read

62 - Na Katika Maneno Yake (A.S)

Na Katika Maneno Yake (a.s) - As-Saduq ameinakili katika Man laa Yahdhuruhu al-Faqih, jalada la kwanza, uk. 329, na Abu Na’im katika al-Hiliyatu, jalada la kwanza, uk. 77, na at-Tusi katika al-Misbahu, uk. 461, na al-Mufid katika al-Amaal, uk. 87.

Pindi Alipohofishwa Kuuliwa Ghafla (Akasema)

“Kwa hakika mimi nina ngao madhubuti kutoka kwa Mungu, siku yangu itakapokuja itajitoa mbali na mimi na kuniachia; wakati huo mshale hautokosea wala jeraha halitopona.”