read

58 - Na miongoni mwa usemi wake (a.s)

Na miongoni mwa usemi wake (a.s) - Ibn Qutaybah ameieleza ndani ya Al’Imama was-siasa Jz. 1, uk.124. Na Sibtu Ibnul’Jauziy katika Tadhkiratul’khawasi uk.100.

Aliwasemesha Khawarij

“Tufani iwakumbeni, wala asibakie miongoni mwenu chakubimbi. Hivi baada ya imani yangu kwa Mungu, na jihadi yangu pamwe na Mtume wa Mungu (s.a.w.w.) nijishuhudie binafsi kuwa ni kafiri!

قَدْ ضَلَلْتُ إِذًا وَمَا أَنَا مِنَ الْمُهْتَدِينَ {56}

“Hivyo basi nitakuwa nimepotea wala sitokuwa miongoni mwa walio ongoka.” (6:56)

Rejeeni marejeo ya shari, rejeeni mkifuata athari ya nyayo. Angalieni! kwa hakika mtapata udhalili baada yangu wa sura ya jumla, na upanga mkali wenye kukata, na hilo litachukuliwa na wadhalimu hao kwenu kuwa ni sunnah.”1

Maelezo

Ar-Radhiy (r.a) amesema: Usemi wake (a.s) huelezwa katika njia tatu: Iwe kama tulivyosema: kwa raa, kutokana na kauli yao kwa mtu ambaye anapandikiza mtende, yaani yuautengeneza vizuri. Na yaelezwa kwa na yakusudiwa kwalo yule aelezaye Hadithi, na kuizungumzia na hii ndiyo njia sahihi kwa maoni yangu. Kama kwamba (a.s) amesema: Habakii kati yenu msimuliaji. Na huelezwa kwa tamko kwa nayo hukusudiwa mwenye kuchupa na mwenye kuhiliki pia huambiwa

  • 1. Aliwaonya kwa watakayokutana nayo miongoni mwa matokeo mabaya, ya kunyimwa ngawira na kuhusika wao (wanyimaji) wenyewe na faida za mali mbali na wao, na kunyimwa kwao kila aina na haki.