read

56 - Na Miongoni Mwa Maneno Yake (A.S)

Na miongoni mwa maneno yake (a.s) - Zamakhshari ameieleza hotuba hii katika Rabiul-Abraar, mlango wa Al-qatil wa shaha- da. Na ibn Muzahim katika kitabu Swifiin, uk. 520.

Siku Ya Siffiin Alipowaamuru Watu Kufanya Suluhu

“Kwa hakika tulikuwa na Mtume wa Mungu (s.a.w.w.); tunawaua baba zetu na watoto wetu na ndugu zetu na ammi zetu. Hilo lilikuwa halituzidishii kitu isipokuwa imani na kusalimu amri, na kuendelea ndani ya njia ya sawa na kuvuta subira kwa machungu yake na umakini katika kumpiga vita adui. Alikuwa mtu kutoka upande wetu na mwingine kutoka kwa adui yetu wanashambuliana kama wanavyoshambuliana maksai wawili kwa pembe wakitoana nafsi zao, yupi miongoni mwao atawahi kumnywesha mwenzake kikombe cha umauti, basi mara ilikuwa sisi twafanikiwa dhidi ya adui yetu na mara nyingine anafanikiwa adui yetu dhidi yetu, Mungu alipoona ukweli wetu aliwateremshia adui zetu udhalili na kutelekezwa, na aliteremsha kwetu nusura, kiasi cha Uislamu kuimarika na kumakinika na kukaa mahali pake.
“Namuapa Mungu lau tungekuwa tunayafanya mliyoyafanya, dini haingekuwa na nguzo,1 ya kutuwama wala imani tawi lake halingesitawi. Wallahi mtamkamua damu2 na mtamfuatilia na majuto.”3

  • 1. Maneno haya kwa utaratibu ujulikanao kwa: Istiara yaani neno huazimwa na kutumika mahali sio pake, mfano: kuimarika kwa Uislamu ametumia neno:
    Mathbuta asili ya maana yake: jiiranu ni sehemu ya mbele ya shingo ya ngamia kutokea sehemu anayochinjwa mpaka kooni, ila hapa limetumika kumaanisha kuimarika kwa Uislamu. Hivyo basi Uislamu umeimarika na kuthibiti kama ngamia anapoitupa shingo yake ardhini tayari kwa kuchinjwa, pia neno: Mutabawau awtami limetumika mfano wa mwili unapochukua nafasi ya kuishi nyumbani kwake, na neno Maqamaliddin umuuda ameifanya dini mfano wa nyumba inayosimama juu ya nguzo. Ameifananisha dini na mti wenye matawi yawezayo kusitawii.
  • 2. Mutamkamua damu, mfano huo huambiwa Alie lifuja jambo: (utakamua damu) na asili yake ni ngamia endapo mkamuwaji atapita kiwango kumkamua kiasi cha kwisha maziwa na kuanza kutoa damu. Hivyo basi kukamua damu ni mfano wa kujikokotea matokeo mabaya wao wenyewe kutokana na matendo yao, kwa hiyo hayo matendo yatafuatiwa na majuto mzunguko wa mambo utakapowasibu nyumbani kwao.
  • 3. Maneno haya aliasema Amirul’Mu’minina (a.s.) kuhusu kisa cha Abdullah ibn Aamir Al-Hadramiy alipokuja Basra kwa upande wa Muawiyah, Amirul-Mu’minina (a.s.) ali- wahimiza swahaba zake kwenda Basra; Hawakumwitika.