read

70 - Na Amesema (A.S)

Na Amesema (a.s)- Ibn Sa’ad ameielezea ndani ya at-Tabaqat, Jz. 3, uk. 36, na Al’Qaaliy ndani ya Dhaylul’amali uk. 190, na Al’Isfahani ndani ya Maqatilu Talibiin uk.16, na Ibn Abdi Rabih ndani ya Al-Iqdul al-Farid Jz. 2, uk. 298, na wengine.

Katika Mkesha Wa Siku Aliyoshambuliwa

“Nilipatwa na usingizi nikiwa nimekaa nikamuona Mtume wa Mungu (s.a.w.w.), nilimuuliza: ‘Ewe Mtume wa Mungu! Kupindama kulikoje na uadui ambao nimekabiliana navyo kutoka kwa umma wako!’ Akasema: ‘Wapatilize,’ Nikasema: ‘Mungu anibadilishie walio bora kuliko wao, na anibadilishe na aliye mbaya zaidi kwao kuliko mimi.”1

Amesema Ar-Radhiy (r.a): Anakusudia kwa neno kupindama, na kwa neno mzozo, na huu ni ufasaha wa hali ya juu mno wa maneno.

  • 1. Sharran: Shari hapa haijulishi kwamba ndani yake kuna shari, ni kama kauli yake swt: “Qul adhalika khairun am janatul-khuldi.” (Swafat) haijulishi kuwa ndani ya moto kuna heri.