read

108 - Na Miongoni Mwa Khutba Zake (A .S)

Na Miongoni Mwa Khutba Zake (a .s) - Zamakhshari ameieleza katika Rabi’ul-Abrar, Jz. 1, mlango wa ‘kubadilika kwa hali’.

Nayo Ni Khutba Ya Hali Ya Mabadiliko, Yaani Matukio Makubwa Vitani

“Mstahiki wa sifa njema ni Mungu Aliye dhahiri kwa viumbe Wake kupitia viumbe wake,1 na mwenye kudhihiri nyoyoni mwao kwa hoja Zake,2 ameumba viumbe bila ya kufikiri, kwa kuwa kufikiri hakumfalii isipokuwa wenye kuwa na dhamiri,3 naye si mwenye dhamiri,4 elimu yake imepenya mpaka ndani ya siri zisizojulikana, na kuzingira itikadi za ndani za siri.”

Na Sehemu Ya Khutba Hii Ni Maelezo Kuhusu Nabii (S.A.W.W.)

“Mungu (swt) amemchagua kutoka mti wa nasaba ya manabii,5 na kutoka mwale wa mwanga, na ni miongoni mwa nywele za utukufu wa kipaji cha uso, kutoka sehemu bora mno katikati ya bonde la Bat’ha’a,6 na taa za kuangazia gizani, na chemchemi za siri za hekima.”

Miongoni mwayo: “Yeye - yaani Nabii (s.a.w.w.) alikuwa mfano wa tabibu anayezunguka na tiba yake, aliyeimarisha marhamu yake, azungukaye na aliye tayari na dawa zake, na amekwisha koleza mawasimu zake.7 Anazitumia – mahali ambapo ipo haja, ili kuziponya nyoyo za vipofu, na masikio ya viziwi na ndimi za mabubu, kwa dawa zake hufu- atilia mahali ulipotawala mghafala na mahali penye mashaka na matata.

Hawakufaidika na mwanga wa hekima zake, na wala hawakuwasha moto kutoka jiwe la elimu litoalo cheche; Hivyo basi wao katika hilo ni kama wanyama watafunao nyasi, na mawe magumu. Siri zimefichuka kwa wenye kufahamu8 njia ya kweli imekuwa wazi kwa wale wasiokuwa na mwongozo na saa ikurubiayo imeondoa kifuniko usoni pake, na alama zimeonekana kwa wanaoangalia kwa makini.
Nimekuwaje mimi! Nawaoneni (mko) miili isiyokuwa na roho, na roho bila ya miili,9 wafanya ibada bila wema,10 na wafanyibiashara bila ya faida,11 wako macho hali wamelala,12wanatazama hali ni vipofu, wanasikia hali ni viziwi na wanaongea hali ni mabubu!

Miongoni Mwayo

“(Nimegundua kuwa) Kuna bendera ya upotovu imejiimarisha katikati, na imetawanyika na watu wa kabila lake, inakupimieni kwa kilo yake,13 na kuwachanganyeni na uzito wake.

Kiongozi wake yuko nje ya mila (ya kiislaamu) yupo katika upotovu, siku hiyo hatobaki miongoni mwenu ila ni kama mabaki ya chungu14 au vumbi kama vumbi lililokung’utwa kutoka kwenye kipeto.15 Hivyo basi itakusugueni kama isuguliwavyo ngozi, na itakukanyageni mkanyago wa mazao yaliyovunwa, na itamdonoa muumini kati yenu kama anavyodonoa ndege punje nene kati ya punje nyembamba.

Madhehebu yanawapelekeni wapi, na giza linawafanya mtangetangie wapi! Na mnapelekwa wapi na matarajio! Kutoka wapi mwaletwa, na mwadanganyiwa wapi? Kila muda una maelezo ya maandishi, na kila aliyetoweka ni lazima arudi, hivyo basi wasikilizeni viongozi wenu wa kiungu, na zihudhurisheni nyoyo zenu, na amkeni atakapowapigieni kelele. Mtangulizi inambidi aongee la ukweli kwa watu wake.

Yampasa azikusanye azma zake na fikra zake ili aangalie, fahamu zake aziweke hadhiri, suala ameliatua uatuaji wa tundu la kizuizi cha vazi, na ameliparua uparuaji wa ulimbo16 (kutoka kwenye kijiti cha mti na kuondolewa). Wakati huo batili itachukuwa nafasi yake, na ujahili utapanda kipando chake, utovu wa nidhamu utakuwa mkubwa, na wito utakuwa mdogo, na wakati utavamia uvamiaji wa mnyama mkali, na dume la ngamia litakoroma baada ya ukimya, na watu watakuwa ndugu katika maovu, watahamana kwa dini.17 Watapendana katika uwongo, na watachukiana kwa sababu ya ukweli.

Hali ikiwa ni hivyo mtoto atakuwa chukizo18 - (yaani atakuwa sababu ya kuchukiza badala ya kuwa kitulizo cha jicho kwa wazazi wake) na mvua - (sababu ya joto), uovu utajaa mno, na maadili mema yatatoweka, na watu wa zama hizo watakuwa mbwa mwitu, na masultani wao ni kama wanyama wavamizi, na watu wao wa hali ya kati watakuwa walafi, na mafakiri wao ni maiti, ukweli umedidimia, na uwongo umefurika, na upendo utakuwa wa maneno, hali watu wakiwa wanagombana kimoyo, na uzinzi ni nasaba, na usafi wa kutozini ni ajabu,19 na uislamu utavaliwa kama ngozi juu chini.”20

 • 1. Maadamu dalili za kuthibitisha kuwepo kwa muumba ziko dhahiri kama jua, amemueleza (a.s) Mungu (.s.w.t) kuwa amedhihiri na kujitokeza kwa viumbe Wake, na kilichowajulisha kuwepo Kwake ni viumbe Wake na kule kuwaumba Kwake wao.
 • 2. Na mwenye kudhihiri nyoyoni mwao: Unaona hakusema machoni mwao, kwa sababu haonwi (s.w.t) kwa macho, huonwa (s.w.t) kwa nguvu za uoni wa kiroho.
 • 3. Mradi wa wenye dhamiri hapa, ni wenye nyoyo.
 • 4. Amemkanushia kuzingatia na kufikiri; kwa kuwa hilo huwa kwa wenye dhamiri na nyoyo wenye upinzani tofauti.
 • 5. Mti wa nasaba ya manabii ni wana wa Ibrahim (a.s) kwa kuwa manabii (wengi) wame- toka kwenye kizazi chake Ibrahim (a.s.).
 • 6. Surrat–ul-Bat’ha’a: Ni katikati ya Bat’ha’a na ni eneo ambalo walikuwa wanaishi makabila ya makuraishi, na walikuwa wakiitwa Maqureishi wa Bat’ha’a.
 • 7. Mawasiimu: Ni vyuma vitumikavyo kuwaweka alama wanyama kwa mfano farasi na aina nyingine za wanyama kama vile ng’ombe nk.
 • 8. Imefichuka yaani siri imeinyenyekea nuru ya ufahamu kwa hiyo (hii nuru) inaifichua na kuimiliki, na wenye fahamu wanaitumia siri wapendavyo.
 • 9. Miili bila ya roho: Yaani watu bila ya roho wala akili, na roho bila ya miili: Inawezekana anakusudia wepesi (wa kichwa) mfano wa roho bila ya mwili, na yawezekana anakusudia kupungua kwao (akili).
 • 10. Ibada bila wema: Amewanasibisha na unafiki,
 • 11. Biashara bila faida: Amewanasibisha na riya’a. Biashara bila faida: Ni ishara ya unafiki.
 • 12. Wako macho usingizini: Yaani wao wako macho, hali wameghafilika na ukweli kama waliolala, hali ni hiyo hiyo katika ibara zinazofutia.
 • 13. Maana inakuwa: Inakubebesheni dini na da’awa yake. Na yawezekana awe anakusudia kwa kauli yake: ‘Anakupimieni kwa kilo yake;’ watu wake wanakulazimisheni kuingia kwenye jambo lao, na wanakuchezeeni, wanakuinueni wanakuteremsheni kama afanyavyo mpimaji wa ngano kwayo apimapo kwa pishi yake - pishi ni kipimo kiasi cha ujazo wa kg.3 na zaidi kidogo, au ikuchukueni kwenda kuhiliki jumla kama mpimaji apelekapo ana- chokipima miongoni mwa punje.
 • 14. Mabaki ya chakula ndani ya chungu kilichokwishapakuliwa (ukoko ukitaka) na mradi wake hapa ni watu duni wa hali ya chini.
 • 15. Ni kinachodondoka baada ya kukung’uta, na mradi ni kinachobakia baada ya kumwa-ga.
 • 16. Suala ameliatua: Yaani ameliatua huyu mliganiaji wa kiungu suala kwenu kama inavyoatuliwa chaza na kujulikana kilicho ndani, na kama unavyomenywa mti na utomvu kutolewa. Na amelitaja hili hususan kwa sababu utomvu utolewapo hakuna athari inay- obakia, hivi ndivyo walivyosema.
 • 17. Watahamana kwa dini: Yaani watafanyiana uadui na kutengana, na mradi wake ni: Mtu wa dini kwao ni wa kuhamwa na kutengwa.
 • 18. Yaani kwa sababu ya watoto kukithiri kutowatii wazazi wao mvua itakuwa haba, yase- mekana hiyo ni miongoni mwa alama za saa Kiyama na sharti zake, mvua itakuwa joto, kwa sababu watu watakuwa hawapati faida yake, na kunufaika na kheri yake, hali hii inashabi- hiana mno na hali ya zama hizi!
 • 19. Yaani mzinzi atakuwa rafiki wa mzinzi kana kwamba kuna nasaba kati yao.
 • 20. Mradi wake: Hukumu za kiislamu zitakuwa kinyume katika zama hizo.