read

106 - Na Miongoni Mwa Khutba Zake (A.S)

Humo Anabainisha Ubora Wa Uislamu, Na Amtaja Mtukufu Mtume (S.A.W.W.) Kisha Anawalaumu Sahaba Zake:

“Shukrani zote anastahiki Allah (swt), ambaye ameifanya sharia ya kiisla- mu na kuifanya nyepesi kwa mwenye kuiendea, na ameziimarisha nguzo zake dhidi ya mwenye kutaka kuushinda, na akaufanya kuwa ni amani kwa wenye kujiambatanisha nao, na salama kwa mwenye kuingia – (yaani hapigwi vita akishaingia uislamu), na hoja kwa mwenye kuueleza, na ni shahidi kwa mwenye kugombana kwa ajili yake, na ni nuru kwa mwenye kujiangaza nao, na ni fahamu kwa mwenye kutumia akili, na ni busara kwa mwenye kuzingatia, na ni alama kwa mwenye kuchunguza, na ni uelewa kwa mwenye kuazimia, na ni funzo kwa mwenye kuwaidhika, na ni uokovu kwa mwenye kusadiki, na ni ithibati kwa mwenye kutegemea, na ni raha kwa mwenye kuitumainia, na ni kinga kwa mwenye kusubiri.

Ni njia maarufu iliyo wazi mno na maingilio yaliyo wazi na ni mnara wa juu, na ni njia iliyo dhahiri, ni taa ziwakazo, ni mahali pa kujivunia, bendera iliyoinuka, yenye kukusanya farasi, ni pa kushindania washindani, mtukufu wa washindi wa farasi.
Wapandaji wake ni wenye kuheshimiwa, kusadiki (Mungu, Mtume…) ndio njia yake, vitendo vyema ndio minara yake, umauti ndio lengo lake,1 na dunia ni kiwanja chake cha mafunzo, na kiyama ni farasi wake, na pepo ni malipo yake ya mashindano.

Na Sehemu Ya Khutba Ni Kumueleza Nabii (S.A.W.W.):

“Mpaka aliwasha mwenge kwa autakaye,2 na aliangaza mwanga kwa mahabusi,3 hivyo basi yeye ni muaminifu wako wa kuaminika, na shahidi wako siku ya malipo, na ni muwakilishi wako akiwa neema, na ni Mtume wako wa kweli akiwa ni rehema.

“Oh Allah! Umgawiye fungu katika uadilifu Wako, na umpe jazaa ya kheri nyingi katika fadhila Zako. Oh Allah! Lirefushe jengo lake zaidi kuliko majengo ya wajengao, na umkirimu mafikio yake Kwako.

Itukuze kwako daraja yake, mtunukie wasila na heshima maalumu na ubora, na tukusanye sisi katika kundi lake, bila ya fedheha wala wenye kujuta, wala wenye kupetuka njia, wala wenye kutengua ahadi, wala wenye kupotea wala wenye kupoteza, wala walioshawishika kwa maovu!”

Ar-Radhiy (R.A) Amesema

Maneno haya yamepita katika habari zilizotangulia, isipokuwa sisi tumeyakariri hapa kwa sababu ya tofauti iliyopo kati ya riwaya hizi mbili.

Miongoni Mwayo Akiwahutubia Sahiba Zake

“Kwa ukarimu Wake Mungu (swt) mmefikia daraja ambayo wanahishimiwa hata vijakazi wenu, na majirani zenu wanatendewa vyema, na anakuheshimuni ambaye hamna fadhila yeyote juu yake, wala hamna hisani juu yake. Na anawahofuni asiyekuwa na maalumati ya kuwa mmepata kumshambulia, wala kuwa na mamlaka juu yake.

Mnaziona ahadi za Mungu zinatenguliwa wala hamkasiriki, hali ninyi mwasumbuka kwa kutanguliwa mila za babu zenu. Na mambo ya Mungu yalikuwa yanakuja kwenu, na yanatokea kwenu, na kwenu yanarejea.4

Mmewawezesha madhalimu sehemu zenu, na kuwaachia majukumu yenu, na mmeweka mambo ya Mungu mikononi mwao. Wanatenda kwa shaka, na wanakwenda katika utashi mbaya wa nafsi. Naapa Mungu hata wangekutawanyeni chini ya kila nyota, Mungu angewakusanyeni katika siku mbaya mno kwao!”

  • 1. Anakusudia umauti ni umauti wa kuwa mbali na matamanio ya kinyama, na maisha ya furaha ya daima kama ijulikanavyo kutoka na kauli yake (Rafi’ul-Ghaayati) vinginevyo, umauti ulio maarufu ni lengo la kila kilicho hai, au linakuwa maana (wal-mautu ghaay- atuhu): Yaani dunia ni jela ya mu’mini, na umauti unamtoa kutoka kwenye jela hiyo, na anapata hadhi ya furaha ya kudumu.
  • 2. Autakaye: yaani atakaye kupata mwanga wa taa, mwenye kuchukua moto kutoka moto mwingi, na mradi wake ni mwongozo katika dini, na ya kuwa Nabii aliwafaidisha watafu- tao haki ambayo kwa ajili yake watapata mwanga ili wafichue.
  • 3. Yaani Mtume (s.a.w.w.) aliipa mwanga alama kwa ajili ya aliyemfunga, yaani alisimamisha kwa ajili ya aliyemfunga ngamia wake kwa sababu ya kupotea - alama ili aongoke kwayo, yaani aliweka moto juu ya kilele cha mlima ili amuokoe kutoka kwenye kuchanganyikiwa kwake.
  • 4. Yaani hukumu za kisharia zinawajieni kutoka kwangu na miongoni mwa mafunzo yangu kwenu, kisha yanatoka kwenu na kuwaendea mnaowaelimisha nayo, kisha yarejea kwenu ili wajifundishe watoto wenu na ndugu zenu kutoka kwa hao wanachuoni.