read

61 - Na Alisema (A.S.)

Kuhusu Khawarij

“Msiwapige vita Khawarij baada yangu; kwa kuwa sisawa kati ya mwenye kuutafuta ukweli na akakosea na ambaye ameitafuta batili na kuipata (amkusudia Muawiya na sahaba zake).”1

  • 1. Madhumuni yake ni kuwa Khawarij wamepotea kwa mkanganyiko uliowaingia, na walikuwa waitafuta haki, hali wao kwa jumla ni wenye kushikamana na dini, na wenye kuihami itikadi waliyoiamini, japokuwa walikosea katika hilo; na kuhusu Muawiyah hakuwa yu atafuta ukweli, bali alikuwa mwenye batili, alikuwa haihami itikadi aliyojijengea kwa mkanganyiko. Hivyo basi wao waliamini kwamba kujitoa katika utii wa Imam ni miongoni mwa ambayo dini inawajibisha juu yao. Wao - yaani Khawarij - walikuwa wametafuta ukweli unaokubalika kisheria, wakakosea usawa wake humo, lakini wao baada ya Amirul-Mu’minina watatoka wakiwa na dhana yao hii kumwendea aliyepata ushindi wa uamiri bila ya haki, nao ni wafalme walioutaka ukhalifa kwa njia ya batili na wakaudiriki hali wakiwa sio wastahiki. Hivyo basi Khawarij pamoja na ambayo waliyonayo wako katika hali nzuri kuliko wao (wakina Muawiyyah).