read

57 - Na miongoni mwa maneno yake (a.s)

Na miongoni mwa maneno yake (a.s) - Khutba hii ameieleza Al-Baladhuriy ndani ya Ansabul-Ashraafi) katika tarjuma ya Ali (a.s), na Al’Haakim ndani ya Al’Mustadrak, Jz. 2, uk. 385, na At-Tuusi ndani ya Al-Amaali uk. 214 na 347, na wengine.

Akiwapa Habari Kuhusu Mtu Atakayeamrisha Atukanwe Imam (A.S)

“Punde baada yangu atapata ushindi juu yenu mtu mwenye koo pana, tumbo kubwa, ala akionacho, na huomba asichoweza kukipata, basi muuweni, na hamtomuuwa.1 Lo! Kwa hakika yeye atawaamrisheni mnitukane, na kujiepusha na mimi; ama kuhusu kutukana nitukaneni, kwa kuwa hiyo kwangu ni utakaso na kwenu ni uwokovu; ama kuhusu kujiepusha na mimi; wala msijiepushe na mimi; kwa kuwa mimi nimezaliwa ndani ya fitra na kutangulia katika imani na hijra.”2

  • 1. Haipingani kati ya kuamrisha kitu na kutoa habari kwamba hakitatokea. Kama ambavyo Mungu swt. amesema: “Fatamannawul-mauta inkutum swadiqiina. Walaa yatamannawunahu abada.......” Myatamani mauti kama ninyi ni wakweli. Wala hawayatamani kamwe. (Al-Jumu’a; 62: 6 na 7).
  • 2. Huenda ukamtukana mtu ukiwa umelazimishwa na huku umeficha upendo wake, kwa hiyo utaiepuka shari ya aliyekulazimisha, na hakukulazimisha ila umtukane isipokuwa anayelitukuza suala lake na yu ataka kumdhalilisha, na huo ni utakaso kwa mwenye kutukanwa. Ama kujiepusha na mtu ni kujivua mbali na madhehebu yake.