read

60 - Na Amesema (A.S)

Na Alisema (a.s) - Ameieleza al-Mubaridu katika al-Kamil Jz. 2, uk. 120, na al-Baihaqiy katika al- Mahasin wal Masawi uk. 380, katika mlango Mahasinus-Swidiqi, na Mas’ud katika Muruj al-Dhahab, Juz. 2, uk. 416.

Walipouliwa Khawarij Aliambiwa: “Ewe Amirul-Mu’minina, Hawa Jamaa Wameangamia Wote!” Ndipo Aliposema

“Lahasha wallahi: wao ni nut’fah ndani ya migongo ya wanaume na mifuko ya uzazi ya wanawake, na kila kiongozi akijitokeza1 kati yao hukatwa mpaka wa mwisho wao wawe wevi vibaka”.

  • 1. Yaani kila ajitokezapo raisi kati yao huuliwa, mpaka mwishowe mambo yao yaishie kuwa wevi na vibaka, hawatokuwa wafalme, wala hawatopata nusra ya kufikia kufanya madh’habu, wala hawatolingania itikadi, hali yao ni hali ya watu wa shari maharamia wajinga.