read

59 - Na Alisema (A.S)

Alipoazimia Kuwapiga Vita Khawarij, Na Aliambiwa: Kwa Hakika Hawa Watu Wamekwishavuka Daraja La An-Nahrawaan

Hapo alisema: “Maangukio yao ni chini ya nutfa, Wallahi hawaponyoki kumi miongoni mwao, 1na wala hawatokufa isipokuwa kumi miongoni mwetu.” Sharifu Ar-Radii (r.a) amesema: nutfa anakusudia maji ya mto wa Furaat na hili ni jina mbadala zuri mno kwa maji japo maji yawe mengi. Na hilo tuliliashiria hapo nyuma wakati wa kulipita linaloshabihiana nalo.

  • 1. Habari hizi ni miongoni mwa habari ambazo zinakaribia kuwa zimezagaa; kwa umashuhuri wake na kunakiliwa kwake na watu wote; nayo ni miongoni mwa miujiza yake na habari zake za ufafanuzi wa mambo yaliyoghibu. Kwa kuwa hakuokoka miongoni mwao ila watu tisa na wametawanyika katika nchi, na hawakuuliwa katika as’habi wa Amirul-Mu’minin ila wanane.