read

103 - Miongoni Mwa Khutba Zake (A. S)

Kuhusu Kujiepusha Na Tamaa Za Dunia

“Enyi watu! Itazameni dunia mtizamo wa watawa wanaojiepusha nayo, wenye kuigeuzia uso, kwa kweli Wallahi ni punde tu itawaondoa wakazi walioifanya maskani, na kumfadhaisha anayeishi kwa anasa na mwenye kujiamini, kilichogeuka na kiendacho kuzimu hakitorudi, na ambacho kinatarajiwa kuja hakina uhakika, furaha yake ni mchanganyiko na huzuni, na watu imara wenye nguvu wanaelekea kwenye ulegevu na udhoofu. Hivyo basi msighurike na mengi yanayokufurahisheni humo kwa sababu ya uchache wa yatakayofuatana na nyinyi kutokana nayo.

“Mungu amrehemu mtu ambaye ametafakari na kujifunza humo, amejinfunza na kufanikiwa mwangaza. Kana kwamba ambacho kipo katika dunia hii kwa muda mfupi kitakuwa kama hakijakuwa. Kama kwamba ambacho kipo katika akhera baada ya muda mfupi kitaonekana kama kwamba hakijakosa kuwa. Kila kihesabiwacho kitatoweka, na kila kitazamiwacho kinakuja. Na kila kinachokuja kimekurubia.”

Sehemu Ya Khutba Hii Hii Kuhusu Sifa Za Mwanachuoni

“Mwanachuoni hasa ni yule mwenye kuitambua thamani yake, yatosha kwa mtu kuwa yu-mjinga kwa kutoijua thamani yake. Kwa hakika miongoni mwa watu awachukiao mno Mwenyeezi Mungu ni yule mja aliyemuachia mambo yake yeye mwenyewe. Anakwenda kombo mbali na njia iliyo sawa, anakwenda bila ya dalili, aitwapo kwenye shamba la dunia atafanya, na aitwapo kwenye shamba la akhera atakuwa mvivu, kana kwamba alilofanya ni wajibu juu yake, na kana kwamba alilolifanyia uvivu si wajibu juu yake.”

Sehemu Ya Khutba Hii Hii Kuhusu Wakati Wa Baadaye

Huo ni wakati ambao hatookoka kutoka humo isipokuwa aliye na usingizi sana,1 akiwa yupo hatambuliki, na akighibu, hakosekani, hao ndio taa za mwongozo na alama za misafara ya usiku, si wasambazaji wa masingizio wala si watoboa siri.

Hao Mungu atawafungulia milango ya rehema Zake, na atawaondolea madhara ya adhabu Zake.2 “Enyi watu! Zitakujieni zama uislamu utapinduliwa juu chini kama ambavyo chombo kifunikwavyo pamwe na kilicho ndani yake.

Enyi watu! Kwa hakika Mungu amekulindeni kwa maana ya kuwa hatowadhulumu, wala hakuwalindeni kwamba hatowafanyieni mtihani,3 na amesema Mtukufu katika wasemaji:4 Hakika katika hayo yapo mazingatio. Na kwa yakini. Sisi ni wenye kuwafanyia mitihani.” (23:30).”

Ar–Radhiy (r.a) amesema: Ama kuhusu kauli yake (a.s): “Kullu mu’minin nuwamatin” Kila muumini mwenye kulala sana, amekusudia kwa hilo: yaani yule muumini asiye kumbukwa au asiyetajika, na si mtu wa shari.

Na al-Masayiihu: Ni wingi wa neno misyahun, naye ni chakubimbi aendaye kwa huyu na kwa huyu ili kufanya ufisadi (umbea). Al-Madhayyiiu: Ni wingi wa midh’yaun, naye ni ambaye asikiapo baya la mwenzake analitangaza na kulieneza.

Ufafanuzi

Usemi wake (a.s): “Mwanachuoni ni yule ambaye ameijua Qadiri yake,” ni miongoni mwa mithali mashuhuri kutokana naye (a.s.) na wamesema watu baada yake na wamekithirisha, mfano wa kauli yao: ‘Ikiwa hutoijua Qadiri ya nafsi yako, kwa hiyo Qadiri ya mwingine hautoijua kabisa.’

Na mfano wa kauli yao: ‘Ambaye hajui Qadiri ya nafsi yake, watu watakuwa hawana kosa endapo watakuwa hawamjui.’

Na miongoni mwa maneno yaliyoelezwa kutoka kwa Abi Abdillah as-Sadiq (a.s.) katika riwaya marfu’u: Ma halakamru’u arifa Qadrahu” yaani hatohiliki mtu aliyeijua Qadiri yake - riwaya hii ni ya Abul’Abbas kutoka kwake katika Al’Kaamil. Na katika Hadithil-Marfu’u:

  • 1. Mwenye usingizi mwingi anamkusudia aliyembali na kujishirikisha na watu wa shari katika shari zao, wamuonapo hawamjui kuwa ni katika wao, na anapoghibu hawamkosi.
  • 2. Na imeelezwa hivi: Kupitia wao Mungu atafungua milango ya rehema yake, na kupi- tia wao ataondoa madhara ya adhabu yake, (yaani kwa baraka zao kheri itakuwapo na shari itatoweka).
  • 3. Ili abainike mkweli mbali na muongo, na mukh’liswi na mwenye shaka, kwa hivyo Mungu atakuwa na hoja dhidi ya viumbe Wake.
  • 4. Yaani kwa kuwa Yeye (swt) watu wanapoharibika hawalazimishi wawe wema, bali huwaacha kama walivyochagua ikiwa mtihani kwao.