini na moja, Qur’ani Tukufu inalitumia neno Ayn kumaanisha kijito cha maji au mto.

Lakini jambo la muhimu ni kwamba zile Ayah zilizonukuliwa na Ibn Khuzaimah kuhakikisha imani yake zote zina maneno hayo yakitumika katika maana ya kitamathali.

Kwa Kiingereza tunasema: To keep an eye on (angalia kwa makini), ikiwa na maana ya kufanya uangalizi kwa makini; in the eyes of the law, (kufuatana na sheria), ikiwa na maana kwa maoni au uamuzi wa kisheria; the eye of the dome (kwa jicho la kuba), ikimaanisha katika sehemu yake kuu – na kadhalika. Ni dhahiri, matumizi kama haya sio ya maana halisi. Vivyo hivyo, maneno haya yametumika kuashiria maana zao za kiistiari.

Katika kitabu maarufu, Majma al-Lughat al-Arabiyyah kilichochapishwa Misri, tunakuta haya:

“Ndani ya Qur’ani Tukufu, neno Ayn limetumika katika maana halisi na ile ya kiistiari vile vile. Kwa mfano, katika Ayah:

وَقَالَتِ امْرَأَتُ فِرْعَوْنَ قُرَّتُ عَيْنٍ لِي وَلَكَ ۖ {9}

i) “Na mkewe Firaun akasema: Ni kiburudisho cha macho kwangu na kwako (Al-Qasas; 28: 9)

فَكُلِي وَاشْرَبِي وَقَرِّي عَيْنًا ۖ {26}

ii) “(Kwa Maryam) Basi ule na unywe na uburudishe macho yako…(Maryam; 19: 26)

Ni dhahiri kwamba hapa vifungu vya maneno vilivyotumika na Aynan na Aynin vyote vinawakilisha furaha na kuridhika.

Historia inatuambia kwamba Mwenyezi Mungu alimuamuru mama yake Nabii Musa (a.s.) kumtupa ndani ya mto. Musa (a.s.) kama mtoto mchanga alilifikia kasiri la Firaun juu ya mawimbi ya mto huo, ili kulelewa naye kama mwana. Maelezo kamili ya Ayah hiyo ni:

وَقَالَتِ امْرَأَتُ فِرْعَوْنَ قُرَّتُ عَيْنٍ لِي وَلَكَ ۖ لَا تَقْتُلُوهُ عَسَىٰ أَنْ يَنْفَعَنَا أَوْ نَتَّخِذَهُ وَلَدًا وَهُمْ لَا يَشْعُرُونَ {9}

“Na mkewe Firaun akasema: Ni kiburudisho cha macho kwangu na kwako, msimuue, huenda atatunufaisha, au tumpange kuwa mtoto hali hawatambui.” (Al-Qasas; 28: 9)

Katika mfano wa pili, Ayah inazungumza na Maryam, mama yake Nabii Isa (a.s.). pale alipomzaa Isa (a.s.) alihuzunika kwa sababu alijua kwamba watu hawatamuamini kwamba alikuwa bikira, na kwamba Isa (a.s.) alizaliwa bila baba, kwa amri tukufu ya Mungu. Hivyo Mwenyezi Mungu anasema:

“Usihuzunike! Kwani Mola wako amekupatia kijito cha maji chini yako na litikise shina la mtende, litakushushia tende zilizoiva. Basi ule na unywe na uburudishe macho yako.”

Sasa zile Ayah zilizonukuliwa na Ibn Khuzaimah nazo zinahitaji uchambuzi kidogo vile vile. Ayah ya kwanza, ilizungumzwa kwa Nabii Nuh (a.s.). Maana yake sahihi ni:

Tengeneza Jahazi chini ya uangalizi na ulinzi wetu.”

Ayah ya pili vile vile ina maana kwamba Jahazi la Nuh linaelea chini ya uangalizi na ulinzi wa Mwenyezi Mungu. Na katika Ayah ya tatu, Mwenyezi Mungu anadhihirisha kwa Musa (a.s.), maana sahihi ya Ayah ni:

“Na niliyakirimu mapenzi yanggu juu yako ili kwamba uwe unalelewa chini ya ulinzi na uangalizi Wangu……”

Hatimae, ile Ayah ya nne iliyozungumziwa kwa Mtukufu Mtume wetu (s.a.w.w.) ina maana kwamba:

“(Ewe Mtume!) – Na ingoje hukumu ya Mola Wako kwa subira, kwani wewe ni kipenzi Chetu na hivyo umelindwa.”

Mwisho kabisa ile hoja kwamba Mwenyezi Mungu sio kipofu kama Dajjal (mpinga Kristo). Vema, hii inatudokezea sisi kwamba yeye anatutaka sisi tuamini kwamba Mwenyezi Mungu anayo macho Yake, mwenye afya na asiyedhurika! Kwa kuzingatia mazungumzo yetu ya hapo juu, tunaweza kudhania ni jinsi gani hadithi hii ingeweza kusadikika! Tumekwisha kuonyesha tayari ni jinsi gani Abu Huraira asivyoaminika na jinsi askari wake walivyokuwa, na walivyokuwa chini ya athari za uenezaji wa Kiyahudi na Kikristo.

Ile itikadi halisi ya Kiislamu kwa hiyo ilivurugwa na hadithi potofu zilizokuwa na msingi juu ya Taurati iliyotomwa maneno yasiyokuwemo na maandishi mengine yasiyokuwa ya Kiislamu